283 111 2MB
Kiswahili (Swahili) Pages 26 [36] Year 1974
KU Biashara ya Utumwa katika Afrika ya Magharibi WALTER RODNEY
WI UNIVERSITY OF C.
3 18222 00780
CHAMA CHA IJITABU C
HISTORIA ILI
TA
I
BIASHARA YA UTUMWA | AFRIKA MAGHARIBI
CHAMA CHA HISTORIA KIJITABU CHA PILI
TANZANIA
BIASHARA YA UTUMWA KATIKA AFRIKA MAGHARIBI Dk. Walter Rodney Chuo
Kikuu,
Dar-es-Salaam
FOUNDATION
BOOKS
LTD
Kitabu hiki ni tafsiri ya West Africa and the Atlantic Slave Trade Kilichotolewa na East African Publishing House katika 1967 Kimechapwa
na kutengenezwa Kenya
Afriki ya Mashariki
na Foundation Books Ltd N.C.M. House, Tom Mboya Street
S.L.P. 73435, Nairobi, Kenya Jalada
limechorwa
na
K.K. Mwajambia
(C) Dk. Walter Rodney na Chama
cha Historia Tanzania
(O) Jalada Foundation
1974
Books Ltd 1974
utangulizi Ili kumwezesha mwananchi kuifahamu historia yake na jinsi alivyoingiliwa na wageni, ni lazima tuwe na vitabu vilivyoandikwa kwa lugha anayoielewa; yaani lugha ya taifa — Kiswahili. Hii ndiyo sababu iliyotufanya tuvitoe vijitabu hivi kwa lugha hii, ambapo mwanzo tulivitoa kwa lugha ya Kiingereza. Kijitabu hiki ni tafsiri ya kijitabu alichokiandika Dk. Walter Rodney kwa Kiingereza kiitwacho West Africa and the Atlantic Slave Trade na kilichochapishwa 1970 na East African Publishing House. Kwa kusoma yaliyomo humu, mwananchi ataweza kuelewa jinsi bara letu la Afrika pamoja na wakazi wake — Waafrika — tulivyoonewa, tulivyonyanyaswa na tulivyopuuzwa mpaka ikatubidi tuanzishe vita
vya kujikomboa
kifikara, kisiasa, kiuchumi
na kitamaduni.
-
Kijitabu hiki ni cha kwanza kati ya vingi ambavyo Chama chetu kimenuia kuvitoa kwa lugha yetu ya Kiswahili. Tunatumaini kwamba vitasaidia katika ufundishaji wa historia mashuleni na pia katika madarasa ya Kisomo cha Watu Wazima.
Chama
Dar-es-Salaam
Aprili, 1974
I.K. Katoke Katibu wa cha Historia Tanzania
Biashara ya Utumwa
Tukio linalohusu mabara matatu NI LAZIMA daima ikumbukwe kwamba biashara ya utumwa ya Bahari ya Atlantiki ilikuwa ni tukio katika historia ya ulimwengu lililohusu
mabara
matatu
—
Ulaya,
Afrika
na Amerika.
Waliotoka
kusaka watumwa walikuwa Wazungu kutoka kila nchi baina ya Sweden kaskazini na Ureno kusini. Wareno walifika Afrika ya Magharibi muda mfupi kabla ya karne ya kuni na tano. Bila kukawia walianza kuwakamata Waafrika na kuwachukua hadi Ulaya, hasa Ureno na Hispania. Lakini matukio muhimu kabisa yalifanyika katika karne ya kumi na sita, wakati mabepari Wazungu walipotambua kwamba wangeweza
kunyonyea wakapelekwa
kupata faida kubwa sana kwa kutumia jasho la Waafrika
utajiri
wa
Amerika
mabara
ya
ya Kaskazini,
Amerika. Amerika
Hivyo,
Waafrika
ya Kati, Amerika
ya
Kusini na Karibbea kufanya kazi za kitumwa kwenye migodi ya dhahabu na fedha, -na kwenye mashamba makubwa ya mazao kama miwa, pamba na tumbako. Biashara hii chafu ya kuuza wanadamu kwa jumla ilichukua zaidi ya miaka mia nne, maana biashara ya utumwa ya Bahari ya Atlantiki haikukoma mpaka katika miaka ya mwisho ya 1870.
Jinsi Afrika ilivyoyamiwa Mengi yanaweza kusemwa kuhusu namna biashara ya utumwa ya Bahari ya Atlantiki ilivyoratibiwa huko Ulaya, na juu ya faida kubwa iliyokusanywa na nchi kama vile Uingereza na Ufaransa. Mengi pia yanaweza kusemwa kuhusu safari iliyokuwa ya shida na dhiki kutoka Afrika hadi nchi za Amerika kupitia Bahari ya Atlantiki. Waafrika walisongamana kama samaki wa makopo katika majahazi ya kuchukulia watumwa, na kwa ajili hiyo walikufa kwa wingi sana. Na mara tu walipotua upande wa pili wa Atlantiki, walikuwa kwa kweli wamefika kwenye 'Dunia Mpya iliyojaa uonevu na ukatili, ambao walipambana
nao
kishujaa kwa kupigana
na kuasi mara
kwa mara.
Hata hivyo, katika kuitalii historia ya Afrika, ni wazi kwamba ni lazima tujishughulishe kwa makini na upande wa Waafrika wa biashara hii; na Afrika ya Magharibi inastahili kuangaliwa vizuri maana watumwa wengi zaidi katika nchi.za Amerika walichukuliwa kutoka
Afrika ya Magharibi. Wazungu waliofunga safari kwenda Afrika ya Magharibi kutafuta watumwa walizipitia wilaya maalumu za pwani pwani baina ya Senegal na Angola ya kusini. Sehemu nyingine, kama Liberia na Ivory Coast za leo, zilikuwa na bahati maana Wazungu wachache sana walifika huko kununua watumwa. Sehemu nyingine, kama Nigeria ya Mashariki na Angola, daima zilitembelewa na meli za watumwa, nazo zilitoa idadi kubwa ya watumwa. Kwanza, waliokamatwa kufanywa watumwa walichukuliwa miongoni mwa watu waliokuwa wakiishi
karibu karibu na bahari; lakini, kadiri miaka ilivyopita, ilionekana ni lazima kusafiriwe ndani zaidi ili kuipata idadi ya watumwa iliyotakiwa na Wazungu. Mwishoni mwa karne ya kumi na nane, Waafrika wengi walioletwa pwani kuuzwa kama watumwa waliwasili katika hali ya udhaifu na uchovu maana walilazimishwa kwenda kwa miguu maili mia nyingi. Wakati huo, hakukuwa na sehemu yoyote kando kando ya mto wa Niger ambako watu hawakukusanywa ili kupelekwa na kuuzwa kwa Wazungu waliokuwako pwani ya Afrika ya Magharibi. Katika Afrika ya Kati wafanya biashara ya utumwa waliingia ndani sana kutoka pwani ya Angola hadi ikawa wanawasiliana na wafanya biashara kutoka Afrika ya Mashariki. Hivi ndivyo biashara ya utumwa ilivyoivamia Afrika.
Idadi ya Waafrika Waliofanywa
Watumwa
Hakuna anayejua kwa hakika ni Waafrika wangapi waliokamatwa makwao na kuuzwa, lakini imekadiriwa kwamba zaidi ya Waafrika 15,000,000 (milioni kumi na tano) walifika bara la Amerika na visiwa vya Karibbea kwa ajili ya biashara ya utumwa ya Atlantiki. Kwa vile asilimia kubwa ya watu walikufa katika majahazi ya watumwa walipokuwa wakivuka bahari ya Atlantiki, idadi ya waliotoka Afrika ilikuwa ni kubwa kuliko 15,000,000 (milioni kumi na tano). Zaidi ya
hayo, Waafrika wengi waliuawa katika ardhi yao wenyewe walipokuwa wakisakwa kikatili kufanywa watumwa. Kwa hiyo haishangazi kuona kwamba wanahistoria wengi wamekisia kuwa kwa jumla Afrika ya
Magharibi ilipoteza baina ya 40,000,000 (milioni arubaini) na 50,000,000 (milioni hamsini) ya watu wake kwa sababu ya biashara ya utumwa ya Atlantiki. Toka kuwasili kwa Wazungu hadi mwaka 1600, karibu milioni moja ya Waafrika walipakiwa katika majahazi ya watumwa. Wakati huo,
Wareno
walikuwa
ndio wafanya biashara wakubwa
wa utumwa
huko
Afrika ya Magharibi. Ama walipeleka Waafrika Brazil, waliyokuwa wameimiliki, au waliwauza kwa walowezi wa Kihispania huko Meksiko, Amerika ya Kusini, na kwenye visiwa vya Karibbea. Katika karne ya kumi na saba, idadi ya Waafrika ilizidi karibu mara tatu; hali katika karne ya kumi na nane, kiasi cha Waafrika wa Magharibi 7,000,000 (milioni saba) hadi 8,000,000 (milioni nane) walivushwa Bahari ya Atlantiki. Biashara ya utumwa ya Atlantiki ilisimamiwa na kulipiwa na Wazungu. Wadachi waliungana na Wareno kuwa viongozi katika biashara ya utumwa katika karne ya kumi na saba, na katika karne ya kumi na nane Waingereza wakawa ndio wafanya biashara wakubwa kabisa wa utumwa. Wakati biashara ya utumwa ya Atlantiki ilipokuwa imestawi sana katika karne ya kumi na nane, majahazi ya Kiingereza yalibeba zaidi ya nusu ya jumla ya watumwa; sehemu iliyobaki wakagawana Wadachi, Wafaransa, Wareno na Wadenishi. Mnamo karne ya kumi na tisa, kulitokea badiliko jingine kuhusu washiriki walioshika hatamu katika kuinyonya Afrika. Nchi za Ulaya zenyewe hazikujishughulisha sana na biashara ya utumwa, lakini badala yake Wazungu waliolowea Brazil, Kyuba, na Amerika ya
Kaskazini ndio waliosimamia sehemu kubwa ya biashara hiyo. Wakati huo nchi za Amerika zilikuwa zaanza kujipatia uhuru wao kutoka kwa Waingereza, na ikawa taifa jipya la Umoja wa Nchi za Amerika ndilo lililochukua sehemu kubwa kabisa katika miaka hamsini ya mwisho ya biashara ya utumwa ya Atlantiki, kwa kubeba watumwa wengi zaidi kuliko wakati wowote kabla ya hapo.
Siyo biashara; ni ushambulizi wa maguvu Biashara ya utumwa ya Atlantiki ilipoanza pwani ya Afrika ya Magharibi, mtindo wake ulikuwa ni wa Wazungu kuwashambulia wale Waafrika waliokuwa wakiishi karibu na mwambao. Wakati Wareno wa kwanza walipofika pwani ya ile nchi iitwayo Muritania sasa, waliyaacha majahazi yao na kuwawinda Wamagharibi walioishi sehemu hiyo. Kwa kweli, hii haikuwa biashara hata kidogo — ilikuwa ni ushambulizi wa maguvu. Lakini baada ya kuvamiwa kwa ghafula mara chache, Waafrika walioishi mwambao walianza kuwashikia zamu washambuliaji wao wa Kizungu na kujihami kwa nguvu. Baada ya muda mfupi sana, Wareno walikuja wakatambua kuwa uvamiaji haukuwa njia ya salama sana ya kujaribu kupatia watumwa. Licha ya watumwa, Wareno pia walitaka dhahabu na bidhaa nyingine za Afrika, ambazo wangezipata kwa kufanya biashara kwa amani tu. Kwa hiyo, badala ya kuvamia Waafrika, Wareno walionelea heri watoe bidhaa zao za viwandani ili kuwapa moyo Waafrika wabadilishe bidhaa zao (za
nyumbani) na kuleta mateka ya Waafrika wenzao kwenye majahazi ya Kizungu. Si Wareno tu, bali Wazungu wengine wote waliona kwamba, kwa ajili ya manufaa yao wenyewe, hii ilikuwa njia bora kabisa ya kupatia bidhaa Afrika; na kwa njia hii ndipo walipoweza kupata
Waafrika milioni nyingi.
Ngome za kuhifadhia watumwa Ili kufanya biashara huko Afrika ya Magharibi, nchi nyingi sana za pwani. pwani “viwanda kujenga ziliamua zilizohusika Ulaya Magharibi, ya Afrika ya pwani ya kibiashara ya “Kiwanda”, kwa lugha kilikuwa ni mahali ambapo bidhaa za Kizungu na za Kiafrika zilihifadhiwa, chini ya usimamizi wa Mzungu aliyeishi hapo na kufanya biashara. Katika biashara ya utumwa, ilikuwa lazima iwepo hizo Bidhaa daima. bidhaa za Kizungu bohari ya kuwekea hayakuwapo majahazi kama hata watumwa zikibadilishwa kwa bandarini ili kusudi kusiweko kucheleweshwa bure bure wakati jahazi liwasilipo kubeba shehena yake ya watumwa. Wakati huo huo, Wazungu walioishi mwambao kwa madhumuni ya kufanya biashara ya watumwa walihitaji uwa mkubwa na uliokuwa imara wa kuwekea wale Waafrika waliowanunua.
Kiwanda
kama hicho, ambacho madhumuni
yake makubwa yalikuwa ni kuwafungia watumwa ndani, kilikuwa kikiitwa barracoon (barakuni). Pwani pwani ya Afrika ya Magharibi kulikuwa na barakuni nyingi mbaya, zilizokuwa na sifa ya kuweza wakati wowote kutoa shehena ya watumwa kwa kila jahazi lililotia nanga. Kiwanda au barakuni ilikuwa ngome halisi wakati kuta ngumu za nje zilipojengwa, wakati mizinga ilipowekwa kutani na wakati askari walipokodiwa. Kila nchi ya Ulaya ilizifanya ngome zake kuwa kinga dhidi ya washindani wengine wa Kizungu na vile vile Waafrika ambao hawakuwa rafiki zao. Katika karne ya kumi na tano na kumi na sita, ngome nyingi zilijengwa na mataifa mbali mbali ya Ulaya pwani pwani ya Ghana ya leo ili kufanya biashara ya dhahabu ambayo kwayo sehemu hiyo ilijulikana sana hata ikaitwa Gold Coast (Pwani ya Dhahabu). Baadhi ya ngome za Ghana zilizojulikana sana ni Elmina, Avim, Cape Coast Castle na Christianburgh. Zote zilitumiwa zaidi na
zaidi kwa biashara ya utumwa kadiri watumwa walivyozidi kuwa muhimu kwa Wazungu kuliko dhahabu. Katika sehemu nyingi nyingine za Afrika ya Magharibi, ngome zilijengwa na kutumiwa zaidi kwa madhumuni ya biashara ya utumwa ya Atlantiki. Hapa, tunaweza kutaja Goree katika Senegal, Bissau katika Guinea ya Kireno (Guinea
Bissau)
na Whydah
kwenye pwani ya Dahome
ambayo wakati huo
ilikuwa sehemu ya Slave Coast (Pwani ya Watumwa) eti.
Kununua Mapema
badala ya kusaka watumwa kama
mwaka
1448
hivi,
Wareno
waliamua
kufanya
biashara na Waafrika kuliko kujaribu kuwawinda. Huo ndio mwaka walipoijenga Arguin huko Muritania kama 'kiwanda' cha kwanza cha Wazungu katika Afrika ya Magharibi. Kuanzia hapo na kuendelea, Wazungu
kwa
kawaida
waliwanunua
badala
ya
kuwakamata
Waafrika na kuwafanya watumwa. Yaani, karibu kwa muda wote wa biashara ya utumwa ya Atlantiki katika Afrika ya Magharibi (na pia Afrika ya Mashariki), walikuwako Waafrika wengi waliokuwa tayari kuwauza wenzi wao kwa kubadilishana na bidhaa za viwandani za Kizungu kama vile nguo, vyungu na sufuria, shanga na silaha. Isipokuwa Wareno huko Angola, Wazungu hawakwenda bara kuchukua mateka. Kusema kweli, Waafrika wa mwambao waliwazuia Wazungu
kuingia bara, kusudi wao
wenyewe
wawalete
watumwa
na
kupokea bidhaa za Kizungu nyingi iwezekanavyo. Lazima isisitizwe kwamba watawala katika Afrika ya Magharibi walikuwa na mamlaka kamili ya kisiasa wakati wa biashara ya utumwa ya Atlantiki. Hivi ndivyo ilivyokuwa hata katika sehemu ambamo Wazungu walijenga ngome
zao,
kwa
sababu
ngome
hizo
kwa
kawaida
zilijengwa
kwa
ruhusa ya watawala Waafrika, na Wazungu walilazimishwa kulipa kodi kwa kukaa mahali pale. Kwa hiyo, kwa kadiri kubwa, Wazungu waliendesha biashara yao ya utumwa pwani pwani ya Afrika ya Magharibi kwa kufuata masharti yaliyowekwa na Waafrika. Wanahistoria wengine wanafika hadi ya kusema kwamba Waafrika walishikilia sehemu kubwa ya biashara ya utumwa. Wazo la namna hii litafurahiwa na adui yeyote wa Waafrika, na kutumiwa kufunikia ile tabia ya kinyama waliyokuwa nayo Wazungu, kwa kuwatupia Waafrika lawama na jukumu. Na hilo si haki hata kidogo, na kwa hakika ni
upuuzi, kwa sababu (kama nilivyosema hapo juu) yaliyotokea Afrika yalikuwa ni upande mmoja tu wa kisa kizima. Biashara ya utumwa ya Atlantiki iliratibiwa na kulipiwa na Wazungu ambao walikuwa wameshafikia kiwango cha kibepari cha maendeleo yao. Waafrika hawakuwa na mamlaka yoyote juu ya upande wa Wazungu wa biashara hiyo. Mabepari wa Kizungu tu ndio waliokuwa na uwezo huu mahali pengi duniani, nao waliwatumia Waafrika kwa manufaa yao wenyewe. Hata hivyo, kwa Waafrika wanaoichungua biashara ya utumwa ya Atlantiki, moja ya mambo muhimu sana ni kutambua ukweli unaoumiza na usiofurahisha kwamba walikuwako Waafrika waliosaidia na kushirikiana na Wazungu katika kuwatia utumwani Waafrika wengine. Yaani hatuwezi kuchukulia sahali na kusema kuwa Wazungu ndio waliokuwa wadhalimu na Waafrika wadhulumiwa. Mfano wa kufaa unaoweza kumsaidia mtu kuelewa yaliyotokea Afrika ya
Magharibi
katika karne za biashara ya utumwa
unaweza
kuonekana
Afrika leo, ambapo viongozi wengi wanashirikiana na mabeberu wa Kizungu na wa Kiamerika kuinyonya idadi kubwa ya watu wa Afrika. Hapa tunaweza kujaribu kuwatambua wale walioshirikiana na wale
Wazungu waliokuwa wakinunua watumwa. Kama tujuavyo, Waafrika wamegawanyika makabila mengi, na kwa kawaida ndani ya makabila hayo mna migawanyiko mingine midogo midogo, kama vile koo. Walilofanya Wazungu ni kuitumia migawanyiko hii kwa faida yao kwa kuchagua Waafrika gani wawe rafiki zao. Kwa mfano, Wazungu wakiona baadhi mbili za Waafrika zinapigana vita, walikiiunga mkono baadhi moja na kuisaidia ishinde ili wapate mateka. Mara nyingi Wazungu walifanikiwa kupata mateka pande zote mbili. Hili liliwezekana kwa kuwa pande zote zilihitaji bunduki na baruti na risasi ambazo Wazungu waliwapa, na kwa kuwa yalikuwapo mataifa mengi ya Kizungu yaliyokuwa yakishindana yenyewe kwa yenyewe. Kwa hiyo, kabila moja likiweza kuungwa mkono na Wadachi na jingine na Waingereza. Lolote lililotokea, hapakuwa na budi baadhi ya Waafrika wasio na bahati kukamatwa na kupelekwa ng'ambo ya pili ya Bahari ya Atlantiki. Ni wazi kwamba haikuwa kitu kwao kama walipakiwa katika majahazi ya Kidachi au ya Kiingereza. Wazungu walifanya mengi kwa kusudi la kupanda mbegu za uadui baina ya kabila moja la Kiafrika na jingine, na hata baina ya sehemu moja na nyingine ya kabila hilo hilo moja. Hata hivyo, inabidi tuelewe kwamba Waafrika walitambua kuwa waliweza kubadilisha mateka yao kwa faida, na hili lilitosha kuwahimiza kwenda na kupigana vita. Baadhi ya wakati waliendelea kuwashambulia watu waliokuwa wameshapigana nao kabla. Wakati mwingine walianzisha vita vipya, na wakati mwingine wakiweza kuungana na adui zao wa zamani,
ikionekana
kwamba
ni faida kubwa
kufanya
jambo muhimu lilikuwa mabavu. Katika Pwani ya Guinea ya Juu, Wamande, Wasusu,
ndio waliokuwa
watoaji wakuu
hivyo.
Katika
hali hii
kama Wamandinga
wa watumwa
na
kwa Wazungu
mpaka mwishoni mwa karne ya kumi na saba. Hapo walipitwa na Wafulani, waliosilimu na kuwashambulia jirani zao wasio Waislamu. Kusini zaidi, kule ambako sasa ni Ghana, Waakani ndio walioongoza katika kusaka watumwa; na hapo ndipo ilipotokea katika karne ya kumi na nane ile dola ya WaAshante iliyokuwa na nguvu na iliyofanya
biashara ya utumwa, ikawa inayashambulia na kuyatisha yale makabila manyonge ya sehemu hiyo. Hivyo pia ndivyo ilivyokuwa dola ya WaFon iliyotokea Dahome. Huko Kongo na Angola hali ilikuwa ngumu zaidi. Katika nyakati mbali mbali, mataifa mbali mbali yalizuka na kufa, lakini daima kulikuwako angalau taifa moja ambalo Wazungu
waliweza kulitegemea kuwapatia watumwa wakati wote. Kama ilivyokuwa, karibu na kila kabila kuu lililosaka watumwa palikuwa na kundi jingine lililoteseka. Misako ya Wamand e na Wafulani ilikuwa na maana kwamba kabila la Wakissi liliumiz wa mno. Katika Gold Coast (Pwani ya Dhahabu), WaAkani waliwatesa mno WaGa mpaka ikawa hadi leo WaGa huikumbuka biashara ya utumwa ya Atlantiki kama wakati ambapo dunia nzima iliharibiwa. Waliokuwa hawana bahati kabisa kuliko wote ni Wambundu wa kaskazin i wa Angola, ambao walikaribia kufagiwa au kumalizwa kwa mashamb ulio ya jirani zao wa Kiafrika na majeshi ya Kireno.
'Watu wakubwa' wanashirikiana na Wazungu Katika kuwachunguza watu wa Afrika ya Magharibi, hawakuona tofauti baina ya kabila na kabila tu, bali pia watawala na waliotawaliwa. Manahodha wa majahazi ya walikuwa siku zote wakishikilia lazima wafanye biashara
wakubwa” maana
wa nchi ile tu. Walipotaja “watu wakubwa”
ya
wafalme,
machifu,
machifu
wadogo,
Wazungu baina ya watumwa na “watu
walikuwa na majumbe,
mabwanyenye, viongozi wa dini, viongozi wa koo na watu wa namna hii ambao tayari walikuwa na uwezo na vyeo vya maana katika kabila lao. Kwa
kawaida,
watu wakubwa
hawa walitawala kwa manufaa ya
watu wote kwa jumla. Waliendesha haki na kuweka sheria za kuendesha vema shughuli za umma za kiuchumi na za kijamii. Katika mambo ya kidini, walidumisha uhusiano mwema wa wahenga, waliwaombea watu wao uongofu na kuwalinda na madhara ya uchawi. Lakini ilipokuja biashara ya utumwa ya Atlantiki, ilionekana kwamba watawala hao walifanya mambo yao kama tabaka mbali lisilo na huruma na makabwela. Hakika, katika nchi nyingi za pwani ya Afrika ya Magharibi, watawala hawakujali kuwauza raia zao wenyewe kwa Wazungu. Mara nyingi tabaka lilikuwa muhimu zaidi kuliko kabila, kama inavyoweza kuonekana tunapochunguza njia zilizotumiwa kupatia watumwa Afrika ya Magharibi. Vita vilikuwa njia moja kuu ambayo kwayo Waafrika walikamatwa na kuuzwa kama watumwa. Kwa jumla, vita hivi vilifanyika baina ya makabila mawili yaliyojitayarisha vema, ambayo yote yaliongozwa na tabaka la watawala. Lakini watu wengi wa Afrika ya Magharibi waliishi katika jumuiya ziitwazo Umuno, yaani hawakuwa na serikali kuu wala tabaka la watawala. Ni muhimu sana kuwa jumuiya hizi 'zisizo na serikali ya nchi” hazikuwashambulia jirani zao kusudi zipate mateka kwa manufaa ya Wazungu. Hii ina maana kwamba palipokuwa na jumuiya isiyo na tabaka la watawala, Wazungu hawakuwa na mtu wa kushirikiana nao katika biashara ya utumwa.
Tabaka la watawala Waafrika liliongoza mno katika biashara ya utumwa hata likawa mara kwa mara linamzuia mtu mwingine yeyote kufanya biashara na Wazungu; kwa hiyo biashara yote ikawa mikononi mwao. Kwa kuwa biashara ya utumwa ilikuwa ndiyo biashara kubwa ya makabila ya Afrika ya Magharibi, kulizuka wawinda-watumwa wengi. Walifanya kazi katika makundi makubwa makubwa kwa kawaida wakiongozwa na mmoja wa 'watu wakubwa, na waliweka juhudi zao katika kushambulia ili wapate watumwa. Ni wazi kwamba uvamiaji na vita ni mambo yanayohusika na watu wamoja kushambulia wengine, kwa hiyo hapa ukabila ulikuwapo. Pia, ni lazima jelezwe kwamba kwa kawaida lile tabaka la watawala lilimudu kuepa kukamatwa na kuuzwa. Na walipokamatwa waliweza kukombolewa, kwa kuwatoa makabwela badala yao. Kitu kimoja ambacho Wazungu
walijifunza kukiepa huko Afrika ya Magharibi kilikuwa ni kung'oa nanga na bwanyenye wa Kiafrika katika majahazi yao ya watumwa, maadamu bwanyenye huyo hakutolewa na mabwanyenye wenziwe kwa hiari zao. Kitendo kama hiki kiliweza kuhatarisha maisha na mali ya Wazungu katika ile sehemu alikochukuliwa bwanyenye huyo. Kuna mifano iliyokijulikana ya mabwanyenye waliouzwa kama watumwa na kuchukuliwa mpaka ng'ambo ya pili ya Atlantiki, na hata hivyo juhudi zilifanywa kuwaokoa watu hao ili kudumisha uhusiano wa amani na wale watawala wengine wa nchi ya “mtu mkubwa yeyote aliyehusika. Ushahidi unaonyesha kwamba lile tabaka la watawala wa Kiafrika, lililokuwa likiwasaidia Wazungu katika biashara ya utumwa,
halikushughulika sana na maslahi ya raia zao. Kwa mfano, hata kama Chifu fulani angejua kwamba raia zake mwenyewe waliibwa na kuuzwa
na Chifu jirani, asingelalamika asilani, kwa sababu na yeye alitegemea kukamata na kuwauza makabwela wa utawala wa Chifu huyo jirani, na hakutaka mwenziwe alalamike. Wakati mwingine njama za tabaka la watawala hao zilipindukia hapo. Ilijulikana kwamba Wafalme na machifu walikuwa wakishambulia sehemu za kando kando za nchi zao wenyewe wakati wa usiku wakiwauza raia zao wenyewe ili wapate bidhaa za Kizungu. Bila shaka, ilibidi mambo hayo yafanywe usiku ' usiku katika giza ili lile tabaka la watawala lisipoteze heshima kwa raia wao. Na lazima, kwa sababu hii hii, ndiyo ikasemwa kwamba machifu jirani wakati mwingine walikuwa wakikubaliana kwamba kila mmoja aishambulie nchi ya mwenziwe. Hii ina maana kwamba wale makabwela walikidanganywa wadhanie kuwa jirani zao ndio waliokuwa adui zao, ambapo kusema kweli makabwela wote wakidhulumiwa na watawala wote, bila kujali kabila lao.
walikuwa
Kwa hiyo, makabwela ndio waliokuwa wakitolewa mhanga siku zote. Wakikamatwa, hakuna aliyetoka kuwasaidia; na hata kama
waliwatoroka Wazungu kabla ya kuwahiwa kutiwa minyororo katika majahazi ya kubebea watumwa, ilikuwa vigumu sana kuepa kukamatwa tena na wale machifu ambao ilibidi kupita nchini mwao. Jambo lililokuwako ni kwamba watawala wa Kiafrika walifanya mikataba na
wafanya biashara wa Kizungu wakiwahakikishia kwamba watumwa wote watoro watakamatwa na kurudishwa kwa malipo kidogo.
Sheria na dini zinatumiwa
vibaya
Silaha kubwa kabisa ya tabaka la watawala wa Kiafrika ilikuwa ni mamlaka waliyokuwa nayo juu ya mambo ya sheria na dini. Kwa sababu mabwanyenye, machifu na wafalme walikuwa ndio mahakimu na wanasheria katika kesi zote za mahakamani, waliyatumia vibaya mamlaka yao, wakawatia hatiani kwa dhuluma watu wengi ambao baadaye waliuzwa kwa Wazungu. Kesi nyingi zilihusiana na ugomvi juu ya wanawake, na zilijulikana kama 'kesi za wanawake” ambazo zilikuwa pamoja na mashtaka ya uzinzi yaliyokuwa yakipendwa sana wakati wa biashara ya utumwa ya Atlantiki. Bwanyenye aliyekuwa na wake wengi aliweza kwa urahisi kuwafanyia mpango wawavutie wanaume wengine, kisha awashtaki mahakamani. Namna nyingine ya “kesi ya mwanamke ilikuwa ni pale mwanamume fulani aliposhtakiwa kwa kumshambulia mwanamke. Hapa tena, mara nyingi ushahidi wa
uongo ulikuwa ukiletwa na watu wale wale waliotarajiwa kufanya haki.
Aina nyingine muhimu ya kesi ilihusu mambo ya fedha. Mtu aliposhindwa “kulipa deni katika muda alioahidi, iliwezekana mwisho wake akaishia kuwa mtumwa mikononi mwa Wazungu, hata kama bidhaa alizokopa zilikuwa za thamani ndogo. Kwa kweli, watu maskini ndio walioumia kuliko wote kwa vitimbi vya namna hiyo. Shtaka moja ambalo kwalo watu wengi walishtakiwa lilikuwa “uchawi, na hapo ndipo makasisi na viongozi wengine wa dini walipoingia. Po pote mtu alipokufa au alipojeruhiwa katika ajali, uchunguzi ulifanywa na makasisi kuangalia kama mtu huyo alikuwa amelogwa au yeye mwenyewe alikuwa mchawi. Vyo vyote itakavyoonekana - iwe amelogwa au yeye mwenyewe ni mchawi - watu wengi waliuzwa kama watumwa, kwa sababu namna jambo lenyewe lilivyoendeshwa ilikuwa vibaya kabisa. Ikiwa mtu aliyejeruhiwa au aliyekufa alifikiriwa kuwa mchawi, basi ukoo wake wote uliuzwa na kufanywa watumwa. Uamuzi huu ndio uliofuatwa mara nyingi sana wakati kifo kilipotokea kwa ajali, kama kufa maji au kuanguka mtini, kwa kuwa iliaminiwa kwamba vifo vya namna hii vilikuwa ni njia ya Mungu kuwaadhibu wachawi wabaya. Mtu alipokufa kwa amri ya Mungu siku za biashara ya utumwa ya Atlantiki, ilikuwa kwa kawaida ikidhaniwa kwamba mtu mwingine amemloga ili afe. Hapo makasisi
walimchagua yule waliyemdhania kuwa ndiye mwenye makosa hayo, na walimlazimisha anywe maji yenye sumu. Ilikuwa si sana mtu kuishi baada ya kuinywa sumu hiyo; na kifo chake kilichukuliwa kuwa ni ithibati ya makosa yake, kwa hiyo ukoo wake uliuzwa na kufanywa
watumwa. Uchawi kwa kweli ni utumiaji wa mazingaombwe kwa madhumuni ya kumdhuru mtu, na kwa kawaida, ilikuwa ni wajibu wa makasisi wa Kiafrika kuwazuza na kuwaadhibu wale waliokuwa wakifanya uchawi. Waafrika waliamini kwamba inawezekana ajali na vifo kusababishwa na uchawi, na pia waliamini kuwahukumu
hukumu za mateso yote kwa
sumu na moto. Jambo muhimu la kukumbuka ni kwamba mambo kama hayo yalifanywa kwa kiwango kidogo na yalikusudiwa kulinda masilaha na manufaa ya umma. Lakini mila zilizokusudiwa kulindia watu binafsi na watu wote kwa jumla ziliharibiwa wakati wa biashara ya utumwa ya Atlantiki, na watu wengi walishtakiwa kwa uwongo kusudi wauzwe kama adhabu, kwa faida ya watawala. Wakati ukoo mzima ulipohukumiwa kuwa na hatia, kwa mfano, ilikuwa ni kwa ajili ya kuongeza idadi ya watu waliouzwa na jumla ya bidhaa za Kizungu zilizopatikana katika ubadilishaji. Ni kweli kwamba, mbali na athari ya biashara hii ya utumwa, ilikuwa ikiwezekana kuutia hatiani ukoo mzima kwa sababu ya vitendo vya mtu mmoja tu katika ukoo huo. Lakini adhabu kuu ambayo ukoo ungeipata ingekuwa ni adhabu ya aibu. Hapo ingewabidi wawe waangalifu zaidi katika kuwaomba babu zao, kuwacha chakula kwenye makaburi yao na kuiga tabia nzuri kabisa za babu zao na wazee wa ukoo. Kwa hiyo, kuhusika kwa ukoo mzima ilikuwa kwa manufaa yao, na kila mmoja alisaidiwa kuishi maisha mazuri zaidi. Mwafrika kwa kweli hakuwa na maisha zaidi ya
yale ya mtumwa katika Amerika.
Mifano ya sheria na dini kutumiwa vibaya Mifano mingi inaweza kutolewa kuonyesha namna sheria na dini za Afrika ya Magharibi zilivyogeuzwa kutumikia biashara ya utumwa ya Atlantiki, na katika kila mfano kikundi cha watawala (ambacho ni pamoja na makasisi) kilikuwa upande wa Wazungu. Walisahau madaraka yao na wajibu wao kwa watu wao, na badala yake
wakawafanya
watumwa.
Hili linaweza
nchi za Liberia, Sierra Leone
kuonekana
na katika Jamhuri
wazi wazi ya Guinea,
katika ambako
watu wa mwambao walitawaliwa na vyama vya siri vilivyokuwa na nguvu sana. Vyeo vya juu kabisa katika vyama hivyo vilishikwa na mabwanyenye na machifu waliotoka katika falme nyingi, na ambao
kwa kawaida walifanya kazi kwa manufaa ya watu wote kwa jumla. Walikuwa na madaraka juu ya maongozi ya siasa, uchumi, elimu na
10
— a...
OO aaa
dini, na walisimamia mambo
muhimu kama vile kutia jando, kutahiri,
kulinda viapo vya siri na vitu vya dini. Vyama vya siri vilikuwa ndio mahakama kuu ya sheria, ambako hata machifu na mabwanyenye waliweza kupelekwa ili wahukumiwe. Kadiri biashara ya utumwa ilivyoendelea, ndivyo vyama hivi vyenye nguvu na manufaa vilivyopoteza madhumuni yao halisi na, kutwaliwa na machifu waliokuwa wakiwinda watumwa. Mfano mwingine unaojulikana sana wa namna mamlaka ya dini yalivyotumiwa vibaya katika Afrika ya Magharibi kwa sababu ya biashara ya utumwa ya Atlantiki, ni ule wa Walbo wanaoishi kwenye mlango wa mto wa Niger, katika sehemu ambayo sasa inaitwa Nigeria ya Mashariki. Walbo waliishi katika jumuiya zisizo na serikali ya nchi wakati Wazungu walipowasili. Hawakuwa na wafalme au machifu walioweza kuliunganisha kabila au hata sehemu zake kubwa; lakini dini yao ilikuwa moja, na hasa waliuamini sana mzimu mmoja waliouita Chukwu. Walbo na watu wengine wa sehemu hiyo walikuwa wakiuhiji mzimu huo wa Chukwu, na wakiupigia bao kuondoa hitilafu baina yao. Sehemu ndogo ya Walbo inayoitwa WaAro, waliusimamia mzimu wa Chukwu na waliutumia vibaya kuwatilia utumwani maelfu ya wenzi wao. Watu walishtakiwa kwa kuukosea mzimu huo. Kisha wakosaji waliambiwa watoe mhanga wa binadamu kwa Chukwu, lakini hao watu waliowatoa mhanga hawakupewa Chukwu bali waliuzwa kwa Wazungu. Kwa sababu ya biashara ya utumwa, miji mingi ya biashara ilizuka kwenye milango mingi ya mto wa Niger na kingoni kingoni mwake. Watawala wake waliendelea kuwapatia Wazungu watumwa waliopatikana kwa kuutumia vibaya mzimu wa Chukwu, na kwa kutumia nguvu ilipokuwa lazima.
Mapatano ya bei
ji
Njia ambayo Waafrika waliuzwa kwa Wazungu ni kitu tunachokijua sana, kwa sababu Wazungu wengi waliokuweko Afrika ya Magharibi wakati huo walieleza namna walivyonunua watumwa. Pande zote mbili
zilibishana sana bei. Wauzaji Waafrika walitaka bidhaa nyingi za vile vitu Kizungu na hasa walivitaka kadiri ilivyowezekana, walivyodhani ni muhimu sana, kama vile bunduki na baruti. Pia kwa walijitahidi kupata faida ya ziada kwa kila walichouza kung'ang'ania kwamba lazima Wazungu wawape zawadi ya pombe kabla ya kuanza biashara. Hakuna haja ya kusema kwamba Wazungu
nao walikakawana kuziweka bei chini, na kwa jumla walifanikiwa. Kwa
upande mmoja, ni kweli kwamba Wazungu waliwanunua watumwa wao
kwa bei kubwa zaidi wakati wa mwisho mwisho wa utumwa ya Atlantiki kuliko ilivyokuwa katika miaka
biashara ya ya mwanzo
11
mwanzo,
lakini idadi zake daima
zilikuwa
ndogo.
Katika karne ya
kumi na tano na kumi na sita, Wazungu walipata watumwa kwa bei ya chini sana. Kipande kidogo cha nguo mara nyingi kilitosha kulipia mtumwa katika miaka ya mwanzo mwanzo. Mpaka hivi karne ya kumi na nane, Mzungu aliweza kumnunua Mwafrika kwa bidhaaa zenye thamani ya shilingi mia moja na hata chini yake. Na majahazi ya watumwa yalipovuka Atlantiki waliweza kuuza shehena zao kwa bei iliyo mara kumi zaidi ya ile waliyolipa Afrika. Wazungu walihitaji Waafrika wenye afya nzuri kuwatumia kama watumwa. Walitaka vijana wenye umri wa baina ya miaka 15 na 25, na walipendelea zaidi wanaume wawili kwa mwanamke mmoja. Pia ilisemwa kwamba watu wa kabila fulani walipendwa zaidi kuliko watu wa makabila mengine, kwa sababu watu wa baadhi moja walikifanya kazi kwa bidii zaidi kuliko wengine, au kwa sababu watumwa wa makabila fulani walikuwa na vurugu na waasi zaidi kuliko wa makabila mengine. Pia ilihisiwa kwamba Waafrika fulani walifaa zaidi kuwa watumwa wa nyumbani, na wengine kuwa . wafanyakazi wa mashambani. Hata hivyo, kwa jumla, yote haya hayakujaliwa pwani ya Afrika ya Magharibi. Wazungu walichukua karibu kila walichopewa. Kwa mfano, maelfu ya watoto walipakiwa katika majahazi ya watumwa,
wakati
mwingine
wakiwa
na
umri
wa
hata
miaka
9.
Wanaume na wanawake wenye umri mkubwa zaidi pia walikubaliwa, ingawa ilijulikana wazi kwamba wasingeishi kwa muda mrefu kwa shida zilizokuweko kwenye mashamba makubwa huko ng'ambo ya Atlantiki. Jambo walilosisitiza Wazungu ni kwamba bei ipunguzwe nusu iwapo walinunua watoto au wazee, na walilipa bei tofauti kufuatana na nguvu na afya ya kila mtu aliyekuwa anauzwa.
Lugha ya biashara ya utumwa Kwa kawaida, mapatano ya bei yalifanywa kwa lugha maalumu za pwani, ambazo asili yake zilikuwa za Kiafrika ingawa zilikuwa na maneno mengi ya kigeni. Lugha hizi zilikua wakati wa biashara, kama vile Kiswahili kilivyokua kwa ajili ya biashara baina ya Waarabu na Waafrika wa Pwani ya Afrika ya Mashariki. Tofauti yake ni kwamba msamiati wa lugha hizo za biashara ulihitalifiana mahali hadi mahali pwani pwani ya Afrika ya Magharibi, ukitegemea ni taifa gani la Wazungu lililofanya biashara zaidi katika sehemu kadhaa. Mahali ambako Wadachi walifanya biashara, watu waliyajua zaidi maneno ya Kidachi, kama ilivyokuwa karibu na maboma ya Wadachi katika Gold Coast. Walikofanya biashara Waingereza kulikuwa na “Kiingereza cha kubabia' (Pidgin English), kama katika miji iliyoko kwenye mlango wa mto wa Niger. Lugha ya biashara iliyoenea zaidi kuliko zote ni
12
lugha ya Machotara wa Kireno (Creole Portuguese) iliyosemwa Angola na Kongo na mwambao wote kati ya Senegal na Sierra Leone. Zaidi ya hayo, maneno mengi ya Kireno yalitumiwa katika kila sehemu ya pwani ya Afrika ya Magharibi, kwa sababu Wareno walikuwa ndio taifa la kwanza la Kizungu lililokutana na wenyeji wa Afrika ya Magharibi. Zaidi ya lugha maalumu ya biashara, Waafrika wengi walisema vizuri lugha mojawapo ya Kizungu. Baadhi ya machifu waliwapeleka wana wao kuishi na wafanya biashara wa Kizungu kwenye viwanda na maboma yao yaliyokuweko pwani pwani, hali wengine waliwapeleka wana wao Ulaya hasa. Katika mwaka 1788, taarifa moja ya Bunge la Uingereza ilieleza kwamba kulikuwako watoto hamsini wa Kiafrika katika jiji la Kiingereza la Liverpool, licha ya wengine waliokuwa sehemu nyingine za nchi hiyo. Wote walikuwa wana wa machifu au wafanya biashara machotara katika Afrika ya Magharibi. Ukweli ni kwamba watawala wa Kiafrika walitaka kuyafahamu zaidi maisha ya na walitumaini kupata baadhi ya maarifa na ujuzi Wazungu waliokuwa nao Wazungu. Kwa bahati mbaya, maarifa ya Wazungu
(hasa
ya ufundi
na
mambo
ya uchumi).
yalitumiwa
kuendelezea
biashara mbaya ya utumwa; na vivyo hivyo watawala wa Kiafrika; walitaka elimu ya Kizungu kusudi waweze kupata faida zaidi kutokana na biashara ya utumwa. Chifu mmoja wa Kiafrika alipoulizwa kwa nini aliithamini sana elimu ya Kizungu, alijibu kwamba alitaka “kujifunza kuwa laghai hodari kama alivyo mtu mweupe.”
Hila za kuendeshea biashara ya utumwa
Ingawa Wazungu walihitaji washirika-Waafrika ili kuiendesha biashara ya utumwa, hakuna mmoja wao aliyemwamini mwenzake, na kila mmoja alijitahidi kumdanganya mwenzake. Wazungu walitia maji ya chumvi katika pombe, waliweka vizibo vya uwongo katika mapipa ya baruti na walidanganya kila wakati ilipobidi kupima kitu chochote. Kusema kweli, walipodhani wangeweza kuondoka bila kulipa chochote, waliondoka huku wamewachukua hata wale Waafrika waliokwenda majahazini kuwauzia watumwa. Watawala wa Kiafrika walikuwa wepesi wa kugundua hila za wafanya biashara wa Kizungu, ingawa na wao walikuwa na hila zao nao. Kwa mfano, walipokuwa wanataka kumuuza mtu mgonjwa, walikuwa wakiupaka mafuta mwili wake ili aonekane ana afya. Hila nyingine ilikuwa ni kuwalazimisha Wazungu kuwanunua watumwa kwa makundi kusudi wapate kuwachanganya wasio na afya na wenye afya, wazee na vijana. Hila nyingine ya Kiafrika iliyokuwa ikitumiwa sana pwani pwani ya Afrika ya Magharibi ilikuwa ni kuwashtaki Wazungu kwamba wamevunja sheria,
13
kuwapeleka mahakamani na kuwalipisha faini kubwa. Wakati mwingine viongozi wa Kiafrika walikuwa wakithubutu hata kumuua Mzungu katika nchi yao na kumnyang'anya bidhaa zake. Hii ndiyo njia ya kikatili na mbaya iliyotumiwa kuendeshea biashara ya utumwa ya Atlantiki, ambapo vita na ghasia zikiweza kutokea siku zote baina ya washiriki Wazungu na Waafrika katika kuifanya dhambi hii kubwa ya biashara ya utumwa.
Mwafrika daima yu katika hatari Hadithi nyingi zinasimuliwa juu ya hali mbaya ya Waafrika waliopatwa na mkosi wa kuletwa pwani ili kuvushwa bahari. Waafrika wengi walibururwa toka majumbani mwao barani mwa Afrika ya Magharibi, na walikuwa hawajawahi kuiona bahari kabla. Pia hawakuwa wamewahi kumwona mtu mweupe, kwa hiyo walitishika kwa sababu walidhani kwamba wangeliwa na wageni hao. Kusema kweli, wale waliouzwa walivuliwa nguo na kuchunguzwa kwa makini kama mnyama yoyote wa kuchinjwa kwa ajili ya kitoweo. Jambo kuu tunalohusika nalo ni wale waliobaki kuliko wale waliochukuliwa; na si vigumu kuelewa kwamba watu wengi wa Afrika ya Magharibi waliteseka sana wakati wa biashara ya utumwa ya Atlantiki. Kwanza kabisa, wengi wao walipoteza ndugu zao na rafiki zao shafiki; na pili, kila mmoja ambaye hakuwemo katika tabaka ya watawala lazima aliishi na hofu ya kukamatwa wakati wowote. Njia ambazo Mwafrika aliweza kutiliwa utumwani zilikuwa nyingi mno hivyo kwamba hakuweza kuhisi kuwa yu salama. Kabila lake lingeweza kushambuliwa na kabila jingine, au kijiji chake kingeweza kushambuliwa na kundi la wawinda watumwa, au angeweza kutekwa nyara na kundi dogo linapomkuta mahali pasipo na watu. Kuteka watu nyara lilikuwa jambo la kawaida Afrika ya Magharibi wakati wa biashara ya utumwa ya Atlantiki hata ikawa kuna neno moja la kukieleza kitendo hicho katika lugha zote za kibiashara za pwani. Neno
lenyewe lilikuwa '“panyar', lililochukuliwa toka apanhar, lenye maana ya '“kukamata' au “kutwaa”.
neno
la Kireno
Zaidi ya mashambulio yote ya watu wa nje, mtu wa kawaida aliweza kuuzwa na chifu wake mwenyewe kwa shtaka la kipuuzi. Wakikabiliwa na hatari zote hizo, si ajabu kwamba watu wengi walianza kutembea na silaha ili kujitayarisha kupambana na jaribio lolote la kuwakamata, hali wengine waliamua kuzihamishia nyumba zao sehemu nyingine zilizoonekana kuwa zi salama zaidi. Hili pengine lilihitaji kuhamia misituni maili chache tu ambako mtu angeweza kujificha, lakini wakati mwingine ilibidi kwenda zaidi. Kwa mfano, Wabapende ambao leo wanaishi kingoni mwa mto wa Kasai wa Zaire zamani waliishi pwani
14
ya Angola, lakini iliwabidi kuwakimbia Wareno waliokuwa wakifanya biashara ya utumwa.
Maisha na sheria za Mwafrika zinachafuliwa Ni wazi kwamba kwa ajili ya biashara ya utumwa ya Atlantiki watu hawakuweza kuishi maisha yao ya kawaida. Watu wengi wa Afrika ya Magharibi waliishi kwa kulima, na bila shaka kilimo kilirudi nyuma hiyo wakati huo. Kwanza, kupungua kwa watu wengi namna hao Pili, mashambani. kazi wafanya kunamaanisha kupungua kwa ambacho kitu kupanda ya sababu na waliobaki nyuma hawakuwa pengine wasingekuwepo kukivuna. Mwishoni mwa karne ya kumi na nane, hoja moja iliyotumiwa na Wazungu waliotaka kukomesha biashara ya utumwa ya Atlantiki, ni kwamba ukomeshaji huo ungewapatia nafasi Waafrika kufanya kazi na kutoa bidhaa nyingine ambazo zingeweza kununuliwa na Wazungu. Walionyesha kwamba, ikiwa biashara ya utumwa itaendelea, watu wataona vigumu sana kuendelea na shughuli zenye maana. Mabadiliko yaliyoletwa na biashara ya utumwa ya Atlantiki sio tu katika maisha ya watu binafsi wa Afrika ya Magharibi, bali pia katika jumuiya yenyewe. Ndiyo kusema, kulikuwako mabadiliko katika sheria na wako la jumuiya. Wakati tabaka la watawala lilipoharibika na kutumia hila katika mahakama ya kienyeji ya sheria, kwa kweli waliubadili msingi wote wa sheria ambayo ilikuwako kuwalinda watu, ambayo badala yake ilitumiwa kuwatengea watu ili kuwatia utumwani. Kabla ya kuwasili kwa Wazungu, Mwafrika wa Afrika ya Magharibi
aliyepatikana na kosa la kuiba ilimbidi kumrudishia mwenye mali thamani ya kile alichoiba. Iwapo mtu alifanya zinaa, ilimlazimu kumlipa mahari mume aliyehusika. Hizi zilikuwa adhabu ndogo, hasa mtu akifikiria kwamba Ulaya wakati huo kulikuwa na makosa mengi ambayo adhabu yake ilikuwa kifo. Kwa kweli, Wazungu Afrika ya Magharibi
wao
wenyewe
walisifu
tabia ya kiungwana
ya sheria
za
Waafrika katika karne ya kumi na sita na kumi na saba. Biashara ya utumwa ikaharibu yote hayo. Ikawa mtu huweza kuuzwa kwa kuiba kitu cha thamani ndogo, kwa kufanya zinaa, kwa kushindwa kulipa deni ndogo, na mengi mengine. Yote haya baada ya kuwa mashtaka yenyewe mara nyingi yalikuwa ya uwongo. Kitu kimoja cha kushangaza kabisa juu ya Afrika ya Magharibi katika karne ya kumi na nane na katika karne ya kumi na tisa ni kwamba kulikuwa na maelfu ya watu walioishi katika hali ya utumwa. Walikuwa mali ya bwana Mwafrika, na ingawa hawakutendewa vibaya kama vile watumwa
huru.
Wazungu
katika Amerika,
walikwenda
Gambia,
hawakuwa
na haki zote za watu
Sierra Leone,
Gold
Coast
na
15
Nigeria na walirudi wakisema kwamba robo tatu ya Waafrika wa huko walikuwa watumwa. Miaka mia tatu kabla, Wazungu walikuwa wameona baadhi ya wafalme wa Afrika ya Magharibi wana idadi kubwa ya watumishi waliokuwa si huru kamili, hali watu wachache walikuwa mali ya bwana fulani wakifanya kazi kama watumwa wa mashambani. Lakini ni hivyo tu — hapakuwapo tabaka kubwa la watumwa, kama ilivyokuwa katika Afrika ya Magharibi siku za mwisho za biashara ya utumwa ya Atlantiki. Kulikuwa na idadi kubwa ya watumwa waliokuwa wakifanya kazi Afrika ya Magharibi mwishoni mwa karne ya kumi na nane na kumi na tisa kwa sababu Waafrika waliopata mateka wa kuwauza kwa Wazungu, kwa kawaida waliwaweka baadhi yao kwa kazi zao wenyewe. Bila shaka tabaka la watawala ndilo lililokuja likawa na watumwa, hali katika makabila yaliyouza watumwa wengi sana kwa Wazungu iliwezekana kuona idadi kubwa ya watumwa waliotumiwa kwa kazi za pale pale.
Machotara Hatimaye,
hata
tabaka
la watawala
Waafrika
halikuweza
kupata
faida nyingi kutokana na biashara ya utumwa ya Atlantiki kama walivyotumaini. Walipata bidhaa za Wazungu zilizotengenezwa viwandani maadamu walikuwa washiriki wenye manufaa kwa Wazungu. Lakini sehemu nyingi, kwa maoni ya Wazungu, hawakuwa wakifanya kazi yao vizuri sana, kwa sababu hawakuwatesa sana watu wao kama walivyotaka wafanya biashara ya utumwa. Katika sehemu nyingi za pwani ya Afrika ya Magharibi tabaka jipya la wafanya biashara lilipata nguvu ya uchumi, na pengine nguvu ya utawala pia. Wengi wao walikuwa machotara - watoto ambao baba zao walikuwa ni Wazungu na mama zao Waafrika - na walikuwa wafanya biashara ya utumwa hodari kabisa. Kwa baba zao walielewa namna biashara ya Kizungu ilivyoendeshwa, hali uhusiano wao na Waafrika uliwafundisha namna ya kufaulu katika kuingiliana na Waafrika. Hawakuwa na uaminifu wa dhati kwa Wazungu wala kwa Waafrika, lakini kwa jumla waliwatumikia Wazungu na kuwanyonya vibaya Waafrika, kwa sababu hiyo ndiyo iliyokuwa njia ya kupatia faida kubwa kabisa. ; Machotara wafanya biashara ya utumwa walionekana kwanza katika Senegambia na Upper Guinea Coast. Baba zao walikuwa Wareno, na kwa kawaida walikuwa na jamaa zao katika visiwa vya Cape Verde
vilivyokuwa vimehamiwa na Wareno na kulimwa kwa jasho la Waafrika watumwa. Machotara wa sehemu hii ya kaskazini ya Afrika ya Magharibi walisaidia kuwapakia maelfu ya Waafrika toka sehemu hiyo na kuwapeleka katika makoloni ya Wahispania huko Amerika
16
mnamo
karne ya kumi na tano, kumi na sita na mwanzo
mwanzo
wa
karne ya kumi na saba. Machotara wengine wa Kireno walifanya kazi ya namna hiyo hiyo Angola na Kongo. Wao ndio waliosafiri ndani sana ya bara la Afrika ya Kati kusudi wawalete watumwa pwani, na wanajulikana kwamba walivuka bara lote toka Angola hadi Msumbiji. Hata hivyo, machotara hao kwa kweli hawakupata uwezo wa kutawala
katika sehemu za Afrika ya Magharibi mpaka karne ya kumi na nane na kumi na tisa. Hasa walikuwa na nguvu Dahome na Nigeria ambako machotara waliotoka Brazil walikuwa washauri wa wafalme, na
wafanya biashara wakubwa kabisa wa utumwa; wakati ambapo huko Waingereza baba zao walikuwa ambao watoto Sierra Leone, waliwapokonya madaraka machifu Waafrika. Kutokea kwa tabaka hili la wafanya biashara machotara ilikuwa ni mfano mwingine wa badiliko katika wako la jamii za Afrika ya Magharibi lililoletwa na biashara na Wazungu, na hasa kwa kufanya biashara ya utumwa.
Maafa yaliyotokea Katika sehemu nyingi za Afrika ya Magharibi, biashara ya utumwa ya Atlantiki ilikwisha mnamo miaka ya 1860, ingawa haikukomeshwa kabisa mpaka karibu na mwaka 1880. Hata hivyo, ilichukua muda hali kurudi kuwa za kawaida, na baadhi ya jamii za Afrika ya Magharibi ziliendelea kuona maafa ya biashara ya utumwa ya Atlantiki muda mrefu baada ya kukoma. Kwa mfano, wale waliofanywa watumwa wa mabwana wa Kiafrika huko Afrika ya Magharibi waliendelea katika hali hiyo mpaka waliporejeshewa uhuru wa kisheria na serikali za kikoloni. Hili lilikuwa tokeo la ajabu kweli kweli. Wazungu walidhani wanaleta maendeleo Afrika kwa kukomesha jambo lisilo la maendeleo. Walidhani
kuwa
siku zote kulikuwa
na watumwa
wengi
Afrika,
na
kwamba watu wengi waliouzwa kwa Wazungu walikuwa tayari ni watumwa Afrika. Kwa kweli, kinyume cha hivyo ndivyo ilivyokuwa, kwa sababu Wazungu wakasaidia kuanzisha
ndio waliokuja Afrika na kuongeza utumwa
kununua watumwa, huko. Vile vile,
unapochunguza jamii za Afrika ya Magharibi katika karne ya kumi na tisa na
ishirini,
utaona
kuwa
Wazungu
walifanya
kosa
la kufikiri
kwamba Waafrika siku zote walitiwa utumwani kwa kufanya hatia fulani. Hapa vile vile, wa kulaumiwa ni hiyo hiyo biashara ya utumwa ya Atlantiki. Baada ya biashara ya kupeleka watumwa nje ya Afrika kwisha, zile jamii za Kiafrika zilizotaka kuendelea kutumia watumwa zilihifadhi zile sheria mbovu za siku za biashara ya utumwa, na kuendelea kuwatia watu utumwani kwa makosa madogo. Kama ilivyosemwa hapo juu, baadhi ya sehemu za Afrika ya Magharibi ziliuza idadi kubwa zaidi ya watumwa kuliko nyingine, kwa
17
hiyo ukubwa wa matokeo ya biashara ya utumwa haukuwa sawa kila mahali. Kwa mfano, biashara ya utumwa ya Atlantiki haikuwafikia
Waafrika waliokuwa wakiishi Ivory Coast (Pwani ya Pembe) hali mtu anaweza kufikiria yaliyotokea mahali kama Angola, ambayo peke yake iliwapatia Wazungu karibu watumwa 3,000,000 (milioni tatu). Angola ilihasirika mno kwa sababu Wareno walipeleka majeshi yao bara na waliwalazimisha wale machifu waliowashinda kutoa watumwa kuwa ndiyo kodi yao. Kulipiganwa sana hata watu wengi wakafa, mbali wale waliokamatwa na kuuzwa kama watumwa. Kwa hiyo, idadi ya watu wa Angola ilipungua sana, na zile dola zilizokuwako karibu na pwani zikaharibiwa. Kaskazini ya Angola kulikuwako dola ya Kongo. Hii ilikuwa moja ya nchi zilizokuwa na nguvu na zilizoendelea kabisa
katika Afrika ya Magharibi, lakini ilidhoofika kwa ajili ya biashara ya utumwa ya Wareno katika karne ya kumi na sita na kumi na saba, nayo vile vile ilitoa watumwa kuwa ndiyo kodi yao. Mwisho ilivunjika baada ya kushambuliwa na kushindwa na Wareno katika mwaka 1665. Kwa bahati nzuri, mambo hayakutokea kuwa mabaya siku zote kama ilivyokuwa Angola na Kongo, hata ilipokuwapo biashara kubwa ya utumwa. Nchi ya Walbo, kwa mfano, ilikuwa moja ya watoaji wakubwa wa watumwa, lakini hata hivyo, nchi hiyo ilibaki na idadi kubwa ya watu. Bila shaka, hii ina maana kwamba idadi hiyo ilikuwa kubwa sana tangu mwanzo, lakini bado inashangaza kwamba nchi hiyo
iliweza kuhimili kupoteza idadi kubwa namna hiyo. Sehemu ya magharibi ya Nigeria pia iliweza kuepuka maafa ya biashara ya utumwa ya Atlantiki. Falme kama zile za Benin na Oyo zilikuwapo kabla ya Wazungu kuwasili katika ile nchi iitwayo Nigeria leo. Zote mbili, Benin na Oyo, ziliweza kujisalimisha muda mrefu zikishiriki katika biashara ya utumwa na kushambulia jirani zao. Wakati mwingine, watu walishirikiana katika kujilinda na wakapata nguvu zaidi licha ya biashara ya utumwa. Hivi ndivyo walivyokuwa WaGa wa Gold Coast (Pwani ya Dhahabu). Walikuwa ni wakulima ambao hawakuwa na dola hasa, kwa hiyo hawakuona lazima ya kuwa na majeshi ya kupigana vita. Lakini baada ya kushambuliwa mara kwa mara na makabila ya WaAkani, walijifunza mipango ya kisiasa na mbinu za kupigania vita za adui zao na wakakaa. pamoja katika miji kama Akra. Hata hivyo, kwa jumla, dola hizi mpya zilizozuka Afrika ya
Magharibi wakati wa biashara ya utumwa ya Atlantiki zilikuwa zoo zenyewe zinafanya biashara ya utumwa. Dahome na Ashante zinajulikana sana. Zilishughulika sana kuwapatia Wazungu watumwa, na zikawa na nguvu kwa sababu ya bunduki za Wazungu walizozipata kwa kubadilishana na hao watumwa. WaFoni wa Dahome walizama
18
sana katika biashara ya utumwa hata wakairatibu dola yao ili kusudi iwe ikipigana vita vya kupatia mateka. Dahome ilifika kiwango cha kuweka kikosi maalumu cha askari wa kike walioogopwa na washindani wao wote. Dahome ilipata hasara kwa kushughulika na vita tu. Kilimo kilipuuzwa na njaa zilitokea mwishoni mwa karne ya kumi na nane. Kwa upande wa uchumi wake, mojawapo ya nchi za Afrika ya Magharibi iliyofuzu sana na ambayo ilishiriki vikubwa katika biashara ya utumwa, ilikuwa nchi ya Wafulani ya Futa Djalon. Watawala wa Kifulani wengi walikuwa wafugaji ng'ombe, na waliweka watumwa wengi kufanya kazi ya kilimo, ambayo ilikuwa pamoja na kulima mazao ya chakula ya kuuzia majahazi ya watumwa. Kwa hiyo, ingawa hakukuwa na usawa, uchumi wa nchi ya Futa Djalon ulikuwa
na nguvu. Ukiitazama mifano kama hiyo ya Futa Djalon, Dahome na Ashante, utaona kwamba biashara ya utumwa ya Atlantiki haikuwa ya uharibifu tu. Ilisababisha dola fulani kuanguka, na nyingine kuinuka. Iliwafanya watu wengi Afrika kuwa watumwa katika nchi zao wenyewe, lakini ikawafanya watu wachache kuwa na nguvu sana. Kwa mfano, machotara walikuwa na watumwa wengi sana wa Kiafrika. Hata Angola, ingawa ile sehemu karibu na pwani ilipatwa na maafa, dola mpya ambazo zilinufaika kwa kushiriki katika biashara ya utumwa ya Atlantiki zilizuka bara. Lakini, itakuwa ni kosa kudhani kuwa biashara ya utumwa ya Atlantiki ilileta mema ya kutosha kufuta madhara yake au hata kutufanya tuhisi kuwa “hata hivyo, haikuwa. Tukipima mema na maovu ya biashara ya utumwa na jinsi yalivyoiathiri Afrika ya Magharibi, mizani itaonyesha wazi kwamba biashara hiyo ilikuwa tukio baya kuliko yote yaliyowapata watu wa sehemu hiyo. Kuna mfano mzuri wa kuonyesha jinsi biashara hiyo ilivyokuwa ya uharibifu. Tunaweza kuzichungua jamii za Afrika ya Magharibi ili tuone matokeo ya biashara ya bidhaa nyingine zisizokuwa watumwa ambazo Waafrika walifanya na Wazungu. Wazungu siku zote walikuwa wanapenda dhahabu, pembe za ndovu na bidhaa nyingine za Kiafrika. Licha ya dhahabu, kwa kawaida walihitaji bidhaa nyingine zaidi ya, siyo badala ya, watumwa; kwa hiyo hakukuwa na biashara yoyote nyingine badala ya ile ya watu. Hata hivyo, tunaweza angalau kuona kuwa watu walifaidika zaidi walipofanya mipango ya kuwinda ndovu badala ya kuwinda binadamu. Hali kadhalika, wakati Waafrika walipowauzia Wazungu bidhaa kama nta, ina maana kwamba Waafrika walikuwa wakishiriki katika shughuli zenye manufaa, kama vile kufuga
nyuki na kutengeneza nta. Mfano mwingine mzuri kama huu ni ule wa mbao. Mti huo ulitumika Ulaya kutengeneza rangi nyekundu za nguo, kwa hiyo Wazungu
walinunua
magogo
ya 'camwood'
Sierra Leone,
19
Gambia na Kamerun. Hii ilizusha biashara ndogo ya mbao, ambapo Waafrika waliohusika waliikata hiyo miti, wakaitoa magamba (magome) na kuikata vigogo vidogo ambavyo walivitupa katika mito iliyovisafirisha masafa marefu hadi pwani. Walilipwa kidogo sana kwa
juhudi zao zote — kidogo zaidi kuliko kama wangaliuza watumwa — lakini angalau bidhaa hii iliwafanya waingilie biashara yenye manufaa. Haiwezekani kufikiria biashara ya namna nyingine yeyote ambayo ingeweza kuwa na madhara kama biashara ya utumwa ya Atlantiki.
Vitisho vya kiuchumi Ni wazi kwamba baada ya biashara ya utumwa ya Atlantiki kilikuja kipindi cha 'Kunyang'aria Afrika (Scramble for Africa) na ukoloni, na hivi Wazungu waliendelea kuinyonya Afrika kwa namna nyingine mpya. Kusema kweli, ni lazima tuitazame biashara ya utumwa ya Atlantiki kama hatua ya kwanza ya ubeberu wa Wazungu katika Afrika. Wakati huo, ubeberu wenyewe ulikuwa wa kiuchumi tu. Wazungu walikuwa na uchumi wa kibepari uliokuwa na nguvu, hali uchumi wa Waafrika ulikuwa ule wa kujipatia riziki ya siku kwa siku. Kwa hiyo Wazungu walipiga ngoma na kuwafanya Waafrika wacheze. Bidhaa fulani zilitengenezwa Ulaya tu. Waafrika wakaambiwa kwamba, ikiwa walitaka bidhaa hizo, iliwabidi watoe binadamu wenzao. Jambo moja la kuhuzunisha sana kuhusu biashara ya utumwa ya Atlantiki,
kwa
upande
wa
Waafrika
wa
Afrika
ya
Magharibi,
ni
kwamba hawakuwa na la kufanya walipokabiliwa na vitisho vya kiuchumi. Walikuwako machifu wachache wa Afrika ya Magharibi
waliojaribu kukomesha biashara ya utumwa katika sehemu zao. Mfalme wa Kongo alijaribu kukomesha biashara hiyo mwanzoni mwa karne ya kumi na sita; mfalme wa Dahome alijaribu katika miaka ya 1730, chifu mmoja wa Kibaga, wa sehemu ambayo leo ni Jamhuri ya Guinea, alijibidiisha kuwapinga wafanya biashara hiyo katikahi ya karne ya kumi na nane, na mfalme wa Kiwolof wa Keya (Cayor) huko Senegal aliipinga biashara ya utumwa mwishoni mwa karne ya kumi na nane. Lakini wote walishindwa, kwa sababu hakuna mtawala hata mmoja wa Kiafrika aliyeweza kuzishinda nguvu za uchumi wa Ulaya. Hatimaye, Waafrika wa Afrika ya Magharibi walikabiliwa na tatizo la kuuza au kuuzwa. Hapo suala la silaha likawa muhimu sana. Ili nchi iwe na nguvu, ilibidi ipate silaha; lakini kuzipata hizo silaha kwa Wazungu, iliwabidi Waafrika watoe watumwa. Hivyo watawala wa Kiafrika wakajiona wanauza watumwa ili wapate silaha za kukamatia watumwa wengine wa kununulia silaha zaidi. Haya yanaweza kuelezwa kama mambo yaliyoambatana. Hata hivyo hayawatoi makosani kabisa wale
20
watawala
wa
Kiafrika
waliowasaidia
Wazungu,
ila yanaeleza
namna gani mwishowe Waafrika hawakuwa washiriki wa Wazungu bali wafanya kazi au vibaraka wao. Wanahistoria wengine wanasema kuwa watawala wa Kiafrika waliwahadaa Wazungu, wakawatumia kama vyombo vyao. Hutoa hoja
kwamba Waafrika walielewa mashindano yaliyokuwako baina ya mataifa ya. Kizungu, kwa hiyo walilitumia taifa moja kugombana na jingine. Kwa mfano, katika Gold Coast hakukuwa na taifa la Kizungu hata moja lililokuwa na ngome mbili au tatu zilizopangana mstari mmoja. Badala yake, ngome ya Wadachi ilikuwa karibu na ya Wadenishi ambayo nayo ilikuwa karibu na ile ya Waingereza, na kadhalika. Mtindo huu ulizuka kwa $ababu mara baada ya taifa moja la Kizungu kujenga ngome yake katika sehemu yoyote ya Gold Coast, Waafrika waliokuwako karibu na hapo nao waliliita taifa jingine lililokuwa likishindana na lile la kwanza kuja kujenga ngome katika nchi yao. Vile vile machifu wa Gold Coast walikuwa hodari sana wa kuwafanya Wazungu wawasaidie katika vita vyao vya kienyeji. Lakini Waafrika walikuwa wakijihadaa wenyewe tu, maana Waafrika wengi zaidi walikuwa wakiuzwa, ambavyo ndivyo hasa walivyotaka Wazungu.
Hata kama nchi moja ya Kizungu haikufanikiwa kama ilivyofanikiwa nyingine, utaratibu wa kibepari haukudhurika.
Faida za watu binafsi ndio msingi wa maafa Siku hizi wanahistoria hawajadiliani tena kama utumwa ulikuwa kitu cha sawa au cha makosa. Wanakubaliana kwamba ulikuwa jambo ovu sana. Hata hivyo, ni rahisi kuendelea kujadili athari ambazo biashara ya utumwa ya Atlantiki ilikuwa nazo juu ya siasa, uchumi na utamaduni, na kuyasahau yale mateso makubwa waliyoyapata binadamu waliouzwa, na pia unyama mkubwa wa wale waliokuwa wakiiendesha biashara hiyo. Mambo yote haya yalifanyika kwa sababu watu walishughulika na faida zao binafsi tu. Hii ni pamoja na tabaka la watawala wa Kiafrika. Wao walijua kwamba walikuwa wakishiriki katika mambo maovu, lakini walihitaji bidhaa za Kizungu, ambazo zilikuwa ni utajiri katika jamii zisizotumia fedha. Wazungu walikutwa tayari wanatumia fedha. Walifanya biashara ili kupata fedha zaidi, ambazo wangezifanya mtaji katika nchi zao na kuwafanya matajiri zaidi. Kwa sababu kulipatikana faida kubwa sana kwa biashara ya utumwa zilizokuwa zao dhamiri kufuata walikataa Wazungu Afrika, walijua Wao hiyo. zikiwaambia kuwa ni makosa kufanya biashara kubebea ya majahazi katika kwamba Waafrika walikuwa wakiteswa, watumwa
kwamba
na katika mashamba
kuuza binadamu
makubwa
wenzao
huko Amererika; na walielewa
ni jambo lisiloweza kuwa ni haki.
21
Hata hivyo, kanisa la Kikristo lilijitokeza na visingizio vya kuunga mkono biashara ya utumwa. Makasisi, wao wenyewe walifanya biashara ya utumwa, hasa katika Angola, na wengine wengi walikuwa na watumwa katika Amerika. Sababu ya pekee iliyotolewa na Kanisa Katoliki kwa vitendo vyao hivyo ni kwamba lilikuwa linaziokoa roho za Waafrika kwa kuwabatiza watumwa. Waprotestanti walikuwa wabaya zaidi, kwani wao hata hawakuweka wazi kwamba wao wanaamini kuwa Mwafrika anayo roho. Badala yake waliunga mkono lile wazo kuwa mtumwa wa Kiafrika alikuwa ni kitu tu kama samani (fanicha) au mifugo. Hakuna sehemu katika historia ya Kanisa la Kikristo ambayo ni ya fedheha kuliko hii ya kuunga mkono biashara
ya utumwa.
Kwa nini Wazungu kukomesha
utumwa
Daima walikuwako watu wachache waliopinga biashara ya utumwa toka mwanzo,
lakini serikali na wafanya biashara waliwapuuza
katika
karne ya kumi na tano, kumi na sita na kumi na saba. Juhudi za kikweli kweli za kuikomesha biashara hii hazikufanywa mpaka mwishoni mwa karne ya kumi na nane. Hapo makundi yaliundwa huko
Amerika na Ulaya ili kuzishawishi serikali kukomesha biashara hiyo, na kulifikia lengo hilo, kila mara walijaribu kushawishi watu wengine katika nchi zao wawaunge mkono. Wanachama wa makundi hayo waliitwa wasamaria, na wale waliokuwa Uingereza walikuwa maarufu kuliko
wote.
Miongoni
mwao
ni .Granville
Sharp,
mwanasheria
aliyepigania haki za watumwa katika mahakama ya Uingereza; Thomas Clarkson, mtu mwenye nia thabiti, aliyejitahidi kuliko wengine wote kupata msaada wa umma wa Kiingereza; na William Wilberforce,
aliyekuwa mbunge wa Bunge la Uingereza, aliyesimamia juhudi za kuishawishi serikali yao kupitisha muswada wa kuwaharamishia raia wa Kiingereza kufanya biashara ya utumwa. Muswada huo ulipitishwa mwaka 1807. Watu wengi huko Uingereza walioshiriki katika ukomeshaji wa biashara ya utumwa walikuwa ni Wakristo wainjilisti, ambao walianza kupinga barabaabara kuwatendea Waafrika kama wanyama. Katika Ufaransa, wapingaji wa biashara ya utumwa walikuwa ni watu wale wale walioleta Mapinduzi ya Ufaransa, ambayo msingi wake ulikuwa ni ile imani kwamba watu wote ni sawa na wana haki ya kuwa huru. Lakini, mambo yakichunguzwa kwa makini, itaonekana kuwa Wazungu (na hasa Waingereza) hawakuikomesha biashara ya utumwa kwa ajili ya uadilifu wa mioyo yao. Walikwisha kupata faida kubwa kwa kuinyonya Afrika kwa njia hiyo, na ilipofika mwisho wa karne ya kumi na nane biashara ya Atlantiki haikuwa tena na faida kama vile
22
ilivyokuwa hapo mwanzo. Hili ndilo jambo lililowezesha biashara ya utumwa kukomeshwa. Denmark ilikuwa nchi ya kwanza ya Kizungu kuwaambia raia wake waiache biashara ya utumwa. Makoloni ya Denmark huko Amerika yalihitaji maelfu machache tu ya watumwa kila mwaka, kwa hiyo Serikali ya Denmark ilionelea bora kuwapeleka wanawake wa kutosha kwenye mashamba yao ili idadi ya watu iongezeke kwa njia ya ilionelea kwamba kikawaida. 1802 Denmark Ilipofikia mwaka ingeweza kutoendelea na sehemu yake katika biashara ya utumwa. Hatua muhimu kuliko zote ni ile ya ukomeshaji wa Kiingereza katika mwaka
1807, maana Uingereza ilishiriki vikubwa mno katika biashara
ya utumwa ya Atlantiki wakati huo. Katika kipindi cha zaidi ya miaka ishirini hivi, sheria za ukomeshaji kama hiyo zilipitishwa huko Amerika, Sweden, Uholanzi, Ufaransa, na Brazili. Ureno na Hispania kwanza zilikataa kupitisha sheria za kuwapigia marufuku raia zao kushiriki katika biashara ya utumwa, lakini katika mwaka 1815 na 1817 walikubali kuzuia biashara hiyo katika nchi zao isipokuwa zile zilizoko kusini ya Ikweta. Mara baada ya mataifa mengi kupitisha sheria za kuwaharamishia raia zao kufanya biashara ya utumwa, lilibaki tatizo la kuhakikisha jinsi sheria hizo zilivyotiiwa. Mataifa mengi hayakufanya juhudi kikweli kweli kuzitekeleza sheria hizo. Ufaransa, Amerika, Brazili, Ureno na Hispania, zote ziliasi sheria hizo. Kwa kweli, Uingereza peke yake ndiyo iliyofanya juhudi za kikweli kweli kuzuia meli zisibebe watumwa kutoka Afrika ya Magharibi. Serikali ya Uingereza ilifanya hivyo kwa sababu ya mawazo adilifu ya kupendelea ubinadamu, kwa upande mmoja, na pia kwa sababu Waingereza waliokuwa na watumwa na waliokuwa wafanya biashara ya watumwa walitaka biashara yote ikomeshwe, baada ya wao kuzuiwa kushiriki. Kwa hiyo, Uingereza ilitumia jeshi lake la wanamaji kuulinda mwambao wa Afrika ya Magharibi ili kuzuia biashara ya utumwa ya Atlantiki. Wakati jahazi lilipokamatwa na manowari ya Kiingereza nje ya pwani ya Afrika ya Magharibi, Waafrika waliokuwa humo walipelekwa Sierra Leone na kuachwa huru. Wachache baadaye walirudi makwao katika sehemu mbali mbali za Afrika ya Magharibi, lakini wengi wao
walibaki Sierra Leone, ambayo ilianzishwa kama makao ya Waafrika ambao hapo mwanzo waliwahi kuwa watumwa huko Amerika na Uingereza. Licha ya kusaidia kuongeza idadi ya watu ya Sierra Leon, ulinzi wa manowari hizo nje ya pwani ya Afrika ya Magharibi haukufanikiwa. Ingawa Uingereza
katika
karne
ilikuwa na jeshi kubwa la wanamaji kuliko yote ya kumi na tisa, haikuweza kutoa meli za kutosha
23
kuulinda mwambao wa Afrika ya Magharibi, ambao urefu wake ni maili elfu nyingi. Kulikuwa na mahali kwingi ambako jahazi liliweza kupakia watumwa na kung'oa nanga bila kuonekana na manowari ya Kiingereza. Kwa vile matumizi ya nguvu katika hali kama hizo hayakuwa
na matokeo
ya kutumainisha,
ilikuwa lazima kuwashawishi
machifu wa Afrika ya Magharibi wasiuze watumwa lijapo jahazi la Kizungu kuwatafuta. Kwa bahati mbaya, juhudi hizi zilikatisha tamaa pande zote mbili. Siku zote ilikuwako ijapokuwa ni serikali moja Ulaya au Amrrika iliyokuwa tayari kuwasaidia wafanya biashara wa utumwa na, kwa hiyo, kuifanya mipango ya Uingereza na nchi nyingine ya kukomesha biashara ya utumwa ya Atlantiki isifaulu. Jambo la kuwa biashara ya utumwa iliendelea kustawi wakati wa karne ya kumi na tisa na haikukoma mpaka karibu na mwaka 1880 lina maana kuwa mahitaji ya watumwa yalikuwa bado yangalipo huko Amrrika, na kwamba Wazungu walikuwa wangali na nia yao ya kuwatia Waafrika utumwani. Pia kuna dalili zinazoonyesha kuwa tabaka la watawala katika sehemu nyingi za pwani ya Afrika ya Magharibi liliendelea kuwatimizia Wazungu mahitaji yao ya watumwa.
Kwa nini Waafrika kupinga
utumwa
kukomeshwa
Pengine itashangaza kuona kwamba Waafrika walipinga vikali wakati Wazungu fulani walipojaribu kukomesha biashara ya utumwa, lakini hivi hasa ndivyo ilivyokuwa, isipokuwa kwa watu wachache sana. Machifu wa Kiafrika walitafuta bandari mpya za kusafirishia watumwa, wakafanya mipango na wafanya biashara ya utumwa kuzikwepa manowari za Kiingereza, na walikuwa wakali sana kwa mtu yoyote aliyewaendea kuwaambia waache kufanya biashara ya utumwa. Msimamo wa machifu wa Kiafrika waliokuwa wakifanya biashara ya utumwa,
kwa kweli ulikuwa unaeleweka wazi wazi.Kukamata
na kuuza
watu kama watumwa ilikuwa ndiyo shughuli yao kubwa toka karne ya kumi na tano na kumi na sita. Walipohitaji bidhaa za Kizungu, njia ya pekee ya kuzipatia ilikuwa ni kutoa watu, kwa sababu Wazungu walikuwa hawakubali chochote badala ya watumwa, isipokuwa dhahabu, iliyokuwa ikipatikana katika sehemu chache tu. Na kwa kweli machifu wa Kiafrika walizitaka bidhaa za Kizungu, ambazo hazikuwa
tena ni anasa tu bali zilionekana kama vitu vya lazima huko Afrika ya Magharibi. Njia moja iliyozungumzwa sana na maafisa wa Kiingereza katika Afrika ya Magharibi kama tatuzi la tatizo hili ilikuwa kuwapa machifu wa Kiafrika bidhaa nyingi sana kama zawadi au fidia ikiwa wangeacha kutoa watumwa.
Kwa mfano, katika mwaka
1839, mfalme wa Bonni,
moja ya nchi zenye nguvu kwenye mdomo wa mto wa Niger, alikubali
24
kukomesha biashara ya utumwa, ikiwa Serikali ya Uingereza ingempa kila mwaka bidhaa zenye thamani ya dala 2,000 (elfu mbili). Serikali ya Uingereza haikuunga mkono mapatano ya wawakilishi wake huko Bonni, kwa hiyo mapatano hayo hayakutimizwa. Hata hivyo, ni kweli
kabisa kwamba hayangefanikiwa. Zawadi iliyotolewa haikuwa na tofauti na ile mikopo midogo ambayo wabeberu wako tayari kuzikopesha dola za Kiafrika hii leo. Jambo lililohitajiwa ni biashara ya aina nyingine ambayo ingewawezesha Waafrika kuuza mazao na bidhaa zao wenyewe kwa bei nafuu. Kwa hiyo, baada ya biashara ya utumwa ya Atlantiki kuzuiwa, siasa nzuri kabisa ingelikuwa ni ile ya kutafuta bidhaa mpya za Kiafrika ambazo zingeweza kuuzwa Ulaya.
Uchumi mpya badala ya utumwa Kwa sababu ya maendeleo ya viwanda huko Ulaya mnamo mwisho wa karne ya kumi na nane na kumi na tisa, ambayo kwa kawaida huitwa “Mapinduzi ya Viwanda, kulitokea mahitaji makubwa ya mafuta ya kupaka sehemu mbali mbali za vyombo viwandani humo. Kujengwa kwa reli Ulaya pia kulimaanisha kwamba mafuta yalihitajika kwa ajili ya mitambo yake na magurudumu. Mafuta huko Ulaya yalitoka katika shahamu za wanyama, nazo hazikuwako za kutosha. Hata hivyo, shahamu za wanyama hazikufaa sana, kwa hiyo mafuta ya mimea yalipendelewa zaidi. Kwa mfano, kiungo kimoja cha kutengenezea sabuni kilikuwa mafuta ya mimea, na utengenezaji wa sabuni uliongezeka sana katika karne ya kumi na tisa. Ili kutosheleza mahitaji hayo Ulaya, Afrika ya Magharibi ilianza kutoa mafuta ya mimea katika karne ya kumi na tisa, ambayo mpaka leo yangali bidhaa yake kubwa ya kuuza nchi za nje. Asili mbili kubwa za mafuta zilikuwa karanga na michikichi, lakini mafuta ya michikichi yalikuwa na thamani zaidi kwa kuwa ndiyo yaliyohitajiwa na watengenezaji wa sabuni. Michikichi iliyotoa mafuta iko kwenye sehemu nyingi za pwani ya Afrika ya Magharibi, lakini ilibidi imee kwa wingi ili iwe badala yenye faida ya biashara ya utumwa ya Atlantiki. Michikichi ilistawi sana Dahome na Nigeria. Delta ya Niger ilikuwa ni moja ya magulio makubwa ya biashara ya utumwa Afrika ya Magharibi, lakini ilipofika katikati ya karne ya kumi na tisa ilikuwa ikitoa mafuta mengi mno ya mchikichi hata ile mikono kadha wa kadha ya mto wa Niger ikawa
inaitwa Mito ya Mafuta. Hili lilikuwa badiliko kubwa sana. Haikuwa jambo rahisi kutoka kwenye uchumi wa biashara ya utumwa kwenda kwenye uchumi wa mafuta ya mawese. Machifu wachache waliamua kujenga uchumi wao kwa kuuza mawese nchi za nje mapema katika karne ya kumi na tisa. Wengine wachache waliendelea na
2:5
biashara ya utumwa na kutojali kabisa uchumi wa mafuta ya mawese. Lakini wengi wa tabaka la watawala wa Kiafrika walikuwa na hadhari sana. Wao walipendelea kuanzisha biashara ya mawese huku wakiendelea na biashara ya utumwa. Kwa jumla, palikuwa na kazi kubwa kabla ya biashara ya mafuta ya mawese iliyokuwa ya amani na ya kisheria kuwa badala ya biashara ya utumwa, ambayo ilikuwa mbovu sana na ambayo ilikuwa imeharamishwa mapema katika karne ya kumi na tisa, kama ilivyoelezwa hapo juu. Kwa upande mmoja, kuwekwa bidhaa nyingine badala ya watumwa kulikuwa ni mapinduzi. Kulisababisha kuondolea mbali zile njia mbovu za kupatia watumwa, na badala yake kukaleta mipango mipya ya manufaa na kazi. Kwa mfano katika utengenezaji wa mafuta ya mawese, ilibidi machikichi yachumwe, yapasuliwe na kokwa zake zitengenezwe kwa njia maalumu ili zitoe mafuta. Ililazimu viwepo vyombo vya kuwekea mafuta, na wafanya kazi wengi zaidi walihitajika kuyapeleka mafuta hayo pwani, kwa vile misitu ya michikichi ilikuwa mbali na pwani. Ilisemwa katika mwaka 1857 juu ya mafuta ya mawese huko Sierra Leone kuwa: “Tabia ya kufanya kazi imewaingia sana watu hata ikawa, katika mwaka uliopita, kiasi cha kasiki 150,000
(mia moja na hamsini elfu) za kokwa zilichumwa na kuuzwa kwenye masoko. Kuzipata kokwa hizo, kwa uchache ilibidi kuzichemsha kasiki 350,000 (mia tatu na hamsini elfu) za machikichi, kuyatoa nyama zake kwa mikono na halafu kuyavunja na kuzitoa kokwa kifuu chake, ndipo zisafirishwe maili nyingi sana mpaka sokoni, hivyo ikibatilisha kwa mkazo mkubwa lile dai kwamba watu weusi hawafanyi kazi ila
kwa kulazimishwa.” Na
kazi
kubwa
zaidi
ilihitajiwa
katika
upandaji
na
uvunaji
wa
karanga. Watu wa Senegambia na Guinea ya Juu (Upper Guinea) walionyesha kuwa walikuwa na msukumo na ari ya kujaribu mambo, kwa sababu hawakuwa wakizijua karanga kabla, lakini hata hivyo walivumbua njia nzuri ya kuzilima. Wakati wa ukoloni, Serikali ya Kiingereza, ilijaribu kuanza kulima karanga Tanzania. Walikuwa na mtaji wa shilingi elfu nyingi na maarifa yao yote ya sayansi, lakini mpango huo ulishindwa vibaya sana. Waafrika wa Afrika ya Magharibi walionyesha busara zaidi na ustadi walipokuwa wanaiacha biashara ya utumwa ya Atlantiki.
Published by Foundation Books Lid. Tom Mboya Street, P.O. Bor 73435 Nairobi, and printed by General Printers Ltd, Dar es salaam Road, P.O. Bor 18001, Nairobi, Kenya.
26
Central University Library University of California, San Diego Please Note: This item is subject to recall.
Date Due
INTE?
CI 39 (7/93)
ARI
nj
UCSD Lib.
Hiki ni kijitabu cha kwanza katika mfululizo wa vitabu vingi katika Tanzania kimekusudia kuvitoa ambavyo Chama cha Historia kwa lugha ya Kiswahili. Lesgo kubwa la mfululizo huu ni kumfahamisha Mwafrika historia yake. Katika kijitabu hiki, mwandishi anaeleza kwa ustadi mkubwa, na kwa namna ambayo haijapata kuelezwa kwa Kiswahili, jinsi Wazungu walivyoivamia Afrika na kuwatia Waafrika utumwani, kwa nini
kufanya
hivyo,
hila walizozitumia,
jinsi walivyozichafua
mila
na
desturi za Waafrika na kuwasaliti wao kwa wao. Kwa lugha nyepesi na iliyo wazi, mwandishi anaonyesha kwamba Wazungu hawakuikomesha biashara ya utumwa kwa kuwa waliamini kwamba ilikuwa chafu na makosa (kama wengi wetu tunavyoamini), bali kwa kuwa ilikuwa njia nzuri zaidi na ya uficho zaidi ya kumtawalia na kumnyonyea Mwafrika na nchi yake. Kwa ufupi, hii ni historia ya jinsi Afrika ilivyonyonywa na inavyoendelea kunyonywa. Ni muhimu kila Mwafrika kuisoma.
Bei Shg. 4.50 (Afrika ya Mashariki tu)