Mfululizo wa Mafundisho katika Teolojia Pangilifu ANTHROPOLOJIA : MAFUNDISHO YA KIKRISTO KUHUSU MWANADAMU [1, 1 ed.] 9789976572698

Kitabu hiki ni mfululizo wa mafundisho ya Kikristo yaliyo kwenye “Teolojia Pangilifu” (systematic Theology). Nakala hii

495 74 693KB

Kiswahili Pages 106 Year 2021

Report DMCA / Copyright

DOWNLOAD PDF FILE

Table of contents :
YALIYOMO
TABARUKU i
UTANGULIZI ii
FINYAZO v
SURA YA KWANZA 1
1. Dhana ya Mwanadamu 1
1.1. Uumbaji wa Mungu kama asili ya Mwanadamu 5
1.2. Mwanadamu kama Mfano na Sura ya Mungu 9
1.2.1. Maoni Kuhusu Sura na Mfano wa Mungu 10
1.2.2. Utambuzi wa Mfano wa Mungu 12
2. Agano la Kwanza 18
2.1. Vipengele vya Agano la Matendo 19
2.1.1. Wahusika wa Agano 19
2.1.2. Ahadi ya Agano 19
2.1.3. Masharti katika Agano 20
SURA YA PILI 21
SEHEMU ZA MWANADAMU NA ASILI YAKE 21
1. Sehemu za Mwanadamu 21
2. Asili ya Nafsi /Roho ya Kila Mtu 24
2.1. Mungu aliumba roho zote mara moja 25
2.2. Roho ya mwanadamu hutoka kwa mzazi 26
2.3. Mungu huumba roho moja moja 28
SURA YA TATU 30
ANGUKO LA MWANADAMU 30
1. Kiini ch Anguko 30
2. Miti ya Aina Mbili 33
2.1. Mti wa uzima 34
2.2. Mti wa Ujuzi 36
3. Dhambi na Kuenea Kwake 37
3.1. Dhambi ya Asili 38
3.2. Dhambi halisi 39
4. Dhambi kubwa na Ndogo 41
3. Kifo 45
3.1. Kinachotokea baada ya kifo 46
3.1.1. Ukomo wa Uhai 46
3.1.2. Mwendelezo wa Uhai 47
3.1.3. Kuangamizwa kwa roho na mwili kwa baadhi ya watu 48
3.1.4. Kulala kwa roho 49
3.1.5. Roho Kuvaa Mwingine 50
3.1.6. Roho na Mwili Hutengana na Kusubiri Ufufuo 52
SURA YA NNE 54
MAMBO YANAYOJADILIWA KUHUSU MWANADAMU YAKIHUSISHA ASILI YAKE 54
1. Jinsi na Jinsia 55
1.1. Nini maana ya kuwa “mwanaume”? 61
1.2. Nini maana ya kuwa “mwanamke.”? 66
2. Jinsi 71
3. Ndoa 73
4. Rangi za Wanadamu 76
5. ndoa za jinsi moja 79
4. Kifo cha Huruma (Uthanasia) 83
HITIMISHO 87
Marejeleo 91
Recommend Papers

Mfululizo wa Mafundisho katika Teolojia Pangilifu 
ANTHROPOLOJIA : MAFUNDISHO YA KIKRISTO KUHUSU MWANADAMU [1, 1 ed.]
 9789976572698

  • 0 0 0
  • Like this paper and download? You can publish your own PDF file online for free in a few minutes! Sign Up
File loading please wait...
Citation preview

ANTHROPOLOJIA

MAFUNDISHO YA KIKRISTO KUHUSU MWANADAMU

Teolojia Pangilifu-1

D.J. SENI

ii

Hakimiliki © 2020 Daniel John Seni Chapa ya kwanza, 2020 [email protected]

Msanifu: Eternal Word and Charity Publishing (EWCP) Dar es salaam [+255-755-643-590] Mchapaji: Truth Printing Press. Dar es salaam [+255764425704] ___________________________________ Haki zote zimehifadhiwa. Hakuna sehemu ya chapisho hili inayoweza kuzalishwa tena, au kuboreshwa au kusambazwa kwa njia yoyote au kwa kubadilisha umbo au kunakili na kupeleka katika umbo lingine bila idhini ya maandishi ya mchapishaji, isipokuwa kwa nukuu fupifupi kwa matumizi yasiyo ya kibiashara. Maandiko ya Biblia yamechukuliwa kutoka kwenye Biblia ya Kiswahili Toleo la shule inayotolewa na Swahili Union Version (SUV). ________________________ kinapatikana Shekinah Mission Centre (SMC) [email protected] S.L.P 32807 Dar es Salaam +255 769 080 629 +255 787 907 347 Madale/Mivumoni, Joshua road, mkabala na Shule ya Msingi-Atlas/ at Shekinah Presbyterian Church in Tanzania, Dar es Salaam.

TABARUKU

Kwa Wanatheolojia wote Wanaopenda kujifunza zaidi.

i

UTANGULIZI Kitabu hiki ni mfululizo wa mafundisho ya Kikristo yaliyo

kwenye

“Teolojia

Pangilifu”

(systematic

Theology). Nakala hii inashughulikia anthropolojia. Katika utangulizi

huu

ningependa

kufafanua

maana

ya

anthropolojia ya Kikristo. Kwa ujumla anthropolojia ni utafiti wa kisayansi unaohusika na kutafiti mwanadamu na sifa zake, biolojia ya binadamu, na jamii, ya sasa na ya zamani, pamoja na spishi za wanadamu za zamani.1 Kwa maneno mengine tunaweza kuita “anthropolojia ya kisayansi” kwa sababu yenyewe inashughulikia masuala ya mwanadamu kwa kutafiti sayansi inasema nini. Hata hivyo, tunapozungumzia “anthropolojia ya Kikristo” tunakuwa na maana zaidi ya hiyo. Katika muktadha wa theolojia ya Kikristo, anthropolojia ya Kikristo ni utafiti wa mwanadamu kama anavyohusiana na Mungu. Inatofautiana na anthropolojia ya kisayansi ambayo hushughulikia sana uchunguzi kwa kulinganisha 1

Ralph W. Nicholas. https://www.britannica.com/science/anthropology

ii

tabia za binadamu na jamii kwa nyakati na maeneo tofauti.2 Katika Anthropolojia ya Kikristo tunajadili kwa undani asili ya mwanadamu katika uhusiano wake na Mungu, chanzo cha matatizo ya mwanadamu na kuelekeza suluhisho lake. Tofauti na anthropolojia ya kisayansi, anthropolojia ya Kikristo hupata kiini chake kutoka kwenye Biblia, na kwamba hairuhusu mawazo ya kawaida yatawale Biblia. Na kwamba, Biblia ndiyo hitimisho la mawazo yote ya mwanadamu, hata pale inapopingana na uelewa

wa

kawaida

wa

mwanadamu,

ni

lazima

iheshimiwe. Kwa hiyo tunafanya utafiti kwa kuangalia Biblia inasema nini kuhusu mwanadamu. Mafundisho kuhusu “mwanadamu” au “mtu” kama tutakavyokuwa tunatumia maneno haya ni mojawapo ya mafundisho ambayo yanapofundishwa yamewavutia watu wengi tangu zamani. Tangu zamani watu wamejaribu kujiuliza maswali, mtu ni nani? Anatoka wapi? Zamani nikiwa mtoto mdogo niliaminishwa watoto wananunuliwa 2

Erickson, Millard (1998). Christian Theology (2 ed.). uk. 537

iii

dukani. Uhai wa mtu uko wapi? Nini Kusudi la kuumbwa kwa mtu? Na mambo mengine mengi yanayohusiana na mtu. Tukubali kwamba kujifunza kuhusu mwanadamu, maana yake unajifunza kuhusu wewe mwenyewe. Hata hivyo, mafundisho kuhusu mwanadamu katika kitabu hiki si yale mafundisho ambayo yamezoeleka mitaani ambayo yanatolewa na wanasaikolojia kuhusu mwanadamu bali ni mafundisho

kuhusu

mwanadamu

kama

ambavyo

ameelezwa katika Biblia. Vilevile somo hili halihusu “uumbaji” ingawa kwa sehemu kubwa litagusia uumbaji wa mwanadamu. Ama kwa hakika, kitabu hiki kitawafaa waalimu na wanafunzi

wa

Anthropolojia

kitawasaidia

kuboresha

mwanadamu,

na

ya

Kikristo.

Vilevile

wao

kuhusu

ufahamu

kuepuka

mawazo

changamani kuhusu mwanadamu.

Daniel John Seni Januari 2021.

iv

ya

wanausasa-

FINYAZO 1. WCF/1/1 -The Westminster Confession of Faith/sura ya 1/sehemu ya 1 2. WLC/1- The Westminister Larger Catechism/Swali la 1

v

YALIYOMO TABARUKU ...................................................................... i UTANGULIZI ................................................................... ii FINYAZO .......................................................................... v SURA YA KWANZA ....................................................... 1 1. Dhana ya Mwanadamu ......................................... 1 1.1. Uumbaji wa Mungu kama asili ya Mwanadamu 5 1.2. Mwanadamu kama Mfano na Sura ya Mungu ... 9 1.2.1. Maoni Kuhusu Sura na Mfano wa Mungu.... 10 1.2.2. Utambuzi wa Mfano wa Mungu ................... 12 2. Agano la Kwanza ............................................... 18 2.1. Vipengele vya Agano la Matendo ................... 19 2.1.1. Wahusika wa Agano .................................... 19 2.1.2. Ahadi ya Agano ........................................... 19 2.1.3. Masharti katika Agano ................................. 20 SURA YA PILI................................................................ 21 SEHEMU ZA MWANADAMU NA ASILI YAKE . 21 vi

1. Sehemu za Mwanadamu .................................... 21 2. Asili ya Nafsi /Roho ya Kila Mtu ....................... 24 2.1. Mungu aliumba roho zote mara moja .............. 25 2.2. Roho ya mwanadamu hutoka kwa mzazi ........ 26 2.3. Mungu huumba roho moja moja ..................... 28 SURA YA TATU ............................................................ 30 ANGUKO LA MWANADAMU ............................. 30 1. Kiini ch Anguko................................................. 30 2. Miti ya Aina Mbili ............................................. 33 2.1. Mti wa uzima .................................................. 34 2.2. Mti wa Ujuzi ................................................... 36 3. Dhambi na Kuenea Kwake ................................. 37 3.1. Dhambi ya Asili .............................................. 38 3.2. Dhambi halisi .................................................. 39 4. Dhambi kubwa na Ndogo ................................... 41 vii

3. Kifo.................................................................... 45 3.1. Kinachotokea baada ya kifo ............................ 46 3.1.1. Ukomo wa Uhai ........................................... 46 3.1.2. Mwendelezo wa Uhai .................................. 47 3.1.3. Kuangamizwa kwa roho na mwili kwa baadhi ya watu48 3.1.4. Kulala kwa roho ........................................... 49 3.1.5. Roho Kuvaa Mwingine ................................ 50 3.1.6. Roho na Mwili Hutengana na Kusubiri Ufufuo 52 SURA YA NNE ............................................................... 54 MAMBO YANAYOJADILIWA KUHUSU MWANADAMU YAKIHUSISHA ASILI YAKE ... 54 1. Jinsi na Jinsia ..................................................... 55 1.1. Nini maana ya kuwa “mwanaume”?................ 61 1.2. Nini maana ya kuwa “mwanamke.”?............... 66 viii

2. Jinsi.................................................................... 71 3. Ndoa .................................................................. 73 4. Rangi za Wanadamu .......................................... 76 5. ndoa za jinsi moja .............................................. 79 4. Kifo cha Huruma (Uthanasia) ............................ 83 HITIMISHO .................................................................... 87 Marejeleo ......................................................................... 91

ix

SURA YA KWANZA

1. Dhana ya Mwanadamu Kuna maneno mengi yanayoashiria “mwanadamu” kwa mfano mtu, mwana wa Mungu, mtoto wa Mungu, Mwana wa Adamu, nk. Lakini katika lugha ya Kiswahili tunatumia

maneno

“Mtu”

na

“mwanadamu”

kwa

kumaanisha kitu kilekile, kwa hiyo maneno haya yatatumika kwa kubadilishana. Hatutatumia neno “Mwana wa Adamu” kwa kumaanisha “mwanadamu” kwa sababu mara nyingi Yesu alitumia jina hili kujirejelea mwenyewe katika Injili. Lakini kuna mawazo mengi kuhusu mwanadamu. Wengine husema, “binadamu ni utu.” Kwa maana ya kwamba umbo la mwanadamu si binadamu haswa, bali ni ule utu wa ndani ndiye binadamu. Hata hivyo mawao haya ni ya kijamii zaidi na yanajaribu kuangalia matokeo ya matendo ya mwanadamu; hata hivyo, bado hayawezi kutuambia mwanadamu alitoka wapi. Kuna mawazo 1

kwamba mwanadamu ni Matokeo ya mkusanyiko wa atomi. Huku mtazamo tunaoujua wengi ni ule ambao tumekaririshwa

tangu

shule

za

msingi

kwamba

mwanadamu ni hatua ya juu kabisa ya mabadiliko ya nyani, kutoka Ausralopethecus, kisha homo erectus, baadaye homo habilis, homo sapiens na Homo sapiens. Haya ni mawazo ya kisayansi, ambayo kwa kweli yamekuwa ni ya muda mrefu, ingawa wateteaji wenyewe hushindwa kuthibitisha na kushindwa kujibu maswali mepesi kabisa kwamba, “je mbona nyani wa leo hawabadiliki? Nini kimewasibu? Katika hadithi nyingi za uumbaji wa mwanadamu kuna mawazo yanayokinzana. Kwa mfano, kulingana na vyanzo vya Mesopotamia, mwanamume na mwanamke waliumbwa ili kupunguza mzigo wa kazi kwa miungu wadogo ambao walilazimishwa kulima ardhi ili kulisha miungu. Hizi ni hadithi za waabudu miungu ambao hawana namna nyingine zaidi ya kutengeneza hadithi ili zifae miktadha yao.

2

Tunazo hadithi nyingi katika makabila ya Kiafrika kuhusu uumbaji, lakini hadithi hizo zote zinazungumzia miungu na namna ilivyosaidiana kuumba ulimwengu na vitu vingine. Hadithi hizi hazihitaji Ushahidi kugundua kwamba ni za uongo kwa sababu zinapishana. Hatuna Mungu wa kabila fulani, tuna Mungu mmoja tu, Muumba wa Mbingu na nchi na wanadamu wote. Kwa hiyo, hadithi ya kweli ni kwamba Mungu ndiye alimwumba mwanadamu. Kwa kweli, mwanadamu ni wa ajabu sana. Mwandishi wa Zaburi 8:4-5 anasema kwamba: “Mtu ni kitu gani hata umkumbuke, Na binadamu

hata

umwangalie?

Umemfanya

mdogo punde kuliko Mungu; Umemvika taji ya utukufu na heshima.” Katika kifungu hiki, heshima ya mwanadamu inasisitizwa kwa njia isiyo na kifani. Pengine tungejiuliza kusudi zima la uumbaji wa Mungu kwa viumbe vyote, lakini

kwa

kuwa

tunajikita

katika

kumzungumzia

mwanadamu, basi tuangalie kusudi la uumbaji wake. 3

Tukisoma WLC/1/1/ kwamba “Kusudi la msingi na la juu zaidi la mwanadamu ni kumtukuza Mungu na

kumfurahia yeye milele. Hapa unaweza kuona lugha ya uhusiano kati ya Mungu na mwanadamu. Samuel Willard (1640-1707) anasema kwamba kumtukuza Mungu ni kuonyesha utukufu wake, kumtangaza kuwa mtukufu zaidi. Tunamtukuza Mungu kwa kufikiria sawasawa kuhusu yeye na kuwa na mioyo ya kumwabudu, kumwogopa, kumtegemea, na kunyenyekea chini ya amri zake na kuwa na utulivu chini ya uongozi wake.3 Kumtukuza Mungu ndicho kipaumbele cha juu cha mwanadamu, na kwa namna moja au nyingine ni sahihi kusema kwamba Mungu alimuumba mwanadamu kwa ajili ya kujitukuza mwenywe, na kwamba atukuzwe na wanadamu. Katika

Bustani

ya

Edeni,

Mungu

alimweka

mwanadamu kulima na kulinda bustani yake. Hiyo bustani ilikuwa bustani ya Mungu, Adamu aliwekwa tu. Lakini, tukubali kwamba Mungu hakupungukiwa na kitu chochote 3

Samuel Willard, A Compleat Body of Divinity in Two Hundred and Fifty Expository Lectures on the Assembly’s Shorter Catechism (Boston: by B. Green and S. Kneeland for B. Eliot and D. Henchman, 1726), 5–6.

4

kisha akaamua kumuumba mwanadamu, na vivyo hivyo hategemei kitu chochote kwa ajili ya uwepo (existence) wake, bali ni kwa utukufu wake mwenyewe, kwa hiari na mapenzi yake yasiyo na kipimo. 1.1.

Uumbaji wa Mungu kama asili ya Mwanadamu

Tunapozungumza

asili

ya

mwanadamu,

hatuzungumzii tu mwanzo wake, kwani neno “mwanzo” linaamaanisha jambo “kutokea tu.” Lakini maana ya jambo kutokea haioneshi asili yake. Neno “asili” linadokeza kusudi la kitu fulani kuwepo, kwa hiyo ikiwa ni kwa mwanadamu, linadokeza kusudi la mwanadamu kuwepo. Maelezo ya Kimaandiko ya asili ya mwanadamu yamo katika Mwanzo 1: 26, 27, “Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi. Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba, mwanamume na mwanamke aliwaumba.” Na Mwanzo 2:7, “BWANA 5

Mungu

akamfanya

mtu

kwa

mavumbi

ya

ardhi,

akampulizia puani pumzi ya uhai; mtu akawa nafsi hai.” Kuna mambo mawili yamejumuishwa hapa; kwanza mwili wa mtu uliumbwa na Mungu. Lakini haukukua, wala kufanya jambo lolote. Pili, roho ilitolewa na Mungu. Alimpulizia mwanadamu "pumzi ya uhai.” Kwa kweli haya mambo ni ya msingi mno tunapotaka kujua asili ya mtu. Mwanadamu “akawa nafsi hai.” (Mwa.2:7). Neno nafsi kwa Kiebrania ni nephesh, ambalo linamaanisha "uhai, kupumua, ufahamu" Mtu hakuwa nafsi hai hadi pale Mungu alipompulizia uzima ndani yake. Mwanadamu ni wa pekee kati ya vitu vilivyo hai duniani. Mwanadamu ndiye kilele cha uumbaji wa Mungu. Kuna tofauti kubwa katika uumbaji wa Mtu na uumbaji wa vitu vingine, kwa mfano wanyama walitolewa na ardhi kwa amri ya Mungu. Biblia inasema “Mungu akasema, Nchi na izae kiumbe hai kwa jinsi zake, mnyama wa kufugwa, nacho kitambaacho, na wanyama wa mwitu kwa jinsi zake; ikawa hivyo ((Mwa. 1: 24). Mwanadamu aliumbwa na Mungu, kwa mkono wa Mungu. Mungu 6

aliumba vitu vingine kwa neno lake, “akasema na iwe.” Lakini

alipofika

kwa

mwanadamu

akasema,

“Na

Tumfanye mtu kwa mfano wetu.” Mungu ndiye aliyemwumba mwanadamu. Hoja hii inapingana

na

mawazo

ya

kwamba

mwanadamu

ametokana na mabadiliko ya wanyama fulani ambao waliwahi kuishi mabilioni ya miaka. Mungu aliwaumba Adamu na Hawa wakiwa na roho safi; kwa maana ya kwamba Adamu na Hawa walipoumbwa hawakuwa na doa lolote, wala dhambi yoyote; kwa hiyo walikuwa wakamilifu kabisa. Ufuatao ni ufupisho wa ukweli kuhusu uumbaji: a) Uumbaji wa mwanadamu ulitokea kama tukio kuu la mwisho la siku ya sita ya wiki ya uumbaji, kama kilele cha shughuli za Mungu. Mungu alikusudia yote ambayo alikuwa amefanya kabla ya uumbaji wa mwanadamu kuwa maandalizi ya uumbaji wa mwanadamu. b) Kuna

tofauti

kubwa

kati

ya

uumbaji

wa

mwanadamu na uumbaji wa vitu vingine. Katika 7

uumbaji wa vitu vingine kuna fomula "Na Mungu akasema:" Na iwe "(Mwa. 1: 3, 6, 9, 14, 20, 24), lakini katika uumbaji wa mwanadamu Mungu hajatumia kanuni hiyo, anatumia usemi mpya kabisa, “Na Tumfanye Mtu” (Mwa. 1:26) siyo “Na iwe.” Usemi “Na tumfanye” unaonesha ukaribu kati ya Mungu na mwanadamu kuliko vitu vingine vyovyote vile. c) Ni mtu peke yake ndiye anafafanuliwa kama ameumbwa kwa mfano wa Mungu (Mwa. 1: 26-27). Wanyama hawajaumbwa kwa mfano wa Mungu. d) Mwanadamu amepewa mamlaka juu ya uumbaji wa Mungu kama makamu wa Mungu (1: 26-28; 2: 1920). Makamu wa Mungu ni neno la kidunia sana, lakini linakusaidia wewe kuelewa maana ya mwanadamu na uhusiano wake na Mungu. e) Kuna hadithi mbili za uumbaji; Mwanzo sura ya 1 na sura ya 2. Hadithi hizi hazipingani, bali hadithi ya pili ambayo ipo katika Mwanzo 2: 5-25 “inafafanua zaidi tendo la uumbaji wa Mungu kwa

8

mwanadamu katika siku ya sita na kujaribu kuonesha namna mwanadamu alivyo wa muhimu.”4 f) Mwanadamu wa kiume aliitwa Adamu (Mwa. 2:19). Jina hili alipewa na Mungu mwenyewe. Jina hili pia wakati mwingine linarejelea wote; mwanamume na mwanamke. (Mwa. 5:2). Mwanadamu wa kike anaitwa Hawa (Mwa. 3:20). Jina hili aliitwa na mumewe Adamu, labda pengine kwa sababu Mungu alikuwa amempa Adamu hapo awali kazi nyingine ya kuviita majina vitu (viumbe) vingine.

(Mwa.

2:20) 1.2.

Mwanadamu kama Mfano na Sura ya Mungu

Biblia

inafundisha

kwamba

mwanadamu

ameumbwa kwa mfano wa Mungu. Kwa mujibu wa Mwanzo 1:26, Mungu alisema, "Na tufanye mtu kwa

mfano wetu, kwa sura yetu." Mara nyingi tunatamka neno “mfano” na badala ya kuyatamka yote kwa pamoja. Watu wengine hudhania kwamba maneno “sura na mfano” 4

Reymond, L. Robert, A New Systematic Theology of The Christian Faith (Nashville: Thomas Nelson Publishers 1998), 437

9

yaanashiria vitu viwili tofauti, lakini inaelekea kwamba yanaashiria kitu kimoja. Vifungu vifuatavyo vinaonyesha kuwa yanatumika kwa kubadilishana: Mwa 1:26, 27; 5: 1; 9: 6; 1 Kor. 11: 7; Kol. 3: 10; Yak. 3: 9. Ni uandishi wa Kiyahudi wa kukazia jambo kwa kuliandika na kisawe chake. 1.2.1. Maoni Kuhusu Sura na Mfano wa Mungu Kwa mujibu wa Maandiko, mwanadamu aliumbwa kwa sura na mfano wa Mungu, na kwa hivyo mwananadamu anahusiana na Mungu au ana uhusiano wa karibu sana na Mungu. Wazo kama hili ambalo ni la ukweli linapatikana hata katika fasihi ya watu wa Mataifa. Paulo aliashiria Waathene kwamba baadhi ya washairi wao wenyewe wamezungumza juu ya wanadamu kama watoto wa Mungu, (Mdo. 17:28). Mababa wa Kanisa la kwanza walikubaliana kabisa kwamba sura ya Mungu ndani ya mwanadamu kimsingi iko katika sifa za busara na maadili ya mwanadamu, na katika uwezo wake wa utakatifu; Irenæus na Tertullian 10

walitofautisha “sura” na “mfano” wa Mungu kwa kudai kwamba “sura” inapatikana katika sifa za kimwili, na “mfano” unapatikana katika sifa za kiroho, lakini wengine walielekea kujumuisha pia sifa za kimwili.5 Clement wa Alexandria na Origen walipinga wazo hilo na kudai kwamba “sura” inaashiria sifa za mwanadamu kama mwanadamu, na neno "mfano," linaashiria sifa ambazo sio muhimu kwa mwanadamu, lakini zinaweza kuwepo au kupotea. Kwa mujibu wa Pelagius na wafuasi wake “sura” inamaanisha kwamba mwanadamu alipewa uwezo wa kufikiri na kuchambua hoja ili kumjua Mungu; kwa hiari, ili aweze kuchagua na kufanya mema; na kuwa na nguvu ya kutawala viumbe dhaifu. Huku wengine wakiwa na mawazo kwamba mwanadamu alipewa haki ya kipekee alipoumbwa, haki ambayo alikuwa nayo wakati wa utii wake wa muda, na baada ya kuanguka katika dhambi haki hiyo ilipotea mara moja.

5

Berkhof, Louis, Systematic Theology (Grand Rapids: Eerdmans) 1974, uk. 219

11

Katika mawazo yote, hakuna wazo linalodokeza kwamba mwanadamu ameumbwa kwa sura ya Mungu kwa jinsi sura zetu za kimwili zilivyo. Sura zetu za kimwili zilivyo hazina uakisi wowote wa sura ya Mungu, kwani Mungu hana mwili wala nyama. Ingekuwa hivyo, basi Mungu angeonekana kuwa na sura nyingi sana. 1.2.2. Utambuzi wa Mfano wa Mungu Baada ya kutoa maoni kadhaa, ningependa sasa nijikite katika kuelezea dhana ya mfano wa Mungu kwa mwanadamu. Kwa hiyo katika kipengele kinachofuata, ndio msimamo wa Kibiblia ambao mimi ninaufuata. Inaweza kuonekana baadhi ya maneno yanajirudia, lakini yana maana kubwa sana. Sura ya Mungu ni ile hali ya kiroho kwa mwanadamu. Mungu ni Roho, na ni kawaida kutarajia kwamba kipengele hiki cha kiroho pia kinapata kujieleza kwa

mwanadamu

kama

sura

ya

Mungu.

Mungu

“alimpulizia puani pumzi ya uhai; na mwanadamu akawa nafsi hai.” (Mwa. 2: 7). "Pumzi ya uhai" ni kanuni ya maisha, na "nafsi hai" ni nafsi ya mwanadamu. Nafsi 12

imeunganishwa na kubadilishwa kuwa mwili, lakini pia inaweza, kama ikihitajika, kuwepo bila mwili. Biblia inasema kwamba mtu, sio roho ya mwanadamu tu aliumbwa kwa mfano wa Mungu, hivyo mwanadamu, "nafsi hai," haijakamilika bila mwili. Isitoshe, Biblia inazungumzia mauaji kama uharibifu wa mwili, (Mat. 10:28), na pia kama uharibifu wa mfano wa Mungu ndani ya mwanadamu. (Mwa. 9: 6). Jambo lingine la mfano wa Mungu ni kutokufa. Biblia inasema kwamba Mungu ana sifa ya kutokufa, yaani, “ambaye peke yake hapatikani na mauti” (I Tim. 6:16). Mwanadamu pia aliumbwa akiwa katika hali ya kutokufa, sio tu kwa maana ya kwamba roho yake ilikuwa imejaliwa kuishi milele, lakini pia kwa maana ya kwamba hakubeba mbegu ya kifo cha mwili, na katika hali yake ya asili hakuwa chini ya sheria ya kifo. Kifo kilikuja kama adhabu ya dhambi, (Mwa. 2:17), Paulo anatuambia kuwa dhambi ilileta mauti ulimwenguni (Rum. 5:12; I Kor. 15: 20,21) ni mshahara wa dhambi (Rum. 6:23), malipo ya dhambi. 13

Calvin anasema kwamba kiti sahihi cha sura ya Mungu kiko ndani ya roho, ingawa miale ya utukufu wake pia huangaza mwilini. Calvin anaona kuwa Sura inajumuisha uadilifu wa asili ya mwanadamu, ambao uliopotezwa na dhambi lakini umerejeshwa katika Kristo. (Efe. 4:24; Kol. 3: 10)”6 Kwa muhtasari tunaweza kusema kuwa; a) Sura ya Mungu ipo katika nafsi au roho ya mtu, ambayo ni hali ya kiroho, kutokuonekana kwa roho, na kutokufa. b) Sura ya Mungu pia imo katika nguvu za kiakili au uwezo wa mwanadamu kama mtu mwenye busara, maadili na utashi. c) Sura ya Mungu ipo katika uadilifu wa kiakili na maadili ya asili ya mwanadamu, ikijifunua katika maarifa ya kweli, haki, na utakatifu (Efe. 4:24; Kol. 3:10). d) Sura ya Mungu ipo katika mwili, mwili siyo “maada”, lakini kama kiungo cha roho, hushiriki 6Calvin,

John, Institutes of the Christian Religion (Louisville: Westminster John Knox Press, 1960),uk.

308.

14

kutokufa kwake; tunaposema kutokufa kwa mwili hatumaanishi kile kifo cha kwanza, baada ya kifo hiki mwili utafufuliwa, hii inaonesha umilele wa mwili. e) Sura ya Mungu iko katika utawala wa mwanadamu juu ya dunia, kwamba mwanadamu anatawala vitu vyote kwa niaba ya Mungu. f) Vilevile, mfano wa Mungu uko katika zile tabia za Mungu. Kuna tabia za Mungu ambazo zimo kwa wanadamu. Ingawa tabia hizo zina mapungufu makubwa kwa sababu ya dhambi, lakini ni dhahiri kuna wakati mwanadamu anakuwa na “huruma, upendo nk” ingawa haya matendo ni madhaifu, lakini asili yake ni Mungu. Na ndiyo maana hata kama mtu akiwa mbaya kiasi gani, kuna kitu kizuri ndani yake, huo ni mfano wa Mungu. g) Mfano wa Mungu haukomei kwa Waamini tu, bali hata wale wapagani wana mfano wa Mungu. Mungu hakuumba mpagani, aliumba Adamu na Hawa, mwanadamu akapotoka. Ingawa bado hawajaokoka, bado mfano wa Mungu uko ndani yao, lakini mfano 15

huo ni ule wa asili, tofauti na Mkristo ambaye, kwake mfano wa Mungu unaendelea kudumishwa kila siku. Zile tabia za Mungu zinaendelea kuimarika na kuonekana kwa Wakristo wanaoamua kujitiisha chini ya mapenzi yake. Hitimisho kuhusu mfano wa Mungu Mwanadamu,

mwanamume

na

mwanamke

ameumbwa kwa mfano wa Mungu. Kama Muumba wake, mwanadamu huthibitisha umoja na utofauti katika uhusiano wa upendo. Neno la Kiingereza “Man" ambalo hutafsiriwa kwa Kiswahili kama “Mwanaume” hujumuisha mwanaume na mwanamke. Hata hivyo mwanamume na mwanamke wako tofauti katika jinsi na jinsia; kwa sababu hiyo wana majukumu tofauti.

Wakati wa uumbaji

mwanadamu alifanya kazi katika uhusiano mzuri na Mungu na viumbe vingine. Hata hivyo, Mwanadamu alivunja agano la muumba wake kwa kutenda kwa uhuru na kumuasi. Sura ya Mungu iliharibika lakini haikupotea kabisa.

Mwanadamu

alivuruga uhusiano wake na Mungu, na matokeo yake, 16

mbele za Mungu mwanadamu amekufa kiroho, lakini pia kuhusu uhusiano wao (mwanadamu kwa mwanadamu) uhusiano wao uliharibika ambapo matokeo yake iliingia laana, na mivutano isiyokoma. Si hivyo tu, badala ya kutawala, mwanadamu akaanza kutawaliwa na baadhi ya viumbe ambavyo alipewa uwezo wa kuvitawala. Mfano wa Mungu umekuwa kamili kupitia Yesu Kristo

peke

yake, ambaye

ni

Mungu-Mtu.

Yeye

hudhihirisha sura hiyo kwa kumpenda kabisa Mungu, kuwapenda watu, na kuwa na mamlaka juu ya viumbe vingine. Wale ambao ni wa Yesu kupitia imani iokoayo wanakuwa

viumbe

vipya

na

kwa

upendo

wao

wanaonyesha sura ya Mungu iliyorejeshwa, ingawa haifai kabla ya ufufuo wa mwisho.

Kila siku Wakristo

wanafananishwa na mfano wa Mungu kupitia “utakaso.”7 Wakati Yesu atakaporudi mara ya pili, Wakristo wote watatukuzwa na kufanywa kama Yesu. Watakuwa wakamilifu kabisa na wataonyesha sura ya mfano wa Mungu kama hapo awali. 7

Hoekema, A. Antony. Created in God’s Image, (Grand Rapids: William B Eerdmans, 1986) Uk.31

17

2. Agano la Kwanza Ingawa hakuna neno “Agano” katika kitabu cha Mwanzo sura ya 1-2 lakini ni dhahiri kwamba Mungu alifanya Agano na Adamu. Agano hili mara nyingi huitwa "Agano la Matendo.” Kwamba, Mungu aliahidi uzima kwa Adamu na watoto wake, maadamu wangemtii kikamilifu. Ilikuwa ni sheria ambayo yeye na uzao wake wote walipaswa kufuata. Walipaswa kuitii milele kabisa. Mungu aliahidi uzima kwa kuitunza na akatishia kifo kwa kutotii, na alimpa mwanadamu nguvu na uwezo wa kuitunza (Mwa. 1:26-27, 2:17, Rum. 2:14-15, 10:5, 5.12,19, Gal. 3:10,12, Mhu. 7:29, Ayu 28:28, Efe. 4:24).8 Paulo

anatusaidia

kuelewa

agano

hili

pale

anapolinganisha kati ya Adamu na Kristo katika Warumi. 5: 12-21. Anadai kwamba katika Adamu watu wote walikufa, lakini katika Kristo wale wote walio wake wamefanywa hai. Hii inamaanisha kwamba Adamu alikuwa kiongozi mwakilishi wa wanadamu wote, kama vile Kristo alivyo kiongozi mwakilishi wa wote ambao ni wake. 8

Linganisha WFC/7/2/Kisw, pia 19/1

18

2.1.

Vipengele vya Agano la Matendo

Kila agano lazima liwe na vipengele muhimu ambavyo vinalifanya Agano hilo liwe halali. Kama nilivyosema hapo juu kwamba hakuna neno Agano katika maelezo ya uumbaji, lakini hakika tukiangalia matukio tunaweza kuona uagano uliopo. 2.1.1. Wahusika wa Agano Agano daima ni makubaliano kati ya pande mbili. Katika hili wahusika ni Mungu wa UTATU, Bwana Mtawala na Mfalme wa ulimwengu, na Adamu kama mwakilishi wa wanadamu wote. 2.1.2. Ahadi ya Agano Ahadi ya agano hili ilikuwa ahadi ya Uzima. Uzima wa milele, maisha ya milele mbele za Mungu. Adamu na Hawa walifurahia sana ahadi hii, walishirikiana na Mungu mara zote. Walikuwa wanaishi mbele za Mungu muda wote. Kuna lugha ya kibinadamu kwamba Mungu alikuwa anawatembelea mida ya jioni ili kupata wasaa wa kujadiliana nao. Ahadi ya agano ilikuwa ni raha milele mbele za Mungu; uhusiano bora kutoka kwake. 19

2.1.3. Masharti katika Agano Masharti katika Agano hili ilikuwa ni utii kabisa (complete obedience). Amri ya kutokula mti wa ujuzi wa mema na mabaya ilikuwa dhahiri mtihani wa utii safi. Siyo kwamba mti wa ujuzi wa mema na mabaya ulikuwa mti wa miujiza, wala haikuwa “tendo la ndoa” kama wengine wasemavyo, bali ulikuwa ni mti wa matunda wa kawaida, ila utofauti wake ni kwamba waliambiwa wasile matunda yake (kwa uelewa wa Hawa, hawakupaswa hata kugusa. ). Hicho kilikuwa kigezo cha Agano. Ili agano lisimame, lazima kigezo kifuatwe, kama mwanadamu akivunja agano kwa kula, basi agano haliwezi kusimama tena, labda kuwepo na Agano lingine. Katika Agano kunakuwepo na adhabu ikiwa upande mmoja wa wahusika utavunja agano hilo. Katika agano hili, adhabu ilikuwa kifo. Hii sio tu katika utenganisho wa mwili na roho, lakini kimsingi zaidi katika kujitenga kwa roho na Mungu. Kwa hiyo Adamu alikuwa amefungwa katika Agano la Matendo, ambapo alipaswa kutekeleza vigezo na 20

masharti yote vya Agano. Jambo hili halikuwa mzigo kwake, kwani alikuwa na uhusiano wa karibu na Mungu.

SURA YA PILI

SEHEMU ZA MWANADAMU NA ASILI YAKE 1. Sehemu za Mwanadamu Kumekuwa na mawazo kadhaa kuhusu sehemu za mwanadamu. Ni muhimu kutalii angalau kidogo mawazo hayo. Uelewa wa kawaida na wa wazi ni kwamba mwanadamu ana sehemu mbili, mwili na roho. Hii inaambatana na kujitambua kwake na pia inayotokana na uchunguzi wa Maandiko, ambayo yanazungumza juu ya mwanadamu kuwa na "mwili na roho. Biblia inasema “Msiwaogope wauuao mwili, wasiweze kuiua na roho; afadhali mwogopeni yule awezaye kuangamiza mwili na

roho pia katika Jehanam.” (Mat.10:28). Pia tunasoma 21

katima Mhubiri 12: 7 kwamba, “Nayo mavumbi huirudia nchi kama yalivyokuwa, Nayo roho humrudia Mungu aliyeitoa. Paulo ana maneno ya kutuambia kuhusu sehemu za mwanadamu anapozungumzia habari ya kumtenga mzinzi katika kanisa la Korintho “Kwa maana kweli, nisipokuwapo kwa mwili, lakini nikiwapo kwa roho, mimi mwenyewe nimekwisha kumhukumu yeye aliyetenda jambo hilo, kana kwamba nikiwapo…kumtolea Shetani mtu huyo, ili mwili uadhibiwe, ili na roho iokolewe katika siku ya Bwana Yesu. (1 Kor. 5: 3,5) Katika kuzungumzia roho, tunapaswa pia kugusia habari ya “nafsi.” Katika Biblia wakati mwingine maneno haya yameonekana kwa pamoja, kwa mfano katika 1 Thes. 5:23 mahali inaposema, “Mungu wa amani mwenyewe awatakase kabisa; nanyi nafsi zenu na roho zenu na miili

yenu mhifadhiwe mwe kamili, bila lawama, wakati wa kuja kwake Bwana wetu Yesu Kristo.” Kwa kuzingatia kifungu hicho, wengi wameng’amua kwamba 'roho' na 'nafsi' ni vitu viwili tofauti, na hivyo mwanadamu ana sehemu tatu, mwili, roho na nafsi. 22

Ni dhahiri, hata hivyo, kwamba maneno haya 'roho' na 'nafsi' hutumiwa kwa kubadilishana. Kwa mfano kifo wakati mwingine huelezewa kama kutoa roho, Mwa 35:18; 1 Wafalme 17:21, na wakati mwingine kama kujitoa nafsi (Mk. 10:45) Wafu katika maeneo mengine wanaitwa

"nafsi," Ufu. 6:9 20:4, ( Kwa kiingereza neno lililotumika ni soul, siyo spirit NIV) na katika maeneo mengine “roho”,' 1 Pet. 3:19; Ebr. 12:23. Kuhusu hili, John Frame ana ufafanuzi kwamba, “mara nyingi waandishi wa Biblia hurudia maneno kama haya kuelezea ukamilifu na utimilifu wa maumbile ya mwanadamu…Maandiko kawaida

hutumia

"Roho"

na

"nafsi"

kwa

kubadilishana.”9 Wengine hudai kwamba maneno haya mawili yanaashiria kitu cha kiroho kwa mwanadamu. roho; ni kanuni ya maisha ambayo inadhibiti mwili, na nafsi ndio kitu cha kibinafsi, ambacho hufikiria na kuhisi na kutaka. Pamoja na ufafanuzi huu, bado kuna wakati Biblia inaelezea mwanadamu kwa namna ambayo inaonekana 9

Frame, M. John, Systematic Theology; An Introduction to Christian belief (New Jersey: P&R Publishing company, 2013), uk. 888

23

kana kwamba yuko na sehemu tano. Kwa mfano katika Luka 10:27 inasema “...Mpende Bwana Mungu wako kwa

moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa nguvu zako zote, na kwa akili zako zote; na jirani yako kama

nafsi yako.” Unazungumziaje mstari huo? Je tunaweza kusema kwamba mwanadamu ana sehemu tano; moyo, roho, nguvu, akili, na nafsi? La hasha, tunahitaji kuelewa tu kwamba mara nyingi maneno kama haya yanapotokea hayamaanishi kitu kingine tofauti na badala yake ni uchaguzi wa maneno ya waandishi wa kale katika kukazia kitu kilekile. Kwa hiyo katika kitabu hiki maneno haya yanabadilishana. 2. Asili ya Nafsi /Roho ya Kila Mtu Kuna maoni kadhaa kuhusu asili ya nafsi ya kila mtu.

Ni

vyema

hapa

tukaweka

wazi

kwamba

tunapozungumzia nafsi ya kila mtu katika muktadha huu tunalo wazo zima kwamba nafsi ilitoka kwa Mungu, swali linaloibuka ni kwamba je, watu wanapozaliwa kwa sasa nafsi au roho zao zinatoka wapi?

24

Pamoja tutachunguza

na

kuwepo

mawazo

kwa

machache

mawazo na

mengi, mwishoni

tutang’amua ni wazo lipi ambalo angalau linakaribiana na msimamo wa Maandiko. 2.1.

Mungu aliumba roho zote mara moja

Huu ni mtazamo wa zamani ambao wanatheolojia wachache wanaushikilia. Wanaoshikilia mtazamo huu wanadai kwamba Mungu amekwisha kuumba roho zote na hivyo wanawake wanapobeba ujauzito, zile roho huingia mara moja na kuungana na mwili. Wanadai kwamba, “Mungu aliumba idadi maalumu ya roho, baadhi yake huungana na mwili na kuwa mwanadamu.”10 Mtazamo huu ulishikiliwa na mwanatheolojia wa mkongwe, Origen (184-254). Kwa kweli mtazamo huu hauna mashiko kutoka kwenye fungu lolote la Biblia. Swali la kawaida tu kujiuliza ni je roho hizo zinakaa wapi? Hewani hewani tu zikisubiri mwili? Mtazamo huu pia unashilikiwa na Waislamu.

10

Macarthur J & Mayhue, R (Ed) A Systematic Summary of Biblical Truth: Biblical Doctrine (Wheaton, Illinois: Crossway, 2017) uk.425

25

2.2.

Roho ya mwanadamu hutoka kwa mzazi

Kwa mujibu wa mtazamo huu wanaume hupata roho zao na miili yao kutoka kwa wazazi wao. Huu ndio Mtazamo wa kawaida katika Kanisa la Kilutheri, labda kama watumishi binafsi wakitofautiana lakini ni msimamo wao. Mtazamo huu hupata nguvu kutokana na ukweli kwamba hakuna chochote kinachosemwa juu ya uumbaji wa roho ya Hawa. Wanadai kwamba Mungu aliacha kazi ya uumbaji tangu Mwanzo 2:2; na kwamba kuanzia hapo wazao wako kwenye viuno vya baba zao, (Mwa 46:26; Ebr. 7: 9, 10.) Kwa sababu hiyo inaashiria kwamba kuna uwezekano kwamba Hawa alipata roho yake kutoka kwa Adamu, na watoto wao kutoka kwa baba zao. (1 kor. 11: 8; Mwa. 2: 23) Berkhof

anasema

kwamba

“mtazamo

huu

unaonekana kuungwa mkono na mawazo kwamba kwa upande wa kila mnyama, vyote mwili na roho hupitishwa kutoka kwa wazee kwenda kwa wadogo, kwa urithi wa sifa za familia na upekee na hata kwa kurithi tabia mbaya,

26

na ufisadi wa dhambi, ambapo mambo haya ni ya kiroho.”11 Hata hivyo, mtazamo huu una changamoto nyingi. Kukubaliana nao inabidi ukubali kwamba wazazi ni waumbaji wa wanadamu. Changamoto nyingine ni kwamba

mtazamo

huu

hudhania

kuwa

roho

ya

mwanadamu inaweza kugawanywa katika sehemu mbali mbali. Mbaya zaidi, mtazamo huu huhatarisha kutokuwa na dhambi kwa Yesu kwa kushikilia kwamba Yesu alipata roho yake kutoka kwa Mariamu. Bavinck

anatuambia

kwamba,

“watetezi

wa

mtazamo huu wanashindwa kufasili asili ya roho wala urithi wa dhambi. Kila wanapojaribu kutatua maswali haya mara nyingi huishia kwa kurudia mawazo kwamba roho za watoto huwa kwa wazazi na mababu au kwamba roho zilikuwepo katika uzao wa mwanamume au mwanamke au wote wawili. Lakini kamwe hawezi kuelezea kusambaa

11

Berkhof, Louis, Systematic Theology (Grand Rapids: Eerdmans) 1974, uk. 214

27

kwa dhambi ulimwenguni.”12mtazamo huu ulishikiliwa pia na Tertullian (160-220) na Gregory na Nyssa (330-395) 2.3.

Mungu huumba roho moja moja

Mtazamo huu uunashikilia kwamba Mungu huumba roho au nafsi ya kila kiumbe. Kwa kuwa uhai wa mwanadamu upo katika roho yake, na mpaji wa roho ni Mungu, basi kila mtoto anayezaliwa anapewa roho yake, si kwamba anaridhi kutoka kwa wazazi wake, na si kwamba roho yake ilikuwa imeumbwa tayari. Wanadai kwamba nafsi inapoumbwa huwa ni safi kabisa, lakini inapoingia katika mwili wa mwanadamu huchafuliwa na kurithi hali ya dhambi. Mtazamo huu unashikiliwa na wanarefomati wengi. Mtazamo huu hupata nguvu na ukweli kutoka kwenye Maandiko yanayodai kwamba mwili na roho ya mwanadamu huwa na asili tofauti, Mhu. 12: 7; Isa. 42: 5; Zek. 12: 1; Ebr. 12: 9. Kwa kweli mtazamo huu unalinda zaidi kutokuwa na dhambi kwa Yesu Kristo, kwa kusisitiza kwamba roho ya Yesu ililindwa na kutokuchafuliwa 12

Bavinck, Herman. Reformed Dogmatics (p. 336). Baker Publishing Group. Kindle Edition.

28

kamwe kwa kuwa ilitoka kwa Mungu moja kwa moja. Hata hivyo, Mtazamo huu nao haukosi changamoto, Haufafanui urithi wa tabia za kifamilia, na inaweza kuonekana kumfanya Mungu kuwa Muumbaji wa roho zenye dhambi. Ubora wake ni kwamba “Mtazamo huu hutosheleza upekee maalum wa kila binadamu na thamani ya binadamu na utu wa kibinafsi wa kila mtu. Sisi ni mawe yaliyo hai ya hekalu la Mungu, kila moja ana hatima yake binafsi.”13 Mtazamo huu ulishikiliwa pia na John Calvin, Thomas Aquinas na Jerome. Binafsi, japokuwa mtazamo huu una udhaifu wake, nakubaliana na maelezo yake kwa sehemu kubwa.

13

Bavinck, Herman. Reformed Dogmatics (p. 339).

29

SURA YA TATU

ANGUKO LA MWANADAMU 1. Kiini ch Anguko Biblia

inatufundisha

kwamba

dhambi

iliingia

ulimwenguni kama matokeo ya kosa la Adamu na Hawa katika Bustani ya Edeni. Dhambi ya kwanza ilisababishwa na jaribu la Shetani aliyekwenda kwa umbo la nyoka. Alichokifanya Shetani ni kwamba alipanda ndani ya moyo wa Hawa mbegu ya kutoaminiana wao kwa wao na kutokuamini neno la Mungu. Maandiko yanaonyesha wazi kwamba nyoka, ambaye anaonekana kama mjaribu katika hadithi ya anguko, alikuwa chombo cha Shetani, (Yn 8:44; Rum. 16:20; II Kor. 11: 3; Ufu. 12: 9.) Hii haimaanishi kwamba nyoka ni Shetani, bali alitumika kwa chambo kwa ajili ya kumfanya mwanadamu kutilia mashaka ahadi za Mungu, atilie shaka agano lake na Mungu. Dhambi ya kwanza ilikuwa ni kwa mwanadamu kula matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya. Kula 30

huku ilikuwa dhambi kwa sababu Mungu alikuwa amekataza. Kwa kweli, kama tulivyobainisha hapo juu kwamba mti wa ujuzi wa mema na mabaya ulikuwa ni mti wa kawaida tu, lakini Mungu alikataza; kiagano tumesema kwamba hicho ndicho kilikuwa kigezo cha agano au kwa lugha nyingine “amana” ya agano. Kwa kuwa mwanadamu alikula matunda hayo, basi alivunja agano lake na Mungu. Katika hadithi ya anguko kuna jambo la kushangaza sana. Mwanzo 3:4-5 inasema, “Nyoka akamwambia mwanamke, Hakika hamtakufa, kwa maana Mungu anajua ya kwamba siku mtakayokula matunda ya mti huo, mtafumbuliwa macho, nanyi mtakuwa kama Mungu, mkijua mema na mabaya.” Ukiangalia katika fungu hili hakuna mahali ambapo Shetani alimwambia Hawa kula matunda, lakini alichokifanya ni kutilia shaka neno la Mungu. Na hivyo ndivyo ambavyo Shetani hufanya siku zote; huweka mashaka maishani mwetu ili tujione hatuko salama, na hapo yeye hafanyi kitu chochote kile, lakini matokeo ya kutilia shaka neno la Mungu ni kuanguka katika mtego wake. 31

Matokeo ya mtego wa Shetani ni kwamba Hawa alichuma matunda, akala, na akampa mume wake, Adamu, naye akala. Matokeo ya tendo hili yalikuwa kama ifuatavyo: Walihisi hatia na aibu, na hivyo walijaribu kujificha mbele za Mungu. Mungu aliachilia adhabu kwa nyoka, kwa mwanamke na kwa Adamu na matokeo yake walifukuzwa katika Bustani ya Edeni ili wasije wakala matunda katika mti wa uzima na kuishi milele wakiwa wenye dhambi. (Mwa. 3:22) Kilichotokea

kwenye

anguko

la

mwanadamu

lilikuwa ni jambo la kusikitisha. Mwanamke alidanganywa na shetani kilaini sana kwa kutilia mashaka neno la Mungu. Baada ya nyoka kumweleza Hawa matokeo ya kula matunda, pengine alichakata kwenye akili zake akaangalia faida na hasara, na baada ya kuona faida ni nyingi, kupitia kwa msukumo wa hamu akala. Huu ulikuwa ukiukaji wa wazi wa amri ya kimungu. Hawa “alimpa pia mumewe naye akala.” Adamu bila kusita au kuhoji, alikubali mara moja matunda kwa faida ya mkewe. John Miley anasema kwamba pengine kuna ukweli fulani ambao ulirukwa na mwandishi kuhusu kula tunda kwa 32

Adamu, kwa sababu maelezo kuhusu anguko lake ni mafupi mno ukilinganisha na yale ya Hawa, lakini bado anapewa wajibu mkubwa kwa dhambi.14 Dhambi ni uasi (1 Yoh.3:4). Adamu na Hawa waliasi sheria ya Mungu, walitumia vibaya uhuru wao wa kuamua. Halikuwa jambo la kusahau kama wanavyodai Waislamu kwamba “dhambi ni kusahau.”15 2. Miti ya Aina Mbili Kuna kila haja ya kuelezea kwa uchache juu ya miti iliyokuwepo katika bustani ya Edeni. Nimeeleza hapo nyuma kwa habari ya mti wa Ujuzi wa mema na mabaya, ambao ndio unaonekana kuhusishwa na anguko. Hata hivyo tunapaswa kukumbuka kwamba katika Bustani ya Edeni kulikuwa na miti ya aina mbili maalumu 1) mti wa uzima (2) mti wa ujuzi wa mema na mabaya. Kwa kweli miti hii yote imeongelewa katika anguko. Ule mti wa kwanza, yaani “mti wa uzima” Mungu hakuzungumzia kwa sababu hakuhitaji kufanya hivyo. Adamu na Hawa 14

Miley, John. Systematic Theology (hakuna mchapishaji, wala mji) Uk. 288 Bennett, Mathew Aaron, 40 Questions about Islam (Grand Rapids: Kregel Academic, 2020) uk. 135 15

33

walikuwa na uzima tele ndani yao. Mti huo ulipata upekee baada ya anguko. 2.1.

Mti wa uzima

Mti wa uzima katika Mwanzo 2:9 ulikuwa ni alama ya uhai. Mungu hakuwazuia Adamu na Hawa kula matunda ya mti wa uzima. Sheria ya kutokula tunda iko katika Mwanzo 2:17 “walakini matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya usile, kwa maana siku utakapokula matunda ya mti huo utakufa hakika.” Mti huu ulikuwa chanzo cha uzima, kwa hiyo Adamu na Hawa wakiwa katika Bustani ya Edeni walikuwa na uzima tele na walifurahia maisha yao. Kuna mawazo kwamba mti huo alikuwa Yesu mwenyewe16 Maandiko yanayochukulia ni pamoja na: Ufu. 2:7 “…Yeye ashindaye, nitampa kula matunda ya mti wa uzima, ulio katika bustani ya Mungu.” Ufu. 22:2 “katikati ya njia kuu yake. Na upande huu na upande huu wa ule mto, ulikuwapo mti wa uzima, 16

Hodge, Charles, Systematic Theology – (Vol. III) (Grand Rapids, MI: Christian Classics Ethereal Library,) uk.132

34

uzaao matunda, aina kumi na mbili, wenye kutoa matunda yake kila mwezi; na majani ya mti huo ni ya kuwaponya mataifa.” Ufu. 22:14 “Heri wazifuao nguo zao, wawe na amri kuuendea huo mti wa uzima, na kuingia mjini kwa milango yake.” Ufu. 22:19 “Na mtu ye yote akiondoa lo lote katika maneno ya unabii wa kitabu hiki, Mungu atamwondolea sehemu yake katika ule mti wa uzima, na katika ule mji mtakatifu, ambao habari zake zimeandikwa katika kitabu hiki.” Katika mafungu hayo, kuna dalili za kuamini kwamba huo mti ni Yesu Kristo, lakini kuna kila uwalakini wa kukataa pia kwamba siyo Yesu. Kwa mfano Ufu. 2:7 haielekei kutushawishi kwamba ni Yesu, kwa sababu hayo maneno ni ahadi ya Yesu kwa washindi. Ufu. 22:2 na 14 zinaashiria kuwa ni Yesu kwa sifa alizo nazo. Lakini ufu. 22:19 inashindwa kuonyesha kwamba ni Yesu. Kwa hiyo tunachoweza kusema kuhusu mti huu ni kwamba ulikuwa ni mti maalumu kwa uhai wa mwanadamu, na ulikuwa ni 35

chanzo cha uzima. Tunashindwa kuthibitisha moja kwa moja kwamba ni Yesu, lakini pia Yesu anahusiana na mti huu kwa namna fulani. Kwani ni dhahiri kwamba Bustani ya Edeni ilikuwa ni alama au picha ya mbinguni ambayo inazungumziwa katika Ufunuo, na hivyo mti uliokuwa katika kitabu cha Mwanzo yamkini ulikuwa unalinda uzima wa Adamu na Hawa. Yesu Kristo anatoa uzima kwa wale wamwaminio, “Mimi nalikuja ili wawe na uzima, kisha wawe nao tele.” (Yn. 10:10) 2.2.

Mti wa Ujuzi

Mti huu ulikuwepo katika Bustani ya Edeni na ulikuwa ni mti wa ujuzi wa aina mbili; ujuzi wa mema, yaani kujua kwamba hili ni jema. Na ujuzi wa mabaya, kujua kwamba hili ni baya. Adamu na Hawa hawakuhitaji kula matunda katika mti huu kwa sababu (1) Mungu alikuwa amekataza wasile na kama wakila watakufa hakika (2) hawakuhitaji ujuzi wa kujua mema na mabaya kwa sababu Mungu alikuwa amewafunulia ujuzi wake.

36

Hodge anasema kwamba, “Mti wa ujuzi ulimpa Adamu maarifa ambayo hakuwa nayo hapo awali...”17 Pengine anachukulia hivyo kwa sababu, baada ya Adamu na Hawa kula matunda ya mtu huo, Mungu baadaye alisema, “Basi, huyu mtu amekuwa kama mmoja wetu,

kwa kujua mema na mabaya; na sasa asije akanyosha mkono wake akatwaa matunda ya mti wa uzima, akala, akaishi milele.” (Mwa. 3:22). Kwa kuwa mwanadamu alikuwa ameasi tayari, angekula matunda ya mti wa uzima angeishi milele na dhambi. 3. Dhambi na Kuenea Kwake Tunajua matokeo ya kutokutii kwa Adamu na Hawa kwamba kuanzia hapo dhambi iliingia ulimwenguni. Kwa hiyo, “kwa kuwa Adamu na Hawa ni shina la wanadamu wote, hatia ya dhambi hii ilipitishwa kwa wanadamu wote ambao ni uzao wao kwa asili na wamerithi kifo katika dhambi na asili ileile ya uchafu. Dhambi zote za kutenda [au dhambi halisi] zinatokana na dhambi hii ya asili, uchafu ambao unatufanya tushindwe kabisa kufanya 17

Hodge, Charles, Systematic Theology – (Vol. III) (Grand Rapids, MI: Christian Classics Ethereal Library,) uk.134

37

mema, na hatutaki kabisa kufanya mema. Kwa kweli, tunapinga mema yote.” (WCF/6/3-4/.) Dhambi inaelezewa kwa usahihi na maandiko kama "uasi" 1 Yohana 3:4. Ni kushindwa kufuata sheria ya Mungu. Biblia huiangalia dhambi kila wakati katika uhusiano na sheria, (Rum. 1: 32; 2: 12-14; 4:15; 5:13). Wanadamu wote wana hatia katika Adamu, na kwa hivyo wamezaliwa na asili ya ufisadi. (Ayu. 14:4; Yer. 17:9; Isa. 6:5; Rum. 8: 5-8; Efe. 4:17-19). Dhambi inakaa moyoni mwa mwanadamu na huathiri mtu mzima. Tunatofautisha dhambi ya asili na dhambi halisi. Wanadamu wote wamezaliwa katika hali ya dhambi ambayo huitwa dhambi ya asili, na ndio mzizi wa dhambi zote ambazo zinatendwa. 3.1.

Dhambi ya Asili

Dhambi ya asili ni pamoja na hatia na uchafu wote wa rohoni. Hatia ya dhambi ya Adamu imewekwa kwa wanadamu wote wanaozaliwa kupitia Adamu kwa sababu Adamu alitenda dhambi. Na kama mwakilishi wetu tuna hatia ndani yake. Wanadamu wanarithi uchafu wake, na 38

sasa tunatamani kuelekea dhambi. Mwanadamu kwa asili ni mchafu kabisa. Hii haimaanishi kuwa kila mwanadamu ni mbaya kama alivyo, lakini kwamba dhambi imeharibu kila sehemu ya maumbile yake na kumfanya ashindwe kufanya mema yoyote ya kiroho. Bado anaweza kufanya vitu vingi vyenye sifa kwa uhusiano na wenzake, lakini hata kazi zake nzuri ni zenye kasoro kubwa, kwa sababu hazijaongozwa na Mungu na wala hazitokani na utii wa sheria ya Mungu. Wanadamu wanaookolewa kupitia Kristo, asili yao iliyochafuliwa inabaki ndani yao wakati wa maisha haya, hata baada ya kuokoka. Ni dhahiri kwamba ingawa tumesamehewa kupitia Kristo, uchafu wa dhambi na athari zake zote bado zipo, na tunaona madhara yake katika maisha yetu ya kila siku. 3.2.

Dhambi halisi

Dhambi halisi ni dhambi ambazo tunatenda kila siku. Hata hivyo haimaanishi tu dhambi zilizo na matendo ya nje, lakini pia “mawazo, matamanio, na maamuzi ambayo hutokana na dhambi ya asili. Wakati dhambi ya 39

asili ni moja, dhambi halisi ni nyingi.”18 Inaweza kuwa dhambi za ndani, kama vile kiburi, wivu, chuki, tamaa za mwili au dhambi za nje, kama vile udanganyifu, wizi, mauaji, uzinzi, na kadhalika. Kati ya hizi kuna dhambi moja isiyosamehewa, yaani, dhambi ya kumkufuru Roho Mtakatifu, ambapo katika hiyo mabadiliko ya moyo hayawezekani, na hatuwezi kuomba kwa ajili mtu aliyetenda dhambi kama hiyo. (Math, 12:31, 32; Mk. 3: 28-30; Lk 12:10; Ebr. 6: 4-6.) Kwa hiyo dhambi halisi ni zile ambazo tunatenda kila siku, kila saa, kila dakika. Ingawa tumesamehewa, lakini udhaifu wa mwili na tamaa mbaya ambazo chanzo chake ni dhambi ya asili ambayo inatoka kwa wazazi wetu wa kwanza, Adamu na Hawa, basi tunaendelea kufanya hivyo. Ashukuriwe Mungu ambaye ndani yake kila siku anatusafisha kupitia kazi ya Roho Mtakatifu. Kwa

ujumla,

Biblia

inafundisha

kwamba

mwanadamu ni mwenye dhambi tangu kuzaliwa, Hata watoto wachanga wanachukuliwa kuwa wenye dhambi, 18

Berkhof, Louis, Systematic Theology (Grand Rapids: Eerdmans) 1974, uk. 268.

40

kwa kuwa wanakabiliwa na kifo, ambacho ni adhabu ya dhambi. Wanadamu wote kwa asili wamehukumiwa, na wanastahili hukumu kwa sababu ya dhambi. Mungu hahurumii dhambi, dhambi ni chukizo mbele za Mungu. Kwa hiyo, anguko ni kwamba sasa tumefungwa na dhambi. na kamwe kwa nguvu zetu hatuwezi kutoka, mpaka aje mwenye nguvu zaidi kuishinda dhambi. Wateule wamesamehewa dhambi ya asili milele; Mungu hawahesabii dhambi hii kwa sababu ya kazi ya Yesu Kristo pale Msalabani. Hata hivyo, wao sio wakamilifu; ingawa wanajitahidi kutokutenda dhambi, lakini bado wanatenda kwa sababu kamwe katika maisha haya hawawezi kuwa wakamilifu. Somo hili liko katika mada ya Soteriolojia. 4. Dhambi kubwa na Ndogo Kumekuwepo na mijadala kadhaa kuhusu dhambi; wapo wanaoamini kwamba dhambi zote zinafanana, hakuna

dhambi

kubwa

na

ndogo,

huku

wengine

wakisisitiza kwamba kuna dhambi kubwa na kuna dhambi ndogo. Akizungumzia uainishaji wa dhambi, Hoekema 41

anasema kwamba kuna aina mbalimbali za dhambi ambazo ni hatari sana. Mwenyewe anakiri kwamba uainishaji huu ni wa kizamani sana; anabainisha "dhambi saba mbaya, wakati mwingine anaziita “dhambi kuu.” Huku akiweka “kiburi, tamaa, wivu, uchoyo, hasira kuwa miongoni mwa dhambi hizo.19 Kwa uainishaji huu, wanaoshadidia mtazamo huu wanamini kwamba kuna dhambi kubwa na ndogo. John Calvin, akinukuliwa na Hoekema anasema kwamba Biblia inapinga dhana ya kutofautisha kati ya dhambi ndogo na dhambi kubwa.20 Anarejelea kitabu cha Wagalatia

3:10

kwamba

“…amelaaniwa

kila

mtu

asiyedumu katika yote yaliyoandikwa katika kitabu cha Torati ayafanye.” Kwa kifungu hicho Calvin anaona kwamba dhambi zote ni hatarishi katika maisha ya mwanadamu. Hata hivyo, wanaosema kwamba kuna dhambi kubwa na ndogo wanadai kwamba katika Maandiko kuna

19

Hoekema, A. Antony. Created in God’s Image, (Grand Rapids: William B Eerdmans, 1986) Uk.177 20 Hoekema, A. Antony. Uk. 178

42

watu ambao watapigwa sana na wengine watapigwa kidogo katika siku ya Hukumu. Wanasema, kwa mtu ambaye anayajua mapenzi ya Mungu na asiyafanye, huyu atapigwa sana. (Lk 12:47) Berkof anatabanaisha kwamba dhambi ambayo imetendwa kwa ufahamu kamili ni tofauti sana na dhambi ambayo inatendwa pasipo kujua.21 Vilevile

wanarejelea

dhambi

isiyosameheka,

ambayo ni dhambi ya kumkufuru Roho Mtakatifu. (Mat.12:31-32) Ambapo mtu anayetenda dhambi kama hii Wakristo hawaruhusiwi kumwombea, wala kuomba kwa ajili yake (1 Yoh. 5:16). Tukisoma katika WLC/151/ inasema “makosa yote ya sheria ya Mungu hayana uzito sawa kwa maana ya kwamba kuna dhambi zingine ambazo zina uzito mkubwa mbele za Mungu kuliko dhambi nyinginezo.” Maandiko yaliyonukuliwa ni pamoja na Yn.19:11; IYoh. 5:16. Ukiendelea kusoma katika swali linalofuatia, kuna mazingira ambayo yanatofautisha dhambi; kwa mfano Kutoka kwa wale ambao wamefanya dhambi hizo, kutoka 21

Berkhof, Louis, Systematic Theology (Grand Rapids: Eerdmans) 1974, uk. 252

43

kwa wale waliotendwa, kutoka kwenye asili na namna dhambi hiyo ilivyo, na kutokana na hali ya wakati na mahali. Kwa kweli, kwa namna fulani kuna uzito katika dhambi fulanifulani kama ambavyo WLC imebainisha. Kwa mfano kama dhambi imetendwa na mtu aliye ndani ya madaraka, matokeo yake yanaweza kuwadhuru watu wengi. Dhambi ambayo imetendwa na mchungaji haiwezi kufanana na dhambi ambayo imetendwa na mshirika wa kawaida kanisani. Ninachojaribu

kuelezea

hapa si

kuhalalisha dhambi, bali ni kuangalia matokeo ya dhambi yenyewe. Kwa mfano kama mchungaji akitenda dhambi kanisani inawezekana kabisa watu wengi wanaweza kuhama kanisa hilo, lakini kama akitenda muumini wa kawaida watu wataendelea kuwepo tu, na pengine wengine hawatajari. Hata hivyo, huku nikikubaliana na dhana kwamba kuna dhambi kubwa na ndogo, niko makini pia kubainisha kwamba kila dhambi inastahili hukumu mbele za Mungu. Niungane na WLC/152/Kisw. Kwamba “Kila dhambi; 44

kubwa au hata ndogo, ikiwa kinyume na mamlaka ya Mungu, wema wake, na utakatifu wake, na pia dhidi ya sheria ya haki yake inastahili ghadhabu na laana ya Mungu, katika maisha haya, na hata yale yajayo; na haiwezi kumalizwa na kitu chochote zaidi ya damu ya Kristo. 3. Kifo Tunapozungumzia ukomo wa mwanadamu maana yake tunazungumzia kifo. Labda niweke wazi tu kwamba kifo siyo ukomo wa uhai wa mwanadamu. labda tujiulize, kifo ni nini? Biblia huelezea kifo kama kutenganishwa, yaani kifo cha kiroho ambacho ni kutenganishwa kati ya roho ya mwanadamu na Mungu; katika Bustani ya Edeni, Adamu na Hawa walitenganishwa na Mungu, uhusiano wao ukaharibika. Katika kifo hiki mwanadamu hakuwezi kumkaribia tena Mungu, isipokuwa Mungu alikuja kwa mwanadamu. Hata hivyo, kifo hiki cha kwanza watu wengi sana hawakijui, wanajua kifo cha pili ambacho ni Kutenganishwa kati ya Mwili na roho.

45

Mtu ni mchanganyiko kati ya mwili na roho, Biblia inasema kwamba mtu anapokufa roho humrudia Yeye aliyeitoa, yaani Mungu, na mwili hurudia mavumbi ya ardhini. Hicho ndicho kifo. (Mh. 12:7) 3.1.

Kinachotokea baada ya kifo

Kuna mawazo kadhaa kuhusu nini kinatokea baada ya mtu kufa, hasa kwenye suala la mwili na roho. 3.1.1. Ukomo wa Uhai Hawa wanashikilia kwamba kifo inamaanisha “ukomo wa uhai.” Wanadai kwamba mtu ni “maada” (matter) kwa hiyo mtu akifa, basi kila kitu kinakuwa kimeishia hapo. Mwili ukishazikwa au kuchomwa, basi hapo ndipo mwisho wa uhai wa mwanadamu. Aliyeshadidia msimamo huu hapo zamani ni mwanafalsafa Epicurus aliyeishi kati ya mwaka 341-270K.K. Huyu alisisitiza kwamba watu hawahitaji kuogopa kifo kwa sababu kifo ni mwisho wa maisha, hakuna maisha mengine zaidi ya hapo, watu wanapaswa kufanya fujo zote duniani maadamu wanaishi kwa sababu hawatakuja kuona uhai tena. Mtu mmoja aliyejulikana kwa jina la Richard Dawkins aliwahi kusema 46

kwamba watu wanapaswa kuridhika kwamba waliwahi kuishi. Kile kitendo cha kujua kwamba wamewahi kuishi inatosha. Alisisitiza kwamba waliowahi kuishi wana bahati sana.22 Kwa kweli, mtazamo huu unaegemea kwenye mawazo ya kifalsafa sana, kwa kudhania kwamba maisha tunayoishi yana ukomo pindi tunapokufa. Misisitizo ya kwamba “tunaishi mara moja” imetawala mawazo ya watu wengi,

na

kupelekea

watu

kuishi

maisha

ya

kutokumpendeza Mungu kwa sababu hawana tumaini tena. Hakuna maisha baada ya kifo. 3.1.2. Mwendelezo wa Uhai Mtazamo huu unadai kwamba mtu ana sehemu mbili; mwili na roho. Mwili ukishakufa, hauwezi kufufuliwa tena, na hapo ndipo mwisho wake. Hata hivyo, roho haifi. Mwanafalsafa

wa

Kiyunani

Socrates

(470-399KK)

aliamini kwamba mwili ni gereza la roho. Socrates alitamani kifo cha kimwili ili roho yake ifunguliwe kutoka 22

Richard Dawkins, Unweving the Rainbow: Science, Delusion, and the Appetite for Wonder (New York: Houghton Miffilin, 1998

47

gerezani. Mtazamo huu pia ulishikiliwa na Mwanafalsafa Plato (428-348KK). Watu wengi, hata miongoni mwa Wakristo wanashikilia mtazamo huu. Inaaminika kwamba mojawapo ya watu walioshadidia katika makanisa ya Kiprotestanti aliitwa bwana Harry Emerson Fosdick. Yeye alisema kwamba “ninaamini katika kupata utu wangu kupitia kifo, lakini siamini katika Ufufuo wa mwili.”23 3.1.3. Kuangamizwa kwa roho na mwili kwa baadhi ya watu Mtazamo huu hudai kwamba kuna baadhi ya watu wachache watakoma kuishi na wengine wataangamizwa kabisa. Tofauti na ule mtazamo wa “ukomo wa uhai” mtazamo huu unaamini kwamba kuna watu waliookoka wataishi milele baada ya kufufuliwa. Wale waovu watakoma kuishi baada ya kifo chao. Katika mtazamo huu kuna ubora, hawa wanakubali kwamba wale waliookolewa wataishi milele, tatizo la 23

Harry, Emerson Fosdick, The Modern Use of the Bible (New York: Macmillan, 1924), 99

48

mtazamo

huu

ni

kuamini

kwamba

wale

waovu

wataangamizwa milele. Kwa mtazamo huu hakutakuwa na hukumu ya milele kwa waovu kwa sababu wataharibiwa na kuangamia milele. Kwao, hakuna mateso ya milele isipokuwa maisha ya furaha milele. Kwa mtazamo huu, basi mtu akishahukumiwa maisha ndiyo yameishia hapo. 3.1.4. Kulala kwa roho Ni mtazamo kwamba mtu akifa hawezi kujitambua na hivyo roho yake hulala kwa muda mpaka siku ya Ufufuo. Kulala huku ni kama mtu anayelala masaa mengi kwa siku moja na asijue kuna kitu gani kimeendelea katika usingizi wake, hivyo ndivyo lilivyo pengo kati ya kifo na Ufufuo. Wananukuu Maandiko kadhaa, kwa mfano Mhubiri 9:5, “kwa sababu walio hai wanajua ya kwamba watakufa; lakini wafu hawajui neno lo lote, wala hawana ijara tena; maana

kumbukumbu

lao

limesahauliwa.”

Na

pia

wanasoma Daniel 12:2, “Tena, wengi wa hao walalao katika mavumbi ya nchi wataamka, wengine wapate uzima wa milele, wengine aibu na kudharauliwa milele.” Kwa hakika watetezi wa mtazamo huu wanashindwa kuchukua 49

maandiko haya kwa kuzingatia miktadha yake. Watetezi wa mtazamo huu ni pamoja na Mashahidi wa Yehova na Wasabato. 3.1.5. Roho Kuvaa Mwingine Kuvaa mwili mwingine kwa kiingereza ni “reincarnation.” Watetezi wa mtazamo huu unadai kwamba roho ya mwanadamu haifi, na badala yake inapotoka kwenye mwili hutafuta umbo lingine la mwili. Huweza kwenda na kuwa mnyama, au hata binadamu mwingine. Mtu anayeishi maisha mazuri hapa duniani baada ya kufa anaweza kuendelea kuishi kama ng’ombe, mbuzi au hata mnyama wa aina nyingine yoyote ile kwa kuzingatia maisha yake aliyoishi. Huamini kwamba uhai huzunguka. Kuzaliwa-kufa-kuzaliwa. Wanaotetea mtazamo huu ni Dini ya Kihindi. Sababu kubwa ya Wahindi kutokula nyama ya ng’ombe ni imani kwamba wanaweza kumla babu yao ambaye ameshabadilika na kuwa ng’ombe. Watu wanaoishi vizuri katika maisha haya husadikika kuvaa mwili wa ng’ombe. Kwa maneno mengine mtu akifa, roho hutafuta mwili mwingine na kuzaliwa tena. Mambo haya 50

ukiyasoma unaweza usiamini lakini ndivyo wanavyoamini. Nilikuwa nasoma binti mmoja kutoka India jina lake Kate, alisisitiza kabisa kwamba mawazo haya yamo pia miongoni mwa baadhi ya Wakristo nchini India, na kwamba wanajaribu kuishi vizuri ili roho zao zivae mwili wa mwanadamu mwema. Mtazamo huu unafanana na hadithi ya Wabushimeni wa Afrika ambao wanaamini kuwa sio tu mimea na wanyama vina uhai, lakini pia mvua, ngurumo, upepo, chemchemi, nk. Wanadai kuwa tunachoona ni umbo la nje au mwili. Ndani kuna roho hai ambayo hatuwezi kuiona. Roho hizi zinaweza kuruka kutoka kwenye mwili mmoja kwenda kwenye mwingine. Kwa mfano, roho ya mwanamke wakati mwingine inaweza kuruka kwenda kwa chui; au roho ya mwanaume inaweza pia kuruka na kuingia ndani ya mwili wa simba.24 Kwa kweli, mtazamo huu hauna msingi wowote kutoka kwenye Maandiko Matakatifu, na kwa kweli, siku hizi unavutia watu wengi sana na kuhamaisha watu kupenda 24

Fahs and Spoerl 6.https://www.cs.williams.edu/~lindsey/myths/myths_14.html

51

Wanyama

kwa

sababu

baadaye

watakuwa

kama

Wanyama. 3.1.6. Roho na Mwili Hutengana na Kusubiri Ufufuo Mtazamo huu hudai kwamba roho au nafsi ya mtu anapokuwa huishi “katikati” ya hali ya kifo cha kimwili na Ufufuo. Mtu anapokufa, roho yake humtoka na kwenda katika ulimwengu mwingine (kwa mtu aliyeokoka huenda mbinguni kwa Mungu, na kwa mtu ambaye hajaokoka huenda Jehanamu). Wakati wa Ufufuo, miili na roho za watu wote zitaunganishwa pamoja tena na kuishi milele, mbinguni au Jehanam. Kwa kweli, mtazamo huu ndiyo mtazamo wa Kibiblia ambao tunaushikilia kuhusu “roho na mwili” wa mwanadamu. Roho au nafsi haifi kamwe, kwa sababu ni pumzi ambayo Mungu aliitoa na ikaungana na mwili. Pumzi ambayo Mungu aliitoa na kuungana na mwili, kamwe haiwezi kufa, na hivyo inaishi milele. Mungu ameweka Uzima wa milele na hukumu ya milele.

52

Ningependa kuhitimisha sehemu hii kwa kunukuu WCF/32/1-3/ Kwamba: “Miili ya wanadamu, baada ya kifo, inarudi kwenye mavumbi na kupata uharibifu; lakini roho zao zikiwa katika hali ya kutokufa, hurudi kwa Mungu ambaye alizitoa, roho za waadilifu, zikiwa zimekamilishwa kwa utakatifu, hupokelewa katika mbingu za juu, mahali wanapouona uso wa Mungu, kwa nuru na utukufu, wakingojea ukombozi kamili wa miili yao. Na roho za waovu hutupwa kuzimu, ambako hukaa kwenye mateso na giza nene, na kuhifadhiwa kwa ajili ya hukumu ya siku kuu. Kwa mujibu wa Maandiko Matakatifu, roho ambazo zimetenganishwa na miili yao zinaweza kwenda moja kwa moja kati ya mojawapo ya maeneo mawili - mbinguni au kuzimu. Siku hawatakufa,

ya

mwisho,

lakini

watakaokutwa

watabadilishwa.

wako

Watu

hai

ambao

wamekufa watafufuliwa na miili ileile (ingawa itakuwa na sifa tofauti), na miili yao itaunganishwa tena na roho zao, milele. 53

Miili ya waovu itafufuliwa na Kristo kwa ajili ya aibu yao. Lakini miili ya wenye haki itafufuliwa na Roho Mtakatifu kwa heshima, na itafanywa kuwa kama mwili wa Kristo uliotukuzwa.”

SURA YA NNE

MAMBO YANAYOJADILIWA KUHUSU MWANADAMU YAKIHUSISHA ASILI YAKE Kuna mambo mengi siku hizi yameibuka katika jamii ambayo kwa namna moja au nyingine yanahusishwa na asili ya mwanadamu pale alipoumbwa. Mambo hayo ni pamoja na “jinsi” na “jinsia,” “ndoa za zinazohusisha jinsi moja na mengine mengi. Katika sura hii nitajadili kwa uchache baadhi ya mambo haya. 54

1. Jinsi na Jinsia Maneno

haya;

jinsi

na

jinsia

yamekuwa

yakichanganywa sana katika matumizi yake. Wakati mwingine hata kwenye maandishi rasmi unaweza kukuta mkanganyiko huo. Jinsi ni zile tofauti za kimaumbile kati ya mwanamke na mwanaume. Jinsi ni kile kinachotufanya tutambue kwamba huyu ni mwanamke au mwanaume kwa maumbile yake ya asili. Lakini “jinsia” ni mgawanyo wa majukumu kati ya mwanaume na mwanamke. Ingawa “jinsia” huwekwa

na jamii

ambayo

mtu

anaishi.

Inasemekana kwamba mwanadamu anaweza kubadili “jinsia” lakini hawezi kubadili “jinsi” yake kwa sababu hiyo ameumbwa nayo, na hata kama akibadilisha, bado hali yake ya asili itabakia. Mawazo mapya ya ufeministi yamekuwa yakijaribu kuleta usawa wa kijinsia. Hivi karibuni kuna Biblia ambazo zimechapishwa zikielezea Mungu kama Mungu Mama ili kujaribu kuleta usawazisho wa kijinsia. Huku

55

wengine, kwa mfano Elizabeth Cady Stanton (1815-1902), aliweka wazi uaduni wake na Biblia.25 Wimbi la ufeministi lililoanza miaka ya 1960, lilichochewa na maandishi ya wanawake kama Simone de Beauvoir (1908-1986) na Betty Friedan (1921-2006).26 Maandishi haya yalijadili kwa undani majukumu ya wanawake

katika

ndoa

na

mama

kama

kiumbe

anayekandamizwa kwa asili, Kanisa limelaumiwa kwa kuongozwa na mfumodume. Na kwa sababu hiyo katika kipindi hiki cha mwamko wa usawa, ni vizuri kujiuliza maswali, je Mungu alimwumba mwanamume na mwanamke sawa? Je walikuwa na majukumu sawa? Je kuna nini ambacho kimetokea hapa katikati mpaka inafikia kundi moja likaonekana kunyanyaswa na kundi lingine?

25

Andreas J. Köstenberger and Margaret E. Köstenberger, God’s Design for Man and Woman: A Biblical-Theological Survey (Wheaton, IL: Crossway, 2014), 295– 301. 26 Simone de Beauvoir, Le Deuxième Sexe (Paris: Gallimard, 1949), kimepigwa chapa kwa kiingereza kama The Second Sex, trans. Howard M. Parshley (London: Jonathan Cape, 1953); and Betty Friedan, The Feminine Mystique (New York: Dell, 1964).

56

Kwa kweli hadithi ya uumbaji iko wazi kwamba Mungu aliumba mwanamume na mwanamke tofauti. Hili si suala la matakwa ya mtu kwa kile ambacho anataka kukisema, bali kile ambacho Biblia inasema. Biblia iko wazi kwamba Mungu alimwumba Adamu kwa mavumbi ya ardhi na kisha akampulizia pumzi ya uhai ndani yake (Mwa. 2:7). Vilevile Biblia inasema kwa habari ya uumbaji wa mwanamke katika Mwanzo 2:21-22 kwamba, “BWANA Mungu akamletea Adamu usingizi mzito, naye akalala; kisha akatwaa ubavu wake mmoja, akafunika nyama mahali pake, na ule ubavu alioutwaa katika Adamu BWANA Mungu akaufanya mwanamke, akamleta kwa Adamu.” Kwa hiyo

mwanamke aliumbwa tofauti,

aliumbwa kutoka kwenye ubavu wa Adamu. Ama kwa hakika Mungu alimpulizia pumzi ya uhai Hawa akawa hai na akamkabidhi Adamu. Adamu hakuletewa mtu mfu, alipewa mtu akiwa hai. Na Adamu anasifu uumbaji wa Mungu kwa kusema, “Sasa huyu ni mfupa katika mifupa yangu, na nyama katika nyama yangu, basi ataitwa mwanamke, kwa maana ametwaliwa katika mwanamume.” (Mwa. 2:23) 57

Ama tusichanganye hadithi ya uumbaji iliyo katika Mwanzo 1 kwa sababu hiyo inazungumzia kwa ujumla tu, lakini hadithi ya pili ya uumbaji inafafanua kwa undani kile ambacho haswa kilifanyika katika uumbaji wa mwanadamu katika ile siku ya sita. Tunakubaliana kwamba mwanamume na mwanamke waliumbwa na Mungu kila mtu kivyake. Kwa namna fulani ninakubaliana na maneno ya Macarthur J na Mayhue kwamba “majukumu kati ya mwanamume na mwanamke katika jamii, katika familia, na katika kanisa yana msingi wake katika tofauti kati ya mwanamume na mwanamke ambayo Mungu aliiweka katika uumbaji.”27 Lakini kwa namna fulani napingana nao kwa sababu jamii tuliyo nayo imechafuka, mwanadamu tangu anguko ameharibika kabisa, hawezi kusimama kwenye kusudi la Mungu, hata hivyo, Yesu Kristo, kupitia kanisa tunaweza kuona usawazisho wa kijinsia ambao ulipotea.

27

Macarthur J & Mayhue, R (Ed) A Systematic Summary of Biblical Truth: Biblical Doctrine (Wheaton, Illinois: Crossway, 2017) uk.426

58

Hata hivyo, ninakubali kwamba kuna majukumu ambayo yanapaswa kufanywa na wanaume, na kuna majukumu ambayo yanapaswa kufanywa na wanawake. Majukumu ninayozungumzia hapa si yale ambayo jamii imeyatengeneza, bali yale ambayo Mungu aliyaanzisha mwenyewe. Kwa mfano mwanaume hawezi kubeba mimba na kuzaa mtoto; hata hivyo mwanamke anaweza kubeba mimba na kuzaa mtoto, na hivyo kuendeleza uumbaji wa Mungu. Tangu anguko, uhusiano wa mwanamume na mwanamke uliiingia doa. Kila mtu alitaka kumtawala mwenzake tofauti na jinsi ambavyo Mungu aliwaumba. Baada ya anguko, Adamu na Hawa walianza kulaumiana. Mwanadamu akaanza kujiingiza katika ndoa za mitala. Katika Mwanzo 4:19 tunasoma, “Lameki akajitwalia wake wawili, jina la wa kwanza ni Ada, na jina la wa pili ni Sila.” Courson anafafanua kwamba “Ada” inamaanisha "pambo." Zila inaweza kumaanisha "atongozaye" au "mchafu." Kwa hivyo Caurson anahitimisha kwamba inaweza kuwa Zila alimtongoza Lameki. Au inaweza kuwa baada ya Lameki kuchukua wake wawili, mmoja akawa 59

mzuri, mwingine akawa mbaya machoni pake.”28 Kwa hiyo utamaduni huo uliendelezwa hata kwa wapendwa wengine wa Mungu, hiyo haimaanishi kwamba Mungu alihalalisha mwanaume kuoa wake wawili; tangu mwanzo Mungu aliumba mwanamume mmoja na mwanamke mmoja. Ndoa za mitala ni matokeo ya dhambi katika maisha ya mwanadamu, yaani tamaa ya tendo la ndoa. Itoshe kusema kwamba wanadamu kwa sababu ya dhambi, wametengeneza matabaka katika jamii, ikiwemo matakaba ambayo yanakandamiza upande mmoja. Jamii ndiyo inayosema kwamba mwanamke apike, afue, asafishe nyumba, na pia mwanaume atafute chakula, ajenge nyumba na mengine mengi. Haya yote yametengenezwa na jamii, na tumeyafanya kuwa sehemu ya Maandiko Matakatifu, na kudai ndiyo Injili halisi. Ni kweli kwamba jamii yoyote ile lazima iwe na mgawanyiko wa majukumu, hata hivyo mgawanyo huu haupaswi kukandamiza kundi lingine bali ufanyike kwa upendo wa Kimungu na kujitolea kwa wanafamilia. Mwanamke atendapo katika 28

Courson, Jon. Jon Courson's Application Commentary: Volume 1, Old Testament, (Genesis-Job) (p. 89). Thomas Nelson. Kindle Edition

60

familia, basi anapaswa kutenda kwa upendo na wala si kwa kukandamizwa. 1.1.

Nini maana ya kuwa “mwanaume”?

Ni swali ambalo ni kama la kizushi, lakini lina msingi wake katika uumbaji. Unaposikia fulani ni mwanaume unapata picha gani? Kila mtu huwa na picha yake kuhusu mtu kuitwa mwanaume. Kuna watu wengine hujaribu kutofautisha maneno haya, “mwanaume na mwanamume” lakini nafikiri maneno haya yana maana ileile tu. Yaani mtu mwenye jinsi ya kiume. Tunapogusa maeneo haya tunagusa masuala ya utamaduni pia, kwamba, je katika jamii tunazoishi watu humtambuaje mwanaume? Jamii nyingi za Kiafrika humtambua mwanaume kwa namna mbalimbali. Kwa mfano mtu anapokuwa na uwezo wa kuzalisha mwanamke, yaani akiweza kumfanya mwanamke

apate

“ujauzito”

basi

huyu

anaitwa

mwanaume. Na kama akishindwa kufanya hivyo, basi uanaume wake unaingia mashakani. Na jambo hili limesababisha wanaume ambao wake zao hawawezi 61

kupata

ujauzito

kutafuta

wanawake

wengine

ili

kuthibitisha uanaume wao. Ashakumu si matusi; mtu mmoja alisema kuwa inadhaniwa katika jamii nyingi kwamba, mwanaume ndiye anayebeba mbegu, mwanamke ni shamba tu; kwa hiyo ikiwa mwanaume na mwanamke watafanya mapenzi na mwanaume asifike mwisho kwa kutoa mbegu zake haihesabiki kwamba hilo ni tendo la ndoa.29 Mwanaume katika makabila mengine hutambulika kwa kutahiriwa na kuwa na uwezo wa kufanya mapenzi. Sherlock mwanaume

anabainisha hasa

uliochanganyikana

kwamba,

katika na

“kujitambua

mazingira

dhambi

ya

mara

kwa

utamaduni kwa

mara

umetambulika kwa neno “uume” au kwa Kigiriki “phallus” na hutambulika kama alama ya utambulisho na nguvu.”30 Jamii zingine zinamtambulisha mwanaume kama mtu ambaye anaweza kukabiliana na hali ngumu, na taabu katika maisha haya. Kwa sababu hiyo, hata mwanamke 29 30

Sherlock, Charles. The Doctrine of Humanity (Illinois: InterVarsity, 1996) uk. 208 Sherlock, Charles. The Doctrine of Humanity (Illinois: InterVarsity, 1996) uk. 204

62

ambaye anakabiliana na hali ngumu na kushinda watu husema, huyu ni mwanaume kwelikweli. Kwa hiyo utambuzi huu ni wa kijamii zaidi, ni jinsi jamii ilivyoamua kumtambulisha

mwanaume

ili

kumtofautisha

na

mwanamke. Utambuzi tuliojadili hapo juu ni wa kijamii; lakini kwa kweli Biblia inamtambua mwanaume kama kiumbe wa pekee wa Mungu aliyeumbwa kwanza, kabla ya mwanamke, akafanya Agano na Mungu, ambalo lilikuwa ni Agano la Matendo. Mwanamke aliingia kwenye Agano hilo kupitia Mwanaume. Adamu alipaswa kutii agano la Mungu lakini alishindwa kwa sababu alianguka. Ni kweli anguko linamhusisha mwanamke, kwani Biblia inasema “Wala Adamu hakudanganywa, ila mwanamke alidanganywa kabisa akaingia katika hali ya kukosa.” (1 Tim. 2:14). Tunachoweza kufafanua hapa ni kwamba

Adamu

hakudanganywa

kama

Hawa

alivyodanganywa na nyoka; lakini alishawishiwa na mkewe (Mwa 3:17) "alisikiliza ... sauti ya ... mke." Lakini katika

Mwanzo

3:13,

Hawa 63

anasema,

"Nyoka

alinidanganya." Hawa alidanganywa kwa urahisi sana, na yeye akadanganya kwa urahisi sana(2Kor 11: 3). Nyoka alijua kwamba Hawa alikuwa "chombo dhaifu" (1Pet 3: 7). Lakini cha ajabu ni kwamba katika Warumi 5:12, Adamu anawakilishwa kama mkosaji wa kwanza na kiongozi wa jamii iliyomwasi Mungu. Kabla ya dhambi, Adamu aliumbwa akiwa safi kabisa, bila dhambi yoyote, na alikuwa mkamilifu. Lakini baada ya dhambi akawa amechafuka. Yesu Kristo anaitwa Adamu wa Pili, ambaye alizaliwa bila dhambi kabisa, na wala hakutenda dhambi kabisa ili aweze kuwaokoa walio dhambini. Wakolosai 1:15 inasema “naye ni mfano wa Mungu asiyeonekana, mzaliwa wa kwanza wa viumbe vyote.” Adamu alipewa majukumu maalumu kama kiongozi wa mataifa. Agizo la “zaeni mkaongezeke...na kutawala” lilikuwa linamlenga Adamu na jamaa zake zote duniani. Adamu alitekeleza agizo hili, kwa sababu ya dhambi, hakuweza kutawala vizuri, na hivyo kushindwa kuvitawala baadhi ya viumbe kwa hofu ya kuuawa. 64

Pia tunasoma katika Waefeso 5:23 kwamba, “Kwa maana mume ni kichwa cha mkewe, kama Kristo naye ni kichwa cha Kanisa; naye ni Mwokozi wa mwili.” Hapa inaeleza wazi kwamba mume ni kichwa cha mkewe, (kama ana mke) na si kichwa cha mwanamke. Nasema hivyo kwa maana ya kwamba ni mwanamke aliye kwenye ndoa tu katika muktadha huu anaweza kujitiisha chini ya mume wake na si vinginevyo. Kuna wanaume wanadai wanawake wamewekwa chini ya wanaume jambo ambalo si sahihi. Adamu wa kwanza anayewakilisha wanadamu, alipewa

mamlaka

juu

ya

ulimwengu

ulioumbwa

(Mwa.1:26). Baada ya kufufuka kutoka kwa wafu, Yesu Kristo aliinuliwa kwenye mkono wa kuume wa Mungu, na kupewa mamlaka juu ya vitu vyote (1 Kor. 15:27; Efe. 1: 20–22). kwa ufafanuzi huo, basi tunaweza kung’amua kwamba maana ya kuwa “mwanaume” ni zaidi ya vile ambavyo jamii inamtambua mwanaume. Ikiwa hivyo, je ni kweli kwamba bila mwanamke, mwanaume hajakamilika? 65

Ni swali gumu kulijibu kwa kifupi; Lakini kwa kudokeza tu ni kwamba Adamu aliumbwa kamili kabisa, Hawa naye aliumbwa mtu kamili. Kwa sababu hiyo tunaweza kusema kwamba utu wa mtu hauegemei katika uhusiano wake na mwenzi. Hatari ya kufikiri kwamba bila mwanamke, basi mwanaume

hawezi

kukamilika

inahatarisha

ukweli

kwamba Yesu hakuwa na mke. Wanaoshikilia mtazamo wa namna hii huenda mbali zaidi na kudai kwamba Yesu alikuwa na mke ambaye aliitwa “Mariam Magdalena.” Ni uongo unaojaribu kutetea hoja dhaifu. Ikiwa ni hivyo Kwa hiyo vipi kuhusu matowashi? Yesu alisema, “maana wako matowashi waliozaliwa hali hiyo toka tumboni mwa mama zao; tena wako matowashi waliofanywa na watu kuwa matowashi; tena wako matowashi waliojifanya kuwa matowashi kwa ajili ya ufalme wa Mbinguni...(Mat. 9:12). 1.2.

Nini maana ya kuwa “mwanamke.”?

Hili nalo ni swali ambalo ni kama la kizushi, lakini ni swali la msingi sana. Unaposikia neno “mwanamke” unapata picha gani? Katika ulimwengu huu ambapo kuna

66

mapambano ya haki za wanawake duniani maana ya mwanamke imeongezeka kuongelewa. Ulimwenguni, mwanamke ameonekana kuonewa, kudhulumiwa, kunyang’anywa haki zake. Ameonekana kuwa daraja la chini katika kila jambo. Jamii nyingi zimekuwa zikijadili masuala mbalimbali ya kuwakomboa wanawake. Duniani kuna siku ya wanawake, kuna mashirika mengi duniani yanayoshughulikia haki za wanawake kuliko haki za wanaume. Kwa kweli hali si nzuri, kwa mfano nchini Saudi Arabia ni hivi karibuni tu wanawake wameruhusiwa kuendesha magari, kabla ya hapo

walikuwa

hawaruhusiwi

kuendesha

magari,

walikuwa wanaruhusiwa kuwa na leseni. Ukristo na Uislamu vimelaumiwa kuongeza tatizo hili, ingawa mimi naona tatizo hili liko katika jamii nyingi duniani. Watu wananyoshea kidole Ukristo na Uislamu kwa sababu hurejelea Maandiko katika kuhakikisha kwamba wanakandamiza haki za wanawake. Mwanamke amekuwa si kitu kupitia mahubiri kanisani na misikitini.

67

Turudi

kwenye

hoja,

nini

maana ya

kuwa

mwanamke? Katika jamii zetu, kuwa mwanamke ni kile kipindi cha kutoka usichana na kuwa mwanamke. Utambuzi huu ni finyu sana kwani wakati mwingine wasichana huitwa wanawake Mwanamke anaendelea kutambuliwa na jamii zetu pale anapokuwa na uwezo wa kubeba ujauzito na kuzaa mtoto. Jamii inamuona mwanamke ambaye hawezi kubeba ujauzito kama mwanamke ambaye hajakamilika; jamii inaona kama amepungukiwa kitu fulani. Mwanamke ni kiwanda cha kuzalisha watoto! Mwanamke kama chombo cha starehe, mwanamke kama mtunzaji wa mumewe, na hoja nyingine nyingi ambazo jamii zetu zimejiwekea. Kwa bahati mbaya sana, japokuwa mwanamke anaweza kubeba ujauzito na kujifungua watoto, hakuna katika Maandiko Matakatifu kwamba ambaye hawezi kufanya hivyo kwa matatizo ya kiafya, au kwa kuamua mwenyewe au kwa sababu zisizozuilika imeshindikana kuzaa hajakamilika. Kama wazo hili lingekuwa na ukweli, basi mtume Paulo asingeshauri wanawali kubaki bila kuolewa. Hebu tumwone Paulo anavyosema, “Basi, hivyo 68

na amwozaye mwanamwali wake afanya vema; na yeye asiyemwoza atazidi kufanya vema.” (1 Kor. 7:38). Ukisoma

mistari

iliyotangulia

fungu

hili

Paulo

anawashauri watu kubaki kama walivyo, hasa kwa ajili ya kujishughulisha na mambo ya Mungu. Mimi hapa sitaki kujadili suala la useja, lakini ninachojaribu kueleza ni kwamba, mwanamwali haitwi mwanamke aliyepungukiwa kwa sababu ya kutokuwa na watoto. Ni hakika kwamba mwanamke ndiye anayebeba ujauzito, na ndiyo njia ambayo Mungu anaitumia kwa ajili ya kuwaleta watu ulimwenguni. Hizi njia zingine za kisasa zina wakati wake wa kujadiliwa katika somo la Maadili ya Kikristo. Lakini si wanawake wote wanaweza kubeba mimba, na kushindikana kwa kubeba mimba kumeleta huzuni kubwa kwa wanawake wengi tangu zamani, ambao wanaona hakuna maana ya kuishi pasipo kuwa na mtoto. (Mwa. 29-30 na 1 Sam.1-2). Kitu

ambacho

Biblia

inatufundisha

kuhusu

mwanamke, kwanza kabisa ni kwamba anabeba mfano wa Mungu kama alivyo mwanaume. Mwanzo 1:27 inasema, 69

“Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu

alimwumba,

mwanamume

na

mwanamke

aliwaumba. Na baada ya hapo tunapata maelezo ya ndani kuhusu uumbaji wa mwanamke katika sura ya pili. Hakuna andiko

ambalo

linasema

kwamba

mwanamke

na

mwanaume wako tofauti kihadhi mbele za Mungu. Maelezo kuhusu uumbaji wa Hawa ni kwamba Mungu alimletea Adamu msaidizi wa kufanana naye. “BWANA Mungu akasema, Si vema huyo mtu awe peke yake, nitamfanyia msaidizi wa kufanana naye.” (Mwa. 2:18). Baada ya Mungu kumwumba mwanamke na kumkabidhi Adamu, Adamu alisema, “Adamu akasema, Sasa huyu ni mfupa katika mifupa yangu, na nyama katika nyama yangu, basi ataitwa mwanamke, kwa maana ametwaliwa katika mwanamume.” (Mwa. 2:23). Mfupa katika mifupa yangu ni usemi katika lugha ya Kiebrania ukimaanisha

“mwenzake

halisi,

mshirika

kamili,

mkusanyiko wake, kutoka kwake.”31

31

https://www.christiantruthcenter.com/biblical-meaning-of-the-word-man-andwoman-in-marriage/

70

Kitendo cha Mungu kuchukua ubavu, na wala si mguu,

wala

mikono

inamaanisha

kwamba

“Hawa

aliumbwa kutoka upande wa Adamu sawa naye, na karibu na moyo wake kuwa mpendwa kwake.”32 Bila shaka Biblia inaonesha kwamba hadhi yao mbele za Mungu ilikuwa sawa, ingawa majukumu yao yalikuwa tofauti. 2. Jinsi Siku hizi kumekuwa na mawazo mchanganyiko kwamba Mungu alipomwumba mwanadamu, hakuumba “jinsi” kwa hiyo mtu baada ya kuzaliwa anaweza kuchagua “jinsi” yoyote anayoitaka. Kwa maana ya kwamba mtu baada ya kuzaliwa, anaweza kuchagua kuwa mwanaume au mwanamke. Wafuasi wa mawazo haya wanatumia sababu ya watu wasio na jinsi au wenye jinsi mbili kwa wakati mmoja ili kuthibitisha mawazo yao. Ni kweli kuna watu ambao kibiolojia wana matatizo ya kiafya ya namna hiyo, lakini bado haiwezi kuthibitisha madai haya. Katika Maandiko kuna jinsi mbili; kike na kiume. Biblia haijataja mtu asiye na jinsi, ingawa kwenye jamii 32

Jamieson, and Brown Commentary, comment on Genesis 2:22

71

zetu wapo. Biblia inazungumzia habari za matowashi, ambao walijitolea wao wenyewe, na wengine ambao wamefanywa kuwa matowashi, lakini bado hatuwezi kusema kwamba mtu anaweza kuchagua jinsi anayopenda. Hata watu ambao hawana jinsi, bado wanaangukia katika mojawapo ya tabia mbili; za kike au za kiume au vyote kwa pamoja. Watu wengi duniani siku hizi wamebadilisha jinsi zao; wanawake wakawa wanaume na wanaume wakawa wanawake na wanaweza kushiriki mahusiano ya kindoa. Ni dhahiri kwamba mwanadamu anatafuta kila aina ya njia kuhalalisha uovu kupitia Maandiko. Ukweli usiopingika ni kwamba mawazo haya hayana msingi wowote kutoka kwenye Maandiko, ingawa watetezi wanajaribu kunukuu Mwanzo sura ya 1-2 kwenye hadithi za uumbaji, lakini bado hawavuti usikivu wa wengi.

Wanasema

kwamba

“Yesu

alitambua

jinsi

isiyokuwa ya kawaida pale alipokuwa akifundisha kuhusu talaka, alisema kuna wale waliojaliwa kuoa na wengine hapana kuoa, na hivyo alikuwa anaongelea watu wenye 72

jinsi tofauti.”33 Mawazo haya hayawezi kuthibitisha uwepo wa jinsi zaidi ya mbili. Tungependa kuhitimisha kwamba, Mungu aliumba jinsi mbili tu; kike na kiume. Mtu hawezi kuchagua kwamba awe na jinsi ya aina gani. Hata wale ambao wana jinsi za aina mbili au wale ambao hawana kabisa, bado hatuwezi kusema kwamba wanahalalisha mawazo haya, bali ni matatizo ya kiafya kama ambavyo wengine huzaliwa wakiwa na matatizo ya aina nyingine. Na yote haya ni kwa sababu ya uovu wa dunia. Jaribio lolote lile kubadilisha jinsi ni uovu wa mwanadamu unaotokana na dhambi ya asili na dhambi za kutenda. 3. Ndoa Ndoa ni umoja kati ya mwanamume na mwanamke iliyoanzishwa na Mungu kuwa ya kudumu muda mrefu maadamu wanandoa wote wako hai “Mume na Mke waliumbwa

kwa

ajili

ya

mahusiano

na

si

utengano.”34Mungu alichukizwa na upweke wa Adamu na 33

https://religiondispatches.org/god-made-them-male-and-femaleand-eunuch-why-the-biblical-casefor-binary-gender-isnt-so-biblical/ 34 Macarthur J & Mayhue. Uk. 427

73

hivyo akasema “si vyema mtu huyu awe peke yake, nitamfanyia msaidizi wa kufanana naye.” (Mwa. 2:18). Kwa hiyo Mungu alimfanyia Adamu “msaidizi.” Mungu aliwaumba mwanamume na mwanamke na kuwaagiza “zaeni mkaongezeke, na kuijaza nchi.” Lakini mwanadamu kwa kuwa ni kiumbe asiyefanana na mnyama yeyote, aliyeumbwa kwa mfano wa Mungu, anaingia katika zoezi zima la kuzaa kwa utaratibu maalumu, ambao kwa kweli ni utaratibu wa ndoa. Ndoa ilianzishwa kwa usaidizi wa pande zote, kwa mume na mke, kwa ajili ya usalama, na kukuza tabia yao ya maadili na ya kiroho kwa kuishi katika nidhamu na maagizo ya Bwana. Ama kwa hakika, ndoa inapaswa kuwa kati ya mume mmoja na mke mmoja, na si vinginevyo. Katika WCF/24/3 tunasoma “watu wote ambao wanaweza kuwa na uamuzi kwa idhini yao wenyewe wanaweza kuoa au kuolewa isipokuwa ndani ya mipaka ya uhusiano wa damu uliokatazwa na Maandiko, mtu hawezi kuoa ndugu yake wa damu, na ndoa ni halali mbele za Mungu

na

machoni

pa

kanisa ikiwa 74

imezingatia

mipaka.…” kwa hiyo mtu anapewa uamuzi wa kuoa ndani ya mipaka. Mara kwa mara watu hujiuliza, kwa nini nisioe au nisiolewe na dada au kaka yangu? Kwani Kaini aliona wapi? (hauna haja ya kuzungumzia Abeli kwa wakati huo kwa sababu alikufa bila kuwa na mtoto) Kwa kweli, Biblia haielezi kwa kina juu ya mke wa Kaini. Biblia pia haielezi umri wa Kaini wakati alipomuua ndugu yake Habili (Mwanzo 4:8). Kwa kuwa wote walikuwa wakulima, lazima walikuwa watu wazima. Adamu na Hawa walikuwa wamepata watoto wengine mbali na Kaini na Habili wakati Habili alipouawa. Walipata wengine baadaye (mwa. 5:4). Ile hali ya Kaini kuhofia usalama wake baada ya kumuua Habili (mwanzo 4:14) inadhihirisha kwamba kulikuwako na watoto wengi wengine pia na wajukuu na hata vitukuu wa Adamu na Hawa. Kwa kuwa Adamu na Hawa walikuwa wanadamu wa kwanza duniani, watoto wao hawakuwa na namna nyingine zaidi ya kuoana wao kwa wao. Mungu hakukataza kuoana kwa jinsi hii mwanzoni mpaka dunia 75

ilipokuwa na watu wengi. Sababu ya madhara ya ndoa za kaka na dada ni kuwa “kama kila mmoja wao alikuwa na hali fulani ya kilema cha kurithi basi atakayezaliwa atakuwa mwenye kurithi kutoka kwa wazazi wake, na hivyo basi kuwa hali mbaya zaidi kuliko waliomzaa. Lakini Adamu na Hawa hawakuwa na kilema chochote ndani yao kwa sababu walikuwa wazazi wa kwanza, na hivyo hakika walikuwa na afya njema sana kuliko zetu hivi sasa.”35 Sasa basi, ingawa ni kweli kwamba watoto wa Adamu na Hawa walioa dada zao wa damu, uhusiano kama huo hauruhusiwi katika Biblia (Mk 6:18, 1 Kor 5:1, Law. 18:6-18) 4. Rangi za Wanadamu Kwa kweli Biblia haisemi chochote kuhusu uumbaji wa mwanadamu akiwa katika rangi tofauti. Haielezi rangi tofauti zilianzia wapi, haielezi kwamba ngozi nyeusi, ngozi nyeupe na hata njano zimetoka wapi. Hata hivyo tunahitaji kuzungumzia hata kwa uchache habari za rangi miongoni mwa wanadamu.

35

https://www.gotquestions.org/Kiswahili/mke-kaini.html

76

Kuna mawazo kadhaa kuhusu rangi. Wengine wanadhania kuwa, wakati Mungu alipovuruga lugha katika mnara wa Babeli (Mwanzo 11:1-9) pia aliumba rangi tofauti. Mtazamo huu ingawa hauonekani kukubalika kwa asilimia mia, lakini si mbaya kufikiri kwamba pengine Mungu alifanya wanadamu kuzalisha chembe za rangi tofauti ili kuweza kuhimili mazingira walikokuwa wanaenda kutawanyika. Kwa mfano ngozi nyeusi kwa Waafrika ingewawezesha kukaa mahali pa joto kali. Kwa mujibu wa mtazamo huu, Mungu alichanganya lugha, na kuwafanya wanadamu kutawanyika kilugha pia, na hapo akaumba chembe chembe za damu tofauti kulingana ni wapi kikundi fulani cha watu kitaishi. Japokuwa mawazo haya yanajaribu kushawishi, lakini bado hakuna andiko linalozungumzia rangi. Baada ya gharika wakati lugha tofauti zilipoanza kuwepo, kikundi ambacho kilizungumza lugha moja kilijitenga mbali na wengine waliozungumza lugha moja. Kwa kufanya hivyo, chembe chembe za damu zikashuka pakubwa sana kwa vile hicho kikundi hakikupata kujumuika na wengine. Uzao wa karibu ulifanyika na 77

baada ya muda tabia fulani zikazingatiwa katika hivi vikundi tofauti. Uzao ulipoendelea zaidi katika vizazi, ule utofauti wa chembe chembe za damu ulipungua zaidi, hadi kiwango kwamba watu wa lugha ya familia moja wote walikuwa na tabia moja. Mawazo mengine ni kwamba Adamu na Hawa walikuwa na chembe chembe za damu na kuzaa rangi nyeusi, na nyeupe (na kitu chochote hapo katikati). Wanadai kwamba pengine jambo ni sahihi kwa sababu wazazi rangi tofauti huzaa watoto wa rangi tofauti (katikati). Kwa kuwa Mungu alikusudia mwanadamu awe na sura tofauti, inaleta maana kwamba Mungu huenda aliwapa Adamu na Hawa uwezo wa kuzaa watoto wa rangi tofauti. Baadaye, waliobaki pekee baada ya gharika mahali ambapo Nuhu na mke wake, watoto wake watatu wa kiume na wake zao, watu nane kwa jumla (Mwa. 7:13). Ingawa wakwe wa Nuhu walikuwa wa rangi tofauti. Labda inawezekana mke wa Nuhu alikuwa na rangi tofauti na ile ya Nuhu. Pengine wote nane walikuwa na rangi tofauti tofauti jambo ambalo linaweza kumaanisha kwamba 78

walikuwa na chembe chembe ambazo zingeweza kuzaa watoto wa rangi tofauti.36 Pamoja na kwamba hatuna maelezo ya kutosha kutoka kwenye Biblia, itoshe kusema kwamba watu wote, Waafrika, Waarabu, Wahindi, na Wazungu, na wengineo wengi si vizazi tofauti bali ni kabila mbalimbali za kizazi kimoja cha mwanadamu. Wanadamu wote wako na tabia sawa, bila tofauti yoyote hata ndogo ya uumbaji. Jambo la muhimu zaidi ni kwamba wanadamu wote wameumbwa kwa mfano wa Mungu (Mwa. 1:26-27). Wote wamefanya dhambi (Rum. 3:23), na wote wanahitaji mkombozi, ambaye ni Yesu Kristo. 5. ndoa za jinsi moja Mada ya ndoa za jinsi moja inashughulikiwa zaidi katika somo la “Maadili ya Kikristo.” Kwenye masomo ya Anthropolojia inagusiwa tu. Hata hivyo napendekeza wana Anthropolojia wajadili kwa undani suala hili badala ya kuliacha kwenye “Maadili.” Maana ya kuliacha kwenye 36

Kwa maelezo zaidi kuhusu rangi za watu tembelea: https://www.gotquestions.org/differentraces.html au https://ebible.com/questions/171-what-scripture-s-speak-on-why-god-made-peoplewith-different-skin-color au https://bible.org/question/why-are-people-differentcolors%E2%80%94black-yellow-brown-etc

79

maadili ni kwamba miongoni mwa Wakristo wanafikiri ni sawa kuwa na ndoa ya jinsi moja, huku wengine wakiona siyo dhambi. Ni suala la mjadala. Ninachoweza kusema kwa sasa ni kwamba Shetani amekuwa akijaribu kuharibu uumbaji wa Mungu na ndoa ambayo Mungu aliianzisha pale Edeni. Kumekuwepo na watu wanadai kwamba Mungu alipomuumba mwanadamu, hakuumba jinsi, na hivyo mwanadamu anaweza kuamua kuchagua jinsi anayoitaka yeye. Kwa sababu hiyo, tumekuwepo na ndoa za jinsi moja (mwanaume kwa mwanaume au mwanamke kwa mwanamke). Kwa kweli tatizo hili lilianzia pale Edeni, pindi Adamu na Hawa walipotenda dhambi waligundua kwamba wako uchi. Kabla ya hapo hawakugundua kwamba walikuwa uchi. Walipogundua kwamba walikuwa uchi wakashona mavazi ya majani kwa ajili ya kujifunika. Kitu ambacho hakikuwa cha aibu kikawa cha aibu. Baada ya hapo tamaa ilimwingia mwanadamu. Badala ya kupenda mke au mume wake anapenda mtu wa jinsi moja na anatamani kuoana naye. 80

Watetezi wa ushoga wanapinga Maandiko yote yanayokataza ushoga na kudai kwamba tafsiri zimekosewa kutoka kwenye lugha ya asili. Wanasisitiza kwamba maana ya awali haikuwa hivyo. Mara nyingi wanatumia maneno ya ujumla kama vile “Mungu anawapenda watu wote.” Mashoga hawafanyi dhambi yoyote iliyoandikwa kwenye Biblia. Watu hawa wamepata watetezi wakubwa ulimwenguni. Siku hizi baadhi ya makanisa ya Ulaya yanafunga ndoa za watu hawa kanisani bila shida yoyote. Siku hizi nchini Marekani huruhusiwi kupinga waziwazi suala la mashoga, bali unapaswa kuwakubali kama walivyo, kwa sababu hivyo ndivyo wamechagua kuwa, na ndivyo Mungu anavyotaka. Mitandao ya watetezi wa LGBT (Lesbian, Gay, Bisexual, Transgender) yaani Wanawake wapendao wanawake

wenzao

kimapezi,

wanaume

wapendao

wanaume wenzao kimapenzi, wanaopenda jinsia mbili na wabadilisha jinsia) imeenea duniani kote. Karibu katika kila lugha kubwa duniani, ikiwemo Kiswahili maandiko yao yanashadidiwa kwa hali ya juu sana. Kwa kweli ni vigumu kupata andiko la kuthibitish hoja zao zaidi ya 81

kusimama katika msingi wa haki za binadamu, jambo ambalo ni nyeti sana duniani katika kipindi hiki. Mtu mmoja anayejihusisha na mapenzi ya jinsi moja alisema hivi, “Kwa sababu sisi wote ni binadamu. Sisi si tofauti na wao. Tunaposema kuwa Tanzania ni ya umoja sisi tumo kati ya huo umoja. Tunalipa kodi kama wao na tunajenga nchi kama wao. Sisi si wahalifu.37 Matamshi kama haya yanaelekea kushika kasi katika jamii yetu. Kwa karibu miaka elfu mbili, makanisa yalipinga vitendo vya ushoga na kukiri wazi kwamba ni dhambi. Makanisa mengi ya Warefomati na wengineo wa Kiprotestanti hata sasa mengine bado yanafundisha kuwa ushoga ni ukiukaji wa sheria za Mungu. Lakini katika kipindi hiki, makanisa mengi yaliyo huru yamewakaribisha mashoga na wasagaji kwa kisingizio cha kuwaonyesha upendo wa Mungu. Watumishi wengi wamekuwa na kigugumizi kuhusu LGBT, jambo ambalo linahatarisha utakatifu wa kanisa.

37

https://rainerebert.com/2020/09/04/interview-the-lgbt-community-in-tanzania/

82

Ningependa kusema kwamba, kwa kweli huu ni upotovu wa mwanadamu, anguko la dhambi na matokeo yake

ndiyo

haswa

yanayosababisha

mambo

haya

yaendelee. Uchafu wa ndoa moja ulianza kitambo. Mungu alikuwa ameonya watu wake kujihusisha na mapenzi ya jinsi moja. Katika Walawi 18:22-23 anasema "Usilale na mwanamume mfano wa kulala na mwanamke; ni machukizo. Wala usilale na mnyama ye yote, ili kujitia unajisi kwake; wala mwanamke asisimame mbele ya mnyama ili kulala naye; ni uchafuko". Biblia lnasisitiza kwamba ushoga na usagaji ni dhambi (Mwa. 19:1-13; Rum.1:26-27; 1 Kor 6:9 Mwa.13:13;18:20). Kwa hiyo tunapaswa kupinga kwa namna yoyote ile ushoga na usagaji kwa sababu Mungu hakuumba mwanadamu mwenye tamaa ya ushoga naa usagaji. 4. Kifo cha Huruma (Uthanasia) Ingawa si jambo la kawaida katika utamaduni wetu wa Kiafrika, lakini ni jambo la msingi pia kulizungumzia hapa tunapojadili kuhusu mwanadamu. 83

Uthanasia hufafanuliwa kama"mauaji ya makusudi ya mtu anayeugua ugonjwa unaosadikiwa kuwa hauwezi kupona.38Waandishi wengine wanasema kwamba neno uthanasia linatokana na Kigiriki (eu + thanatos) na haswa lina maana "kifo kizuri." Kitendo hiki kufanyika kwa makubaliano ya ndugu na madaktari kwa kumchoma sindano ya usingizi mgonjwa ambayo itapelekea kifo chake. Wanaokubaliana na mawazo haya hudai kwamba si vizuri kumwacha mtu anateseka na ugonjwa ambao hauwezi kupona, na kwa hiyo ni bora kumpumzisha haraka. Wananukuu Maandiko kadhaa, “heri wafu wafao katika Bwana, tangu sasa. Naam asema Roho, wapate kupumzika baada ya taabu zao.” (Ufu. 14:13). Andiko hili halithibitishi kuondoa uhai wa mtu mwingine, ila linaonesha furaha kwa mtu anayemaliza mwendo wake hapa duniani. Wakati maisha ya mwanadamu ni zaidi ya kuwapo kwa kibaolojia, heshima kwa maisha ya mwili wa mtu 38

Davis, John Jefferson. Evangelical Ethics: Issues Facing the Church Today, 4th ed. . P&R Publishing. Kindle Edition

84

ndio kielelezo muhimu kwa heshima ya maisha yake kwa ujumla. Shida ya kutathmini thamani ya maisha ya mwanadamu kwa kutumia akili za kibinadamu ni kwenda kinyume na yule aliyeutoa uhai. Watetezi wa jambo hili pia hunukuu Mhubiri 3:3 kwamba “wakati wa kuua, na wakati wa kupoza.” Huamini kwamba kila jambo linapokuwa limefikia wakati wake, basi wale wanaohusika wanapaswa kuchukua hatua. Hivyo basi katika kumsaidia mtu kupunguza maumivu yake, basi ni bora kumsaidia kwa kumwondoa duniani. Kimaandiko, jambo hili linahesabika kama kujiua. Kwa hakika hakuna mtu anayeruhusiwa kujiua katika Maandiko Matakatifu. Kwa upande wangu naona kwamba uthanasia ni haipaswi kutekelezwa kwa sababu inakiuka amri ya "Usiue" (Kut. 20:13). Kuchukua uhai wa mwanadamu kwa sababu yoyote ni marufuku kabisa katika Maandiko. Hata hivyo kuna mazingira ambayo yanaweza kuruhisiwa ikiwa ni pamoja na kujilinda au adhabu ya kifo. Maisha ya mwanadamu ni matakatifu kwa sababu Mungu alimfanya mtu kwa mfano wake na kwa sura yake (Mwa. 1: 26-27). 85

Kwa mujibu wa Davis mawazo ya uthanasia humwona mwanadamu kama bwana wa maisha yake mwenyewe; Mkristo huona maisha ya mwanadamu kama zawadi kutoka kwa Mungu, na hivyo maisha yanafaa kushikiliwa katika udhamini katika maisha yote ya mwanadamu hapa duniani.39 Kwa hakika, kuamua wakati upi wa kufa ni haki ya Mungu, sio ya mwanadamu (Ayu. 14: 5). Mwanadamu hachagui kifo chake mwenyewe, lakini anakubali mapenzi ya Baba wa mbinguni, tukijua kuwa kwa Mwamini, kifo ni adui wa mwisho. Kwa sababu mwanadamu anayo sura ya Mungu, maisha yake ni matakatifu katika kila hali ya uwepo wake, kwa ugonjwa au kwa afya, tumboni, utotoni, katika ujana, katika ukomavu, katika uzee, au hata katika mchakato wa kufa. Kwa maelezo haya, utoaji mimba na kujinyonga ni dhambi mbele za Mungu, na uhai wa mwanadamu unapaswa kulindwa na kutunzwa kwa nguvu zote.

39

Davis, John Jefferson. Evangelical Ethics: Issues Facing the Church Today, 4th ed. . P&R Publishing. Kindle Edition.

86

HITIMISHO Mungu, katika siku ya sita, baada ya uumbaji wa viumbe

vingine

mwanamume

na

vyote,

alimuumba

mwanamke

mwanadamu,

aliwaumba.

Mungu

aliwabariki Adamu na Hawa na kuwaambia wazae na waongeze na kuijaza dunia, siyo kuijaza tu, na kuitiisha pia. Mungu alimwumba mwanadamu kwa sura na mfano wake, kwa maana ya kwamba mwanadamu anamwakilisha Mungu hapa duniani, ingawa Mungu yupo mahali pote. Kwa maelezo hayo, haimaanishi kwamba mwanadamu ni Mungu, ingawa yeye ni mfalme kwa vitu ambavyo vimewekwa chini yake, lakini Mungu ndiye mfalme wa vitu vyote, kwa sababu ndiye Bwana wa uumbaji wote. Mwanadamu amewekwa kwenye uhusiano wa aina tatu; kwanza uhusiano wake na Mungu, pili uhusiano wake na wanadamu wengine, tatu, uhusiano wake na viumbwa vingine. Kama mfano wa Mungu, mwanadamu alipaswa kukuza uhusiano huo na kuuendeleza zaidi na zaidi. Hata hivyo, mwanadamu alimwasi Mungu na matokeo yake alishindwa kuvitiisha viumbe vingine. 87

Wakati huo mwanadamu alikufa kiroho, na huku kifo cha kimwili kilikuwa kinamnyemelea. Kwa sababu ya anguko viumbe vingine pia viliathirika, pia hata ardhi ambayo ilikuwa baraka kwa mwanadamu ikawa kinyume chake. Hata hivyo, mwanadamu alikuwa bado mfano wa Mungu, lakini mfano huu ulikuwa na mapungufu makubwa na kuharibiwa na dhambi. Mwanadamu akawa amepotoka kabisa. Yule mtu wa ndani, hali ya ndani ilikuwa imechafuka

kabisa,

kamwe

hakuweza

kujiokoa

mwenyewe. Japokuwa

mwanadamu

aliasi,

bado

tumaini

halikupotea. Mungu alianzisha mpango wa kumwokoa mwanadamu kupitia mbegu ya mwanamke (Mwa. 3:16). Mwanadamu kamwe hangeweza kuwa Mwokozi wa ulimwengu; bado Adamu na Hawa kwa hakika walitarajia mkombozi

mwingine

wa

kuwatoa

katika

dhambi-

Mwanadamu Yesu Kristo. Yesu alipokuja, aliitwa Adamu wa Pili (1 Kor. 15:45), Masihi, ambaye ndiye mbegu ya kweli ya mwanamke (Gal. 3:16). Yesu alikuwa ndiye sura na mfano 88

kamili wa Mungu. Yesu alitimiza mpango wa wokovu kwa wanadamu

ambao

Mungu

aliuweka kwa

ajili

ya

kumwokoa. Tunasoma katika WCF/8/1 Mungu, katika kusudi lake la milele ilimpendeza kumchagua na kumteua Bwana Yesu, Mwana pekee, kuwa mpatanishi kati ya Mungu na Mwanadamu; Yesu ndiye Nabii Kuhani na Mfalme kichwa na Mwokozi wa Kanisa lake, mrithi wa vitu vyote, na Mwamuzi wa ulimwengu. Tangu milele yote Mungu alimpa watu kuwa uzao wake na kwa

wakati,

uzao

wake

wakombolewe,

waitwe,

wahesabiwe haki, watakaswe na watukuzwe naye. Vilevile tunasoma katika WCF/8/4 kwamba Bwana Yesu alichukua kazi ya Upatanishi kwa hiari yake mwenyewe. Ili kuifanya kazi hiyo, alishushwa chini na akaitimiza sheria kikamilifu. Alivumilia mateso makali sana katika roho yake na maumivu makali sana katika mwili wake; Alisulubiwa na akafa akazikwa na akabaki chini ya nguvu ya mauti, lakini mwili wake haukuona uharibifu; siku ya tatu alifufuka kutoka kwa wafu na mwili 89

uleule ambao ulipata mateso na akiwa na mwili huohuo alipaa mbinguni. Huko ameketi mkono wa kuume wa Baba yake

akiwaombea

Waamini

atarudi

kuwahukumu

wanadamu na malaika wakati wa mwisho wa ulimwengu.

90

Marejeleo Andreas J. Köstenberger and Margaret E. Köstenberger, God’s Design for Man and Woman: A BiblicalTheological Survey (Wheaton, IL: Crossway, 2014) Bavinck, Herman. Reformed Dogmatics. Baker Publishing Group. Kindle Edition. Bennett, Mathew Aaron, 40 Questions about Islam (Grand Rapids: Kregel Academic, 2020) Berkhof, Louis, Systematic Theology (Grand Rapids: Eerdmans, 1974) Calvin, John, Institutes of the Christian Religion (Louisville: Westminster John Knox Press, 1960) Courson, Jon. Jon Courson's Application Commentary: Volume 1, Old Testament, (Genesis-Job). Thomas Nelson. Kindle Edition. Davis, John Jefferson. Evangelical Ethics: Issues Facing the Church Today, 4th ed. P&R Publishing. Kindle Edition 91

Erickson, Millard (1998). Christian Theology (2 ed.) Frame, M. John, Systematic Theology; An Introduction to Christian belief (New Jersey: P&R Publishing company, 2013) Harry, Emerson Fosdick, The Modern Use of the Bible (New York: Macmillan, 1924) Hodge, Charles, Systematic Theology – (Vol. III) (Grand Rapids, MI: Christian Classics Ethereal Library,) Hoekema, A. Antony. Created in God’s Image (Grand Rapids: William B Eerdmans, 1986) Jamieson, and Brown Commentary, comment on Genesis 2:22 Macarthur J & Mayhue, R (Ed) A Systematic Summary of Biblical Truth: Biblical Doctrine (Wheaton, Illinois: Crossway, 2017) Miley, John. Systematic Theology (hakuna mchapishaji, wala mji)

92

Reymond, L. Robert, A New Systematic Theology of The Christian Faith (Nashville: Thomas Nelson Publishers 1998) Richard Dawkins, Unweving the Rainbow: Science, Delusion, and the Appetite for Wonder (New York: Houghton Miffilin, 1998) Samuel Willard, A Compleat Body of Divinity in Two Hundred and Fifty Expository Lectures on the Assembly’s Shorter Catechism (Boston: by B. Green and S. Kneeland for B. Eliot and D. Henchman, 1726) Seni, Daniel John (Mf.) Misingi ya Imani; Mafundisho ya Kibiblia kuhusu Imani ya Kikristo: Tafsiri ya The Westminster Confession of Faith and Larger Cathecism, 2020) Sherlock, Charles. The Doctrine of Humanity (Illinois: InterVarsity, 1996) Simone de Beauvoir, Le Deuxième Sexe (Paris: Gallimard, 1949), kimepigwa chapa kwa kiingereza kama The 93

Second Sex, trans. Howard M. Parshley (London: Jonathan Cape, 1953); and Betty Friedan, The Feminine Mystique (New York: Dell, 1964) Marejeleo ya Mitandaoni https://www.cs.williams.edu/~lindsey/myths/myths_14.ht ml https://rainerebert.com/2020/09/04/interview-the-lgbtcommunity-in-tanzania/ https://religiondispatches.org/god-made-them-male-andfemaleand-eunuch-why-the-biblical-case-for-binarygender-isnt-so-biblical/ https://www.christiantruthcenter.com/biblical-meaning-ofthe-word-man-and-woman-in-marriage/ https://www.gotquestions.org/different-races.html https://www.gotquestions.org/Kiswahili/mke-kaini.html https://www.britannica.com/science/anthropology

94