EKKLESIOLOJIA: MAFUNDISHO YA KIKRISTO KUHUSU KANISA (MTAZAMO WA KIHISTORIA) [1 ed.] 9789976572605

Mwandishi wa kitabu hiki ni mbobevu katika masuala ya Teolojia Pangilifu (Systematic Theology) katika nyanja ya wanarefo

298 75 1MB

Kiswahili Pages 195 Year 2020

Report DMCA / Copyright

DOWNLOAD PDF FILE

Table of contents :
YALIYOMO
TABARUKU i
UTANGULIZI ii
SURA YA KWANZA 1
KANISA NA DHANA ZAKE 1
1. Maana ya Kanisa 1
2. Kanisa katika Agano la Kale na Agano Jipya 4
3. Kanisa na Ufalme wa Mungu 10
4. Taswira za Kibiblia kuhusu Kanisa 12
5. Kanisa kama Kiumbe Hai na Taasisi 15
SURA YA PILI 16
MAENDELEO YA KANISA KATIKA NYAKATI MBALIMBALI ZA HISTORIA 16
1. Enzi za mababa wa Kanisa 17
2. Zama za kati za Kanisa 18
3. Zama za Matengenezo ya Kanisa 20
a. Martin Luther 22
b. Wa-Anabaptisti 24
c. Wana-Refomati 25
SURA YA TATU 28
AINA, SIFA, ALAMA NA MAKUSUDI YA KANISA 28
I. Aina za kanisa 28
1. Kanisa la Ulimwengu na Kanisa la Mbinguni 28
2. Kanisa linaloonekana na Kanisa lisiloonekana 28
3. Uhusiano Kati ya Kanisa Lisiloonekana na Kanisa Linaloonekana 29
II. Sifa za Kanisa 31
1. Umoja 32
2. Utakatifu 37
3. Kanisa la Ulimwenguni pote (Ukatoliki) 38
4. Utume 39
5. Kutokuwa na Makosa kwa Kanisa 43
III. Alama za Kanisa 45
1. Kuhubiriwa kwa Neno 49
2. Kupokea kwa usahihi Sakramenti 52
3. Utekelezaji wa dhati wa Nidhamu ya Kanisa 52
IV. Makusudi ya Kanisa 58
1. Kumtukuza Mungu 59
2. Kuwajenga Waumini 61
3. Kufanya Uinjilisti. 63
SURA YA NNE 66
SERIKALI YA KANISA 66
I. Aina Anuwai za Serikali ya Kanisa 68
1. Wasiona na serikali: Quakers na Darbyites (Kwaka na Dabite) 68
2. Serikali ya Ki-Erastiani 69
3. Serikali ya Ki-askofu (Episcopal) 70
4. Serikali ya Ki-Kusanyiko (Congregationalism) 75
5. Serikali ya Ki-Kipresbiteri 78
II. Kanisa na serikali za Kiraia 86
1. Nguvu ya Kanisa 86
1. Nguvu ya serikali ya kiraia 88
SURA YA TANO 93
WATUMISHI WA KANISA 93
I. Watumishi Wasio wa Kawaida 94
1. Mitume 94
2. Manabii 96
3. Wainjilisti 98
II. Watumishi wa Kawaida 99
1. Wazee wa Kanisa 100
Sifa za mzee wa Kanisa 104
Idadi ya Wazee kwa Kila Kanisa la Mahali 107
2. Mchungaji au mwalimu 108
3. Shemasi (Dikoni au Mhudumu) 109
III. Usimikaji 111
SURA YA SITA 116
NJIA ZA NEEMA 116
I. Neno 120
II. Sakramenti 126
1. Ubatizo 134
Dhana ya Ubatizo katika Dini za Kiafrika 135
Ibada za Kuosha katika Agano la Kale 136
Ubatizo katika Dini ya Kiyahudi (Judaism) 136
Aina za Batizo Zinazojulikana katika Maandiko 137
1. Ubatizo wa Yohana 138
2. Ubatizo wa Wanafunzi wa Yesu 140
3. Ubatizo wa Kikristo 141
A. Utafiti wa Kihistoria na Nadharia za Ubatizo. 141
B. Kusudi la Kubatizwa 144
C. Njia Sahihi ya Ubatizo 146
D. Mamlaka ya Kubatiza 150
2. Meza ya Bwana 153
Utafiti wa kihistoria 153
Utendaji wa Ekaristi 162
1. Uvunjaji wa mkate 162
2. Mvinyo (divai) 163
SURA YA SABA 164
IBADA NA SIKU YA KUABUDU 164
1. Siku ya kuabudu: Jumamosi au Jumapili? 164
2. Namna ya Kuabudu 165
3. Utoaji katika ibada 167
3. Matumizi ya muziki kanisani 168
4. Kucheza kwenye ibada 170
SURA YA NANE 173
KUWA MWANACHAMA WA KANISA 173
1. Mfano wa Kanisa la Kwanza 175
2. Uwepo wa Serikali ya Kanisa 177
Marejeleo 180
Recommend Papers

EKKLESIOLOJIA: MAFUNDISHO YA KIKRISTO KUHUSU KANISA (MTAZAMO WA KIHISTORIA) [1 ed.]
 9789976572605

  • 0 0 0
  • Like this paper and download? You can publish your own PDF file online for free in a few minutes! Sign Up
File loading please wait...
Citation preview

EKKLESIOLOJIA

MAFUNDISHO YA KIKRISTO KUHUSU KANISA MTAZAMO WA KIHISTORIA

D.J. SENI 2

Hakimiliki © 2020 Daniel John Seni Chapa ya Kwanza, 2021

ISBN Msanifu: Eternal Word and Charity Publishing (EWCP) Dar es salaam [+255-755-643-590] Mchapaji: Truth Printing Press. Dar es salaam [+255764425704] ___________________________________ Haki zote zimehifadhiwa. Hakuna sehemu ya chapisho hili inayoweza kuzalishwa tena, au kuboreshwa au kusambazwa kwa njia yoyote au kwa kubadilisha umbo au kunakili na kupeleka katika umbo lingine bila idhini ya maandishi ya mchapishaji, isipokuwa kwa nukuu fupifupi kwa matumizi yasiyo ya kibiashara. Maandiko ya Biblia yamechukuliwa kutoka kwenye Biblia ya Kiswahili Toleo la shule inayotolewa na Swahili Union Version (SUV). Tafsiri iliyotumika kwenye marejeleo yaliyokuwa kwenye lugha ya kiingereza si tafsiri rasmi; hivyo inaweza kuendelea kuboreshwa kwa kila toleo la kitabu hiki. ________________________

Msambazaji Shekinah Mission Centre (SMC) [email protected] S.L.P 32807 Dar es Salaam +255 769 080 629 +255 787 907 347 Madale/Mivumoni, Joshua road, mkabala na Shule ya Msingi-Atlas/ at Shekinah Presbyterian Church in Tanzania, Dar es Salaam

TABARUKU

Kwa Wazazi wangu, John Seni na Rachel Lutelengu.

i

UTANGULIZI Ni mfululizo wa masomo katika uwanja wa Teolojia Pangilifu (systematic

Theology).

Katika

kitabu

hiki

tunashughulikia

mafundisho ya Kikristo kuhusu kanisa. Hiki siyo kitabu cha Historia ya Kanisa, bali ni mafundisho kuhusu kanisa, yaani “eklezia.” Katika kitabu hiki nimefanya uchambuzi wa kanisa kwa kuzingatia mtazamo wa kibiblia, kihistoria, na kitamaduni. Hata hivyo, mahitimisho yote yamezingatia mtazamo wa Teolojia Iliyoboreshwa au Refomati (Reformed Theology), kwani ninaamini kwamba ndio mtazamo wa Kibiblia, ingawa ama kwa hakika hauwezi kukosa changamoto. Ikumbukwe kwamba kanisa ni mojawapo ya taasisi ambayo inavutia watu wengi katika dunia hii. Na pengine, mojawapo ya sababu kuu ni kwamba kanisa lilianzishwa na Mungu mwenyewe kwa ajili ya kusudi lake maalumu. Katika muono huo, tunahitaji sasa kujua kanisa ni kitu gani, lilianzia wapi? Liliendeleaje na linaendeleaje? Kipi kinachoonesha kwamba hili ni kanisa? Zipi ni sifa anuwai za kanisa la kweli? Haya ni maswali machache ambayo yamejibiwa katika katika kitabu hiki.

Daniel John Seni Januari 2021 ii

YALIYOMO TABARUKU ............................................................................ i UTANGULIZI.......................................................................... ii SURA YA KWANZA ................................................................ 1 KANISA NA DHANA ZAKE ................................................................. 1 1.

Maana ya Kanisa .............................................................................. 1

2.

Kanisa katika Agano la Kale na Agano Jipya .................................. 4

3.

Kanisa na Ufalme wa Mungu ......................................................... 10

4.

Taswira za Kibiblia kuhusu Kanisa ................................................ 12

5.

Kanisa kama Kiumbe Hai na Taasisi.............................................. 15

SURA YA PILI ...................................................................... 16 MAENDELEO YA KANISA KATIKA NYAKATI MBALIMBALI ZA HISTORIA ............................................................................................. 16 1. Enzi za mababa wa Kanisa ................................................................. 17 2. Zama za kati za Kanisa....................................................................... 18 3. Zama za Matengenezo ya Kanisa ....................................................... 20 a.

Martin Luther ................................................................. 22

b.

Wa-Anabaptisti ............................................................... 24

c.

Wana-Refomati ............................................................... 25 iii

SURA YA TATU ................................................................... 28 AINA, SIFA, ALAMA NA MAKUSUDI YA KANISA .................... 28 Aina za kanisa ............................................................... 28

I. 1.

Kanisa la Ulimwengu na Kanisa la Mbinguni ................................ 28

2.

Kanisa linaloonekana na Kanisa lisiloonekana .............................. 28

3.

Uhusiano Kati ya Kanisa Lisiloonekana na Kanisa Linaloonekana29 Sifa za Kanisa ............................................................... 31

II. 1.

Umoja ............................................................................................. 32

2.

Utakatifu ......................................................................................... 37

3.

Kanisa la Ulimwenguni pote (Ukatoliki) ....................................... 38

4.

Utume ............................................................................................. 39

5.

Kutokuwa na Makosa kwa Kanisa ................................................. 43

III.

Alama za Kanisa ............................................................ 45

1.

Kuhubiriwa kwa Neno.................................................................... 49

2.

Kupokea kwa usahihi Sakramenti .................................................. 52

3.

Utekelezaji wa dhati wa Nidhamu ya Kanisa ................................. 52

IV.

Makusudi ya Kanisa ....................................................... 58

1.

Kumtukuza Mungu ......................................................................... 59

2.

Kuwajenga Waumini ...................................................................... 61 iv

3.

Kufanya Uinjilisti. .......................................................................... 63

SURA YA NNE ..................................................................... 66 SERIKALI YA KANISA .......................................................... 66 Aina Anuwai za Serikali ya Kanisa ..................................... 68

I. 1.

Wasiona na serikali: Quakers na Darbyites (Kwaka na Dabite) .... 68

2.

Serikali ya Ki-Erastiani .................................................................. 69

3.

Serikali ya Ki-askofu (Episcopal) .................................................. 70

4.

Serikali ya Ki-Kusanyiko (Congregationalism) ............................. 75

5.

Serikali ya Ki-Kipresbiteri ............................................................. 78 Kanisa na serikali za Kiraia .............................................. 86

II. 1.

Nguvu ya Kanisa ............................................................................ 86

1.

Nguvu ya serikali ya kiraia ............................................................. 88

SURA YA TANO ................................................................... 93 WATUMISHI WA KANISA ...................................................... 93 Watumishi Wasio wa Kawaida .......................................... 94

I.

II.

1.

Mitume ........................................................................................... 94

2.

Manabii........................................................................................... 96

3.

Wainjilisti ....................................................................................... 98 Watumishi wa Kawaida ................................................... 99

1. Wazee wa Kanisa ............................................................................. 100 v

Sifa za mzee wa Kanisa ..................................................... 104 Idadi ya Wazee kwa Kila Kanisa la Mahali ........................ 107 2.

Mchungaji au mwalimu ................................................................ 108

3.

Shemasi (Dikoni au Mhudumu) ................................................... 109

III.

Usimikaji ................................................................... 111

SURA YA SITA .................................................................. 116 NJIA ZA NEEMA ................................................................. 116 I.

Neno......................................................................... 120

II.

Sakramenti ................................................................. 126 1.

Ubatizo ......................................................................................... 134

Dhana ya Ubatizo katika Dini za Kiafrika .......................... 135 Ibada za Kuosha katika Agano la Kale ............................... 136 Ubatizo katika Dini ya Kiyahudi (Judaism) ......................... 136 Aina za Batizo Zinazojulikana katika Maandiko ................................. 137 1.

Ubatizo wa Yohana ........................................................ 138

2.

Ubatizo wa Wanafunzi wa Yesu ........................................ 140

3.

Ubatizo wa Kikristo ....................................................... 141

A.

Utafiti wa Kihistoria na Nadharia za Ubatizo. ..................... 141

B.

Kusudi la Kubatizwa ...................................................... 144 vi

C.

Njia Sahihi ya Ubatizo .................................................... 146

D.

Mamlaka ya Kubatiza ..................................................... 150 2.

Meza ya Bwana ............................................................................ 153

Utafiti wa kihistoria ............................................................... 153 Utendaji wa Ekaristi ............................................................... 162 1.

Uvunjaji wa mkate........................................................................ 162

2.

Mvinyo (divai).............................................................................. 163

SURA YA SABA ................................................................. 164 IBADA NA SIKU YA KUABUDU .................................................... 164 1.

Siku ya kuabudu: Jumamosi au Jumapili?.................................... 164

2.

Namna ya Kuabudu ...................................................................... 165

3. Utoaji katika ibada............................................................................ 167 3.

Matumizi ya muziki kanisani ....................................................... 168

4.

Kucheza kwenye ibada ................................................................. 170

SURA YA NANE................................................................. 173 KUWA MWANACHAMA WA KANISA ................................... 173 1.

Mfano wa Kanisa la Kwanza........................................................ 175

2.

Uwepo wa Serikali ya Kanisa....................................................... 177

Marejeleo ............................................................................ 180 vii

SURA YA KWANZA KANISA NA DHANA ZAKE 1. Maana ya Kanisa Kanisa ni “sehemu pendwa kuliko zote hapa duniani. “Kwa wale wanaompenda Bwana wetu Yesu Kristo, hakuna sehemu nyingine ambayo wanaweza kufurahia zaidi ya kanisani.”1 Neno la Kigiriki "ekklesia” linatafsiriwa kama “Kanisa” katika lugha ya Kiswahili. Hivyo basi Ekklesiolojia ni somo linalohusu mafundisho ya Kanisa. Neno ekklesia linaonekana mara 114 katika Agano Jipya). Kietimolojia, neno hili lina kiunganishi cha maneno mawili; 'ek,' lenye maana "nje ya" na kitenzi, kaleo, lenye maana ya "kuita" – Maneno haya yakiwekwa pamoja yanamaanisha “walioitwa kutoka nje" ikihusishwa na ile dhana ya kwamba Kanisa limeitwa kutoka ulimwenguni. Vilevile neno la hili limehusishwa na neno la Kigiriki “kyriakos,” ambalo linamaanisha "mali ya Bwana." Na baadaye kuja kujulikana kama mahali ambapo Wakristo walikutana

1

Macarthur J & Mayhue, R (Ed) A Systematic Summary of Biblical Truth: Biblical Doctrine (Wheaton, Illinois: Crossway, 2017) 739

1

kuabudu na baada ya muda lilitumiwa kama "jengo la kiroho" la Bwana.2 Toleo la Septuagint lilitafsiri neno ekklesia, “Kanisa” kama “kutano takatifu.” Na katika Matendo ya Mitume 7:38 Stefano anasema “huyu ndiye aliyekuwa katika Kanisa jangwani pamoja na yule malaika aliyesema naye katika mlima wa Sinai, tena pamoja na baba zetu; ndiye aliyepokea maneno ya uzima atupe sisi. “Neno Kanisa katika lugha ya asili ya Kiyunani limeandikwa “ekklesia”.3 Hata hivyo wanatheolojia wengi wanasitasita kukubali kushughulika etimolojia ya neno “ekklesia” wanaposhughulikia somo la Ekklesiolojia na hivyo wanapendekeza kwamba neno litafsiriwe kulingana na muktadha wake. Ambapo miktadha ifuatayo imejidhihirisha katika Agano Jipya a) Nneo

“ekklesia”

linawakilisha

mwili

wa

Kristo

ulimwenguni kote, ambapo yeye ni kichwa (Mt. 16:18; Efe. 1: 22; 1 Tim. 3:15). b) Neno “ekklesia” pia linamaanisha watu wa Mungu katika eneo maalumu (Mdo 9:31).

2

Reymond, Robert, A New Systematic Theology, (Nashville: Thomas Nelson Publishers 1998) p.387 3 Williams, Ernest. Swing, Systematic Theology: Pneumatology Ecclesiology Eschatology (Springfield: Gospel Publishing House, 1981) uk. 91

2

c) Neno “ekklesia” humaanisha kusanyiko la wakristo la Wakristo (1 Kor 1: 2; Ufu. 1:11). d) Pia neno “ekklesia” linaweza pia kuashiria kikundi cha watu wa Bwana waliokusanyika kwa ajili ibada. 4 Michael Dusing ana mawazo kama haya anaposema, “katika Agano Jipya neno Ekklesia kamwe halitumiki kumaanisha jengo wala mahali pa kukutania, lakini hurejelea watu ambao wanaabudu, wanapokea maelekezo au ushirikiano wa pamoja.”5 Kwa maana ya ujumla “ekklesia” ni jamii ya waumini wanaoshiriki katika baraka za wokovu, kwa hiyo washirika wa Kanisa “wanashiriki baraka ya wokovu” na hii ndiyo baraka kubwa kuliko baraka zote. Tukirudi nyuma kwenye Agano la Kale tunaweza kusema kwamba Adamu na Hawa kabla ya anguko hawakuwa Washirika wa Kanisa, kwa sababu hawakuhitaji mpatanishi. Malaika siyo sehemu ya Kanisa kwa maana hawakufanya dhambi na hawakuokolewa kupitia Kristo, hata shetani ingawa alimwasi Mungu, uasi wake hauhesabiki kama dhambi inayohitaji upatanisho kutoka kwa Mungu, bali yeye aliasi 4

Gordon R. Lewis and Bruce A. Demarest. Integrative Theology. Volume 3. (Grand Rapids, MI: Zondervan Publishing House, 1994), 260. 5

Michael L. Dusing, "The New Testament Church," in Systematic Theology: A Pentecostal Perspective, ed. Stanley M. Horton (Springfield, MO: Logion Press, 1995), 526.

3

moja kwa moja. Kristo ndiye ambaye hufanya jamii ya waumini kwa kuwaunganisha watu ndani Yake na kuwapa imani. Katika eneo la wokovu, Roho Mtakatifu huwaunganisha watu pamoja naye, huwatia imani ya kweli, naKwa hiyo hufanya Kanisa kama mwili wake. 2. Kanisa katika Agano la Kale na Agano Jipya Wanatheologia wenye mtazamo wa Kipentekoste huamini kwamba “hapakuwepo na Kanisa kabla ya Pentekoste ya Matendo ya Mitume sura ya pili” 6 Mwelekeo huu unashindwa kuleta mwendelezo wa familia ya Mungu kutoka Agano la Kale na Agano Jipya. Tunahitaji kuweka kwenye akili kwamba kila kitu ambacho kipo katika Agano Jipya kinao msingi katika Agano la Kale. Hata katika Habari ya Agano Jipya, Mungu alisema tazama nitafanya Agano Jipya. Maana ya Agano Jipya maana yake kuna la Zamani, na hivyo linahitaji maboresho, maana limekuwa kuukuu. Haya yapo katika Waebrania 8:13, “Kwa kule kusema, Agano jipya, amelifanya lile la kwanza kuwa kuukuu. Lakini kitu kianzacho kuwa kikuukuu na kuchakaa ki karibu na kutoweka.” Kwa hiyo tunaweza kufafanua kwamba, Kanisa lilianzia katika Agano la Kale; tofauti na Agano Jipya ni mwelekeo mpya wa Ufalme wa

6

Williams, Ernest. Swing, Systematic Theology: Pneumatology Ecclesiology Eschatology (Springfield: Gospel Publishing House, 1981) uk. 95

4

Mungu. Kwamba katika Agano Jipya Kristo anafunuliwa wazi, ambapo katika Agano la Kale ilikuwa kivuli tu. Kanisa la Mungu katika nyakati za Agano la Kale linaanzia kwenye unabii wa injili ya kwanza au Injili ya mwongozo (kilatini

“protevangelium” (Mwa. 3:15) na katika hali ya kiagano ya Mababu wa Mwanzo (Warumi 11: 28), na ikaja kuthihirika zaidi hasa kwa taifa la Israeli. Hapo awali tulidokeza kwamba, Adamu na Hawa kabla ya anguko hawakuwa Washirika wa Kanisa. Pale mwanzo wa upatanisho ulipoanza, ndipo mwanzo wa Kanisa ulipoanzia. Katika kitabu cha Mwanzo tunaona kwamba Kaini na Abeli walileta dhabihu kwa Bwana, na hii inatuthihirishia kwamba kulikuwepo na jamii ya watu waliokuwa wakiabudu. Sethi, mwana wa tatu wa Adamu na Hawa, alikuwa na mtoto wa kiume anayeitwa Enoshi. Na Maandiko yanatuambia kwamba "wakati huo (wakati wa Sethi na Enoshi) watu walianza kuliitia jina la BWANA" (Mwa. 4:26). Hivyo basi, kumekuwa na jamii ya watu duniani wakimwabudu

Mungu

wa

kweli.

Hata

hivyo,

Mungu

alipowaongoza Waisraeli kutoka Misri kukutana naye kwenye Mlima Sinai (Kutoka 19-20). Watu walipokuwa wakipiga kambi kuzunguka mlima, hawakuona umbo la Mungu, lakini mlima ulikuwa umejaa uwepo wake. Kulikuwa na ngurumo, umeme, 5

milio ya baragumu, wingu zito, moshi; mlima wenyewe ukatetemeka. Watu walipaswa kujiosha, ili kuwa safi mbele ya Mungu. Ndipo Mungu akasema nao maneno. Hii ilikuwa wakati pekee katika historia kwamba Mungu anaongea na watu wake wakiwa “wamekusanyika” na kuisikia sauti yake. Ukiendelea kusoma utaona Mungu anawapa Amri Kumi, sheria ya msingi ya agano. Watu waliposikia maneno haya, ndio wakaogopa sana. Hawakutaka kumsikia Mungu akiongea nao tena. Walimwambia Musa aseme na Mungu halafu yale maneno watayasikiliza kupitia Musa. Waliogopa kufa” (Kutoka 20:19). Hapo baadaye Katika Kumbukumbu la Torati, habari hii ilirudiwa kuelezwa kwamba mkutano huu ulikuwa ni mkutano wa kushangaza sana kati ya Mungu na watu wake. Na siku hiyo inaitwa "siku ya kusanyiko" (Kum. 9:10; 10: 4; 18:16; linganisha. 4:10). Kusanyiko kwa kiebrania ni “qahal” ambapo wakati mwingine hutafsiriwa "mkutano." Kwa maana ya awali kabisa tunaweza kusema kwamba huu ndio ulikuwa mwanzo wa Kanisa. Ilikuwa siku hii ndipo taifa la Israeli lilipokuwa taifa rasmi, taifa takatifu la Mungu, lililotengwa kutoka kwa mataifa mengine yote duniani. Mungu aliwakomboa Waisraeli kutoka Misri; ni hazina yake. Milki yake (Kutoka 19: 4-5). Wao ni ufalme wa makuhani na taifa takatifu (mst. 6).

6

Tunasikia majina haya ya Israeli, ufalme wa makuhani na taifa takatifu, katika Agano Jipya. Katika 1 Petro 2: 9, tunasoma"Bali ninyi ni mzao mteule, ukuhani wa kifalme, taifa takatifu, watu wa milki ya Mungu, mpate kuzitangaza fadhili zake yeye aliyewaita mtoke gizani mkaingie katika nuru yake ya ajabu.” Kwa hiyo Kanisa la Agano Jipya, ndilo Kanisa la Agano la Kale. Ni mali ya Mungu. Kanisa ni watu maalumu wa Mungu, mwendelezo wa Israeli. Tumeng’amua kwamba Ekklesia ni neno la Kigriki lenye maana ya “Kusanyiko la watu wa Mungu.” Agano Jipya linasema Kanisa ni Israel wa Mungu (Wagalatia 6:16). Sweet anasema kwamba “Kanisa ni 'ekklesia ya Mungu', lakini kimsingi ni ya Masihi wa Mungu.”7 Siku hizi makundi kadhaa ya wanatheologia wanatofautisha Israeli na Kanisa. Lakini ukweli ni kwamba Maandiko hufundisha kwamba watu wa Mungu ni mwili mmoja. Kuna tofauti kadhaa kati ya Israeli na Kanisa la Agano Jipya. Katika Agano la Kale Mungu aliwachagua Waisraeli kama Kanisa kule Kanaani, na katika Agano Jipya Kanisa ni mwili wa Kristo. Kanisa la Agano Jipya ni Kanisa la kimisheni limetumwa kwa sehemu zote za ulimwengu, na hekalu lake linapatikana katika miili ya waumini. Lakini kuna wokovu mmoja tu, aina moja tu ya

7

Sweet, J. P. M. A Vision for the Church (Edinburgh: T&T Clark, 1997) uk. 14

7

ahadi, ambazo zote zinatimizwa katika Yesu Kristo. Pia tunaweza kuona kwamba Kanisa la Agano Jipya linachukua majina yaleyale ambayo Mungu aliwapatia Israeli katika Kutoka 19: 5-6. Pia Kanisa la Agano Jipya, linajumuisha watu wote; Wayahudi na watu wa mataifa (Warumi 11:11-24, Efe. 2: 11- 22; 3: 6; Mdo 10; 11: 1-18). Mataifa hawahitaji kuwa Wayahudi ili waokolewe (Wagalatia 3:29). Hawahitaji kutahiriwa. Badala yake, ni watoto wa Ibrahamu kwa imani, Israeli wa Mungu (Wagalatia 6: 16), sehemu ya mwili mmoja katika Kristo (Warumi 12:13). Kuna familia moja. Familia ya Mungu. Hivyo basi, “Kanisa la Agano la Kale ni Kanisa la Kikristo ambalo limefunuliwa katika Agano Jipya. Katika Agano Jipya, Yesu ndiye kaulimbiu.”8 Watakatifu wa Agano la Kale kama vile Ibrahimu ni mifano ya imani ileile ambayo Agano Jipya linazungumzia (Warumi 4; Waebrania 11), na wanasimama kama mashahidi wa maisha ya imani. Pia ni wazi kwamba unabii wa Agano la Kale kuhusu Israeli unatimizwa katika Kanisa la sasa. Katika Yoeli 2:28–32, nabii anasema kwamba Mungu atamwaga Roho wake juu ya Israeli. Katika Matendo 2:17–21, Petro anasema kwamba Mungu ametimiza unabii huu kwa kumtuma Roho wake kuleta idadi kubwa ya kwanza ya waongofu katika Kanisa. Vivyo

8

Frame, M. John, Salvation belongs to the Lord; An Introduction to Systematic Theology (New Jersey: P&R Publishing company, 2006), uk. 1016

8

hivyo, linganisha Amosi 9:11-12 na Matendo 15:16-17, na Yeremia 31:31-34 na Waebrania 8:8–12. Hapa na mahali pengine, Maandiko yanatumia ahadi za Agano la Kale kwa Kanisa la Agano Jipya. Agano la Kale hutoa msingi wa Agano Jipya, yaani uwakilishi wa Agano la Kanisa kama “ekklesia” ya Mungu. Baada ya Yesu kukamilisha kazi yake ya wokovu kwa wanadamu, alilitenga Kanisa na kuunda mfumo wa kujitegemea ambao si wa kikundi kidogo, bali kundi kubwa. Yale mambo yahusuyo ibada kama vile kutoa sadaka za wanyama, pamoja na mengineyo yakahamishiwa rohoni. (Yoh. 4:24). Kanisa la Agano Jipya badala ya kuwa ni la sehemu moja, likawa la sehemu pote, yaani “Katholiki” lakini siyo Roman Catholic. Kwa hiyo Kanisa katika Agano Jipya linajumuisha watu wote. Tukitaka kujua ufanano wa Kanisa la Agano Jipya na lile la Agano la Kale tunaweza kusema kwamba Kanisa ni jamii ya waamini. Linaishi katika wakati uliopita, (Agano la Kale) uliopo (Agano Jipya) na litaendelea kuwepo hata kwa wakati ujao, wakati wa ukamilifu wa mwisho. Kristo atakapokuja mara ya pili atakuja kuchukua Kanisa, wakati huo Kanisa litakuwa kamili milele.

9

3. Kanisa na Ufalme wa Mungu Katika huduma yake hapa duniani, Bwana Wetu Yesu Kristo alithihirisha wazi kwamba yeye ndiye masihi na mfalme aliyeahidiwa. hata hivyo Wayahudi walimkataa kuwa yeye siye waliyemjua. Na baadaye tukisoma Maandiko kwamba Yesu aliwaambia wale viongozi wa Wayahudi kwamba, “Kwa sababu hiyo nawaambia, Ufalme wa Mungu utaondolewa kwenu, nao watapewa taifa lingine lenye kuzaa matunda yake. “(Math. 21:43). Na kwa sababu hiyo ufalme wa Kristo ukawa umeelekezwa kwa watu wote wampokeao. Ingawa ufalme wa Kristo unasubiri utimilifu wake wa baadaye, Bwana Yesu alileta ufalme wa ndani kwetu, ufalme wa kiroho (Mt. 13: 3-52; Lk. 17:20-21). Ufalme huo unaweza kufafanuliwa kama eneo la wokovu. Ni kwa wale tu ambao wamefanywa upya na Roho Mtakatifu (Yn. 3:3; taz. Mt 13: 11-16), wakiwa wametubu dhambi zao (Mt. 3: 2; 4:17; taz. 5:3) na kumkumbatia Bwana Yesu kwa imani (Mt. 19:13-14) ufalme wa Mungu unapata nafasi katika maisha yao. Agano Jipya linawaelezea waumini kama watu ambao wamekombolewa kwa maneno haya; "naye alituokoa katika nguvu za giza, akatuhamisha na kutuingiza katika ufalme wa Mwana wa pendo lake; ambaye katika yeye tuna ukombozi, yaani, msamaha wa dhambi" (Kol. 1:13-14). Kwa hawa waliokombolewa 10

wanaingizwa katika ufalme wa Mungu, yaani raia wa mbinguni (Wafilipi. 3:20-21) na wanakuwa watumwa wa kifalme katika kumtumikia Mfalme wao (taz. Mt 25:21, 23; 1 The. 2:12). Kwa hiyo, Bwana Yesu anatawala katika mioyo ya watu wake wanapotii mapenzi yake na kumheshimu yeye katika maisha yao (Tito 2:14). Ukweli mzuri wa wokovu ni kwamba, kupitia imani, wenye dhambi wanaweza kuingia katika ufalme wa Mungu ambapo Mungu wa UTATU anakaa mioyoni mwao (Yn. 14:17, 23). Ufalme wa kiroho wa Kristo unakua na kusonga mbele kupitia kuhubiriwa kwa Injili (Marko 1:14-15; taz. Mt 22: 1-14; 2 Kor. 7: 9-11), wale walio gizani wanapobadilishwa kuwa watoto wa nuru (Efe. 5: 5, 8). Injili iliyohubiriwa na Bwana ndiyo haswa "habari njema ya ufalme wa Mungu na jina la Yesu Kristo" (Mdo. 8:12; taz. Mt. 4: 23; 9: 35; 13: 19; 24:14). Watu wanabadilishwa kanisani. Kwa hiyo, kwa namna fulani, kuna uhusiano wa karibu sana kati ya ufalme wa Mungu na kanisa. Nakubaliana na Michael Dusing kwamba, “Kanisa ni kituo cha ufalme duniani, kilicho na wanadamu ambao wamezaliwa mara ya pili na wanaishi chini ya mamlaka ya Kristo, wakifanya kazi kama mabalozi wake katikati

11

ya utamaduni mwingine.”9 Na hivyo tunaweza kuthubutu kusema Kanisa la Mungu hapa duniani linasimama kama ufalme wa Mungu. 4. Taswira za Kibiblia kuhusu Kanisa Agano Jipya hutumia vielelezo vingi kuonyesha uhusiano wa Mungu na watu wake. Yeye ndiye Mfalme wao; wao ni raia wake (Mt. 25:34; 1 Kor. 4:20; Fil. 3:20; Kol. 1:13-14). Yeye ndiye Muumba; wao ni viumbe vyake (2 Kor. 5:17; Efe. 2:10). Yeye ndiye Mchungaji wao; hao ni kondoo wake (Yn. 10:3, 11, 14, 26; Ebr. 13:20; 1 Pet. 2:25; 5: 2-4). Yeye ndiye Bwana, na wao ni watumwa wake (Mt. 10: 24-25; Rum. 14: 4; Efe. 6: 9; Kol. 4: 1; 2 Tim. 2:21; Yuda 4). Yeye ndiye Baba yao (Mt. 6: 9; Rum. 1: 7); na wao ni watoto wake anaowalea (Yn. 1:12; Rum. 8: 16-17, 21; Fil. 2:15; 1 Yoh. 3: 1-2; taz. Rum. 8:14, 19; 2 Kor. 6: 18; Gal. 3:26; 4: 6; Ebr. 12: 7) wamefanywa wana (Gal. 6:10; Efe. 2:19; 1 Tim. 3:15; 1 Pet. 4:17), na kwamba Bwana Yesu "haoni haya kuwaita ndugu" (Ebr. 2:11) na "Mungu haoni haya kuitwa Mungu wao" (Ebr. 11:16).

9

Michael L. Dusing, "The New Testament Church," in Systematic Theology: A Pentecostal Perspective, ed. Stanley M. Horton (Springfield, MO: Logion Press, 1995), 542.

12

Kanisa linaelezewa zaidi kama bibi arusi wa Kristo (2 Kor. 11: 2; Efe. 5: 23-32; Ufu. 19: 7-8; 21: 9) na mwili wa Kristo (Rum. 12: 4-) 5; 1 Kor. 12:12, 27; Efe. 4: 12,25; 5:23, 30; Kol. 1:24), ambapo yeye ni Kichwa (Efe. 1:22-23; 4:15.; Kol. 1:18; 2:19). Taswira zote hizi zinasisitiza muungano wa kiroho uliopo kati ya Kristo na watu wake (taz, Gal. 2:20). Maandiko yanazungumza juu ya waamini kuwa ndani ya Kristo na Yeye kuwa ndani yao (Yn. 17:23; linganisha. 2 Kor. 5:17; Kol. 1:27). Bwana Yesu ni zaidi ya kuwa pamoja na Kanisa; bali Yeye yuko ndani ya Kanisa, na Kanisa lake liko ndani yake. Kanisa ni udhihirisho hai wa Yesu Kristo katika maisha ya milele ya Mungu. Sifa kubwa ya Waumini wote ni kwamba wanamiliki maisha ya kimungu. Yesu alisema, "Kwa sababu mimi ni hai, nanyi pia mtakuwa hai" (Yn. 14:19). Maandiko mengine ya Agano Jipya yanarudia ukweli huo: "Yeyote aliye na Mwana ana uzima" (1 Yoh. 5:12), kwa sababu " Lakini yeye aliyeungwa na Bwana ni roho moja naye. "(1 Kor. 6:17). Taswira ya mwili ni ya kipekee katika kuonyesha uhusiano kati ya Kristo na Kanisa. Mungu aliumba mwili wa mwanadamu kama kiumbe wa ajabu sana, chenye uhusiano wa hali ya juu na maelewano naye. Kuna mashirika mengi ya kidini, lakini Kanisa tu, ndio mwili wa Kristo, ambapo kila mwamini wa kweli wa Kristo ni mshiriki. Bwana Yesu hawezi kutengwa na Kanisa lake kama ambavyo kichwa hakiwezi kutengwa na mwili wake. 13

Kinyume chake, wale ambao ni sehemu ya Kanisa lake hawawezi kutenganishwa naye (Yn. 10: 28-29; Rum. 8: 38-39) Mfano mwingine wa Agano Jipya ambao unaonyesha umoja muhimu ambao waumini hushiriki na Kristo ni ule wa mzabibu na matawi (Yn. 15: 1-11; taz. Rum. 11:17). Kwa njia ileile ambayo tawi hutegemea kabisa mzabibu kwa maisha yake, lishe, na ukuaji, Kwa hiyo waamini wanategemea kabisa Mwokozi kama chanzo cha nguvu zao za

kiroho.

Tawi ambalo

halijaunganishwa na mzabibu haliwezi kuzaa matunda. Vivyo hivyo waamini hawawezi kuzaa matunda ya kiroho wakiwa nje ya Kristo (Yn. 15: 4-10). Ni kwa kukaa ndani yake tu ndipo Wakristo wanaweza kuonyesha matunda ya toba (Math. 3: 8) na tunda la Roho (Gal. 5: 22-24; Efe. 5: 9). Ushirika wa karibu ambao Kanisa hufurahia na Mungu kupitia Kristo (Yn. 17:21; 1 Kor. 1: 9; 1 Yoh. 1: 3; 2:24) unaonyeshwa zaidi na maelezo ya Agano Jipya ya Kanisa kama “hekalu la Mungu.” Katika Agano la Kale, hekalu lilikuwa kitovu cha ibada kwa Waisraeli. Ilikuwa mahali ambapo watu wa Mungu walienda kumwabudu kupitia upatanishi wa kuhani. Pazia lilitenganisha watu kutoka Mahali Patakatifu pa Patakatifu ambapo uwepo wa Mungu ulidhihirishwa (Kut. 26: 31-35). Lakini Agano Jipya linafunua kwamba waumini wenyewe ni hekalu la Mungu na kwamba kila Mkristo anaweza kumfikia Mungu kupitia Kristo 14

(Ebr. 4:14-16; 10:19-23). Baada ya kujengwa juu ya msingi wa Bwana Yesu (1 Kor. 3: 10-11; 1 Pet. 2: 7), Wakristo wanaelezewa kama mawe hai ambao hufanya hekalu la Mungu (1 Pet.2:4-8). Wanaelezewa pia kama ufalme wa makuhani (1 Pet. 2: 9-10; Ufu. 1: 6; 5:10). Mtume Paulo anatumia taswira ya hekalu kuwaonyesha waamini kibinafsi (1 Kor. 6: 19-20 na kijumuiya (1 Kor. 3: 16-17; Efe. 2: 21-22). Kristo ndiye mjenzi (Mt. 16:18); waumini ni jengo (Efe. 2: 20-22; taz. Ebr. 3: 3-6). Kanisa, basi, ni jengo la kiroho (1 Pet. 2: 5), makao ya Roho Mtakatifu (1 Kor. 3: 16-17; 2 Kor. 6:16), mahali ambapo utukufu wa Mungu unadhihirishwa wazi kabisa hapa duniani, na kiini cha mafundisho ya kiroho na ibada ya pamoja

kwa

waliokombolewa.

Tofauti

na

majengo

yaliyotengenezwa kwa mawe, Kanisa ni jengo lililotengenezwa na nyama hai. Waumini ni mawe yaliyo hai katika hekalu la Mungu (taz. Rum 12: 1; Ebr. 13: 15-16) 5. Kanisa kama Kiumbe Hai na Taasisi Calvin na Luther walikubaliana na Wakatoliki kwamba Kanisa ni jamii iliyokusanyika (coetus) na mama wa waumini (mater fidelium),10 na kwamba Kanisa kama kiumbe hai ni jamii ya waumini ambapo Washirika wake wameunganishwa na kamba ya 10

Bavinck, Herman, Reformed Dogmatics (p. 607). Baker Publishing Group. Kindle Edition.

15

Roho Mtakatifu, lakini Kanisa kama taasisi lina ofisi. Kanisa kama kiumbe linalinganishwa na mwili wa mwanadamu (Rum.12: 5; 1Kor.12: 13), lakini Kanisa kama taasisi iliyo na jengo (Mt.16:18; Efe.2: 20-22). Kanisa kama kiumbe na Kanisa kama taasisi halionyeshi makanisa mawili tofauti lakini tabia mbili za Kanisa linaloonekana.

SURA YA PILI MAENDELEO YA KANISA KATIKA NYAKATI MBALIMBALI ZA HISTORIA Kupitia historia ya Kanisa, tunaweza kuona namna Kanisa lilivyotambuliwa katika nyakati tofautitofauti. Kila kipindi watu walikuwa na msisitizo fulani kuhusu Kanisa. 16

1. Enzi za mababa wa Kanisa Mababa wa Kanisa la kwanza walifafanua Kanisa kama mkutano wa waumini waliochaguliwa. Hii ndio ufafanuzi wa msingi na wa kawaida wa Kanisa. Wakati waasi walipoonekana katika nusu ya mwisho ya karne ya pili, kwanza, Kanisa la Othodoksi lilizingatia tabia za nje za Kanisa zilivyokuwa. Kwa maana huwezi kujua tabia za ndani bila kuzingatia tabia za nje. Sifa za nje za Kanisa ilikuwa ni pamoja na: Kwanza, Kanisa lazima liwe chini ya uangalizi wa askofu (episcopos), ambaye alikuwa mrithi wa mtume na mmiliki wa mapokeo. Pili, Kanisa la Othodoksi lilisisitiza umoja wa Kanisa dhidi ya jaribio la wazushi la kutenganisha Kanisa lao la kweli. Wakati Montanus katika karne ya pili, Novatiaus katika karne ya tatu, na Donatus katika karne ya nne walipoonekana kusisitiza utakatifu wa Kanisa hilo kibinafsi, Kanisa la Othodoksi walitumia mfumo wa kiaskofu dhidi ya changamoto hizi. Walisisitiza umoja wa Kanisa linaloongozwa na uaskofu. Watu ambao walishindwa kutii maagizo ya kiaskofu, walionekana kuwa nje ya Kanisa. Augustino alisisitiza kwamba Kanisa ni kusanyiko la watakatifu waliochaguliwa kwa upande mmoja, lakini aliunga 17

mkono maoni ya kwamba askofu ndiye mrithi wa mitume kwa upande mwingine. Augustino alikubali kwamba kuna makapi (watu ambao hawakuchaguliwa) na pia ngano (watu ambao walichaguliwa) katika Kanisa linaloonekana. Maganda na makapi vinakua pamoja katika Kanisa linaloonekana. Kanisa huwa takatifu kila wakati, hata mabaki yanajumuishwa kanisani, kwa kuwa utakatifu haupatikani katika Washirika wa Kanisa lakini katika mafundisho, njia za neema, huduma za ibada nk. Kwa maana hii, tunaweza kusema kwamba hakuna wokovu nje ya Kanisa linaloonekana. Kwa hiyo maoni ya Augustino juu ya Kanisa yaliweka msingi wa mafundisho kwamba Kanisa la kidunia ndio ufalme wa Mungu. Na bila askofu hakuna Kanisa. Wazo ambalo baadaye liliungwa mkono na John Calvin ambap kwake askofu ni mzee au mchungaji. Ingawa ni hoja ya kujadiliwa, hata hivyo inayo mapungufu mengi, hasa tunaporudi nyuma na kuangalia maana ya Kanisa.

2. Zama za kati za Kanisa Katika zama za kati, mafundisho kuhusu Kanisa yalibuniwa si kitheolojia bali kihalali (kisheria). Ukuaji huu wa kisheria wa kikanisa ulisababisha Kanisa kuanzishwa kama taasisi. Kwa mujibu wa Hugo kutoka kundi la Mtakatifu Victor, Kanisa na serikali zilianzishwa na Mungu. Kanisa ni mamlaka iliyoanzishwa kwa ajili ya wokovu wa mwanadamu, na serikali kwa upande 18

mwingine ilianzishwa kwa ajili ya ustawi wa watu. Lakini Kanisa ni bora kuliko serikali. Kichwa cha Kanisa ni papa, wakati kichwa cha serikali ni Kaisari (Mfalme). Gregory VII aliweka wazi ukuu wa papa juu ya Kaisari kwa kusisitiza kwamba papa ni jua, lakini Kaisari ni mwezi tu. Kanisa linajumuisha makuhani na watu wa kawaida. Katika kipindi hiki yaliendelezwa mawazo kwamba Kanisa haliwezi kukosea chochote, “na ukweli huu ulidumishwa hasa kwa kukaza uaminifu wa maaskofu, na katika mabaraza ya Kanisa.”11 Maana yake ni kwamba kama maaskofu, wakifanya maamuzi kupitia baraza la Kanisa, maamuzi yao ni kama maamuzi ya Mungu, na hivyo hakuna mtu yeyote anayeweza kuyapinga. Kwa sababu Kanisa lina nguvu ya Mungu kupitia wawakilishi wake. Na ikiwa Papa atafanya maamuzi yoyote, kwa kuwa yeye ni mwakilishi wa Mtume Petro hapa duniani, basi maamuzi yake hayana makosa na yanapaswa kupokelewa na waamini wote. Hiyo ndiyo nguvu ya Kanisa. Ekklesiolojia ya Kanisa Romani Katoliki ilionyesha matokeo matatu. Kwanza, familia, shule, sayansi, sanaa, biashara, na viwanda ziko chini ya usimamizi wa Kanisa. Pili, baraka zote za wokovu zinatambuliwa hutolewa kupitia maagizo ya Kanisa, i.e.,

11

Berkhof, Louis. Systematic Theology (Grand Rapids: Eerdmans 1974), uk. 623

19

Sakramenti. Tatu, Kanisa likawa la kidunia zaidi; mfano Kanisa lilikuja kujiingiza kwenye siasa zaidi kuliko kushughulikia masuala ya wokovu. Wakati huo hapakuwa na tofauti kati ya Kanisa na siasa, vyote vilienda pamoja. Papa alipotaka mji fulani uwe wa Kikristo, alimwamrisha Kaisari ili watumie nguvu kuwalazimisha watu kubatizwa. Utake usitake, wakati huo ilikuwa ni lazima kuamini kwa sababu Kanisa lilitumia nguvu ya dola kufanya watu waamini. Ama kwa hakika Kanisa lilipoteza ushawishi kwa watu wa nje. Ukuzaji wa taasisi za kikanisa kulisababisha kuinuka kwa madaraka makubwa na wakati mwingine kujaribu kupotosha maana halisi ya Kanisa.

3. Zama za Matengenezo ya Kanisa Wanamatengenezo waliachana na wazo la Wakatoliki na kuonesha tofauti kadhaa katika kujaribu kuelezea Kanisa. Kwa Luther na Calvin, Kanisa lilikuwa jamii ya watakatifu, ambayo ni, jamii ya wale wanaomwamini na kutakaswa katika Kristo, na ambao wameungana na Yeye kama Kichwa chao.12 Mawazo haya yalikuwepo kwa Agostino, mojawapo ya mababa wa muhimu wa Kanisa. Hii ni maana ambayo hata Wakatoliki wanakubaliana, lakini shida kubwa ya Katoliki ni mkazo katika taasisi za Kanisa 12

Berkhof, Louis. uk. 624

20

na kulingezea haki Kanisa. Kwa hiyo Wanamatengenezo hawa walilinyima Kanisa haki ambayo Wakatoliki walilipa na kuliinua kupita kiasi. Hebu ngoja tujaribu kutalii haki kadhaa ambazo Kanisa lilipewa na Wakatoliki: Kwanza, Kanisa Katoliki lilikuwa na haki ya kuamua ikiwa andiko fulani ni canon au la. Hii inamaanisha kwamba ikiwa Maandiko fulani yalikuwa yanaenda kinyume na tamaduni yaliweza kuondolewa, na ikiwa Maandiko fulani hata kama si ya asili na yanaenda kinyume na Canon basi yaliongezwa kuwa sehemu ya Biblia. Na ndiyo maana Biblia ya Wakatoliki ina vitabu saba zaidi kuliko Biblia ya Wanamatengenezo. Hivyo basi Wanamatengenezo waliamini kwamba Maandiko ndiyo asili ya mamlaka yote, pamoja na mamlaka ya Kanisa. Huku Wakatoliki wakiamini kwamba Kanisa lina mamlaka hata juu ya Maandiko Matakatifu. Maana yake ni kwamba Kanisa linaweza kukosoa Maandiko. Pili, Kanisa Katoliki lilisisitiza kwamba Kanisa Katoliki ndiye mpatanishi kati ya Kristo na waumini, na linaweza kutangaza kwamba waumini fulani ni wenye haki au la. Kitendo hiki kiliweza kumfanya kuhani wa Kikatoliki kutangaza msamaha kwa watu na kuzuia msamaha kwao. Tunadhania kwamba ni tafsiri ya

Yn.

20:23,

wameondolewa;

na

“Wowote wo

wote 21

mtakaowaondolea

dhambi,

mtakaowafungia

dhambi,

wamefungiwa.” Hata hivyo andiko hili linapaswa kusomwa kwa kuzingatia muktadha wake. Ukisoma mstari 21 Yesu anawaambia kwamba

“kama

alivyotumwa

na

Baba

yake,

“ndivyo

anavyowatuma wanafunzi wake. Mstari wa 22 Yesu anawaambia wapokee Roho Mtakatifu; na ndipo tunaona mstari wa 23 unaeleza kuhusu nguvu ya kusamehe dhambi. Kwa kuwa msamaha wa dhambi unapatikana kwa Kristo peke yake, wanafunzi wa Yesu walikuwa wametumwa ulimwenguni (Yn 20:21) kwa maana ya kwamba wasipoenda kuhubiri Injili watu walio gizani hawawezi kupokea msamaha wa dhambi. haimaanishi nguvu binafsi ya mtumishi yeyote. Wanamatengenezo walifafanua wazi kwamba mtu hawezi kupatanisha Mungu na Mwanadamu. Kwa sababu, “Kwa sababu Mungu ni mmoja, na mpatanishi kati ya Mungu na wanadamu ni mmoja, Mwanadamu Kristo Yesu;” (1 Tim. 2:5). Wana

matengenezo

walisisitiza

kwamba

Kanisa

haliwezi

kusimama badala ya Kristo. Na kwamba mwanadamu anaweza kuwa mwadilifu kupitia imani peke yake, kwa neema pekee na bila kulipa gharama yoyote. a. Martin Luther Luther alifikiria kwamba Kanisa la kidunia (Kanisa Romani Katoliki wakati wa Luther) halikuwa ufalme wa Mungu usio na kosa. Luther alikosoa maoni ya Kanisa Katoliki kuhusu Kanisa hilo kwamba makuhani pekee wanaweza kuokoa watu kwa 22

kushika Sakramenti. Alisisitiza kwamba Kanisa ni kusanyiko la kiroho linalojumuisha waumini. Luther alilitofautisha Kanisa, yaani Kanisa lisiloonekana na Kanisa linaloonekana, kisha, alifafanua Kanisa lisiloonekana kama Kanisa la ulimwenguni linalojumuisha waumini, na akaelezea Kanisa linaloonekana kama muundo wa nje kwa Neno na Sakramenti. Walakini, tofauti ya Luther kati ya Kanisa lisiloonekana na Kanisa linaloonekana haikukusudia kusema juu ya makanisa mawili tofauti lakini kusema juu ya athari za Kanisa moja katika hali mbili.

Yeye alikaza kwamba siku zote kuna

wacha Mungu na wabaya katika Kanisa linaloonekana. Luther alieleza kuwa umoja na utakatifu wa Kanisa sio katika ushirika wa watakatifu bali katika Kanisa kama taasisi na kwa kushika Neno na Sakramenti. Hapa pana changamoto kwa Luther kwa sababu anaona utakatifu wa Kanisa katika taasisi zake pia. Na hili linatuthihirishia wazi kwamba Luther hakuacha dhana ovu za Kanisa Katoliki kuhusu Kanisa. Kuna maeneo mengi Luther alikuwa sahihi, kwa mfano alipinga kwa usahihi maoni ya Kanisa Katoliki kwamba Kanisa hilo linapaswa kutawala serikali, lakini kitu cha kushangaza kidogo alisisitiza kwamba haki zote isipokuwa haki ya kutangaza Neno la Mungu ni haki ya serikali.

23

b. Wa-Anabaptisti Kwa kifupi sana nitasema juu ya kikundi hiki ndani ya wanamatengenezo. Waanabaptisti inatokana na neno la Kilatini “anabaptista,” na hapa pana maneno mawili “ana” na baptismos,” neno la kwanza “ana” inamaanisha "tena" baptismos, "ubatizo."13 Kwa hiyo tunapata neno “batiza tena.” Hawa walisusia na kukataa ubatizo jinsi ulivyotolewa na Kanisa Katoliki na madhehebu mbalimbali ya Uprotestanti. Kweli wenyewe hawapendi kuitwa hivyo kwa madai kwamba hawarudii ubatizo, bali wanautoa kwa usahihi kwa mara ya kwanza. Nimeona niwatambulishe kidogo kwako uweze angalau kuwafahamu kwa uchache. Nizungumze kidogo dhana yako kuhusu Kanisa. Wa-Anabaptisti walitupilia mbali hoja ya Luther ya kwamba wasioamini hupatikana katika Kanisa linaloonekana na walisisitiza kwamba Kanisa linaloonekana lina waumini wa kweli peke yao. Kwa maelezo yao mtu yeyote anayeonekana kanisani ni Mkristo wa kweli kabisa na hakuna wanafiki kanisani. Kwa kuongezea, walisisitiza kwamba Kanisa linaloonekana na serikali zinapaswa kuwa tofauti kabisa. Kwa upande wa kutofautisha kati ya serikali na Kanisa walikuwa sahihi kwa namna fulani, ingawa serikali na Kanisa vina uhusiano wa karibu na kutegemeana kwa 13

"Anabaptism, n.", Oxford English Dictionary (Oxford University Press), December 2012, retrieved 21 January 2013

24

namna fulani. Lakini kutegemeana huku si katika masuala ya kiutendaji ya Kanisa. c. Wana-Refomati Tunaposema “wanareformati”14 tunamaanisha kundi kubwa la wanatheolojia waliojipambanua kwa kufanya maboresho makubwa katika Nyanja ya theolojia. Walifafanua uhusiano kati ya Kanisa lisiloonekana na Kanisa linaloonekana kutoka kwa mtazamo wa uchaguzi (election). Kwa mfano Zwingli, mojawapo ya wana-Refomati aliamini kwamba Kanisa ni mkutano wa watu waliochaguliwa. Calvin, Mwana-Refomati alitofautisha kati ya Kanisa lisiloonekana, kwamba lina watu waliochaguliwa ambao Mungu pekee anawajua na Kanisa linaloonekana, linajumuisha wanafiki. Wakati Walutheri wakiamini kwamba ushirika na utakatifu wa Kanisa upo katika maagizo na utunzaji wa Neno na Sakramenti, Calvini alisisitiza ushirika wa kibinafsi wa waumini. Vilevile Calvin aliliona kanisa kama chombo cha neema ya Mungu. Kanisa kama taasisi halidhibiti wokovu au neema, lakini linaweza tu kutangaza Injili na kuhubiri kwamba wokovu unawezekana kupitia neema katika Yesu Kristo. Herman Bavinck anasema kwamba “Wana-Refomati walisisitiza kwamba watu wa Mungu wapo pale ambapo Neno la 14

Kwa kiingereza hawa wanaitwa “Reformed Theologians.”

25

Mungu liliko, lakini Kanisa linaweza kuwepo hata pale ambapo hakuna kuhani au papa, mchungaji au askofu. Walakini, Kanisa kama mkusanyiko wa waumini linao mfumo wake kimuundo.”15 Hii inatuelekeza kwamba Kanisa haliwezi kufanya kazi zake bila serikali yake (yaani muundo wa kiserikali). Kama vyombo vingine, Kanisa haliwezi kuwa na mamlaka ya kuongoza bila kuwepo na muundo maalumu. Hata hivyo, mamlaka ya mwisho kwa Kanisa ni Kristo, kama Mpatanishi, Kuhani na Nabii wa milele. Na kwamba anatawala Kanisa lake akiwa ameketi mkono wa kuume wa Mungu Baba Mwenyezi. Ukiangalia hapo, hata miongoni mwa wana Refomati kulikuwa na mawazo tofauti. Nukuu ya Bavink inaenda kinyume na kile ambacho Calvin aliamini. Niliwahi kudokeza kule nyumba kwamba Calvin aliamini pasi na askofu hapana Kanisa, na kwamba kwake askofu alikuwa anaamanisha mchungaji. Lakini nukuu ya Bavink inaonesha si lazima askofu awepo ili Kanisa liwepo. Na huu ndio ukweli halisi, kwamba Kanisa si lazima awepo askofu/mchungaji au mtu mwingine yeyote yule bali Kristo kama kichwa ndiye wa muhimu; kwani hakuna kitu kinachoishi ambacho kinaweza kuishi bila kichwa. Na kwa kuwa Kanisa li hai, na kichwa cha Kanisa ni Kristo, basi popote pale palipo na Kristo

15

Bavinck, Herman. Reformed Dogmatics (p. 608). Baker Publishing Group. Kindle Edition.

26

ndipo palipo na Kanisa. Hakuna Kristo hakuna Kanisa, na si kinyume chake.

27

SURA YA TATU AINA, SIFA, ALAMA NA MAKUSUDI YA KANISA Kuna uainishiaji wa aina mbalimbali wa makanisa. Ninaainisha makanisa kwa kuzingatia wana-Refomati (au hata Waprotestanti wengine wenye mawazo kama hayo) I. Aina za kanisa 1. Kanisa la Ulimwengu na Kanisa la Mbinguni Kanisa la ulimwengu huu mara nyingine huitwa Kanisa lenye mapigano makali. Liko kwenye mapigano ya kiroho dhidi ya nguvu ovu za Ibilisi. Kanisa la mbinguni ni Kanisa ambalo lilishinda vita takatifu ya kiroho. Vita vya kiroho vinaisha. Kanisa linashinda vita vyake. Watakatifu wanatawala ulimwengu milele pamoja na Kristo. Kanisa la mbinguni ni Kanisa kamili kama nilivyodokeza

huko

nyuma

wakati

nazungumzia

juu

ya

mwendelezo wa Kanisa kutoka Kanisa la Agano la Kale na Agano Jipya. 2. Kanisa linaloonekana na Kanisa lisiloonekana Kanisa linaloonekana ni Kanisa ambalo linaonekana kwa macho ya kibinadamu kupitia kukiri kwa imani, mahubiri ya neno la Mungu, kushiriki Sakramenti, na miundo ya kitaasisi na mifumo 28

ya kisiasa. Kanisa linaloonekana ni Kanisa lenye serikali yake, na inaonekana wazi. Kanisa linaloonekana linajumuisha wanafiki (wale ambao hawajaitwa), watu ambao wamejiingiza kwa siri. Kwa sababu sisi hatuwezi kuwatambua wanafiki, basi wataendelea kuwepo ndani ya Kanisa linaloonekana, na hata wataonyesha sifa za kuwa Wakristo wema, lakini ni Yesu peke yake anawafahamu. Kanisa lisiloonekana ni Kanisa bora na kamili ambalo litafunuliwa katika siku ya mwisho, linapatikana kila mahali katika ulimwengu wote, na haliwezi kuonekana machoni pa wanadamu. Kanisa hili halina wanafiki. Limetakaswa kabisa. Halina uchafu wa aina yoyote ile kwa sababu anayelijua ni Kristo peke yake. Hili ni Kanisa la wateule pekee. Tofauti na Kanisa la mbinguni ni kwamba Kanisa hili nalo lipo duniani lakini anayelijua ni Kristo peke yake. Hata hivyo tunapaswa kukumbuka kwamba Kanisa linaloonekana na Kanisa lisiloonekana haionyeshi makanisa mawili tofauti lakini nyanja mbili za Kanisa moja la Yesu Kristo. 3. Uhusiano Kati ya Kanisa Lisiloonekana na Kanisa Linaloonekana Tunaweza kusema kwamba Kanisa la kidunia la sasa ni Kanisa linaloonekana na Kanisa lisiloonekana. Kwa maana ya kwamba haliwezi kuonekana machoni pa wanadamu, na kwamba;

29

kwanza, ni la kiroho, na, pili, haiwezekani kujibu swali la kwamba nani hayupo kwenye Kanisa hilo. Lakini, kama vile roho ya mwanadamu inavyochukua mwili

na kujielezea

kupitia mwili,

vivyo

hivyo

Kanisa

lisiloonekana huchukua umbo linaloonekana. Kwa maneno mengine, Kanisa lisiloonekana linaonekana wazi kupitia kukiri na mazoezi ya imani, Neno la Mungu na kufanya Sakramenti, na mifumo ya kisiasa. Lakini makanisa haya mawili hayafanani kila wakati. Kwa mfano

kuna wakati

Washirika wa Kanisa

lisiloonekana huwa sio Washirika wa Kanisa linaloonekana kwa mfano, mtu anayetubu wakati wa kifo, huyu hakuwa mshirika wa Kanisa linaloonekana au mtu ambaye alitengwa kwa muda mrefu lakini ni mshirika wa Kanisa lisiloonekana, lakini aliondolewa katika Kanisa linaloonekana. Kung Hans, anafafanua uhusiano wa Kanisa linaloonekana na Kanisa lisioonekana kwa maneno yafuatayo; “Kanisa halisi ni Kanisa tunaloamini, na bado linaonekana, lakini wakati mwingine Kanisa hilohilo kwa wakati mmoja halionekani. Sifa zake za kuonekana zina sura ya ndani isiyoonekana sawa. Sifa zake za kutokuonekana zina sifa za ndani zilizofichwa. Sifa zinazoonekana za Kanisa hudhibitiwa na sifa zisizonekana. Hii inamaanisha kwamba Kanisa kimsingi ni zaidi ya kile kinachoonekana. Sio watu wa kawaida au kikundi, lakini watu waliochaguliwa; sio 30

mwili wa kawaida, lakini mwili wa fumbo; sio jengo la kawaida, lakini jengo la kiroho.”16 Kuna umuhimu wa kuelezea kidogo hapa kwamba kuelezea aina ya makanisa kwa namna hii haifanyi mtu aanze kujitafakari kwamba yeye yuko kwenye Kanisa gani. Sisi hatuwezi kujua kwamba mtu fulani yupo upande wa Kanisa lipi, ni Mungu peke yake. Na kwa kuwa ni Mungu peke yake, basi sisi tunachoweza kuangalia ni Kanisa linaloonekana peke yake, na tunatumia sifa hizo za Kanisa linaloonekana kujaribu kujua sifa za Kanisa lisiloonekana. Kwa hiyo, wale wote walioitwa na Mungu katika wokovu ni Washirika wa Kanisa lisiloonekana. Wacha nikutoe wasiwasi, kwamba kwa kweli, tunahakikishwa kwa Imani tuliyo nayo katika Bwana kwamba tupo katika Kanisa lipi. Kwani sifa kubwa bado ni ileile, kumwamini Kristo, ingawa imani siyo yako, inaotoka kwake, kwa sababu amekuchagua. Uaminifu wako katika Kanisa linaloonekana pengine unaweza kuonesha wazi kwamba wewe ni muumini wa Kanisa lisiloonekana pia. II. Sifa za Kanisa Kanisa Katoliki hupata sifa za Kanisa katika mashirika ya Kanisa lake, lakini Kanisa la Kiprotestanti linapata sifa za msingi katika Kanisa lisioonekana, na sifa zingine ni katika Nyanja za 16

Kung, Hans, The Church (New York, sheed and ward, 1967) uk. 37

31

taasisi zake. Ukristo wa Kiprotestanti hubainisha sifa zifuatazo: umoja, utakatifu, ukatoliki na utume. Kanisa Katoliki wanaongeza sifa ya “kutokuwa na makosa kwa Kanisa.” Nitafafanua kwanza sifa nne za Waprotestanti, nikilinganisha kwa namna fulani na Kanisa Katoliki, na kisha nitafafanua ile sifa moja ambayo inapatikana kwa Wakatoliki. 1. Umoja Kanisa la Kiprotestanti hupata sifa ya Umoja wa Kanisa katika Kanisa lisiloonekana. Yaani linaona umoja wa Kanisa wa ndani na wa kiroho: umoja wa mwili wa Kristo. Mwili ambao unajumuisha waumini unaongozwa na Yesu Kristo, kichwa kimoja na Mfalme wa Kanisa, ukiendeshwa na Roho wa Kristo, umefungwa na imani ya pamoja na upendo, na una maono ya pamoja ya siku zijazo. Vivile Waprotestanti hupata kamba ya umoja wa Kanisa sio katika mfumo wa Kanisa lakini kwa Neno, Sakramenti na Nidhamu. Tofauti na Kanisa Katoliki ambalo linaona umoja wake katika mfumo wa Kanisa; kwa kuzingatia mashemasi, mapadri, maasikofu, makardinari na Papa. Kanisa la Kiprotestanti hupata umoja wa Kanisa sio tu katika umoja wa Kanisa lisiloonekana peke yake bali pia katika Kanisa linaloonekana. Tunaweza kujua hili tukisoma Maandiko. Kwa mfano wakati Paulo alipolinganisha Kanisa na mwili, 32

alikumbuka makanisa ya mahali hapo (1Kor.12, 12-31) kama Kanisa la Korintho (1Kor.12: 12-31) au Kanisa la Efeso ambalo lilichagua watumishi (maafisa). Kwa sababu makanisa yote ya mahali

pamoja

(Local

Churches)

ambayo

ni

makanisa

yanayoonekana tayari ni Kanisa moja, Kanisa la Yerusalemu lilisaidia Kanisa la Antiokia, lilipokabiliwa na shida ya mafundisho (Mdo 15), na, kwa upande mwingine, makanisa mengine kama makanisa ya Makedonia na Kanisa la Korintho yalilisaidia Kanisa la Yerusalemu lilipokabiliwa na shida ya kiuchumi. Kwa hiyo basi tunasema kwamba katika ulimwengu wa roho Kanisa ni moja na halina mgawanyiko wowote. Na tuseme tena

kwamba

hasa

tunauona

umoja

huu

katika

Kanisa

lisioloonekana. Kila tunapokaza kuhusu umoja wa Kanisa, Kanisa Katoliki hupenda kuuliza mbona makanisa ni mengi sana siku hizi? Kwa nini kuna mgawanyiko ndani ya Kanisa? Tungependa kusema kwamba mgawanyiko wa Kanisa umetokea na hutokea kwa sababu ya mafundisho ya uongo ndani ya Kanisa au mapigano ya nguvu ya kisiasa, na ni dhambi kubwa ambayo inaharibu umoja wa Kanisa. Lakini pia ni ujinga na upumbavu wa hali ya juu kujaribu kuunganisha makanisa ya uongo ili kuwa Kanisa moja na kujaribu kuzidi nguvu ya kiasiasa ya Kanisa Katoliki. Wakati wa matengenezo, hata Martin Luther hakutaka kuondoka katika Kanisa Katoliki, lakini mazingira yalimlazimisha kuondoka, 33

alifukuzwa na Kanisa Katoliki kwa sababu ya kusimama kwenye sehemu ya ukweli wa neno la Mungu. Kwa kweli hatuwezi kuunganisha makanisa ya uongo ili tupate nguvu ya kisiasa. Kuna majaribio kadhaa ambayo yamefanyika kuunganisha madhehebu yawe kitu kimoja, kwa mfano jaribio moja la kipuuzi la kuunganisha makanisa ni jaribio la WCC (World Council of Churches) kuwaunganisha makanisa ya uongo ingawa makanisa mengine yana mafundisho potofu. Umoja wa aina hii hutoa tabia na taswira mbaya kwa Kanisa, na zaidi Kanisa la kweli kupoteza sifa zake. Huharibu utambulisho wa Kanisa, na kwamba Kanisa haliwezi kuonekana katika hali yake. Kwa hiyo, hata katika kujiunga na umoja wa makanisa ni lazima tujaribu kuangalia imani ya makanisa mengine, na ikiwa imani yetu inatofautiana sana na makanisa yaliyo ndani ya umoja huo ni heri kutokujiunga kuliko kujiunga. Kwa mfano WCC wanaamini kwamba katika dini zote hupatikana wokovu, isipokuwa mlango tofauti tu. Imani kama hii inashusha hadhi ya Kanisa na msalaba wa Kristo. Ni heri kutokujiunga na umoja wa makanisa yasiyo sahihi kuliko kujiunga. Katika umoja wa makanisa mengi pia siku hizi hatari kubwa ipo, kwamba serikali nyingi duniani zimekuwa zikitumia mwanya huu kwa kuwaunganisha watumishi wa Mungu wa kweli na watu wa dini tofautitofauti na hata kufanya ibada za kiumoja 34

nchini. Hapa pana tatizo kidogo kwa sababu unaunganisha ibada ya sanamu na ibada ya kweli. Tangu zamani Mungu hapendi mambo kama haya yafanyike. Hivi karibuni katika nchi fulani kuna ibada iliandaliwa ya kusifu na kuabudu katika makanisa ya Kiprotestanti ambapo makanisa kama ya Wakatoliki, Wasabato na hata Mashahidi wa Yehova waliungana katika ibada moja. Ni harakati za kurudisha umoja, lakini mimi naona ni harakati hatari sana. Wanaoona umoja wa Kanisa kwanza katika Kanisa lisiloonekana wako sahihi, na hivyo ndivyo inavyopaswa kuwa. Makanisa ya kweli yameunganishwa kiroho na Kristo ambaye ndiye kichwa cha Kanisa. Na ikiwa hapa duniani makanisa yanayoonekana yanaonekana kutenganishwa na mafundisho ya uongo, basi hakuna shida kwa sababu Kanisa la kiroho liko katika umoja, na umoja wake unadumu katika Kristo na Roho Mtakatifu, na Mungu baba akidumisha umoja huo. Baadhi ya Maandiko yanayosaidia kuelewa umoja wa Kanisa ni pamoja na: 1 Kor 1:10-13 “Basi ndugu, nawasihi, kwa jina la Bwana wetu Yesu Kristo, kwamba nyote mnene mamoja; wala pasiwe kwenu faraka, bali mhitimu katika nia moja na shauri moja. Kwa maana, ndugu zangu, nimearifiwa habari zenu na wale walio wa nyumbani mwa Kloe, ya kwamba iko fitina kwenu. Basi, maana yangu ni hii, ya kwamba kila mtu wa kwenu kusema, Mimi 35

ni wa Paulo, na, Mimi ni wa Apolo, na, Mimi ni wa Kefa, na, Mimi ni wa Kristo. Je! Kristo amegawanyika? Je! Paulo alisulibiwa kwa ajili yenu? Au je! Mlibatizwa kwa jina la Paulo?” Fungu hili linazuia kabisa kuwepo kwa umoja wa Kanisa kupitia wanadamu, bali kwa Kristo peke yake. Pia katika 1 Kor. 12.12-15 “Maana kama vile mwili ni mmoja, nao una viungo vingi, na viungo vyote vya mwili ule, navyo ni vingi, ni mwili mmoja; vivyo hivyo na Kristo. Kwa maana katika Roho mmoja sisi sote tulibatizwa kuwa mwili mmoja, kwamba tu Wayahudi, au kwamba tu Wayunani; ikiwa tu watumwa au ikiwa tu huru; nasi sote tulinyweshwa Roho mmoja. Kwa maana mwili si kiungo kimoja, bali ni vingi. Mguu ukisema, Kwa kuwa mimi si mkono, mimi si wa mwili; je! Si wa mwili kwa sababu hiyo?” Ningependa kuhitimisha hoja hii kwamba ingawa msisitizo wetu wa umoja ni katika Kanisa lisiloonekana, ni muhimu pia kudumisha umoja wa Kanisa linaloonekana; kwani kwa kufanya hivyo tunatimiza sheria ya Kristo ya upendo kwa watu wengine. Tusimamie umoja kwa kadri iwezekanavyo, ila tafadhali tusilazimishe umoja ambao hauwezekani. Tumeshang’amua kwamba umoja kamili upo katika Kanisa lisiloonekana kupitia Kristo. Kwa hiyo hata Kanisa linaloonekana lazima kuanzisha umoja wetu kupitia Kristo peke yake.

36

2. Utakatifu Utakatifu ni sifa muhimu sana ya Kanisa. Kanisa linatofautishwa na ulimwengu kwa sababu ya utakatifu. Kanisa Katoliki linasisitiza kwamba Kanisa lake pekee yake ndilo takatifu. Utakatifu wa Kanisa Katoliki kimsingi ni utakatifu katika mila zake. Kanisa Katoliki ni takatifu katika mafundisho yake, mafundisho ya maadili, ibada na nidhamu, kufuata mila na desturi za Kanisa ni utakatifu. Hasa Kanisa linachukuliwa kuwa takatifu, kwa kuwa kuna watakatifu katika Kanisa. Na ndiyo maana ndani ya Kanisa Katoliki watakatifu wakuitwa ni wengi sana, kwa sababu ni sifa ya Kanisa. Kanisa ni takatifu kwa maadili yake. Hata hivyo, Kanisa la Kiprotestanti linaonyesha utakatifu katika sehemu tatu: Kwanza, Kanisa ni takatifu kwa kweli tunapomwona Yesu Kristo. Pili, Kanisa ni takatifu wakati tunapoona utakaso wa Roho Mtakatifu katika sehemu ya ndani ya mwamini. Tatu, Kanisa ni takatifu kwa maana ya kuwa limetofautishwa na ulimwengu na limewekwa wakfu kwa Mungu. Kanisa lina jukumu la kupigana na nguvu za mpinzani (giza) ambazo zinajaribu kuharibu utakatifu wa Kanisa na kuendelea kuelekea utakatifu wa juu. Utakatifu wa utu wa ndani lazima uonekane kwa utu wa nje. Kanisa haliwezi kufikia utakatifu wa mwisho kwamba limeshakamilika hapa duniani mpaka Kristo atakapokuja tena hapa duniani. Naunga mkono wazo la Berkhof 37

kwamba “Kanisa ni takatifu kwa maana ya kuwa limetengwa na ulimwengu katika kujitolea kwa Mungu.”17 3. Kanisa la Ulimwenguni pote (Ukatoliki) Kuna watu wengine wakiona sifa hii wanaweza kufikiri kwamba makanisa ya Kiprotestanti yameungamanishwa na Kanisa Katoliki. Ama kuhusu sifa ya ukatoliki, Kanisa Katoliki linadai kwamba lina haki ya Katoliki. Hebu tuzungumze kidogo juu ya neno “Katoliki.” Katoliki kwa Kiswahili limetokana na neno la Kigiriki “katholikos” maana yake "kadiri ya utimilifu", "zima." Katika ekklesiolojia, jina hilo lina historia ndefu na matumizi tofauti kadhaa. Kwa mfano neno zima "Kanisa Katoliki" linahusu Kanisa ambalo lina ushirika kamili na Askofu wa Roma (maarufu kama Papa). Wakatoliki na vilevile Waothodoksi wanaamini kwamba Kanisa lao ni la kwanza na ndilo Kanisa pekee la kweli. Waanglikana, Walutheri na baadhi ya Wamethodisti huamini kuwa makanisa yao ni ya Kikatoliki kwa maana ya kwamba yako katika mwendelezo na asili ya Kanisa lililoanzishwa na Mitume wa Yesu. Warefomati kwa upande mwingine hutumia neno "Kanisa Katoliki" kwa kutaja waumini wote wa Yesu Kristo duniani, bila kujali "madhehebu." Kwa hiyo katika imani ya mitume ya makanisa mengi inasema hivi “na Kanisa Katoliki moja” (siku hizi

17

Berkhof, Louis, Systematic Theology (Grand Rapids: Eerdmans 1974), uk. 633

38

wamebadilisha na kuandika, “na Kanisa takatifu la waamini wote), lakini maana ile ni Katoliki.18 Sasa basi, Kanisa Katoliki hudai kwamba lina haki pekee ya kutumia neno “Katoliki” kwa sababu limeenea pote ulimwenguni. Hata sisi tunakaza kwamba Ukatoliki wa kweli wa Kanisa lazima upatikane katika Kristo, kwa kuwa Kristo pekee ndiye "Bwana wa wote" na hutoa "utajiri wake kwa wote wanaomwomba," na "kila mtu atakayeliitia jina la Bwana ataokoka" (Rom.10: 12,13). Kwa kuongezea, "hakuna Myahudi au Mgiriki, hakuna mtumwa wala huru, hakuna mwanamume au mwanamke, kwa kuwa nyote ni mmoja katika Kristo Yesu" (Gal.3:28) Vitu vyote vitapatanishwa na Mungu Baba. Hata hivyo, makanisa mengi ya Kiprotestanti huepuka kutumia neno “Katoliki” kwa kuhofia kuwachanganya Wakristo wachanga ili wasichanganye Kanisa Katoliki na Ukatoliki wa Kanisa la Kristo. Kwa hiyo ni bora kutumia neno, “Kanisa la Waumini wote.” 4. Utume Karl Barth anasema "utume" inamaanisha kuwa "kuwa katika uanafunzi, kujifunza katika shule yao, kuwa chini na kukubaliana na maelekezo yao.” 19

18 19

Hii inamaanisha kwamba

FL Msalaba, Oxford Dictionary la Kanisa la kikristo, 1977. Uk 175. Karl Barth, Church Dogmatics (Edinburgh: T. & T. Clark, 1960), uk. 714

39

Kanisa katika kushikilia utume wa mitume si kwa kubadilishana madaraka, bali ni kujifunza kwao. Kama vile uzao wa kweli wa Ibrahamu ni wale wanaotembea katika imani ya Ibrahimu, bila kujali asili ya ukoo, vivyo hivyo Kanisa la kitume ni lile ambalo linatembea kwa imani ya mitume, bila kujali "suala la urithi.” Utii wa mafundisho ya mitume unatuhakikishia utume wa Kanisa. Utume hauwezi kamwe na kamwe hautawahi kutazamwa tu katika suala la kurudiwa kwa ofisi ya mitume.20 Neno la Mungu linasema katika Mathayo 10:40: kwamba "Awapokeaye ninyi (mitume wake) anipokea Mimi." Hapa haimaanishi kuwapokea mitume kama mitume, bali ni kupokea mafundisho yao. Waefeso 2:20 inasema “Mmejengwa juu ya msingi wa mitume na manabii, naye Kristo Yesu mwenyewe ni jiwe kuu la pembeni.” Msingi hapa ni mafundisho yao. Anaposema “manabii” anazungumzia “Agano la Kale” na mitume kama wawakilishi wa Agano Jipya. Tunafuata mafundisho ya mitume kwa sababu mitume walimfuata Kristo. Katika 1 Kor. 11:1 Mtume Paulo anasema “Mnifuate mimi kama mimi ninavyomfuata Kristo.” Kanisa Katoliki linasisitiza kwamba ni mrithi wa kweli wa mitume wa kwanza. Kanisa la Othodoksi la Ugiriki na Kanisa la 20

Raymond, L. Robert, A New Systematic Theology of The Christian Faith (Nashville: Thomas Nelson Publishers 1998), uk. 852.

40

Episcopal la Uingereza yanadai kupata mamlaka ya Kanisa moja kwa moja kwa Mitume. Sasa hapa unaweza kuona mkanganyiko huo. Pana makanisa matatu: Kanisa Katoliki la Roma, Kanisa la Othodoksi la Ugiriki, na Kanisa la Kiasikofu la Uingereza (Episcopal England Church), yote yanadai kuwa yanapata mamlaka moja kwa moja kutoka kwa mitume. Hoja yao kubwa ni kwamba ile hadhi ya mitume ni ya kuridhishwa. Kwa mfano Papa wa Roma yeye anaridhi kiti cha Mtume Petro, ambaye alikabidhiwa Kanisa na Bwana Yesu. Yesu alimkabidhi Kanisa Petro aliposema kwamba “juu ya mwamba huu nitalijenga Kanisa: Yesu anasema “Nami nakuambia, Wewe ndiwe Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga Kanisa langu; wala milango ya kuzimu haitalishinda (Mat. 16:18). Bila kuzingatia muktadha wa andiko, kwa makusudi kabisa Kanisa Katoliki waliamua kupotosha ukweli wa andiko hili. Yesu alisema kwamba atalijenga Kanisa juu ya ukiri wa Petro. Kabla ya andiko hilo, Petro alikiri kwamba “Wewe ndiwe Kristo, Mwana wa Mungu aliye hai.” (Mat. 16:16). Ndipo Yesu alisema kwamba atalijenga Kanisa lake juu ya maneno hayo. Kanisa kweli limejengwa juu ya maneno aliyokiri Petro kwamba Yesu ndiye Kristo Mwana wa Mungu aliye hai, na kwamba Kristo peke yake ndiye kichwa cha Kanisa. Sasa hawa Wakatoliki wanasema papa ndiye kichwa cha Kanisa, wakidai kwamba Petro alikuwa kichwa cha Kanisa. 41

Calvin anapinga vikali mawazo ya Kanisa Katoliki kwa hoja zifuatazo: a) Hakuna mahali kwenye Biblia kwamba mwanadamu anaweza kuwa kichwa cha Kanisa. Anadai kwamba ingawa Petro alionekana kuwa mkubwa miongoni mwa mitume, lakini haina maana kwamba yeye ni kichwa cha Kanisa b) Umoja wa Kanisa upo katika Kristo na wala siyo katika Upapa. Yale madai ya Kanisa Katoliki kwamba yeyote aliye nje ya Kanisa Katoliki, basi huyu yuko nje ya Kristo ni uongo, kwani umoja wa Kanisa upo katika Kristo na wala siyo kwa Kanisa Katoliki.21 c) Ofisi ya Mitume kumi na mbili haiwezi, kuhamishwa kwa watu wengine kwa asili yake na haikuhamishiwa kwa wengine. Masharti ya mtu kuwa mtume yalikuwa ni kwamba alipaswa kuwa katika huduma ya Yesu hapa duniani na awe shahidi wa ufufuo. Hakuna mtu anayeweza kutosheleza masharti haya baada ya kumalizika kwa miaka ya mitume. Paulo ni mtume maalumu kwa sababu hakuwa na Yesu wakati wa uhai wake duniani, lakini aliishi katika umri uleule kama Yesu. Paulo hakuwa shahidi wa ufufuko wa mwili wa Yesu, lakini alikutana na Kristo aliye

21

Battles, Ford Lewis, Analysis of the Institutes of the Christian Religion of John Calvin (Phillipsburg: P & R Publishing Company, 1980), uk. 312-314

42

mbinguni, aliyefufuka. Katika 1 Wakorintho 15:8 tunasoma hivi “Na mwisho wa wote, akanitokea na mimi, ambaye ni kama nilizaliwa kwa hali isiyo ya kawaida.” inamaanisha kwamba Paulo ndiye Mtume wa mwisho na Utume ulimalizika kwake. Huu ndio msimamo wetu katika kipindi hiki ambapo pana mitume na manabii wengi nchini. Tunaamini kwamba hadhi ya mtu kuitwa mtume ilishia kwenye karne ya kwanza, na hakuna mtu anayeweza kujiita mtume tena baada ya Paulo. Mitume wote wa leo, kwa kawaida si mitume kwa hadhi ingawa wanadai kwamba ni mitume. 5. Kutokuwa na Makosa kwa Kanisa Kanisa Katoliki wanaposema kwamba Kanisa halina makosa wanaamanisha kwamba Papa hana makosa. Wanadai kwamba Yesu alimpa Petro nguvu ya kutokuwa na makosa na kwamba anaweza kufanya jambo lolote lile duniani pasipo makosa kwa sababu kazi ya Petro ilikuwa ni kuwapa wengine na kuimarisha imani yao. Wanasoma katika Lk. 22:32 kwamba “lakini nimekuombea wewe ili imani yako isitindike; nawe utakapoongoka waimarishe ndugu zako.” Hapa pana upotoshaji wa hali ya juu, kwa sababu Yesu aliahidi kumwimarisha Petro katika kipindi ambacho imani yake ingetindika, na hili lilitimia baada ya ufufuo wa Yesu. 43

Tunajua wazi kwamba hakuna mwanadamu asiyekuwa na makosa. Lakini Kanisa Katoliki wamejaribu mara nyingi kubadilisha maneno yao. Siku hizi wanasema kwamba Papa anaweza kufanya makosa kama atakuwa nje ya Kanisa la Mtakatifu Petro kule Roma na kama asipokaa kwenye kiti cha Petro. Hii inamaanisha kwamba ikiwa Papa atakaa kwenye kiti ambacho kinadaiwa kuwa cha Petro hawezi kufanya makosa yoyote. Na ndiyo maana Papa akiandika waraka wowote (wanauita Mtaguso wa Papa) wakatoliki wote wanaupokea kama Neno la Mungu bila kukosoa. Tofauti na mitume wa kileo ambao hawadai kuridhi kiti cha Petro, Wakatoliki hukaza kwamba Papa anasimama badala ya Petro. Sisi tunakaza kwamba watumishi wa Mungu wote wanaweza kufanya makosa. Hata Kanisa pia kupitia taasisi zake linaweza kufanya makosa kadhaa ya kimaamuzi kwa sababu wanaoongoza ni wanadamu wa kawaida. Wachungaji na watumishi wengine hawana chanjo ya kutokukosa kwa sababu ya upotofu wa dunia hii, na wakati wowote wasipolinda mioyo yao shetani anaweza kutumia mwanya kuharibu Kanisa. Na ndiyo maana tumeshuhudia maamuzi ya watumishi wengi wa Mungu yakiharibu makanisa mbalimbali. Kuna vikao vingi vya makanisa ambavyo vilipofanya maamuzi kulitokea mgawanyiko mkubwa. Kwa hiyo haiwezekani kwamba watumishi wa Mungu hawana 44

makosa; kwa vyovyote vile, hata kama wanahubiri, au wako kwenye minbari, wanaweza kufanya makosa. Kwa hiyo. kazi ya waumini wa Kanisa ni kuomba kwa ajili ya watumishi wa Mungu ili wadumu katika kuongoza vizuri Kanisa kama taasisi na liendelee vizuri. Hata hivyo, kwa kuwa Kristo ndiye kichwa cha Kanisa, anaongoza Kanisa lisianguke katika maasi ya shetani. Kanisa linaloonekana linaweza kujikuta limetumbukia katika maasi hayo, lakini kamwe Kanisa lisiloonekana litaendelea kuwa safi. III. Alama za Kanisa Tangu wakati wa matengenezo, Kanisa limekuwa katika kipindi kigumu cha kutambulika. Wakati wa mwanzo walijadili uwepo wa watumishi wa Mungu kama ndiyo alama ya Kanisa; yaani kuwepo kwa mchungaji ambaye ataongoza neno ndiyo ilikuwa alama kuu ya Kanisa. Wakatoliki walidai kwamba, “pale palipo na askofu ndipo palipo na Kanisa” na usemi huu uliungwa mkono John Calvin, ambapo kwake “askofu” maana yake ni mchungaji.”22 Kama nilivyodokeza kule nyuma kwamba mawazo haya si rahisi kukubaliana nayo, hasa tunaporejea kwenye maana ya Kanisa.

22

Bavinck, Herman. Reformed Dogmatics (p. 601). Baker Publishing Group. Kindle Edition.

45

Kuna alama anuwai za Kanisa, tutaangalia katika historia ya Kanisa namna ambavyo alama za Kanisa zilitambuliwa: Martin Luther alipendekeza mambo saba kama alama za Kanisa la kweli: ambayo ni Neno, Ubatizo, Meza ya Bwana, utekelezwaji wa haki ya kanisani, kuchambua wasioamini ndani ya Kanisa, sala ya umma, msalaba kama ishara za Kanisa. Hata hivyo, nyakati zingine, alipendekeza Neno na Sakramenti kama ishara mbili za Kanisa la kweli. Melanchton aliongeza kwamba Kanisa la kweli linapaswa si kuwepo tu kwa Neno na Sakramenti, bali linapaswa pia kuzitii na kuzifanya kwa uaminifu. Ukiangalia mawazo ya Luther yanaonesha kwamba kuna aina saba za alama za Kanisa. Kwa sasa unaweza kuanza kuelewa kwa nini katika Makanisa ya Kilutheri kuna misalaba kadhaa kanisani; ni kwa sababu ya Imani kwamba msalaba nao ni alama ya Kanisa. John Calvin alipendekeza alama kuu mbili: kwanza, Neno, anadai kwamba pale ambapo neno la Mungu linahubiriwa kwa usahihi na linasikilizwa pia, na Sakramenti, kwamba Sakramenti ifanyike sawasawa na jinsi Kristo alivyoagiza.23 Calvin alisisitiza umuhimu wa nidhamu (discipline), lakini hakuipendekeza kama

23

Battles, Ford Lewis, Analysis of the Institutes of the Christian Religion of John Calvin (Phillipsburg: P & R Publishing Company, 1980), uk. 284.

46

ishara ya Kanisa. Wazo la Calvin linafanana na lile la Melachton. Ingawa madhehebu mengine yana mfumo wa nidhamu kama alama ya Kanisa, lakini hakupinga hoja kwamba nidhamu lazima ijumuishwe kwenye orodha ya ishara za Kanisa. Grudem24 anabainisha kwamba ili Kanisa liwe safi kabisa linahitaji kuwa na alama zifuatazo:

1. Mafundisho ya Biblia (au kuhubiriwa kwa neno la Mungu kwa usahihi

2. Matumizi sahihi ya Sakramenti 3. Utekelezaji wa nidhamu ya Kanisa 4. Ibada ya kweli 5. Maombi yenye ufanisi 6. Ushuhuda mzuri (Efe. 5:18-20; Wakolosai 3:16-17) 7. Ushirika mzuri (Math. 28:19-20; Yn. 1:34-35; Mdo 2: 44-47; 1Yoh 4:7)

8. Serikali ya Kanisa la Biblia (1 Tim. 3:1-13) 9. Nguvu ya kiroho katika huduma (Mdo 1:8; War.1:1,16; 1 Kor 4:20; 2 Kor 10:3-4; Gal 3:3 - 5; 2 Tim. 3: 5; Yak. 5: 1 6),

24

Grudem, Wayne. Systematic Theology (Grand Rapids: MI: Inter-Varsity Press) 1994, Uk. 1142

47

10.

Utakatifu wa kibinafsi wa maisha kati ya Washirika (1Thes. 4:3)

11.Kujali masikini ((Mdo 4:32- 35; Warumi 15:26; Gal 2:10)

12.Upendo kwa Kristo (1Pet. 1:8; Ufu. 2:4). Wanateolojia

wa

refomati

(Reformed

Theologians)

wanatofautiana kuhusu idadi ya alama za Kanisa. Kuna waliosema kwamba alama ni moja tu; yaani mafundisho safi ya Neno la Mungu. Walioshikilia msimamo huu ni pamoja na Beza, Alsted, Amesius, Heidanus, Maresius. Wengine walishikilia alama mbili tu, ambazo ni mahubiri safi ya Neno na usimamizi sahihi wa Sakramenti mbili za Ubatizo na Meza ya Bwana. Wanatheologia walioshikilia msimamo huu ni pamoja na John Calvin, Bullinger, Zanchius, Junius, Gomarus, Mastricht, a Marck. Hata hivyo wengine walisisitiza aina tatu, ambazo ni; mahubiri safi ya Neno la Mungu, Sakramenti na Nidhamu. Wanatheologia hao ni pamoja na Hyperius, Martyr, Ursinus, Trelcatius, Heidegger, Wendelinus. 25 Wengi wanaokataa kuongeza nidhamu kuwa sehemu ya alama ya Kanisa husisitiza kwamba hata Kanisa lisilo na nidhamu bado ni Kanisa la Mungu, kama ilivyokuwa katika Kanisa la Korintho (1 Kor 5), ambapo Paulo bado aliendelea kuwaita Watakatifu. 25

Berkhof, Louis, Systematic Theology, uk. 638

48

Baada ya majadiliano hayo, Wana-Refomati walihitimisha kuwepo kwa alama tatu za Kanisa, kwanza, kuhubiriwa kwa Neno, pili, kushiriki kwa usahihi Sakramenti na tatu utekelezaji wa dhati wa Nidhamu ya Kanisa. Nitafafanua kwa kila moja ya hizi alama. Kwanza, Kutangazwa/kuhubiriwa kwa Neno, pili, kushiriki kwa usahihi Sakramenti, na tatu ni utekelezaji wa nidhamu ya Kanisa.26 Nitafafanua kila moja ya alama hizi kwa kina. 1. Kuhubiriwa kwa Neno Kutangazwa kwa Neno la Mungu ndiyo alama ya kwanza ambayo ni muhimu sana ndani ya Kanisa. Watu wanaweza kuwa wanafunzi wa Yesu kupitia Neno la Mungu. Hivyo basi kama Kanisa halihubiri Neno la Mungu kwa usahihi hilo siyo Kanisa la kweli. Kuhusu hoja hii John Calvin anatabanaisha kwamba “hii ndio alama ya kudumu ambayo Bwana wetu ameweka muhuri wake mwenyewe: "Kila aliye wa hiyo kweli, huisikia sauti yangu" (Yn. 18:37). Vivyo hivyo: "Mimi ndimi Mchungaji Mwema: nao walio wangu wanijua mimi." (Yn. 10:14.) "Kondoo wangu waisikia sauti yangu; nami nawajua, nao wanifuata." 10:27.) Lakini zamani kidogo alisema: "Kondoo humfuata mchungaji wao, kwa sababu wanajua sauti yake. Hawamfuati mgeni lakini humkimbia, kwa maana hawajui sauti yake” (Yn. 10:4-5). Kristo 26

Frame, M. John, Systematic Theology

49

ameweka alama hiyo kwa Kanisa la kweli. Paulo anatukumbusha kwamba Kanisa halijaundwa kwa mapenzi ya wanadamu, sio juu ya ukuhani, bali juu ya mafundisho ya mitume na manabii (Efe. 2:20). John Calvin anasema “Yerusalemu inapaswa kutofautishwa na Babeli, Kanisa la Kristo litenganishwe na Shetani kupitia Neno la Mungu. ”27 Popote pale palipo na Kanisa, basi lazima Neno la Mungu lihubiriwe, siyo maneno ya wanadamu. Changamoto katika ulimwengu wa leo ni kwamba watu wanaenda kanisani si kwa ajili ya kusikiliza Neno la Mungu. Si kwa ajili ya kusikiliza Mungu anasema nini kwa ajili ya maisha yao, bali wanaenda kwa ajili ya kuombewa tu. Kama Kanisa likikaza maombi kuliko Neno la Mungu, basi kuna shida kubwa ya kimafundisho. Neno la Mungu limekuja kabla ya maombi. Mungu ametupatia Neno lake, hajatupatia maombi kwanza. Kwa hiyo Lazima Neno lipewe kipaumbele kwa sababu kupitia Neno, Mungu anazungumza pamoja nasi. Jambo ambalo tunaweza kukaza hapa ni kwamba kwa kweli si rahisi siku hizi kupata mahubiri ya Neno la Mungu yaliyo kamili bila mawaa. Kwanza kuna matatizo mbalimbali ya kutafsiri Biblia, pamoja na pengo kubwa la wakati na utamaduni wa kipindi 27

Calvin, John, Institutes of the Christian Religion (Louisville: Westminster John Knox Press, 1960),Uk. 1142

50

Biblia ilipoandikwa. Hata hivyo tunachojaribu kukaza ni kwamba mahubiri yanapaswa yawe yameegemea kwenye mafundisho ya kweli ya Kanisa (sound doctrines). Kwa mfano tunaposema kwamba “tumeokolewa kwa neema, wala si kwa matendo yetu” basi halafu mwingine akaja na kusema “tumeokolewa kwa neema lakini na matendo nayo yanasaidia sana katika kupata wokovu.” Huyu wa pili tayari amepotosha ukweli, na ukweli uliopotoshwa ni hatari sana kwa sababu ukweli huo ndio msingi wa Ukristo. Mkazo wa wokovu kwa matendo unashadidiwa na Kanisa Katoliki. Siku hizi makanisa mengi ya Kipentekoste yamekuwa na mtazamo huu wa wokovu kwa matendo. Watu wanahubiriwa kwamba waache dhambi ndipo waje kwa Yesu. Makanisa kama hayo yanakuwa na dosari kubwa. Binafsi siwezi kusema moja kwa moja kwamba hayo ni makanisa ya uongo, lakini wewe unaweza kuamua kupitia sifa ya Neno la Mungu. Yaani neno la Mungu angalau lifundishwe kwa kuzingatia mafundisho sahihi (sound doctrine) za Kikristo. Neno la Mungu linasema katika Wagalatia 1: 8-9: "Lakini ijapokuwa sisi au malaika wa mbinguni atawahubiri ninyi Injili yoyote isipokuwa hiyo tuliyowahubiri, na alaaniwe. Kama tulivyotangulia kusema, na sasa, nasema tena, mtu awaye yote akiwahubiri ninyi Injili yo yote isipokuwa hiyo mliyoipokea, na alaaniwe."

51

2. Kupokea kwa usahihi Sakramenti Nitazungumza kwa undani kuhusu Sakramenti huko mbele, lakini hapa ninachotaka ujue ni kwamba katika Protestanti kuna aina mbili za Sakramenti: Ubatizo na Kushiriki Meza ya Bwana (Ekaristi Takatifu). Sakramenti hizi zinapaswa kufanya pamoja na Neno la Mungu. Yaliyomo kwenye Sakramenti hutokana na Neno la Mungu.Kwa hiyo, Sakramenti lazima zitekelezwe na Mwalimu wa Neno la Mungu (Math.29: 18; 1kor.11: 23-30). Calvin alipendekeza kwamba kila Neno linapohubiriwa, basi lazima Sakramenti ya Meza ya Bwana ifanyike. Tunazo changamoto siku hizi kwa baadhi ya makanisa kufanya Sakramenti ya Meza ya Bwana na Ubatizo mara moja kwa mwaka. Tukifanya hivyo, tunapoteza ile maana halisi ya Kanisa la Kristo. Sakramenti zinayo kazi ya kukuza neema katika maisha ya Wakristo, kwa hiyo ni lazima zifanywe mara kwa mara. Inasemekana kwamba katika Kanisa ambalo John Calvin alikuwa akiongoza, kila Jumapili baada ya mahubiri walishiriki meza ya Bwana na ubatizo ulifanyika wakati wowote kwa mtu aliyemkiri Kristo. 3. Utekelezaji wa dhati wa Nidhamu ya Kanisa Ingawa Calvin hakuweka hoja hii kuwa alama ya Kanisa, lakini aliongeza na kukubaliana na wale waliopendekeza kuwa alama ya Kanisa kama tulivyojadili hapo juu. Nidhamu 52

inatekelezwa ili kuweka usafi wa mafundisho na kutetea utakatifu wa Kanisa (1Kor.5). Nidhamu ya Kanisa inaenda sambamba na Neno la Mungu. Berkhof anasema kuwa “Kwa kweli, inaweza kusemwa kwamba uhubiri wa kweli wa Neno na kutambuliwa kwake kama kiwango cha mafundisho na maisha ya Wakristo, ni alama moja ya Kanisa. Bila hiyo, hakuna Kanisa, na hiyo ndiyo huamua usimamizi sahihi wa Sakramenti na zoezi la uaminifu la nidhamu ya Kanisa.” 28 Baadhi ya Maandiko yanayoeleza kuhusu nidhamu ya Kanisa ni pamoja na:Mathayo. 18:17 “Na asipowasikiliza wao, liambie Kanisa; na asipolisikiliza Kanisa pia, na awe kwako kama mtu wa mataifa na mtoza ushuru.” Hapa Kanisa linapewa kazi ya kusimamia nidhamu ya mtu binafsi ndani yake. Matendo ya Mitume 20:28-31 “Mtakatifu amewaweka ninyi kuwa waangalizi ndani yake, mpate kulilisha Kanisa lake Mungu, alilolinunua kwa damu yake mwenyewe. Najua mimi ya kuwa baada ya kuondoka kwangu mbwa-mwitu wakali wataingia kwenu, wasilihurumie kundi; tena katika ninyi wenyewe watainuka watu wakisema mapotovu, wawavute hao wanafunzi wawaandamie wao. Kwa hiyo kesheni, mkikumbuka ya kwamba miaka mitatu, 28

Berkhof, Systematic Theology, 577.

53

usiku na mchana, sikuacha kumwonya kila mtu kwa machozi.” Hapa wazee wa Kanisa wanapewa wajibu wa kuchunga kundi la Bwana kwa uaminifu. Kuchunga ni kusimamia nidhamu ya Kanisa, hasa pia katika kuhakikisha kwamba mafundisho ndani ya Kanisa yanaendana na Neno la Mungu. Warumi 16:17-18 “Ndugu zangu, nawasihi, waangalieni wale wafanyao fitina na mambo ya kukwaza kinyume cha mafundisho mliyojifunza; mkajiepushe nao. Kwa sababu walio hivyo hawamtumikii Bwana wetu Kristo, bali matumbo yao wenyewe; na kwa maneno laini na ya kujipendekeza waidanganya mioyo ya watu wanyofu.” 1 Kor 14:33, 40 “Kwa maana Mungu si Mungu wa machafuko, bali wa amani; vilevile, kama ilivyo katika makanisa yote ya watakatifu… Lakini mambo yote na yatendeke kwa uzuri na kwa utaratibu. Wagalatia 6:1 “Ndugu zangu, mtu akighafilika katika kosa lo lote, ninyi mlio wa Roho mrejezeni upya mtu kama huyo kwa roho ya upole, ukijiangalia nafsi yako usije ukajaribiwa wewe mwenyewe.” Efe. 5:6, Mtu asiwadanganye kwa maneno yasiyo na maana; kwa kuwa kwa sababu ya hayo hasira ya Mungu huwajia wana wa

54

uasi. Wala msishirikiane na matendo yasiyozaa ya giza, bali myakemee; 2 Thesalonike 3:14 “Na ikiwa mtu awaye yote halishiki neno letu la waraka huu, jihadharini na mtu huyo, wala msizungumze naye, apate kutahayari; lakini msimhesabu kuwa adui, bali mwonyeni kama ndugu. 1 Timotheo 1:20 “Katika hao wamo Himenayo na Iskanda, ambao nimempa Shetani watu hao, ili wafundishwe wasimtukane Mungu.” Tito 1:10-11 “Kwa maana kuna wengi wasiotii, wenye maneno yasiyo na maana, wadanganyaji, na hasa wale wa tohara, ambao yapasa wazibwe vinywa vyao. Hao wanapindua watu wa nyumba nzima, wakifundisha yasiyowapasa kwa ajili ya mapato ya aibu.” Ufunuo 2:14-16a “Lakini ninayo maneno machache juu yako, kwa kuwa unao huko watu washikao mafundisho ya Balaamu, yeye aliyemfundisha Balaki atie ukwazo mbele ya Waisraeli, kwamba wavile vitu vilivyotolewa sadaka kwa sanamu, na kuzini. Vivyo hivyo wewe nawe unao watu wayashikao mafundisho ya Wanikolai vilevile. Basi tubu;” Maandiko hayo juu yanathibitisha kwamba nidhamu ndani ya Kanisa ni ya muhimu sana. Reymond anachambua kwamba, 55

“wakati alama zote tatu ni vipimo sahihi vya Kanisa la kweli na muhimu sana, alama ya pili na ya tatu ni muhimu kwa ustawi wa Kanisa, sio lazima kwamba ili Kanisa liwepo basi lazima zionekane hizo Kanisa. Ya kwanza tu ni muhimu sana kwa Kanisa, na kwamba isipokuwepo hakuna Kanisa. 29 Kwa namna fulani nakubaliana naye, kwa maana ya kwamba hata kama hakuna mchungaji wa kubatiza au kushirikisha Meza ya Bwana, kwa kuwa neno lipo, basi hilo ni Kanisa, na kwamba kukosekana kwa nidhani hakuwezi kuondoa hali ya Kanisa hilo. Pengine tungependa kusisitiza kwamba nidhamu ni jambo muhimu sana Kibiblia. Nidhamu siyo “adhabu.” Kama tukiwa na mawazo ya adhabu wakati tunapotekeleza nidhamu ndani ya Kanisa, basi tekelezo la nidhamu hiyo halifai. Nidhamu ni zaidi ya kumtenga mtu kanisani, au kukemea dhambi ndogo. Lakini kila Kanisa linapaswa kufanya mazoezi ya nidhamu. Angalau madhumuni matatu ya nidhamu yanaweza kuainishwa. Kwanza ni kumrudisha mwamini anayetenda dhambi (Mat. 18: 15; 1 Kor 5: 5; Gal. 6: 1; 1 Tim. 1:20; Yakobo 5: 20). Ni kwa ajili ya kumsaidia mkosaji dhambi zake ili atubu. Kwa hiyo nidhamu ya Kanisa sio jambo la kikatili, lakini ni jambo la kupenda. Pili, nidhamu inatolewa ili kuzuia dhambi za wengine, kufundisha waumini ni

29

Raymond, L. Robert, A New Systematic Theology of The Christian Faith (Nashville: Thomas Nelson Publishers 1998), uk. 862

56

nini kisichokubalika ndani ya Kanisa (1 Kor 5: 2, 6-7; 1 Tim. 5:20; Ebr. 12:15). Tatu, nidhamu inatolewa ili kulinda heshima ya Kristo na Kanisa lake (Rom. 2:24; 1 Kor. 6: 6; Efe. 5:27). Ni dhahiri kwamba pindi makanisa yanapopuuza dhambi, ulimwengu unamdharau Kristo. Walimwengu wanajua dhambi za Wakristo kuliko wao Wakristo wanavyozijua. Sio kwamba kila mtu kanisani lazima awe mkamilifu, kwa kuwa hiyo haiwezekani. Kila mtu huanguka dhambini na kila mtu ana mapungufu mengi tu. Kanisa kwa njia fulani ni hospitali kwa wale ambao wanajua ni wagonjwa. Ambao wamemwamini Kristo kama Mwokozi na wanataka kumfuata kama Bwana wao. Kuna wale ambao, kwa makusudi na kwa kuendekeza udhaifu wao huendelea

kutenda

dhambi;

wameonywa

mara

nyingi,

wamekaripiwa mara kadhaa, lakini bado wanaanguka kwa dhambi zillezile; basi wanahitaji kupewa karipio la kinidhamu ili watubu kwelikweli. Hata hivyo taratibu zote za Kibiblia lazima zifuatwe ili kuondoa ile dhana ya “chuki binafsi” kwa mtu mwingine. Swali la mjadala: 1. Je kuna utata gani umepata katika kuelewa aina ya Kanisa; la ulimwenguni na la mbinguni? 2. Je unaweza kueleza kwa maneno yako tofauti kati ya Kanisa linaloonekan na lisiloonekana? 57

3. Je ungefafanua vipi maana ya Kanisa kama kiumbe hai? 4. Ni zipi sifa za Kanisa kama taasisi? 5. Je unazungumziaje Wakristo ambao wanafanya dhambi fulani kwa kujua kwamba watafungiwa miezi kadhaa tu na kumaliza vifungo vyao? Je unaweza kuwasaidiaje watu kama hawa? 6. Unazungumziaje kwamba kanisani kuna magugu na ngano, lakini wakati huohuo unapotaka kufanya mazoezo ya nidhamu unataka kuchambua magugu na ngano? 7. Je kuna alama yoyote ya Kanisa ambayo unaitilia mashaka, ipi hiyo na kwa nini? 8. Kwa nini unadhani Wakatoliki wanakaza “kutokuwa na makosa” kama alama ya Kanisa? IV. Makusudi ya Kanisa Kuna mitazamo kadhaa kuhusu makusudi ya kuwepo kwa Kanisa. tunapotazama kwa mtazamo wa historia ya wokovu, Kanisa lipo ili kuonyesha hekima na rehema za Mungu katika kipindi hiki (Efe. 3:10; taz. Rum. 9: 23-24; 11:33; 1 Kor. 1:20-31) kwa kutangaza Injili ya Yesu Kristo ulimwenguni kote (Mt. 28: 19-20; Mdo. 1: 8; 1 Pet. 2: 9), ili wenye dhambi kutoka kila kabila na kila taifa (Ufu. 5: 9-10) waweze kuokolewa kutoka kwenye ufalme wa giza na kuingizwa katika ufalme wa Mungu (Kol. 1: 1258

13). Pia Israeli wasioamini waweze kuchochewa na wivu na toba ya watu wa mataifa na waweze kuamini (Rum. 10:19; 11:11). Kwa mtazamo wa “ki-Eskatolojia” Kanisa litatawala na Kristo katika utukufu wake (1 Kor. 6: 2; taz. 2 Tim. 2: 11-13; Ufu. 20: 4-6). Lakini pia, kwa mtazamo namna Kanisa linavyohuka na Washirika wake, kusudi lake linaweza kusemwa kama ifuatavyo: Kanisa lipo kwa ajili ya kumtukuza Mungu (Efe. 1: 5-6, 12-14; 3: 20-21; 2 The. 1: 12) kwa kujenga kikamilifu Washirika wake katika imani (Efe. 4:12-16), likifundisha Neno kwa uaminifu (2 Tim. 2:15; 3: 16-17), likizingatia maagizo mara zote (Luka 22:19; (Mdo 2: 38-42), likiimarisha ushirika kati ya waamini (Mdo 2: 4247; 1 Yoh. 1:3), na kwa ujasiri kupeleka ukweli wa Injili kwa waliopotea (Mt. 28: 19-20). Macarthur na Mayhue30 wanabainisha makundi matatu ya makusudi ya Kanisa yaani; kwanza Kanisa lipo kwa ajili ya kumtukuza Mungu, pili Kanisa lipo kwa ajili ya kuwajenga waamini na mwisho Kanisa lipo kwa ajili ya kufanya unjilisti. 1. Kumtukuza Mungu Kwa sababu Mungu ni mwenye wivu kwa utukufu wake (Isa. 48: 9-11; taz. Isa. 43: 6-7; 49: 3), watu wake vilevile wanapaswa kuwa hamu ya kumtukuza na kumtukuza (1 Kor. 10: 30

Macarthur J & Mayhue, R (Ed) A Systematic Summary of Biblical Truth: Biblical Doctrine (Wheaton, Illinois: Crossway, 2017) 751-3

59

31; taz. 6:20). Kanisa limekombolewa ili waamini waweze kumtukuza Mungu kwa kuhudumiana (1 Pet. 4:11) na kwa kutangaza wema wake yeye aliyewaita (kutoka) gizani ili kuingia katika nuru yake ya ajabu" (1 Pet. 2:9) Njia moja na ya msingi ambayo Kanisa linamwinua Mungu kikamilifu ni kwa njia ya ibada na sifa. Wakati wowote, Kanisa linapokusanyika, ibada inapaswa kuwa kipaumbele cha kwanza (Yn. 4:23-24) Ibada inajumuisha kutoa heshima kwa Mungu kwamba anastahili, kutangaza utukufu wake kwa maneno ya sifa (kama vile Zab. 29: 2; 95: 6; 99: 5, 9; Ebr. 12:28) na kupitia matendo ya utii (Rum. 12: 1). Ibada ya kweli lazima ijumuishe kuinuliwa kwa Yesu Kristo, ambaye Baba amemtukuza kwa kumpa jina lililo juu ya kila jina (Fil. 2:9; taz. Mdo 5:31, Ebr. 7:26). Ni dhahiri kwamba, kwa milele yote, waliokombolewa watasifu jina lake (Ufu. 4:10; 5: 12-13; 7:12; 14: 7; 15: 4, na hawa waliokombolewa ndio Kanisa lenyewe. Hivyo basi tunaweza kusema kwamba Kanisa ndiyo taasisi maalumu ya kimwili na kiroho ambayo inamtukuza Mungu kwa uaminifu. Walio nje ya Kanisa pengine wanaweza kumtukuza Mungu, lakini sifa zao ni bure tu, kwa sababu “waniabudu bure, wakifuata mafundisho yaliyo maagizo ya wanadamu.” (Mat.15:9). Hawa walio nje ya Kanisa hawawezi kuwa na ibada sahihi mbele za Mungu kwa ajili ya kumtukuza yeye. 60

2. Kuwajenga Waumini Katika 1 Wakorintho 14, Paulo alielezea mkutano wa kawaida katika Kanisa la kwanza kwa maneno haya: "Basi, ndugu, imekuwaje? Mkutanapo pamoja, kila mmoja ana zaburi, ana fundisho, ana ufunuo, ana lugha, ana tafsiri. Mambo yote na yatendeke kwa kusudi la kujenga.” (14:26). Vivyo hivyo aliwaamuru waumini wa Thesalonike" Basi, farijianeni na kujengana kila mtu na mwenzake, vilevile kama mnavyofanya."(1 Wathesalonike 5:11). Kujengana kama huko kunafanyika kupitia huduma ya Neno. (Mdo. 20:32; 2Tim. 3:15-17; 1 Pet. 2:2), ushauri wa uongozi wa Kimungu (Efe. 4: 11-12), Matumizi sahihi ya karama za kiroho (1 Kor. 12: 7; 1 Pet. 4:10). Katika Agano jipya kuna amri ambayo tunaweza kuita ni amri ya "kila mmoja." Au “ninyi kwa ninyi” Yaani maagizo ya kufanyiana jambo kwa Wakristo kwa kila mmoja. Hebu tuone orodha ifuatayo: 1)

Kupendana (Rum. 12:10; 13: 8; 1 The. 3:12; 4: 9; 2 The. 1: 3; 1 Pet. 1:22; 4: 8; 1 Yn. 3:11, 23; 4: 7, 11-12; 2 Yn. 5).

2)

Kuishi kwa umoja (Warumi 12:16; 15: 5; taz. Gal. 5:26; 1 The. 5:13).

3)

Kukaribishana (Rum. 15: 7; taz. Rum. 16:16).

4)

Kuonyana (Warumi 15:14; Kol. 3:16).

5)

Kujaliana (1 Kor. 12:25). 61

6)

Kutumikiana (Wagalatia 5:13; 1 Pet. 4:10).

7)

Kuchukuliana mizigo (Wagalatia 6: 2).

8)

Kuvumiliana (Efe. 4: 2; Kol. 3:13).

9)

Kufadhiliana (Efe. 4:32).

10) Kusameheana (Efe. 4:32; Kol. 3:13). 11) Kuimba sifa pamoja (Efe. 5:19; Kol. 3:16). 12) Kuchukulia umuhimu (Flp. 2: 3). 13)

Kuambiana ukweli (Kol. 3: 9).

14) Kutiana moyo (1 The. 4:18; 5:11; Ebr. 3:13; 10:25). 15) Kutafuta mema (1 The. 5:15). 16) Kuchocheana kwa upendo (Ebr. 10:24; taz. 1 Tim. 6: 1718). 17) Kuungama dhambi (Yakobo 5:16). 18) Kuombeana (Yakobo 5:16). 19)

Kukaribishana (1 Pet. 4: 9).

20) Kunyenyekeana (1 Pet. 5: 5). Maagizo haya yote yanaonyesha kwamba Kwa uhusiano wa waumini katika ni wa muhimu sana. na katika kutekeleza maagizo haya, watu wa Mungu hutimiza Amri Kuu ya pili, ya kumpenda jirani yako kama nafsi yako (Mk. 12:31; Yn. 13:34; 15:12), na hivyo kuuimarisha mwili wa Kristo (taz. Rum. 14:19; 15: 2) na kuonyesha upendo wa Kristo kwa ulimwengu unaotutazama (Yn. 13:35). Tukifanya mambo haya tunakuwa 62

tunauvuta ulimwengu kwa Kristo kwa kuona upendo wetu sisi kwa sisi. Mambo haya si magumu kuyatekeleza kwa kila mmoja, bali yanahusu namna ambavyo unamuona muumini mwenzio. Hivyo Kanisa linapaswa kusisitiza kwa nguvu zote Waumini kutekeleza mambo hayo 20 ili mwili wa Kristo ujengwe. 3. Kufanya Uinjilisti. Kanisa ambalo linafuata kwa bidii utukufu wa Mungu moja kwa moja litakuwa na msisitizo mkubwa juu ya uinjilisti, katika maeneo ya jirani na hata ulimwenguni kote. Utume Mkuu wa uinjilisti umeelezwa na Yesu mwenyewe katika Mat. 28:18-20. Kwamba “Yesu

akaja

kwao, akasema nao, akawaambia,

Nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani. Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu; na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi; na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari.” Utume Mkuu unaonyesha kwamba uinjilisti wa kweli unahusisha kufanya wanafunzi, na siyo tu kuwashawishi wasioamini ili wafanye maamuzi yao. Wenye dhambi wanapoitikia kwa imani

ujumbe wa

Injili,

wanapaswa

kuingizwa na

kuorodheshwa kanisani kwa njia ya ubatizo na kufundishwa na Kanisa kupitia mafundisho mazuri. Makanisa mengi hutumia 63

katekisimu kuwafundisha wanafunzi kabla ya kuwabatiza ili kuwafanya kuwa wanafunzi wa Yesu. Kanisa linaweza kubuni mbinu mbalimbali za kuwafundisha waongofu wapya. Mfano wa kufanya wanafunzi ulianzishwa na Yesu mwenyewe, ambaye alitaka kufanya wanafunzi wakati wake alipokuwa katika huduma yake duniani (Marko 1:16-22; 2:14; Yn. 8:31). Mfano wake unapaswa kuendelezwa na watu wake. Wafuasi wa kweli wa Kristo wanakuwa "wavuvi wa watu" (Mt. 4:19), maana yake ni kwamba wale ambao wanakuwa wanafunzi wake wanapaswa kufanya wanafunzi wengine. Kwa kila mwanafunzi wa Yesu lazima kufanya mwanafunzi mwingine. Kanisa linawajibika kuwafundisha Waumini wote kuwa wanafunzi na kufanya wanafunzi. Waumini wa Kanisa la kwanza walitambuliwa na shauku yao kubwa ya kuhubiri Injili na kufanya wanafunzi (Mdo. 2:47; 14:21). Bidii yao iliwafanya viongozi wa Kiyahudi kuwa na uhasama kwa mitume na waliwaambia “mmeijaza Yerusalemu mafundisho yenu, na mnataka kuileta damu ya mtu yule juu yetu."(Mdo. 5:28). Paulo na wamishonari wenzake walishtakiwa vilevile kwa kuupindua ulimwengu (Mdo 17: 6). Tangazo lao la ujasiri la wokovu kupitia Yesu Kristo lilisikika ulimwenguni kote (Mdo. 1:8; 19:10). Kanisa linapaswa kutambuliwa kwa ujasiri wa kuhubiri Injili; mara nyingi mimi hupenda kutumia “vurugu za 64

kiroho.” Kanisa halipaswi kunyamaza hata kidogo, ni lazima lipige kelele, lipige mbiu ili wenye dhambi waje kwa Yesu. Kristo ameamua kutumia Kanisa kama njia ya kuwaleta watu wengine kwake, Kanisa linapawa kutii agizo hili muhimu. Waamini wanapaswa kuwa na hamu ya kutangaza habari njema ya wokovu. Ingawa Kanisa litaendelea kumuinua Kristo na kujengana katika utukufu wa mbinguni, uinjilisti ni jambo linaloweza kufanywa tu katika maisha haya.

Kwa ujumla

tunaweza kusema kwamba Agano Jipya linaonyesha uinjilisti kama jukumu la viongozi wa Kanisa (2 Tim. 4: 5; cf. Efe. 4:11), Ni jukumu pia la Wakristo binafsi (1 Pet. 3:15), na Kanisa kwa ujumla (1 Pet. 2: 9). Kanisa linapaswa kuwekeza nguvu nyingi katika kuwafikia watu walio nje, na baada ya kuwaleta ndani linapaswa kuwachunga ili wasiraruliwe na adui. Kwa kuwa Kanisa linao mwongozo wake mzuri wa namna linavyowalea waongofu wapya na wale walio ndani ya Kanisa kwa muda mrefu, ni jukumu la wazee na viongozi wengine kuhakikisha kwamba wanatekeleza jukumu hili muhimu. Waamini wa kawaida hawawezi kwenda kuinjilisha bila kuona moto na nia ya viongozi wa Kanisa. Tutekeleze makusudi ya Kanisa kama ambavyo Bwana ametuagiza.

65

Hivyo basi japokuwa inawezekana kukawepo na makusudi mengine mengi ya Kanisa, haya ambayo tumejifunza, ambayo ni; kumtukuza Mungu, kuwajenga waumini na kufanya uinjilisti ni ya muhimu mno katika Kanisa ili Kanisa liweze kusimama katika nafasi yake.

SURA YA NNE SERIKALI YA KANISA Kanisa ni jamii ya watu wengi. Jamii ya watu wengi inahitaji muundo na mfumo maalumu. Inahitaji siasa kusimamia mfumo huo. Wanafunzi wa Yesu walikuwa ni aina ya jamii ambayo ilionesha mfeumo fulani wa siasa katika uongozi wao. Jumuiya ya wanafunzi wa Yesu walikuwa na mhasibu. Katika 66

Yohana. 13:29, tunasoma kwamba "Yuda alikuwa na mkoba wa pesa" na walisherekea Sakramenti (Mt.26: 26-29). Ushuhuda wa mfumo ulionekana wazi katika kipindi cha mitume. Kulikuwa na mikutano ya ibada (Mdo 20: 7, "Siku ya kwanza ya juma, tulipokusanyika pamoja kuvunja mkate"). Maafisa walichaguliwa kwa kupiga kura. Katika Matendo 1: 23-26 tunaona kwamba Yusto na Mathias walipendekezwa kabla ya kupigiwa kura. Tukisoma Matendo 6:5-6, kuna mashemasi saba ambao walichaguliwa kwa kura. Kuna maafsa wa Kanisa kama vile wazee (Mdo .20: 17), waangalizi (maaskofu) (Mdo 20:28; Phil.1:1), na mashemasi (dikoni) (Phil. 1:1). Masuala ya kinidhamu yalizingatiwa ndani ya Kanisa (Mt.18:18, "chochote utakachofunga duniani kitafungwa mbinguni, na chochote utakachofungia duniani kitafunguliwa mbinguni). Katika 1Kor5:4,5, 13, tunaona kwamba Washirika wa Kanisa ambao waliojihusisha na uzinzi walifukuzwa kutoka katika ushirika. Changizo kwa Washirika masikini wa Kanisa la Yerusalemu lilifanyika (Rom.15: 26; 1Kor.16: 1,2; 1Kor 8,9). Pia tunaona kwamba kulikuwa na orodha ya Washirika wa Kanisa (1Tim5:9, orodha ya wajane), kulikuwa na ubatizo (Mdo 2:41) na masharti ya Ushirika Mtakatifu (1Kor. 11: 23-26), kulikuwa na maagizo (Kol.2:5), kulikuwa na masharti ya kuingia kanisani (Mt.28:19, kwamba lazima aokoke na kubatizwa (Mdo 2:47). Kwa maelezo hayo ni Dhahiri kwamba kulikuwa na serikali ya kanisa, 67

kulikuwa na muundo fulani kwa ajili ya kuongoza jamii hii ya kiroho na kimwili. Katika sehemu inayofuata, tutaangalia aina anuwai za serikali za kanisa. I. Aina Anuwai za Serikali ya Kanisa Kuna aina mbalimbali za serikali za Kanisa hapa duniani. Kila serikali hujinasibu kutokana na neno la Mungu. Tutachambua baadhi ya serikali hizo, na mwisho tutang’amua ni serikali ipi ya Kanisa ambayo inafuata angalau misingi wa Kibiblia kwa sababu hakuna serikali ya Kanisa ambayo ni kamilifu. 1. Wasiona na serikali: Quakers na Darbyites (Kwaka na Dabite) Hawa, wanakataa aina yoyote ile ya serikali ya Kanisa, wanadai kwamba serikali za Kanisa mara zote huenda kinyume na Ukristo wa asili. Wanadai kwamba serikali ya Kanisa inamkuza na kumtukuza mwanadamu kwa mgongo wa Mungu. Hakuna haja ya kuwa na muundo maalumu wa serikali ya Kanisa, hivyo Kanisa linahitaji kuongozwa na Roho Mtakatifu. Na kama Kanisa likiongozwa na Roho Mtakatifu, basi mwenye kuanzisha serikali hiyo ni Mungu mwenyewe. Wao wanaamini kwamba Mungu anaweza kuwaongoza leo kwa njia hii, na kesho kwa njia nyingine. Hivyo kuunda serikali ya Kanisa ni kupuuza maelekezo ya Kimungu katika maisha ya mwanadamu. 68

Kwa kifupi, hawa wananaamini kwamba wote wanaweza kuwa viongozi. Na ndiyo maana jina lao la asili wanaitwa “marafiki” hakuna kiongozi maalumu, wala mgawanyiko wa majukumu. Kila mmoja anaweza kufanya kitu kwa kutegemea maelekezo ya Roho Mtakatifu. Makanisa haya yalianzia kule Uingereza na siku hizi yako kule Marekani. Berkhof anatujuza kwamba siku hizi wanasimika wachungaji na kuchagua wazee wa Kanisa. 31 Hapo tunaweza kugundua kwamba ingawa wanakataa kwamba Kanisa halihitaji kuwa na serikali yake, bado wenyewe wameona ni vigumu sana kuendesha shughuli za Kanisa bila kuwepo kwa serikali ya Kanisa. 2. Serikali ya Ki-Erastiani Mfumo huu unatokana na jina la Thomas Erastus (15241583). Huyu alikuwa ni daktari huko Heidelberg katika karne ya kumi na sita, alipendekeza mfumo wa serikali ya Erastian ambao ulitafsiri Kanisa kama aina ya jamii inayoundwa na sheria za kitaifa. Kulingana na mfumo huu, maafisa wa Kanisa wana haki tu ya kutangaza Neno na haki ya nidhamu imekabidhiwa kwa serikali. Makanisa ya namna hii yalikuwepo huko Uingereza, Skotland, na makanisa ya Kilutheri ya Ujerumani kwa wakati ule. Mfumo huu unazipa serikali za kidunia madaraka makubwa kwa 3131

Berkhof, Louis. Systematic Theology (Grand Rapids: Eerdmans 1974), uk.

642

69

Kanisa. Kanisa linatoka kwenye nafasi yake na kuruhusu utawala wa serikali kuingilia masuala ya Kanisa. Ikumbukwe kwamba ingawa kuna uhusiano kati ya Kanisa na serikali za kiraia, bado pana tofauti kubwa sana. Yesu aliwahi kusema vya kaisari mpeni kaisari, na vya Mungu mpeni Mungu. (Luka 20:25). 3. Serikali ya Ki-askofu (Episcopal) Ifahamike kwamba mfumo wa kiasikofu wa Kanisa Katoliki, una tofauti kidogo na mfumo wa kiaskofu wa makanisa mengine yanayoongozwa na maaskofu. Hata hivyo, nitajadili kwa ujumla wake; huku nikigusa Ukatoliki, na hata makanisa mengine kwa namna moja au nyingine. Mfumo wa kiaskofu unahusu aina ya serikali ya Kanisa ambayo ofisi ya Askofu ina mamlaka makubwa. Neno episcopal limetoka kwa neno la Kiyunani kwa Askofu. Katika mfumo huu, Kanisa la mahali ni sehemu ya uongozi wa makasisi ambao husimamia na kudhibiti Kanisa. Hii kwa kawaida inajumuisha maaskofu wa kikanda (dayosisi) inayoongozwa na Askofu Mkuu.32 Madhehebu ambayo hufanya kazi na aina hii ni pamoja na

32

Mock, J. Dennis, Church Ministry Administration-Education (Atlanta: BTCP, 1989), 80

70

Othodoksi ya Mashariki, kanisa la Romani Katoliki, Anglikani, Wamethodisti, na Kilutheri.33 Mfumo huu umekuwa wa muda mrefu, ingawa umekuwa ukiboreshwa mara kwa mara. Lakini kwa asili mfumo wa Kiaskofu au episcopali unakaza kwamba Kristo alikabidhi haki ya usimamizi wa Kanisa kwa maaskofu ambao ni warithi wa mitume. Ushiriki wa waumini wa kawaida katika serikali ya Kanisa hairuhusiwi. Kanisa la awali la Roma Katoliki lilichukua mfumo huu. Lakini ikumbukwe kwamba ofisi ya mtume ilimalizika hata kabla ya mwisho wa karne ya kwanza. Taarifa ya Paulo kwamba yeye ndiye "Mwisho wa wote" inamaanisha kuwa hakutakuwa na ofisa ambaye ana nguvu na haki za mitume baada yake. Maandiko ya Agano Jipya hayasemi kwamba kutakuwapo na kundi la makuhani wakuu, ingawa katika Kanisa Katoliki maaskofu ni aina fulani ya makuhani. Kabla askofu hajafikia nafasi hiyo huanzia daraja la ukuhani (mapadri). Mfumo huu katika kanisa Kikatoliki tunaweza kuita ni mfumo kamili wa kifalme ni hitimisho la mfumo wa kiaskofu. Kanisa Katoliki linafikiria kwamba mrithi wa Petro yumo ndani, ambaye ni papa. Kanisa Katoliki linasisitiza kwamba ufunguo ambao Yesu alikuwa amempa Petro (Mat.18:19) ulihamishiwa kwa 33

Ezamo Murry, An Introduction to Pastoral Care and Counselling (Delhi: ISPCK, 2011). 89

71

papa. Papa ana haki ya kuamua mafundisho, ibada, na serikali ya Kanisa. Papa ana mamlaka ambayo yaweza kuwa ni bora kuliko yale ya Maandiko, kwani ana haki ya kupendekeza tafsiri ya mwisho ya Maandiko. Kwa upande mwingine, wafuasi hawana haki katika serikali ya Kanisa. Hakuna msingi wa kibiblia kwa hoja kwamba waumini wa kawaida hawana haki ya kutoa maoni yao juu ya maswala ya Kanisa. Kanisa Katoliki wakizungumzia juu ya Baraza la Yerusalemu

wanadai

kwamba

Petro

ndiye

aliyehitimisha

majadiliano katika kikao hicho. Hivyo, wanadai kwamba Petro alikuwa anamwakilisha Yesu Kristo kwenye Mkutano huo, na hivyo ni dhahiri kwamba alikuwa na mamlaka kuliko mitume wengine. Tunahitaji kujua kwamba Kanisa Katoliki lilipotoka katika hoja zao. Kwani kile ambacho Mitume walikihamishia kwa watumishi wa Mungu si mamlaka bali ni mamlaka ya Injili ambayo ni msingi wa ushuhuda wa Kristo. Isitoshe, mitume hawakutoa madaraka ya serikali. Kwa hali hii, walikuwa tofauti na wale ambao walijifanya kuwa wafuasi wa mitume na walipata nguvu ya serikali kutoka kwa yule mwingine. Kwa mfano, mitume waliamua juu ya maswala muhimu ya Kanisa sio kwa hiari yao bali kupitia mabaraza ya Kanisa (Mdo 15). Isitoshe, msimamizi wa baraza la Kanisa la Yerusalemu hakuwa mtume bali ni Yakobo. 72

Peter na Paulo walishiriki kujadiliwa chini ya uongozi wa Yakobo (Mdo 15: 7,12). Katika mfumo huu, kwa wale ambao wanatekeleza mamlaka yake, ni kwamba askofu anaweza kuamua jambo lolote lile kwa niaba ya Kanisa. Askofu anaweza kumfukuza mchungaji wa Kanisa fulani wakati wowote kama ataona kwamba hafai, au hata akionekana kumpinga katika mambo fulanifulani. Askofu anaweza kufanya jambo lolote lile ikiwa anaona ni kwa manufaa ya kanisa, hata bila kujadiliana na kanisa. Lakini hoja hizi zinapingana na serikali ya Kanisa la kwanza. Ile hali ya ushirikishwaji wa waumini na viongozi wengine ilikuwa ndiyo inatawala Kanisa la kwanza. Kama tulivyosema hapo juu kwamba mfumo huu umekuwa ukirekebishwa mara kwa mara. Makanisa ambayo yanatumia mfumo huu yamejaribu kuchanganya na mifumo mingine na kujaribu kupunguza nguvu ya askofu ili asitumie mamlaka yake binafsi. Hata hivyo, bado Kanisa Katoliki linashikilia ukuu wa maaskofu katika majimbo yao. Askofu ana mamlaka juu ya makutaniko kadhaa katika eneo fulani, ambalo mara nyingi huitwa dayosisi. Makanisa ya Methodist, Wesley, Anglikana, Kilutheri na Kanisa la Wazawa la Africa Inland Church in Tanzania liliamua kuchukua

muundo

mfumo

huu

ingawa

umechanganywa

changanywa na mifumo mingine ya kanisa. Siku hizi kuna tofauti 73

na zamani kidogo kwani kumekuwepo na namna fulani ya mgawanyo wa madaraka kwa watu wa kawaida, hata hivyo kwa kuwa wana maaskofu, basi wapo katika kundi hili. Makanisa mengi ya Kipentekoste pia yana mifumo ya kiaskofu, lakini ama kwa hakika walio wengi hulitumia neno hili bila kujua asili yake, huku wengine wakidai ni cheo cha heshima; jambo ambalo ni hatari kwa kanisa zima. Sitazungumza kuhusu mfumo huu katika makanisa ya Kipentekoste kwa sababu kwani vitabu vinavyozungumzia masuala ya utawala wa makanisa ya kipentekoste si rahisi kuvipata. Kuna kitu cha muhimu mahali hapa cha kujifunza. Kila kitu huwa kina ubora wake. Kuna faida kadhaa za muundo wa serikali ya kiasikofu. Kwanza, serikali ya aina hii ni rahisi katika kufanya maamuzi, hasa ikiwa askofu husika atakuwa na nidhamu katika utumishi na akaongozwa na Roho Mtakatifu katika maamuzi yake. Pili, hurahisisha utendaji kazi kwa kutokuchelewesha suala zima la maamuzi. Badala ya kuwa na vikao vingi, na kupitia demokrasia ya hali ya juu, basi askofu akishaamua, ndio mwisho wa malumbano. Inaweza kusaidia kukua kwa Kanisa haraka, kuliko demokrasia. Hata hivyo, tungependa kusema kwamba wanadamu ni wenye dhambi. Maamuzi ya binadamu mmoja hayawezi kufaa kwa ajili ya mustakabari wa Kanisa zima. Hivyo kuna mifumo mingine ya serikali inayoweza kufaa zaidi. Serikali ya kiaskofu 74

inamwinua mtu mmoja kuliko watu wengine, na ndiyo maana hata watumishi walio katika mifumo hii mara nyingi wanalalamika kuhodhiwa kwa madaraka na mtu mmoja. Tunahitaji kuangalia mifumo mingine zaidi 4. Serikali ya Ki-Kusanyiko (Congregationalism) Mfumo wa kusanyiko unaonyesha kuwa kusanyiko la Kanisa ni Kanisa huru na kamili. Kwa hiyo, haki ya nidhamu ni ya Washirika wote wa Kanisa. Maafisa wameteuliwa kusimamia maswala yote ya Kanisa. Nguvu ya maafisa haiwezi kuwa juu ya ile ya Washirika wa Kanisa. Makanisa ya kawaida yanaweza kuungana na kuunda baraza, lakini baraza hili halina nguvu ya kudhibiti kitu chochote kwa sababu nguvu kubwa iko kwa “kusanyiko.” Kama waumini wa Kanisa fulani wasipompenda mchungaji, basi wanaweza kumfukuza mara moja kwa sababu wao ndio wana mamlaka ya mwisho kuhusu masuala ya Kanisa. Kutaniko linachagua bodi ya watu wanaosimamia mapenzi ya kusanyiko na kutoa maoni yake, lakini mwishowe ni mkutano ambao unasimamia maisha ya Kanisa. 34 Wanashikilia kwamba "kusanyiko linajisimamia chini ya ukuu wa Yesu Kristo (Christocracy)

na

kwa

uongozi

34

wa

Roho

Mtakatifu

Lloyd M. Hall & Karl D. Schimpf, Principles and Practices: The Congregational Way of the Churches of the National Association, (Olivet: Congregational Press, 1995), 3

75

(pneumatophoria) bila ya mkuu au kiongozi wa kikanisa (uhuru) na kwa kila mshiriki kuwa na sauti katika maswala ya kimaamuzi (demokrasia)."35 Mfumo huu unapata msingi mpana wa msaada wa Biblia katika Agano Jipya ikijumuisha Baraza la Yerusalemu (Mdo 15), ambapo mitume, wazee na mkutano wote walikuwa wamehusika katika mchakato wa utoaji wa maamuzi. Pia kwamba Kanisa la kwanza walichagua maafisa wake wenyewe na wajumbe (Mdo 6: 1-6; 15: 2-3), na kwamba nguvu ya kutekeleza nidhamu yake ya Kanisa ilikuwa juu ya waumini wote 1 Kor 5: 1-13 2 Kor 2: 5-11 2 Thess. 3: 14-15 na Kanisa pamoja na maafisa wake walihusika katika kufanya maamuzi (Mdo 15:22) kupokea wawakilishi (Mdo 15: 4; 18:27 na kuwatuma wamishonari (Mdo 13: 3; 14:26). Karibu makanisa yote ya Ki-Baptist yana aina hii ya serikali ya Kanisa, na baadhi ya makanisa ya Kipentekoste.36 Ubora wa mfumo huu ni kwamba hutoa usawa kwa washirika wote kushiriki katika maamuzi ya Kanisa, na hivyo hufanya waumini wakomae zaidi katika kufanya maamuzi. Pia, ni mfumo unaotoa demokrasia kanisani, ambayo kila mshiriki wa

35

James Leo Garrett, Jr., Systematic Theology: Biblical, Historical, and Evangelical, 2d ed. (BIBAL Press: North Richland Hills, TX, 2001), 2:644. 36 Henry G. Weston, Constitution and Polity of the New Testament Church (Philadelphia: American Baptist Publication Society, 1895), uk. 66.

76

Kanisa anahusika katika kufanya maamuzi, na hii inapunguza malalamiko pale ambapo mambo yaliyoamuliwa yanapoenda sivyo yalivyokusudiwa. Robert anasema kwamba "mara nyingi watu walio chini hulalamika kwa kutoshiriki katika maamuzi.” 37 Kwa hiyo mfumo huu unawafaa sana. Labda udhaifu mkubwa wa mfumo huu ni kwamba nguvu za maamuzi mara nyingi zinaweza kubaki mikononi mwa wengi ambao hawana uzoefu na wala hawajapewa mafunzo ya kiuongozi au vipawa vya kuongoza Kanisa au dhehebu. Hali hii ya utawala inazuia utendaji kazi ambapo upo Kibiblia Vile vile maamuzi ya Kanisa la mtaa (local church) kuwa ya mwisho ni hatari sana; kwa mfano makosa yanapofanywa katika Kanisa la mahali, sio rahisi kusahihisha uamuzi wa Kanisa hilo, na hii inasababisha kuvunjika kwa umoja kanisani. Na tena ikiwa uamuzi ni mbaya huvuruga Kanisa zima. Vilevile ni dhahiri kwamba si rahisi kuendesha Kanisa kwa mfumo huu. Ni mfumo ambao upo katika maandishi zaidi lakini kiutekelezaji ni vigumu sana. Katika nchi nyingi umekabiliwa na changamoto. Kwa mfano huko Korea, "makanisa ya Kikorea na Amerika ya Baptist yalipata changamoto na kuamua kutumia

37

Robert D. Dale, Pastoral Leadership: A Handbook of Resources for Effective Congregational Leadership (Nashville: Abingdon, 1986) uk. 15.

77

mfumo wa Kipresbiteri. Haishangazi wakati hata wao wenyewe wanadai kwamba "Ni lazima ikubaliwe kuwa, si katika kila nyanja ya siasa demokrasia ni njia sahihi ya serikali kuna wakati mwingine udikteta unaweza kuwa na ufanisi mkubwa."38 Walakini, tukiri kwamba mfumo wa kusanyiko ni bora zaidi kuliko wa kiasikofu kwani ndani yake kuna ushahidi wa msingi wa Maandiko, lakini tunashindwa kuona ni wapi katika historia ya Kanisa la kwanza mfumo huu ulifanyika. Wengi wanaamini kwamba serikali ya Kanisa la kwanza ilikuwa na mfumo changamani; kusanyiko na Upresibiteri. Karibu makanisa yote ya Ki-Baptist yana aina hii ya serikali ya Kanisa, na baadhi ya makanisa ya Kipentekoste. 39 Ingawa wamechanganya mifumo kadhaa ili kuboresha kulingana na mazingira ya Kanisa lilipo. 5. Serikali ya Ki-Kipresbiteri Presibiteri (Presbyterian) inatokana na neno la kigiriki presbyteros, ikimaanisha "mzee” au “mtu mzima" na Presbiteri ikimaanisha "mwili au baraza la wazee." Neno la Agano la Kale ni

38

Young Sik Noh, “Equipping Church Leadership to Implement Baptist Congregational Polity for New hope Korean Baptist Church, Lake Forest, California” (D. Min. project, Southern Baptist Theological Seminary, 1997), esp. 1-2 haijapigwa chapa. 39 Henry G. Weston, Constitution and Polity of the New Testament Church (Philadelphia: American Baptist Publication Society, 1895), uk. 66.

78

“Zaqen” ambalo linamaanisha "mzee (kiumri) au ndevu"40 Kuna uhusiano wa wazi unaoonesha kwamba huu ndio mfumo wa serikali uliodhamiriwa kutumiwa katika Biblia. Njia hii ya serikali ina jina la dhehebu la "Kanisa la Kipresbiteri 41 ” Kanisa la Presbyterian linasimamiwa na wawakilishi, yaani wazee.”42 Chini ya mfumo kama huo, makanisa ya kawaida yanasimamiwa, na wazee waliochaguliwa na mkutano."43 Wapresibiteri wanaamini kwamba Agano Jipya hutumia maneno "Askofu" na "mzee" kurejelea huduma ileile iliyoamriwa. Uongozi wa Wapresibiteri huwa na aina mbili ya wazee: wazee wafundishao na watawala watawalao. Hii ni katika kutofautisha majukumu yao. Inaaminika kuwa "Kanisa" huko Antiokia lilikuwa ni “Presibiteri”44 yenye makanisa kadhaa ambapo ilituma wawakilishi

40

Miller, Hays Park, Why I am a Presbyterian (New York: Stratford Press, 1959),73 41 Neno la Kiingereza “Presyterian” linabeba jina la “dhehebu” hivyo basi haifai kulibadilisha jina kwa kutafsiri kwamba Kanisa la wazee. Katika kitabu hiki tunatohoa neno hili na kulitumia kama “Kipresbiteri” 42 Julie Bowe, et al.., The Presbyterian Handbook (Louisville: Geneva Press,2006)180 43 McKim, K. Donald, More Presbyterian Questions, More Presbyterian Answer: Exploring Christian Faith, (Louisville: Geneva Press,2011)2 44 Presibiteri (kwa kiingereza Presbytery) ni eneo lenye makanisa kadhaa; katika muktadha wa Tanzania ni majimbo. Hata hivyo katika kitabu hiki kwa ajili ya kutunza uasilia wake tutatumia “presibiteri” tukimaanisha “baraza la jimbo”

79

kwenda kwenye Mkutano Mkuu kule Yerusalemu (General Assembly) 45 . Mkutano huo na wazee huko Yerusalemu (baraza kuu la Yerusalemu) "mkutano mkuu."

Katika mkutano wa

Kipresibiteri, wazee wote wako sawa. 46 Wazee wa aina mbili: wazee wafundishao ndio wachungaji waliosimikwa katika majimbo (presbytery) zao, na wazee watawalao ni wale waliosimikwa katika makanisa yao ya mahali (Local church) na hawa kwa pamoja hutengeneza bodi ya maamuzi ndani ya Kanisa. Wapresibiteri wanaamini kuwa Roho Mtakatifu huongea waziwazi juu ya maswala ya serikali kupitia maombi ya vikundi vya wasimamizi. Wanaamini kuwa vikundi kwa kawaida haziwezi kuingia katika makosa kuliko watu binafsi. Kwa maana ya kwamba mtu binafsi kama vile askofu ni rahisi sana kuingia kwenye makosa kuliko kundi la watu maalumu waliochaguliwa kuwakilisha kundi la watu wengi. Tofauti ya mfumo huu na ule wa kusanyiko ni kwamba katika ule mfumo wa kusanyiko waumini wote wanaingia katika baraza la maamuzi ya Kanisa. Lakini katika mfumo

huu

waumini

wanachagua

wazee

kwa

ajili

ya

kuwawakilisha katika mabaraza ya juu. yaani jimbo ni eneo lenye makanisa mengi. Makanisa mengine hutumia neno “Chalo.” 45 Mkutano Mkuu (General Assembly) ndilo baraza kuu la kitaifa katika Kanisa la Kipresbiteri. 46 Henderson, G.D, Why we are Presbyterians (Edinburgh: C.J.Cousland & Sons LTD, (n.d),31

80

Asili Upresbiteri Kibiblia Inasemekana kwamba huu ndio mfumo mkongwe wa kiuongozi ndani ya Biblia ambao umefichwa na watu wanaopenda mamlaka makubwa ndani ya Kanisa. Mkutano Mkuu wa kwanza ulitishwa na Musa, na kukusanyika huko Misri (Kutoka 4:29), mamlaka yake ya kutoa wito huu imetolewa katika Kutoka 3:16. Kitabu cha Kumbukumbu la Torati ndio maelezo ya mwisho ya Musa kwa wazee hawa katika masikio ya watu. Vivyo hivyo katika kitabu cha Yoshua sura ya 23- 24 kwa wazee kama wawakilishi wa watu. Tena, kama wawakilishi wa watu, wazee waliweza kumwendea Samweli kumuuliza juu ya kupata mfalme (1 Samweli 8:4). Pia tunaona kwamba wazee kwa niaba ya watu walikuja kwa Daudi huko Hebroni kumualika awe mfalme (II Sam 5: 3). Na wakati wa uhamishoni, walihusika (Eze. 8: 1; 14: 1; 20:12). Wazee walitoa uongozi katika ujenzi wa hekalu baada ya kurudi kutoka uhamishoni (Ezra 5: 5, 9; 6:78, 14). Katika kipindi cha Agano Jipya, wakati wa ujio wa Kristo, taarifa zinatolewa kwa "wazee," "watawala," na "watawala wa sinagogi" (Math. 15: 2; Marko 7: 3; Yoh. 3: 1; 7:26, 48; Marko 5:22; Luka 8:41; angalia. Mdo 18: 8,17). Kinyume na mfumo wa kiasikofu, Mfumo wa Kipresibiteri hautoi madai yoyote kuhusu kazi za wachungaji kuwa kama kazi za mitume. 81

Kanuni za Msingi wa Wapresibiteri ni kwamba; Kristo ndiye Mkuu wa Kanisa ulimwenguni. Serikali zote za Kanisa lazima ziwe chini yake (Efe. 5:23; Wakolosai 1:18). Watu wana haki ya kushiriki katika serikali ya Kanisa. Na bado vitu vyote vinapaswa kufanywa kwa heshima na kwa utaratibu (1 Wakorintho 14:40). Wazee, (wachungaji) wanaofanya kazi kwa neno na mafundisho, ni maafisa wa kudumu wa Kanisa (Mdo 14: 23; 1 Timotheo 5:17; 1Petro 5: 1). Wazee watawalao wanawajibika kuhakikisha usalama wa Kanisa na kuangalia adui asiingie kanisani kuharibu. Wazee hawa wanawakilisha washirika wa Kanisa la mahali ambao hawawezi kushiriki moja kwa moja katika mabaraza ya juu. Kila mfumo una udhaifu wake, Upresibiteri pia una mapungufu yake. Mara nyingi kumekuwepo na malalamiko kwamba mfumo huu unaweza kuzuia mpango wa Kanisa la mahali kwa kuunga mkono maamuzi ya mabaraza ya juu. Vilevile mfumo huu unalaumiwa vikali kwamba miongoni mwa wachungaji katika vikao vya mabaraza hawaheshimiani; kwa maana kwamba wajumbe wa mkutano hawana heshima yoyote kwa mwenyekiti kwa sababu yeye hana mamlaka kama askofu, na kwamba wachungaji wote wako sawa tu. Vilevile mfumo huu umelaumiwa vikali kwa kuchelewesha maamuzi kwa ajili ya maendeleo ya Kanisa. Kwamba mwenyekiti 82

hawezi kufanya maamuzi peke yake, hata kama yakiwa ni maamuzi ya haraka kiasi gani; anahitaji kuitisha kikao na kujadili jambo hilo ili kuweza kuamua kwa pamoja. Jambo hili limekuwa likileta usumbufu mkubwa kwa sababu hakuna kitu ambacho kiongozi huyu anaweza kukifanya zaidi ya kusikiliza mabaraza tu. Pia, udhaifu mwingine ambao umekuwa ukilalamikiwa ni kwamba Kanisa hili linashadidia utengano wa kimakanisa. Kwamba kila Kanisa la mahali lina mamlaka kamili kupitia wazee wa Kanisa la mahali. Kwa sababu hiyo, uongozi wa mabaraza hauna mamlaka yoyote wala kuwa na maono ya kanisa kwa ujumla Kanisa kwa sababu kila Kanisa lina maono yake. Hizo ni baadhi ya changamoto ambazo zinatolewa na watu mbalimbali. Hata hivyo, kama tulivyokiri hapo juu kwamba mifumo yote ina udhaifu, hasa kwa sababu inaongozwa na wanadamu. Pamoja na udhaifu huo, bado tunashikilia kwamba Kanisa la Agano Jipya liligundua wazi uhuru wa kila Kanisa la mahali. Kulingana na majadiliano hapo juu, maoni yangu ni kwamba serikali ya Kanisa la Kipresbiteri ndiyo serikali bora ya Kanisa ambayo imeidhinishwa na Maandiko; hata Agano la Kale linathibitisha juu ya jambo hilo. Ninashikilia aina hii ya utawala wa aina hii ni wa Kibiblia zaidi: 83

Kwanza, serikali ya Kanisa la Kipresbiteri inaungwa mkono na Maandiko. Tumejadili hapo juu jinsi Maandiko yanavyounga mkono kwa wazi kabisa. Hata hapa naweza kuongeza dondoo kutoka kwenye Maandiko Matakatifu: mitume waliteua wazee katika makanisa (Matendo14: 23, katika makanisa ambayo Paulo alikuwa ameyapanda katika safari ya kwanza ya kimisheni; (Mdo 20:17), wazee wa Kanisa la Efeso; Tit.1:5, Paulo alimwagiza Tito achague wazee huko Krete). Wazee waliitwa kama waangalizi (maaskofu) (Matendo20: 28). Yaani askofu kibiblia ni mwangalizi wa kanisani. Ni mchungaji wa kawaida kabisa. Si mtu mwenye mamlaka kama inavyodhaniwa. Kanisa la kwanza liliwateua wazee ambao walifanya kazi katika kuhubiri na kufundisha na kwa kuongezea wazee wanaotawala vyema (1Tim.5:17). Wazee walichaguliwa kwa kura (Mdo 14:23, Mabaraza makubwa ya Kanisa

yalitayarishwa

kama

kusanyiko

la

Yerusalemu

(Matendo15) au baraza la wazee (1Tim.4: 14). Kwa kulinganisha serikali na serikali tulizojadili hapo juu ni wazi kwamba Kipresbiteri ni ya Kibiblia zaidi. Pili, serikali ya Kanisa la Kipresbiteri inaungwa mkono na mababa wa Kanisa pia. Lazima tukumbuke kuwa mila za Kanisa ni nzuri kwani zinatusaidia kuelewa zama za kitume. Mababa wa

84

karne ya nne kama Ambrose na Jerome "kwa kweli wanaona Kanisa la kwanza lilikuwa la Kipresibiteriani."47 Tatu, hata watu wanaoamini mfumo wa “kusanyiko” wanakiri kwamba inawezakana mwanzoni kabisa serikali ya Kanisa ilikuwa ya Kipresibiteri na kikusanyiko.

Serikali ya

Kipresibiteriani inatofautishwa na makanisa ya Kiasikofu kama Kanisa Katoliki, Kanisa la Uingereza au Kanisa la Kiaskofu la Kiprotestanti (kama la Lutherani) ambalo mamlaka zote ziko mikononi mwa Askofu. Katika Kanisa la “kusanyiko” tunaona Washirika wote wa Kanisa wana mamlaka sawa; hii sio ya Biblia, kwani Mungu amekuwa akichagua vikundi kadhaa vya watu kuwakilisha.48 Binafsi naamini kuwa serikali ya Kanisa la Kipresibiteri haiwezi kuelezewa kwa maandishi yenye ufanisi, ingawa inahitaji mabadiliko kadhaa katika utekelezaji wake kwa kuzingatia eneo husika, lakini ni mfumo wa kibiblia.

Hitimisho dogo kwenye serikali Ni kweli kwamba kila mfumo wa serikali ya kikanisa una changamoto

zake,

lakini

tunahitaji

47

angalau

kufuata

John, Calvin, Institutes of Christian Religion, (Philadelphia: Westminster Press, 1959),IV.4.2 48 Cunningham, William, Historical Theology, (Banner of Truth, 1960), 76

85

ule

unaokubaliana na Biblia. Siku hizi makanisa mengi yamekuwa yakichanganya mifumo ya kiutawa; Mchanganyiko wa kiaskofu “kusanyiko” na Kipresbiteri. Kwa mfano Kanisa la Africa Inland Church Tanzania (AICT) linaongozwa na serikali ya kiaskofu), lakini huku chini linayo mabaraza ya Wazee (mifumo ambayo inashadidiwa na Upresibiteri). Pia hata makanisa ya Kibaptisti yaliyo mengi yameondoa aina ya utawala wao na kuchanganya na Upresibiteri. Hii inamaanisha kwamba Upresibiteri ni mfumo wa utawala wa Kibiblia. II. Kanisa na serikali za Kiraia Kama tulivyoona hapo awali kwamba serikali ya Erastiani wanasema kwamba serikali iko juu ya Kanisa. Kwa hiyo Kanisa linapaswa kutii serikali kwa kila jambo. Rais wa nchi ndiye kiongozi wa Kanisa. Hata hivyo, tunahitaji kujiuliza, je ni uhusiano upi ambao Kanisa linahitaji kuwa nao. Kuna mambo mawili ya msingi ambayo tunapaswa kuyazingatia mahali hapa; jambo la kwanza ni nguvu ya kanisa, kwamba kanisa linapata wapi nguvu yake, na pili, nguvu ya serikali, je serikali inapata wapi nguvu zake. 1. Nguvu ya Kanisa Ingawa kanisa lina serikali yake, hata hivyo nguvu ni nguvu ya kiroho. Kwa kweli, chanzo cha nguvu ya Kanisa ni Yesu 86

Kristo, kichwa na mfalme wa Kanisa. Ukweli kwamba Yesu Kristo ndiye kichwa na mfalme wa Kanisa lazima ueleweke pia sio tu kwa maana ya kiroho lakini pia kwa suala la muundo wa utawala wa Kanisa. Kwa maneno mengine Yesu Kristo ndiye mfalme na mkuu wa Kanisa kwa maana ya kuwa yeye ndiye kiongozi wa Kanisa. Hii ni nguvu ambayo milango ya kuzimu haiwezi kuishinda (Mt.16:18), nguvu ya kuufungua na kuufunga ufalme wa mbinguni na kuifunga na kuufungua kutoka duniani (Mt.16: 19). Nguvu hii ilitolewa kwanza kwa mitume kikamilifu, na kisha kwa makanisa yote. Nguvu hii inahusu mamlaka ya kuamua kile kinachoruhusiwa na kile kinachopaswa kukatazwa. Hasa, Yohana 20:23 inasema kwamba mitume na Kanisa wamepewa nguvu ya kusamehe dhambi. Sababu ya Yesu Kristo kuwapa nguvu hii ni kwamba msamaha wa dhambi ndio ufunguo wa kuamua ikiwa mtu anaweza kwenda kwenye ufalme wa mbinguni au la. Walakini, hii haimaanishi kwamba Petro au Kanisa lenyewe lina nguvu ya kusamehe watu dhambi, lakini neno la Injili ambalo Petro au Kanisa lilipokea kutoka kwa Bwana na kutangazwa lina nguvu ya kusamehe dhambi. Ikiwa watu wanakubali neno la Mungu, dhambi zao

zitasamehewa,

na

ikiwa

hawatakubali,

dhambi

zao

hazitasamehewa. Kanisa linayo nguvu ya kushughulikia nidhamu ndani ya Kanisa kwa ustahilivu (1Kor 5: 7,13; 6: 2,4). 87

Viongozi wa Kanisa hupokea ofisi zao kupitia mkutano, lakini nguvu ya ofisi zao hupewa moja kwa moja na Kristo. Ni dhahiri kwamba kamwe hawezi kupokea nguvu yao kutoka kwa serikali za kiraia. Kwa mujibu wa Kanisa Katoliki, nguvu ya Kanisa inapatikana kwa Papa ambaye anasimama kwa niaba ya Mtume Petro. Na kwamba Papa hakosei kitu chochote katika maamuzi yake. Hata hivyo siku hizi wamebadilisha na kudai kwamba Papa anaweza kukosea ikiwa atazungumza nje ya Kiti cha Petro kilichopo Roma katika Kanisa la Mtakatifu Petro. Kinyume na Wakatoliki mfumo wa serikali ya Erastiani unatafsiri Kanisa kama sehemu ya serikali. Hali serikali ni aina ya taasisi ya Kiungu.Kwa hiyo ina jukumu la kutangaza mafundisho na kutekeleza Sakramenti na nidhamu, pamoja na kuteua maafisa wa Kanisa, na kusimamia usimamizi wa Kanisa. 1. Nguvu ya serikali ya kiraia Kwa mujibu wa Maandiko, serikali ya kiraia ni taasisi ya Kiungu ambayo imekabidhiwa wito wa kulinda haki za raia. Maafisa wa serikali ni watumishi wa Mungu. Katika Warumi 13:14 “Kila mtu na aitii mamlaka iliyo kuu; kwa maana hakuna mamlaka isiyotoka kwa Mungu; na ile iliyopo umeamriwa na Mungu. Hivyo amwasiye mwenye mamlaka hushindana na agizo 88

la Mungu; nao washindanao watajipatia hukumu. Kwa maana watawalao hawatishi watu kwa sababu ya matendo mema, bali kwa sababu ya matendo mabaya. Basi, wataka usimwogope mwenye mamlaka? Fanya mema, nawe utapata sifa kwake.” Lazima serikali itambue haki kwa kuwalinda na kuwatia moyo wale watendao mema na kuwaadhibu wale wanaotenda mabaya (Rum.13: 5). Kwa kuwa Kristo ndiye Mfalme wa ulimwengu na pia kichwa cha Kanisa, basi: kwanza, serikali lazima itambue kwamba Kristo ndiyo mamlaka ya juu zaidi, na kwamba kufuata mapenzi yake katika uongozi ndilo jambo muhimu. Hata sasa nazungumzia viongozi serikali za kiraia ambao ni Wakristo. Viongozi hawa wanapaswa kuongoza kwa kufuata mapenzi ya Kristo, kwa sababu sheria za nchi zote zimelenga kuboresha maisha ya raia wake. Katika serikali za kiraia unapoona kuna mambo ya rushwa yametawala zaidi, ujue kwamba viongozi hao hawajamruhusu Kristo kuwa ndiye mwenye mamlaka kuu. Viongozi wengi wa serikali za kiraia wanapoingia madarakani huonekana kuwa na sura mbili; wakitenda yaliyo kinyume na kanuni za Kimungu, wakipokea rushwa kwa kisingizio cha kwamba “Ya Kaisari Mpeni Kaisari,” nukuu ambayo imenukuliwa vibaya. Nukuu ya “Kaisari Mpeni Kaisari” maana yake ni utofauti kati ya Kanisa na serikali tu. Kwa maana ya kwamba mchungaji au askofu hawezi kumwamrisha raisi 89

wa nchi afanye jambo fulani, (lakini raisi huyu pia ni muumini wa kanisani, na anatii sheria za kikanisa); vilevile serikali haiwezi kusema kitu chochote kuhusu masuala ya ndani ya Kanisa. Pili, viongozi wa serikali hawapaswi kuwabagua raia kwa kuzingatia madhehebu yao, bali wanapaswa kuhakikisha uhuru wa kuabudu unazingatiwa. Serikali inawajibika kulinda usalama wa Kanisa (raia/waumini) hata wanapokuwepo kanisani. Kwa mfano kama kanisani kukitokea shida inayohatarisha usalama wa waumini, serikali inajukua jukumu lake mara moja kuhakikisha kwamba usalama unaimarishwa. Na ndiyo maana kwenye mikutano ya Injili ya nje viongozi wa Kanisa wanapaswa kutoa taarifa kituo cha polisi kilicho karibu ili kuhakikisha kwamba pana usalama. Hii haimaanishi kwamba Mungu anashindwa kulinda mkutano huo, bali ndivyo alikusudia kutenda kazi kwa kutumia serikali za kiraia. Kwa hiyo tunasema; polisi ni watumishi wa Mungu, ikiwa watatenda haki. Kwa sababu wanafanya mapenzi ya Mungu. Tunaweza kuhitimisha kwa usahihi kwamba serikali na Kanisa ni taasisi mbili huru za Kiungu ambazo zina malengo yake. Uhusiano wake ni kwamba washirika wa Kanisa ni raia wa serikali, na waumini wengine ndio watumishi wa serikali. Lakini maafisa au viongozi wa Kanisa hawana mamlaka juu ya serikali, na pia serikali haina mamlaka juu ya Kanisa (Mk.12:17, " Mpeni 90

Kaisari yaliyo ya Kaisari, na yaliyo ya Mungu mpeni Mungu.” Hata hivyo ni mwito wa Kibiblia kwa watu kutii serikali iliyopo madarakani; naweza kusema kwamba haijalishi serikali hiyo imeingia katika mamlaka kwa udanganyifu au kwa kweli. Kwa kweli, Wakristo wanapaswa kutii hata serikali za kidikiteta, kwani kunakuwepo na kusudi la Mungu katika hilo. Je serikali iliingilia masuala ya Kanisa wakati wa (COVID-19)? Mwishoni mwa mwaka 2019 kuliibuka ugonjwa wa Homa ya Mapafu au kwa kitaalamu “COVID-19. Tulisikia serikali mbalimbali duniani zikipiga marufuku kwa makanisa kufunguliwa katika kwa kipindi fulani ili kuzuia maambukizi ya ugonjwa huu. Watu mbalimbali walikuwa na maoni tofauti kuhusu jambo hili. Lakini kwa maoni ya ujumla tungependa kusema kwamba serikali kwa namna fulani haikuingilia masuala ya Kanisa; bali ilichokuwa inaangalia ni kulinda usalama wa raia wake. Serikali inao wajibu wa kuhakikisha kwamba watu wake wanakuwa salama kila wakati. Na ndiyo maana tuling’amua hapo nyuma kwamba serikali za kiraia ni za Kiungu. Zinafanya kazi ya Mungu kwa ajili ya kuwalinda watu wake. Hivyo basi, kwa kuwa hakuna aliyekuwa anajua ni lini ugonjwa ungeweza kupotea, au ni lini chanjo ya ugonjwa ingeweza kupatikana. 91

Nchi nyingi za Ulaya zilifunga makanisa, na kuruhusu watu wachache kuongoza ibada ambazo ziliweza kurushwa moja kwa moja katika mitandao ya kijamii au kwa njia nyinginezo. Hata hivyo baadhi ya nchi hazikuweza kukomesha moja kwa moja watu kukusanyika katika ibada; ila walishauri tu kwamba makanisa yachukue tahadhari kubwa, au kama wakiona vyema, basi wanaweza kufunga makanisa yao ka muda. Kwa mfano nchini Korea Kusini, kati ya mwezi Februari mpaka Julai 2020 makanisa mengi yalifunga ibada zake; huku baadhi ya makanisa yakawa yanaendelea na ibada zake kama kawaida bila kubughudhiwa. Afrika Mashariki, nchi za Kenya, Uganda na Rwanda vilipiga marufuku mikusanyiko ya ibada zozote zile, na kupendekeza njia mbadala za mitandaoni zitumike kufanya ibada; hata hivyo, nchi za Tanzania na Burundi ziliendelea kuruhusu ibada ziendelee kama kawaida. Ilisikiwa mara mbili nchini Tanzania raisi Dkt. John Pombe Magufuli aliitisha maombi ya kitaifa kwa ajili ya kuzuia janga la homa ya mapafu. Pamoja na hayo yote, sisi hatuwezi kulaumu serikali zilizokuwa zimechukua hatua kuzuia mikusanyiko ya ibada, kwa sababu hakuna aliyejua ni kwa vipi ugonjwa huu ungeendelea mpaka lini. Katika mazingira ya namna hii kunahitajika hekima ya namna ya pekee; serikali na Kanisa kushirikiana pamoja, kwa sababu kusudi la Kanisa ni kumtukuza Mungu na serikali 92

inahakikisha waumini wako salama. Kwa hiyo tunasema kwamba serikali hazikuingilia Kanisa kwa sababu zilipendekeza njia mbadala ya kufanya ibada kwa ajili ya kuwalinda raia wake.

SURA YA TANO WATUMISHI WA KANISA Watumishi wa Kanisa wanaotambulikana katika historia ya Kanisa tangu awali tunaweza kuwagawa katika makundi mawili; watumishi (maafsa) wasio wa kawaida na watumishi wa kawaida.

93

I. Watumishi Wasio wa Kawaida Maafisa wasio wa kawaida ni wale ambao Mungu aliwaita kwa kipindi maalumu. Walikuwa tu katika wakati maalumu na kwamba baada ya kizazi chao kazi zao zilikoma. 1. Mitume Hapa tunazingatia wale wanafunzi kumi na wawili isipokuwa Yuda, Paulo, wengine wa huduma za kitume kama vile Barnaba (Mdo 14:14). Kazi yao kubwa ilikuwa ni kuweka msingi wa makanisa yote. Waefeso 2:20 inasema, “Mmejengwa juu ya msingi wa mitume na manabii, naye Kristo Yesu mwenyewe ni jiwe kuu la pembeni.” Wanahistoria wengi wamedai kwamba huduma ya mitume ilikoma wakati wa karne ya kwanza; kwa maana ya kwamba wale waliokuwa pamoja na Yesu alipopotea katika uso wa dunia, basi hapana mtu mwingine anayeweza kujiita mtume akidai kuwa na hadhi sawa na mitume wa awali. Asili ya kazi ya mitume ni wazi kutoka kwenye agizo la Kristo: "Enendeni, mkahubiri Injili kwa kila kiumbe" (Marko 16:15). Kwa hiyo, Paulo, kwa kutaka kudhibitisha utume wake, anakumbuka kwamba hakupata mji wowote wa Kristo lakini alieneza Injili kwa bidii lakini kamwe hakuweka mikono yake kwa msingi wa mtu mwingine lakini alipanda makanisa pale ambapo jina la Bwana lilikuwa halijasikiwa (Rom. 15: 19-20). Mitume 94

walitumwa kuanzisha Ufalme Mungu kila mahali kwa kuhubiriwa Injili, kama wajenzi wa Kanisa la kwanza, kuiweka misingi katika ulimwengu wote (1 Kor. 3:10) hata kwa makanisa ya baada yao. Tuone sifa zinazowapa mamlaka makubwa ya kufikia kuweka msingi wa Kanisa. Kwanza, mitume walipokea wito wao moja kwa moja kutoka kwa Yesu Kristo (mitume kumi na wawili, Mk.3:14-19; Lk.6: 13-16, Paulo, Gal. 1:1). Pili, mitume walikuwa mashuhuda wa maisha ya kidunia ya Yesu na ufufuo wake. Alipaswa awe shuhuda wa macho, “Kuanza tangu ubatizo wa Yn., hata siku ile alipochukuliwa kwetu kwenda juu, inapasa mmoja wao awe shahidi wa kufufuka kwake pamoja nasi.” (Mdo 1:22) Tatu,

mitume

walikuwa

wanajua

ukweli

kwamba

mafundisho yao yaliongozwa na Roho Mtakatifu, kwa hiyo walikuwa na haki ya kuweka msingi wa makanisa yote. Nne, mitume waliunga mkono mamlaka yao wenyewe kwa kufanya miujiza. Mungu aliwatumia kwa namna ya ajabu. Kusema kwamba walifanya miujiza, haimaanishi kwamba miujiza haipo sasa hivi; lakini miujiza ya mitume ililenga kuthibitisha mamlaka yao.

95

Nne, Maandiko ambayo mitume waliandika; barua zao kwa makanisa kwa ajili ya miongozo mbalimbali ni moja ya sehemu ya Maandiko Matakatifu. Kwa hiyo walikuwa na mamlaka makubwa kwa wakati. Tunaposema kwamba cheo cha utume kilikoma tunajaribu kuzingatia sifa za mitume wa awali. Na kama nilivyosema hapo juu kwamba Maandiko ya mitume yaliingizwa katika Maandiko Matakatifu; tofauti na mitume wa leo ambao Maandiko yao hayawezi kuwa sehemu ya Maandiko Matakatifu, bali wao wanatumia mafundisho ya mitume. Hata hivyo, bado tunakubali kwamba huduma ya kitume ipo, lakini haiwezi kamwe kufanana na mitume wa awali. 2. Manabii Manabii waliongozwa na Roho Mtakatifu na kutumiwa na Mungu ili kuweka wazi siri za Injili na kutabiri matukio yajayo. Kuna Agabo alitabiri njaa kubwa, “Siku zizo hizo manabii walitelemka kutoka Yerusalemu hata Antiokia. Na tulipokusanyika akasimama mmoja wao, jina lake Agabo, akaonyesha kwa uweza wa Roho Mtakatifu kwamba njaa kubwa itakuja karibu katika dunia nzima, nayo ikatukia katika siku za Klaudio (Mdo 11:27,28). Pia Barnaba (Matendo13: 1, " Na huko Antiokia katika Kanisa lililokuwako palikuwa na manabii na waalimu, nao ni Barnaba, na 96

Simeoni aitwaye Nigeri, na Lukio Mkirene, na Manaeni aliyekuwa ndugu wa kunyonya wa mfalme Herode, na Sauli" Katika mistari hii, manabii hujitokeza kwanza kwenye orodha ya maafisa, na, basi, Barnaba anaonekana kwanza katika orodha ya majina halisi. Mpangilio huu unamaanisha sana kwamba Barnaba alikuwa nabii), na Yuda na Sila (Mdo 15:32, “Tena Yuda na Sila, kwa kuwa wao wenyewe ni manabii, wakawausia ndugu kwa maneno mengi, wakawathibitisha." Hivyo hapa walitambulishwa kama “manabii.” Zawadi ya unabii katika 1Kor 12: 10; 13: 2; 14: 3 inaweza kueleweka kama ilivyo kwa manabii hawa. Katika Maandiko nabii alitambulishwa mara tu baada ya mtume na, wakati huohuo, au sambamba na mtume (Efe.2: 20; 3: 5; 4:11). Katika hili tunahitimisha kwamba cheo cha kinabii pia kilikoma wakati wa manabii wa Kanisa la kwanza kwa sababu ilikuwa ni kwa kusudi maalumu tu. Hata hivyo tunakubali kwamba huduma ya kinabii bado ipo; Mungu bado anazungumza na watu wake kuhusu mambo yajayo, lakini watu ambao Mungu anawatumia kwa karama ya kinabii hawawezi kujiita kwa vyeo vya kinabii, na wala maneno yao hayawezi kuwa na mamlaka kama ya Kibiblia.

97

3. Wainjilisti Uinjilisti ni mojawapo ya zawadi. 'Naye alitoa wengine kuwa mitume, na wengine kuwa manabii; na wengine kuwa wainjilisti na wengine kuwa wachungaji na waalimu; '(Efes. 4:11). Filipo (Mdo 21:8) na Timotheo (2Tim.4:5) waliitwa kama wainjilisti. Tito na Marko wanaeleweka kama wainjilisti. Calvin alitafsiri wale watu sabini ambao Yesu alikuwa amewatuma kuhubiri Injili (Lk.10: 1) kama wainjilisti. Wainjilisti walihubiri Injili, walibatiza, wakachagua wazee (Tit.1: 5), na walitekeleza nidhamu (Tit.3: 10). Ofisi ya mwinjilisti ilimalizika wakati utume ulipomalizika, kwani lao kubwa lilikuwa kuwasaidia mitume. Wainjilisti hawa si kama wainjilisti ambao wanaitwa makanisani kwa jina la “mwinjilisti fulani.” Cheo cha Uinjilisti kilishakoma, kwa sababu watu wote wanapaswa kuwa wainjilishaji sehemu zozote zile wanazokuwa. Kwa hiyo kuitwa mwinjilisti haimaanishi kwamba umepokea cheo Kibiblia. Mara nyingi sana madhehebu ya Kiprotestanti yametumia cheo hiki kwa ajili ya kuwaitwa wale wanaosubiri daraja ya uchungaji. Kwa hiyo imekuwa ikitumika kama “kingojeo” tu. Kwa hiyo siku hizi hatuna cheo cha mtume. Siku hizi kuna changamoto kwamba ukisikia mtu anahubiri Injili ambayo mimi huita “Injili ya Mipasho” na kwa sauti kubwa, watu wanasema, “kweli huyu ni mwinjilisti.” Hapana. Si sahihi. Hata wale wanaohubiri mikutano ya watu maelfu, 98

hawana uhalali wa kuitwa kwa vyeo vya Uinjilisti, bali ni watenda kazi kama walivyo wengine, kwa nafasi ambazo Mungu amewaita. Tuhitimishe watumishi wasio wa kawaida kwa maneno ya John Calvin kwamba, “kazi hizi tatu hazikuanzishwa kanisani kama kazi za kudumu, lakini ni kwa wakati huo ambao makanisa yalipaswa kujengwa ambapo hayakuwepo hapo awali, au ambapo yalipaswa kutolewa kutoka kwa Musa hadi kwa Kristo. Bado, sikatai kuwa wakati mwingine Bwana amewainua mitume, au angalau wainjilisti mahali pao, kama ilivyotokea katika siku zetu wenyewe.” 49 Hapa Calvin anajirejelea mwenyewe kwa kuwa “Mtume” wa kipindi cha Matengenezo ya kanisa. Mara nyingi ameitwa, “Mtume Afundishaye.” Alijulikana sana kwa maandishi yake kwa kanisa. Kazi zake mpaka leo zipo kila mahali. Ni hazina kubwa kwa kanisa. II. Watumishi wa Kawaida Kuhusu maafsa wa kawaida, John Calvin anasema kwamba “Wale ambao husimamia serikali ya Kanisa kulingana na taasisi ya Kristo wamebainishwa kama ifuatavyo: kwanza mitume, pili, manabii, tatu wainjilisti, nne, wachungaji na tano, waalimu (Efe. 4:11). Anaendelea kusema, kati ya hawa, wawili tu wa mwisho; yaani Wachungaji na Waalimu wana ofisi ya kawaida kanisani; 49

Calvin, John, Institutes of the Christian Religion (Louisville: Westminster John Knox Press, 1960), uk.1089

99

Bwana aliinua hizi ofisi tatu; Mitume, Manabii na Wainjilisti mwanzoni mwa Ufalme wake, na sasa na tena anazihuisha kama hitaji kwa kulingana na hitaji.”50 Maafisa wa kawaida hawa tunasema kwamba wameitwa na Mungu kwa ajili ya Kanisa ambalo tayari msingi wake ulishawekwa na mitume. Calvin alitafsiri wachungaji na waalimu katika orodha ya huduma tano za Waefeso 4: 11 kama maofisa wa kawaida ambao walisimamia serikali ya Kanisa. Aliongeza pia mzee anayesimamia na shemasi (dikoni) kwenye orodha ya maafisa wa kawaida kwa msingi wa Warmi 12:7,8 na 1kor.12: 28. Alidai kwamba jukumu la mwalimu ni jukumu la mchungaji, na kwamba mzee, mchungaji, na mwangalizi (askofu) ni majina anuwai ya ofisi moja.51 1. Wazee wa Kanisa Mzee (presbyter) ni neno lilitumika kama mwangalizi au askofu. Pia liliendana na maneno kama vile “anayeongoza" (Rum.12:8; 1Thess.5:12), "kiongozi" (Heb.13:7,17,24 Efe.4: 11). Jukumu la msingi la mzee ni kutunza washirika wa Kanisa. Tunaona neno Mzee linaonekana kwanza katika Matendo 11:30, lakini, wakati Paulo na Barnaba wapolifika Yerusalemu, wazee 50

Calvin, John, Institutes of the Christian Religion (Louisville: Westminster John Knox Press, 1960),uk.1088 51 Calvin, John, uk.1088

100

walikuwa tayari wameteuliwa. Tunaona pia kwamba ofisi ya mzee iliteuliwa katika Kanisa la Yudea kwa mara ya kwanza (Yak.5:14), na, kisha, kuteuliwa katika makanisa ya watu wa Mataifa.52 Wakati Kanisa lilipokua na watu wengi walikuwa wakijiunga na Kanisa, basi, lilianza kutenganisha wazee wa kufundisha na wazee wanaotawala ili kukidhi mahitaji ya Kanisa (1Tim.5: 17). Wazee wa kufundisha wakawa watenda kazi kudumu. Hivyo basi, kuanzia hapa tunapata wazee wa aina mbili; wazee wafundishao ambao ni wachungaji, na wazee watawalao ambao ni wazee wa Kanisa wa kawaida na ni watumishi wa Kanisa kwa wakati wote. Wazee wa Kanisa husimikwa mara moja tu katika maisha yao, na kwamba utumishi wao hauna ukomo isipokuwa kama wameingia doa la utumishi; na hata kusitaafu kwao hakuwezi kuwaondolea hadhi yao, isipokuwa baadhi ya kazi za kikanisa na kimabaraza kwa kutegemeana na Kanisa husika. Mzee aliweza kuteuliwa na mchungaji, lakini mchungaji aliteuliwa na presibiteri (baraza la presibiteri). Mzee yuko chini ya usimamizi wa baraza la wazee, lakini mchungaji yuko chini ya 52

Mataifa mahali hapa inamaanisha makanisa ambayo hayakuwa Yudea (yaani makanisa yaliyokuwa na waumini ambao si Wayahudi kwa asili). Kwa hiyo lisieleweke kwamba watu wa mataifa hapa ni wenye dhambi.

101

usimamizi wa baraza la presibiteri. Mzee hawezi kuweka mikono juu ya mchungaji, na pia hawezi kutekeleza Sakramenti. Mchakato wa kumpata mzee wa Kanisa ni mfupi, ukilinganisha na mchungaji. Hata hivyo Mchungaji kamwe hawezi kutekeleza ofisi ya mzee atawalaye. Kwa hiyo kila mmoja anasimama kwenye nafasi yake kwa ajili ya ufanisi wa kanisa. Mzee pamoja na Mchungaji wanashirikiana kutawala na kuongoza Kanisa. Wakati mchungaji hayupo, mzee peke yake anaongoza mchakato wa kukaribisha mchungaji kwa msaada wa washirika kamili (yaani waliobatizwa). Kunapokuwa hakuna mhubiri, Mzee wa Kanisa anayo mamlaka ya kuita mhudumu wa neno (Mhubiri). Kama isipowezekana, basi mzee mwenyewe anaweza kuongoza ibada, pamoja na kuhubiri. Makanisa mengi ya ki-refomati huchagua mzee mmoja wa Kanisa pindi waumini wanapofikia angalau ishirini hivi. Lakini inashauriwa kuchagua wazee kwa kulingana na uhitaji wa Kanisa; lakini sifa za wazee wa Kanisa, ziko karibu sawa na sifa za wachungaji kwa sababu wote hawa ni watumishi wa Mungu. Neno “mzee

afundishaye au

mzee atawalaye” na

“mwangalizi” au “askofu” kama tulivyosema hapo awali yalitumika yakiwa na maana sawa kabisa na wala hapakuwa na kitu chochote cha zaidi katika masuala ya kiutawala. Grudem 102

anasema kwamba “Ninaamini kuwa maneno mzee, mwangalizi, mchungaji, na Askofu ni majina yaliyotumika kwa kubadilishana yakiwa na maana moja.”53 Kwa kadri muda ulivyokuwa unaenda, viongozi kadha wa kadha walianza kubadilisha matumizi ya maneno haya na kuanza kuyatofautisha. Ilianza kutofautishwa kwamba mwangalizi (askofu) ni mkubwa kuliko wengine. Ikaonekana kwamba Askofu ana nafasi ya juu kuliko mzee au shemasi. Wakatoliki walikaza kwamba askofu alikuwa anasimama badala ya Yesu duniani katika nafasi aliyo nayo.

Baada ya

kuinuliwa na kukuzwa kwa askofu, basi moja kwa moja miongoni mwa maaskofu aliinuka mwingine aliyedai kwamba yeye ndiye mwakilishi wa Mtume Petro, Msimamizi wa wote, Mkuu wa Kanisa ambaye anaitwa Papa. Binafsi sibezi makanisa yanayotumia viongozi kama vile maaskofu; lakini sikubaliani kamwe na dhana kwamba watumishi hawa wako tofauti kimadaraja na wachungaji wengine wa kawaida. Tofauti iliyopo ni majukumu aliyo nayo mtu; kwamba yupo mtu mwingine ambaye anapewa majukumu makubwa, na yupo mtu mwingine ambaye majukumu yake yako kidogo. Ni kawaida kwamba mtu mwenye majukumu makubwa, pale 53

Grudem, Wayne. Systematic Theology (Grand Rapids: MI: Inter-Varsity Press) 1994, Uk. 1123

103

anapokuwa ameyatenda kwa usahihi huheshimiwa, lakini ni kawaida kwa mtu ambaye amepewa majukumu makubwa, lakini hawezi kuyatenda, hudharauliwa. Kwa hiyo, si kwamba askofu ni bora kuliko mchungaji mwingine, bali hayo ni majina tu ambayo yanatumika kwa kubadilishana, ingawa mwanadamu siku zote hutafuta heshima kupitia vyeo kama hivi.

Sifa za mzee wa Kanisa Kabla mzee wa kanisa hajaingizwa katika utumishi, ukiachilia kufundishwa na kufunzwa, anapaswa angalau kuwa na sifa zifuatazo ambazo ni za Kibiblia. Nitazitaja kwa uchache hapa chini: a) Asiye na kashfa. (asiwe mtu mwenye kulaumika) (I Tim. 3: 2; Tito 1: 6) Juu ya lawama haswa inamaanisha, 'asiyeweza kushikwa.' Sifa hii inahusiana na kuwa na sifa nzuri. Pengine sifa hii inaweza kubeba sifa zote zinazofuatia. Mzee wa Kanisa anapokuwa na kashfa ndani ya Kanisa na nje ya Kanisa husababisha Kanisa kupoteza ushuhuda wake. Ndiyo maana hii ni sifa ya kwanza kwa ajili ya mzee. b) Asiye na mitala. (I Tim. 3: 2; Tito 1: 6) Maneno ya Kiyunani, ambayo tunatafsiri kama "mume wa mke mmoja,” yanatokeza zaidi kuhusu uaminifu katika ndoa, sio hali ya ndoa. Kwa muktadha huu hata mtu ambaye alishatalikiana kwa halali, basi 104

anaweza

kuingizwa

kwenye

uzee,

ikiwa

tu

atakuwa

ametekeleza vigezo halali. c) Awe mwenye kiasi. (I Tim. 3: 2) yaani mwenye kujidhibiti. (Tito 1: 8) "Kiasi" inahusu mwelekeo wa mtu kuelekea maisha. Inazungumza juu ya mtu anayeishi maisha yenye usawa, asiye na msimamo mkali. Mzee lazima awe na maisha yaliyojaa ibada, ambayo inamruhusu Yesu kuwa Bwana katika maisha yake. d) Mwenye busara. (I Tim. 3: 2) Akili. (Tito 1: 8) Ni lazima mzee atumie busara. Utimamu huu wa maamuzi hukua kutokana na maoni ya unyenyekevu kwake mwenyewe na utambuzi wa utoshelevu wote wa Kristo. Mzee wa Kanisa anapojaa hekima, huamua mambo kwa kutumia busara na uongozi wa Roho Mtakatifu aliye ndani yake. e) Mtu wa utaratibu. (I Tim. 3: 2) Lazima mzee awe na tabia nzuri, aliye na mpangilio mzuri, mtu ambaye maisha yake ni sawa. f) Mkarimu. (I Tim. 3: 2; Tito 1: 8) Mzee lazima moyo wake uwe wazi kwa ajili ya watu wengine. mtazamo kuelekea watu. introvert au extrovert, mzee lazima awe na mwelekeo wa watu. g) Uwezo wa Kufundisha. (I Tim. 3: 2) Uwezo wa kufundisha kwa mzee ni muhimu. Yawezekana hapa ikimaanisha mzee afundishaye. Lakini moja kwa moja mzee wa Kanisa lazima 105

ajue kufundisha. Mzee wa Kanisa asipokuwepo mchungaji lazima ahubiri neno la Mungu kwa ujasiri. Mzee wa Kanisa ili ajue kufundisha lazima awe na tabia ya kujifunza neno la Mungu. h) Sio mraibu wa pombe. (I Tim. 3: 3; Tito 1: 7) Mzee wa Kanisa ambaye amekubuhu kwenye ulevi hapaswi kuchaguliwa na kuwekewa mikono. Lazima pia tukumbuke yale Maandiko yanafundisha katika Warumi 14:21 na 1 Wakorintho 10:31. Kuna sababu nyingi kwa nini mzee atakuwa vizuri kujiepusha kabisa na pombe. i) Si Mpiga watu. (I Tim. 3: 3; Tito 1: 7) Mzee lazima asiwe mwepesi wa hasira. Mtu mwenye hasira hawezi kuwa mzee wa Kanisa. Ningependa kukamilisha kipengele hiki kwa kusema kwamba, kusimika wazee ni suala la Kibiblia ambalo linaonesha kutengwa kwao kwa wazi kwa ajili ya kazi ya uzee wa Kanisa. Pamoja na utayari wa kutenda kazi ya uzee, ni lazima kabla ya kuwekwa wakfu wachunguzwe kwa makini kwa kuzingatia sifa za Kibiblia. Sifa hizo juu hazimaanishi kwamba mzee wa Kanisa ni “mkamilifu” bali ni mwajibikaji kwa ajili ya kazi ambayo anaitenda.

106

Idadi ya Wazee kwa Kila Kanisa la Mahali Wazee wa kanisa ndio wawakilishi haswa wa Wakristo ndani ya kanisa katika mabaraza ya kanisa. Hata katika mifumo ya Kiaskofu, kuna idadi maalumu ya watu wanaopaswa kuingia kwenye mabaraza hayo. Kwa kawaida watu hao ndio haswa wazee wa Kanisa. Ama kuhusu idadi ya wazee wa kanisa kwa kila kanisa la mahali inategemea idadi ya washirika katika kanisa hilo. Mara nyingi imechukuliwa kwamba ikiwa kanisa lina waumini kuanzia 20-25 linapaswa kuwa na mzee wa kanisa mmoja (1) na ikiwa litafika watu kuanzia 40-50 linakuwa na wazee wa kanisa wawili (2) na kuendelea kwa uwiano huo. Uwepo wa wazee hawa haimaanishi kwamba wao ndio wanaotenda kazi peke yao, lakini kwa sababu ya unyeti wa nafasi ya mzee ndani ya kanisa na utumishi wake, idadi yake imewekewa ukomo kwa kuzingatia washirika. Kwa kweli hakuna andiko linaloonesha kwamba kila kanisa liwe na wazee wangapi, lakini tukiangalia tu hata katika historia wazee hawakuwa wengi ndani ya kanisa. Mara kwa mara wachungaji hujaribiwa kuchagua wazee wengi, na kutumia nafasi ya uzee kama “kitia moyo” kwa watu. Kwa kweli tunaonywa na maandiko kwamba tusiwe na haraka ya kuwawekea mikono ya uzee watu. Usitumie uzee kama rushwa 107

kwa wale wanaopenda madaraka. Wazee wa kanisa hawapaswi kuchaguliwa wengi kwa mkupuo kwani ni hatari kwa usalama wa kanisa. Ikiwa watumishi wanahitaji kuwa na watumishi wengi ndani ya kanisa, basi wanaweza kuteua mashemasi na watenda kazi wengine, badala ya kusimika wazee waliozidi idadi. 2. Mchungaji au mwalimu Tukiangalia maneno “Mchungaji na Mwalimu” katika Waefeso4:11 sio ofisi mbili tofauti, bali ni kazi mbili za ofisi moja. Tofauti ndogo kati ya hizi mbili ni kwamba mwalimu hashiriki kazi za kiinjili za Kanisa kama nidhamu au utekelezaji wa Sakramenti lakini hujishughulisha katika utafsiri wa Maandiko, wakati mchungaji anashiriki katika kazi za kiutawala za Kanisa.54 Mapema katika historia ya Kanisa mitume, manabii na wainjilisti walichukua jukumu la wachungaji na waalimu. Baada ya mitume kufa, idadi ya wazushi iliongezeka. Ongezeko hili la wazushi lilihitaji Kanisa kusisitiza umuhimu wa ofisi ya kufundisha. Kwa hiyo wazee wafundishao walianza kutengwa na wazee wanaotawala (1Tim.5: 17). Wazee hawa wa kufundisha wakawa watenda kazi wa kudumu ambao Kanisa liliwahudumia huku wakifanya kazi kwa muda wote. Hakukuwa na kiongozi wa wachungaji, bali wachungaji wote walikuwa sawa. 54

Calvin, Institutes, IV.3.4).

108

Vilevile

tunapaswa

kukumbuka

kwamba

Maandiko

hayakuwaita wachungaji au wazee kama makuhani. Ofisi ya kuhani ilifutwa mara tu baada ya kazi ya wokovu ya Kristo kukamilika. Inashangaza kuona Kanisa Katoliki wanaendelea kuwepo makuhani; kazi ya kuhani ilikuwa ni kutoa sadaka, hivyo kama kukiwepo na kuhani maana yake Kristo hakufa kwa ajili ya dhambi za watu, na hivyo kuhani anahitajika kwa ajili ya kufanya upatanisho. Mchungaji hufundisha neno la Mungu kwa msingi wa Maandiko, hubariki washirika wa Kanisa, na huteua wazee. Mchungaji anatawala washirika wa Kanisa kwa msaada wa wazee wanaotawala, na anafanya kazi za uwasilishaji, za kipresibiteri au kazi za Mkutano Mkuu. Mchungaji hupaswa kuwajali waumini wote bila upendeleo wowote; kwa kushirikiana na wazee na mashemasi, anaweza kuwa na utaratibu mzuri wa kuwatembelea na kuwatia moyo wanaopitia vipindi vigumu katika maisha yao. 3. Shemasi (Dikoni au Mhudumu) Tunakutana na neno shemasi au mhudumu katika 1Tim.3: 8,10,12. Tunaweza kupata ushahidi wa uwasilishaji wa ofisi ya shemasi kwanza katika uteuzi wao wakati wa Kanisa la kwanza katika Matendo 6: 1-6. Haionekani wazi kwamba ilikuwa ni ofisi maalumu, labda pengine ilikuwa ni kwa ajili ya kutatua 109

changamoto katika kanisa la Yerusalem, lakini hata hivyo baadaye tunaona mwendelezo wa huduma yao. (Mdo 11: 29; 2Kor.8: 4; 9: 1,12,13). Kazi ya mashemasi ni kuwasaidia na kuwajali watu masikini na wagonjwa (Institute IV.3.9.). Ukweli kwamba "dhamiri iliyo wazi" ilisisitizwa (1Tim.3: 9) inamaanisha kwamba ofisi ya shemasi ina uhusiano na usimamizi wa fedha. Hivyo shemasi anahusika moja kwa moja na masuala ya huduma za kimwili kanisani. Kazi ya shemasi si ya kutawala, bali ni kuhudumu peke yake. Hata hivyo, uteuzi wao unapaswa kuwa na umakini mkubwa kwa sababu ya ofisi yao. Mtume Paulo anasema hivi: “Vivyo hivyo mashemasi na wawe wastahivu; si wenye kauli mbili, si watu wa kutumia mvinyo sana, si watu wanaotamani fedha ya aibu; wakiishika siri ya imani katika dhamiri safi. Hawa pia na wajaribiwe kwanza; baadaye waitende kazi ya shemasi, wakiisha kuonekana kuwa hawana hatia. Vivyo hivyo wake zao na wawe wastahivu; si wasingiziaji; watu wa kiasi, waaminifu katika mambo yote. Mashemasi na wawe waume wa mke mmoja, wakiwasimamia watoto wao vizuri, na nyumba zao. Kwa maana watendao vema kazi ya shemasi hujipatia daraja nzuri, na ujasiri mwingi katika imani iliyo katika Kristo Yesu.” (1Tim 3:8-13) 110

Ingawa kazi ya Mashemasi si kutawala, hata hivyo, kuna wakati wanaweza kushirikiana na mchungaji katika uongozi wa Kanisa; hasa ikiwa Kanisa bado halijachagua wazee wa Kanisa. Mashemasi wengine wanakuwa na vipawa vya kuhubiri neno la Mungu, na wanaweza kupewa nafasi ya kuhubiri ikiwa wamethibitishwa na kupewa mafunzo ya kuhubiri, hata hivyo wajibu wa kufundisha ni wa mchungaji mwenyewe, na kama mchungaji atamkabidhi kuhubiri shemasi, basi atawajibika kwa mafundisho yote. III. Usimikaji Usimikaji wakati mwingine huitwa “kuwekwa wakfu” au kuwekewa mikono ya kutengwa. Tunatambua kwamba wito wa maafsa wa kawaida (Wazee, wachungaji na mashemasi) ni kwamba wameitwa kufanya kazi ya Mungu kwa kuwahudumia watu kimwili na kiroho. Kwa hiyo maandalizi yao kwa mara ya kwanza lazima yaanzie rohoni na si mwilini. Hivyo basi, mtu yeyote anayetamani kazi ya utumishi wa kawaida ndani ya Kanisa anapaswa kujichunguza kwa makini kwa sababu anaenda kufanya kazi ya Mungu moja kwa moja. Ajichunguze kabla ya kusimikwa rasmi kwa kazi ya Mungu. Hili linawahusu wachungaji, wazee na mashemasi. Wacha nizungumzie kusimikwa au kuwekewa mikono. 111

Katika Agano Jipya, wazee walitengwa kipekee kwa ajili ya ofisi yao ya uzee. Neno la Kiyunani kathistēmi, linalomaanisha "kuamuru," kwa kawaida lilitumika kuelezea uteuzi wa wazee, likiwa na maana kwamba wazee wanapoingia katika ofisi ya uzee wanakuwa wametengwa kwa ajili ya kazi ya Mungu (kuwekwa wakfu). Mchakato wa kuwekwa wakfu unaashiria wito wa Kimungu na kutangaza kwa wazi katika Kanisa wito wa kutumika katika nafasi ya uzee. Paulo anatoa maelezo muhimu juu ya mchakato wa kuwekwa wakfu wakati anamwambia Timotheo, " Usiache kuitumia karama ile iliyomo ndani yako, uliyopewa kwa unabii na kwa kuwekewa mikono ya wazee." (1 Tim. 4:14). Maana yake wazee wa Kanisa walimsimika Timotheo katika kazi ya uzee, siyo kwamba yeye mwenyewe alijisimika. Kwa hiyo tunasema “kusimikwa” inakuwa ni ishara ya nje ya kutengwa kwa watumishi wa Mungu. Kusimika kwa kuweka mikono juu kunapata mizizi yake katika Agano la Kale kwa Waisraeli. Waisraeli walipoleta dhabihu ili kutolewa kwa Bwana waliweka mikono yao juu ya dhabihu ili kujitambulisha nayo (Law. 1: 4; 3: 2-13; 4: 4-33; 8:14, 18, 22; 16:21).

112

Vile vile katika Agano la Kale, kuwekewa mikono kulitumika kuashiria uhamishaji wa mamlaka (Hes. 27: 18-23; Kum. 34: 9) au kutoa baraka iliyotolewa kutoka kwa upande mmoja hadi mwingine (Mwa. 48: 13-20; 2 Wafalme 13:16; Ayubu 9:33; Zab. 139:5). Mamlaka na baraka pia zinaonyeshwa katika kuwekwa wakfu katika Agano Jipya, kwani uongozi wa Kanisa unamthibitisha mzee aliyewekwa wakfu katika kutenda majukumu yake rasmi. Usimikaji

katika

Agano

Jipya

vilevile

unaonyesha

mshikamano kati ya wazee hao wanaoenda kutenda kazi pamoja na mzee mchungaji. Kwa sababu hiyo, mzee wa Kanisa anapaswa kutenda kazi ya uzee katika Kanisa lake la mahali tu, na kwamba hapaswi kutumika kwa mikono hiyohiyo katika Kanisa lingine, bali anapaswa kuwekewa mikono tena kwa ajili ya kujenga mshikamano na wazee wengine. Kusimika

mzee

hakupaswi

kufanyika

kwa

haraka,

isipokuwa kuwepo na uhakika wa wito wa mzee huyo katika kutenda kazi ya uzee. Paulo alivyomwonya Timotheo, " Usimwekee mtu mikono kwa haraka, wala usizishiriki dhambi za watu wengine. Ujilinde nafsi yako uwe" (1 Tim. 5:22). Kwa kuzingatia fungu hili, watu wanaotakiwa kuwekwa wakfu ni lazima wajaribiwe vya kutosha, kuonyesha kwamba wanastahili kutumikia katika huduma ya kizee. Usijaribu kumweka mtu kuwa 113

mzee wa Kanisa kama sifa kwa sababu unaogopa atahama Kanisa. Usijaribu kumsimika mtu kuwa mzee kwa sababu unaogopa atakukasirikia, bali sifa za Kibiblia zinapaswa kuzingatiwa. Wachungaji husimikwa kwa kuwekewa mikono na Presibiteri; lakini pia wazee wa Kanisa huweza kusimikwa na mchungaji wa Kanisa husika. Makusudi ya sherehe hizi ni kuonesha kwamba wamejitenga wenyewe kwa ajili ya kazi ya Bwana. Hata hivyo, sherehe za usimikaji siyo za lazima sana ikiwa mtu ameitwa na Mungu. Kwa mfano, Yesu hakuweka mikono yake juu ya wanafunzi wake, wakati alipowachagua kuwa mitume. Mathiya, Paulo, Sila, na Luka walichukua ofisi zao bila kuwekewa mikono. Kuwekewa mikono ni taratibu ambazo zimewekwa kwa ajili ya kurasimisha ofisi hizi, na pia kuzuia utitiri wa watu kujiingiza katika ofisi kwa siri na kuharibu Kanisa la Mungu. Pia zawadi za Roho Mtakatifu zilitolewa kwa (Mdo 8:17). Paulo na Barnaba waliwekewa mikono baada ya kuteuliwa katika ofisi zao (Mdo 13: 3). Kwa hiyo kuwekewa mikono ni alama tu, lakini tayari watumishi wanakuwa wameshapokea mwito kutoka kwa Mungu kwa ajili ya ofisi ya utumishi wao. Sherehe hizi za kuwasimika ni kuungazia umma kwamba wameteuliwa kazi maalumu ya utumishi katika daraja lao.

114

Ama kuhusu usimikaji wa Mashemasi, Makanisa mengine hayaweki mikono juu ya mashemasi kwa kudai kwamba wanataka kutofautisha na wazee. Lakini kuwa wawazi katika hili ni kwamba kukataa kuweka mikono juu ya mashemasi kunatokana na mawazo ya Kikatoliki ya kujaribu kuweka madaraja katika watumishi wa Kanisa ambayo mwishowe humwinua mtu mmoja kuwa mkubwa kuliko wenzake. Kwa kutambua utumishi wa mashemasi, napendekeza wawekewe mikono katika kazi hiyo ya ushemasi, na kama wataenda katika daraja nyingine ya uzee wa Kanisa pia wawekewe mikono, na hata kama wakienda kusoma zaidi na kuwa waalimu wa neno (wachungaji) pia wawekewe mikono ya uchungaji kwa sababu nia ya kuweka mikono siyo kupandikiza utumishi (maana utumishi wanao tayari) bali ni kutangaza kwa umma na kuwakabidhi rasmi katika kazi maalumu. Kuwanyima mikono mashemasi ni kuzuia tangazo kwa umma juu ya wito wao wa kutumika.

115

SURA YA SITA NJIA ZA NEEMA Mwanadamu aliyeanguka dhambini, amebarikiwa kwa baraka ya wokovu kupitia msingi wa neema, kupitia kazi ya Yesu Kristo na huduma ya Roho Mtakatifu. Walakini, Roho Mtakatifu hutumia njia fulani kufikisha baraka za wokovu. 116

Mkristo anahitaji kukua katika neema na katika ufahamu wa Mungu wake na Mwokozi Yesu Kristo. Kama vile mwili wake unavyohitaji chakula chenye lishe kukua, vivyo hivyo naye anahitaji chakula cha kiroho ili kukua kiroho. "Chakula" hiki cha kiroho ambacho Mungu ametoa kwa ukuaji wa Wakristo katika theolojia tunaita "njia ya neema."55 Hizi “ni njia ambazo Mungu hulipa nguvu za kiroho Kanisa lake.”56 Katika Ukiri wa Westminista tunasoma kwamba “Kwa kanisa hili linaloonekana, Kristo ametoa huduma, mafundisho, na maagizo ya Mungu, kwa kukusanyika na kuwakamilisha watakatifu, katika maisha haya, hadi mwisho wa ulimwengu: na hufanya hivyo kwa uwepo wake mwenyewe na Roho, kulingana na ahadi. (I Kor. 12:28; Efe. 4: 11, 12, 13; Mt. 28:19, 20; Isa. 59:21).” 57 Kwa hiyo, njia za neema maana yake ni mambo ya muhimu ambayo kwayo Kristo anarutubisha Kanisa lake ili liendelee kuishi na kutimiza kusudi lake. Kumekuwepo na maoni kadhaa kuhusu aina za njia za neema ambazo Kristo amelipatia Kanisa. Raymond anabainisha

55

Kwa Kiingereza ni “means of grace.” Frame, M. John, Salvation Belongs to Christ: An Introduction to Systematic Theology (New Jersey: P&R Publishing Company, 2006), uk. 172 57 Westminster Confession of Faith, sura 25 sehemu ya 3) 56

117

aina tatu za njia za neema: Neno, Sakramenti na Maombi”58 Beeke na Smalley wanabainisha aina mbili tu, “Neno na Maombi.”59 John Frame anaainisha aina tatu, ambazo ni “Neno, Ushirika (Diakonia) na Maombi.” Berkhof anasema anataja njia za neema mbili tu ambazo ni “Neno na Sakramenti,”60 ambapo kupitia hizo Mungu huwasiliana na watu wake kwa kuwapatia neema ya kuendelea kuishi katika maisha ya hapa duniani kwa kumtukuza yeye. Berkhof anaungwa mkono na Herman Bavinck anayetambua njia za neema kuwa mbili tu: Neno ndilo la msingi, na Sakramenti inafuatia baada ya Neno.61 Kwa mujibu wa majadiliano hapo juu tunapata “njia za neema” zifuatazo: Neno, Sakramenti, Maombi na Ushirika (Diakonia). Wana Refomati huchukua ule mlengo wa aina mbili; Neno na Sakramenti, huku wakiacha maombi na Diakonia. Pengine wanaacha Maombi na Ushirika kwa sababu ni matokeo ya Neno na Sakramenti. Kwamba pale neno linapohubiriwa, basi matokeo yake moja kwa moja ni watu kumwomba Mungu na kutaka ushirika pamoja naye, na ushirika kati ya ndugu na ndugu.

58

Reymond, L. Robert, A New Systematic Theology of The Christian Faith (Nashville: Thomas Nelson Publishers,1998) uk. 918 59 Beeke, R. Joel na Smalley, M. Paul, Reformed Systematic Theology (Illinois: Crossway, 2019), uk. 1182 60 Berkhof, Louis, Systematic Theology (Grand Rapids: Eerdmans, 1974), uk 670 61 Bavinck, Herman. Reformed Dogmatics (ukurasa wa. 643). Baker Publishing Group. Kindle Edition.

118

Wazo hili linaungwa mkono na Grudem anaposema, “kuna njia kadhaa ambazo Roho Mtakatifu hutumia kufikisha baraka katika maisha ya mwamini. Ama kwa hakika, maombi binafsi, ibada, kusoma Biblia, na imani ya kibinafsi, zote ni njia ambazo Mungu hufanya kazi ya kuleta neema kwetu kama Wakristo, lakini katika mafundisho ya Ekklesiolojia tunahitaji kujua ni njia zipi rasmi ambazo

Mungu

anazitumia

moja

kwa

moja

kupitia

Kanisa….orodha ifuatayo inaweza kuwa si kamili, lakini inajumuisha njia nyingi za neema ambazo waumini wanazo katika ushirikiano na Kanisa; Mafundisho ya Neno, Ubatizo, Meza ya Bwana, Kuombeana, Kuabudu, Nidhamu ya Kanisa, Kutoa, Zawadi za kiroho, Ushirika,Uinjilishaji na Huduma ya kibinafsi kwa watu.”62 Tutajadili aina hizi mbili; Neno na Sakramenti ambazo wana Refomati wengi wamekubaliana kwamba hizo ndizo za msingi; kwa maana ya kwamba kama zisipokuwepo hizo, basi Kanisa linakuwa halipati zile neema zinatotakiwa kwa ajili ya kuendesha maisha ya Kristo. Lakini pia hizi mbili, ni msingi wa zile ambazo Grudem ameorodhesha pale juu.

62

Grudem, Wayne. Systematic Theology (Grand Rapids: MI: Inter-Varsity Press) 1994, Uk. 1218-19

119

I. Neno Kile tunachokiita neno la Mungu katika muktadha huu ni Biblia Takatifu. Katika Biblia, Mungu ameweka kila kitu tunachopaswa kujua kuhusu mapenzi yake na kusudi la maisha yetu. Neno la Mungu liko katika Agano la Kale na Agano jipya. Maagano yote yanafaa kutumika kwa ajili ya kufundisha Kanisa la Mungu. Imani ya Westiminster Sura ya 1 sehemu ya 6 inasema hivi: Mungu ameweka katika Biblia kila kitu tunachohitaji kujua juu ya utukufu wake na pia wokovu wetu, imani, na maisha. Yeye ameandika vitu hivi katika Biblia moja kwa moja, na alituruhusu kuvichunguza kwa kutumia hoja zetu. Hakuna kitu kinachohitajika kuongezwa kwenye Biblia, iwe ni "ufunuo mpya kutoka kwa Roho" au iwe ni mila na tamaduni za mwanadamu. Walakini, tunatambua kuwa mwangaza wa ndani wa Roho wa Mungu ni muhimu kwa ufahamu wa kuokoa wa vitu vilivyofunuliwa katika Neno.Tunatambua pia kuwa vitu muhimu vya ibada ya Mungu na serikali ya Kanisa ni sawa na shughuli za ulimwengu na mashirika; haya yanapaswa kuelekezwa kulingana na uelewaji wetu wa asili na busara yetu ya Kikristo na inapaswa kufuata sheria za jumla za Neno, ambazo zinapaswa kuzingatiwa kila wakati. 120

Nukuu hii inasisitiza mambo kadhaa kuhusu neno la Mungu; kwanza kila kitu kinachohusu maisha yetu au kile tunachopaswa kuamini kipo kwenye Biblia, na hivyo hakuna haja ya kutafuta ufunuo mpya kutoka ndani au nje ya Kanisa. Pili, hatuwezi kuelewa Biblia pasipo kuwepo kwa mwangaza wa Roho Mtakatifu. Tunapokuwa tumepewa ule mwangaza wa Roho Mtatifu ndipo neno la Mungu linakuwa lenye manufaa katika maisha yetu. Kanisa linahitaji neno la Mungu kama njia ambayo Mungu anaitumia kwa ajili ya kurutubisha Kanisa (waumini ambao ni mwili wa Kristo) likue kutoka hatua moja kwenda nyingine. Maisha ya Kikristo ni siri kubwa katika Kristo Yesu. Watu wengi hawawezi kuelewa; kwa sababu kupitia neno la Mungu, watu wanakua katika kiwango chao cha kiroho polepole. Kwa kadri wanavyoendelea kujifunza na kusikiliza neno la Mungu wanapata maarifa ya Kimungu. Biblia ina habari ya kutosha kwa mtu sio tu kupata wokovu katika Kristo lakini baadaye kupata mafundisho na mwongozo katika kila nyanja ya mawazo na maisha, ama kwa taarifa za wazi za Maandiko au kwa uvumbuzi muhimu kutoka kwake.”63

63

Cheung, Vincent, Systematic Theology (Zondervan Publishing House, 2010) Uk. 29

121

Neno la Mungu ndiyo baraka kubwa ambayo Mungu amelipatia Kanisa. Kanisa linaongozwa na neno la Mungu. Hata kabla watu hawajakuwa Wakristo, Neno la Mungu kama linavyohubiriwa na kufundishwa huleta neema ya Mungu kwao kwa kuwa ni kifaa ambacho Mungu hutumia kuwapa maisha ya kiroho na kuwavuta katika wokovu. Paulo anasema kwamba injili ni "nguvu ya Mungu iletayo wokovu" (Warumi 1:16) na kwamba kuhubiri Kristo ni "nguvu ya Mungu na hekima ya Mungu" (1 Kor 1:24). Mungu alitufanya kuzaliwa tena au "alituzaa kwa neno la ukweli" Yakobo 1: 18 inasema “Kwa kupenda kwake mwenyewe alituzaa sisi kwa neno la kweli, tuwe kama limbuko la viumbe vyake.” Pia, Peter anasema, " Kwa kuwa mmezaliwa mara ya pili; si kwa mbegu iharibikayo, bali kwa ile isiyoharibika; kwa neno la Mungu lenye uzima, lidumulo hata milele” (1 Petro 1:23). Ni Neno la Mungu lililoandikwa, Biblia, ndilo "…tangu utoto

umeyajua

Maandiko

matakatifu,

ambayo

yaweza

kukuhekimisha hata upate wokovu kwa imani iliyo katika Kristo Yesu." (2 Tim 3: 15). Hata hivyo, hata baada ya kuwa Wakristo, neno la Mungu ndilo hutujenga. Paulo anasema kwamba “Basi, sasa nawaweka katika mikono ya Mungu, na kwa neno la neema yake, ambalo laweza

kuwajenga

na

kuwapa

urithi

pamoja

nao

wote

waliotakaswa" (Mdo 20:32). Katika maisha ya Kikristo, inahitajika 122

lishe ya kiroho kwa ajili ya kuendesha maisha ya kiroho, kwa sababu hatuishi kwa mkate peke yake lakini kwa "kila neno linalotoka kinywani mwa Mungu" (Math 4: 4). Ni Neno la Mungu ambalo linatuhukumu kuhusu dhambi na kutubadilisha kuwa watu wa haki, kwa hiyo lina faida, na hivyo " lafaa kwa mafundisho, na kwa kuwaonya watu makosa yao, na kwa kuwaongoza, na kwa kuwaadibisha katika haki; 1 Tim 6:11, ili mtu wa Mungu awe kamili, amekamilishwa apate kutenda kila tendo jema"(2 Tim. 3:16-17). Neno linatoa mwelekeo na mwongozo katika maisha, “Kitabu hiki cha torati kisiondoke kinywani mwako, bali yatafakari maneno yake mchana na usiku, upate kuangalia kutenda sawasawa na maneno yote yaliyoandikwa humo; maana ndipo utakapoifanikisha njia yako, kisha ndipo utakapositawi sana.” (Yosh. 1:8). Neno la Mungu ni mwongozo katikati ya mwitu usio wa Kimungu, “Nasi tuna lile neno la unabii lililo imara zaidi, ambalo, mkiliangalia, kama taa ing’aayo mahali penye giza, mwafanya vyema, mpaka kutakapopambazuka, na nyota ya asubuhi kuzuka mioyoni mwenu" (2 Pet. 1: 19). Pia neno ni uhai wetu. Mwandishi wa

Zaburi

anasema,

“Sheria

ya

BWANA

ni

kamilifu,

Huiburudisha nafsi. Ushuhuda wa BWANA ni amini, Humtia mjinga hekima "(Zab. 19:7) Neno hutoa tumaini kwa wale ambao wamekata tamaa, kwa sababu Paulo anadadavua kuhusu neno 123

lililoandikwa kwamba, “Kwa kuwa yote yaliyotangulia kuandikwa yaliandikwa ili kutufundisha sisi; ili kwa saburi na faraja ya Maandiko tupate kuwa na tumaini"(Warumi 15: 4). Neno la Mungu kila linapohubiriwa linakuwa na makusudi maalumu kwa kila mtu. Isaya 55:10-11 inasema, “Maana kama vile mvua ishukavyo, na theluji, kutoka mbinguni, wala hairudi huko; bali huinywesha ardhi, na kuizalisha na kuichipuza, ikampa mtu apandaye mbegu, na mtu alaye chakula; 11ndivyo litakavyokuwa neno langu, litokalo katika kinywa changu; halitanirudia bure, bali litatimiza mapenzi yangu, nalo litafanikiwa katika mambo yale niliyolituma.” Neno la Mungu sio dhaifu lakini lina nguvu yake ya kiungu inayoambatana nayo: " Je! Neno langu si kama moto? Asema BWANA; na kama nyundo ivunjayo mawe vipandevipande? (Yeremia 23:29). Ni mkali na nguvu sana kwamba ni "upanga wa Roho '' (Efe.6:17). Neno la Mungu siyo mfu, ni hai kabisa. Tunasoma, “Maana Neno la Mungu li hai, tena lina nguvu, tena lina ukali kuliko upanga uwao wote ukatao kuwili, tena lachoma hata kuzigawanya nafsi na roho, na viungo na mafuta yaliyomo ndani yake; tena li jepesi kuyatambua mawazo na makusudi ya moyo."(Ebr. 4: 12).

124

Biblia ni muhimu kama njia ya msingi ya neema ambayo Mungu huwapa wake. Katika historia, neno la Mungu ndilo lilitumika katika kuleta mapinduzi kipindi Kanisa lilipokuwa linayumba. Wanamatengnezo walirudi kwenye Biblia. Neno la Mungu ndilo mwamuzi wa kila jambo katika maisha yetu. Kiri ya Westimister, sura ya kwanza, Sehemu ya 10, inasema “Roho Mtakatifu anayezungumza katika Biblia ndiye hakimu (mwamuzi) mkuu wa mabishano yote ya kidini, maamuzi yote ya mabaraza ya kidini, maoni yote ya waandishi wa zamani, mafundisho yote ya wanadamu, na kila maoni ya kibinafsi.22 Tunapaswa kuridhika na hukumu yake ambaye ndiye mwamuzi wa pekee (Mt 22:29,31, Efe. 2:20, Mdo 28:25, Lk 10:26, Gal 1:10, 1 Yn 4:1-6).” Watumishi wa Mungu wanapaswa kuhubiri neno la Mungu kwa usahihi ili kuwafanya waumini waendelee kuwa na afya njema za kiroho. Kama Kanisa halifundishi kwa usahihi neno la Mungu, matokeo yake tunakuwa na waumini wasio na afya njema kiroho na walio na utapiamlo. Kipindi ambapo Kanisa liliacha neno la Mungu liliangukia katika ushirikina wa hali ya juu. Kanisa Katoliki mpaka leo linakumbatia ushirikina kwa sababu ya kuacha neno la Mungu na kuanza kufundisha mapokeo yao. Hata Kanisa la leo linaweza kwenda Babeli kama halitafundisha mafundisho ya kweli. Watu badala ya kutegemea neno la Mungu wanaanza kutegemea vitu. Mtu fulani alisema wanatumia vitu kanisani (kwa 125

mfano vitambaa, sabuni nk) kwa ajili ya kusaidia imani ya washirika. Mtumishi mmoja alisema ni sawa na mtu anakimbia kujiokoa akakutana na mti unamsaidia kujihami; huo ni uzushi na uongo mkubwa. Kama wachungaji wasiporudi kwenye neno la Mungu, tutarajie kuona jamii ya waumini iliyochoka kiroho na isiyo na matumaini. Lakini kama tukifundisha neno la Mungu, neema ya Mungu itazidi ndani ya Kanisa. na hizi ndizo baraka za kweli kutoka kwa Mungu. II. Sakramenti Neno

"Sakramenti" halipatikani katika Maandiko

Matakatifu. Berkhof anasema neno hili linatokana na neno la Kilatini, “sacramentum” ambalo hapo awali lilionyesha jumla ya pesa zilizowekwa na pande mbili katika mashtaka. Baada ya uamuzi wa korti pesa za mshindi zilirudishwa, wakati ile ya yule aliyeshindwa ilichukuliwa. Hii inaonekana iliitwa “sacramentum”, kwa sababu ilikusudiwa kuwa aina ya toleo la upatanisho kwa miungu.” 64 Inafikiriwa kwamba matumizi ya neno hili katika nyanja ya Kikristo pengine ilifikiriwa kurejelea katika mawazo yafuatayo;

“kwanza, katika matumizi ya kijeshi ya neno,

inadokeza kiapo cha utiifu cha askari kwa kamanda wake, kwa 64

Berkhof, Louis, Systematic Theology (Grand Rapids: Eerdmans 1974), uk. 684

126

kuwa katika ubatizo Mkristo huahidi utii kwa Mungu wake hivyo neno hili lilitumika; na pili, kwa maana ya kidini ambayo ilipata kuwapo wakati Vulgate, inahusishwa na neno "Musterion" lenye kufanana maana na Sakramenti, hivyo kwa sababu yanafanana kabisa na siri zingine za dini za Ugiriki, basi neno Sakramenti linahusisha masuala ya ibada. Pia Katika Kanisa la kwanza, neno "Sakramenti" lilitumiwa kwanza kuashiria kila aina ya mafundisho na maagizo.”65 Kwa sababu hii, wanatheologia wengine wanakataa kutumia jina hili "Sakramenti", na badala yake wanapendelea kutumia "ishara," "mihuri" au "siri." Kuna wengine ambao hawataki kusikia kabisa neno Sakramenti kwa madai kwamba lina UKatoliki ndani yake. Hata wakati na baada ya Matengenezo, watu wengi hawakupenda kutumia jina "Sakramenti." Melanchton, kwa mfano alitumia "saini," yaani "ishara." Tukiri kwamba, hata Luther na Calvin hawakuafiki moja kwa moja matumizi ya neno hili. Hata Calvini aliwahi kusema Neno Sakramenti haliakisi maana yake ya asili na matumizi ya sasa, na hata halipatikani popote katika Maandiko

Matakatifu.

Lakini

mapendekezo

ya

kuendelea

kulitumia kwa sababu ya dhana ya utiifu iliendelea na kuleta

65

Berkhof, Louis, uk. 685

127

maana ifuatayo, kwamba, " Sakramenti ni agizo takatifu lililowekwa na Kristo, ambapo katika hilo kunawakilishwa neema ya Mungu katika Kristo, na faida za agano la neema zilitotiwa mhuri na kutumika kwa waumini na hizi, zinaonyesha imani yao na utii kwa Mungu.66 Sakramenti hazileti wokovu kwa mwanadamu, bali ni njia ambazo kupitia hizo Mungu huachilia neema zake. Tofauti na jinsi tunavyoamini,

Kanisa

Katoliki

wanaamini

kwamba

bila

Sakramenti mtu hawezi kupata wokovu, na kwa sababu hiyo wanasisitiza ubatizo kwa haraka sana; hata kwa mtu anayekaribia kufa, kama alikuwa hajabatizwa, lazima abatizwe haraka, la sivyo hataingia mbinguni. Kwa sababu hiyo Wakatoliki wameainisha Sakramenti saba muhimu kwao kwa ajili ya wokovu. Hata wanakaza kwamba, “kwamba Sakramenti ya toba (kwao toba ni Sakramenti) ni muhimu kwa wale ambao wamefanya dhambi za kifo baada ya kubatizwa.”67 Vifaa kwenye Sakramenti. Sakramenti zinajumuisha maji, mkate, divai na liturgia kwa nje, lakini kwa ndani Sakramenti ni ishara au alama kwa mambo fulani makubwa (Mwa. 17: 1; Rom.4: 11). Kuondoa govi

66 67

Berkhof, Louis, uk. 686 Berkhof, Louis, uk. 686

128

katika tohara inamaanisha kuondoa uchoyo wa mwili. Maji yanamaanisha kutakasa hatia na uchoyo wa mwili. Damu ya Pasaka (kikombe cha Meza ya Bwana) inamaanisha upatanisho. Kula mwanakondoo (mkate wa Meza ya Bwana) inamaanisha tendo la imani ambalo kwa kumpokea Yesu Kristo kama Mwokozi. Kwa hiyo, ni makosa kuweka uhusiano kati ya neno na ishara kama "umoja wa Sakramenti." Kwani umoja ni uhusiano kati ya vitu viwili, lakini kwa upande wa Sakramenti Neno ni ukweli, lakini Sakramenti siyo halisi. Ni ishara. Kwa sababu hiyo hatupaswi kuweka uzito sawa kwa neno la Mungu na Sakramenti. Umuhimu wa Sakramenti Kanisa Katoliki wanaamini kwamba Sakramenti ni muhimu sana kwa wote wanaopokea wokovu na toba kwa wale ambao wamefanya dhambi inayopelekea kifo. Katika Uprotestanti, kwa upande mwingine, Sakramenti hazionekani kuwa lazima kabisa. Kwanza, Maandiko yanapendekeza imani pekee kama kifaa cha wokovu, sio Sakramenti (Yn.5: 24; 3: 36; Mdo 16: 31). Pili, hata hivyo, Kanisa linapaswa kushika Sakramenti kwa sababu Bwana aliamuru Kanisa hilo lishike (ubatizo-Mt.28: 19, Meza ya Bwana (Meza ya Bwana)1Kor.11 Yaliyomo ndani ya Sakramenti ni neema ya kiroho ya ndani. Kwa maneno mengine, zinaonyesha agano la neema (Mwa. 129

7: 11), haki ya imani (Warumi 4: 11), ondoleo la dhambi (Mk.1: 4, Ubatizo wa toba; Mt.26: 28), imani (Mk.16: 16), uongofu (Mk.1: 4), ushiriki wa kifo cha Kristo na ufufuko wake (Rum.6: 3-5), na uimarishaji wa imani. Yaliyomo ya ishara hayakujumuishwa katika ishara yenyewe. Kwa maana hii tafsiri ya Kanisa Katoliki la Roma ni ya uwongo. Kwa kuongeza, haipo kwenye nafasi moja na ishara. Kanisa Reformed inasisitiza kwamba Sakramenti zinaonyesha neema ya Mungu wakati wale wanaoshiriki kwenye Sakramenti wanapokea Sakramenti kupitia imani. Ishara za nje huwa njia ya neema tu wakati zinapotumiwa na Roho Mtakatifu. Sakramenti kama vile Ubatizo na Meza ya Bwana, pia hutumika kama "udhibiti wa uanachama" ndani ya Kanisa. Ubatizo ni njia ya kukubali watu kuingia kanisani, na Meza ya Bwana ndiyo njia ya kuruhusu watu kutoa ishara ya kuendelea katika ushirika wa Kanisa. Kanisa huwachukulia watu wanaoshiriki Meza ya Bwana kama watu ambao kweli wameokoka.68 Sakramenti za Agano la Kale na Sakramenti za Agano Jipya Kanisa Katoliki la Roma Katoliki linasisitiza kwamba Sakramenti za Agano la Kale hazikuwa za ndani lakini zilikuwa za kisheria tu, na vitangulizi tu vya neema iliyopatikana katika 68

Berkhof, Louis, uk. 866

130

Kristo.Kwa hiyo Sakramenti za Agano la Kale zinachukuliwa kuwa tofauti kabisa na zile za Agano Jipya ambazo zina malengo madhubuti. Tunaweza kukubaliana kwa sehemu na wazo la Katoliki, lakini changamoto yao ni kwamba wanakataa kwamba Katika Agano la Kale hapakuwa na Sakramenti kwa sababu wanataka kuthibitisha nyongeza ya Sakramenti zao. Biblia ina ushikamani; kile kilicho katika Agano la Kale kinapata mwendelezo katika Agano Jipya. Lakini kimsingi hakuna tofauti kati ya Sakramenti mbili. I Wakorintho 10: 1-4 inasema kwamba kiini cha batizo mbili (Ule wa Agano la Kale na Agano Jipya) ni sawa kwa sababu Wote Agano Jipya na watakatifu wa Agano la Kale walikula "chakula kilekile cha kiroho na kinywaji" kutoka kwa Kristo, mwamba uleule. Warumi 4:11 inasema kwamba tohara ya Agano la Kale, kama ubatizo wa Agano Jipya, "ni muhuri wa haki ... kwa imani." Maneno ya kubatizwa (1Kor.10: 2) na Sakramenti (1Kor.10: 3,4) yanatumika kwa matukio yanayohusiana na Agano la Kale, na neno tohara pia linatumika kwa matukio yanayohusiana na Agano Jipya (Wakol.2: 11). Sakramenti hiyo inamaanisha Pasaka, na tohara inatumika kumaanisha ubatizo. Lakini Sakramenti za Agano la Kale na Agano Jipya zinatofauti katika hali ifuatayo: Sakramenti za Israeli zina sura ya kitaifa kwa kuongeza maana zake za kiroho. Kulikuwa na sherehe nyingi za kujitolea na 131

za utakaso katika Israeli zilizokuwa zikiambatana na Sakramenti, ambapo hakuna sherehe ngumu kama hizo katika Agano Jipya. Wakati Sakramenti za Agano la Kale zinaelezea kuja kwa Kristo, Sakramenti za Agano Jipya zinakumbuka dhabihu kamili ya Kristo. Neema ya Mungu katika Sakramenti za Agano la Kale ni chini ya neema ya Mungu katika Sakramenti za Agano Jipya Idadi za Sakramenti Katika Agano la Kale kuna aina mbili yaani: kutahiriwa (dhabihu ya damu, ikionyesha kuwa uchafu wa dhambi huondolewa, hii inafafa na Ubatizo) na Pasaka (Sakramenti ya damu, inayoashiria kifo cha Kristo, dhabihu ya ukombozi, hii inafanana na Ekaristi (Meza ya Bwana), ambapo sasa tunaweza kusema kwamba Agano Jipya kuna Ubatizo na Ekaristi.69 Kwa

hivyo,

Waprotestanti

na

Kanisa

Katoliki

wanatofautiana sana kuhusu aina za Sakramenti. Waprotestanti wanaamini hizo mbili tu: Ubatizo na Meza ya Bwana. Wakatoliki wanazo aina saba za Sakramenti ambazo ni: Ubatizo, Ekarisiti Takatifu, Kipaimara, Mpako Mtakatifu, Kitubio, Daraja Takatifu, na Ndoa.

Kanisa Katoliki

wanasema kwamba kila kitu

69

Maneno “Ekaristi Takatifu” yanasimama kama visawa vya neno “Meza ya Bwana, au Ushirika Mtakatifu.” Katika kitabu maneno haya yanatumika kwa kupokezana. Likionekana moja, basi inapaswa lihusishwe moja kwa moja na maana ya lile lingine.

132

kinachohitajika kwa ajili ya wokovu wa mwenye dhambi ni Sakramenti, Kwa hiyo kwao “neno” halihitajiki sana. Hata hivyo katika Kanisa la Kiprotestanti neno ni la lazima katika kukuza maisha ya Kikristo. Hata hivyo, Wakatoliki hawana sababu za msingi kwa nini wamechagua mpaka Sakramenti saba peke yake ilhali kuna mambo mengi yanayohitajika kwa ajili ya maisha ya Wakristo. Wamewahi kujitetea kwamba walichagua namba saba kama namba ya ukamilifu wa Mungu. Hata hivyo wakiulizwa swali kwamba, mbona hata namba kumi na mbili ni namba ya ukamilifu, hawana majibu. Kwa kweli ni vigumu sana kuthibitisha kimaandiko Sakramenti tano (ukiondoa Ubatizo na Meza ya Bwana) ambazo Wakatoliki wanasimamia. Kwa kweli mtu anahitaji kuwa Mkatoliki ndipo aamini uwepo wa Sakramenti saba. Aina mbili za Sakramenti Zinazotambulika Kimaandiko Kama tulivyojulisha hapo juu kwamba kuna aina kuu mbili za Sakramenti ambazo ziko Kibiblia; Ubatizo na Ekaristi Takatifu (Meza ya Bwana, au Ushirika Mtakatifu). Sasa tutajadili kwa undani aina hizi;

133

1. Ubatizo Neno

“ubatizo”

linatokana

na

neno

la

Kiyunani

“baptisma” lililo na maana pana. Maana yake ni kuzama, kuzamisha, kuchovywa, kusafisha, kuosha, kunawa, kunawisha nk. Ubatizo wa Agano Jipya uliandaliwa na tohara katika Agano la Kale. Njia ya nje ya tohara inatokana na ibada ya watu wa kale na kale. Kutahiriwa katika ulimwengu wa kale kwa watu wa mataifa ulifanyika kwa kikundi kidogo cha watu na hakukuwa na maana ya Sakramenti. Mungu alileta aina ya tohara kutoka kwa ulimwengu wa ukombozi na akaipa maana ya Sakramenti. Tohara kwa watu wa Mungu ilifanyika kwa Washirika wote wa jamii ya waumini wakiwemo watoto wachanga. Hii ilikuwa vivyo hivyo na ubatizo. Katika ulimwengu wa kale, ubatizo ulitolewa kwa watu ili kuwaosha kiroho. Mungu alitumia maana ya kuosha kutoka kwa mazoea ya zamani ya kubatiza na aliipa maana mpya ya Sakramenti. Hebu tupate dondoo muhimu kutoka kwenye Katekisimu kongwe duniani. Kwa mujibu wa Katekisimu Kubwa ya Westminister, katika majibu ya Swali la 165: “Ubatizo ni Sakramenti ya Agano Jipya, ambayo Kristo ameamuru kwa kuosha kwa maji kwa jina la Baba, na Mwana, na la Roho Mtakatifu, kuwa ishara na muhuri 134

ndani yake Kristo, ishara ya ondoleo la dhambi kwa damu yake, na kuzaliwa upya na Roho wake; ishara ya kufanywa Wana, na ishara ya ufufuo wa uzima wa milele;

ambapo

wanaobatizwa

kimsingi

wanajiungamanisha na Kanisa linaloonekana, na kuingia katika uhusiano kamili na Kristo.” Tamaduni Zinazofanana za Ulimwengu wa Watu wa Mataifa Dini za kipagani za Wamisri wa kale, Uajemi, Uhindi, Ugiriki, na Roma zilikuwa na sherehe za kuosha miili kwa kupiga mbizi baharini au kunyunyizia maji. Walakini, ibada hizi hazionyeshi ushahidi kwamba watu walibatizwa kwa jina la Mungu, au kwamba ushawishi wa kiungu ulihusiana na maagizo ya utakaso, au kifo au ufufuko.

Dhana ya Ubatizo katika Dini za Kiafrika Labda pengine katika Afrika kuna wazo la kuosha kama ishara ya kubatiza? Utafiti mdogo tuliofanya unaonesha kwamba katika makabila mengi Afrika, wanayo matambiko yanayohusisha maji. Kuna baadhi wana utaratibu wa kuoga mwili mzima kama familia imepitia matatizo mengi ili kujisafisha. Wengine hata huenda kuoga njia panda (nzila maka) kwa ajili ya kuondoa laana, huku wakichinja wanyama na kunyunyiza 135

damu katika maeneo mbalimbali. Hata hivyo, wazo hili nalo halina uhusiano wowote na maelekezo ya mungu wa kijadi. Hata hivyo, miongoni mwa makabila barani Afrika, kwa mfano miongoni mwa Wasukuma, baadhi yao wanaamini kwamba maji ni baraka, na hivyo kila kitu lazima kioshwe kwenye maji ili kuondoa uchafu; hasa katika masuala ya kiroho. Kwa kweli hatujui hili wazo la kuosha kwa Wasukuma lilianzia wapi, labda pengine kwa ajili ya kutekeleza maelekezo ya miungu. Hata hivyo, huu nao si ubatizo ambao upo kwenye Maandiko.

Ibada za Kuosha katika Agano la Kale Kulikuwa na matambiko yanayofanana na ubatizo katika nyakati za Agano la Kale. Kwa mfano, makuhani walipaswa kunawa mikono na miguu yao kabla ya kuingia kwenye maskani Takatifu. Walilazimika kuosha miili yao na maji baada ya kugusana na vitu vichafu. Walilazimika kuosha vyombo na nguo zisizo safi. Walakini ibada hizi hazikuwa na maana ya Sakramenti ya ubatizo.

Ubatizo katika Dini ya Kiyahudi (Judaism) Katika karne ya tatu Kabla ya Kristo (KK) Uyahudi walikuwa wakifanya kazi ya umishenari na walipata waumini wengi wapya wa mataifa (Mt.23: 15). Baada ya kuanguka kwa 136

Yerusalemu shughuli hii ya umishonari ilidhoofika kwa sababu ya mateso kadhaa na vikwazo vya kisheria kutoka kwa viongozi wa Kirumi. Dini ya Kiyahudi ilitoa "Ubatizo wa waongofu" kwa watu wa mataifa ambao walitaka kuingia kwenye dini ya Kiyahudi. Njia ya kwanza ya Ubatizo ilikuwa tohara, kwamba mtu wa mataifa alitakiwa kutahiriwa kabla ya kuingia kwenye Uyahudi. Hata hivyo njia hii ilibadilishwa baadaye na kuwa ubatizo. Ubatizo wa waongofu ulitolewa mbele ya mashahidi wawili au watatu. Kwa upande wa mtoto wa mzazi aliyebatizwa, aliyezaliwa kabla ya mzazi kubatizwa: ikiwa ni mvulana ambaye alikuwa na umri chini ya miaka 13 na kama ni msichana ambaye alikuwa na umri chini ya miaka 12 alibatizwa kwa ombi la baba. Mtoto alipokuwa mtu mzima, alibatizwa kwa ombi lake mwenyewe. Mtoto aliyezaliwa baada ya mzazi kubatizwa, hakuhitaji kubatizwa, kwa sababu alikuwa akichukuliwa kuwa msafi. Sherehe hii ililenga kurudisha hadhi hiyo katika jamii ya Kiyahudi kwa kuondoa uchafu wa kiibada.70

Aina za Batizo Zinazojulikana katika Maandiko Tumekwisha kueleza hapo jinsi ibada za kuosha miili zilivyofanyika katika makundi kadha wa kadha. Tumeona pia ubatizo wa Kiyahudi ambao kwa namna fulani umetajwa katika 70

Berkhof, Louis, uk. 689

137

Maandiko, lakini si moja kwa moja. Zifuatazo ni batizo ambazo zinajulikana katika Maandiko Matakatifu. 1.

Ubatizo wa Yohana Huu ndio ubatizo unaojulikana sana katika Biblia. Pia jina

la Yohana linaonekana mara nyingi na kivumishi cha neno “Mbatizaji.” Inaonekana kwamba Ubatizo huu pia ulikuwa aina ya sherehe ya kuosha. Tofauti na Ubatizo wa waongofu, Ubatizo wa Yohana ulilenga kuandaa vizuri ufalme wa Mungu unaokuja kwa kusafisha akili ya waliobatizwa, Kwa hiyo ulikuwa na maana halisi ya maadili na kiroho. Kumekuwa na tafsiri tofauti juu ya uhusiano kati ya Ubatizo wa Yohana na Ubatizo ulioanzishwa na amri ya Yesu baada ya kukamilika kwa kazi ya wokovu. Kanisa Katoliki lilitafsiri kwamba Ubatizo wa Yohana ni ishara tu inayoonyesha ubatizo wa kweli unaokuja na ulifanya kazi tu kwa imani na toba ya yule aliyebatizwa, Kwa hiyo haikujumuisha neema ya kweli, lakini Ubatizo wa Kikristo unatoa neema ya kuhesabiwa haki. Wanatheolojia kama Luther, Zwingli, Calvin waliamini kwamba Ubatizo wa Yohana na Ubatizo wa Kikristo ulikuwa sawa katika kiini chake. Berkhof pia alihitimisha kuwa batizo hizi mbili ni sawa kwa asili kwa maana ya kwamba zilianzishwa moja kwa moja na Mungu (Yn. 1: 33, Lk.3: 3), Hii ni tofauti na Ubatizo wa 138

Kiyahudi. Unaweza hata kuona kwamba kwa sababu ya kazi ya kubatiza, Mungu alimlazimisha Yohana abadilishwe hata maisha yake (Lk.3: 1-17), na alitumia maji.71 Walakini, Kuyper alidhani ya kwamba batizo hizo zilikuwa tofauti, kwa maana Ubatizo wa Yohana tu ni Ubatizo wa maji ambao haukufuatwa na kazi ya Roho Mtakatifu. Kwa kutegemea maelezo ya John Murray, Park Hyung Nong alidhani kwamba Ubatizo wa Yohana na Ubatizo wa Kikristo sio sawa, kwa maana kazi ya Yohana ilikuwa maandalizi tu, utangulizi. Kazi ya Yohana ilikuwa kuandaa njia ya Bwana. Park alipendekeza sababu zifuatazo kwa nini Ubatizo wa Yohana na Ubatizo wa Kikristo ni tofauti. Kwanza, Yohana alikuwa wa kipindi cha Agano la Kale, sio wa Agano Jipya. Pili, Ubatizo wa Yohana uliuliza toba, lakini haikuhitaji utii wa uaminifu kwa Kristo. Tatu, Jumuiya ya Wakristo ambayo ubatizo ulitolewa kulingana na agizo la Kristo haikuwa katika jamii ya Ki-Yohana. Wakati wa uhai wa Yohana jamii ya Ki-Yohana na Jumuiya ya Wakristo walikuwa tofauti. Nne, Ubatizo wa Yohana haukutolewa kwa jina la Mungu wa UTATU. Tano, sababu dhahiri kabisa kwa nini batizo mbili ni kwamba waliobatizwa na Yohana walibatizwa tena. (Mdo. 19: 1-

71

Berkhof, Louis, uk. 690

139

6). Hodge anasema, Ubatizo wa Yohana haikuwa Sakramenti ya Agano Jipya bali ni ibada ya kuandaa njia ya Masihi.72 Kwa kweli hoja hizo hapo juu zina mashiko, lakini wacha tukamilishe kipengele hiki kwa kusema kwamba, asili ubatizo wa Yohana uliamuriwa na Mungu mwenyewe; kwa sababu Mungu alimtuma kubatiza. Yeye mwenyewe anasema, “lakini yeye aliyenipeleka kubatiza kwa maji, huyo aliniambia...” (Yn 1:33); na ulitolewa kwa Makusudi maalumu kwa wakati huo, na naweza kukaza kwamba ubatizo huu ulikoma baada ya Yesu kuanza kazi yake. 2. Ubatizo wa Wanafunzi wa Yesu Wanafunzi wa Yesu walikuwa wamewabatiza watu kwa agizo la Yesu kabla ya kazi ya wokovu kukamilika. Biblia inasema, “Kwa hiyo Bwana, alipofahamu ya kuwa Mafarisayo wamesikia ya kwamba, Yesu anafanya wanafunzi wengi kuliko Yohana, na kuwabatiza, (lakini Yesu mwenyewe hakubatiza, bali wanafunzi wake, (Yoh 4: 1,2). Ubatizo huu unaweza kueleweka kama ubatizo maalumu unaoonyesha tabia za mpito za wakati wa mpito wa agano. Kama Hodge asemavyo, “Ubatizo huu ulikuwa wa maandalizi kwa kuwa ilikuwa ni aina ya ibada ya utakaso

72

Hodge, Charles, Systematic Theology - Volume III (Grand Rapids: MI: Christian Classics Ethereal Library, 1940) uk.548

140

ikisisitiza toba kama Ubatizo wa Yohana.” 73 Walakini, inaweza kuwa sio tu kwa kutaka toba lakini kuhitaji watu kumkubali Yesu Kristo kama mwokozi. Hata hivyo, hatuwezi kusema kwamba ulikuwa ni mwendelezo wa ubatizo, bali kile ambacho tunaweza kusema hapa ni kwamba kwa kuwa ubatizo tayari ulikuwa umeshakuwa njia ya kuandaa watu, basi yamkini kabisa, baada ya Yohana kutiwa gerezani, basi kazi za Yesu ziliandaliwa tena. Hatuna uhakika wa kimaandiko kwamba wale waliokuwa wamebatizwa na Yohana walibatizwa tena na wanafunzi wa Yesu. 3. Ubatizo wa Kikristo Ubatizo wa Kikristo ni ibada iliyoanzishwa na Yesu Kristo baada ya kumaliza kazi ya wokovu (Mt.28: 19,20; Mk.16: 15,16) Ubatizo huu, kwanza, ulitolewa na mhubiri wa neno, na, pili, kwa jina la Baba Mtakatifu, Mwana, na Roho Mtakatifu. A. Utafiti wa Kihistoria na Nadharia za Ubatizo. Kanisa la kwanza la Kikristo lilichukulia kwamba Ubatizo ulikuwa njia ya kuingilia kanisani na ilikuwa na uhusiano wa karibu na msamaha wa dhambi na kufikiwa kwa maisha mapya. Wengine waliamini kuzaliwa upya wakati wa kubatizwa. Kwa upande wa mtu mzima, hali ya roho yake na ufanisi wa ubatizo vilizingatiwa kuwa na uhusiano. Kanisa la kwanza halikufikiria 73

Hodge, Charles, uk.534

141

kwamba ubatizo ni lazima kabisa wakati watu wanaingia kwenye maisha mapya. Ubatizo ulikuwa tu mchakato wa marekebisho ya maisha. Baada ya karne ya pili watu walianza kusisitiza nguvu ya kishirikina ya ubatizo. Kama matokeo ya asili yake, maoni yalionekana kuwa njia ya nje ya ubatizo yenyewe ilikuwa na nguvu za maumbo bila kujali hali ya akili ya yule aliyebatizwa. Augustino aliunga mkono maoni haya. Augustino alihitimisha kwamba mtu ambaye hajapata ubatizo hangeweza kuokolewa. Mtazamo wa Augustine kuhusu Sakramenti ulifuatiwa na wanatheologia wengi. Kanisa Katoliki lilifafanua ubatizo kama Sakramenti ya kuzaliwa upya na kuingia kwenye Kanisa. Ubatizo ni (1) ishara ambayo haiwezi kufutwa inaonyesha ushirika wa Kanisa, (2) Dhambi ya asili, hatia na uchafu wa dhambi, uhuru kutoka kwenye adhabu ya milele na adhabu ya kidunia, (3) kuingizwa kwa neema ya utakaso, (4) kuwafanya watu kuwa Washirika wa Kanisa linaloonekana. Katika Kanisa la kwanza, wakati mtoto mchanga alipobatizwa, wazazi wake wa kibaolojia walikuwa wadhamini. Kwa upande wa mayatima na watumwa, wamiliki wao na mashemasi walisimama kama wadhamini. Wakati mtu mzima 142

ambaye alikuwa akiugua hakuweza kuongea, alihitaji mdhamini. Tamaduni hii iliongezwa zaidi na zaidi na kuzalisha mfumo wa mungu baba na mungu mama miongoni mwa Wakatoliki Luther hakuishinda kabisa nadharia ya Kanisa Katoliki kuhusu Sakramenti ya Ubatizo. Alidhani kwamba maji katika ubatizo sio maji ya kawaida, lakini yalikuwa maji ya maisha yenye neema, yaani maji ya kuosha kwa kuzaliwa upya kupitia Neno. Kwa maana hiyo ya Luther na Kanisa Katoliki, ubatizo husababisha kuzaliwa upya. Kwa upande wa watu wazima, athari ya Ubatizo inategemea imani, lakini kwa watoto, neema inayofaa ya Mungu ilichochea imani kwa mtoto. Hata hivyo baadaye, Luther alisema hakujua juu ya shida hii. Kundi lingine la Anabaptist hawakukubali uhalali wa ubatizo wa watoto wachanga na waliamini kwamba mtu aliyepokea ubatizo wa watoto wachanga anapaswa kubatizwa tena. Hawa pia walikataa ubatizo wa kunyunyiza na badala yake walisisitiza kwamba mtu lazima abatizwe kwenye maji mengi yanayotiririka. Kama maji hayatiririki, basi mtu atakayebatizwa kwa mara ya pili kwa maji hayohayo atachukua uchafu wa mtu huyo; kimwili na kiroho. Kanisa la Baptist linaona kwamba wale tu walio na imani ndio wanaostahili kubatizwaKwa hiyo ni marufuku kuwabatiza 143

watoto wachanga ambao hawawezi kuwa na imani peke yao. Pia wanadai kwamba ubatizo lazima uwe ule wa kuzamisha majini, kwani hiyo ndiyo maana halisi ya neno batiza. Lakini sijui wanazungumziaje ubatizo wa Kumwagia maji mwili mzima. Inakuwaje kama hakuna maji katika eneo hilo? Haya ni maswali ambayo Mbaptisti atakujibu kwa wepesi, “Mungu ataleta maji.” Hata hivyo, mkazo huo unatokana na maana ya ubatizo kwao. Wana-Refomati waliona kwamba Ubatizo ulifanywa kwa waumini siyo kwa ajili ya kuzaliwa maisha mapya, bali kuimarisha maisha mapya. Watoto wa waumini ni watoto wa agano. Ahadi ya kuzaliwa upya wamepewa. Wanaamini kwamba kuna athari za kiroho za ubatizo zinazoendelea katika kipindi chote cha maisha ya muumini. Calvin, katika mazungumzo yake juu ya ubatizo wa watoto wachanga, aliweka wazi uelewaji wake wa kanisa kwa kuzingatia agano; na kwa sababu hiyo, agano linajumuisha watu wote walio katika familia (Inst. 4.16). B. Kusudi la Kubatizwa Maji yanayotumiwa katika Ubatizo yana maana mbili. Kwanza, maji yanamaanisha kutakaswa kutoka kwenye dhambi (Efe.5: 26). Maji yanamaanisha utakaso kutoka kwenye hatia ya dhambi (msamaha wa dhambi) na utakaso kutoka kwa uchafu wa dhambi (kuzaliwa upya). Pili, waumini waliotakaswa wamejitolea 144

kumtumikia Mungu. Ubatizo unatolewa "kwa jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu." Hata hivyo, lazima tuwe na uangalifu kwa hoja mbili zifuatazo. Kwanza, kuna aina nyingine ya Ubatizo kama "(batiza) kwa jina la Yesu Kristo." Kwamba ubatizo unapaswa kuwa kwa “Jina la Yesu tu” (Mdo 2:38; 19: 5; 10:48). Je! Ni aina ipi bora? Tungependa kukiri kwamba aya za Kipaulo ambazo Paulo alisisitiza jina la Yesu Kristo zinalenga kuonyesha waziwazi tofauti kati ya Ubatizo wa Kikristo na batizo nyingine kama Ubatizo wa waongofu wa Kiyahudi na Ubatizo wa Yohana, au hata ule ubatizo wa Wanafunzi wa Yohana 4:1-2). Tunapaswa kujua kwamba Mathayo 28: 19,20 ni agizo la Bwana mwenyewe, na ndipo hapo ambapo Ubatizo wa Kikristo unaanzia. Pili, usemi "kwa jina" inamaanisha kwamba Ubatizo umetolewa kwa mamlaka ya Mungu wa UTATU. Mbali na maana hii, hata hivyo, ina maana nyingine muhimu ya kwamba Ubatizo ni kuingia ndani ya Mungu UTATU na kuunganishwa pamoja Naye, kwa maana "katika” ina maana sahihi "(ingia) kuelekea." Hasa tafsiri hii inaungwa mkono na Warumi 6: 3-6 ambayo inaelezea Ubatizo kama "kuzikwa pamoja naye katika kifo" (mstari 4) na 'kuungana naye katika kifo' (mstari 5).

145

Kusudi la kwanza la Ubatizo ni kusaini na kuridhia kuwa aliyebatizwa ameunganishwa na Kristo na anashiriki katika faida zote za agano la neema. Kusudi la pili la Ubatizo ni kukiri kwamba aliyebatizwa atakuwa na ameridhia kuwa yeye ni mshirika wa Kanisa linaloonekana na ameungana na waumini wenzake katika kumtii Kristo. C. Njia Sahihi ya Ubatizo Siku hizi kuna njia mbalimbali za ubatizo, ambapo kila anayetumia hudhania kwamba ndiyo njia sahihi kabisa. Makanisa mengi ya Kipentekoste hudhania kwmaba njia halali ya kubatiza ni kuzamisha mtu ndani ya maji. Kwa kweli si mawazo mapya kwani hata Wa-Abaptisti tangu karne ya 16 mpaka leo wanaamini kuwa njia pekee halali ya kubatiza ni kubatiza ndani ya maji kabisa (yaani kuzamisha majini au siku hizi wanaita Ubatizo wa Maji

Mengi). Wanaoshadidia mtazamo huu hudai kwamba ubatizo sio tu kuashiria kifo na ufufuko wa Yesu Kristo lakini pia unaashiria kwamba aliyebatizwa alikufa na kufufuka pamoja na Kristo. Maswali mawili yanaibuliwa: Kwanza, je nini kiini cha ubatizo? Pili, Je! Kuzamisha ndio njia halali pekee ya kubatizwa? Ukiachilia wapambe wa kisasa wa kuzamisha, Wabaptisti ni leo ni wakongwe katika kutetea mtazamo huu. Wao hudai kuwa njia ya kuzamishwa kabisa ni kiini cha ishara ya Ubatizo kwa 146

sababu ni mfano wa kifo na ufufuko wa Yesu Kristo. Wanapendekeza Mk.10: 38,39 na Lk.12: 50 kama msingi wa hoja yao. Hata hivyo, kubatizwa katika maandishi haya ni mfano wa mateso ambayo Yesu alikuwa anaenda kupata pale msalabani. Ubatizo sio mfano wa kifo na ufufuo wa Yesu Kristo. Kwa hiyo aya hizo hapo juu hazijishughulishi na hoja ya ubatizo wa Kikristo. Wabatisti wanapendekeza pia Warumi 6: 3,4, na 2:12 kama sababu nyingine ya Ubatizo wa kuzamisha. Ikumbukwe kwamba, Maandiko haya mawili ni mfano tu wa Ubatizo wa kiroho, kifo cha Kristo. Aya hizi hazijishughulishi na namna ya kubatiza, wala maana ya ubatizo. Wana-Refomati huona kiini cha ubatizo kama "utakaso" (Ez.36: 20; Mdo 22:16; Waebrania 10:22). Wabaptisti wanakaza kwamba neno “baptize lina maana mbili: "kuzamisha" na "kuchovya." Kwa kuwa baptize (Greek βαπτιζ), hivyo wao waliamua kuchukua maana ya kwanza ya kuzamisha kwa kuwa walidhania kwamba ndiyo yenye maana muhimu zaidi ya nyingine.74 Walakini, neno baptizo lina maana nyingine kama "safisha," "bafu," "jitakasa kupitia kunawa." Baadaye "safisha" na "jitakasa" ikazidi kutawala. Katika Agano Jipya hakuna mfano 74

Hodge, Charles, Systematic Theology - Volume III (Grand Rapids: MI: Christian Classics Ethereal Library, 1940) uk.488

147

maalumu wa kuzamishwa. Ripoti kwamba Filipo alimbatiza mtawa katika mto (Mdo 8:36,38) haithibitishi kwamba alimbatiza yule aliyebatizwa kwa kuzamishwa. Kusema kwamba Filipo alikuwa amembatiza mtawa majini kwa kuzamisha haipendekezi sana kwamba mitume waliweza kupata maji ya kutosha kwa kuwabatiza watu elfu tatu huko Yerusalemu. Ni jambo la shaka pia kufikiria kwamba Paulo alizamishwa katika ziwa au mto, wakati alipobatizwa na Anania (Mdo 9: 18). Pia kuna mashaka makubwa kwamba Kornelio alipobatizwa na Petro kwamba alizamishwa kwa maji kwenye maji mengi. Hatuoni kabisa katika Matendo10:47,48 kwamba waliandamana kwenda mtoni. Luka alikuwa makini kuelezea matukio yote, ama kuhusu tukio la kuelekea mtoni asingekosa kulieleza. Pia kuna wasiwasi mkubwa kama mlinzi wa gereza alibatizwa kwa kuzamishwa majini, kwani hatuoni chochote kuhusu maji mengi (Mdo 16: 22,23). Kutokana na mashaka hayo, tungependa kusisitiza kwamba “kuzamisha ni njia sahihi ya kubatiza, lakini pia kunyunyiza ni njia halali ya ubatizo. Sio vigumu kubaini wazi kwamba Maandiko hayajataja aina ya ubatizo, lakini mitume wa Agano Jipya wangerejelea maagizo ya utakaso yaliyotolewa katika Agano la Kale, wakati walipobatiza. Walakini, hata hiyo, sio wazo la kuzamishwa kwa mwili mzima katika ibada ya utakaso iliyotumiwa katika kipindi cha Agano la Kale. Badala yake, 148

kuosha mikono na miguu kwa maji (Law 30:18-27), kunyunyiza maji (Law.14: 51; Hesabu 8: 7), maelezo ya Agano Jipya juu ya upya wa kiroho kama kunyunyiza maji safi (Eze.36: 25; Ebr.10: 22), na kumwagwa kwa Roho Mtakatifu (Matendo2:33). Hii inaweza kutufanya kuamini kwamba kunyunyiziwa maji ilikuwa ishara ya ubatizo, na pengine ndiyo njia ya ubatizo iliyotumika kwa wakati huo. Lakini sisi hatukatai kwamba ubatizo wa kuzamishwa si ubatizo halisi, ila tunachojaribu kusema ni kwamba hatuwezi kukaza namna moja ya kubatiza kama ndio njia halali na kuwa zingine si halali.75 Baada ya kipindi cha Kanisa la kwanza kuisha, inasemekana ubatizo wa kuzamishwa ndani ya maji badala ya kunyunyiza maji ulianza kutumika kama njia ya Ubatizo. Mwanzoni mwa karne ya 13, njia zote mbili zilitumika wakati huohuo. Walakini, hatari ya watoto wachanga na sababu za usafi kwao ilisababisha Kanisa liachane na kuzamisha. Watu wengi hubishana kuhusu ubatizo wa kuzamisha na kunyunyiza kwa sababu hawajui maana ya asili ya ubatizo wa Kikristo, na kwa sababu hiyo kwa sababu za Kimisiolojia, hata makanisa ya KiRefomati na mengineyo yamekuwa yakibatiza kwa kuzamisha;

75

Hodge, Charles, Systematic Theology - Volume III (Grand Rapids: MI: Christian Classics Ethereal Library, 1940) uk.483

149

lakini haina maana kwamba ubatizo wa kuzamisha ni halali na ule wa kunyunyiza si halali. Ama kwa kweli, changamoto ya kubatiza kwa kuzamisha huja kwenye eneo la watoto; kamwe huwezi kumzamisha mtoto kwenye maji mengi kwa sababu za kiafya. Kwa watu wenye uelewa wa neno la Mungu, ubatizo si suala la mabishano katika kipindi chetu. Tatizo la ziada ni kutoka kwa baadhi ya makanisa ya Kipentekoste, wasiojua neno la Mungu hushadidia ubatizo bila kujua hasa maana yake. Hivyo basi, kama nilivyodokeza hapo juu kwamba kwa sababu za kimisiolojia, basi kanisa liamue ni namna njia gani bora kwao itumike kubatiza. Lakini namna yoyote ile inayohusu kuosha ni sahihi. Kwa hiyo ubatizo wa kuzamisha ni sahihi. Ubatizo wa kunyunyiza ni sahihi. Ubatizo wa kumwagia maji kwa ndoo ni sahihi. Ni wakati wa kuondokana na uchanga wa kudhania njia fulani ya ubatizo ni sahihi kuliko nyingine. D. Mamlaka ya Kubatiza Kwa upande wa kutahiriwa, haikuainishwa wazi kwamba ni nani aliyepaswa kufanya zoezi la kutahiri. Waisraeli wote waliweza kutahiriwa. Kwa ujumla, mwenye nyumba alitahiriwa (Mwa. 17:23). Wakati mwingine mama alifanya (Kutoka.4: 25). Kanisa Katoliki linaona kuwa ubatizo ni muhimu kabisa kwa wokovu. Ikiwa mtoto angefariki wakati wa mchakato wa 150

kuzaliwa, na kwa sababu ya kukosekana kwa kuhani kwenye eneo la kuzaliwa mtoto huyo, basi wakatoliki waliwapa haki wakunga kuwabatiza watoto hao haraka. Wakatoliki wanakubali ubatizo kutoka kwa mtu yeyote kwa sababu wanaamini kwamba mtu akifa bila kubatizwa haendi mbinguni. Wana-Refomati wanaamini kwamba ni wachungaji pekee wanaweza kubatiza, kwa maana Sakramenti ni aina tu za ishara au ishara inayoambatana na neno. Ubatizo kama Sakramenti, hupaswa kutolewa na Mhubiri wa Neno ambaye ni Mchungaji. Kwa kutegemea na makanisa, hata hivyo, makanisa mengi ya Kiprotestanti huruhusu wachungaji waliosimikwa rasmi kwa kazi ya uchungaji. Wale ambao hawajasimikwa (yaani hawajawekewa mikono) hawaruhusiwi kubatiza. Hii haina maana kwamba watu waliosimikwa wana kitu cha ziada, bali ni taratibu katika Kanisa. Neno linasema “kila kitu kiende kwa utaratibu.” Ni utaratibu mzuri kwa sababu anayepewa mamlaka ya kutoa ubatizo ni yule aliyepewa mamlaka ya kuhubiri neno la Mungu. Wana-Refomati

wanapokea

ubatizo

unaotolewa

na

Wakatoliki, kwa sababu ya kuamini kwamba ni ishara tu ya nje. Hata hivyo Kanisa la Refomati la Korea Kusini, hivi karibuni wameanza kuwabatiza tena waumini wanaotoka katika Kanisa Katoliki kwa kudai kwamba kama wanakataa mafundisho yao, basi haina maana yoyote kupokea ubatizo wao. Pengine tunaweza 151

kufikiri zaidi juu ya hoja hii; kwa mfano kama watu wanakataa UTATU Mtakatifu, je tunaweza kupokea mtu aliyebatizwa huko na kupokelewa katika ushirika wa Kanisa lenye mafundisho ya kweli? Kwa mfano Kanisa la Mashahidi wa Yehova, Watakatifu wa Siku za Mwisho; tunaacha mjadala wa kitheologia kwa wale wanaotaka kuchunguza kuhusu hili. Wakati Gani wa Kubatizwa Watu walitahiriwa katika siku ya nane baada ya kuzaliwa. Katika Agano Jipya ubatizo ulitolewa papo hapo wakati mtu anayetaka kubatizwa alikiri imani. Wakati wageni walipoanza kuingia kanisani, umuhimu wa uchunguzi uliongezeka zaidi na tabia ya kubatiza baada ya kipindi cha masomo cha Ubatizo kilianzishwa. Walakini, Kanisa Katoliki la Roma na Kanisa la Orthoksi, la Kilutheri, na hata wana Refomati wanakaza watu wanaobatizwa ikiwa ni watu wazima lazima wathibitishwe katika imani yao. Na katika kuthibitisha imani yao wamekuwa wakifanya kwa kupitia mafundisho ya ubatizo na mengineyo, isipokuwa kwa watoto wachanga. Tunaweza kusema kwamba watu wanahitaji kubatizwa mara tu wanapomkiri kwa imani Yesu Kristo kuwa Bwana na Mwokozi wa maisha yao. Lakini kwa kuwa ni vigumu kuthibitisha haya, tunahitaji angalau kuwa na mafunzo kwa ajili ya watu 152

wanaohitaji kubatizwa ili kuimarisha imani zao. Hata hivyo, isiwe mzigo mkubwa kwa watu walioamini kwamba wanakaa miaka kadhaa ndani ya Kanisa bila kubatizwa. Ingawa ubatizo hauwezi kumpatia wokovu yule anayebatizwa, lakini ni muhimu kubatizwa kwa sababu Bwana wetu Yesu Kristo aliagiza. 2. Meza ya Bwana Ni aina ya pili ya Sakramenti ambayo inasherehekewa na makanisa mengi ya Ki-Protestanti. Mara nyingine inajulikana kama “ushirika mtakatifu,” au “Ekaristi takatifu.” Tutayatumia maneno haya kwa kubadilishana. Utafiti wa kihistoria Sadaka katika Agano la Kale kama Pasaka na sadaka ya amani ni ilijumuisha tendo la kula (Pasaka: Kutoka 112: 8-10; Law. 7: 28-34). Sherehe hii ya kula ni mfano kwa Ekaristi ya Agano Jipya. Watu safi wanaweza kushiriki katika Ekaristi Takatifu. Chakula hiki kinamaanisha kuwa Mkristo anayepata udhibitisho kupitia imani anafurahi amani na Mungu na Bwana Yesu Kristo, na kwamba Mungu anakaribisha watu wake mwenyewe

ndani

ya

nyumba

yake

kama

wageni

na

huwaunganisha kwenye ushirika wa kupendeza na maisha ya jamii.

153

Yesu aliamuru Ekaristi juu ya msingi wa chakula cha Pasaka ya Agano la Kale. Yesu alishiriki katika ibada ya sikukuu ya Pasaka iliyofanywa na Wayahudi. Chakula hiki kina maagizo kumi na mbili:1.

Kuingia ndani ya nyumba na meza ya unga, wakiimba nyimbo za Aleluya na nyimbo za Pasaka katika Zaburi 113-118.

2.

Baraka ya kichwa cha familia.

3.

Kunywa glasi ya kwanza ya divai.

4.

Kula

mkate

usiotiwa

chachu,

mimea

yenye

uchungu, mbogamboga, kitoweo cha matunda, na kondoo aliyechemshwa 5.

kiongozi wa familia anauliza jinsi chakula cha Pasaka kinatofautiana na mlo mwingine.

6.

Kiongozi anaelezea tukio la Kutoka.

7.

Kuimba Zaburi 113-115.

8.

Kunywa glasi ya pili ya divai.

9.

Kuchukua mkate, kuiweka kwenye kitoweo cha matunda

10. Kula mwanakondoo wa kuchoma, 11. Kunywa glasi ya tatu ya divai. Kisha imba Zaburi 116118.

154

12. Kunywa kikombe cha nne. Hapa ndipo mwisho wa Pakasa.76 Mkate ambao Yesu aliwapatia wanafunzi wake (Mk.14: 22) ulikuwa mkate wa agizo la tisa. Divai ambayo Yesu aliwapatia katika Mark14: 23 ilikuwa divai ya utaratibu wa kumi na moja. Katika Mark.14: 25, lakini, Yesu aliahirisha kuchukua kikombe cha nne hadi wakati wa Parousia

77

(Math 26:29 “Lakini

nawaambieni, Sitakunywa kabisa tangu sasa uzao huu wa mzabibu, hata siku ile nitakapokunywa mpya pamoja nanyi katika ufalme wa Baba yangu.” Kwa hiyo Ekaristi ya Yesu haikuwa sherehe iliyokamilishwa. Ekaristi itaisha kwenye parousia. Ekaristi zote ambazo tumekuwa tukishiriki katika historia ni mila zisizo kamili. Ekaristi iliyokamilishwa ni ile itakayokuwepo wakati Yesu na Wakristo wote watakapokunywa divai mpya katika ufalme wa Mungu.

Maoni ya Kipindi cha Mitume Paulo

alifuata

Ekaristi

iliyoanzishwa

na

Yesu

na

akaisimamisha kama Sakramenti. Paulo anasema, “kwa maana mimi nalipokea kwa Bwana niliyowapa ninyi.” (1 Kor.11:23a). Meza ya Bwana (au Chakula cha jioni) inaonyesha chakula cha 76

Mhadhara wa somo la Ekklesiolojia, Chongshin Theological Seminary, November 2018. Uk. 70 77 Parosia ni kurudi kwa Yesu mara ya pili.

155

jioni cha Wayahudi. Jina hili lilitumiwa, kwa Ekaristi kama chakula cha jioni. Ekaristi lazima ifanyike sio kwenye madhabahu bali kwenye meza ya kula. Msalaba wa Kristo unapindua wakati madhabahu nyingine imejengwa" 78 Dhabihu ya Kristo msalabani haipaswi kurudia, kwa sababu ilitolewa mara moja na kamili. Sadaka ya msalabani

inatosha, hakuna dhabihu nyingine

inayohitajika, na ikiwa dhabihu nyingine inahitajika, sadaka ya msalabani haifai. Katika “meza” kuongeza kivumishi cha "Bwana" inakusudia kutofautisha vyakula vingine katika dini za kipagani.

Maoni ya Kanisa la Kwanza Tangu karne ya pili “mlo wa upendo” na Ekaristi ilianza kutengwa katika ibada ya kula ambayo iliwahudumia masikini na ambayo waumini na wasioamini walishirikiana pamoja, na Ekaristi ya kumbukumbu iliadhimisha mwili na damu ya Kristo na ambayo waumini peke yao walikuwa sehemu yake. Ekaristi ambayo haikuwa na dhana ya huduma na ushirika ilianza kuwa aina ya ibada ya fumbo la ajabu. Katika kipindi hiki, wazo la kiroho na mfano lilisisitizwa kwa (Origene, Basil, Gregory wa Naziansus). Kwa upande mwingine mkazo ulikuwa juu ya hoja kwamba mwili na damu ya Kristo imeunganishwa na mkate na divai ya Ekaristi;

78

Calvin, Institutes, IV.18.3.

156

ilijulikana kama “transubstantiation” (Gregory wa Nyssa, Chrysostom).

Maoni ya Augustino Maoni ya Augustino kuhusu Ekaristi yamechanganyikana sana. Alisema kwa upande mmoja kuwa mkate na divai ya Ekaristi ni mwili na damu halisi ya Kristo, lakini, kwa upande mwingine, alitofautisha kati ya ishara na yaliyomo kwenye alama hiyo na alifikiria kwamba Ekaristi inafanya kazi kama ukumbusho wa kifo cha Kristo msalabani, na kiini cha mkate na divai haikubadilika. Baadaye alihitimisha kwamba kula na kunywa katika Ekaristi maana yake ni kumwamini Yesu, na kuwa na ushirika pamoja naye. Ni dhahiri kwamba mawazo ya Agostino yaliweka msingi na kuendelezwa na Kanisa Katoliki katika Imani yao ya mabadiliko halisi ya Ekaristi Takatifu.

Maoni katika Enzi za zama za kati Katika kipindi cha enzi za zama za kati, maoni ya Augustino kuhusu Ekaristi yalibadilishwa na fundisho la mabadiliko halisi” yaani “Transubstantiation” 79 Fundisho la

79

Imani kwamba katika Ekarist Takatifu, mkate na divai hubadilika kabisa na kuwa mwili na damu halisi ya Yesu Kristo. Kazi hii inafanywa na kuhani (padri)

157

mabadiliko halisi lilipendekezwa na Paschasius Radbertus mnamo mwaka 818. Baada ya hayo ilipitia majadiliano makali kwa sababu ya utata wake. Mnamo 1134 hatimaye ilifafanuliwa na Hildebert wa Tours. Mnamo 1215 Baraza liliipitisha rasmi kuwa fundisho la Kanisa, na kuimarishwa katika Baraza la Trent. Kulingana na fundisho hili Yesu Kristo huja katika Sakramenti kwelikweli. Katika Ekaristi mkate na divai hubadilishwa na kuwa mwili na damu ya Kristo. Hii inamaanisha kuwa Kristo anakuja kabisa katika Ekaristi. Ekaristi hutoa neema ya utakaso, msamaha wa dhambi ndogo, uokoaji kutoka kwenye dhambi za kibinadamu, na tumaini fulani la wokovu wa milele. Ekaristi ni ileile na sadaka iliyokamilishwa msalabani. Tofauti pekee kati ya hizo mbili ni kwamba dhabihu msalabani ni ile ya damu, lakini Ekaristi kwenye misa ni dhabihu isiyo na damu. Ufanisi wa Ekaristi hufanya kazi kwa wale wanaoshiriki katika misa, na pia kwa waumini wanaotubu katika toharani.80

Maoni Wakati wa Matengenezo Wanamatengenezo walipinga fundisho la “mabadiliko halisi.” Hata hivyo. Luther alielewa Ekaristi halisi. Aliunga mkono pale anapoendesha misa ya ekaristi. Kwa hiyo Padri humshusha Yesu kwelikweli kwenye mkate na divai 80 Wakatoliki hutumia neno “toharani” ni sehemu inayodhaniwa kuweka kati ya mbingu na dunia, kwa katikati sasa. Hapo mtu anapofariki roho yake huenda hapo kwa ajili ya kuadhibiwa. Na hivyo dhana ya kwamba “Mlaze Mahali Pema Peponi,” pia ina shina lake kutoka kwenye dhana ya Purgatori

158

uwepo halisi wa Kristo katika mwili. Maoni yake juu ya Ekaristi yalikuwa fundisho la consubstantiation. Kulingana na fundisho hili, Kristo yuko "ndani na chini" ya mkate na divai. Kwa upande wa Zwingli yeye alidai uwepo wa kiroho wa Kristo kwa wale walioshiriki Ekaristi, na kwa ujumla tunaweza kusema kwamba Zwingli aitafsiri maneno ya Ekaristi kwa analogia na akasema kuwa ni ukumbusho tu. Hata hivyo, Calvin alipinga wazo la Wakatoliki na Wazo la Luther. Alikubali kwa sehemu wazo la Zwingli kwamba kwa sehemu Kristo anakuwepo kwenye mwili katika Ekaristi kiroho. Dhana hii Calvin aliita “uwepo wa Kiroho wa Bwana.” Calvin alienda mbali zaidi katika ufafanuzi wake na kusema kwamba Ekaristi ilibidi ieleweke kwanza kama zawadi ya neema ya Mungu kabla ya kueleweka kama tabia ya mwanadamu. Kwa mujibu wa Calvin, Ekaristi inaimarisha imani. Ekaristi ilithibitisha na kuiona umoja wa fumbo kati ya Kristo na waumini kupitia uwepo wa kiroho wa Kristo. Walakini, Bavinck anaonya kwamba taarifa ya Calvin kwamba maisha ya Kristo yanamwagika kwa mwamini kwa wingi, wakati wa kushiriki Ekaristi ni ya kusadikika.81 Na hivyo umakini unapaswa kuwepo.

81

Bavinck, Herman. Reformed Dogmatics (p. 661-75). Baker Publishing Group. Kindle Edition.

159

Maoni ya Friedrich Schleiermacher (1768–1834) Schleiermacher alikuwa mwanatheolojia wa Ujerumani, mwanafalsafa, na msomi wa Biblia. Alikuwa mwanatheolojia mwenye ushawishi mkubwa baada ya John Calvin. Karl

Barth

anamwelezea

Schleiermacher

kwamba

alipokuwa karibu na kufa, akiwa kwenye kitanda chake cha mauti alisherehekea Ushirika Mtakatifu na familia yake: na alitumia maji badala ya divai, kwa sababu daktari alikuwa amemkataza kutumia mvinyo, na alidai kwamba, Kristo, kwa kubariki divai, pia alikuwa amebariki maji. Karl Barth anaendelea kumtetea Schleirmacher kwamba “hakuna shaka yoyote kwamba Schleiermacher alitaka kusherehekea Ushirika Mtakatifu. Alitaka katika Kristolojia yake, ambapo maudhui yake yanaweza kulinganishwa na maji, kumtangaza Kristo…Mwishowe tunaweza kuamini tu kwamba Schleiermacher, pia, alikuwa mwanatheolojia Mkristo; hiyo, narudia, ni kitu anachofanana na Luther na Calvin na (isije ikasahaulika!)”82 Hata hivyo, wachambuzi wa Kirefomati wanahitimisha kwamba Schleiermacher alichukulia Ekaristi kama njia ya kuhifadhi ushirika wa mwamini na Kristo. Kwake, hakuna maana

82

Karl Barth, Protestant Theology in the Nineteenth Century, (London: SCM Press, 2001), 418.

160

ya kiroho kushiriki meza ya Bwana zaidi ya kutunza washirika wasiondoke kanisani. Kwa maelezo yake, ni kwamba wale ambao wanashiriki Meza ya Bwana ndio washirika halisi wa kanisa linaloonekana, na hiyo ndiyo alama ya Mkristo wa Kweli. Na ndiyo maana aliweza kushiriki Meza ya Bwana yeye mwenyewe pamoja na familia yake katika kipindi cha kifo chake, kwa maana ya kuendelea kujiungamanisha na kanisa linaloonekana. Mwanatheolojia huyu alivunja utaratibu wa kutumia divai na badala yake akatumia maji, hili linaweza kutufanya tutilie mashaka msimamo wake wa Kibiblia kuhusu suala hili. Ilisikika mahala fulani kwamba mwanatheolojia wa Kenya, John Mbiti alipendekeza kutumia maziwa na ugali kwenye Meza ya Bwana ili kuwafanya washirika waelewe kabisa kile wanachofanya. Kwa ujumla maoni ya haya yanapingana na kile ambacho Biblia imesema. Tumeona maoni mbalimbali kuanzia kipindi cha kanisa la kwanza na kuendelea miongoni mwa wanatheolojia wengine waliofuatia. Ama kwa hakika hatuwezi kusema kwamba kipi ni bora zaidi. Tunaendelea kudadavua kwamba ni muhimu kutambua Ekaristi Takatifu kwa kuzingatia mtazamo wa Wanarefomati, ambao kwa kweli ndio msimamo mzuri, na kwamba uko Kibiblia. Mtazamo wa Wakatoliki na Walutheri umechanganya ushirikina mwingi kwenye Ekaristi Takatifu. 161

Utendaji wa Ekaristi Maneno yanayoanzisha Ekaristi ni katika Math.26:26-29, Mk.14: 22-25, Lk.22: 17-20. Ekaristi lazima ifanyike kulingana na taarifa hizi. Ekaristi ilianzishwa kabla ya kumalizika kwa pasaka. Badala ya Mwana-Kondoo wa Pasaka mkate ulitumika. Ekaristi ikawa ibada isiyo ya damu, kwa maana Kristo tayari alijitoa mwenyewe kikamilifu msalabani. 1. Uvunjaji wa mkate Mkate unaashiria mwili wa Yesu (Yn.6:51, " Mimi ndimi chakula chenye uzima kilichoshuka kutoka mbinguni; mtu akila chakula hiki, ataishi milele. Na chakula nitakachotoa mimi ni mwili wangu, kwa ajili ya uzima wa ulimwengu." Mikate isiyotiwa chachu ilitumiwa wakati wa Pasaka, lakini hakukuwa na amri kamili ya kutumia mkate usiotiwa chachu peke yake. Bwana alitumia mkate usiotiwa chachu, kwa kuwa wangeipata kwa urahisi. Hata ingawa ukweli kwamba chachu ilimaanisha dhambi (1Kor 5: 6,7), Wakristo wa Kanisa la kwanza walitumia mkate wa chachu, ambao ulitumiwa katika milo ya kawaida, pia katika Ekaristi. Kanisa Katoliki linatumia mkate usiotiwa chachu. Makanisa ya Kirefomati hutumia ain azote za mikate. Uvunjaji wa mkate unafananishwa na mwili wa Yesu na ulitolewa kwa wokovu wa wanadamu. Wale ambao husimamia 162

Ekaristi huvunja mkate mbele ya macho ya waumini, kwa sababu Yesu alimega mkate mbele ya wanafunzi. 2. Mvinyo (divai) Divai inaashiria damu ya Kristo iliyomwagika msalabani. Juisi ya zabibu ilitumiwa (Mt.26:29; Mk.14: 25; Lk.22:18). Juisi hii ilikuwa inatumiwa kila siku huko Palestina. Maandiko hayakuelezea kama juisi ya zabibu lazima itumike au divai inapaswa kutumika, lakini itakuwa inafaa kutumia juisi ya zabibu kwa sababu ya athari za pombe. Kanisa Katoliki hutumia juisi ya zabibu na kuchanganya na maji, kwa Imani kwamba damu na maji vilitoka kwenye mwili wa Yesu. Kuhusu kunywa ile divai, hakuna kiashirio ikiwa kila mwamini alitumia kikombe chake mwenyewe au kikombe kimoja. Lakini pengine kwa upungufu wa vifaa kipindi kile, pengine walitumia kikombe kimoja na kilikuwa kinasafishwa. Hata sasa kuna makanisa yanatumia kikombe kimoja kwa watu wote. Lakini ni bora kila mwamini atumie kikombe chake kwa ajili ya usalama wa afya. Wakati wa Yesu, walikaa kwa mzunguko, huku meza ikiwa katikati. Na walikula na kunywa (kuchukua na kugawanya, Lk.22: 17). Ekaristi inajumuisha kuwa na mwili wa Kristo kiroho kupitia imani na vilevile kula na kunywa kwa mwili. 163

SURA YA SABA IBADA NA SIKU YA KUABUDU Siku ya kuabudu ni mojawapo ya suala muhimu sana katika Eklesiolojia. Kuna wengine ambao wanaona kwamba siku ya kuabudu ni siku ya Jumamosi, huku wengine wakisema ni Jumapili, na wengine wanasema siku yoyote tu ilimradi umetenga siku moja katika siku saba. 1. Siku ya kuabudu: Jumamosi au Jumapili? Japokuwa sitaki kuingia majadiliano ya kiapolojia kuhusu siku ya kuabudu; kwamba ni Jumamosi ama Jumapili, ni ukweli usiopingika kwamba Biblia haitaji mkusanyiko wowote wa siku ya sabato ya Jumamosi katika Agano Jipya. Tunasoma katika Matendo Ya Mitume 20:7 “Hata siku ya kwanza ya juma, tulipokutana ili kumega mkate.” Katika 1 Wakorintho 16:2 Paulo anawasihi Wakristo wa Korintho, “Siku ya kwanza ya juma kila mtu kwenu na aweke akiba kwake, kwa kadri ya kufanikiwa kwake.” Pia Paulo anayataja haya matoleo kuwa “huduma” katika 2 Wakorintho 9:12, haya matoleo lazima yamehusishwa na ibada ya siku ya Jumapili ya Wakristo. 164

Utekelezaji wa Sabato ya Agano la Kale ni tofauti sana na utekelezaji wa Sabato ya Kikristo. Katika Sabato ya Agano la Kale watu hawakutakiwa kuondoka katika maeneo yao; lakini katika Sabato ya Kikristo tunafanya mambo yote kwa utukufu wa Mungu. 2. Namna ya Kuabudu Ama kuhusu ibada, maana ya neno la Kigiriki la Agano Jipya mara nyingi hutafsiriwa "ibada" (proskuneo) ni "kuanguka mbele ya" au "kuinama mbele ya." Kuabudu ni jambo la kiroho. Kwa kuwa ni hatua ya ndani, ya kibinafsi, Wakristo wanaabudu wakati

wote,

siku

saba

kwa

wiki.

Wakati

Wakristo

wanapokusanyika kwa pamoja katika ibada, kila mmoja anapaswa kumwabudu Mungu kibinafsi, ingawa wamekusanyika pamoja. Lazima tuabudu "kwa roho na kwa kweli" (Yn. 4: 23-24). Kuabudu katika roho hakuhusiani na hali yetu ya kimwili. Inahusiana na hali yetu ya ndani na inahitaji vitu kadhaa. Kwanza, lazima tuzaliwe tena. Bila Roho Mtakatifu kuishi ndani yetu, hatuwezi kumjibu Mungu katika ibada kwa sababu hatumjui Yeye. "Hakuna mtu anayejua mambo ya Mungu isipokuwa Roho wa Mungu" (1 Wakorintho 2: 11b). Roho Mtakatifu ndani yetu ni yule anayeimarisha ibada kwa sababu Yeye hujitukuza Mwenyewe, na ibada yote ya kweli inamtukuza Mungu.

165

Vilevile, kuabudu katika roho inahitaji mawazo juu ya Mungu. Paulo anasema "itoeni miili yenu iwe dhabihu iliyo hai, takatifu, ya kumpendeza Mungu, ndiyo ibada yenu yenye maana. Wala msiifuatishe namna ya dunia hii; bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu "(Warumi 12: 1b, 2b). Katika ibada mawazo yetu yanapaswa kuhamishwa kutoka kwenye hali ya ulimwengu na changamoto zake, na kuelekezwa kwa Mungu peke yake. Katika ibada ya Kikristo hakuna kanuni maalumu ya matendo katika ibada, kwa mfano labda kama tunapaswa kukaa, kusimama, kuanguka chini, utulivu, au kuimba sifa kwa sauti wakati, au kucheza, au kupiga mziki. Kanisa linahitaji kuweka mazingira mazuri ambapo watu wote wataelekeza mawazo yao kwa Mungu. Na ikiwa kusimama, kukaa, kuimba, kucheza, na mambo mengine yanaweza kusababisha watu waelekee kwa Mungu, basi vinapaswa kuwepo ndani ya Kanisa. Na kwa sababu hiyo hakuna utaratibu wa ibada ambao unatoka kwa Mungu moja kwa moja bali taratibu zote za ibada huandaliwa na wanadamu kwa ajili ya kusaidia watu namna wanavyopaswa kumwabudu Mungu katika uzuri. Jambo muhimu zaidi ni kwamba tunamwabudu

166

Mungu kwa roho (ndani ya mioyo yetu) na kwa kweli (katika mawazo yetu). 83 3. Utoaji katika ibada Katika ibada za Kikristo, utoaji ni sehemu muhimu sana. Kila watu wa Mungu wanapokutana katika ibada wanapaswa kutoa matoleo ya shukrani na mengineyo. Siku hizi kumekuwa na changamoto kuhusu matoleo ya zaka. Watu wengine wamekuwa wakidadisi kama bado wanahitaji kutoa zaka ilihali hawako chini ya sheria. Ingawa makanisa hayajapewa asilimia ya kutoa katika Agano Jipya, kanuni ya kutoa kwa uwiano inafundishwa (1 Wakorintho 16: 2;2 Wakorintho 8), na waumini wengi wanaona kuwa ni fursa ya kutumia zaka kama sehemu ya kutoa. Agano Jipya pia linaandika kuwa waumini katika Kanisa walikuwa wakikusanya ili kutoa kwa huduma zingine. Ingawa inaweza kuwa hakuna mstari fulani unaoashiria kuwa Kanisa linapaswa kutoa zaka kwa huduma zingine, inaonekana kwamba makanisa yanapaswa kutoa kwa ukarimu katika kusaidia huduma zingine kama Bwana alivyowajaalia. Makanisa mengine yanaweka kiasi fulani katika bajeti yao kuelekea "huduma za nje" kama njia ya kuwasaidia kuzingatia uwiano kwa mahitaji makubwa ya ulimwengu unaowazunguka. 83 https://www.gotquestions.org/Kiswahili/kikristo-ibada.html 167

Kwa kweli washirika wanapaswa kufundishwa namna ambavyo wanaweza kumtolea Mungu pasipo maumivu yoyote. Utoaji wa Kikristo unapaswa kuwa sherehe. Washirika wanapaswa kujua kwamba “utoaji wa zaka ni kiwango cha chini sana cha kumtolea Mungu,” kwa maana ya Wakristo wanapaswa kutoa zaidi ya zaka; kwa hiyo yule anayeshindwa hata kutoa hicho kiwango cha chini anahitaji kusaidiwa ili ajue kutoa kwa furaha. 3. Matumizi ya muziki kanisani Suala la mziki limekuwa la mjadala katika Kanisa. Kuna wengine wanaodai kwamba watu walioitwa wanapokuwa katika ibada hawapaswi kuchanganya na mziki wowote, bali wanahitaji kuweka mawazo yao kwa Mungu peke yake. Katika Agano la Kale vyombo vya muziki vilitumiwa kwa hakika katika ibada (1Nyak.15:16, 16:42; 23:5; 2Nyak. 7:6; 23:13; 29:26-27; 30:21; 34:12: Neh.12:36; Zab.4:1; 6:1, 54:1, 55:1, 61:1, 67:1, 76:1, Isa. 38:20; Amo. 6:5 Hab. 3:19). Kanisa la kwanza lilihusishwa kwa karibu sana na Wayahudi. Kuna uwezekano mkubwa sana kwamba waliendelea kutumia vyombo vya mziki katika Kanisa, kama walivyofanya katika ibada zao za awali. Kwa hiyo, hata bila kumbukumbu la wazi katika Agano Jipya, ni wazi Kanisa linaweza kutumia vyombo vya mziki katika ibada yake.

168

Katika Waefeso 5:19 tunasoma, "mkisemezana kwa zaburi na tenzi na nyimbo za rohoni, huku mkiimba na kumshangilia Bwana mioyoni mwenu;" Maneno "tenzi na nyimbo" ni tafsiri ya neno la Kiyunani psallontes, mzizi ambao ulimaanisha "kusugua au kugusa" au "kusonga au kuvuta nyuzi." Biblia haipingi au kuamuru matumizi ya vyombo vya mziki katika Kanisa.Kwa hiyo, Kanisa lina uhuru wa kuitumia au kutokutumia vyombo vya mziki. Kwa maelezo haya, yule anayetumia, asilaumiwe, na yule ambaye hatumii halaumiwi pia. Makatazo ya kutumia vyombo vya muziki kanisani yanaegemea katika upande wa kitamaduni zaidi kuliko ya kiroho. Washirika wengi wa Kanisa waliotoka katika dini za kipagani walijitahidi

kuachana

na

mazoea

ya

kitamaduni

ambayo

yaliwakumbusha maisha yao ya zamani yasiyo ya kiungu. Kwa mfano, ili kuonyesha kwamba waamini watafufuka, Wakristo wengi walizika wafu wao badala ya kuwateketeza kwa moto jambo ambalo lingeleta usumbufu wakati wa Ufufuo wa mwisho. Wengine walikuwa waachana kabisa na shughuli zozote za kijamii ambazo hazina uhusiano na Kanisa, na matokeo yake Kanisa lilionekana kana kwamba watu wengine hawahitaji kujiunga nalo. Ilionekana kama dini ya siri, ambapo mtu akijiunga anajitenga moja kwa moja na jamii yake.

169

Vyombo vya mziki vilianza kuonekana katika makanisa mengi katika karne ya 7 na viliongezeka kutumiwa katika karne ya 13. Bado, wanatheolojia wengi kama John Calvin, John Wesley, Martin Luther, na Charles Spurgeon, hawakukubali vyombo kutumika katika Kanisa, na Kanisa la Greek Orthodox bado halitumii vyombo. 4. Kucheza kwenye ibada Nimeona ni vyema kutokeza jambo la kucheza kwenye ibada za Kikristo. Utafiti unaonesha kwamba wanatheolojia wengi hawajafanya utafiti kuhusu suala hili. Linaonekana ni jambo la kitamaduni sana. Kuna wale wanaokaza kwamba kucheza ndani ya ibada ni chukizo machoni pa Bwana, huku wengine wakidai kwamba Wakristo wako huru kucheza mbele za Bwana. Kucheza mara nyingi hutajwa katika Biblia kwa namna tofauti. Kisa cha kwanza kinapatikana katika Kutoka 15:20 wakati Miriamu, dada ya Musa na Haruni, alipowaongoza wanawake wa Israeli katika kucheza kufuatia muujiza kwenye Bahari ya Shamu. Ilikuwa kama kielelezo cha ibada na sherehe. Daudi pia ni mfano mzuri wa kucheza katika Agano la Kale. Katika 2 Samweli 6:16 inasema, tunasoma "Sanduku la BWANA lilipokuwa likiingia katika mji wa Daudi, Mikali binti Sauli akatazama dirishani akamwona Mfalme Daudi akiruka na kucheza 170

mbele za BWANA." Zaburi pia zilitaja kucheza kama njia ya ibada katika Zaburi 30:11; 149: 3; na 150:4. Mat. 11:17 inabainisha kucheza kama ishara ya furaha iliyoambatana na muziki (pia Lk. 7:32). Hata hivyo rejea hizi hukosolewa kwamba Daudi alicheza nje ya muktadha wa Kanisa, alikuwa nje ya kusanyiko takatifu katika ibada, hakucheza kwenye hema ya kukutania, kwa hiyo kucheza kwake kunatiliwa mashaka kama kunaweza kuwa rejea halisi kwenye Agano Jipya. Mbali na mifano mizuri hapo juu, kucheza pia kulihusishwa na ibada za kipagani (Kutoka 32:19). Uchezaji wa binti ya Herodias ulitumika katika kumwua Yohana Mbatizaji (Marko 6: 17-28) Kucheza kwenye ibada hakujatajwa waziwazi katika Maandiko yanayohusiana na makusanyiko ya Kanisa la Agano Jipya. Hakuna mahali katika Agano Jipya kwamba katika kusanyiko fulani watu walikuwa wanacheza katika ibada. Hata hivyo, Biblia inatoa ushauri kwamba, "Vitu vyote vifanyike kwa adabu na kwa utaratibu" (1 Kor,14:40). Kwa hiyo, kila Kanisa la mahali linaweza kuamua ni jinsi gani, na wakati gani kucheza kunaruhusiwa ndani ya ibada ilimradi kucheza huko kunamtukuza Mungu.

171

Kwa hiyo wale wanaokataa kucheza kanisani wako hawatendi dhambi ilmradi wanafanya hivyo kwa kumtukuza Mungu. Wale wanaokubali kucheza kanisani nao hawatendi dhambi ilmradi wanafanya hayo kwa utukufu wa Mungu. Mwisho ningependa kusema kwamba Wakristo wanapaswa kutafuta kutimiza 1 Wakorintho 10:31 inayofundisha, "Basi, mlapo, au mnywapo, au mtendapo neno lo lote, fanyeni yote kwa utukufu wa Mungu. Msiwakoseshe Wayahudi wala Wayunani wala Kanisa la Mungu."

172

SURA YA NANE KUWA MWANACHAMA WA KANISA Kabla

hatujaangalia

ulazima

wa

Mkristo

kuwa

mwanachama wa Kanisa linaloonekana, ni muhimu sasa tuone tujiulize swali hili, “Je kuna wokovu nje ya Kanisa?” Kuna wanaoamini kwamba “Yesu Kristo pekee ndiye mwokozi wa ulimwengu, kwamba ni neema yake ambayo hupenya kwenye dini zote na tamaduni, ama kwa kujua kama ilivyo kwa Ukristo, ama kwa kutokujua kama ilivyo katika dini zingine.”84 Wanaamini kwamba mtu hahitaji kuingia katika ushirika wa Kanisa ili kufanyika mkristo kwa sababu wokovu ni tendo la rohoni, na si la mwilini. Wana Refomati wengi huamini kabisa kwamba mtu hawezi kusema kwamba ameokoka huku akiwa nje ya Kanisa (si lazima Kanisa Katoliki) Herman Bavink anakubali kwamba Kanisa linawakumbatia watu wote walio nje ili waingie ndani, na nje ya Kanisa hakuna wokovu. 85 Anasisitiza kwamba “Japokuwa ni kawaida kwa Mungu hutoa faida za Kristo kupitia Neno na

84

Nicholas M. Heal, Y. Church, World and the Christian Life (New York: Cambridge University Press, 2004) 145 85 Bavinck, Herman. Reformed Dogmatics (p. 592). Baker Publishing Group. Kindle Edition.

173

Sakramenti, yeye hafungwi na njia hii na mara chache sana hutoa wokovu nje ya taasisi ya Kanisa.”86 Tukija kwenye upande wa Watu kuwa wanachama wa Kanisa linaloonekana, siku hizi kuna watu wengi ambao hawaoni maana na faida yoyote ya kujiunga na Kanisa, na hivyo wanapookoka wanaamua kukaa nyumbani na kujisomea Biblia kwa ajili ya ukuaji wao. Na wengine huamua kutokujiandikisha katika Kanisa lolote. Tumekubaliana kwamba mtu akiokoka lazima awe mwanachama wa Kanisa. Ningependa kuelezea zaidi. Wakati mtu anapookolewa, anakuwa mwanachama wa mwili wa Kristo (1 Kor. 12:13). Kwa sababu ameunganishwa na Kristo na viungo vingine vya mwili, na kwa hiyo anastahili kuwa mshiriki wa kielelezo cha mwili huo mahali alipo. Kuwa mshirika wa Kanisa ni kujitolea rasmi kwa kikundi kinachotambulika cha waumini ambao wamejiunga pamoja kwa madhumuni maalumu yaliyowekwa na Mungu. Madhumuni haya ni pamoja na kupokea maagizo ya Mungu kupitia Neno la Lake (I Tim.4: 13; 2 Tim. 4: 2), kutumikiana na kujengana kupitia matumizi sahihi ya karama za kiroho (Rum. 12: 3-8; 1 Kor. 12: 431; 1 Pet. 4: 10-11), kushiriki katika ibada (Lk. 22:19; Mdo 2: 3842), na kutangaza injili kwa wale waliopotea (Mt. 28: 18-20). Vile 86

Bavinck, Herman. Reformed Dogmatics (p. 594).

174

vile mtu anapokuwa mshirika wa Kanisa, huamua kujitoa chini ya utunzaji na mamlaka ya wazee wa kibiblia ambao Mungu amewaweka kwa ajili ya kuchunga roho yake. Kwa hiyo, kujiunga na Kanisa la mahali baada ya kuokoka linakuwa ni jambo muhimu na la Kibiblia. Ingawa Maandiko hayana amri ya waziwazi kujiunga na Kanisa la mahali, msingi wa kibiblia wa ushirika wa Kanisa umeenea katika Agano Jipya. Msingi huu wa kibiblia unaweza kuonekana wazi kabisa katika (1) mfano wa Kanisa la kwanza, (2) kuwapo kwa serikali ya Kanisa, (3) utekelezaji wa nidhamu ya Kanisa, na mahimizo la kujengeana. 1. Mfano wa Kanisa la Kwanza Katika Kanisa la kwanza, kuja kwa Kristo kulimaanisha kuja kwa Kanisa. Wazo la kupata wokovu bila kuwa mshirika wa Kanisa la mahali ni jambo geni katika Agano Jipya. Wakati watu walipotubu na kumwamini Kristo, walibatizwa na kuletwa kanisani (Mdo 2:41, 47; 5:14; 16: 5). Hii ilimaanisha kuungana rasmi na waumini wengine katika kutano la mahali hapo na kujitolea kwa mafundisho ya mitume, ushirika, kuumega mkate, na sala (Mdo 2:42). Nyaraka za Agano Jipya ziliandikwa kwa makanisa, ni nyaraka chache tu ambazo ziliandikwa kwa ajili ya watu kwa 175

mfano 1 na 2 Timotheo, Tito, na Filemoni, lakini hata hivyo, watu hawa walikuwa viongozi katika makanisa, hata Filemoni pengine alikuwa kiongozi wa Kanisa. Kama vile Nyaraka za Agano Jipya zinavyodhihirisha,

Bwana

alidhamiria

kwamba

waumini

wanapaswa kujitolea kwenye kutano la Kanisa la mahali. Agano Jipya pia lina ushahidi kwamba kulikuwepo na orodha ya wajane wanaostahili msaada wa kifedha (1 Tim. 5: 9), kuna uwezekano kwamba kulikuwa na orodha ya Washirika ambayo ilikuwa imewekwa;

kwani

watu

walikuwa

wakibatizwa

walikuwa

wanahesabiwa, maana yake wakaingizwa katika ushirika wa Kanisa (Mdo 2: 41, 47; 5:14; 16: 5). Kwa kweli, wakati muumini alipohamia mji mwingine, Kanisa lake mara nyingi liliandika barua ya kumpongeza kwa Kanisa lake jipya (Mdo. 18:27; Rum. 16: 1; Kol. 4:10; taz. 2 Kor. 3:1- 2). Barua hizo hazingeweza kuandika ikiwa waumini hawa hawakujulikana na kuwajibika kwa viongozi wao. Katika kitabu cha Matendo tunaona maneno kama vile "mkutano wote" (Mdo 6: 5), "Kanisa la Yerusalemu" (Mdo 8:1), "wanafunzi" huko Yerusalemu (Mdo 9:26), "katika kila Kanisa" (Mdo 14: 23), "Kanisa lote" (Mdo. 15:22), na "wazee wa Kanisa" huko Efeso (Mdo. 20:17) wote wanapendekeza ushirika wa Kanisa unaotambulika na mipaka iliyoelezewa (angalia pia 1 Kor. 5: 4; 14:23; Ebr. 10:25. Kwa maneno mengine, kujua kwamba "Kanisa 176

lote" limekusanyika inamaanisha kuwa uongozi unafahamu kila mtu ambaye ni mwanachama wa Kanisa hilo. Kwa hivyo tunapata Ushahidi wa wazi kwamba kulikuwa na uandishwaji wa kanisani, na kwamba watu walijitolewa kwa makanisa hayo katika kumtumikia Mungu. Ama kwa hakika tunapokuwa tumejiungamanisha na Kanisa la mahali, ndipo tunapoweza kujitolea kwa bidii kwa ajili ya kazi ya Mungu, na tunaweza kuwajibika ipasavyo. 2. Uwepo wa Serikali ya Kanisa Agano Jipya linaonyesha muundo thabiti wa wingi wa wazee wanaosimamia kila kikundi cha waumini. Wajibu maalumu waliopewa wazee hawa unadhibitisha kikundi kilichofafanuliwa wazi cha washirika wa Kanisa walio chini ya uangalizi wao. Miongoni mwa mambo mengine, watu hawa wacha Mungu waliwajibika kuwachunga watu wa Mungu (Mdo 20:28;1 Pet. 5: 2), kufanya kazi kwa bidii (1 The. 5:12), kuwa na wajibu juu yao (1 The. 5:12; 1 Tim. 5:17), na kulinda roho zao (13:17). Maandiko yanafundisha kwamba wazee watatoa hesabu kwa Mungu kwa ajili ya watu waliopewa kuwa chini yao (Ebr. 13:17; 1 Pet. 5: 3-4). Kwa hivyo basi, majukumu hayo yanahitaji kuwe na ushirika wa kutofautisha na kueleweka katika Kanisa la mahali. Wazee wanaweza kuwachunga watu wao, kuwapa uangalizi, na 177

kutoa hesabu kwa Mungu kwa ustawi wao wa kiroho ikiwa tu wanajua ni akina nani walio katika kundi lao. Huwezi kutoa hesabu

bila

kujua

ni

akina

nani

ambao

umekabidhiwa

kuwachunga. Hii ni wazi kwamba Wazee wa Kanisa hawawajibiki kwa ustawi wa kiroho wa kila mtu anayetembelea Kanisa au wale wanaohudhuria bila kujitoa kwa Kanisa, na badala yake, wana jukumu la kuwachunga wale ambao wamejitiisha chini ya utunzaji na mamlaka ya wazee, na hii inafanywa kupitia ushirika wa Kanisa la mahali. Kama tulivyoeleza huko nyuma kwamba kuna wachungaji wa aina mbili; wazee wafundishao (wachungaji) na wazee watawalao (wazee wa kawaida ambao wanashughulika na utawala wa Kanisa) hawa wote wanawajika kwa wale walio chini yao. Makanisa mengi huweka wazee wawili kwa washirika ishirini na tano (yaani mchungaji mmoja na mzee mmoja). Kwa hivyo tunakubali kwamba Maandiko yanafundisha kwamba waumini kuwa chini ya wazee a wanapaswa kutii wazee wao (Webrania 13:17 inasema, "Watiini viongozi wenu, na nyenyekeni kwao." Swali kwa kila muumini ni, "Je! Viongozi wako ni kina nani?" Yule ambaye amekataa kujiunga na Kanisa la mahali na kukubali kuongozwa na kujikabidhi kwa utunzaji na mamlaka ya wazee hana viongozi. Mambo mengineyo ambayo yanaonesha kwamba kuwa mwanachama wa Kanisa la mahali ni muhimu ni kwamba 178

kujengeana katika imani na kutiana moyo kunaweza kufanyika kwa ufanisi zaidi ikiwa tu utakuwa katika muktadha wa mwili wa ushirika wa Kristo. Kuishi kwa kujitolea kwa Kanisa la mahali kunajumuisha majukumu mengi, ambayo ni pamoja na kuonyesha mfano wa maisha ya Kimungu katika jamii, kutumia karama za kiroho kwa bidii, kufanya huduma, kuchangia kifedha kwa kazi ya huduma, kutoa na kupokea ushauri kwa upole na kwa upendo, na kushiriki kwa uaminifu katika ibada ya ushirika.Kwa hiyo tunahitaji kusisitiza kwamba uanachama wa Kanisa ni muhimu sana, na pia watu wanapaswa kufundishwa kuacha kuyumba kila wakati, bali wajiandikishe kwa usahihi katika Kanisa. Kanisa ambalo lina washirika wanaoeleweka hata wasipokuwa wengi linaweza kutekeleza mipango na makusudio ya kumtukuza Mungu kuliko Kanisa ambalo wanachama wake wanajiandikisha na kuondoka bila kuwajibika kikamilifu. Byron anasema kwamba “Ukristo ni jambo la ushirika, na maisha ya Kikristo yanaweza kutimizwa kikamilifu katika uhusiano na wengine.”87

87

Byron D. Klaus, "The Mission of the Church," in Systematic Theology: A Pentecostal Perspective, ed. Stanley M. Horton (Springfield, MO: Logion Press, 1995), 571.

179

Marejeleo Anabaptism, n.", Oxford English Dictionary (Oxford University Press), December 2012, retrieved 21 January 2013 Byron D. Klaus, "The Mission of the Church," in Systematic Theology: A Pentecostal Perspective, ed. Stanley M. Horton (Springfield, MO: Logion Press, 1995), 571. Battles, Ford Lewis, Analysis of the Institutes of the Christian Religion of John Calvin (Phillipsburg: P & R) Company, 1980) Bavinck, Herman, Reformed Dogmatics, Baker Publishing Group. Kindle Edition. Beeke, R. Joel na Smalley, M. Paul, Reformed Systematic Theology (Illinois: Crossway, 2019) Berkhof, Louis, Systematic Theology (Grand Rapids: Eerdmans 1974) Calvin, John, Institutes of the Christian Religion (Louisville: Westminster John Knox Press, 1960) Cheung, Vincent, Systematic Theology (Zondervan Publishing House, 2010)

180

Cunningham, William, Historical Theology, (Banner of Truth, 1960) Ezamo Murry, An Introduction to Pastoral Care and Counselling (Delhi: ISPCK, 2011) FL Msalaba, Oxford Dictionary la Kanisa la kikristo, 1977. Frame, M. John, Salvation Belongs to Christ: An Introduction to Systematic

Theology

(New

Jersey:

P&R

Publishing

Company, 2006) Frame, M. John, Salvation belongs to the Lord; An Introduction to Systematic

Theology

(New

Jersey:

P&R

Publishing

company, 2006) Grudem, Wayne, Systematic Theology (Grand Rapids: MI: InterVarsity Press, 1994) Henderson, G.D, Why we are Presbyterians (Edinburgh: C.J.Cousland & Sons LTD) Henry G. Weston, Constitution and Polity of the New Testament Church

(Philadelphia:

American

Society, 1895)

181

Baptist

Publication

Henry G. Weston, Constitution and Polity of the New Testament Church

(Philadelphia:

American

Baptist

Publication

Society, 1895) Hodge, Charles, Systematic Theology - Volume III (Grand Rapids: MI: Christian Classics Ethereal Library, 1940) James Leo Garrett, Jr., Systematic Theology: Biblical, Historical, and Evangelical, 2d ed. (BIBAL Press: North Richland Hills, TX, 2001) John, Calvin, Institutes of Christian Religion, (Philadelphia: Westminster Press, 1959) Julie Bowe, et al.., The Presbyterian Handbook (Louisville: Geneva Press 2006) Karl Barth, Church Dogmatics (Edinburgh: T. & T. Clark, 1960) Karl Barth, Protestant Theology in the Nineteenth Century, (London: SCM Press, 2001) Keene, Michael, Introducing Christianity (Louisville: Westminster John Knox Press, 1998) Kung, Hans, The Church (New York, sheed and ward, 1967) Kung, Hans, The Church (New York, sheed and ward, 1967)

182

Lloyd M. Hall & Karl D. Schimpf, Principles and Practices: The Congregational Way of the Churches of the National Association, (Olivet: Congregational Press, 1995) Macarthur J & Mayhue, R (Ed) A Systematic Summary of Biblical Truth: Biblical Doctrine (Wheaton, Illinois: Crossway, 2017) 739 McKim, K. Donald, More Presbyterian Questions, More Presbyterian

Answer:

Exploring

Christian

Faith,

(Louisville: Geneva Press, 2011) Miller, Hays Park, Why I am a Presbyterian (New York: Stratford Press, 1959) Mock, J. Dennis, Church Ministry Administration-Education (Atlanta: BTCP, 1989) Nicholas M. Heal, Y. Church, World and the Christian Life (New York: Cambridge University Press, 2004) Reymond, Robert, A New Systematic Theology, (Nashville: Thomas Nelson Publishers 1998) Robert D. Dale, Pastoral Leadership: A Handbook of Resources for

Effective

Congregational

Abingdon, 1986) 183

Leadership

(Nashville:

Sweet, J. P. M. A Vision for the Church (Edinburgh: T & T Clark, 1997) Williams,

Ernest.

Pneumatology

Swing,

Systematic

Ecclesiology

Theology:

Eschatology

Peter’s

(Springfield:

Gospel Publishing House, 1981) Young Sik Noh, “Equipping Church Leadership to Implement Baptist Congregational Polity for New hope Korean Baptist Church, Lake Forest, California” (D. Min. project, Southern Baptist Theological Seminary, 1997) Gordon R. Lewis and Bruce A. Demarest. Integrative Theology. Volume 3. (Grand Rapids, MI: Zondervan Publishing House, 1994), 260. Michael L. Dusing, "The New Testament Church," in Systematic Theology: A Pentecostal Perspective, ed. Stanley M. Horton (Springfield, MO: Logion Press, 1995), 526.

184

185