Mfululizo wa Mafundisho katika Teolojia Pangilifu NIAMUE LIPI? MAADILI YA KIKRISTO

Dunia nzima inahangaika siku hizi kuhusu suala la maadili. Kwa sasa tunazo changamoto mpya ambazo kanisa halijawahi kuzi

314 153 453KB

Kiswahili Pages 40 Year 2013

Report DMCA / Copyright

DOWNLOAD PDF FILE

Table of contents :
YALIYOMO
NIAMUE LIPI? 4
MAADILI YA KIKRISTO 5
Maadili ni nini? 5
Maadili binafsi 7
Maadili ya kijamii 7
Chanzo cha maadili ya Kikristo 9
Ufunuo wa Kawaida 10
Ufunuo maalum 10
Neno lililo hai 10
Masuala ya Siasa 13
Kanisa na siasa 14
Hoja za wanaataa kujihusisha na siasa 15
Hoja kwa wale wanaokubali kujihusisha na siasa. 15
Maswali la mjadala: 16
Vita katika agano la kale 17
Vita katika agano jipya 17
Kanuni za kutumia kunapotokea vita kati ya wakristo na wasio wakristo 17
Swali la mjadala 18
Umaskini 18
Rushwa 19
Harambee/fund rising 19
Kuomba msaada kwa wasio wakristo 21
Kutangaza fedha zilizotolewa katika harambee au kama ni msaada wa mtu. 21
Mhubiri kuomba fedha ili aje kufanya kwenye mkutano 22
Utasa/Ugumba 23
Chanzo cha utasa/ ugumba 24
Kwa wanaume 24
Kwa wanawake 25
Namna ya kushughulikia ugumba/utasa 26
Ndoa ya Lameki Mwanzo 4:19-25 27
Ndoa ya Ibrahimu Mwanzo 16-17 na 28-30 27
Talaka 29
Nini sababu ya talaka?. 29
Mitazamo mbalimbali kuhusu talaka 32
Nini madhara ya talaka kwa maisha ya wanandoa? 33
Kileo katika maandiko matakatifu 35
Mkristo na kunywa pombe. 36
Misingi ya mkristo kunywa pombe 37
Misingi ya mkristo kutokunywa pombe 38
Recommend Papers

Mfululizo wa Mafundisho katika Teolojia Pangilifu 
NIAMUE LIPI? MAADILI YA KIKRISTO

  • 0 0 0
  • Like this paper and download? You can publish your own PDF file online for free in a few minutes! Sign Up
File loading please wait...
Citation preview

NIAMUE LIPI?

Hakimiliki Daniel John Seni@2013

Unaruhusiwa kunakili, kutumia na kusambaza maneno yaliyo katika kitabu hiki bila kuomba kibali kutoka kwa mwandishi. Lengo la mwandishi si kutumia kitabu hiki kwa mauzo, lakini ni kuufahamisha umma wa wakristo kuhusu masuala ya kimaadili.

Kwa mara ya kwanza kilipigwa chapa na Shekinah Press-Dar es salaam

1

YALIYOMO NIAMUE LIPI? ...................................................................................................4 MAADILI YA KIKRISTO .................................................................................5 Maadili ni nini? ..............................................................................................5 Maadili binafsi................................................................................................7 Maadili ya kijamii ..........................................................................................7 Chanzo cha maadili ya Kikristo...................................................................9 Ufunuo wa Kawaida ...................................................................................10 Ufunuo maalum ...........................................................................................10 Neno lililo hai ...............................................................................................10 Masuala ya Siasa ..........................................................................................13 Kanisa na siasa .............................................................................................14 Hoja za wanaataa kujihusisha na siasa .....................................................15 Hoja kwa wale wanaokubali kujihusisha na siasa. .................................15 Maswali la mjadala: .....................................................................................16 Vita katika agano la kale .............................................................................17 Vita katika agano jipya ...............................................................................17 Kanuni za kutumia kunapotokea vita kati ya wakristo na wasio wakristo.........................................................................................................17 Swali la mjadala ...........................................................................................18 Umaskini .......................................................................................................18 Rushwa ..........................................................................................................19 Harambee/fund rising................................................................................19 Kuomba msaada kwa wasio wakristo ..................................................21 2

Kutangaza fedha zilizotolewa katika harambee au kama ni msaada wa mtu.......................................................................................................21 Mhubiri kuomba fedha ili aje kufanya kwenye mkutano .................22 Utasa/Ugumba ............................................................................................23 Chanzo cha utasa/ ugumba .......................................................................24 Kwa wanaume .............................................................................................24 Kwa wanawake ............................................................................................25 Namna ya kushughulikia ugumba/utasa................................................26 Ndoa ya Lameki Mwanzo 4:19-25 .............................................................27 Ndoa ya Ibrahimu Mwanzo 16-17 na 28-30 .............................................27 Talaka ................................................................................................................29 Nini sababu ya talaka?. ...............................................................................29 Mitazamo mbalimbali kuhusu talaka .......................................................32 Nini madhara ya talaka kwa maisha ya wanandoa? ..............................33 Kileo katika maandiko matakatifu ............................................................35 Mkristo na kunywa pombe. ......................................................................36 Misingi ya mkristo kunywa pombe ....................................................37 Misingi ya mkristo kutokunywa pombe ..............................................38

3

NIAMUE LIPI? Dunia nzima inahangaika siku hizi kuhusu suala la maadili. Kwa sasa tunazo changamoto mpya ambazo kanisa halijawahi kuzipitia hata siku moja. Ingawa Neno linasema kwamba mambo yote yanayotokea yalishawahi kutokea, lakini jinsi yanavyotokea ni kwa kiwango cha juu sana. Watu wengi hawaelewi waamue lipi katika maisha yao. Tunashuhudia masuala ya kimaadili ambayo hatuna hakika kama yanaenda kinyume na mapenzi ya Mungu ingawa yako katika mjadala mkubwa, na hapa kutoa hitimisho ni kwenda kinyume na masuala ya kitaaluma yanayofanyiwa utafiti. Kuna mambo kama vile; uvutaji wa sigara, je Biblia imekataza kuvuta sigara? Kuna masuala kama vile ndoa za jinsi moja, je Biblia imekataza? Kuna masuala kama vile unywaji wa pombe, masuala ya kingono ambayo hayako wazi katika Biblia. Hapa ndipo sasa tunapohitaji kitu kinachoitwa “kujua maadili ya kikristo.” Hivi unajua kwamba siku hizi ni jambo la kawaida kwa mkristo kupokea rushwa? Kwa madai kwamba hiyo ni fedha ya shukrani au ya maji? Je kubadilika kwa jina ndio kumehalalisha suala hili? Hivi pia unajua kwamba siku hizi kijana wa kiume/kike kushiriki ngono na mchumba wake ni jambo la kawaida sana? Hata hivyo mtu atakuuliza kwani ni dhambi? Si nitamuoa mwenyewe? Mambo kama haya yanachanganya jamii kwa ujumla. Tunahitaji kuwa na mwongozo wa kuamua katika mambo yetu.

4

Kitabu hiki ni mwongozo mfupi wa maadili ya Kikristo kwa sehemu fulani. Tutaangalia hoja za msingi kwa ujumla halafu tunaweza kutabanaisha nini tufanye sasa katika maisha yetu ya kila siku. MAADILI YA KIKRISTO Maadili ni nini? Maadili ni “Ni mpangilio wa kanuni bora zinazotawala mwenendo wa kundi maalum la watu.1” Fasili hii inamaanisha kwamba maadili ni: Kwa mujibu wa maana hii kumbe kila kundi la watu lina kanuni zake zinazotawala mwenendo mzima wa kundi hilo. Kwa maana hiyo ni sahihi kusema kuna maadili ya kikristo, maadili ya kiualimu, maadili ya kiuongozi nk. 2 maadili ni “maelekezo yanayofaa ambayo hutolewa kupitia wasilisho fulani.” Ukiangalia vizuri zaidi fasiri hii utagundua kuwa mwandishi anakaza juu ya maelekezo yanayofaa, kwa maana hiyo yale maelekezo yasiyofaa hayo siyo maadili. Watu wengine hutumia neno ‘maadili’ kumaanisha mafundisho kuhusu ‘ukweli na uongo’ uzuri na wema. Wengine wanasema kwamba maadili yanahusika na tabia za watu zilizo nzuri au mbaya. Kulingana na fasili hii tunaweza kupata maana moja ya maadili kwamba ni mpangilio wa kanuni bora ambazo zimelenga kutoa 1 2

Kunhiyop, S.Y. (2008:). African Christian Ethics. Nairobi: Wordalive Publishers Ndallu na wenzake (2014). Kamusi Teule ya Kiswahili Sanifu. NairobiL: EEP

5

maelekezo yanayofaa kwa ajili ya kundi fulani la watu katika jamii husika. Maadili ya kikristo ni mpangilio wa kanuni bora ambazo zimelenga kutoa maelekezo yanayofaa kwa ajili ya wakristo. Wataalam wengine hudai kuwa Maadili ya Kikristo muhtasari wake umetolewa na Wakolosai 3:1-6: "Basi mkiwa mmefufuliwa pamoja na Kristo, yatafuteni yaliyo juu Kristo aliko, ameketi mkon wa kuum wa Mungu. Yafikirini yaliyo juu, siyo yaliyo katika nchi. Kwa maan mlikufa na uhai wenu umefichwa pamoja na Kristo katika Mungu. Kristo atakapofunuliwa, aliye uhai wetu, ndipo na ninyi mtafunuliwa pamoja naye katika utukufu. Basi, vifisheni viungo vyenu vilivyo katika nchi, uasherati, uchafu, tamaa mbaya, mawazo mabaya, na kutamani, ndiyo ibada ya sanamu; kwa ajili ya mambo hayo huja ghadhabu ya Mungu3. Huku zaidi ya orodha ya "kufanya" na ya "kutofanya," Biblia inatupa maelekezo ya kina juu ya namna tunapaswa kuishi. Biblia ndio kila kitu tunahitaji kujua kuhusu jinsi ya kuishi maisha ya Kikristo. Hata hivyo, Biblia haifundishi kila hali ambayo sisi hukumbana nayo katika maisha yetu. Ni jinsi gani sasa tunaweza kuamua hali kama hizo ambazo Biblia haiko wazi kihivyo katika kuamua mambo? Hapa ndipo maamzi ya kikristo yanapokuja sasa kutumika! Sayansi hudai maadili ni "seti ya kanuni za maadili, utafiti wa maadili." Kwa hiyo, maadili ya Kikristo itakuwa kanuni inayotokana na imani ya Kikristo ambayo sisi hutenda. Wakati neno la Mungu linaweza kukosa kuangazia kila hali sisi hupitia 3

www.gotquestions.org/Kiswahili/Maadili-ya-Kikristo.html

6

katika maisha yetu, kanuni zake hutupatia viwango vya kujiendesha katika hali hizo ambapo hamna maelekezo ya wazi. Kwa mfano, Biblia haisemi chochote kwa wazi kuhusu matumizi ya dawa za kulevya, lakini kulingana na kanuni sisi hujifunza kwa njia ya maandiko, tunaweza kujua kwamba ni makosa. Kwani Biblia inatuambia kwamba mwili ni hekalu la Roho Mtakatifu na kwamba tunapaswa kumheshimu Mungu nao (1 Wakorintho 6:19-20). Tunahitaji kujua wazi kwamba neno la Mungu halitoi kila hali ambayo sisi tunakumbana nayo katika maisha yetu, Katika mambo mengi, tunaweza tu kuona ni nini Biblia inasema na kufuata mwendo sahihi kwa kuzingatia kanuni hizo. Katika maswali ya kimaadili ambapo maandiko hayatoi mwelekeo wa wazi, sisi tunapaswa kuangalia kanuni ambayo inaweza kutumika katika hali hiyo. Tunapaswa kuomba juu ya neno lake, na kujiachilia sisi wenyewe kwa Roho wake. Roho atatufundisha na kutuongoza katika Biblia kupata kanuni ambazo sisi tunahitaji kusimama kwayo ili tuweze kuishi kama iwapasavyo Wakristo. Maadili binafsi Haya ni maadili yanayohusu mtu binafsi kwa kile ambacho anatakiwa kukifanya katika jamii. Inahusu hasa na namna mtu anavyotakiwa kufanya kwa upande wake yeye kama yeye. Maadili ya kijamii Maadili haya yanahusu mwenendo mzima katika jamii. Katika nchi kama Tanzania mara nyingi mkazo uko katika maadili ya kijamii kuliko maadili ya kibinafsi. Katika kufunza maadili 7

tunahitaji pia kujua maana ya maneno haya ili ya yatusaidie kujua zaidi mila na desturi za jamii husika. Mara nyingi jamii zetu zinaongozwa na maadili ambayo yametawala kama mila na desturi. Lakini swali la kujiuliza, je mila na desturi hizo ni nzuri? Tusichanganye maana ya maadili na mila na desturi. Tamaduni/Utamaduni : Ni desturi fulani za maisha zilizozoelewa au mila au ustaarabu. Desturi ni kawaida ambazo jamii fulani inaona kuwa ni za lazima au ni jambo la kawaida litendwalo na watu kila siku au ni ile hali ya mazoea. Desturi zinaweza kuwa nzuri au mbaya ili mradi watu wamezoea hivyo! Mila ni mambo yanayofanywa kulingana na chanzo na mazoea ya jamii asili. Mila na desturi mara nyingi sana zinapingana na maadili ya kikristo. Wakati mwingine watu unaweza kuwauliza kwa nini mnafanya hivi? Jibu watakalokwambia ni kwamba kwa sababu tumekuta wazazi wetu wakifanya hivi, yaani mazoea! Mara nyingi mazoea yanaenda kinyume na mwenendo wa kikristo. Wakristo wanaongozwa na neno la Mungu. Lakini hata katika neno la Mungu wakati mwingine watu wanapofasili tofauti baadhi ya vifungu vya Biblia wanaibuka na maana mpya na kupelekea kuwa na maadili tofauti tofauti ya kikristo. Kwa hiyo tunahitaji kujua maana halisi katika kufasili baadhi ya vifungu vya kibiblia ili tuweze kufuata kile ambacho Neno la Mungu limeagiza kuhusu maisha yetu kwa ujumla.

8

Kila jamii ina maadili yake lakini maadili ya kikristo ya pote! Si kwa watu wa sehemu fulani tu. Kwa mfano hapa Tanzania tuna makabila zaidi ya 125 lakini ukiangalia kila kabila lina maadili yake fulani ambayo yanaambatana na mila na desturi (ndani yake kuna miiko kadha wa kadha) ndani yake lakini maadili ya kikristo yanahitaji kutumika katika hali zote katika makabila haya. Tunahitaji pia kujua kwamba Biblia kama mwongozo wetu iliandikwa katika utamaduni wa watu fulani, hata hivyo yapo mambo ya kitamaduni na mambo ambayo Biblia imekaza kama mwongozo kwa kanisa. Jambo fulani inaweza kuliona jamii totauti na jinsi Biblia inavyolijadili. Kwa mfano suala la kuacha mke/mume katika jamii nyingi za kiulimwengu ni jambo la kawaida kabisa lakini Biblia inalijadili kwa upana zaidi. Chanzo cha Maadili ya Kikristo Maadili ya kikristo chanzo chake kikuu Biblia. Biblia ndiyo kiongozi mkuu katika maadili ya kikristo. Jamii inaweza kuliona jambo fulani kuwa ni zuri lakini Biblia ikaliona kuwa ni baya. Kwa mfano suala la kuwa na Boy/Girl Friend na mkawa mnashiriki kimwili ni suala la kawaida kabisa katika jamii yetu kwa leo lakini jambo hili kibilia linahesabika kama uasherati! Nadhani katika jambo hili hakuna mjadala sana kwa sababu hakuna andiko lolote linashadidia dai kama hilo katika maandiko. Kwa hiyo tunahitaji kujua Biblia inasema nini hasa katika jambo fulani kuliko kuangalia jamii inasema nini. Chanzo cha maadili yote ni Mungu mwenyewe. Kwa hiyo Mungu ndiye chanzo kikubwa cha maadili. Mungu ameyafunua 9

maadili hayo kupitia ufunuo wake. Tunajua wazi kwamba Mungu amejifunua kwa mwanadamu kwa namna mbili; ufunuo wa kawaida/ujumla na ufunuo maalum. Ufunuo wa Kawaida Ufunuo wa kawaida ni ule ufunuo ambapo Mungu amejifunua mwenyewe kupitia asili, historia na dhamira za watu. Zab. 19:1 inasema Mbingu zauhubiri utukufu wa Mungu, na anga laitangaza kazi ya mikono yake. Soma pia maandiko haya. Zaburi 147:8-9, Mdo 14:15-17, Rum 2:14-15, Rum 1:21. Nadhani baada ya kusoma mafungu haya umepata kitu pale kwamba Mungu amejifunua kwa watu kwa namna ya jinsi alivyoumba vitu vyote duniani na kwa dhamira ndani ya kila mtu. Ni dhahiri kwamba kila mtu anao ufahamu wa ndani kuhusu Mungu. Hakuna mtu anayeweza kusema kwamba hakumjua Mungu kwa sababu Mungu ameweka ufahamu wake ndani yako. Ufunuo maalum Mungu amejifunua katika ufunuo huu kwa njia ya Neno. Kwa nini ni ufunuo maalum ? Kwa sababu ni njia ya pekee kabisa ambayo Mungu ameitumia ili kujifunua kwa wanadamu, yaani njia hii inaonyesha suluhisho la dhambi za mwanadamu kwa kumtuma Yesu KRISTO kama Neno la Mungu halisi yaani lililo hai na kuwa kuwa mwili (Yn 1:14) “Neno akafanyika mwili, akakaa kwetu” Ufunuo wa Mungu kwa njia ya Neno umegawanyika katika aina mbili: Neno lililo hai Neno lililo hai ni Yesu KRISTO mwenyewe aliyekuja kwa jinsi ya Mwili huku akiwa Neno halisi yaani akiwa Mungu. Yohana 10

1:1,14. “hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu…naye Neno akafanyika mwili akakaa kwetu” 1.1.Neno kama Biblia. Maandiko yote yameandikwa kwa msaada wa Roho Mtakatifu (2Petro1:20-21) yaani wanadamu waliandika yaliyotoka kwa Mungu wakiongozwa na Roho Mtakatifu (2Tim 3:16). Katika kutafuta maarifa katika neno la Mungu tunahitaji kusoma kwa makini, kwa kuzingatia kanuni za kisarufi na tafsiri ya neno la Mungu kwa wakati huo na wakati wa leo. Inashauriwa unaporejelea Biblia uwe na usuli wa Biblia nzima. Huwezi kupata usuli huo bila ya kusoma Biblia nzima. Inashauriwa kusoma Biblia yote ili kujua jambo fulani katika maandiko. Kwa mfano ukisoma katika Agano la Kale peke yake unaweza kujikuta ukakubaliana na hoja kwamba kuoa wake wengi ni sawa kwa sababu Biblia inasema hivyo jambo ambalo linatakiwa liangaliwe katika Biblia nzima. Kwa hiyo kuwa makini kusoma fungu au mstari mmoja katika Biblia na kutoa mahitimisho yake kwa haraka haraka. Hitimisho lolote lile linalohusiana na masuala ya kimaadili lazima yafikiwe kama tu Neno la Mungu limeshadidia suala hilo katika mawanda yake. Kila unaposoma neno la Mungu lazima ukusudie kulitii na wala sio kwa kufuata mawazo yako. Watu wengi sana hufuata mawazo yao badala ya neno la Mungu. Biblia katika Zaburi 119:11 inasema Moyoni mwako nimeliweka Neno lako nisije nikakutenda dhambi. Kwenda kinyume na kile ambacho neno la 11

Mungu linasema inaweza kusababisha wewe kutenda dhambi hivyo unapolisoma uwe na lengo la kutii na kukubali matokeo yoyote yale yatakayotokea. Hata hivyo katika kutatua masuala ya kimaadili tunahitaji kuwa makini zaidi. Kwa mfano katika maadili ya kikristo kutoa mimba ni kitendo kiovu ambacho ni dhambi kwa mtoaji lakini je itakuwaje kama ujauzito huo ukiendelea kuwepo tumboni mwa mama inaweza kupelekea kifo chake? Je atoe mimba ili kutunza mama au mama afe na mtoto abaki? Haya ni baadhi tu ya mambo ambayo yanahitaji kujadiliwa kwa makini sana kabla ya kutolewa maamzi sahihi huku maadili ya kikristo yakizingatiwa.

12

CHANGAMOTO ZA KIMAADILI ZINAZOKABILI UKRISTO SIKU HIZI Kuna changamoto za kimaadili nyingi sana ambazo katika kitabu hiki hatuwezi kuzijadili kila moja. Ni kweli kwamba katika Ukristo kila siku changamoto mpya inazaliwa/inajitokeza. Sasa ni vigumu sana kushughulikia changamoto hizi kwa muda wa siku nne na hata kama tungepata muda wa kutosha si rahisi sana kuzimaliza. Nadhani watu wanaoshughulika na masuala ya ushauri wanajua ni mambo gani wanapambana nayo kila siku. Unaweza kushangaa kila siku watu wanakuja kupokea ushauri lakini kila mtu ana hoja yake ya pekee kabisa. Hivyo basi kwa minajili ya kozi ya Biblia nimechagua baadhi ya changamoto tu. Zifuatazo ni changamoto za kimaadili kwa kanisa la leo Masuala ya Siasa Hatuwezi kujua zaidi kuhusu masuala ya siasa bila kujua kuhusu serikali. Serikali ni watu waliochanguliwa kwa ajili ya kuwaongoza watu wengine. Kunhiyop (khj) 4 anafafanua kuwa kazi kubwa ya serikali ni kuwaadhibu wale ambao wanavunja sheria za nchi fulani. Sheria hizo zinakuwa zimeandaliwa kwa ajili ya kuwaongoza watu wa makundi yote katika nchi. Yaani hakuna cha dini fulani bali watu wa dini zote huunganishwa na kuwa wamoja kwa kutii sheria moja. Serikali imetawaliwa na wanasiasa. 4

Khj-kirefu chake ni kama hapo juu au keshatajwa

13

Wanasiasa ndio wanaoshika nchi kwa sasa, bila siasa hakuna serikali. Sasa kanisa linajikuta likiwa katikati ya siasa na kushindwa cha kufanya. Kanisa na siasa Kanisa wakati mwingine limekuwa katika changamoto katika siasa. Baadhi ya marais wamekuwa wakitangaza hadharani upande wa dini wanaoushadidia. Katika historia kwa mfano, mwaka 1991 raisi wa Zambia Fredrick Chiluba alitangaza kuwa Zambia ni taifa la Kikristo. 5 Huku akitubu kwa ajili ya uovu ambao umewahi kufanywa na watu wa taifa la Zambia. Mfano mwingine ni raisi wa Nigeria, Obasanjo alidai kuokoka baada ya kufungwa kwa makosa ya kijeshi. Katika kipindi cha uchaguzi alitangaza kwamba yeye atakuwa raisi wa Kikristo jambo ambalo lilisababisha wakristo wengi kumpigia kura. Inawezekana kabisa mchungaji ukawa na kanisa halafu ukaingia katika siasa? Je kanisa linaweza kutoa mwongozo wa jinsi ya kuchagua kiongozi anayefaa katika serikali? Nakumbuka Mwaka 2010 kanisa Katoliki liliandika waraka kwa washirika wake kuonyesha aina gani ya kiongozi aweze kuchaguliwa. Je ilikuwa sahihi? Haya ni baadhi ya maswali ya msingi tunapoendelea kujadili suala la siasa katika maadili ya kikristo. Katika maandiko serikali imeelezwa katika mazingira kadha wa kadha. Ukianzia katika agano la Kale wakati wa utawala wa Wafalme inadhihilisha wazi kwamba Mungu alikubali tawala za wanadamu katika mazingira hayo. 5

Paul Freston (2001). Evangelicals and Politics in Asia, Africa and Latin America. Cambridge: Cambridge University press, Uk 158

14

Kuna makundi mawili yanayozungumzia ujihusishaji wa kanisa katika siasa. Kuna kundi la kwanza linadai kuwa ni kanisa linapaswa kujihusisha kikamilifu katika siasa na wale wanaokataa kwamba kanisa halipaswi kujihusisha na siasa. Hoja za Waonaataa Kujihusisha na Siasa Wale wanaoshadidia upande huu wanadai kuwa kanisa limetengwa kabisa na Yesu Kristo na hivyo lenyewe si la ulimwengu huu. Katika Yohana 17:16 “ninyi si wa ulimwengu huu.” Warumi 12:2 inasema “wala msiifuatishe namna ya dunia hii bali mgeuzwe upya nia zenu mpate kujua hakika yaliyo mapenzi ya Mungu yaliyo mema ya kumpendeza na ukamilifu.” Pia katika 2Kor 6:17 inasema “tokeni kati yao mkatengwe nao asema Bwana.” Kulingana na maandiko haya wanaoshadidia upande huu wanadai kuwa kanisa haliwezi kujihusisha na mambo ya siasa wala watumishi wake kuhusika katika siasa kwa sababu wao ni watu tofauti katika ulimwengu huu. Hoja kwa Wale Wanaokubali Kujihusisha na Siasa. Wanaoshadidia upande huu wanadai kuwa kila mkristo lazima awe hai katika mambo ya kiulimwengu. Wanadai kuwa kanisa haliwezi kukaa nje ya ulimwengu kwa sababu linahitaji kuonyesha upendo wa Mungu kwa watu wa ulimwengu. Wanadai kuwa bila kanisa kujihusisha na siasa na pamoja na serikali wakristo hawawezi kuishawishi jamii kubadilika.kwa mfano katika Biblia akina Mordekai na Danieli waliweza kubadilisha serikali zikawa za kumtii Mungu. Kwa upande mwingine wanakaza kwamba kanisa halingii kichwa kichwa tu

15

katika siasa bali linahusika na mambo ya siasa kwa namna ifuatayo: i. ii. iii.

Kuombea serikali na watu wake kwa ujumla Kuikosoa serikali kama inaenda kinyume na maadili yanayotakikana Kushirikiana na serikali katika kuondoa maovu katika nchi

Kambi hii pia ina misingi mingine kutoka katika maandiko ikidai kwamba: i. ii. iii.

Serikali inaanzia kwa Mungu Mwenyewe. Rom 13:1 Serikali hufanya kazi kwa niaba ya Mungu. Rom 13:4 Serikali ipo kwa ajili ya kuhamasisha mazuri kufanyika. Rum. 13:4-5.

Kwa minajili ya kozi hii nakubaliana na kambi pili kwamba kanisa linaweza kujihusisha na siasa. Kanisa lijihusisha katika siasa ili kupata nafasi katika masuala ya kiuchumi, kijamii na kiafya. Kama kanisa likipata nafasi kama hizo ndani ya kanisa basi ufalme wa Mungu hapa duniani utaendelea kuinuliwa zaidi na zaidi. Maswali la mjadala: 1. Je mchungaji anaweza kugombea uongozi katika siasa, kwa mfano ubunge huku akiendelea kuongoza kanisa? Kubali au kataa kwa hoja kuntu. 2. Tunawezaje kukemea viongozi wanaofanya maovu zaidi katika nchi zetu zinazoendelea? Je unaweza kumkabili raisi kama amefanya ubaya? 16

3. Kama tukikubaliana kwamba serikali zote zinatoka kwa Mungu, je unasema nini kuhusu serikali za kijeshi ambazo wakati mwingine huua umati wa raia wasio na lawama? 4. Msimamo wako ni upi kuhusu kanisa na siasa? (hakikisha unatumia maandiko)

VITA NA MAASI Suala la vita na maasi linahitaji mjadala mkubwa sana. Kuna watu wengine wanaodai kwamba mkristo haruhusiwi kujihusisha na vita vya aina yoyote ile isipokuwa vita vya kiroho tu. Lakini wengine wanadai kwamba wakristo wanaweza kwenda kwenye vita ili kusaidia kukomboa katika vita. Vita katika agano la kale 1.1.1.1.Waisrael waliagizwa kuwafukuza Wakanaani kwa vita ( Hes. 33:50-56) 1.1.1.2. Mfalme Sauli aliagizwa kuwaua Waamaleki kwa vita (Isam.15:2-3) 1.1.1.3. Mungu ni mtu wa vita nk Vita katika agano jipya 1.1.1.4.Kununua panga. Luka 22:36-38 1.1.1.5.Ufalme wa Yesu sio wa dunia hii ( Yoh. 18:36) Kanuni za kutumia kunapotokea vita kati ya wakristo na wasio wakristo 1.1.2. kutafuta suluhu kila inapowezekana. Math 26:52 1.1.3. kuhamasisha haki duniani 17

1.1.4. Kuondoa ukabila ndani ya kanisa (Gal 3:28) 1.1.5. Upendo na msamha kwa maadui Swali la mjadala Je mkristo anaweza kwenda katika vita? Kama anaweza kwenda ni kwa namna gani anaweza akatunza amri inayosema usiue? Jadili kwa hoja maridhawa.

MASUALA YA KIUCHUMI Uchumi ni kipengele kingine muhimu katika kanisa la leo. Kuna mambo mengi yanayohusiana na masuala ya kiuchumi ambayo yaliyo mengi yanahitaji mwongozo wa kimaadili. Yafutayo ni baadhi ya mambo hayo: Umaskini Suala la umasikini katika jamii nyingi za kiafrika ni suala tete. Watu wengi wengi wanahangaika kwa sababu ya maisha magumu. Wakati mwingine wanakosa hata mavazi, malazi na hata chakula. Lakini je ni mapenzi ya Mungu watu kuwa maskini ? Nafikiri sio mapenzi ya Mungu bali ni matokeo ya dhambi, na kwa sababu hiyo Mungu aliamua kuweka utaratibu wa namna ya kutoka katika hali ya umasikini. Wakati Mungu alipomuumba mwanadamu alikusudia aishi maisha tele lakini anguko limesababisha matatizo makubwa sana katika jamii zetu. Lakini swali la msingi, je kwa nini nchi nyingi za kiafrika ni maskini sana kuliko za Ulaya ? Je madhara ya anguko yako kwetu tu? Kwa nini hali ya maisha ni tofauti kiasi hicho ? Je matajiri wamewaibia maskini mali zao? Je nini maadili ya kikristo katika jambo hili? 18

Je Mungu amepanga umaskini kwa watumishi wake? kwa nini tunahangaika na umaskini? jadili Rushwa Siku hizi watu hujaribu kupunguza ukali wa neno ‘rushwa’ ‘hongo’ kwa kusema; zawadi, hongera, maji, chai nk. Watu wengi hutoa na kupokea rushwa kwa namna tofauti tofauti. Wengine hudai ni shukrani tu, wengine hudai ni mshahara kwa kazi yangu na wengine hudai ni haki yangu kupokea rushwa. Ili rushwa iitwe rushwa mazingira ya utoaji wake yanahitaji yaangaliwe. Kazi ya rushwa ni kununua haki Biblia imekataza kupokea rushwa ya aina yoyote ile na kwa mazingira yoyote yale. (soma mafungu haya Kumb. 10:16-18, 2Nyak 19:7, Mhub. 7:7, Zab 62:10) nk Swali la mjadala: 1. Je unakubaliana na msemo kwamba “rushwa haiepukiki katika jamii yetu?” Tuchukulie unaendesha gari, unasimamishwa na trafiki na gari lako linaonekana lina kosa dogo tu la rangi kuchubuka. Na asikari anakuomba faini ya shilingi 30.000/= hapo hapo anakwambia ‘hebu naomba unipe ya maji nikuache uende na safari zako, leta 2000/- ‘je utakubali kumpa? Kama utakubali toa hoja madhubuti na kama hautakubali toa hoja kuntu. Harambee Harambee au kwa lugha nyingine ‘changizo’ ina asili yake. Jamii nyingi za kiafrika zina utamaduni wa kusaidiana kwa pamoja kama kazi inahitaji watu wengi. Hiyo nayo tunaweza kusema kuwa ni aina fulani ya harambee. Kila kabila lina aina 19

yake ya kufanya harambee; kwa mfano katika jamii ya wasukuma kuna maneno maalum yanayotumika kuelezea harambee ya aina hiyo kwa mfano ‘lubili’ ‘buyobe’ ‘ikhuma lya busiga’ nk. Kwa Wakulya wanasema’irika.’ Kwa hiyo suala la harambee si suala geni katika jamii nyingi za kiafrika. Watanzania wana msemo ‘umoja ni nguvu, utengano ni udhaifu’ Changizo au kufanya kitu katika hali ya umoja ni jambo la kawaida katika ukristo. Katika biblia kuna sehemu nyingi ambapo changizo liliweza kufanyika kwa ajili ya kuinua huduma fulani iendelee kwa nguvu. a) Musa alifanya harambee kwa ajili ya ujenzi wa hema. Kut. 20-34 b) Mfalme Daudi alifanya harambee kwa ajili ya ujenzi wa hekalu. INyak. 28:12, 19. 29:2-9 c) Nehemia alifanya harambee kwa ajili ya kurekebisha mji wa Yerusalemu. Neh. 1:4-11, 2:1-18; 3:1-5 nk (au soma kitabu chote cha Nehemia) d) Ezra alifanya harambee kwa ajili ya ujenzi wa hekalu. Ezra 2:68-69 e) Hagai naye katika huduma yake alifundisha watu kujitoa kwa ajili ya kazi ya Mungu. Hag. 1:1-14 f) Yesu pia alihudumiwa katika huduma yake na wanawake kadha wa kadha. Luka 8:1-3 g) Mitume nao walihitaji fedha kwa ajili ya kuendeleza huduma yao. Mdo. 4:32-5:11 h) Mtume Paul alifanya changizo kwa ajili ya huduma. I Kor 16:1-3, 2Kor 8:1-24 Swali la msingi ni kwamba kwa nini suala hili liko katika maadili ya kikristo? 20

Kwa kuwa ni muhimu katika huduma ya BWANA kuwa na changizo la watu wengi, au mtu mmoja/supporter, au kanisa maalumu linaweza kukusapoti lakini bado kuna mambo ya kimaadili ambayo yanahitaji kuzingatiwa katika upataji wa huduma hizo. Mambo yafuatayo yanahitaji kuangaliwa kwa makini sana katika huduma Kuomba Msaada kwa Wasio Wakristo Swali ambalo mara nyingi tunapaswa kujiuliza ni je tunaweza kwenda kuomba msaada wa kifedha labda kwa ajili ya kujenga kanisa kwa watu wasio waamini? Je mtu ambaye pengine tunajua wazi kwamba labda amepata fedha kwa njia ya rushwa/au jambo lolote lile baya, je tunaweza kuzipokea fedha kama hizo? Je tunaweza kuwaendea Waislamu matajiri na kuwaomba wachangie huduma zetu? Maswali haya yote yanahitaji uchunguzi wa hali ya juu sana. Wengi wanaoshadidia upande wa kwamba inawezekana kuchukua fedha kwa wasio waamini wanadai kwamba fedha walizo nazo watu sio za kwao. Wanatoa mfano wa Ezra na Nehemia waliopokea msaada wa mfalme wa Babel ambaye alikuwa mwabudu miungu. Hili ndilo suala la kimaadili katika harambee! Kutangaza fedha zilizotolewa katika harambee au kama ni msaada wa mtu. Hii inatokea hasa kama katika changizo umeita MC anayejulikana kabisa. Anahamasisha watu na watu wanatoa fedha nyingi. Je fedha hizo zitangazwe?

21

Mhubiri kuomba fedha ili aje kufanya kwenye mkutano Hili nalo siku hizi linasumbua sana jamii za Kikristo. Watumishi mbalimbali wanaomba fedha kabla ya kufika katika mkutano wa Injili. Waimbaji wengi wa injili siku hizi bila kuweka chochote kwenye akaunti yake hawezi kwenda kwenye mkutano wa Injili. Je hayo ni maadili ya Kikristo. Je ni maadili ya kikristo kutoa namba zako za akaunti za benki kwa umati wa watu? Je ni sawa kwa mtu akitaka kuombewa atoe kwanza fedha kwa ajili ya huduma hiyo? Haya ni baadhi ya maswali ya msingi ambayo tunahitaji kujiuliza na kuyatolea majibu sahihi. Watumishi wa Mungu tunahitaji kuwa makini katika masuala haya ya kimaadili. Lakini kwa ujumla tunaweza kusema kwamba, mambo yafuatayo katika masuala ya kifedha katika huduma yanapaswa yafuatwe: Angalia nia ya mtoaji ni ipi? Kama ni ya kisiasa zaidi au anataka kumteka mchungaji/mwinjilisti au anataka kupata sifa fulani ndani ya kanisa hilo? Usipokee fedha ovyo ovyo maana ni hatari sana! Kwa wewe unayepokea lazima uwe mwaminifu na muwazi. Kama umepewa fedha kwa ajili ya kujenga kanisa unapaswa kujenga kanisa tu. Kuna wachungaji wengi wakishapata misaada ya aina hiyo tayari wanaibadilishia matumizi, wananunua magari nk. Jambo hili ni hatari sana. Kuwepo na mrejesho kwa kile ulichotumia. Ni vizuri zaidi kuelezea vizuri kile ambacho umetumia. Ikiwezekana andika kila kitu, itakusaidia sana maana kuna wafadhili wengine wanataka kujua kila kitu. Baada ya kuangalia mambo ambayo ni ya muhimu; epuka mambo yafuatayo: 22

• •



Epuka kupotosha ukweli. Kama una mradi utagharimu shilingi laki tano sema laki tano. Epuka kuwashawishi watu kutoa hata pale wasipotaka kutoa. Kuna watu makanisani wanatoa vitu huku wakinugh’nuka mioyoni mwao Epuka kuwa ombaomba/ Mungu hasemi kwamba tuombe kwa watu.

MASUALA YA FAMILIA NA NDOA Suala la familia na ndoa ni suala ambao linahitaji kujadiliwa kwa undani zaidi. Ndoa ni taasisi pekee ambayo Mungu huitumia kuendeleza uumbaji wake hapa duniani. Lakini wakati mwingine ndoa hizi hizi zinakuwa na changamoto nyingi ambazo zinapelekea mambo fulani fulani ambayo sio mazuri kutokea katika maisha ya kila siku. Katika sehemu ya familia na ndoa tutaangalia masuala ya utasa, mitara, talaka na mahusiano. Utasa/Ugumba Utasa katika nchi nyingi za kiafrika ni suala mtambuka. Kwa maana ya kwamba waafrika wanaamini kwamba watoto ndio urithi wa pekee kabisa. Sasa inapotokea kwamba kuna tatizo la utasa mambo haya yanakuwa ni shida kubwa. Watu wengi wametoa talaka kwa sababu ya kutokupata watoto kwa wake zao wa kwanza. Watu wengi wanaamini kwamba ndoa bila kuwa na mtoto bado haijawa ndoa sahihi bali ni ndoa nusu. Tunahitaji kujifunza na kujua mapenzi ya Mungu nini katika maisha ya ndoa zetu. Kama tukikaza kwamba lazima tuwe na watoto je inapotokea hakuna watoto inakuwa ni laana au? Watu wengi 23

wanatembea usiku na mchana kwenda kwa waganga wa kienyeji kwa ajili ya kutafuta watoto. Lazima tuwe makini katika jambo hili. Kuna wachungaji wengi ambao wamejikita katika huduma ya kuombea tu watu wasio na watoto huku wakikaza kwamba mtu asiyekuwa na watoto ana laana kutoka kwa Mungu na yeye anaondoa laana hizo. Chanzo cha utasa/ ugumba Kabla ya kwenda mbali zaidi hebu tuangalie maana ya utasa na ugumba. Kwa mujibu wa kamusi ya Kiswahili sanifu (2004:398)6 tasa ni “kiumbe chochote cha kike kisichoweza kuzaa” kwa hiyo tunapozungumzia tasa tunamaanisha mwanamke asiyeweza kuzaa. Neno ‘mgumba7’ maana yake ni “mtu aliyefikia umri wa kuzaa lakini akawa hajazaa wala kupata au kutia mimba” kwa hiyo neno ugumba ni kwa watu wote. Sasa tuangalie kwa ufupi sababu za kuwa mgumba kwa:Kwa wanaume • Uhanithi-huyu ni mwanaume asiyekuwa na nguvu za kiume kabisa, yaani ni dhaifu. Uume wake hauwezi kusimama sawasawa na hivyo hawezi kufanya mapenzi na mke wake. tatizo hili husababishwa na masuala ya kiafya,kwa mfano kupiga punyeto kwa muda mrefu na hata masuala ya kisaikolojia. Kama mtu akiwa na tatizo hili tunawashauri kwenda kupima hospital ili kubaini chanzo cha tatizo. 6

TUKI (2004). kamusi ya Kiswahili sanifu. Nairobi: Oxford khj

7

24

Swali: wewe kama mchungaji ukiletewa suala la mtu ni kuwa hanithi utafanyaje ili uweze kunusuru ndoa yao? Utawashauri vipi? •

Tatizo katika kutoa mbegu- wanaume wengine hawawezi kuwapa wake zao uja uzito kwa sababu shahawa/mbezi zao haziwezi kufikia yai la mtoto. Yaani katika kutoa mbegu/shahawa hazina spidi ya kufikia yai. • Kukosekana kwa mbegu katika shahawa-wanaume wengine hawana mbegu katika shahawa zao. Wanamwaga shahawa kama kawaida lakini hazina mbegu. Hili nalo ni tatizo kubwa. • Kuharibika kwa mbegu za kiume-wakati mwingine mbegu za kiume zinaharibika na kufa kabisa. Wanaume wengi wanaopenda kuvaa chupi zinazowabana hupatwa na tatizo hili mapema sana. Maana kwa kawaida mbegu haziwezi kukaa katika joto kali. • Matatizo ya kiroho, wakati mwingine masuala ya kiroho yanaweza kusababisha kuwa mgumba mwanaume tafuta sababu za kiroho za ugumba katika maandiko matakatifu kisha yaelezee kwa undani na chanzo cha matatizo hayo. Kwa wanawake Wanawake wengi wanakuwa matasa kwa sababu zifuatazo • Tatizo la homoni za uzazi • Tatizo la tumbo la uzazi/hakuna kizazi • Maambukizi katika uke • Chango la kike • Tatizo kiroho

25

Namna ya kushughulikia ugumba/utasa Kila kundi la watu lina namna yake ya kutatua tatizo hili kubwa katika jamii. Jamii nyingi zisizoamini hukimbilia kwa waganga wa kienyeji na kujikuta wanagawa ngono kwa kudanganywa ili wapate watoto. Wanaume wengine wanaambiwa mashariti magumu. Kwa mfano jamaa mmoja alienda kwa mganga wa kienyeji akaambiwa kwamba alale na mama yake mzazi ndipo kizazi cha mke wake kitafunguka. Kwa ushauri wangu ni bora:• Kumwomba Mungu sana na kutambua nini hasa kusudi la ndoa katika maisha yenu. • Kwenda kuwaona wataalamu wa afya ili waone suala hili kitabibu zaidi. Na kama hakuna tatizo la kitabibu basi ni vizuri kusubiri mpango wa Mungu • Kujifunza namna ya kujua siku ambazo mwanamke anaweza kuchukua mimba au la • Kujua kusudi la Mungu katika uumbaji. Kila kitu kinachokuja duniani kinakuwa na kusudi la Mungu katika maisha ya mwanadamu. Kwa mtu aliyeokoka si jambo la kulazimisha upate mtoto wakati Mungu hajaamua kufanya hivyo. Usije ukachanganyikiwa na kuanza kukimbilia maombezi kila kukicha Mitara (ndoa za wake wengi Waafrika wengi hawaoni kwamba ni jambo geni kuingia katika ndoa za mitara. Hii ni kutokana na ukweli kwamba mwanaume wa kiafrika anaweza kuoa mwanamke mwingine wakati wowote ule bila shida. Hili nalo ni tatizo kwa wakristo wengi. Nakumbuka 26

kanisa moja niliwahi kusali nilipokuwa kijana mdogo lililoitwa Last Church/Batola mhali (kwa kisukuma) lilikuwa linahalalisha kabisa kuoa wake zaidi ya mmoja. Mwinjilisti kanisa hilo alikuwa na wake wawili Ada na Sila. Kuna siku waligombana sana hao wake zake na kubebeana mapanga na hapo hapo ndipo kikawa chanzo cha familia yetu kuhama kanisa hilo!! Mpango wa Mungu haikuwa kwamba mwanadamu aweze kuoa wake wengi, kwani alipomuumba Adamu alimwomba na Hawa nao walikuwa wawili tu. Hata hivyo kwa sababu ya anguko la mwanadamu, kwa sababu ya dhambi mwanadamu alijitwalia wake zaidi kwa kadri alivyotaka. Hebu tuangalie ndoa za mitara katika biblia na madhara yake. Ndoa ya Lameki Mwanzo 4:19-25 Huyu ndiye mtu wa kwanza kabisa kujitwalia wake wawili. Ukisoma mistari hiyo utaona kwamba huyu jamaa alikuwa roho ya kisasi kama ya Kaini. Kwa hiyo moja kwa moja makosa yake yanaelekezwa kwa uasi aliokuwa nao. Matokeo yake yeye mwenyewe anakiri kwamba anaweza kulipizwa kisasi na Mungu. Hapa tunaona kwamba madhara yake ilikuwa kwenda kinyume na Mungu.ukoo wa Kaini mara nyingi imeonekana katika maandiko kwamba ni ukoo wa kigaidi uliokataa kwenda katika sheria ya Mungu. Ndoa ya Ibrahimu Mwanzo 16-17 na 28-30 Ni dhahiri kwamba Ibrahimu alizaliwa katika familia yenye kushika msimamo wa ndoa za wake wengi(20:12). Katika ndoa yao Ibrahimu alichelewa sana kupata mtoto wa ahadi, lakini mke 27

wake Sarah,kwa sababu tayari ndani yake yalikuwepo mawazo ya kuwa na wake wengi kwa mume wake,alimshauri amchukue Hajiri. Hapa ndipo chanzo cha matatizo ya ndoa hii. Katika agano jipya hakuna mahali popote ambapo tunakuta kuna mtu alikuwa na wake zaidi ya mmoja. Lakini tukiangalia maandiko inaonekana kwamba kuna waliokuwa na wake zaidi ya mmoja. Hebu soma mafungu haya (I Kor 5:1-9) hapa tunaona jamaa ambaye alikuwa ni mzinzi kiasi cha kulala na mke wa baba yake, je wewe unadhani ni mama yake mzazi? Labda nafikiri kwamba huyu baba yake alikuwa hawara/nyumba ndogo. Sio hapo ukisoma katika I Tim 3:1ff utaona sifa za asikofu na shemasi kwamba wawe waume wa mke mmoja. Hii inatudhihilishia kwamba kulikupo na watu ndani ya kanisa wenye wake zaidi ya mmoja. Maandiko hakuna sehemu ambapo yameruhusu mwanaume kuoa wake wengi au mwanamke aolewe na wanaume wengi, kinachofanywa na binadamu ni ugumu wa mioyo yao. Wengine katika kipindi hiki kwa sababu ya changamoto za ndoa wanaamua kuwa na nyumba ndogo ili kunusuru maisha yao. Hii ni hatari sana, kwani kufanya hivyo ni kwenda kinyume na neno la Mungu. Kwa kawaida hakuna mtu anayeweza kugawa upendo wake katika sehemu mbili. Na ndiyo maana ndoa za wake wengi zinakuwa na matatizo mengi sana. Unakuta wanawake hao hawaelewani kila siku. Kuna mifano mingi katika agano la kale ambayo inaonyesha madhara ya ndoa za mitara. Ushauri wangu ni kwamba ni lazima tufundishe watu wafuate utaratibu wa Mungu kwamba ndoa ni ya mke mmoja. Hakuna sababu ya kuoa 28

mke wa pili. Na kuoa mke wa pili ni kwenda kinyume na neno la Mungu. Swali: je kama kanisani kwako kuna waumini ambao kabla ya kuokoka walikuwa na wake zaidi ya mmoja, utawashauri wawaache au utafanyaje? Jadili kwa mapana huku ukizingatia maadili ya kikiristo ni pamoja na hekima ya Roho Mtakatifu kufanya kazi

Wewe kama mchungaji umeitwa kwenda kumbatiza mtu aliye na wak utafanyaje?

Talaka Suala la talaka ni suala nyeti sana katika kanisa. Watumishi wengi wanahangaika kutatua masuala yanayohusiana na talaka. Katika kipindi hiki suala la talaka ni jambo la kawaida miongoni mwa wapendwa. Hasa kunapokuwa na tatizo ambalo wanandoa wamekosana na jamii pamoja na kanisa inaliona wazi basi talaka hutolewa. Nini sababu ya talaka? Kwa ujumla kuna sababu nyingi ambazo zinasababisha talaka kutolewa. Nitajaribu kutaja baadhi ya hayo matatizo kama ifuatavyo;• Kukosekana kwa watoto miongoni mwa wanandoa ni sababu kwa Waafrika. Na hasa lawama zinapelekwa kwa wanawake 29

• • • •









Kusalitiana kimapenzi, yaani kama kuna mmoja anatoka nje ya ndoa basi yule mwingine anaamua kuachana naye Kulazimishwa na wazazi wa upande mmoja kuachana kwa sababu za kimila na kitamaduni Mmojawapo wa wanandoa hao kupatwa na magonjwa ya kuambukizwa hasa UKIMWI Sababu za kiuchumi katika wanandoa. Wengine wanapooana huonekana wakiwa na mali mara baada ya kuisha mali hizo huachana mara moja Huko Ulaya wengine wanaona kwamba kama mtu amemchoka mwenzake anaamua kuachana naye tu bila hata sababu za msingi Ugomvi wa mara kwa mara ndani ya nyumba hupekea talaka kwa wanandoa hao. Ugomvi huo unaweza kusababishwa na tabia sugu za wanandoa hao kutokubadilika ili kuendana pamoja. Matumizi ya mabavu ndani ya nyumba husababisha talaka miongoni mwa wanandoa. Kwa mfano kwa waafrika walio wengi kumpiga mwanamke ni jambo la kawaida sana, lakini kuna wakati inafikia hali ngumu ndipo mwanamke huamua kuondoka na kudai talaka. Ni mara chache kukuta familia mwanaume anapigwa na mwanamke japo kuna familia za namna hii nyingi. Kunyimana kitandani. Nazungumzia hapa ile hali ya kumnyima mwenzi tendo la unyumba hupelekea talaka miongoni mwa wanandoa. Hii inatokea pale ambapo miongoni mwa wanandoa anatoa tendo la ndoa kama silaha

30









ya kumwadhibu mume/mke wake. jambo hili huvunja ndoa nyingi kila siku. Wivu wa kimapenzi huvunja ndoa nyingi, unaweza kukuta miongoni mwa wanandoa anakuwa na wivu kiasi kwamba hataki kumwona mwenzi wake anaongea na mtu mwingine. Mfano unakuta baba akimwona mke wake ana mtu mwingine wa kiume basi moja kwa moja anasema kwamba huyu anakutongoza na hivyo kudai talaka kwa haraka sana. Ndoa za mitara huvunja ndoa ya kwanza. Mara nyingine kwa wapenzi ambao hawakukusudia kuwa ndoa yao itakuwa ya wake wengi wakiona kwamba kuna mwanamke mwingine ameletwa ndani mara moja hudai talaka. Ulevi wa kupindukia, hili mara nyingi linatokea hasa ikiwa mmojawapo wa wanandoa hao akiwa mlevi kupindukia na mwingine hana tabia za ulevi ikifikia hatua fulani mmoja anachoka kumvumilia mwenzake kwa ajili ya ulevi wake basi huamua kuvunja ndoa Maendeleo ya sayansi na teknolojia yanasababisha ndoa nyingi kuvunjika. Kwa mfano matumizi mabaya ya simu yanavunja ndoa za watu. Nakumbuka kijana mmoja alikosea akatuma massage ya mapenzi katika simu ya mke wa mtu, ujumbe huo ulileta mtafaruku ndani ya ndoa hiyo. Pia matumizi ya mitandao ya kijamii kama vile facebook na twitter yanasababisha kuvunjika ndoa. Pale ambapo mmoja wa wanandoa anasahau ku-log out kama alikuwa ameingia mtandaoni na mtu mwingine mbaya akiingia kwenye akaunti yake na kuweka picha mbaya itampa shida kubwa sana.

31



Watoto wa kambo huvunja baadhi ya ndoa za watu. Hii inatokea pale ambao mmoja wa wanandoa hao alikuwa na mtoto wakati wa kuolewa, watoto wa aina hiyo wakati mwingine huleta matatizo makubwa ya kuchonganisha wanandoa hao Hizi ni sababu chache tu miongoni mwa sababu nyingi zinazosababisha kuvunjika kwa ndoa. Na kumbuka kwamba kila ndoa ina sababu yake ya pekee ambayo haifanani na nyingine inayopelekea kuvunjika kwa ndoa hiyo. Fungu la kwanza ambalo linazungumza juu ya talaka kwa mara ya kwanza ni katika Kumbukumbu la Torati 24:1-5 mahali ambapo tunaona kwamba Musa aliwaelekeza watu namna ambavyo wanaweza kuwapa talaka wake zao. Lakini jambo hili Yesu alisema kwamba sababu za Musa kuruhusu talaka ilikuwa ni ugumu wa mioyo ya watu Mitazamo Mbalimbali Kuhusu Talaka • Kuna wanaosema hakuna kutoa talaka kabisa katika maisha ya mwanadamu. Soma Warumi 7:2-3,I kor 7:39, Mal 2:16 • Kuna wanaosema kuwa ni ruksa kutoa talaka lakini usioe tena. Hawa nao wanasimama na mafungu mbalimbali, mfano. Math 19:9 wanafafanua kwa namna ya pekee sana • Kuna wale wanakubali kwamba kama mwanamke/mwanaume umemkamatisha kwenye uzinzi unaachana naye mara moja. Nao wanasimama na fungu hili la Math 19:9 na Kumb 24:1-5 wakifasiri neno OVU kuwa ni uzinzi 32

Kila kundi la watu wana msimamo wao juu ya suala hili lakini cha kuzingatia ni kwamba tunahitaji kumwomba Mungu hekima ya pekee katika kujadili suala la talaka makanisani huku tukijua mambo yafuatayo: • Ndoa ya kikristo imekusudiwa kuwa ni ya milele. Mal 2:16 • Kuna wakati inaweza kutokea talaka. Math 19:8 • Talaka ni hatari sana kwa wanandoa • Hatuwezi kujumuisha moja kwa moja masuala ya talaka lazima yaangaliwe kwa undani zaidi • Kuna matumaini ya ziada baada ya talaka na kuoa tena, kwa maana ya kwamba hilo si suluhisho la maisha ya mwanadamu • Kabla ya kufanya uamuzi wa haraka wa kuvunja ndoa yako, fikiria. Mara nyingi talaka haimalizi mahangaiko ya maisha. Badala yake, inatatua tatizo moja, na kutokeza lingine. Katika kitabu chake, The Good Enough Teen, Dakt. Brad Sachs anaonya hivi: “Wenzi wa ndoa wanaotalikiana huwazia kwamba kufanya hivyo kutafaa kabisa, yaani, talaka yao itawaondolea kabisa huzuni na ugomvi mkali, na badala yake wapate utulivu mwanana. Lakini kutarajia hilo ni sawa tu na kutarajia kuwa na ndoa kamilifu, haiwezekani.” Hivyo, ni muhimu kuwa na habari kamili na kuona talaka kihalisi. • Talaka huweka majeraha yasiyokoma mpaka kaburini Nini madhara ya talaka kwa maisha ya wanandoa? • Huharibu afya ya kiroho • Huharibu afya ya kimwili • Kuchanganyikiwa miongoni mwa wanandoa 33

• •

Watoto kukosa malezi ya wazazi wote wawili Matatizo ya kifedha. Daniella, anayeishi Italia, alikuwa katika ndoa kwa miaka 12 alipogundua kwamba mume wake alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na mfanyakazi mwenzake. Daniella anasema hivi: “Nilipogundua jambo hilo, mwanamke huyo alikuwa na mimba ya miezi sita.” • Kuna matatizo ya kifedha. hebu ona mfamo huu baada ya kutengana kwa muda, Daniella aliamua kumtaliki mume wake. “Nilijaribu kuiokoa ndoa yangu,” anasema, “lakini mume wangu hakuacha kuwa na uhusiano nje ya ndoa.” Daniella anahisi kwamba alifanya uamuzi unaofaa. Lakini anasema hivi: “Mara tu tulipotengana, hali yangu ya kiuchumi ikawa mbaya. Nyakati nyingine nilikosa hata mlo wa jioni. Nilikunywa tu maziwa.”8

Swali:1 je kama miongoni mwa washirika wako amepatikana na ugonjwa wa UKIMWI ilhali mwenzi wake hana, utaamuaje suala la kuzuia talaka isitolewe? swali 2. Hebu tuchukulie kwamba umemkamata mume/mke wako ana kwa ana (ready handed) akiwa katika kifua cha kahaba utavumilia kuishi naye au utampa talaka? Swali 3.wewe kama mwanadamu umewahi kufumaniwa? Ulimalizaje mgogoro huo nyumbani kwako? MATUMIZI YA VILEO

8

http://www.jw.org/sw/machapisho/magazeti/g201002/mambo-manne-kuhusutalaka/

34

Matumizi ya vileo ni jambo la kawaida kwa watu wengi, wakristo na wasio wakristo. Ni jambo ambalo ni la muda mrefu hata kabla ya histori ya binadamu kuanza kurekodiwa katika maandishi. Kinaachofanya unywaji wa pombe/divai uwe ni wa kawaida ni kwa namna ambavyo inatengenezwa. Pombe/divai nyingi inatengenezwa kutokana na nafaka, kwa mfano mtama huweza kutengeneza aina mbalimbali ya vileo. Kwa mfano kwa wasukuma mtama huweza kutengeneza pombe iitwayo ‘gongo’ au ‘mapuya’ au ‘mataputapu’ nk. Pia nafaka za mahindi hutengeneza pombe. Lakini zamani za siku hizi nimesikia kwamba watu hutengeneza hata pombe kwa kutumia kinyesi cha wanyama na wanadamu. Hii ni katika kuhakikisha kwamba wanaongeza ukali katika vileo hivyo. Maendeleo ya viwanda yamehamasisha unywaji wa pombe za kawaida na pombe kali kwa kutengeneza vileo hivyo kwa njia ya kisasa kabisa. Hapa Tanzania, kampuni ya bia inatengeneza aina mbalimbali ya bia kwa mfano Safari lagar, Serengeti larga, tusker lagar. Bia hizi zote utafiti unaonyesha kwamba sio kali sana. lakini nimewahi shuhudia mtu amekunywa bia mbili aina ya ‘Ze bingwa’ na kuishiwa nguvu kabisa. Kuna vinywaji vingine vinatoka nje ya nchi kama vile whisky ambayo ina 50% ya kileo. Daniel Jakes nk. Hata konyaji ni kileo kikali sana . Kileo katika maandiko matakatifu Kileo kinaonekana kutajwa katika maandiko kwa namna mbalimbali na kuonyesha umuhimu wake kwa watumiaji.

35



Divai inatajwa kama dawa ya tumbo kwa anayesumbuliwa na tumbo na kwa ushauri wa daktari anaweza kutumia. I Tim 5:23 • Yesu alitengeneza divai kwenye arusi ya kana ya Galilaya na watu wakanywa na kulewa. Yoh 2:1-11 • Divai inatumika kuponya vidonda/majeraha ya vidonda. Lk 10:31 • Divai inasaidia kupoteza mawazo ya umasikini. Mith 31:7 • Divai hufurahisha moyo wa mwanadamu. Zaburi 104:15 • Divai ilitumika katika sadaka kwa Bwana. Hes. 15:5-7 Japokuwa divai/pombe imeongelewa kwa mlengo chanya katika mafungu haya lakini pia tukumbuke kwamba kwa upande mwingine imeongelewa kwa mlengo hasi. Yaani kwamba ina madhara kwa maisha ya wanadamu. Mfano mafungu haya yanaonyesha hivyo, Kumb 21:20 IKor 6:7-9 nk Mkristo na kunywa pombe. Swali hili limekuwa ni swali la siku nyingi na kila siku wakristo wengi wanapingana katika hili. Kwa baadhi ya madhehebu ya Kikristo yanaruhusu kunywa pombe ila usilewe tu. Lakini kwa upande mwingine wengine wanasema kwamba kunywa pombe ni dhambi kubwa mbele za Bwana. Huku wengine wakidai kwamba kunywa pombe ni tabia mbaya tu ila siyo dhambi. Hebu tujaribu kuangalia hoja za kila upande unavyodai.

36

Misingi ya mkristo kunywa pombe Biblia haikatazi unywaji wa pombe bali inakataza ulevi wa pombe. Ndiyo maana katika I Tim 3:3 ‘si mtu wa kuzoelea ulevi’ kuzoelea ni kitenzi cha ‘kuzoea’ maana yake kuendekeza tabia ya kufanya hivyo. Na hapa Paul anatoa sifa za kiongozi wa kiroho. Kumbe wakiristo wengine wasio viongozi wanaweza kunywa pombe. • Biblia imeagiza mkristo aweze kujitawala sio kuacha kunywa pombe, hivyo basi kama mkristo anaweza kunywa bia moja na akalala bila kumbughudhi mtu basi anaweza kunywa ili mradi tu atawale hali yake. • Biblia inatambua kwamba pombe inaweza kutumika kama dawa, basi si mbaya kunywa pombe kwa ajili ya afya9. • Si kila mtu anayekunywa pombe anakuwa mlevi. Na biblia imekataza ulevi sio unywaji wa pombe. • Kukataa kunywa pombe unaweza kujitenga na jamii. Kwa mfano kuna jamii zingine kama ukienda kwenye sherehe lazima uzimue kidogo ndipo uonekane unashirikiana nao.

9

Mtu mmoja anaitwa nabii Tito (Nabii wa pombe- a prophet of beer) ni nabii anayehubiri watu kunywa pombe akitumia maandiko matakatifu ya Biblia na kudai kuwa Biblia inaruhusu kunywa pombe.Hufanya mahubiri yake maeneo ya posta mpya hapa jijini Dar es Salaam. Nabii Titto yeye anadai kuwa ameoteshwa na mungu kuwa watu wanywe pombe kwani ni tiba sahihi tosha kwa magonjwa mbalimbali na si pombe tu mpaka sigara. Dini yake aliyoianzisha inarushu watu kuoa wake wengi,kuvuta sigara na kunywa pombe.Huyu ndiye nabii Tito (a prophet of beer)

37





Unapokunywa pombe unatuliza akili yako na hivyo kukufanya siku nyingine ukitaka kufanya kazi ufanye kwa bidii kubwa Suala la kunywa pombe halihusiani na masuala ya uzima wa milele. Kwa kuwa mtu amempokea Yesu kuwa Bwana na Mwokozi wa maisha yake basi amehesabiwa haki na ana uzima wa milele. Hivyo si dhambi kunywa pombe.

Misingi ya mkristo kutokunywa pombe • Biblia inaonya juu ya matokeo ya matumizi ya pombe • Mtu aliyeweka nadhiri haruhusiwi kunywa kileo. Hes 6:2-3 • Makuhani hawakuruhusiwa kunywa vileo. LAW 10:9 • Wafalme hawakupaswa kunywa vileo katika falme zao. MIT 31:4 • Kileo hupotosha watumishi wa Mungu wanaojaribu kunywa. ISA 28:7 • Si vizuri mtu aliyekusudiwa kuwa mkuu kutumia kileo. LK 1:15 • Kunywa pombe kwa mkristo ni kuonyesha na kuendelea kuishi maisha ya zamani. 1PET 4:3-4 • Pombe huleta magomvi katika nyumba za watu • Ulevi huua idadi kubwa ya watu. Nadhani hata wewe umeshuhudia watu ambao wamekufa kwa sababu ya pombe • Pombe huvunja ndoa nyingi sana • Hakuna anayeanza kunywa pombe na kusema kwamba hatakuwa mlevi bali hustukia mlevi tu

38



Matokeo ya ulevi ni mabaya mno. Mfano kwa habari ya Lutu kulala na watoto wke wakati wa ulevi na Nuhu wakati wa ulevi alilaani mjukuu wake Kanaani. • Kila mlevi unayemwona alianza kama mnywaji halafu polepole akawa mlevi mkubwa. Ushauri Kuhusu Pombe Ukizingatia vizuri neno la Mungu, hakuna mstari wa Biblia ambao unazuia moja kwa moja kwa mtu kunywa pombe. Lakin katika hali ya uzoefu wa kibinadamu na maadili ya kimaadili na kwa kuwa hoja zinazopinga kunywa pombe ni nyingi sana, kwa ushauri wangu usijaribu kunywa pombe hata siku moja. Usijaribu hata kutaka kujua ladha yake ikoje. Achana na misemo ya wataalam soda ni hatari kuliko bia kwa afya !! Eti uache kunywa soda ugeukie kunywa bia ni hatari sana.

Mch: Daniel John Seni S.L.P 32807/[email protected]/ 0769080629 Dar es salaam Ni mchungaji wa kanisa la Shekinah Presbyterian Church Tanzania

39