267 66 564KB
Kiswahili Pages 154 Year 2021
SOTERIOLOJIA MAFUNDISHO YA KIKRISTO KUHUSU WOKOVU
TEOLOJIA PANGILIFU-2
1
Hakimiliki © 2020 Daniel John Seni Chapa ya January, 2021
Msanifu: Eternal Word and Charity Publishing (EWCP). Dar es Salaam [+255-755-643-590] Mchapaji: Truth Printing Press. Dar es Salaam [+255764425704] ___________________________________ Haki zote zimehifadhiwa. Hakuna sehemu ya chapisho hili inayoweza kuzalishwa tena, au kuboreshwa au kusambazwa kwa njia yoyote au kwa kubadilisha umbo au kunakili na kupeleka katika umbo lingine bila idhini ya mwandishi. _______________________________________ Maandiko ya Biblia yamechukuliwa kutoka kwenye Biblia ya Kiswahili Toleo la shule inayotolewa na Swahili Union Version (SUV). Tafsiri iliyotumika kwenye marejeleo yaliyokuwa kwenye lugha ya kiingereza si tafsiri rasmi; hivyo inaweza kuendelea kuboreshwa kwa kila chapa ya kitabu hiki. ________________________ Msambazaji Shekinah Mission Centre (SMC) [email protected] S.L.P 32807 Dar es Salaam +255 769 080 629 +255 787 907 347 Madale/Mivumoni, Joshua road, mkabala na Shule ya Msingi-Atlas/ at Shekinah Presbyterian Church in Tanzania, Dar es Salaam
TABARUKU Kwa wanazuoni wote wa teolojia
i
UTANGULIZI Huu ni mfululizo wa masomo katika uwanja wa
“Teolojia
Pangilifu”
(Systematic
Theology). Sasa tunashughulikia somo la Soteriolojia, yaani somo linalohusu “wokovu wa mwanadamu.” Siku
hizi
pengine
inaweza
kudhaniwa
kwamba kila Mkristo anajua maana ya wokovu na upatikanaji wake. Watumishi wengi wasiopenda kujishughulisha huishia kusema “Yesu anaokoa” bila kufafanua maana ya sentensi hii nyepesi na rahisi sana.
Ni
misiolojia
kweli
katika
tunaweza
muktadha
kutumia
wa
sentensi
nyepesi kama hizi bila kuzitolea ufafanuzi kwa
sababu
tunachukulia
wale kwamba
chochote.
ii
tunaowaambia hawajui
kitu
Siku
hizi
“makanisa
kuna ya
makanisa
wokovu”
yanayojiita,
ambayo
hudai
kuhubiri wokovu wa kweli. Hata hivyo, nimegundua mafundisho
mapungufu yao
mengi
kuhusu
katika
wokovu
kwa
kudhania kwamba wokovu ni tukio la sekunde moja. Ama kwa hakika, wokovu ni mchakato; ingawa
yawezekana
michakato
hiyo
isipangiliwe vizuri na kuleta maana, lakini bado tunapaswa kujua kwamba wokovu ni mchakato. mwanadamu
Mchakato
wa
unaanzishwa
kumwokoa na
Mungu
mwenyewe na kumaliziwa pia na Mungu mwenyewe. Katika kitabu hiki, kwa namna ya upekee nimejaribu kufafanua kwa undani kuhusu michakato hiyo kwa kuzingatia ufafanuzi
iii
wa
teolojia
iliyoboreshwa
(Reformed
Theology) Kitabu
hiki
wameshazaja
si
kwa
akili
wale
zao
ambao
mafundisho
mbalimbali ya wokovu, na hivyo hawataki kubadilisha mwelekeo na kujifunza upya. Pia kitabu hiki si kwa wazembe, wasiopenda kushughulisha
akili
zao.
Si
kwa
wale
wanaopenda kutafuniwa tu, bali ni kwa wale ambao wanaweza kuvunja mifupa na kuelewa. Ninakutia moyo kwamba unaposoma kitabu hiki
unahitaji
kusoma
katika
hali
ya
utulivu, na kumwomba Roho Mtakatifu akusaidie ili uweze kuelewa zaidi na zaidi somo hili muhimu. Marejeleo mengi yaliyotumika katika kitabu hiki yanatokana na lugha ya Kiingereza, iv
hivyo basi, kwa wale ambao wana uwezo wa kusoma Lugha ya Kiingereza wanashauriwa kupata baadhi ya nakala za vitabu hivyo kwa sababu ni muhimu sana. Yawezekana katika kitabu hiki ninaweza nisikubaliane na baadhi ya tafsiri ya kambi ya Teolojia Iliyoboreshwa kwa asilimia zote, lakini
kwa
kweli
kwa
sehemu
kubwa
inakubaliana na mafundisho halisi ya Neno la Mungu.
v
Yaliyomo TABARUKU .................................................i UTANGULIZI .............................................. ii Yaliyomo ................................................... vi SURA YA KWANZA .....................................1 Maana ya soteriolojia ...............................1 Kila Dini Hutafuta Wokovu ......................4 Hitaji la Wokovu kwa Mwanadamu ..........7 Mpango wa Wokovu wa Mungu kwa Wokovu wa Mwanadamu .......................10 Mungu alijua mapema kila kitu .............12 Mpango wa Kusudi la Mungu la Milele ..19 Wito wa Kupokea Wokovu......................21 SURA YA PILI ...........................................25 MPANGILIO WA WOKOVU ........................25 SURA YA TATU .........................................34 KUCHAGULIWA MAPEMA NA KUITWA .....34 vi
a.
Kuchaguliwa ..................................34
Dhana potofu kuhusu kuchaguliwa mapema ................................................42 Majibu kwa dhana potofu ......................44 Ni Wateule tu.........................................46 b.
Kuitwa............................................55
Maswali fikirishi ....................................66 SURA YA NNE ..........................................67 KUZALIWA UPYA NA KUHESABIWA HAKI 68 a.
Kuzaliwa Upya................................68
b.
Kuhesabiwa Haki ...........................75
SURA YA TANO ........................................88 TOBA NA UTAKASO .................................88 a.
Toba ...............................................88
b.
Utakaso ..........................................97
SURA YA SITA ........................................ 103 vii
KUFANYWA WANA ................................. 103 SURA YA SABA ...................................... 111 KUHIFADHIWA, UHAKIKISHO NA KUTUKUZWA ......................................... 111 a.
Kuhifadhiwa ................................. 111
b.
Uhakikisho ................................... 122
c.
Kutukuzwa ................................... 127
SURA YA NANE ...................................... 129 TULIP ..................................................... 129 T-Total depravity (Upotovu Kamili) ....... 130 U-Unconditional election (Uchaguzi usiokuwa na masharti) ........................ 132 L-Limited atonement (Upatanisho wenye Mipaka) ............................................... 133 I-Irresistible grace (Neema Isiyoweza Kuzuiliwa) ........................................... 134
viii
P-Perseverance of the saints (Uvumilivu wa Watakatifu) .................................... 135 Marejeleo ................................................ 138
ix
SURA YA KWANZA DHANA YA WOKOVU Maana ya soteriolojia Soteriolojia (Kiingereza Soteriology) ni tawi la teolojia linahusika na wokovu. Neno hili
linatokana
na
neno
la
Kigiriki
“soterion” lenye maana ya "wokovu," na pia linahusiana na neno “soter,” yaani "mwokozi."1
Mtu
mwingine
huenda
akajiuliza, ya nini kuandika maneno ya Kigriki katika andiko la Kiswahili? Ni sahihi kujiuliza hivyo, lakini ikumbukwe kwamba Biblia katika Agano Jipya iliandikwa kwa Kigiriki kabla ya kutafsiriwa katika lugha za makabila mbalimbali duniani, kwa sababu hiyo kurejelea maana ya neno kwa asili yake inasaidia
kuelewa
vizuri
Bruce Demarest, The Cross and Salvation (Wheaton: Crossway Books, 1997), 28-29 1
1
kile
kilichokusudiwa awali. Hata hivyo maneno haya mara nyingi yanakuwa ni ya kitaaluma sana; hivyo basi ili kusaidia watu wote waweze kuelewa, na kwa kuwa “soteriolojia” ni neno la kitaaluma, basi katika kitabu hiki tutatumia neno ambalo ni mbadala wake kwa Kiswahili, yaani “Wokovu.” Soteriolojia ni somo linaloshughulikia uwasilisho
wa
baraka
za
wokovu
kwa
mwenye dhambi na kurudishiwa upendeleo wa kimungu katika ushirika wa karibu na Mungu. Huonyesha ujuzi wa Mungu kama chanzo cha kutosha cha maisha, nguvu na furaha ya wanadamu. Inafaa zaidi kujifunza “soteriolojia”
ukiwa
umekamilisha
kujifunza “Kristolojia” Wanazuoni wengi huweka “soteriolojia” pamoja na “pneumatolojia” (Elimu kuhusu Roho Mtakatifu) kwa sababu inaaminika 2
kwamba “soteriolojia” ni kazi ya Roho Mtakatifu kutumia kile ambacho Kristo amekinunua pale msalabani kwa ajili ya Wateule wake. Roho Mtakatifu anaweka wokovu kwa Wateule kwa wakati ambao umeamriwa na Mungu Baba. Kitu ambacho hapa
ninaweza
kusema
ni
kwamba
“wokovu” ni tendo zima la Utatu wa Mungu. Kwamba Mungu Baba anachagua wateule, Yesu Kristo ananunua wokovu wao, na kisha Roho Mtakatifu anautumia wokovu huo kwa Waamini. Wokovu ni tukio na mchakato
ambao
watu
huletwa
katika
uhusiano mzuri na Mungu. Mafundisho kuhusu wokovu yanaweza kuonekana kama rahisi na mepesi sana, lakini yamekuwa na changamoto kubwa katika Ukristo. Si katika Ukristo peke yake, katika dini mbalimbali duniani wokovu wa 3
mwanadamu ni ajenda ambayo haielezeki kirahisi. Somo hili ni nyeti sana kiasi kwamba linashikilia mandisho mengine ya Biblia.2 Kila Dini Hutafuta Wokovu Dhambi imetafuna sehemu zote za mwanadamu,
na
matokeo
yake
kila
mwanadamu kwa namna fulani hujaribu kutafuta wokovu kwa njia ambayo anaona yeye ni sahihi. Kwa hiyo kiini cha kila dini ni kutafuta wokovu. Dini zote hutafuta njia ya wokovu; wanadamu wote wanatamani furaha kwa sababu moyo wa mwanadamu umeumbwa kwa ajili ya Mungu na hauwezi kupumzika mpaka
amupate
(Augustine).
Walakini,
katika giza la ufahamu wetu na mawazo Samuel Waje Kunhiyop, African Christian Theology (Kenya: HippoBooks, 2012) 77. 2
4
mabaya ya mioyo yetu, hatumtafuti kwa njia sahihi. Dini za kipagani hazina dhana juu ya utakatifu wa Mungu; hawaelewi dhambi sawasawa na hawajui chochote kuhusu
neema.
Hawamjui
Kristo,
wanatafuta wokovu kwa njia ya matendo. Buddha mwanafunzi
aliwahi wake,
kumwambia
“Kuwa
nuru
mwenyewe!"
“Kuwa
kimbilio
mwenyewe.
Usikimbilie
kitu
chochote.
Shikilia
ukweli
yako lako
kingine
kama
taa.
Usitafute kimbilio kwa mtu mwingine yeyote isipokuwa wewe mwenyewe.”3 Kwa hiyo kwa mujibu wa dini ya Buddhism kila mtu ni mwokozi wake mwenyewe. Hakuna mtu au mungu
anayeweza
kumwokoa
mtu
mwingine zaidi ya mtu mwenyewe.
Bavinck, Herman. Reformed Dogmatics (pp. 473-474). Baker Publishing Group. Kindle Edition. 3
5
Katika
Uislam,
mtu
anakombolewa
kwa kumwamini Mungu mmoja na mtume Muhammad
kama
nabii
wake
na
kwa
kufanya majukumu ya kidini kama vile sala, sadaka, kufunga, kuhiji. Kwa hiyo kwa mujibu wa Waislam wokovu si zawadi, bali ni matendo binafsi ya mtu, ni juhudi zako binafsi ambazo zinakufanya uepuke adhabu ya kuzimu. Dini
nyingi
zinatafuta
ukombozi
kupitia hatua za wanadamu. Kwa maana hiyo,
dini
hizi
zinawataka
wanadamu
kutimiza sheria fulani iliyowekwa. Mkazo wa maadili
na
matendo
ndiyo
husisitizwa
katika dini hizi kwa ajili ya kuwapatia watu wokovu wao wa milele. Kwa hakika maisha ya baadaye huangaliwa kwa umakini na hivyo mtu kuishi maisha ya mzigo kwa ajili ya kujaribu kupata wokovu kwa njia yake 6
binafsi.
Mara
nyingi
utasikia
watu
wakisema, “wokovu ni matendo tu.” Au “wokovu ni wewe mwenyewe tu ulivyojiweka kwa
Mungu.”
Au
utasikia
wapendwa
wakisema “shikilia wokovu wako.” Katika mawazo
haya
mwanadamu
wokovu sana,
unaegemea
badala
ya
kwa
Mungu.
Mungu ni hakimu tu, wa kuangalia makosa ya mwanadamu na kuhukumu; rehema na neema zake zinaachwa. Mpango wake wa wokovu kwa wanadamu haujulikani katika dini nyingi kwa sababu shetani ameelekeza moyo wa wanadamu huko. Utafutaji wa wokovu kwa njia za wanadamu katika dini nyingi huonesha wazi kwamba mwanadamu anahitaji wokovu. Hitaji la Wokovu kwa Mwanadamu Wokovu si tukio la kushtukiza kwa Mungu,
bali
Mungu 7
kwa
kusudi
lake
takatifu, aliruhusu mwanadamu aanguke katika majaribu katika Bustani ya Edeni, na hivyo dhambi iliingia ulimwenguni. Dhambi ilisababisha utengano kati ya Mungu na mwanadamu, na hivyo, “…wote wamefanya dhambi, na kupungukiwa na utukufu wa Mungu.” (Rum 3:23). Nabii Isaya 59:2 anatuambia
“Lakini
maovu
yenu
yamewafarikisha ninyi na Mungu wenu, na dhambi
zenu
zimeuficha
uso
Wake
msiuone, hata hataki kusikia.” Kwa nukuu hizi, hakuna mwanadamu ambaye anaweza kujiokoa
mwenyewe.
Hakuna
ambaye
anaweza kutimiza matakwa ya sheria ya Mungu. Kuna mawazo mbadala kwamba hitaji la wokovu si kwa mwanadamu peke yake, hata kwa viumbe wengine nao wanahitaji wokovu.
Wanaosisitiza 8
hili
wananukuu
Warumi 8:19-22 “Kwa maana viumbe vyote pia
vinatazamia
kwa
shauku
nyingi
kufunuliwa kwa wana wa Mungu. Kwa maana viumbe vyote pia vilitiishwa chini ya ubatili; si kwa hiari yake, ila kwa sababu yake yeye atiyevitiisha katika tumaini; kwa kuwa viumbe vyenyewe navyo vitawekwa huru
na
kutolewa
katika
utumwa
wa
uharibifu, hata viingie katika uhuru wa utukufu wa watoto wa Mungu. Kwa maana twajua ya kuwa viumbe vyote pia vinaugua pamoja, navyo vina utungu pamoja hata sasa.” Japokuwa kuashiria
fungu
uumbaji
kurejeshwa
upya,
hilo
linaweza
mwingine
kuhitaji
haimaanishi
kwamba
vinahitaji wokovu kama ulivyo wokovu wa wanadamu; bali vitafurahia matunda ya wokovu
wa
mwanadamu 9
wakati
wa
kutukuzwa. Kwa hiyo katika maisha haya viumbe vingine havihitaji wokovu kama ilivyo kwa mwanadamu. Mpango
wa
Wokovu
wa
Mungu
kwa
Wokovu wa Mwanadamu Mara
nyingi
maneno
"mpango
wa
milele wa Mungu wa wokovu" hutumiwa katika uinjilishaji kwenye zile karatasi kwa kutaja vitu vitatu au vinne Mungu anataka mtenda dhambi afanye ili aweze kuokolewa, kwanza, Tambua kwamba wewe ni mwenye dhambi na unahitaji wokovu, pili, amini kwamba Yesu alikufa msalabani kwa ajili ya dhambi
zako,
tatu,
Muombe
Mungu
akusamehe dhambi zako, nne, mtumaini Yesu.
na
baada
ya
hapo
mhusika
anasalishwa sala ya toba. Mambo haya ni ya muhimu, lakini hayaonyeshi mpango wa Mungu wa wokovu. Ni taratibu nzuri katika 10
kuelewesha mtu aitikie mwito wake, lakini huenda isieleze usahihi wa mpango wa Mungu wa wokovu. Neno wokovu laweza kuonekana kuwa ni rahisi lakini kwa kweli linajumuisha dhana nyingi ambazo haziwezi kueleweka kikamilifu kwa akili ya kawaida. Tunaweza kujiuliza maswali ya kawaida tu, Je, wokovu ni kwa ajili tu ya kuikimbia jehanamu? Je, ni jambo ambalo Mungu alihitaji kulifikiria wakati Adamu na Hawa walipomwasi? Je Mungu
kweli
wataokoka
anajua
kwa muda
ni
akina
nani
gani? Jambo
la
kuzingatia katika maswali haya ni kuwa Biblia
inatufundisha
kwamba
Mungu
alipanga wokovu wetu kabla ya msingi wa ulimwengu, kwa kuwa anajua mambo yote, alijua kwamba mwanadamu atauhitaji, na
11
huu si utabiri wa Kimungu, bali ni ujuzi wa mapenzi yake yasiyo na kipimo. Mungu alijua mapema kila kitu Katika WCF/3/14 Tunasoma, “tangu asili, Mungu ameamua na kuweka kila kitu kinachotokea. Yeye hufanya maamuzi haya kwa uhuru kwa mapenzi Yake ya busara na utakatifu. Hakuna kitu ambacho ameamua tangu asili kinaweza kubadilika. Maamuzi haya haimaanishi kwamba Mungu ndiye mwanzilishi wa dhambi na kwamba Yeye hatulazimishi kufanya vitu kinyume cha mapenzi yetu. Yeye ndiye chanzo cha kila kitu, lakini hii haimaanishi kwamba vitu vingine havijahusika; hata hivyo, Mungu ndiye sababu ya vitu vingine kuwepo.” Kitabu hiki katika lugha kimetafsiriwa kama “Misingi ya Imani: Mafundisho ya Msingi ya Kibiblia: Kuhusu Imani Ya Kikristo.” The Westminster Confession of Faith and Large Catechism. Kimefasiriwa na D.J. Seni, 2020. Katika kifupisho hicho WCF/sura/sehemu 4
12
Hoja hii iko katika “amri za Mungu”5 (kiingereza “God’s decrees”) maana yake ni kusudi lake au uamuzi wake kwa mambo yajayo; au, shauri la uamuzi wake, ambalo tangu milele aliamua mapema chochote atakachofanya, au anachoruhusu kufanywa au kufanyika kwa wakati. Ufafanuzi huu huenda sambamba na ukweli linaweza
kwamba
hakuna
kumshangaza
jambo Mungu
ambalo pale
linapotendeka kana kwamba ni jipya na kwamba alikuwa hajui kama litatendeka. Tujue kwamba, “hakuna dhambi, ambaye inaweza kufanyika, hata ile ambayo tayari imeshafanyika Mungu hakujua.”6 Kwa hiyo Neno “amri za Mungu” hapa si zile amri kumi. Mara nyingi linapokuja suala la amri kumi huwa zinaandikwa kwa pamoja kwa kirai, “amri kumi” na kama hakuna neno la amri kumi basi pengine yaweza kuwa ni decree au laws nk. 6 Brown, John. Systematic Theology: A compendious View of Natural and Revealed Religion (Grand Rapids: Reformation Heritage Books, 2002) uk. 159. 5
13
amri ya Mungu inahusu mambo yajayo ambayo Mungu anayajua tangu asili. Pamoja na kuwa Mungu alipanga kila kitu, na kwamba yeye ni sababu ya kila kitu; haimaanishi kwamba “sababu ya pili” (second cause) haipo. Kwa mfano ingawa Mungu alijua kwamba kuna anguko, si kwamba aliwatega Adamu na Hawa ili waanguke, bali kwa uhuru wao wenyewe, waliruhusu majaribu ya Shetani (sababu ya pili kwenye anguko); basi wakaanguka. Na kwa sababu hiyo Mungu halaumiwi kwa anguko lakini bado anajitukuza katika hilo. Kwa hiyo uweza wa Mungu na mapenzi yake
vinafanya
ajue,
na
kung’amua
mapema kuhusu wokovu wa mwanadamu. Hata hivyo, kama tulivyoeleza hapo juu, visababishi
vya
pili
(second
cause)
vinasababisha. Hata visababishi vya pili, 14
bado vimo katika mpango wake. Mungu anapokuwa ametumia visababishi vya pili haimaanishi kwamba anategemea kiumbe chake chochote au wakala yeyote.7 Ingawa Mungu
anajua
chochote
kinachoweza
kutokea katika hali zote zinazowezekana hata hivyo, hajaamuru chochote kitokee kwa sababu aliona tangu asili kwamba kitatokea kwa namna yoyote ile. Mwanadamu
baada
ya
anguko
alipotoka kabisa, “hali nzima imeharibiwa na dhambi, na dhambi hiyo imeenea kwa watu wote na katika maeneo yote kiasi kwamba hakuna kitu kwa mwanadamu
Brown, John. Systematic Theology: A compendious View of Natural and Revealed Religion (Grand Rapids: Reformation Heritage Books, 2002) uk. 149. 7
15
ambacho
kinaweza
kumfanya
akubalike
mbele za macho ya Mungu.”8 Mpango wa wokovu wa mwanadamu ni wa kushangaza, Charles Hodge9 anaweka bayana mchanganuo wa Augustino kuhusu mpango wa Mungu wa wokovu, na hapa chini tutafupisha. 1. Kwamba
utukufu
wa
Mungu,
au
udhihirisho wa ukamilifu wake, ndio Fatima ya juu kabisa na ya mwisho ya vitu vyote. 2. Kwa
hatima
uumbaji
wa
hiyo
Mungu
ulimwengu
alikusudia
na
mpango
mzima wa wokovu. 3. Kwamba Mungu alimweka mwanadamu katika
hali
ya
majaribio,
akimfanya
Charles Ryrie, Basic Theology: A Popular Systematic Guide to Understanding Biblical Truth Kindle Edition 9 Hodge, Charles, Systematic Theology – (Vol. III) (Grand Rapids, MI: Christian Classics Ethereal Library,) 8
16
Adamu, mzazi wao wa kwanza, mkuu wao na mwakilishi. 4. Kwamba anguko la Adamu lilileta wazao wake wote katika hali ya hukumu, dhambi, na taabu, ambapo hawawezi kujikomboa wenyewe 5. Kutoka
miongoni
walioanguka
Mungu
mwa
wengi
alichagua
idadi
isiyohesabika ya watu kwa uzima wa milele, na wengine akawaacha ili wapate malipo ya haki ya dhambi zao. 6. Kwamba msingi wa uchaguzi huu sio utabiri
bali
mwenyewe
ni bila
uamuzi
wa
kuingiliwa
Mungu na
kitu
chochote 7. Kwa wokovu wa wale waliochaguliwa kwa uzima wa milele, Mungu alimtoa Mwanawe
mwenyewe,
kuwa
mwanadamu, na kutii na kuteseka kwa 17
ajili ya watu wake, na hivyo kuleta haki kwao milele na kutoa wokovu wa mwisho kwa wateule. 8. Roho Mtakatifu katika kazi zake za kawaida, yuko kwa kila mtu, maadamu anaishi, na anazuia uovu kuendelea, lakini nguvu zake zenye ufanisi na za kuokoa hutumika kwa wateule. 9. Kwamba
wale
amewachagua, alijitoa
wote kwa
ajili
mwenyewe
ukombozi, wakiwa
hakika
ambao
Mungu
yao
katika
Kristo
agano
(isipokuwa
wachanga),wataletwa
la
wakifa kwenye
ujuzi wa ukweli, kwa mazoezi ya imani, na
kwa
uvumilivu
katika
maisha
matakatifu hadi mwisho. Kwa hakika, huenda Augustino alieleza kwa usahihi kuhusu mpango wa wokovu wa
mwananadamu. 18
Katika
vipengele
vifuatavyo
tutajaribu
kuelezea
kwa
undani mpango huu wa milele ambao Mungu aliuweka tayari kwa ajili ya watu wake. Mpango wa Kusudi la Mungu la Milele Wokovu wa mwanadamu haukuanzia pale
mwanadamu
alipoumbwa,
bali
ni
mpango wa Mungu wa milele, wa tangu asili.
Kwa
mwanadamu
hiyo si
Mungu kwa
anamwokoa
kumwepusha
na
Jehanamu, (ingawa, wasiiokoka wataishia Jehanamu), bali ni “kwa kadiri ya kusudi la milele alilolikusudia Bwana
wetu.”
katika
(Efe.
3:11),
Kristo “kabla
Yesu ya
kuwekwa misingi ya ulimwengu” (Efe. 1:14) Katika Warumi 8:28 Paulo anasema kwamba Wakristo waliitwa "kwa wokovu" kulingana na kusudi lake.” Katika Waefeso 1:11
anasema
kwamba 19
Wakristo
“Walifanywa warithi [wa Mungu], wakiwa wamechaguliwa tangu zamani kulingana na kusudi
lake
yeye
afanyaye
vitu
vyote
kulingana na kusudi la mapenzi yake.” Na katika 2 Timotheo 1: 9 Paulo anathibitisha kwamba “Mungu alituokoa na kutuita sisi kwa
wito
mtakatifu,
sio
kulingana
na
matendo yetu bali kulingana na makusudi yake na neema tuliyopewa katika Kristo Yesu tangu milele. Katika Luka 22:22 Yesu aliwafundisha wanafunzi Mwana
wake
wa
kwamba
Adamu
ilivyokusudiwa
(kama
Mungu).
Petro
kwamba
ingawa
"
aenda
Kwa
kuwa
zake
kama
ilivyokusudiwa
anafafanua Herode,
kwa
Wafalme,
na wazi na
wengineo walihusika katika kifo cha Yesu, walihusika kwa sababu ya kutimiza kusudi la milele la Mungu. Anasema, “ili wafanye 20
yote ambayo mkono wako na mashauri yako yamekusudia tangu zamani yatokee.” (Mdo 4:28) Wito wa Kupokea Wokovu Kwa kweli ningeweza kuita, wito wa kudhihirisha wokovu, lakini kwa sababu za kiteolojia tutumie neno “wito wa kupokea wokovu.” Ingawa Mungu aliandaa kila kitu kwa ajili ya wokovu wa wateule, ni kwa wakati
maalumu
alimua
kufanya
udhihirisho wa kile alichokipanga mapema. Katika WCF/8/1 tunasoma kwamba, “Mungu, katika kusudi lake la milele ilimpendeza Bwana
kumchagua
Yesu,
mpatanishi
Mwana kati
ya
na
kumteua
pekee, Mungu
kuwa na
Mwanadamu…” Mwana wa Mungu, nafsi ya pili ya Utatu, ni Mungu wa milele, ni sawa 21
na
Baba.
Katika
utimilifu
wa
wakati
alichukua asili ya mwanadamu (Gal. 4:4) alichukua sifa muhimu na udhaifu wa kawaida
wa
mwanadamu-isipokuwa
kwamba alikuwa hana dhambi, (Ebr 2:14, 16-17, 4:15) kwa sababu angekuwa na dhambi
asingeweza
kuwa
Mwokozi
wa
wateule. Mwenye dhambi hawezi kumwokoa mwenye
dhambi
asemavyo
mwenzake.
Athanasi,
Kama
akinunuliwa
na
Geoffrey W Bromiley kwamba, “kwa upande mwingine, hakuna mtu anayeweza kufa kwa ajili ya wote na asiharibike.”10 Tunasoma kwamba, Yesu alichukuliwa mimba
kwa
nguvu
ya
Roho
Mtakatifu
tumboni mwa Bikira Mariamu, ambapo alichukua
mwili.
Ingawa
ni
maneno
Geoffrey. W Bromiley, Historical Theological: An Introduction (T&T Clark: Edinburgh,1979) uk. 72 10
22
yaliyozoeleka sana katika Imani ya Mitume, lakini hapa yana maana sana. Maana yake ni kwamba Yesu alizaliwa kwa uwezo wa Roho Mtakatifu. Kwa hiyo, akachukua mwili wa mwanadamu, huku yeye akiwa na asili ya uungu; kwa hiyo Yesu ana asili mbili tofauti - ya Kimungu na ya Kibinadamu. Katika WCF/8/3 tunasoma kwamba, “Yesu
alipofanyika
mwanadamu,
alitakaswa na kutiwa Mafuta na Roho Mtakatifu zaidi ya kipimo. Katika yeye mna hazina zote za hekima na maarifa, na ndani yake ilimpendeza Baba kwamba utimilifu wote ukae.
Kusudi la Mungu lilikuwa
kwamba Yesu, Mtakatifu, asiye na ila, wala uchafu
wowote,
na
amejaa
neema
na
ukweli, atekeleze jukumu lake la kuwa Mpatanishi na Mdhamini. Yesu hakujifanya mwenyewe kuwa Mpatanishi, bali aliitwa na 23
Baba yake ambaye alimpa nguvu zote na uwezo kamili wa kuhukumu.” Kwa hiyo kazi ambayo Yesu alikuja kufanya duniani si kwamba
alishuka
tu;
kama
wengine
wanavyodhani kwamba Mungu aliposhuka duniani alifanyika kuwa Yesu. Yesu Kristo alijitoa kama dhabihu kwa Mungu mara moja na milele kupitia yule Roho wa milele, alitimiza haki ya Baba yake (Rum 3:25-26). Kwa dhabihu yake, alilipa deni letu, lakini pia alitununulia urithi katika
ufalme
wa
mbinguni
ambao
utadumu milele. Kwa kweli, ilikuwa tu baada ya Yesu Kristo kufanyika mwanadamu ndipo kweli tumeokolewa, na tunaweza kusema "malipo yamekamilika". Lakini hata kabla ya hapo, tangu mwanzo wa ulimwengu, watu wa Mungu wameweza kuona wema na nguvu 24
ya kuokolewa. Hii ni kwa sababu Mungu alifunua wokovu wake kwa watu wake kama ambavyo
tunaambiwa
"Mwanakondoo
aliyechinjwa" tangu mwanzo wa ulimwengu. Kwamba Yeye ni Yeye yule jana, leo, na hata milele. Hata hivyo wokovu kamili tunaupata Kupitia Kristo peke yake, aliyefanyika mwili, ukamilifu wa Mungu duniani.
SURA YA PILI MPANGILIO WA WOKOVU Wokovu tofautitofauti;
hutazamwa katika
kwa
nyakati
wakati
uliopo
mkamilifu inaaminika kwamba wokovu ni tukio
moja mwanzoni mwa maisha ya
Kikristo. Katika wakati uliopo unaoendelea inaaminika kuwa ni mchakato unaoendelea katika maisha yote ya Kikristo. Na katika 25
wakati ujao, wanaona wokovu ni tukio la baadaye.
Erickson
anatupa
kwamba,
“Wakristo
wanasema,
"Sisi
ufafanuzi
wengine
tumeokoka.”
huwa Wengine
wanaona wokovu ukiwa katika mchakato "tunaokolewa." Bado wengine wanafikiria wokovu kama kitu ambacho kitapokelewa baadaye - "tutaokolewa."11 Kwa namna fulani kila kundi liko sawa, cha msingi inategemea
mtu
amesimama
kwenye
upande gani anapotoa tafsiri hiyo. Hata hivyo,
tumeshang’amua
tangu
awali
kwamba wokovu ni kazi ya Mungu, siyo ya mwanadamu, na ugawaji wa nyakati kama huo wakati mwingine unaweza kutusaidia tu katika maisha haya na namna ya kuishi ndani ya wokovu, lakini ukweli, Kristo alikamilisha
kazi
yake
ya
wokovu.
Erickson J. Millard, Christian Theology (3rd Ed) (Grand Rapids: Baker Academic, 2013), 826. 11
26
Je
unafikiri sentensi gani ni sahihi katika nyakati tatu katika uzoefu wako binafsi wa wokovu? Kwa kweli, ukiachilia kwamba wokovu wa mwanadamu ni mpango wa Mungu, mpango
huo
unachukuliwa
kama
mchakato; mchakato huu ama unafanyika mara moja, ama kwa utaratibu maalumu. Mpangilio huu kwa kiratini huitwa “ordo salutis”
au
kwa
kiingereza
“order
of
salvation.” Michakato ya Wokovu Sasa tutazingatia kwa njia gani na kwa utaratibu
gani
faida
za
ukombozi
zinatumika kwa wateule. Cheung anasema kwamba, “baadhi ya faida hizi huanza pale mteule
anapomwamini
Kristo.”12
Kwa
Vincent Cheung, Systematic Theology (Michigan: Zondervan Publishing House, 2003), uk. 265 12
27
maneno
mengine
ni
kwamba
hatuwezi
kujua hakika baadhi ya michakato inaanza kufanyika
lini,
wakati
gani.
Kweli
tumeshajua kwamba Mungu alituchagua tangu asili, lakini hatujui udhihirisho wa uchaguzi huo unaonekana wazi lini. Katika sehemu inayofuata, tutaangalia michakato hii kwa ukaribu zaidi. Muhtasari wazi wa matumizi (application) ya ukombozi ni ule wa Warumi 8:29-30, ingawa lazima pia tutakuwa tunaangalia vifungu kadhaa vya kibiblia ili kupata orodha kamili. Warumi
8:29-30
inasema,
“maana
wale aliowajua tangu asili, aliwachagua tangu asili wafananishwe na mfano wa Mwana wake, ili yeye awe mzaliwa wa kwanza miongoni mwa ndugu wengi. Na wale
aliowachagua
akawaita;
na
tangu
wale 28
asili,
hao
aliowaita,
hao
akawahesabia aliowahesabia
haki; haki,
hao
na
wale
akawatukuza.
Katika fungu hili kuna michakato minne; kuchaguliwa, kuitwa, kuhesabiwa haki na kutukuzwa. kirefomati
Hata
hivyo
wanaongeza
wanazuoni michakato
wa kwa
utaratibu ufuatao:13 Hata hivyo, wanazuoni hao
pia
wanatofautiana
kidogo
katika
upangiliaji wa michakato hii. Tazama mfano katika chati ifuatayo na ubainishe tofauti zake. MCHAKATO REYMOND, L. ROBERT Kuchaguliwa Mapema Kuitwa Kuzaliwa Upya
Reymond, L. Robert, A New Systematic Theology of The Christian Faith (Nashville: Thomas Nelson Publishers 1998), 720-765 13
29
Kuongoka/Kuokoka Kuhesabiwa Haki Kutakaswa Kuhifadhiwa Kutukuzwa MACARTHUR J na MAYHUE Kuchaguliwa Mapema Wito wenye ufanisi Kuongoka/kuokoka Kuhesabiwa haki Kufanywa wana Kutakaswa Uvumilivu wa watakatifu Kutukuzwa
FRAME M. JOHN14
John M. Frame, Salvation Belongs to the Lord: An Introduction to Systematic Theology (New Jersey: P & R Publishing, 2006), 123. 14
30
Kuchaguliwa Kuitwa Kuzaliwa mara upya Kuhesabiwa haki Utakaso Uhakikisho Uvumilivu wa Watakatifu Kutukuzwa
Ukichunguza utagundua
kwa
umakini
kwamba
jedwali
wanazuoni
hilo hawa
hawatofautiani sana. Vipengele ambavyo wanakubaliana
ni;
1)
Kuchaguliwa
2)
Kuitwa 3) Kuhesabiwa Haki 4) Utakaso 5) na Kutukuzwa. Pengine tuchukulie kwamba Reymond,
L.
Robert
anatumia
neno
“kuhifadhiwa” badala ya “Uvumilivu wa Watakatifu.”
Mkanganyiko
upo
katika
“kuzaliwa upya, kuongoka (kuokoka kama 31
ilivyozoeleka), kuhifadhiwa, Uhakikisho, na kufanywa michakato
wana. yote
Nitajaribu
kuifafanua
ambayo
wanazuoni
wamejadili, ingawa mingine nitajadili kwa ufupi sana. Wana Refomati wengi hutumia WCF kama msingi wa kujadili hoja hizi, Ninakushauri upate kitabu hicho. Pamoja na uchambuzi huo, kuna wengine ambao wanaweka mpangilio wa wokovu mpaka hatua kumi. Kwa mfano Wayne Grudem, yeye anapanga hatua kumi kama ifuatavyo:l. Uchaguzi wa Mungu (chaguo la Mungu la watu kuokolewa) 2. Wito wa injili (kutangazwa kwa ujumbe wa injili) 3. kuzaliwa upya (kuzaliwa mara ya pili) 4. Uongofu (imani na toba) 5. Kuhesabiwa haki (haki ya kisheria) 32
6. Kufanywa wana (ushiriki katika familia ya Mungu) 7. Utakaso (mwenendo sahihi wa maisha) 8. Uvumilivu (kubaki Mkristo) 9. Kifo (kwenda kuwa na Bwana) 10. Kutukuzwa (kupokea mwili wa ufufuo) Kwa hakika, huenda mpangilio wa Grudem unapendwa na wanausasa kwa sababu kuna
hatua
ambazo
zimeongezwa.
Mwenyewe anafafanua kwamba “Tunapaswa kutambua hapa kwamba namba 2 hadi 6 na sehemu ya 7 zote zinahusika katika "kuwa Mkristo." Namba 7 na 8 zinafanya kazi
katika
maisha
haya,
namba
9
hufanyika mwishoni mwa maisha haya, na namba 10 hufanyika wakati Kristo anarudi. Ninachoweza
kusema
hapa
ni
kwamba
hakuna mwenye makosa katika mipangilio hiyo. Mambo yote waliyoainisha yanatukia 33
katika maisha ya wokovu wa mwanadamu ingawa hatuwezi kujua ni lini na katika hali gani.
SURA YA TATU KUCHAGULIWA MAPEMA NA KUITWA a. Kuchaguliwa Kwa sababu wale aliowajua tangu asili, aliwachagua
tangu
awali,
afanane
na
mfano wa Mwanawe, ili yeye awe mzaliwa wa kwanza kati ya ndugu wengi. na wale aliowateua aliwaita;
na
tangu
mwanzo,
hao
pia
wale
aliowaita,
hao
pia
aliwatangaza kuwa waadilifu. na wale 34
aliowatangaza kuwa waadilifu, hao pia aliwatukuza.15 Wanazuoni wa Kirefomati na wale wa Kimatengenezo
wanakubaliana
kuhusu
hatua hii ya mwanzo kabisa ya wokovu wa mwanadamu. Ni mojawapo ya hoja muhimu sana katika soteriolojia ya Kibiblia kwa sababu
usipoelewa
“kuchaguliwa unaweza mingine, kujikuta
mapema”
kushindwa na
vizuri basi
yamkini
kuelewa michakato
matokeo
umeingia
kuhusu
yake
katika
unaweza
mikanganyiko
mikubwa.” Kabla hatujaendelea ningependa kukushauri chochote sababu
tu
kwamba, kuhusu
mafundisho
usisome
kitabu
“soteriolojia” ya
kwa
Arminianism16
Tafsiri yangu kutoka “Young Literal Translation Bible.” Arminianism ni tawi la Uprotestanti linalotegemea maoni ya kiteolojia ya mwanateolojia wa Uholanzi Jacobus Arminius (1560-1609) na wafuasi wake wa kihistoria wanaojulikana kama Remonstrants. 15 16
35
yametapakaa nitakuwa
makanisani.
sahihi
mafundisho
Huenda
nikisema
mengi
kwamba
ambayo
huwa
ninayasikia makanisani kuhusu wokovu yameegemea
kwenye
Arminianism.
Sitakuwa
kujadili
upinzani
mlengo na
wa
wa
muda
wa
Arminianism
kihistoria. Katika
Maandiko
Matakatifu
kuna
maeneo mengi ambayo yanaonyesha Mungu aliwachagua watu kwa kazi fulani au kazi maalumu. Kwa mfano aliwachagua watu kwa
ajili
ya
uongozi
maalumu,
mfano
alivyomchagua Musa kuwaongoza wana wa Israeli, huu nao ulikuwa ni uchaguzi wa Mungu 2:23).
(Hes. Vilevile
16:5-7), Mungu
Zerubabeli,
(Hag.
alichagua
kabila
fulani kwa ajili ya kazi maalumu, kwa ajili ya huduma fulani. 36
Tunapokuja kwenye Agano Jipya, tuna maandiko mengi sana ambayo yanaonyesha kwamba Mungu amewachagua watu kwa ajili ya wokovu. WCF/3/2/ inasema “ili kudhihirisha
utukufu
wake,
Mungu
amewachagua watu wengine (na malaika) kwa uzima wa milele na kwamba wengine amewachagua kwa kifo cha milele.” (1 Tim 5:21, Mt 25:31,41, Mdo 13:48, Rum 8:2930, Yn 10:27-29, Mk 8:38, Yud 6. Rum 9:22-23, Efe. 1:5-6, Mith 16:4, Mt 25:41, Yud 4). Fundisho
hili
kuchaguliwa”
(kwa
predestination) mstakabari mbinguni
linaitwa
ambapo
wetu ama
wa
“kutangulia kiingereza,
Mungu
aliamua
maisha;
kwenda
kuzimu
hata
kabla
hatujazaliwa. Mungu amechagua wengine kuokolewa, na wengine ameruhusu kuvuna 37
matokeo ya dhambi zao. Huu ni uchaguzi usio na masharti; kwa maana ya kwamba anayechaguliwa hajafanya jambo lolote lile la kumpendeza Mungu, bali Mungu, kwa hiari yake mwenyewe bila kulazimishwa na matendo ya mtu anayechaguliwa. Mara nyingi
udhihirisho
wa
uchaguzi
huu
hujidhihirisha kwa njia ya huduma ya Roho Mtakatifu
kupitia
Neno
la
Mungu
linalohubiriwa. Wale
ambao
wamechaguliwa,
si
kwamba wamechaguliwa kwa sababu ya imani yao, na wala si kwa sababu ya matendo
yao
kwamba
Mungu
amewachagua, bali ni kwa sababu ya uhuru wake mwenyewe kwa jinsi alivyoamua bila kuingiliwa na kiumbe ambacho amekiumba. Katika hili wengi huuliza “imani” ina kazi gani sasa? Ama kwa hakika imani ni 38
matokeo ya uchaguzi wa Mungu ambao hautegemei mwenyewe. kisoteriolojia
mwanadamu, Katika
bali
Mungu
muktadha
tunamwamini
Kristo
wa kama
matokeo ya kile ambacho Kristo amekifanya katika maisha yetu. Uchaguzi wa Mungu kwa ajili ya wokovu ni “uchaguzi usio na vigezo”
(unconditional
election).
Warumi
9:10-13 inasema: Wala si hivyo tu, lakini Rebeka naye, akiisha kuchukua mimba kwa mume mmoja, naye ni Isaka, baba yetu, (kwa maana kabla hawajazaliwa
wale
watoto,
wala
hawajatenda neno jema wala baya, ili lisimame kusudi la Mungu la kuchagua, si kwa sababu ya matendo, bali kwa sababu ya nia yake aitaye), aliambiwa hivi, Mkubwa atamtumikia mdogo. Kama ilivyoandikwa,
39
Nimempenda
Yakobo,
bali
Esau
nimemchukia. Ingawa wote wawili Yakobo na Esau walikuwa wazao wa asili wa Isaka, Mungu aliwatendea mdogo
tofauti
kuliko
kwa
mkubwa.
kumpendelea Uamuzi
huu
haukutegemea "chochote kizuri au kibaya" ambacho
walikuwa
wamefanya,
lakini
ilikuwa ili kusudi la Mungu katika uchaguzi lisimame.
Chaguo
hilo
halikuwa
na
masharti, ikimaanisha kwamba haikuwa kwa matendo ilikuwa kwa Yeye mwenye kuita. Yakobo alipendelewa kwa sababu ya mapenzi makuu ya Mungu, sio kwa sababu ya kitu ambacho alikuwa amefanya au angefanya; Chaguo la Mungu lilikuwa huru kabisa. Luther anasema kwamba, “Mungu anaona mapema, anakusudia, na hufanya vitu vyote kulingana na mapenzi Yake 40
yasiyoweza kubadilika, ya milele na yasiyo na makosa."17 Katika "Maana yeye
Warumi
amwambia
Musa,
nimrehemuye,
nimhurumiaye.” hitimisho
9:15
tunasoma, Nitamrehemu
nitamhurumia
Mstari
wa
linalodhihirisha
16
yeye
unatoa
mamlaka
ya
Mungu ya kuchagua, “Basi, kama ni hivyo, si katika uwezo wa yule atakaye, wala wa yule apigaye mbio; bali wa yule arehemuye, yaani, Mungu.” Paulo anasema kwamba Mungu alituokoa kwa sababu ya kusudi na neema yake mwenyewe, sio kwa sababu yoyote wala hali yoyote ambayo aliona ndani yetu. Fundisho
hili
halitoki
kwa
John
Calvin, kama wapinzani wa fundisho hili Martin Luther, The Bondage of the Will; (Grand Rapids, Michigan: Fleming H. Revell, 2000) 80. 17
41
wanavyodai, bali linatoka kwenye Biblia. Neno "tangu asili aliwachagua” ndiyo haswa “kutangulia
kuchaguliwa"
linapatikana
katika Warumi 8: 29,30 na Waefeso 1: 5,11. Maneno
"wateule"
na
"uchaguzi"
yametumika mara 14 katika Agano Jipya. Wazo la udhibiti wa Mungu kuhusu wokovu wa
wenye
dhambi
linapatikana
katika
vifungu mbalimbali vya Biblia (Mt. 24:22; Mk. 13:27; Rum. 11: 7; II Tim. 2:10; Tito 1: 1; 1 Petro 1: 1; Mdo. 13:48; Yoh.6:37; 10: 27-29; 6:39, 44, 65; (17: 6,9) Dhana potofu kuhusu kuchaguliwa mapema Fundisho hili “kiwepesi sana limekuwa halieleweki
na
linapotoshwa.18
Nitaweka
hoja nne ambazo wapotoshaji wa fundisho hili hudai. 18
Mayhue uk. 505
42
Kwanza,
wanaopinga
fundisho
hili
hudai kwamba kutangalia kuchaguliwa ni “hatma
isiyowajibisha”
(kiingereza
fatalism). Wapotoshaji husema kwamba watu wengine wanataka kuja kwa Yesu lakini
hawawezi
hawajachaguliwa
kwa
sababu
mapema.
Sentensi
mashuhuri inayotumika ni hii "Unaweza, lakini huwezi, utaweza lakini hutafanya hivyo, utahukumiwa ukifanya hivyo, na utahukumiwa ikiwa hutafanya hivyo.” Pili, wanadai kwamba, kama Mungu amewachagua watu wengine kwa uzima wa milele na wengine kwa hukumu ya milele, basi mwenye shida ni yule anayechagua; kwani mchaguliwa hana tatizo lolote. Tatu, ikiwa ni hivyo, basi, hatuhitaji kuhubiri
Injili
ameshachagua
kwa walio 43
sababu wake;
hata
Mungu kama
tukihubiri
haiwezi
kubadilisha
kitu
chochote. Nne, vilevile
ikiwa ni hivyo, basi,
hatuhitaji hata kuomba kwa ajili ya watu ambao hawajaokolewa kwa sababu maombi yetu hayawezi kubadilisha kusudi la Mungu la tangu asili. Majibu kwa dhana potofu Kuchaguliwa
mapema
kamwe
hakuwezi kufuta jukumu la kibinadamu. Waislamu husisitiza “majaliwa ya Mwenyezi Mungu.” Fundisho la majaliwa ya Mungu huondoa
wajibu
kuweka
wajibu
kwa
mwanadamu,
wote
kwa
na
Mungu.
kuchaguliwa mapema haifundishi hivyo, watu
wote
wanapaswa
kuwajibika
dhambi na makosa yao yote.
44
kwa
Pia,
kuchaguliwa
mapema
haifuti
mwito wa watu wote kuitikia Injili na kwamba wajibu wa mwanadamu ni kufanya kile ambacho Mungu ameagiza.
Wito wa
Mungu ni kwa watu wote. (Mt. 11:28). Upendo wa Mungu ni kwa watu wote. (Yn. 3:16). Watu wote wanapaswa kutubu. (Mdo. 17:30). Kuna ahadi kwa wale wanaotii. (Rum 10:13). Maagizo na ahadi za Mungu yanayopatikana katika Maandiko yanabaki palepale
na
mapema.
Katika
tunaangalia
hayatangui
kuchaguliwa
kuchaguliwa
hasa
mapema,
kile ambacho
Mungu
alifanya, amefanya na atafanya kwa maisha ya
mwanadamu;
mwanadamu
na
si
alifanya,
kile
ambacho
amefanya
na
atafanya kwa ajili ya Mungu. Fundisho
hili
linaegemea
kwenye
uhuru wa Mungu wa kufanya kila kitu 45
apendacho kwa wakati wake; na pia wajibu wa mwanadamu hautanguki kwa sababu ya uhuru
wa
Mungu.
Tunakiri
kwamba
fundisho la kuchaguliwa mapema ni gumu kueleweka,
lakini
halifundishwi
na
haimaanishi Biblia.
Si
kwamba kila
kitu
tunaweza kuelewa katika Biblia, bali kwa sehemu tu tunaweza kuelewa. Ni Wateule tu Tunapaswa
kuwa
makini
tunapozungumzia hoja hii ili kutokuleta mkanganyiko kwa wengine. Ninachoweza kubainisha
mapema
hapa
ni
kwamba
wokovu siyo kwa watu wote, ni kwa wateule tu, kwa sababu kamwe dhabihu ya Kristo haiwezi
kufanyika
Vilevile,
hatukubaliani
kwamba
pasipo
wanadamu
na wote
na
ufanisi.
mawazo
ya
wataokolewa
mwishoni (universal salvation) kwa sababu 46
ingekuwa
hivyo,
basi
watu
wengine
wasingefia dhambini. Kwa hiyo wokovu unathibitiwa kwa idadi maalumu ya watu. Kwa hiyo ni sahihi kusema kwamba Kristo alikufa kwa ajili ya Wateule, si watu wote. Najua unaweza kushangaa! Biblia inasema, “kwa maana mwana wa Adamu naye hakuja kutumikiwa, bali kutumika, na kutoa nafsi yake iwe fidia ya WENGI” (Mk. 10:45). Angalia neno hilo, fidia kwa wengi siyo kwa WOTE. Wanaookolewa ni wengi sana sana, lakini pia watu wanaofia dhambini na watahukumiwa adhabu ni wengi. Tunasoma katika WCF/3/5 kwamba, Mungu,
kabla
hata
ya
kuumba
ulimwengu, kulingana na mpango wake wa milele, usiobadilika, na kusudi lililofichika na
mapenzi
yake
mema
amewachagua
baadhi ya wanadamu katika Kristo, ambao 47
amewaamuru kwa uzima na utukufu wa milele.
Amefanya
hili
kwa
rehema
na
upendo wake na kwa sifa ya neema yake ya ajabu, alifanya uchaguzi huu kwa uhuru wake
mwenyewe,
kwa
jinsi
alivyotaka
viumbe vyake viwe. Uteuzi huu hautegemei imani yao au matendo mema au uvumilivu wao,
bali
inategemea
yeye
mwenyewe
Mungu katika uchaguzi wake. Efe. 1:4, 9, 11, 2Tim 1:9, Rum 8:30, 1Thes 5:9, 1 Pet 5:10 Efe. 1:5-6, 12 Rum 9:11, 13, 15-16, Efe. 1:4,6,9, 2 Tim 1:9, Efe. 2:8-9). Katika sehemu inayofuatia, WCF/3/6 inasema, Kwa kuwa Mungu ameamuru Wateule watukuzwe katika yeye, vivyo hivyo, katika kusudi lake la milele na huru kabisa la mapenzi yake, amepanga namna ambavyo uchaguzi huo unatimizwa. Na hivyo, wale 48
waliochaguliwa, katika
wakiwa
Adamu,
wameanguka
wamekombolewa
katika
Kristo. Wameitwa kwa imani kwa Kristo na Roho wake anafanya kazi ndani yao kwa wakati unaofaa, na wamehesabiwa haki, wamefanywa
wana,
wamehifadhiwa
wametakaswa,
na
nguvu
zake
na
kupitia
imani kwa ajili ya Wokovu, Ni Wateule tu, na hakuna
wengine,
wanaokombolewa
na
Kristo, wanaoitwa, wanaohesabiwa haki, wanaofanywa
wana,
wanaotakaswa,
na
wanaookolewa.” Mungu, kulingana na makusudi ya siri ya mapenzi yake mwenyewe, ambayo yeye hutoa au huzuia rehema kwa utukufu wa uweza wake wa kutawala juu ya viumbe vyake, ilimpendeza kutowaita baadhi ya watu wengine na kuwaweka kwa uharibifu na hasira kwa dhambi zao kwa sifa ya haki 49
yake tukufu. Kwa hiyo “maamuzi ya Mungu ni
kutokuwachagua
wengine
na
hivyo
kuwaacha katika uangamivu wa dhambi zao.19 Haishangazi
kuona
kwamba
kuna
idadi maalumu ya watu ambao wataokolewa kwa sababu Mungu ndiye ambaye anajua kila kitu, na kwa hivyo hata watu ambao hatawaokolewa tayari Mungu amekwisha panga. 1 Pet. 2:8b inasema, “wasiliamini nao waliwekwa kusudi wapate hayo.” Watu Mungu,
ambao
hawakuchaguliwa
wanaendelea
na
kufanya
yanayomchukiza Mungu ili wapate hukumu ya haki. Yuda 4 inasema, “Kwa maana kuna watu
waliojiingiza
kwa
siri,
watu
walioandikiwa tangu zamani hukumu hii, Macarthur J & Mayhue, R (Ed) A Systematic Summary of Biblical Truth: Biblical Doctrine (Wheaton, Illinois: Crossway, 2017) uk. 504 19
50
makafiri, wabadilio neema ya Mungu wetu kuwa ufisadi, nao humkana yeye aliye peke yake Mola, na Bwana wetu Yesu Kristo.” Kwa maelezo haya, ningependa kusisitiza kwamba ni dhahiri kabisa kwamba kuna watu ambao Mungu amewakataa, yaani hajawachagua. Grudem anatupa ufafanuzi katika hili kwamba, “amri ya kukataliwa ni chaguo huru la Mungu, lililofanywa katika umilele
uliopita
akichagua
kutoweka
upendo wake wa kuokoa juu yao lakini badala yake akiamua kuwaadhibu kwa dhambi zao...”20 WCF/3/8
inamalizia
kwa
kusema
kwamba, “fundisho hili muhimu na la kushangaza
la
kuchaguliwa
na
Mungu
lazima lishughulikiwe kwa busara sana, ili
Wayne Grudem, Systematic Theology (Grand Rapids: MI: Inter-Varsity Press 1994),678. 20
51
kutii mapenzi ya Mungu yaliyofunuliwa katika neno lake, watu wengine wanaweza kuwa
na
hakika
kuwa
wamechaguliwa
milele kutoka kwa ukweli wa wito wao wenye ufanisi. Kwa njia hii, fundisho la uchaguzi wa Mungu
litazidi kuwafanya
watu wamsifu Mungu na kuendelea kuwa wanyenyevu na kutii Injili.” Kwa fundisho
yeyote
ambaye
ameshaelewa
hili na kupokea moyoni kwa
kuamini kwamba wokovu wake si kwa sababu yake mwenyewe, bali Mungu pekee amemteua kwa ajili ya kupokea wokovu huo,
basi
atakuwa
na
sababu
ya
kumshukuru Mungu, na kuwa mtu mwenye wivu zaidi kwa ajili ya kazi ya Mungu. Hata hivyo,
kwa
fundisho
yeyote hili,
ambaye anaweza
hajaelewa kujikuta
ametumbukia kwenye maisha ya dhambi 52
yasiyo na mfano, na ikionekana hivyo, moja kwa moja ataonesha wazi dalili za kuwa mwana wa upotevu. Kwa chochote
hiyo,
fundisho
kile
ambacho
hili
haliondoi
mwanadamu
anapaswa kufanya katika maisha haya kama
kilivyofunuliwa
katika
Maandiko
Matakatifu; Hakuna mwanya wa kuacha kuhubiri Injili kwa kigezo cha kwamba Mungu amechagua baadhi na kuwaacha baadhi. Kile ambacho Mungu ameagiza katika Maandiko kifanywe. Wakati wote tunapaswa
kutii
kile
ambacho
Mungu
amesema katika neno lake hata kama usipojua sababu za kutii kwake. Hata
hiyo,
tunahubiri
Injili
kama
mwito wa kuwakusanya wateule wa Mungu, sisi hatujui ni nani mteule Yesu alisema, “Kwa maana waitwao ni wengi, bali wateule 53
ni wachache.” (Mat. 22:14). Tunapohubiri ndipo wateule wanaitikia mwito wao. Mungu anavumilia matukio kadhaa kwa ajili ya kuwaokoa
wateule,
“Na
kama
Bwana
asingalizikatiza siku hizo, asingeokoka mtu ye
yote;
lakini
kwa
ajili
ya
wateule
aliowateua amezikatiza siku hizo.” (Mk. 13:20) Maswali fikirishi 1. Je
kuchaguliwa
kunakusaidiaje
mapema
wewe
kutambua
wokovu wako? 2. Je kuna uhusiano gani kati ya “kuchaguliwa
mapema”
“kushikilia
wokovu
na usije
ukakuponyoka.”? 3. Unafikiri kwa nini fundisho hili, pamoja
na
kuwa
54
linafundishwa
vizuri
katika
Biblia
watu
wengi
wanashindwa kuelewa? b. Kuitwa Warumi mchakato
8:30 wa
inatuelekeza kuitwa,
kwenye
“Na
wale
aliowachagua tangu asili, hao akawaita; na wale aliowaita, hao akawahesabia haki; na
wale
aliowahesabia
haki,
hao
akawatukuza.” Mara nyingi wito huu huitwa “wito wenye ufanisi” (effectual calling).
Katika
maisha ya kawaida tunasema kwamba mtu akiitwa
lazima
aitike,
kama
asipoitika
maana yake wito utampita. Hata hivyo, kama lilivyo jina lake kwamba “wito wenye ufanisi”
hakuna
namna
yoyote
ya
kupingana nao, kwa sababu ni wito wenye ufanisi.
Sinclair
B.
Ferguson
anasema
kwamba “kwa kuwa wito wenye ufanisi ni 55
ule ambao matokeo yake yamehakikishwa, sio
kama
"mwaliko"
kwamba
wateule
wanaweza kukubali au kukataa.”21 Grudem anaongezea kwamba “Wito huu wito ni aina ya "wito" kutoka kwa Mfalme wa ulimwengu na una nguvu ambayo inaleta majibu katika mioyo ya watu.”22 John Frame anasema kwamba wakati mwingine wito humaanisha tangazo la injili kwa wote, ambapo Mungu huita au hualika kila mtu amwamini Kristo na kuokolewa (Mt. 20:16; 22:14). Huo wakati mwingine huitwa wito wa injili au wito wa nje. Hayo pia ni mafundisho muhimu ya kibiblia. Lakini sio maana ya wito wenye ufanisi.23 Katika wito wenye ufanisi Mungu hufanya Vincent Cheung, Systematic Theology. 190. Wayne Grudem, Systematic Theology (Grand Rapids: MI: Inter-Varsity Press 1994),961. 23 John M. Frame, Salvation Belongs to the Lord: An Introduction to Systematic Theology (New Jersey: P & R Publishing, 2006), 123. 21 22
56
kwanza
kwetu
kabla
ya
sisi
kuitikia
chochote.24 Sinclair Ferguson anafafanua kwamba, "Yeye anayewaita huunda ndani yao uwezo wa kuitikia ili kwamba katika kitendo cha wito
wake
huwaingiza
katika
maisha
mapya."25 Katika WCF/10/1 tunasoma kwamba, “Mungu huwaita kwa wakati unaofaa wale tu ambao yeye amewaandaa kwa uzima wa milele. Anawaita kwa Neno lake na Roho wake kutoka kwenye hali yao ya asili ya dhambi na kifo ili kuingia katika neema na wokovu kupitia Yesu Kristo. Anawaangazia katika akili zao za kiroho uelewa uokoao wa vitu vya Mungu. Anaondoa mioyo yao ya John M. Frame, Salvation Belongs to the Lord: An Introduction to Systematic Theology. 124. 25 Sinclair B. Ferguson, The Christian Life: A Doctrinal Introduction (Carlisle, Pennsylvania: The Banner of Truth Trust, 1997), 34. 24
57
mawe na huwapa mioyo ya nyama. Yeye huboresha mapenzi yao kwa uweza wake uwezao kuwaongoza kwa yaliyo mema. Na kwa hiyo anawavutia kwa Yesu Kristo. Lakini wanakuja kwa Yesu kwa hiari yao wenyewe,
wakiwezeshwa
na
neema
ya
Mungu. Swali hapa tunalopaswa kujiuliza ni je Mungu
hutoa
wito
wake
kwa
kulenga
wateule tu, au hata watu wengine wasio wateule? Katika kujibu swali hili tunahitaji kujua kwanza ni kwa namna gani Mungu hufanya wito wake na wakati gani. Mungu hutoa wito wake kwa njia ya Neno lake, kwa njia ya mahubiri. Mungu huwaita wateule kawaida kwa njia ya kuhubiri injili. Injili haihubiriwi kwa wateule tu, bali ni kwa kila kiumbe
“Akawaambia,
Enendeni
ulimwenguni mwote, mkaihubiri Injili kwa 58
kila
kiumbe.
ataokoka;
Aaminiye
asiyeamini,
na
kubatizwa
atahukumiwa.
"(Marko 16: 15-16). Kwa hivyo, iwe ni kwa njia ya mahubiri ya mikutano ya Injili, mazungumzo ya kibinafsi, au kwa kusoma vitabu vya kidini na kuguswa na kuweza kuja kwa Kristo. Wito wenye ufanisi ni kwa Wateule tu, ingawa
hata
wale
ambao
si
wateule
wanaweza kuja kwenye nuru kupitia wito wa ujumla. Tunasoma ufafanuzi katika WCF/10/4
kwamba,
“Wengine,
wasio
Wateule, wanaweza kuitwa na huduma ya Neno, na Roho anaweza kufanya kazi ndani yao kwa njia ambazo hufanya kwa Wateule. Walakini, kamwe hawatakuja kwa Kristo na kwa hiyo hawawezi kuokolewa. Katika 1 Yohana 2:19 tunasoma kwamba, “Walitoka kwetu, lakini hawakuwa wa kwetu. Maana 59
kama wangalikuwa wa kwetu, wangalikaa pamoja nasi. Lakini walitoka ili wafunuliwe kwamba si wote walio wa kwetu.” Katika fungu hili, “hawakuwa wa kwetu” maana yake ni watu waliosikia Injili wakaitikia lakini kwa sababu si wateule hawakuweza kuendelea. Na kwa kweli, watu bila kumkiri Kristo
hawawezi
kuokolewa
kwa
njia
nyingine yoyote; Maandiko yanasema, “Wala hakuna wokovu katika mwingine awaye yote, kwa maana hapana jina jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo.” (Mdo. 4:12) haijalishi wanajaribu sana kuishi maisha ya maadili kulingana na uelewa wao wenyewe au kujaribu kufuata sheria za dini nyingine. Kwa hiyo ile dhana iliyozoeleka kwamba “wokovu ni matendo yako” haifai kwa lolote 60
kwa sababu wokovu unapatikana kupitia Kristo peke yake. Ukisema kwamba “wokovu ni matendo tu” jiulize pia kwamba je, Mungu anafaikaje na matendo yako mema (haimaanishi kwamba matendo mema si muhimu, lakini si muhimu kwa kupata wokovu) Wanateolojia
wengine
hutofautisha
kati ya “wito wa nje” na “wito wa ndani” kwa maelezo kwamba wito wa nje unahusu mahubiri ya injili kwa wanadamu wote; kwa wateule na wasio wateule. Wito wa ndani au ambao ndio huitwa “wito wenye ufanisi” ni kazi ya Mungu inayoambatana na wito wa nje ili kusababisha wateule kuja kwenye imani katika Kristo. Kuhubiriwa kwa injili inaonekana kama wito wa nje kwa watu wote, lakini pia inakuwa wito wa ndani kwa wateule. Wito wa nje hutolewa na wahubiri, 61
lakini wito wa ndani ni kazi ya Mungu ambayo hufanyika kwa wateule tu. Na wito huu
wa
ndani
kwa
kawaida
huenda
sambamba na wito wa nje. Kwa maneno mengine, watu “wengi wanaweza kusikia injili katika mazingira fulani, lakini Mungu atasababisha
wateule
tu
kuamini
kile
kinachohubiriwa, wakati huo pia anafanya wagumu wasio wateule dhidi yake.”26 Wito wa nje ambayo ndiyo mahubiri ya umma ni ya muhimu sana kwa sababu pasipo kusikia neno la Mungu hatuwezi kuja kwenye wito wetu. (Rum. 10: 14). Ni njia ya kawaida ambayo Mungu ameichagua kuwatumia watumishi wake kwa ajili ya kuwaita wateule wengine kupokea wokovu wao.
26
Vincent Cheung, Systematic Theology. 191.
62
Wito
wenye
ufanisi
unatuita
sisi
kushiriki katika baraka zote za wokovu: ufalme (1Thes. 2:12), utakatifu (Rum. 1: 7; 1 Kor. 1: 2; 1 The. 4: 7), amani (1 Kor. 7:15), uhuru (Gal. 5:13), tumaini (Efe. 1:18), subira (1 Petro 2: 20-21), uzima wa milele (1 Tim.
6:12).
Mwishowe,
wito
ni
katika
ushirika na Kristo, umoja na Kristo; 1 Wakorintho 1: 9 inasomeka, “Mungu ni mwaminifu ambaye mliitwa na yeye mwingie katika ushirika wa Mwanawe, Yesu Kristo Bwana wetu.” Baraka ya wokovu ni Kristo mwenyewe, na kila kitu yeye hufanya kwa niaba yetu; Kwa hiyo, Paulo anasema katika Wafilipi 3: 7-8, " Lakini
mambo
yale
yaliyokuwa
faida
kwangu, naliyahesabu kuwa hasara kwa ajili
ya
Kristo.
Naam,
zaidi
ya
hayo,
nayahesabu mambo yote kuwa hasara kwa 63
ajili ya uzuri usio na kiasi wa kumjua Kristo Yesu, Bwana wangu; ambaye kwa ajili yake nimepata
hasara
ya
mambo
yote
nikiyahesabu kuwa kama mavi ili nipate Kristo;” Je Mungu hawalazimisha Wateule Kuitikia Wito? Ingawa wengi wanakataa utashi huru wa
mwanadamu,
kwamba
“Mungu
WCF/9/1 amempa
inafafanua mwanadamu
utashi, ambao kwa asili ni utashi huru, yaani
sio
wa
kulazimishwa
au
lazima
kuelekea mema au mabaya (Mt 17:12, Yak. 1:14, Kumb. 30:19, Yn 5:40, 7:17, Ufu 22:17, Mdo 7:51, Yak 4:7.)” Kwa misingi hiyo, Mungu hamlazimishi mwanadamu, bali
hulainisha
utashi
wake
ili
aweze
kupokea au kutokupokea Injili. Kwa hiyo si sahihi
kusema
kwamba 64
Wateule
wanalazimishwa
kuitikia
mwito,
bali
“wanawezeshwa” kuitikia. Katika Yohana 6:44 tunasoma, “Hakuna mtu awezaye kuja kwangu, asipovutwa na Baba aliyenipeleka; nami nitamfufua siku ya mwisho.” Kupitia
Injili
Mungu
hutuambia
katika ukamilifu wa ubinadamu wetu. Kwa kuwa sisi ni wateule, lakini Mungu hatuokoi kama “roboti” bali “kutafuta jibu kutoka kwetu kama watu wazima, kupitia akili zetu,
hisia
zetu,
na
mapenzi
yetu.
Anazungumza na akili zetu kwa kuelezea ukweli
wa
wokovu
katika
Neno
lake.
Anazungumza na mihemko yetu kwa kutoa mwaliko wa kibinafsi, anazungumza na mapenzi
yetu
kwa
kutuuliza
kututaka
kuitikia mwaliko wake kwa hiari yetu.”27
27
Wayne Grudem, Systematic Theology. 964.
65
Kwa
hiyo,
tunaitwa
kupitia
neno
linahubiriwa, na wakati huo Roho Mtakatifu hufanya kazi ya kutufanya kujua dhambi zetu na kutufanya kupokea kwa hiari wito wa
Mungu.
Wakati
mwingine
Mungu
ametumia mazingira kadhaa kwa ajili ya kuwaita wateule; kwa mfano kuna watu ambao walikuwa katika Uislamu, ambao walisoma Biblia peke yao na kugundua ukweli wa Biblia. Wengine walipookoka walisema
kwamba
walitokewa
na
Yesu
Kristo katika ndoto, kwa hiyo hawawezi kupingana na wito wake. Maswali fikirishi 1. Vipi kuhusu watu ambao hawawezi kuonesha mwitikio wao wa wito wao wa nje, na mwishowe wanakufa bila kuonyesha
mwitikio?
66
Kwa
mfano
watoto, au wagonjwa mahututi? Nini ufafanuzi wako kwenye hili? 2. Kama
wokovu
unapatikana
katika
Kristo peke yake, je watu wa Agano la Kale waliokolewaje? Rejea (WCF/8/4)
SURA YA NNE
67
KUZALIWA UPYA NA KUHESABIWA HAKI
a. Kuzaliwa Upya Maana ya kuzaliwa upya: tunahitaji ufafanuzi wa kutosha kuhusu maana ya kuzaliwa upya. Wayne Grudem anasema kwamba, ni “neno la kimaandiko (Yohana 3: 3-8) likimaanisha kazi ya Mungu ambayo kwayo
anatupatia
maisha
mapya
ya
kiroho.”28 Grudem anasema kwamba ni tendo la siri la Mungu, na wakati mwingine huitwa “regeneration.”29 Ni tendo la siri la Mungu kwa sababu linafanyika bila sisi kujua kitu chochote, ni kazi
ambayo
Roho
Mtakatifu
huifanya
katika maisha ya Wateule. Kwa kweli, hakuna jukumu lolote ambalo mwanadamu 28 29
Wayne Grudem, Systematic Theology. 964. Wayne Grudem, Systematic Theology. 670.
68
anaweza kufanya katika tendo la kuzaliwa mara
ya
pili.
kunatangulia
Kuzaliwa kuitwa,
mara
kwa
ya
pili
maana
ya
kwamba mtu hawezi kupokea wito wenye ufanisi ikiwa hajazaliwa mara ya pili. Kwa maneno
mengine
“kuzaliwa
upya”
haimaanishi uongofu kwa ujumla, bali ni ile kazi ya ndani ya Roho Mtakatifu kwa maisha
ya
wateule.
Cheung
anasema
kwamba, “Kuzaliwa upya, au "kuzaliwa mara ya pili," hufanyika kwa kushirikiana na wito wa Mungu kwa wateule wake (1 Petro 1:23; Yakobo 1:18), na huwawezesha kumpokea Kristo kwa imani na toba. Hii inamaanisha
kuwa
kuzaliwa
upya
hutangulia imani; yaani mtu hazaliwi mara ya pili kwa imani, lakini amewezeshwa kuamini
kwa
amemfanya
sababu
upya.
Imani 69
Mungu sio
tayari
sharti
la
kuzaliwa upya; badala yake, kuzaliwa upya ni
sharti
ya
imani.
Sababu
kwa
nini
Wakristo wengine kufikiria kuwa kuzaliwa upya hutokea kwa imani ni kwa kwamba huchanganya maana ya “kuzaliwa upya” na “wokovu” Neno "wokovu" linapotumiwa kwa mwenye dhambi, ni neno la kawaida ambalo linamaanisha idadi ya mambo mengi.”30 Kama
ambavyo
tumejifunza
hapo
nyuma kwamba Mungu amechagua watu kadhaa kwa ajili ya kupokea wokovu. Kristo alikuja duniani kwa ajili ya kulipa la dhambi kwa hawa wateule. Kwa hiyo, ila mteule ameitwa kuamini injili kwa nyakati maalum zilizowekwa na Mungu. Walakini, kwa
kuwa
wateule
wamezaliwa
wenye
dhambi, ndani yao kuna mwelekeo wenye nguvu kuelekea uovu, ambao huwafanya 30
Vincent Cheung, Systematic Theology. 192.
70
wasiweze kuitikia mwito wao, kwa hiyo, Mungu kufanywa upya wenye dhambi na kuwaita. Katika
kuzaliwa
upya,
moyo
wa
mwanadamu hufanywa mwepesi kupokea mapenzi ya Mungu na kuamini neno lake. Biblia inasema habari ya kuokolewa kwa mwanamke mmoja aliyeitwa Lidya. Inasema kwamba
“Mwanamke
mmoja,
jina
lake
Lidia, mwenye kuuza rangi ya zambarau, mwenyeji
wa
akatusikiliza,
Thiatira, ambaye
mcha
Mungu,
moyo
wake
ulifunguliwa na Bwana, ayatunze maneno yaliyonenwa na Paulo.” (Mdo 16:14) Katika kuzaliwa upya, Roho Mtakatifu, “kupitia mahubiri ya Injili huweka uzima wa kiroho kwa mwenye dhambi, akimtoa
71
kutoka kwenye kifo cha kiroho na kumwingiza katika uzima wa kiroho.”31 Yakobo 1:18 inasema, “Kwa kupenda kwake mwenyewe alituzaa sisi kwa neno la kweli, tuwe kama limbuko la viumbe vyake.” Yesu Kristo anatuonyesha jinsi ya kuzaliwa mara ya pili. Katika Yohana 3:3 Yesu anaonyesha umuhimu wa kuzaliwa mara ya pili, “Yesu akajibu, akamwambia, Amin, amin, nakuambia, Mtu asipozaliwa mara ya pili, hawezi kuuona ufalme wa Mungu.” Katika Mstari wa 7-8 anasem, “Usistaajabu kwa
kuwa
nilikuambia,
Hamna
budi
kuzaliwa mara ya pili. Upepo huvuma upendako, na sauti yake waisikia, lakini hujui
unakotoka
wala
unakokwenda;
kadhalika na hali yake kila mtu aliyezaliwa Macarthur J & Mayhue, R (Ed) A Systematic Summary of Biblical Truth: Biblical Doctrine. 585. 31
72
kwa Roho.” Yesu hapa anaonyesha namna tukio
la
kuzaliwa
linavyofanyika, kuonekana
mara
kama
kwa
ya
upepo;
macho,
pili
haliwezi
hata
hivyo
tunaweza kuona matokeo yake. Matokeo ya kuzaliwa mara ya pili ni mtu kupokea Injili, kumpokea Yesu Kristo kuwa Bwana na Mwokozi
wa
maisha
yake.
Nikodemo
hakuelewa, kwa hiyo anauliza katika mstari wa 9, “Nikodemo akajibu, akamwambia, Yawezaje kuwa mambo haya?” Aliona ni mambo ambayo hayawezekani hata kidogo, lakini
Yesu
yanawezekana.
alimwambia Ni
jambo
kwamba la
kiroho,
linalofanywa na Roho Mtakatifu. Matokeo ya wazi kabisa ya kuzaliwa mara ya pili ni kuonyesha matunda ya Roho Mtakatifu, kwa sababu umezaliwa upya. Kwa hiyo ni muhimu matunda ya Roho 73
Mtakatifu
yaonekane,
akiendelea
kufanya
vinginevyo maovu
mtu
yamkini
atakuwa bado hajazaliwa mara ya pili, kwa hiyo ana wokovu feki. Paulo anatusaidia kutambua matunda hayo; “Lakini tunda la Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu, upole, kiasi; juu ya mambo kama hayo hakuna sheria.” (Gal. 5:22-23), na Yesu alibainisha wazi kwamba “Mtawatambua kwa matunda yao. Je! Watu huchuma zabibu katika miiba, au tini katika mibaruti? Vivyo hivyo kila mti mwema huzaa matunda mazuri; na mti mwovu huzaa matunda mabaya. Mti mwema hauwezi kuzaa matunda mabaya, wala mti mwovu kuzaa matunda mazuri. Kila
mti
usiozaa
tunda
zuri
hukatwa
ukatupwa motoni. Ndiposa kwa matunda yao mtawatambua.(Mat. 7:16-20) 74
Maswali fikirishi 1. Je
kuna
ufahamu
mpya
kuhusu
“kuzaliwa mara ya pili” tofauti na ule uliousikia kwenye mahubiri ya Injili? 2. Ni kwa vipi mwanadamu anaweza kushiriki katika “kuzaliwa upya?” 3. Je kuna uwezekano wale waliozaliwa upya wakashindwa kuitikia mwito? b. Kuhesabiwa Haki Wanazuoni wanatofautiana kimpangilio na matumizi ya maneno kuhusu hatua hii. Kwa mfano Wayne Grudem anatumia neno, “Uongofu (imani na toba.)”32 Frame yeye anatumia “imani na toba.”33 Vincent Cheung anatumia neno “kuongoka.”34 Mpangilio wa Macarthur J & Mayhue, unaonesha Wayne Grudem, Systematic Theology. 978. John M. Frame, Salvation Belongs to the Lord: An Introduction to Systematic Theology. 127. 34 Vincent Cheung, Systematic Theology. 193. 32 33
75
kwamba baada ya Kuzaliwa Upya inakuja, “toba.”35 Kwa kuwa hawajafafanua kwa nini wamepangilia hivyo, ni vigumu kujadili mpangilio wao.
Herman Bavinck naye
anatumia neno, “Imani na uongofu.”36 Nisingependa kujadili kwa undani sana tofauti hizo, lakini ninachoweza kusema hapa
ni
kwamba
mambo
yote
haya
yanapatikana katika wokovu. Ili kutatua tofauti ya maneno haya tutatumia neno “kuhesabiwa haki” kama tulivyobainisha kwenye kichwa hicho. Maneno
yanayohusiana
“kuhesabiwa
haki”
ni
na pamoja
neno na
“kuhesabiwa haki kwa imani” au “kuwa na haki. Maneno haya yanatofautiana kwa Macarthur J & Mayhue, R (Ed) A Systematic Summary of Biblical Truth: Biblical Doctrine. 591 36 Herman Bavinck, Reformed Dogmatics (p. 523). Baker Publishing Group. Kindle Edition. 35
76
namna fulani ingawa yanakaribiana sana. Wakristo wamezoea wazo kwamba "wokovu" huja kwa imani, haswa pale wanapopinga wokovu
kwa
matendo.
Ingawa
imani
inatumika kwa kila nyanja ya maisha ya Kikristo, ina umuhimu maalum linapokuja suala la kuhesabiwa haki kwa wateule wa Mungu. Kuhesabiwa haki ni tendo la Mungu ambapo
anaweka
haki
ya
Kristo
kwa
mteule, na anatangaza kwamba mteule huyu ni mwadilifu kwa msingi wa haki ya Kristo.
Katika
WCF/11/1
tunasoma
kwamba, “wale ambao Mungu amewaita, pia amewahesabia haki. Yeye hajaweka haki ndani yao lakini anasamehe dhambi zao na kuwakubali kana kwamba ni waadilifu, sio kwa sababu ya kitu chochote kinachofanya kazi ndani yao au kinachofanywa na wao, 77
lakini kwa ajili ya Kristo peke yake. Mungu hazingatii imani yao; yaani kile kitendo cha kuamini, kama ndiyo haki yao au mwitikio wowote mwingine wa utii kwa Injili kwa upande wao. Badala yake, ameweka utii wa Kristo kwao ambapo wao wanapokea na kupumzika juu ya Kristo na haki yake kwa imani (na imani hii sio yao wenyewe lakini ni
zawadi
ya
Mungu.)”
Kifungu
hiki
kinafafanua vizuri asili ya kuhesabiwa haki. Anaposema “yeye haweki haki ndani yao” maana yake ni kwamba Haki ya Kristo inahesabiwa kwao, si kwamba inawekwa ndani yao. Tunapata
ufafanuzi
katika
WLC/70
kwamba, Kuhesabiwa haki ni tendo la neema ya bure ya Mungu kwa wenye dhambi,(Rum. 3:22, 24-25; 4:5) ambapo katika hiyo husamehe dhambi zao zote, 78
huwapokea na kuwahesabia haki machoni pake; (II Kor. 5:19, 21; Rum 3: 22-25, 2728) siyo kwa kitu walichofanya kwa ajili ya kupokea haki hiyo(Tit. 3: 5, 7; Efe. 1: 7) bali ni kwa utii na utoshelevu kamili wa Kristo (Rum.
4:
6-8;
5:
17-19
na
wao
hupokelewa kwa imani tu.(Mdo 10:43; Gal. 2:16; Fil. 3: 9). Ni
tendo
la
Kimahakama
zaidi;
kwamba Kristo alisimama kama mtetezi wetu, kama wakili wetu. Tulisitahili mauti, lakini
Kristo
alilipa
deni
hilo
pale
Msalabani. Watu wengi hujiuliza, kwani Mungu alishindwa kumwokoa mwanadamu kwa njia nyingine mpaka kuruhusu Yesu afe Msalabani? Jibu litakuwa jepesi kwa upande wa Mungu, kwamba inawezekana Mungu angeweza kutumia njia nyingine, lakini muhimu hapa ni kwamba Mungu 79
katika umilele wake tayari aliandaa wokovu wa wateule kupitia mwanaye Mpendwa Yesu Kristo. Mungu anahukumu dhambi, kile ambacho Kristo alikifanya pale msalabani ilikuwa ni kurithisha haki ya Mungu. Kwa hiyo, WCL/71 ipo sahihi kusema kwamba…kwa sababu Mungu, anakubali kuridhika kwa malipo ambayo yalitolewa na Kristo
yaliyopaswa
waliohesabiwa
haki,
kulipwa Yeye
na
mwenyewe
alijitolea malipo haya kupitia kwa Mwana wake pekee, akaweka haki yake kwao; na hahitaji kitu chochote kutoka kwao ili kuhesabiwa haki isipokuwa imani pekee, ambayo pia ni zawadi kutoka kwake; kwa hivyo kuhesabiwa haki kwao ni kwa neema ya bure. Kuna wazo jipya, lakini si jipya kwa muktadha
wetu,
kwamba 80
tunahesabiwa
haki kwa imani, WCL/71 inasema, Mungu “hahitaji kitu chochote kutoka kwao (kwetu) ili kuhesabiwa haki isipokuwa imani pekee.” Ufafanuzi rahisi ni kwamba tunahesabiwa haki baada ya kuamini kazi ya Kristo pale msalabani, tunapomwamini Yesu Kristo; hata hivyo, sisi hatuna imani kama
hiyo,
na
badala
yake
Mungu
anatupatia imani hiyo, ndiyo maana inaitwa wakati mwingine “imani ya bure.” Imani hii ni tofauti na kile kitendo cha kuamini kwamba leo kutatokea muujiza, ni tofauti na kuomba kwa imani; ni kujenga tumaini ndani ya moyo wako baada ya kuona kwamba huna msaada mwingine wowote zaidi ya Kristo na kuweka tumaini kwake. Imani
ya
kuhesbiwa
haki
wakati
mwingine huitwa “imani iokoayo.” Jambo la muhimu
hapa
ni
kwamba 81
imani
hiyo
inatoka kwa Mungu. Jambo la muhimu siyo kuamini tu, chanzo cha imani hiyo ni nini? Kwa mfano katika Yakobo 2:19 inasema kwamba, “wewe waamini ya kuwa Mungu ni mmoja;
watenda
vema.
Mashetani
nao
waamini na kutetemeka.” Hapa imani si ile ya
kuhesabiwa
haki.
Mapepo
hayawezi
kuhesabiwa haki. WCL/72
ina
maelezo
ya
kujitosheleza
kwamba, “imani ya kuhesabiwa haki ni neema
iokoayo
ambayo
inafanya
kazi
mioyoni mwa wenye dhambi kwa njia ya Roho Mtakatifu, na Neno la Mungu. Kwa hiyo wenye dhambi wanahakikishwa juu ya dhambi zao na hali mbaya na hugundua kuwa wao au mtu yeyote au kitu kingine chochote hakiwezi kuwaondoa katika hali hiyo ya upotevu na kwa hiyo wanatoa uthibitisho kamili kwa ukweli wa ahadi ya 82
Injili; na wanapokea pumziko juu ya Kristo na haki yake kwa kusamehewa dhambi kama
Injili
inavyotuambia,
na
kwa
kukubalika na kuhesabiwa kuwa wenye haki mbele ya Mungu kwa ajili ya wokovu.” Kwa
hiyo
kazi
ya
imani
katika
kumhesabia mtu haki ni “kumstahilisha mwenye dhambi machoni pa Mungu (Gal. 3:11; Rum 3:28) sio kwa sababu ya neema zingine ambazo huongozana na imani kila wakati, au kwa sababu ya kazi nzuri ambazo ni matunda yake, au kana kwamba neema
ya
linalojitokeza
imani, kutoka
au
tendo
kwake,
lolote kwamba
Mungu aliamuru kwa ajili kuhesabiwa haki kwake,
bali
imani
inakuwa
chombo
ambacho hupokea na kutumia Kristo na haki yake.”
83
Je imani ya kuhesabiwa haki inakuwepo kwa muda gani katika maisha ya Mkristo? Je
inakuwa
katika
hali
hiyohiyo
au
hubadilika? Inakuwaje pale mtu anapoanza kuwa na mashaka na wokovu wake, je imani hii inafanyaje kazi kwake? Maswali hayo yanaweza kupata majibu kutoka kwenye WCF/14/1-3 Zawadi ya imani inafanya uwezekano wa
mioyo
ya
Wateule
kuokolewa
kwa
kumwamini Yesu Kristo. Zawadi hii ni kazi ya Roho wa Kristo ndani ya mioyo ya Wateule (Ebr 10:39, 2Kor 4:13, Efe 1:17-20, 2:8, 1Kor 12:3, Ebr 12:2) na inakamilishwa kwa kawaida na huduma ya Neno.( Rum 10:14,17, Mt 28:19-20, 1Kor 1:21) Pia inaongezwa na kuimarishwa kwa Neno, kwa maombi, na kwa utekelezaji wa sakramenti. (1Pet 2:2, Mdo 20:32, Rum 4:11, Lk 17:5, 84
Rum 1:16-17, Mt 28:19, 1Kor 11:23-29, 2Kor 12:8-10, Lk 22:19, Yn 6:54-56, Lk 22:32) Kwa imani hii, Mkristo anaamini kile kinachofunuliwa
katika
Neno
kuwa
ni
ukweli kutoka kwa Mungu mwenyewe.( Yn 4:42, 1Thes 2:13, 1Yn 5:10, Mdo 24:14).) Kwa
imani
hii,
muumini
pia
hutenda
kulingana na Neno la Mungu. Kwa imani hii, Muumini hujitiisha kwa unyenyekevu na kumtii Mungu na maagizo yake anuwai (Rum 16:26, Mt 22:37-40) Yeye hutetemeka mbele za Mungu (Isa 66:2) na anakubali ahadi zake juu ya maisha haya na maisha ya baadaye.( Ebr 11:13, 1Tim 4:8).)Lakini hatua kuu za imani iokoayo ni kukubali, kupokea, na kupumzika juu ya Kristo (Yn 1:12, Mdo 16:31, Gal 2:20, Mdo 15:11.)
85
Imani hii ina viwango tofauti vya nguvu na udhaifu (Ebr 5:13-14, Rum 4:1920, Mt 6:30, 8:10.) Inaweza kushambuliwa na kudhoofishwa mara kwa mara na kwa njia nyingi, lakini inapata ushindi.( Lk 22:31-32, Efe 6:16, 1Yn 5:4-5, 1Kor 10:13) Waamini huimarika na kuwa na uhakika kabisa kupitia Kristo (Ebr 6:11-12, 10:22, Kol 2:2, 2Tim 1:12) ambaye hukamilisha imani yao (Ebr 12:2.) Ili
kila
kumwamini
mtu
aokolewe
Yesu,
anahitaji
“kumwamini
Yesu
kumetumika katika Injili ya Yohana kama kuhesabiwa
haki.”37
Mifano
ifuatayo
inathihirisha kwamba kuamini, ni lazima. Amwaminiye yeye hahukumiwi; asiyeamini amekwisha
37
kuhukumiwa;
kwa
Vincent Cheung, Systematic Theology. 199
86
sababu
hakuliamini
jina
la
Mwana
pekee
wa
Mungu.( Yn. 3:18) Basi wakamwambia, Tufanyeje ili tupate kuzitenda kazi za Mungu? Yesu akajibu, akawaambia, Hii ndiyo kazi ya Mungu, mmwamini yeye aliyetumwa na yeye. (Yn 6:28-29) Lakini hizi zimeandikwa ili mpate kuamini ya kwamba Yesu ndiye Kristo, Mwana wa Mungu; na kwa kuamini mwe na uzima kwa jina lake. (Yn 20:31)
87
SURA YA TANO TOBA NA UTAKASO a. Toba Toba ni nini? Neno toba lina maana ya "kubadili mawazo ya mtu."38 Katika toba, mtenda dhambi huziona dhambi zake kama vile ambavyo Mungu anavyoziona; kama
https://www.gotquestions.org/Kiswahili/toba-nawokovu.html 38
88
mchafu na mwenye kuchukiza, na kuiona hatari kubwa iliyo mbele yake, kwa sababu dhambi zake zinapingana kabisa na asili takatifu na sheria ya haki ya Mungu (WCF/15/2). Wengine huona toba kama “kugeuka” au kuongoka”39 WLC/76 inasema “toba iletayo uzima ni neema iokoayo, ambayo inafanywa na Roho Mtakatifu na Neno la Mungu moyoni mwa mwenye dhambi ambapo mwenye dhambi anahuzunika sana, na anachukia dhambi zake, na kwa hiyo, yeye hubadilika na kumgeukia Mungu, akikusudia na kujaribu kila wakati kutembea naye katika njia zote za utii mpya.” Katika
toba,
utambuzi
wa
mwenye kweli
wa
dhambi dhambi
hufikia yake.
utambuzi wa aina hii hutokea kwa sababu 39
Vincent Cheung, Systematic Theology. 193.
89
Mungu, tayari amekwisha kumzaa mara ya pili na anawezeshwa na Roho Mtakatifu kuzichukia
dhambi
zake
na
kuendelea
kuachana nazo. Tofauti kati ya Kuhesabiwa Haki na Toba ni kwamba katika kuhesabiwa haki, Mungu anaonyesha haki ya Kristo; lakini katika utakaso; Roho wa Mungu husababisha neema, na huwezesha kuitumia. Katika kuhesabiwa haki, dhambi imesamehewa.” Toba haikomei kwenye mhemko tu, bali inahusisha akili, ufahamu na ujuzi wa mtu wa kuweka matumaini yake kwa Mungu. Katika
toba
kuimarika tunaweka
kwa
imani
yetu
Mungu
matumaini
yetu
inaendelea
kwa yote
sababu kwake.
Maarifa au ujuzi ni wa lazima katika toba, kwani haiwezekani kuweka matumaini yetu kwa kitu ambacho hatuna ujuzi wowote 90
nacho. Mungu hutoa ujuzi kama sehemu ya maisha Hutumia
ya
wokovu
mahubiri
wa ya
mwanadamu. neno
lake
ili
kuwavuta watu waje kwake na kutubu dhambi kutoka mioyoni mwao. Huu ni ujuzi wa ajabu ambao ni zao la Roho Mtakatifu. Toba ni ya lazima kwa Wateule kwa sababu hapo ndipo wanapona uchafu wa dhambi zao, hata hivyo si kwa sababu ya toba Mungu anatusamehe dhambi zetu, bali ni kwa sababu ya wingi wa rehema zake; mtu yeyote asijaribu kujisifu. Toba haifanyi sisi tupate wokovu. Hakuna mtu anayeweza kutubu na kuja kwa Mungu, isipokuwa Mungu amvute huyo mtu kwake (Yn 6:44). Matendo
5:31
na
11:18
zinaonyesha
kwamba toba ni kitu ambacho Mungu anatoa - inawezekana tu kwa sababu ya neema
yake.
Hakuna 91
mtu
anayeweza
kutubu,
isipokuwa
Mungu
ampe
toba.
Wokovu wote, ikiwa ni pamoja na toba na imani, ni matokeo ya Mungu kutuvuta kwake,
kuyafungua
kubadilisha
mioyo
macho yetu.
yetu,
na
Uvumilivu
wa
Mungu hutuongoza sisi kutubu (2 Pet. 3:9), kama
ilivyo
wema
wake
(Rum.
2:4).40
Pamoja na ukweli huo, vilevile ni sahihi kwamba bila kutubu kibinafsi tunaweza kukosa matarajio yoyote ya kusahemehewa dhambi zetu, na ufahamu wetu wa kawaida unaweza
kusaliti
WCF/15/3
imani
tunasoma,
yetu. “Ingawa
Katika toba
hairidhishi chochote kwa dhambi na wala haisababishi
msamaha
wa
dhambi(kwa
kuwa msamaha ni tendo la neema ya Mungu katika Kristo) lakini ni muhimu kwa wenye dhambi, na hakuna mtu anayeweza https://www.gotquestions.org/Kiswahili/toba-nawokovu.html 40
92
kutarajia kusamehewa bila toba (Eze 36:3132, 16:61-63, Tit 3:5, Mdo 5:31, Hos 14:2,4, Rum 3:24, Efe 1:7,Lk 13:3,5, Mdo 17:30-31) Katika toba, Muumini hutumia ujuzi wake wa kawaida kutambua dhambi zake; kubwa na ndogo, na hili ni tukio la kukumbuka katika maisha yake, lakini pia ni tukio endelevu ambapo mmoja mmoja hutuba kwa
ajili
ya
dhambi
zake.
Na
hivyo
“Waamini hawapaswi kutosheka na toba ya jumla, badala yake, ni jukumu la kila mtu kujaribu kutubu kila dhambi yake kibinafsi mbele za Mungu (Zab 19:13, Lk 19:8, 1 Tim 1:13,15, Dan 9, Neh 9).” (WCF/15/5) Katika
Biblia,
toba
matokeo
yake
ni
mabadiliko ya tabia. Hiyo ndio sababu ni kwa nini Yohana Mbatizaji aliwaita watu "kuzaa matunda yapasayo toba" (Mat. 3:8). Mtu ambaye kwa kweli ametubu atatoa 93
ushahidi wa maisha yaliyobadilishwa (2 Kor. 5:17.) Toba ya kibiblia ni kubadilisha mawazo
yako
kumgeukia wokovu
kuhusu
Mungu
(Mdo
Yesu
katika
3:19).
Kristo imani
Kugeuka
na kwa
kutoka
dhambi sio fafanuzi sahihi ya toba, lakini
ni
mojawapo
ya
matokeo
ya
kweli, toba iliyoweka misingi yake katika kuelekea kwa Bwana Yesu Kristo. Je maneno haya ni sawa? Kuungama, Kutubu na Kuomba Rehema? Mara nyingi wanazuoni hujaribu kutofautisha maneno haya na kuyafafanua kila moja kwa maelezo yake. Ingefaa tuone ufafanuzi mmojawapo. Kuungama ni sawa na kukiri au kukubali. Kwa
kiingereza
wanasema
“confess.”
Kuungama ni kukiri na kukubali kwa kinywa chako makosa yako uliyofanya. Wengine
husema
kwamba 94
kuungama
dhambi maana yake ni kujuta kwa ajili ya dhambi
ambazo
mtu
ametenda,
huku
wakitofautisha na dhana ya kutubu kwa kudai kwamba kutubu ni pale ambapo mtu ametambua hali yake ya asili. Wanadai kwamba mtu baada ya kuokoka hahitaji tena kutubu bali anapaswa kuungama tu. Maandiko haya yanashadidia hoja hii: 1 YOH. 1:9-10 Tukiziungama dhambi zetu, Yeye
ni
mwaminifu
na
wa
haki
hata
atuondolee dhambi zetu, na kutusafisha na udhalimu hatukutenda kuwa mwetu.
wote.
Tukisema
dhambi,
mwongo Fungu
wala hili
kwamba
twamfanya neno
lake
Yeye halimo
linazungumzia
mtu
ambaye tayari ni Mkristo, lakini kwa sababu ya asili ya dhambi kuna uwezekano wa kutenda dhambi katika maisha haya, na hivyo anapaswa kuungama dhambi zake 95
kila mara. Pia tunasoma katika Mithali 28: 13 Afichaye dhambi zake hatafanikiwa, bali yeye
aziungamae
na
kuziacha
atapata
rehema.” Katika neno “kutubu” mara kwa mara linatumika
kwa
waongofu
wapya.
Kwa
mfano katika Matendo ya Mitume 3:19, “Tubuni basi, mrejee, ili dhambi zenu zifutwe,
zipate
kuja
nyakati
za
kuburudishwa kwa kuwako kwake Bwana.” Hapa
dhambi
inayozungumziwa
ni
ile
dhambi ya asili. Maneno
kuomba
rehema
yawezekana
yakawa ni misamiati yenye kurejelea kitu kilekile cha kutubu na kuungama dhambi. Hata hivyo, katika kuomba rehema inaweza kujumuisha matukio fulani fulani kwa nia ya kuhurumiwa na Mungu. Mara nyingi hutokea hasa pale ambapo matokeo ya 96
dhambi
yamejidhihirisha
katika
maisha
yetu. b. Utakaso WLC/75 inasema “Utakaso ni kazi ya neema ya Mungu, ambapo Wateule wa Mungu, waliochaguliwa kuwa watakatifu kabla ya msingi wa ulimwengu, kwa wakati, kupitia kazi ya Roho Mtakatifu hutumia (apply) kifo na
ufufuko
wa
Kristo
kwa
ajili
yao,
huwafanya upya katika miili yao wote kwa mfano wa Mungu. Hupewa mbegu za toba iletayo
uzima,
na
neema
ziokoazo
zinaongezeka na kuwa na nguvu, kwamba wanazidi kufa kwa dhambi, na kuwa hai katika maisha mapya. Tunasoma
katika
WCF/13/1
kwamba,
“wale ambao wameitwa na kuzaliwa upya wana moyo mpya na roho mpya iliyoundwa ndani yao. Kwa kweli wametakaswa kwa 97
nguvu ya kifo cha Kristo na ufufuo na kwa Neno lake na Roho anayeishi ndani yao. Nguvu ya dhambi inayotawala juu ya mwili wote imeharibiwa, na tamaa za ubinafsi za kidunia
zinazoofishwa.
Wakati
huohuo
uwezo wa kutenda utakatifu wa kweli, ambapo bila huo hakuna atakayemwona Bwana
unaimarishwa
na
neema
zote
ziokoazo.” Wanateolojia hutumia neno Kutakaswa kwa maana mbili; Kwanza utakaso kama tukio la mara moja kwa
Mkristo
kutoka
ambapo
kwenye
kwamba
yeye
dhambi
hatawaliwi
anapumzika
yake
tena
na
ya
asili;
dhambi.
Kwamba hatendi dhambi tena kwa sababu tayari
amekwisha
kutakaswa.
Kwamba
Mungu amemtakasa Mkristo na kumtenga na ulimwengu. Maandiko ya kuthibitisha 98
wazo hili ni pamoja na Yohana 15:3 “Ninyi mmekwisha kuwa safi kwa sababu ya lile neno nililowaambia.” Pili, utakaso kama tukio endelevu, ambapo inahusisha
Mkristo
katika
ukuaji
wa
polepole katika maarifa na utakatifu, ili kwamba baada ya kupokea kuhesabiwa haki,
sasa
anaweza
kukuza
haki
ya
kibinafsi katika fikira na mwenendo wake. Watu wengine hufanya makosa kufikiria kwamba utakaso ni kama kuhesabiwa haki kwa maana ya kwamba ni tendo la Mungu mara la moja ambapo yeye hutufanya watakatifu
kamili
katika
fikira
na
mwenendo, na hii inamaanisha kwamba Wakristo
wa
kweli
dhambi.
99
hawawezi
kufanya
Hata hivyo, ingawa utakaso huanza wakati wa kuzaliwa upya, Biblia inaelezea kuwa ni mchakato wa ukuaji, ili mtu azidi kufikiria na
kutenda
Mungu,
na
kwa hivyo
njia
inayompendeza
aendelea
kila
siku
kufanana na mfano wa Kristo. Na kwa sababu
hiyo,
inakuwa
vigumu
katika
maisha haya kutakaswa kikamilifu kwa sababu
tunaishi
katika
ulimwengu
uliopotoka. WCF/13/2 inasema “…lakini hawawezi kuwa wakamilifu katika maisha haya. Asili ya zamani ya dhambi inajaribu kuthibiti mwili, akili, na roho. Na hivyo vita vya daima na visivyopatana vinaendelea kwa kila Mwamini. Asili ya zamani inajaribu kupingana na Roho, na Roho anapigana kudai mamlaka yake juu ya mwili.” Katika kushiriki
utakaso,
Wakristo
kikamilifu. 100
Katika
wanapaswa matukio
mengine
ya
wokovu,
ushiriki
wa
mwanadamu ni mdogo sana, na pengine tunaweza kusema hamna ushiriki, bali ni kazi ya Mungu asilimia mia; lakini katika utakaso, mwanadamu anapaswa kushiriki. Kuacha
kuishi
kuungama
maisha
ya
siku
ili
kila
dhambi,
na
kutakaswa.
Anapaswa kuelekeza moyo na mawazo yake katika kumtii Mungu kikamilifu. anasema sehemu
“Mkristo yake
anapaswa
katika
utakaso,
Vincent
kuchukua na
kwa
makusudi afanye maisha ya utii kwa Mungu "kwa hofu na kutetemeka."41 Tunasoma katika Wafilipi 2:12-13 Basi, wapendwa wangu, kama vile mlivyotii sikuzote, si wakati mimi nilipokuwapo tu, bali sasa zaidi sana
mimi
nisipokuwapo,
utimizeni
wokovu wenu wenyewe kwa kuogopa na
41
Vincent Cheung, Systematic Theology. 206
101
kutetemeka. Kwa maana ndiye Mungu atendaye kazi ndani yenu, kutaka kwenu na kutenda kwenu, kwa kulitimiza kusudi lake jema.” Kwa maelezo mengine, hata katika juhudi zetu za kumtii Mungu, ni dhahiri kwamba Mungu ndiye hutenda kazi ndani yetu, na si kwa nguvu zetu wenyewe. Utakaso hauwezi kukamilika katika maisha haya kwa sababu ya mabaki ya dhambi iliyo ndani ya kila sehemu yao, na tamaa za “mwili dhidi ya roho;” (WLC/78 na kwa hiyo ni lazima kila siku kutakaswa na Roho Mtakatifu na kuendelea kudumu katika imani yetu kwa Kristo. Kama asemavyo Bakize kwamba “shughuli za ukombozi wa mwanadamu zilikusudiwa ziwe
endelevu”42
na
mojawapo
ya
Leonard Herman Bakize, Ili Niokoke ninahitaji Kanisa (Dar es salaam: EWCP,2019) 29 42
102
mwendelezo
huo
kwa
upande
wangu
ninadhani ni utakaso. Haukamiliki katika Maisha haya. Unaendelea mpaka mwisho wa Maisha yetu hapa duniani. Maswali fikirishi 1. Je,
kwa
kuwa
Wakristo
wametakaswa, je ni wakamilifu? 2. Je, ni watu wanaposema “usijihesabie haki” wana maanisha nini haswa?
SURA YA SITA KUFANYWA WANA Kufanywa wana ni kitendo cha Mungu ambapo huwaingiza wateule katika familia 103
yake, kwa hiyo wanaitwa watoto wa Mungu. katika Yohana 1:12 tunasoma, “Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake.” Labda
pengine
tujiulize
maswali
kadhaa, je wale ambao si wateule hao si watoto wa Mungu? Kuna dhana kwamba watu wote ni watoto wa Mungu. Nasita kukubaliana na dhana hii, ingawa pengine naweza
kukubali
kwamba
watu
wote
waliumbwa na Mungu, lakini linapokuja suala la kuwa wana linapaswa kuchukuliwa kwa upekee sana. Biblia inazungumzia habari ya watu wengine kuwa “wana wa Ibilisi” (Shetani). Maandiko yafuatayo yanathibitisha hoja hii;
104
Mathayo 13:38 “lile konde ni ulimwengu; zile mbegu njema ni wana wa ufalme; na yale magugu ni wana wa yule mwovu.” Yohana 6:70 “Yesu akawajibu, Je! Mimi sikuwachagua ninyi Thenashara, na mmoja wenu ni shetani?” Yohana 8:44 “Ninyi ni wa baba yenu, Ibilisi,
na
tamaa
za
baba
yenu
ndizo
mpendazo kuzitenda. Yeye alikuwa mwuaji tangu mwanzo; wala hakusimama katika kweli, kwa kuwa hamna hiyo kweli ndani yake. Asemapo uongo, husema yaliyo yake mwenyewe; kwa sababu yeye ni mwongo, na baba wa huo.” Matendo 3:10 “akasema, Ewe mwenye kujaa hila na uovu wote, mwana wa Ibilisi, adui wa haki yote, huachi kuzipotoa njia za Bwana zilizonyoka?” 105
1 Yohana 3:10, 12 “Katika hili watoto wa Mungu ni dhahiri, na watoto wa Ibilisi nao. Mtu ye yote asiyetenda haki hatokani na Mungu, wala yeye asiyempenda ndugu yake.”…“si kama Kaini alivyokuwa wa yule mwovu,
akamwua
ndugu
yake.
Naye
alimwua kwa sababu gani? Kwa sababu matendo yake yalikuwa mabaya, na ya ndugu yake yalikuwa ya haki.” Kwa sababu hiyo, ni vigumu kukubali kwamba wasio Wakristo nao ni watoto wa Mungu. Mara nyingi napenda kutumia neno “watu wa Mungu” na wala si “watoto wa Mungu.” Neno “mtoto” au “mwana” lina upekee sana. Mwana ana hadhi tofauti na mtu au kiumbe cha Mungu kinginecho. Biblia inathibitisha wazi kwamba wale waliomwamini Yesu Kristo, yaani wateule wamefanywa kuwa wana wa Mungu, na 106
hivyo wanakuwa na sifa tofauti na wengine. Neno la Mungu linasema “Kwa kuwa wote wanaoongozwa na Roho wa Mungu, hao ndio
wana
wa
Mungu.
Kwa
kuwa
hamkupokea tena roho wa utumwa iletayo hofu; bali mlipokea roho ya kufanywa wana, ambayo kwa hiyo twalia, Aba, yaani, Baba. Roho mwenyewe hushuhudia pamoja na roho zetu, ya kuwa sisi tu watoto wa Mungu; na kama tu watoto, basi, tu warithi; warithi wa Mungu, warithio pamoja na Kristo; naam, tukiteswa pamoja naye ili tupate na kutukuzwa pamoja naye. (Rum. 8:14-17) Hatujui
kwa
hakika
ni
katika
mchakato upi tunafanywa wana, lakini Biblia inathibitisha kwamba kwa kuwa sisi ni Wakristo, basi tu wana, na ndivyo tulivyo. Anasema “Tazameni, ni pendo la 107
namna gani alilotupa Baba, kwamba tuitwe wana wa Mungu; na ndivyo tulivyo. Kwa sababu hii ulimwengu haututambui, kwa kuwa haukumtambua yeye.” (1 Yoh. 3:1) Kwa hiyo, mtu anapookoka anakuwa mwanachama wa familia mbili muhimu; kwanza familia ya Mungu, yaani ile familia ya wateule wa Mungu, kwamba anakuwa na ushirika wa karibu na Mungu wake. Pili, familia ya wapendwa katika Bwana, yaani ule ushirika pamoja na waumini wengine. Mtu hawezi kujitenga na familia yake mpya ya Kikristo pale anapokuwa ameokoka. Ingawa bado ana uhusiano wa damu na ndugu zake, bado uhusiano wa kiroho ambao uko kwa Mungu na ndugu zake wa kiroho. Kupitia ushirika wa Wakristo, Biblia inatuambia
kwamba 108
“Kwa
hiyo
kadiri
tupatavyo nafasi na tuwatendee watu wote mema; na hasa jamaa ya waaminio.” (Gal. 6:10). Katika fungu hili Paulo anaweka mkazo kwa watu kusaidiana, ambapo kwa Wakristo
kipaumbele
cha
kwanza
kinapaswa kuwasaidia Wakristo wengine si vinginevyo. Tuhitimishe mada hii kwa kunukuu WCF/12/1
ambayo
inasema,
“Mungu
anathibitisha kufanywa wana kwa wale wote ambao wamehesabiwa haki kwa ajili ya Mwana wake pekee, Yesu Kristo. Wale waliofanywa wana wanafurahia uhuru na haki za watoto wa Mungu, jina la Mungu limewekwa juu yao, wanapokea Roho wa kufanywa wana, wanaweza kukikaribia kiti cha neema kwa ujasiri, na wamewezeshwa kulia,
Abba,
Baba.
Wamehurumiwa,
wanalindwa, wametengwa, wanarudiwa na 109
Mungu kama baba yao. Hawatupiliwi mbali, Wametiwa
muhuri
mpaka
siku
ya
ukombozi, na kurithi ahadi kama warithi wa wokovu wa milele.
110
SURA YA SABA KUHIFADHIWA, UHAKIKISHO NA KUTUKUZWA a. Kuhifadhiwa Wale ambao wamechaguliwa mapema, wameitwa,
wamezaliwa
wamehesabiwa
haki,
upya
na
kwa
hakika
watavumilia mpaka mwisho. Kwa lugha nyingine wokovu
watu
hao
wao,
kwa
ya
kile
matokeo amekifanya
ndani
hawawezi sababu
wokovu
ambacho yao.
kupoteza ni
Mungu
Ingawa
wao
wanawajibika katika kuamini, hata ile imani haitokani na wao wenyewe. Kwa namna moja au nyingine kusema kwamba mteule anaweza kupoteza wokovu wake ni sawa na kusema kushindwa
kwamba kazi
Mungu yake
anaweza
aliyoianzisha
mwenyewe katika maisha ya wanadamu. 111
Tunaposema mtu hawezi kupoteza wokovu wake hatushadidii hata kidogo Maisha ya dhambi,
kwani
yanaonesha
Maisha
wazi
ya
kwamba
dhambi
mtu
fulani
hajaokolewa au si miongoni mwa wateule wa Mungu. Mteule wa Mungu anapaswa kuishi Maisha ya kumpendeza Mungu. Katika
teolojia
neno
linalojulikana
sana kuhusu kuhifadhiwa ni “uvumilivu wa watakatifu.”
Nimeamua
kutumia
neno
“kuhifadhiwa” kwa sababu linalenga hasa kile
ambacho
Mungu
hukifanya
kwa
wateule wanapokuwa katika maisha ya wokovu.
Tofauti
na
matumizi ya
neno
“uvumilivu wa watakatifu” ambapo mara nyingi Wakristo hudhania kwamba kwa sababu ya uvumilivu wao wanaweza kupata wokovu.
John
Frame
anaona
kwamba
maneno haya mawili hayana tofauti kwa 112
sababu
yanaelekea
kuelezea
kwamba
Mkristo wa kweli hawezi kupoteza wokovu wake.
43
Kuhifadhiwa
humaanisha
kwamba
Mungu ndiye anayeendesha wokovu wa Mkristo, na sio mwamini mwenyewe. Hii haimaanishi
kwamba
Mkristo
anaweza
kuishi maisha yoyote yale yasiyo na wajibu kwa
sababu
Mungu
mwenyewe
ndiye
anayemwendesha. Kwa hiyo siyo wazo la kibiblia kusema kuwa kwa kuwa ni Mungu ambaye hututunza, basi hakuna haja kwetu kufanya kiroho.
bidii Ili
yoyote
tuwajibike
ya
maendeleo
ipasavyo,
ya
Mungu
hutupatia uwezo na ujuzi wa kukua katika maisha yetu ya wokovu.
John M. Frame, Salvation Belongs to the Lord: An Introduction to Systematic Theology (New Jersey: P & R Publishing, 2006), 149 43
113
Kwa
hivyo,
wale
ambao
kweli
wameokolewa, ambao ni wateule wa Mungu, kamwe hawawezi kuanguka katika hali yao ya neema kwa sababu Mungu huwawezesha kuvumilia, lakini pia Mungu huwavumilia mpaka mwisho. Hii inathihirisha kwamba wokovu wa mwanadamu ni tendo la Mungu, na wala si la mwanadamu mwenyewe. Tunasoma katika WCF/17/1 kwamba “wale ambao Mungu amewakubali katika Mwana wake Yesu Kristo, na kwa kweli amewaita na kuwatakasa na Roho wake Mtakatifu, kamwe hawawezi kutoka katika hali yao ya neema. Badala yake, hakika wataendelea katika hali hiyo hadi mwisho na wameokolewa milele.” Uvumilivu
huu
wa
Watakatifu
hautegemei hiari yao lakini kwa amri ya Mungu
ya
uchaguzi 114
isiyobadilika,
inayotokana na upendo wake wa hiari, usiobadilika. Inategemea pia ufanisi wa huduma na maombezi ya Yesu Kristo. Maombezi ya Yesu juu ya ujazo wa Roho Mtakatifu na uwepo wa mbegu ya Mungu inayokaa ndani ya Watakatifu. Inategemea pia
asili
ya
Agano
la
Neema
ambalo
halitanguki. Hizi zote zinathibitisha ukweli wa
kutokubadilika
kwa
uhifadhi
wao.
(WCF/17/2) Walakini,
majaribu
ya
Shetani,
ulimwengu, na tabia zao [Watakatifu] za asili za kimwili, pamoja na kupuuza njia ya kuhifadhiwa kwao, inaweza kusababisha Waamini
kufanya
dhambi
kubwa
na
kuendelea na dhambi hiyo kwa muda. Matokeo yake ni kutokumpendeza Mungu na kumhuzunisha Roho Mtakatifu. Katika hili, baadhi ya matokeo ya neema ya Mungu 115
na faida zake huondolewa kwao, na hivyo wanafanya mioyo yao kuwa migumu, na dhamiri
zao
zinajeruhi,
zinaumiza
na
kuwachukiza wengine, na hivyo kujiletea hukumu ya muda juu yao wenyewe. [Hii haimaanishi kwamba Wateule wanaweza kuondoka katika hali yao ya neema, bali Mungu huwarudi kwa njia mbalimbali, kwa sababu ya maovu yao.] WCF/17/3 Maandiko yanaeleza wazi ukweli wa jambo hili; Wote anipao Baba watakuja kwangu; wala ye yote ajaye kwangu sitamtupa nje kamwe. Kwa kuwa mimi sikushuka kutoka mbinguni ili niyafanye mapenzi yangu, bali mapenzi yake aliyenipeleka. Na mapenzi yake aliyenipeleka ni haya, ya kwamba katika wote alionipa nisimpoteze hata
116
mmoja, bali nimfufue siku ya mwisho. (Yn. 6:37-39) Nami niliaminilo ndilo hili, ya kwamba yeye aliyeanza kazi njema mioyoni mwenu ataimaliza hata siku ya Kristo Yesu. (Fil. 1:6) Nami nawapa uzima wa milele; wala hawatapotea kamwe; wala hakuna mtu atakayewapokonya
katika
mkono
wangu. Baba yangu aliyenipa hao ni mkuu kuliko wote; wala hakuna mtu awezaye kuwapokonya
katika
mkono
wa
Baba
yangu. (Yn. 10:28-29) Kwa maana nimekwisha kujua hakika ya kwamba, wala mauti, wala uzima, wala malaika,
wala
wenye
mamlaka,
wala
yaliyopo, wala yatakayokuwapo, wala wenye uwezo, wala yaliyo juu, wala yaliyo chini, 117
wala kiumbe kinginecho chote hakitaweza kututenga na upendo wa Mungu ulio katika Kristo Yesu Bwana wetu. (Rum. 8:38-39). Kwa sababu hiyo nimepatikana na mateso haya, wala sitahayari; kwa maana namjua yeye niliyemwamini, na kusadiki ya kwamba
aweza
kukilinda
kile
nilichokiweka amana kwake hata siku ile. (2 Tim. 1:12) Bwana ataniokoa na kila neno baya, na kunihifadhi hata nifike ufalme wake wa mbinguni. Utukufu una Yeye milele na milele. Amina. (2 Tim. 4:18) Kwa uchache, mistari hiyo inaonesha namna
ambavyo
mtu
yeyote
ambaye
amemkiri Kristo kwa kweli kutoka moyoni mwake
hawezi
kupoteza
wokovu
kwa
sababu analindwa na Mungu peke yake 118
katika wokovu huo. Fundisho hili halisemi kwamba mtu hawezi kupoteza wokovu ila Mkristo wa kweli hawezi kupoteza wokovu wake. Mkristo wa kweli ni yule ambaye ana "imani ya kweli" (1 Timotheo 1: 5) na inathihirishwa
kupitia
fikra,
mawazo,
mwenendo na usemi wa Mkristo huyo. Fundisho hili halitoi nafasi yoyote ya kutenda dhambi kwa sababu ikiwa mtu atasema kwamba ameokoka, basi ni lazima kuonesha matendo kwa nje. Neno linasema, “mtawatambua kwa matunda yao.” Mtu ambaye
ameokolewa
hadumu
katika
dhambi (1 Yoh. 3: 9). Mtu wa namna hii akitenda dhambi huhuzunika sana moyoni mwake
na
kutubu
haraka.
Ikiwa
mtu
amemkiri Kristo kwa unafiki, mara zote hana maumivu yoyote na dhambi, hutenda dhambi
kwa
kisingizio 119
cha
uhuru
wa
Kikristo. Mtu aliyekiri kinafiki mara nyingi hurudi nyuma na kuanguka haraka wakati wa shida na mateso (Mat. 13:21). Wakati mwingine hata Mkristo wa kweli anaweza kuanguka katika dhambi kubwa, lakini anguko kama hilo kamwe halidumu. Walakini, ikiwa Mkristo kama huyu ataendelea na maisha ya dhambi, hatuna sababu kuamini kukiri kwake kwa imani, na kwa hivyo tunapaswa kumfikiria kama
kafiri.
Na
watu
kama
hawa
wanapaswa kutengwa na kanisa, ikiwa ni pamoja na kufukuzwa kama ikiwezekana ((Mat.18:15-17) Wale ambao wanaanguka kabisa na wanakataa
kutubu
hao
hawajawahi
kuokolewa kwa kweli. Yohana anasema, "Walitoka kwetu.
kwetu,
Maana
lakini
kama 120
hawakuwa
wa
wangalikuwa
wa
kwetu,
wangalikaa
pamoja
nasi.
Lakini
walitoka ili wafunuliwe kwamba si wote walio wa kwetu. (1 Yoh. 2:19). Tunayo mifano kadhaa kwenye Biblia kuhusu watu wanaoonekana kuokoka na baadaye kuanguka moja kwa moja. Kwa mfano Yuda alionekana kumfuata Yesu kwa miaka kadhaa, lakini Yesu anasema, "Je! Mimi sikuwachagua ninyi kumi na mbili? Lakini mmoja wenu ni Ibilisi! "(Yn 6:70). Na mstari waa 64-65 anasema, Lakini kuna wengine miongoni mwenu wasioamini. Kwa maana Yesu alijua tangu mwanzo ni nani wasioamini, naye ni nani atakayemsaliti. Akasema, Kwa sababu hiyo nimewaambia ya kwamba hakuna mtu awezaye kuja kwangu
isipokuwa
amejaliwa
na
Baba
yangu. Kwa hiyo mtu anaweza kuonekana katika njia ya unyofu kwa muda, lakini 121
anguko lake linaweza kuthihirisha unafiki wake, ya kwamba hakukiri kutoka moyoni mwake, na kwmaba hakuwa na imani katika Kristo Yesu. Kwa hiyo WLC/61 inasema, “…Sio kila mtu anayesikia Injili na kuwa mshirika katika kanisa linaloonekana ameokoka,
bali
ni
wale
tu
ambao
ni
washirika wa kweli wa kanisa lisiloonekana. (Yn. 12: 38-40; Rum 9: 6; 11: 7; Mt. 7:21; 22:14)” b. Uhakikisho Uhakikisho
si
miongoni
mwa
michakato ya wokovu lakini ni sehemu ndogo
ya
ufafanuzi
wa
“kuhifadhiwa.”
Kwamba mtu anajua ukweli na uhakika wa wokovu wake. Ningependa kufafanua dhana ya uhakikisho wa wokovu kupitia WCF sura ya kumi na nane kwa kuzingatia sehemu zake zote:122
Wanafiki na wasiozaliwa mara ya pili wanaweza uongo
kujidanganya
na
hisia
wanampendeza
za
Mungu
na
tumaini
mwili na
la
kwamba kwamba
wameokolewa. Walakini hisia zao zitakufa pamoja nao. Wale wanaomwamini kwa kweli Bwana Yesu, wanaompenda kwa dhati na wanajaribu kutembea kwa dhamiri njema mbele yake, wanaweza kuwa na hakika katika maisha haya, kwamba wapo katika hali ya neema. Wanaweza pia kufurahi katika tumaini la utukufu wa Mungu, na hawataona
aibu
kwa
tumaini
hilo.
(WCF/18/1) Uhakikisho huu haujaegemea katika tumaini la kubahatisha au kukisiakisia tu. Na badala yake, ni uhakikisho usiotanguka wa imani iliyowekwa juu ya ukweli wa ahadi za
Kimungu
za
wokovu. 123
Pia,
kuna
uthibitisho kiroho,
wa
ndani
ambao
wa
ufahamu
tumepewa
na
wa
Mungu,
ambapo ahadi hizi zinatimilizwa. Na kuna ushuhuda wa Roho wa kufanywa watoto, akishuhudia pamoja na roho zetu kwamba sisi ni watoto wa Mungu. Roho huyu ndiye kiapo cha urithi wetu. Kwa yeye tumetiwa muhuri
mpaka
siku
ya
ukombozi.
(WCF/18/2) Uhakikisho
huu
usiotanguka
sio
muhimu sana kwa imani, kwani Mwamini wa kweli hawezi kuwa na mashaka na migongano juu uhakikisho huu, wakati mwingine
hungoja
kwa
wakati
mpaka
uhakikisho huo utakapokua ndani yake [Hoja hapa ni kwamba kama binadamu, haimaanishi kwamba uhakikisho ni sehemu ya imani. Mtu anaweza kuwa na mashaka na
migongano
ya
kiimani 124
ndani
yake.
Wakati mwingine anaweza kujiona kama hayuko salama, lakini kitu cha muhimu ni kwamba anakua katika uhakikisho huo mpaka kurudi kwa Kristo]. Lakini kwa kuwa Roho huwawezesha Waamini kujua vitu walivyopewa na Mungu kwa bure, kila Mwamini anaweza kujawa na uhakikisho kamili wa wokovu na kazi ya kawaida ya Roho pasi na ufunuo usio wa kawaida. Kwa hiyo ni jukumu la kila Mwamini kujua ukweli wa wito wake na uchaguzi, ili moyo wake ujazwe na amani, furaha katika Roho Mtakatifu, upendo, kumshukuru Mungu, na furaha ya utii, ambayo ndiyo matokeo ya uhakikisho. Uhakikisho hautufanyi tuishi maisha ya dhambi bali kuepuka kuishi maisha ya dhambi ya aina yoyote ile. [Kwa hiyo,
wale
wanaofanya
dhambi
kwa
kisingizio cha uhakikisho wa wokovu wao ni 125
dhahiri
kwamba
bado
wapo
gizani,
wanahitaji mwangaza wa kuona mambo ya kiroho; au labda pengine si Wateule, bali ni waovu walioitikia wito kwa huduma ya Neno,
na
kamwe
hawataokolewa].
(WCF/18/3) Hata Waamini ambao wana uhakika kuwa
wameokolewa
wanaweza
kuyumbishwa [kutikiswa]. Wakati mwingine wanaweza kuwa na uhakika kidogo au kupoteza kwa muda uhakika huu. Hii inaweza
kutokea
kwa
sababu
kadhaa:
kwanza, ikiwa hawajali kuwa wanaweza kuanguka katika dhambi fulani ambazo huumiza dhamiri zao na kumhuzunisha Roho Mtakatifu, pili ikiwa watajaribiwa ghafla, na tatu, ikiwa Mungu ataondoa mwangaza
wa
uwepo
wake
kwao,
na
matokeo yake hata yule anayemwogopa 126
Mungu,
kwa
muda
anaweza
kutembea
gizani. Walakini, kamwe mbegu ya Mungu ndani yao haitoki; yaani maisha ya imani, upendo wa Kristo na upendo wa Waamini wengine, moyo wa dhati na dhamiri ya utii, ambayo kwa hiyo Roho anaweza kufufua tena
uhakikisho
huu
kwa
wakati
ili
wasipotee gizani kabisa (WCF/18/4) c. Kutukuzwa Hatimaye tunafikia tamati ya mpangilio wa wokovu
wa
mwanadamu.
Kwa
kuwa
waumini huvumilia hadi mwisho, baraka yao ya mwisho isiyoepukika ni kutukuzwa. Katika
soteriolojia
ya
Kikristo
wengi
tunaamini kwamba hili ni tukio la baadaye. Ni
tukio
hugawanywa
katika
vipengele
viwili; a) wakati wa kufa b) wakati wa kurudi kwa Bwana wetu Yesu Kristo hapa duniani.
Kwa
upande 127
wangu
naamini
kwamba kipengele cha pili ndicho chenye ufanisi zaidi kuliko kile cha kwanza. Hii inatokana
na
ukweli
kwamba
ingawa
Mkristo anapokufa anakuwa na ushirika na Kristo, hata hivyo ushirika huo haukamiliki mpaka Ufufuo wa wafu. Ufufuo wa wafu ndio
ukamilifu
wa
kutukuzwa
kwa
Wakristo. Katika kutukuzwa, dhambi zinaondolewa kabisa katika maisha ya watakatifu katika hali ya milele (Rum 8:18; 2 Kor.
4:17).
Wakati wa kuja kwa Kristo, utukufu wa Mungu (Rum. 5: 2) -Heshima yake, sifa, ukuu, na utakatifu-vitatambuliwa ndani yetu; badala ya kuwa wanadamu wenye kulemewa
na
tutabadilishwa
asili kuwa
ya
dhambi,
watakamilifu
wasiokufa na tutafurahia ushirika wetu kamili na Kristo milele yote. 128
SURA YA NANE TULIP Ukalviniti kufupisha
kwa
huelezea kutumia
wokovu neno
kwa TULIP
ambayo ni finyazo ya maneno ya Kiingereza. Mara nyingi hujulikana kama hoja tano za 129
Ukavinisti
kuhusu
linawakilisha
hoja
wokovu.
Kila
neno
muhimu;
na
ndiyo
maana wakati mwingine huandikwa pamoja na nukta T.U.L.I.P T-Total depravity (Upotovu Kamili) U-Unconditional
election
(Uchaguzi
usiokuwa na masharti) L-Limited
atonement
(Upatanisho
wenye
Mipaka) I-Irresistible
grace
(Neema
Isiyoweza
Kuzuiliwa) P-Perseverance of the saints. (Uvumilivu wa Watakatifu) T-Total depravity (Upotovu Kamili) Baada Anguko mwanadamu aliingia katika hali ya dhambi. Kwa kweli dhambi imeenea
katika
kila 130
hali:
moyo,
hisia,
mapenzi, akili, na mwili. Hii inamaanisha kwamba
watu
hawawezi
kujitegemea
kumchagua Mungu, kwa sababu sehemu zao zote muhimu za utambuzi zimepotoka kabisa.
Ni
upotofu
kamili,
kwa
hiyo
mwanadamu hawezi kujiokoa mwenyewe. Ni lazima Mungu aingilie kati ili kutatua tatizo hili la dhambi. Ijapokuwa
tunao
ufahamu
wa
kawaida wa uumbaji wa Mungu kupitia vitu vinavyoonekana, bado ufahamu wa namna hii
hauwezi
kumchagua
kutusaidia Mungu.
kumjua
Utashi
huru
na wa
mwanadamu umepotoshwa, na hivyo mara zote huelekea maovu. Hata matendo mema ya mwanadamu hayasaidii kitu chochote kwa
sababu
nayo
yamepotoka.
anahitajika kuingilia kati tatizo hili.
131
Mungu
Kwa hiyo, ni lazima Mungu afanye kazi yote ya wokovu, kuanzia kuwachagua wale ambao wataokolewa na kuwatakasa katika maisha yao yote hadi watakapokufa na kwenda mbinguni. (Mk. 7: 21-23, Rum. 6:20, 1 Kor. 2:14). U-Unconditional election (Uchaguzi usiokuwa na masharti) Mungu
anachagua
ni
nani
atakayeokolewa bila masharti na vigezo vyovyote.
Kwa
sababu
watu
wamekufa
katika dhambi zao, hawawezi kuwa na mwitikio kwa Mungu. Katika umilele wake Mungu aliwachagua watu fulani kuokolewa. Watu waliookoka wanaitwa Wateule. Mungu huwachagua sio kwa tabia zao kibinafsi au sifa,
lakini
kwa
sababu
ya
fadhili
na
mapenzi yake. Kuchaguliwa katika wokovu hautokani na ujuaji wa Mungu wa nani 132
atakayekuwa na imani katika siku zijazo. (soma ufafanuzi wa kutosha kwenye mada ya kutangulia kuchaguliwa) L-Limited atonement (Upatanisho wenye Mipaka) Upatanisho wenye mipaka ni hoja kwamba Yesu Kristo alikufa tu kwa ajili ya dhambi za wateule. Mara nyingi fundisho hili hupotoshwa kwa kutokujua “ukamilifu wa
dhabihu
ya
Kristo.”
Kristo
alijitoa
dhabihu pale msalabani, na kwa hiyo kwa vyovyote vile dhabihu yake ni kamilifu na inawafanya
kamili
wale
ambao
kwao
imefanyika. Haiwezekani dhabihu ya Kristo ikashindwa kutimiza makusudi yake. Ikiwa tutasema kwamba dhabihu ya Kristo ni kwa watu wote, basi tunahitaji pia kuamini
kwamba
watu 133
wote
duniani
wataokolewa,
na
hapo
tutakuwa
tumetumbukia kwenye dhana ya “wokovu kwa wote” (universal salvation). Kwa hiyo tunasema kwamba Yeyote ambaye Kristo alikufa kwa ajili yake, ni lazima ataokolewa. Na pia ni sahihi kusema kwamba watu wote hawataokolewa;
kuna
wengine
ambao
wataenda motoni, na wengine mbinguni. I-Irresistible grace (Neema Isiyoweza Kuzuiliwa) Neema inamaanisha
isiyoweza kwamba
isiyozuiliwa
Mungu
huwaleta
Wateule wake kwenye wokovu kupitia wito wa
ndani,
ambao
hawana
nguvu
ya
kuipinga. Roho Mtakatifu huwapatia neema mpaka watubu na kuzaliwa mara ya pili. (ufafanuzi kuhusu hoja hii uko katika mada ya kuitwa)
134
P-Perseverance of the saints (Uvumilivu wa Watakatifu) Hoja kwamba
hii
imejikita
wateule
katika
hawawezi
ukweli kupoteza
wokovu wao. Kwa sababu wokovu ni kazi ya Mungu Baba; Yesu Kristo, Mwokozi; na Roho Mtakatifu, kwa hiyo haiwezi kuzuiliwa. Hakuna
ambaye
atapotea,
yuko
Mungu
salama
amemwita
mikoni
mwake
milele. Hata hivyo, wateule hawana nguvu ya kuvumilia mpaka mwisho, ila Mungu ndiye anayevumilia,
sio
watakatifu
wenyewe.
Mafundisho ya Ukalvini juu ya uvumilivu wa watakatifu ni tofauti na teolojia ya Kilutheri
na
wanashikilia
Kanisa kwamba
kupoteza wokovu wao.
135
Katoliki watu
ambao
wanaweza
Vifupisho vya TULIP hupanga hoja tano
za
Ukalvini
kimwendelezo, nyingine.
Kwa
na
kimantiki
kila
mfano
na
hoja
inategemea
ikiwa
wanadamu
wamepotoka kabisa, basi wao hawawezi kuanza
kumwitia
Mungu,
hawawezi
kumchagua Mungu. Mungu lazima awaite watu kwenye wokovu kupitia uchaguzi usio na masharti. Mungu lazima pia atoe njia ya wokovu kwa kifo cha Yesu Kristo. Mungu hufanya wokovu udhihirike kwa wito wenye ufanisi wa Roho Mtakatifu. Anawaweka salama wale waliookolewa ili warithi uzima wa milele ambao amewaahidi.
Hitimisho
136
Wokovu ni zawadi ya Mungu kwa manadamu aliyepotoka. Mwanadamu huyu huipokea zawadi hii kwa imani katika Yesu Kristo na kujitoa ili kusamehewa dhambi. Tunaamini
kwamba
mwanadamu
huhesabiwa haki kwa neema kwa imani na si kwa matendo (Mdo. 13:38-39, Rum. 6:23, Efe. 2:8-10). Tunaamini kwamba wateule wote
wameokolewa
na
wataokolewa
na
kuhifadhiwa salama milele (Rum. 8:1, 3839; Yn. 10:27-30)
137
Marejeleo Bakize,
Leonard
Herman.
Ili
Niokoke
ninahitaji Kanisa (Dar es salaam: EWCP,2019) 29 Bavinck,
Herman.
Reformed
Dogmatics.
Baker Publishing Group. Kindle Edition.
138
Brown,
John.
Systematic
Theology:
A
compendious View of Natural and Revealed Religion (Grand Rapids: Reformation
Heritage
Books,
2002) Bruce Demarest, The Cross and Salvation (Wheaton: Crossway Books, 1997) Charles Ryrie, Basic Theology: A Popular Systematic Guide to Understanding Biblical Truth. Kindle Edition Cheung,
Vincent.
Systematic
Theology
(Michigan: Zondervan Publishing House, 2003) Erickson J. Millard, Christian Theology (3rd Ed)
(Grand
Academic, 2013)
139
Rapids:
Baker
Geoffrey. W Bromiley, Historical Theological: An
Introduction
(T&T
Clark:
Edinburgh,1979) Grudem,
Wayne.
Systematic
Theology
(Grand Rapids: MI: Inter-Varsity Press 1994),678. Hodge, Charles, Systematic Theology – (Vol. III) (Grand Rapids, MI: Christian Classics Ethereal Library,) John M. Frame, Salvation Belongs to the Lord: An Introduction to Systematic Theology (New Jersey: P & R Publishing, 2006) Kunhiyop, Samuel Waje. African Christian Theology
(Kenya:
2012)
140
HippoBooks,
Louis Berkhof, Systematic Theology (Grand Rapids: Eerdmans, 1974) Macarthur J & Mayhue, R (Ed) A Systematic Summary of Biblical Truth: Biblical Doctrine
(Wheaton,
Illinois:
Crossway, 2017) Martin Luther, The Bondage of the Will; (Grand Rapids, Michigan: Fleming H. Revell, 2000) Reymond, L. Robert, A New Systematic Theology of The Christian Faith (Nashville:
Thomas
Nelson
Publishers 1998) Sinclair B. Ferguson, The Christian Life: A Doctrinal
Introduction
Pennsylvania:
The
Truth Trust, 1997) 141
(Carlisle,
Banner
of
142