Wanawake wa TANU. Jinsia na Utamaduni katika Kujenga Uzalendo Tanganyika: 1955-1965 9987600115, 9789987600113

Kimetafsiriwa na Kurahisishwa na Elieshi Lema.

294 61 5MB

Kiswahili (Swahili) Pages 116 [134] Year 2005

Report DMCA / Copyright

DOWNLOAD PDF FILE

Recommend Papers

Wanawake wa TANU. Jinsia na Utamaduni katika Kujenga Uzalendo Tanganyika: 1955-1965
 9987600115, 9789987600113

  • 0 0 0
  • Like this paper and download? You can publish your own PDF file online for free in a few minutes! Sign Up
File loading please wait...
Citation preview

mu

WANAWAKE WA Tanu ai

Kimetafsiriwa na Kurahisishwa na Elieshi Lema

WANAWAKE WA TANU Jinsia na Utamaduni katika Kujenga Uzalendo Tanganyika: 1955 - 1965

Susan Geiger

ii

Kimetafsiriwa na Kurahisishwa

na Elieshi Lema

| |

e.. 9 aa

AI Ten

AI

le£o

UNIVERSITY LIBRARY UNIVERSITY OF NORTH CAROLINA AT CHAPEL HILL

Limited

—uuuiiilililililiiAAAAAAAAAA Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) S.L.P. 8921 Dar es Salaam Tanzania

Tafsiri ya Kiswahili - Wanawake wa Tanu: Jinsia na Utamaduni katika Kujenga Uzalendo Tanganyika: 1955 - 1965

O TGNP, 2005

ISBN 9987 -600-11-5

Kitabu hiki ni tafsiri rahisi ya TANU WOMEN Gender and Culture in the Making of Tanganyika Nationalism, 1955 - 1965, kilichoandikwa na Susan Geiger, na kuchapishwa na Heinemann, James Curry, E.A.E.P, Mkuki na Nyota, 1997.

Toleo la Kiswahili limechapishwa na ED Limited kwa niaba ya Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP).

Haki zote za toleo la Kiswahili zimehifadhiwa.

Aa

——

UA

WANAWAKE WATANU..——

YALIYOMO

iii

iii

Aa



SEHEMU YA KWANZA: Kuvunja Ukimya

SURA YA KWANZA Wanawake na Siasa Wakati wa Ukolomi --------- 1 SURA YA PILI Itikadi za Kikoloni na Uhalisi wa Maisha ya Mijini --- 15 SURA YA TATU Wanawake Waafrika Walioishi Dares Salaam ----- 23

SEHEMU YA PILI: Wanawake na Ujenzi wa Uzalendo SURA YA NNE Bibi Titi Mohamed: Dar es Salaam -----------SURA YA TANO Bibi Titi na Harakati za TANU Nje ya Dar es Salaam -SURA YA SITA Wanawake wa TANU: Kuinuka kutoka Gizani -----SURA YA SABA Wanaharakati wa Kilimanjaro na Moshi Mjini ----SURA YA NANE Wanaharakati kutoka Mwanza --------------

31 39

47 62 82

SEHEMU YA TATU: Uzalendo na Harakati za Wanawake Baada ya Uhuru

SURA YA TISA Bibi Titi Mohamed: Uhuru na Baada ya Uhuru

----- 95

SURA YA KUMI A Kutoka Kitengo cha Wanawake Hadi Umoja wa Wanawake - 106 SURA YA KUMI NA MOJA lucy Lameck -----------------------...... 113

Ni

MU NNYI DIV NYAMA VM

Bibi Titi Mohamed na Susan Geiger, 1998



WANAWAKEWATANU..—

v

|| | |

UTANGULIZI Wanawake Wanachama

|

wa TANU

Wananchi wa Tanganyika walijipatia uhuru wao kutoka kwa Waingereza mwaka 1961 kupitia mapambano yaliyoongozwa na jumuiya yenye

nguvu chini ya uratibu wa chama cha TANU. Wanawake wazalendo walikuwa ni viongozi mashuhuri katika medani zote kwenye ngazi mbalimbali. Wanachama wengi wa TANU walikuwa wanawake na walihusika na majukumu ya kuchangisha fedha, uhamasishaji wa nyumba hadi nyumba na ushawishi wa wanachama katika makundi mbalimbali. Hii ni kawaida ya wanawake katika harakati kama hizi duniani.

Susan Geiger akiwa katika majadiliano na wanaharakati wa utetezi wa wanawake

|

|

|

|

l

vi



WANAWAKE WATANU..——

Zaidi ya hapo, wanawake hawa wazalendo ndio waliojenga uelewa wa ni nini maana ya utaifa hapa Tanganyika. Utamaduni wa wanawake na hasa vikundi vya ngoma kama vile vya "lelemama" na matumizi ya lugha ya Kiswahili, viliwaunganisha na kuleta umoja uliowezesha kuandaliwa kwa mikakati na kuinua upeo wa uelewa wao, ambao hatimaye ulileta mapambano ya kitaifa yenye nguvu na ya mafanikio makubwa. Mmoja wa wanaharakati katika ngazi ya kitaifa kwenye mapambano haya alikuwa Bibi Titi Mohamed. Bibi Titi alionesha uongozi mahiri akishirikiana na wanawake wengine waliokuwa mashuhuri katika miji mbalimbali hapa nchini. Wanahistoria,

wanasayansi

wa

siasa

na

watalaamu

wengine

wamepuuza kwa kiwango kikubwa mchango wa wanawake wanaharakati wa Tanganyika katika mapambano dhidi ya wakoloni. Makundi mengine yaliyosahaulika ni pamoja na wanasiasa na wananchi kwa ujumla. Hata hivyo, wakati watathmini wa masuala ya jinsia na wengine wanapotambua mchango wa wanawake kama ule wa Bibi Titi Mohamed, wamesisitiza zaidi idadi yao na mchango wao kama 'wanawake' katika kuendeleza mapambano ya kumng'oa mkoloni. Lakini mchango mkubwa ambao wanawake hawa wazalendo waliutoa katika ujenzi wa taifa na kufahamika kwa Tanganyika - sasa Tanzania umepuuzwa. Susan Geiger ametoa mchango muhimu sana katika kuelewa historia ya Tanganyika. Tathmini kuhusu mchango wa wanawake katika kuujenga uzalendo wa Mtanzania imeelezwa kwenye kitabu hiki, Wanawake wa TANU; Jinsia na Utamaduni katika Kujenga Uzalendo Tanganyika, 1955 - 1965.

Kitabu hiki kina umuhimu gani? Mchanganuo wake ni wa kipekee katika maudhui, mbinu za uandishi na

mpangilio. Kitabu hiki kinatoa changamoto kuhusu historia ya utaifa katika Tanzania na duniani kote. Pia, inatoa fikra mbadala ambazo zinalenga katika kuleta utambuzi unaoonesha nguvu za wanaharakati

——

WANAWAKEWATANU..———

vii

wengi na jinsi wapigania uhuru walivyokuwa wamejiandaa. Je, wanawake na wanaume wengi namna ile, mijini na vijijini, walijipanga vipi? Mwandishi mwenyewe anasema, “Kwa nini wanawake waliitikia wito kwa wingi namna ile, na walijikusanya vipi? Je, ni kundi gani la wanawake waliitikia kwa haraka zaidi harakati za kisiasa, na je, tunauelezeaje utashi huu?

Ukiangalia wanawake, na kuibuka wanawake

matatizo ya kijamii na kiutamaduni katika shughuli za kulikuwa na changamoto zipi ambazo ziliandamana kwa hamasa hii ya kisiasa miongoni mwa vikundi vya katika jamii?

Kitabu hiki kinauliza maswali kadhaa:

e o

o

Ni kwa nini utaifa wa Mtanzania ulichukua sura mpya baada ya uhuru kuliko ilivyokuwa katika nchi nyingine ? Je, tunauelezeaje ukweli kwamba, licha ya tabia, utaifa wa Tanganyika umebaki kuwa alama tu ya utambulisho kwa wanawake? Je, ukiangalia ukweli kuwa utaifa na utamaduni katika Tanganyika vilikuwa kazi zilizoendeshwa na wanawake wa TANU, matokeo ya kazi yao ni yapi? Je, tunauelezeaje ukweli kuwa utaifa hapa Tanzania haukujengwa na kikundi cha wanamapinduzi au haukuwa ni matokeo ya kuibuka kwa matabaka kutaka kudhibiti dola?

Hali kadhalika, njia alizotumia Susan Geiger "kukusanya habari au takwimu” za kitabu hiki ni za kipekee pia. Chanzo chake kikubwa cha kupata habari na tathmini kilikuwa wanawake wanaharakati wenyewe. Kwa kupitia utafiti uliofanyika, walipewa nafasi ya kuelezea maisha yao wenyewe kama walivyoishi ndani ya jamii. Hizi ni simulizi zao pamoja na mkusanyiko wa matukio mengine ya historia. Wanawake walielezea

vili

——

WANAWAKEWATANU..————

mbinu na mikakati waliyoitumia kuwashawishi waume zao pamoja na jamaa waliowahusu ili wapate fursa ya kuendesha harakati zao. Katika nyakati nyingi, wanaelezea machungu yaliyowakuta wakati ndoa zao zilipovunjika kutokana na kujihusisha katika harakati za kugombea uhuru. Haya ni masuala ya binafsi, lakini yenye uhusiano mkubwa na uongozi wao. Wanaharakati hawa wanaelezea mikakati waliyoitumia kama viongozi wa TANU kuuhamasisha umma ili uweze kuwaunga mkono. Walitumia mbinu bunifu kuwalinda viongozi wa ngazi za juu ili wasibughudhiwe na polisi wa kikoloni. Susan Geiger pia amefanya utafiti wa kina kwenye nyumba za makumbusho ya mambo ya kale hapa Tanzania na huko Uingereza. Nyaraka muhimu za Serikali ya kikoloni hapa Tanganyika zilipatikana huko na katika vyanzo vingine vya habari. Alifanya tathmini ya maandishi ya wanahistoria na watu wengine walioandika kuhusu historia ya harakati za kupigania uhuru. Tathmini yake ya habari za wanaharakati wengine zilielezwa katika maandishi aliyoyakuta. Wakati huohuo, alitumia uelewa wake wa mambo ambayo yalikosekana katika taarifa rasmi za serikali na kuziunganisha na yale aliyojifunza kutoka kwa wanawake aliowahoji. Historia ya maisha ya wanawake inachukua nafasi kubwa katika mpangilio wa kitabu. Tathmini ya mwandishi inakuwa kama uzi uliounganisha maudhui ndani ya kitabu, lakini chachu ya maelezo yaliyomo yanabaki ni yale ya historia ya wanawake wanaharakati wenyewe. Sehemu kubwa inahusu tathmini ya Bibi Titi Mohamed mwenyewe, kama ishara ya shukrani kwa mchango wake katika historia ya Tanzania. Huu ni uthibitisho mpya kuhusu uwezo aliokuwa nao Bibi Titi Mohamed, ambao ulimfanya awe maarufu kama mwanaharakati mpigania uhuru wa Tanganyika katika miaka ya 1950, akimfuatia Mwalimu Julius Kambarage Nyerere mwenyewe. Kitabu hiki ni tafsiri iliyowekwa katika lugha rahisi kwa madhumuni ya kuwezesha watu wengi wakisome na kupanua uelewa wao kuhusu harakati za wanawake Tanganyika katika miaka ya 1950. Susan Geiger

——

WANAWAKE WATANU..———

IK

alikiandika kitabu hiki katika lugha ya Kiingereza na katika mtindo wa kisomi ambao kwa kiwango fulani unawazuia watu wa kawaida wasiweze kupata maudhui yaliyomo. Pia hakipatikani kwa urahisi hapa nchini. Susan mwenyewe alikiri kuwa hili ni pengo kubwa ambalo angependa kulisahihisha katika kazi yake. Hivyo, toleo hili la Kiswahili linaunganisha nguvu ya toleo la awali la Kiingereza.

Kwa nini ni muhimu kukitangaza kitabu hiki cha Wanawake wa TANU? Malengo makuu ya kitabu hiki yamegawanyika katika sehemu tatu: e

>

Kutambua, kuweka kumbukumbu, na kusherehekea mchango wa wanawake wanaharakati ambao walishiriki katika mapambano ya kuzikomboa nchi zao. Kusambaza kwa wingi kadri itakavyowezekana, maarifa haya na masomo tunayoyapata kutokana na mapambano ya wanawake wanaharakati,

hapa Tanzania

na katika

ukanda

wa

Afrika ya

Mashariki. Kuleta matumaini mapya kwa wanawake kwamba ni muhimu kuendeleza harakati za kijinsia na maendeleo shirikishi ili kuhamasisha jamii na kutoa mategemeo mapya kwa vijana na wazee kwamba dunia mbadala yenye kuzingatia haki na usawa inawezekana. Kitabu hiki pia kinatoa changamoto kwa wale wanaoandika mambo ya e

kurudiarudia

kuhusu

wanawake.

Kwa

mfano,

wajibu

wa

wanawake

Waislamu katika harakati za mapambano ya kudai uhuru ni kielelezo tosha kuwa wanawake wa Kiislamu sio watu wasiokuwa hata na uwezo wa kupaza sauti zao zikasikika hadharani. Wanawake Waislamu walionesha ukakamavu katika mazingira magumu. Walivipuuza vishindo vya serikali za kikoloni na viongozi uchwara. Walitumia njia za amani katika kudai haki, walikabiliana na polisi wa kikoloni na walihakikisha kuwa walifanya maandamano ya amani ambayo yaliwavutia watu

wengi kwa maelfu. Watu wengi walijiunga nao.

K



WANAWAKE WATANU..

——

Suala la wasomi pia linazungumziwa katika historia hii. Kitabu kinatukumbusha jinsi itikadi za kikoloni zilivyounda tabaka la 'wasomi' ambalo liliwatambulisha wanawake na wanaume kwa kuiga tabia za wazungu. Kama kitabu hiki kinavyoonesha, tabaka la wanawake wasomi

lilitengwa katika 'vilabu' maalumu ambavyo viliongozwa na wanawake Wazungu. Wasomi katika tabaka hili, walikuwa Wakristo. Wengi wao hawakuwa na elimu kubwa lakini walihusishwa katika masomo ya dini katika shule za kanisa. Sambamba na hilo, wanawake wengi wanaharakati walikuwa wamepata elimu ya msingi angalau mwaka mmoja au miwili ikiwa ni pamoja na 'madrasa' kwa wanawake wa Kiislamu. Hata hivyo, hawakutambuliwa kama 'wasomi' na wakoloni na hata wafanya tathmini wa leo wameshindwa kuwatambua kuwa ni 'wasomi.' Kitabu hiki pia kinaweka kumbukumbu ya ukweli kuwa mapambano ya kudai uhuru hayakufanikishwa na mtu mmoja tu, bali uongozi wa pamoja. Wanawake kwa wanaume walitoa mawazo yenye kuona mbali, walitoa ujuzi na walijitoa mhanga ili kufanikisha azma ya kupata uhuru. Tofauti na historia ya 'Mtu mmoja kiongozi', hii ni historia ya viongozi wengi wakiwemo wanawake wengi wa kawaida tu ambao walifanikisha kupatikana kwa uhuru wa Tanganyika. Mfano mzuri ambao unajieleza wenyewe unatolewa mwanzoni mwa kitabu hiki, ambacho kinaelezea jinsi TANU ilivyoweza kuwakusanya zaidi ya wanawake na wanaume 40,000

katika

mkutano

wa

hadhara

Umma uliendesha mapambano vinginevyo.

bila kuwepo

Mwalimu

Nyerere.

hayo pamoja na viongozi wao na SIO

Kwa nini tunachapisha kitabu kinachohusu mapambano ya kupinga ukoloni leo? Tunaamini kwamba vikaragosi vya wakoloni vimejitokeza tena hivi leo kutokana na kuwepo kwa sera za soko huria na kudhihirika kwa nguvu mpya za ubeberu. Tanzania inaweza kujikuta ina "uhuru wa bendera" hasa ukitilia maanani kwamba uchumi wake sasa unamilikiwa na

——

WANAWAKEWATANU..———

yi

mashirika na watu wengi wa kigeni. Serikali inaelekea kuwa tegemezi mno kwa wale wale waliotutawala, wakiwemo Wajerumani, Waingereza

pamoja na Marekani, Japan na nchi tajiri duniani ambazo zinajiita "kundi la nchi nane.” Tukiwa

tumeelemewa

na madeni,

Serikali

haiko huru

kufanya maamuzi yake yenyewe kuhusu sera za uchumi. Kwa njia hiyo, Serikali, kwa upande mkubwa, inaendelea kutegemea misaada kutoka nje. Jambo hili linazuia uhuru kamilifu wa kisiasa. Kwa mfano, uwezo wetu wa kufanya maamuzi kuhusu mambo ya msingi na jinsi ya kugawa rasilimali zetu ni mdogo na umefifishwa na hali yetu ya utegemezi. Mfano mwingine unahusu mapambano yetu kuhusu umilikaji wa ardhi, jambo ambalo tangu mwanzo lilikuwa ni moja ya sababu iliyowapelekea Watanganyika kupambana na ukoloni. Sehemu kubwa ya ardhi yenye rutuba katika nyanda za juu za Tanganyika ilikuwa mikononi mwa Wazungu. Wazalendo walinyang'anywa ardhi hii. Sehemu kubwa ya ardhi iliporwa katika maeneo mengine na kufanywa mashamba ya katani na miwa. Katika kila eneo, wamiliki walikuwa ni Wazungu ambao walijipatia faida kubwa huku wakiwanyonya Waafrika kwa kuwatumikisha kazi zenye ujira mdogo. Sehemu kubwa ya wafanyakazi ilikuwa ni wanawake na watoto wadogo. Muda mfupi baada ya uhuru, Serikali ilipitisha sera ya ardhi ambayo ilitambua umiliki wa ardhi kuwa wa jamii na kuwazuia wageni wasimiliki ardhi. Sera hii ya ardhi imekuwa ikipigwa vita na wawekezaji tangu miaka

ya

1980,

na

hatua

kwa

hatua,

Serikali

imekuwa

ikiruhusu

matumizi ya ardhi kwa wageni katika sekta za kilimo, utalii, uchimbaji wa madini na mabenki yanayowekeza hapa nchini. Hivyo basi, suala la ardhi limeanza kuibuka upya na wanaharakati pamoja na jamii katika sehemu mbalimbali wameanza kujipanga upya ili kulipinga.

Susan Geiger ni nani? Marehemu Susan Geiger ni msomi mwanaharakati ambaye alifundisha masomo ya Kiafrika na yale ya Jinsia katika Chuo Kikuu cha Minnesota/Twin

Cities, huko

Marekani

kwa

muda

wa

miaka

mingi.

E

AA sii

——

WANAWAKE WATANU..

——

Alikuja Tanzania kwa mara ya kwanza akiwa mwalimu wa kujitolea katika miaka ya 1960. Baadaye aliendelea kurudi katika nyakati tofauti katika kipindi chote cha maisha yake. Kazi yake kubwa ya utafiti ilikuwa juu ya historia ya uchifu wa Wachagga. Utafiti huo ndio uliokuwa chimbuko la kujipatia Shahada ya Udaktari wa Falsafa. Makusanyo ya tathmini ya historia ya wanawake wanaharakati wapigania uhuru yalifuata. Susan alitokea kuwa msomi maarufu aliyeheshimika kimataifa kwa kutetea historia za maisha ya watu kama nguzo muhimu ya njia za utafiti wake. Susan aliweza pia kuwandaa wanaharakati wanawake wasomi. Wanafunzi wake wameenea duniani kote na wengi wao wanatoka Tanzania na baadhi ya nchi nyingine za Afrika. Susan aliunganisha kazi yake ya darasani na uanaharakati wa kisiasa katika maisha yake yote. Akiwa kiongozi wa wanaharakati wa jinsia, Susan alipigania suala la nafasi ya mafunzo ya jinsia ili mafunzo hayo yatolewe katika ngazi zote za jamii. Alishiriki kikamilifu katika harakati za mapambano hata nje ya vyuo vya masomo. Susan alikuwa chachu



WANAWAKE WATANU..——

a vikundi vya mshikamano

ambavyo

viliunga

zili

mkono

harakati

za

ukombozi katika Bara la Afrika huko Marekani. Susan alikuwa mwanaharakati aliyejitolea kwa michango ya hali na mali hadi mwisho wa maisha yake. Alitoa mchango mkubwa kwa wanamtandao wa masuala ya jinsia hapa nchini ili waweze kuendeleza shughuli zao. Kabla ya kifo chake, Susan Geiger aliandika mirathi iliyotoa sehemu ya rasilimali yake kwa wana TGNP pamoja na wana mtandao wengine. Rasilimali hiyo ni pamoja na vitabu vya maendeleo na vya uanaharakati katika Bara la Afrika, vilivyokuwa sehemu ya maktaba yake. Pia, Susan Geiger alitoa fungu la fedha lenye lengo la kusaidia ukuaji wa vipaji vya waandishi chipukizi, kuweka kumbukumbu na kuwezesha uandishi wa masuala ya historia ya wanajumuiya na hasa wanawake. Susan alifariki mwaka 2001, akawa ameacha pengo kubwa kwa wanaharakati na wapenda maendeleo. Maisha na kazi yake yamebaki kuwa mfano na kichocheo kwa wanaharakati, wanawake na wanaume

wanaojihusisha na historia za wanawake. Mtandao wa Jinsia Tanzania unatoa shukrani kwa wachapishaji wa toleo la kwanza lililo katika lugha ya Kiingereza kwa kutoa ruhusa ya kutafsiri na kurahisisha TANU Women: Gender and Culture in the Making of Tanganyikan Nationalism, 7955-7965. Wachapishaji hao ni Heinemann na James Currey wa Uingereza, E.A.E.P wa Kenya na Mkuki na Nyota Publishers wa Tanzania.

Mary Rusimbi na Marjorie Mbilinyi Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP)

WA

p ——

WANAWAKE WATANU..——

SEHEMU YA KWANZA San maaana 4

Kuvunja Ukimya Kwa nini wanawake waliitikia wito wa TANU kwa hamasa kiasi hicho? Walijipanga vipi? Wanawake wapi walihamasika zaidi kisiasa? Shauku hiyo inaweza kuelezwa vipi? Tukizingatia vipingamizi vya kijamii na kiutamaduni ambavyo vilizuia wanawake kushiriki katika shughuli za umma, ni changamoto zipi ziliandamana na kuibuka kwa uelewa wa kisiasa miongoni mwa vikundi fulani fulani vya wanawake wa Tanzania?

———

WANAWAKEWATANU..———

1

SURA YA KWANZA Wanawake

na Siasa Wakati wa Ukolomi

Utangulizi Tanzania ilitawaliwa na Ujerumani tangu 1885 hadi Vita Kuu ya Kwanza. Ujerumani iliposhindwa katika vita, Tanzania ikawekwa chini ya Shirikisho la Mataifa chini ya udhamini wa Uingereza.

Kama ilivyokuwa katika sehemu nyingine Afrika, Watanganyika nao walizidisha nguvu kuonesha kutoridhika kwao na utawala wa kikoloni.

Kufikia mwaka 1950, viongozi walijaribu kufufua Tanganyika African Association (TAA), ambayo ilikuwa inasuasua. Waliunganisha nguvu na taasisi nyingine kupinga vitu kama vile taratibu gandamizi za masoko zilizozuia uuzaji wa mazao; matumizi ya majosho ya ng'ombe; n a Wazungu kujinyakulia ardhi. Watawala wa Uingereza nao walikuwa n a hisia kinzani kuhusu Tanganyika, na wakati huohuo wakitaka kuepuka

vurugu za harakati za kizalendo huko Kenya. Katika hali hii, ndipo Julius Nyerere, akiwa ameungwa mkono na viongozi wa matawi ya TAA, alikigeuza TAA kuwa TANU kwa madhumuni mahususi ya kupigania uhuru kutoka kwa Waingereza. Maandishi mengi yanayohusu kuibuka kwa harakati za kizalendo Tanganyika yanazungumzia nafasi ya wanasiasa wasomi. Hawa walikuwa na uelewa wa matarajio ya watu na waliweza kuyaeleza kwa ufasaha zaidi na hivyo kupata wafuasi wengi. Waliweza kuunganisha

harakati za kujitawala na hisia za watu za kupinga ukoloni. Hisia hizi zilijidhihirisha sehemu mbalimbali nchini kwa njia mbalimbali. Lengo kuu la wanaharakati wazalendo lilikuwa kupata nguvu za kutawala na kuwaondoa wakoloni, na kwa njia hiyo kuweza kuleta mabadiliko ya watu kutoka kuwa watawaliwa na kuwa raia wa nchi.

2



WANAWAKE WATANU..

——

Kwa mujibu wa maelezo haya ya uzalendo Afrika, ni Waafrika wanaume waliosoma nchi za Magharibi ndio waliowezesha yote haya. Wao ndio waliozishikilia harakati hizi pamoja na kuzifanya ziwe za 'kizalendo'. Kundi hilihili la wasomi ndilo lililowajibika kuleta na kutafsiri mawazo

na itikadi za Kimagharibi,

ambazo

zilikuwa

muhimu

katika

mageuzi haya. Hivyo basi, maelezo ya harakati za kizalendo Afrika, ya wakati uliopita na ya sasa, yanaanzia mwanzoni mwa karne ya ishirini. Yanaelezea jinsi upinzani dhidi ya ukoloni ulivyokua katika sehemu maalumu na hivyo kuonesha sababu za kuibuka kwa aina fulani ya viongozi wasomi Waafrika. Katika hali hii, kazi ya mwanahistoria mwenye shauku na historia ya uzalendo wa Kiafrika ni kuweka wazi ni vipi na ni kwa nini makundi fulani fulani ya Waafrika yalikuwa tayari kuchochewa na ule uzalendo ulioanzishwa na wanaume wasomi. Maoni ya hivi karibuni yanasema kuwa kazi kubwa ya wajenzi wa taifa ni kuunganisha nguvu tofauti katika nchi, na kisha kuuwezesha

muungano huo kupata uelewa wa utaifa. Walitakiwa wafanye kazi ngumu ya kuhamisha utii kutoka kwenye mamlaka za jadi na kuuleta katika taifa. Kwa mujibu wa Jeanette Hartman, katika makala yake iliyotoka kwenye gazeti la Business Times la Decemba 9, 1988, wakati wa maadhimisho ya miaka 27 ya uhuru, changamoto ya kwanza iliyomkabili Nyerere na Chama cha TANU ni kuunda taifa lenye mshikamano na utambulisho imara kutokana na jamii ya makabila tofauti. Hili lilifanikiwa, siyo kwa kukandamiza (tofauti hizo), bali kwa kutumia itikadi iliyohubiri usawa pamoja na ujenzi wa usawa katika

jamii. Bibi Titi na Nyerere : Kuvunja Ukimya Mwezi Octoba, 1985, siku sita kabla ya Julius Nyerere kung'atuka kutoka

uongozi wa siasa uliodumu takriban miongo mitatu, alipokea wanawake elfu tano katika viwanja vya Ikulu, Dar es Salaam. Hafla hii ilikuwa moja ya sherehe nyingi za kumuaga mwasisi huyu wa TANU. Nyerere alikuwa na umri wa miaka sitini na mitatu.

——

WANAWAKEWATANU.————

3

Mkusanyiko wa wanawake kama huu haukuwa jambo la ajabu. Mwaka 1955, maelfu ya wanawake kutoka Dar es Salaam walijiunga na

chama cha kizalendo kilichokuwa kimeanzishwa. Katika kipindi cha miezi mitatu, kufikia mwisho wa mwaka huo, wanawake wengi zaidi ya wanaume walikuwa wamepata kadi za uanachama. Kutoka wakati huo, kilikuwa kitu cha kawaida kuyaona makundi makubwa ya wanawake yakitembea na kuimba, yakiunga mkono chama. Pia, mazungumzo kati ya wanawake na Rais Nyerere

hayakuwa kitu cha ajabu. Nyerere alijibu hotuba za wanawake hao kwa kuhusisha harakati za uhuru wa Tanganyika na harakati za kupigania haki za wanawake. Alirejea katika mila za Kizanaki zilizobagua wanawake na kuwaasa wanawake kukomesha mila zote za kibaguzi na kushiriki katika siasa ili kuendeleza usawa uliopatikana kisheria. Halafu la ajabu likatokea: Nyerere alimwita jukwaani mwanamke mmoja mzee, mwenye mvi na haiba nzuri. Alikuwa Bibi Titi Mohamed, aliyewahi kuwa kiongozi wa Taifa wa Umoja wa Wanawake. Nyerere alisema kwamba Bibi Titi alikuwa kiongozi wa kweli wa chama,

3

AAA WANAWAKEWATANU..———

——-

4

kisha akamwacha akae. Nyerere alitabasamu na kusema kwa sauti ya chini, "Baada ya hapo aliteleza kidogo, lakini ni sawa tu, hayo hutokea.”

Halafu naye akakaa. Siku iliyofuata Nyerere alikubali kwamba

kumtambulisha

Bibi Titi

hadharani ilikuwa ishara ya kumsamehe. Mwaka mmoja kabla, alionesha ishara kama hiyo, bila kusema chochote. Bibi Titi alikuwa miongoni mwa

halaiki ya wanawake walioshiriki maandamano ya kuadhimisha kazi ya Umoja wa Wanawake

wa Tanzania (UWT). Wakati huo, wito maalumu

ulikuwa umetolewa kwa wanawake waliokuwa wanaharakati wakati wa kupigania uhuru kutoka utawala wa kikoloni wa Uingereza. Bibi Titi alikaa katika jukwaa moja na Nyerere kwa mara ya kwanza katika muda wa

takriban

miaka

ishirini.

Hivyo,

hilo tendo

la ajabu

lilikuwa

ni

utaratibu wa msamaha. Bibi Titi alikuwa anasamehewa kwa kushiriki katika njama za kuipindua serikali ya Nyerere mwaka 1969. Ingawa alishikilia kwamba hana hatia wakati wote wa kesi.ndefu na ya kwanza ya uhaini katika historia ya Tanzania, (1970/71), hata hivyo alihukumiwa kifungo cha maisha pamoja na wengine kadhaa, akiwemo Oscar Kambona. Mwaka

1972, alisamehewa na Rais na kutolewa kifungoni.

Ni vigumu kufahamu kama msamaha huu ulitokana na Nyerere kuwa

na huruma au mashaka kuhusu Bibi Titi kuwa na hatia. Ni vigumu pia kuthibitisha kama maisha ya ukimya aliyoishi Bibi Titi nje ya siasa kwa miaka mingi baada ya kuachiwa, aliyachagua ama alishurutishwa kufanya hivyo. Katika mahojiano na Ruth Meena baada ya kutoka kifungoni, Bibi Titi alieleza kuwa hakuwa huru sana kushiriki na wenzake kwa sababu walikuwa waangalifu mno wakiwa naye. Alitania akisema, "Mtu angeweza kufikiria kwamba nilikuwa na ugonjwa wa kuambukiza.” Labda msamaha huu ulitokana na mashaka kwamba Bibi Titi hakujihusisha kwa undani katika njama za kuipindua serikali. Swali ni: Je, mwanamke huyu, ambaye alijitolea kwa moyo wake wote kuhamasisha watu wakiunge mkono chama cha TANU na uongozi wa

Nyerere, angeweza kupanga uhaini?

——

Bibi Titi alionesha

WANAWAKEWATANU..———

kutoridhika

kwake

na sera

5

ya chama

wakati

alipopinga kutofuatwa kwa demokrasia katika mchakato ulioambatana

na kutangazwa kwa Azimio la Arusha, Februari 1967. Pia, hakukubaliana na kipengele (a) sehemu ya 5 ya Azimio kilichohusu maadili ya uongozi. Hususan, hakukubaliana na kipengele kilichosema kwamba kiongozi wa TANU au serikali hawezi kumiliki au kupangisha nyumba. Hakukataa kwa siri, na hivyo alijiuzulu kutoka Kamati Kuu ya Chama kwa mujibu wa maadili ya uongozi, kuliko aachie haki yake ya kujipatia kipato. Jambo hili lilielezwa katika vyombo vya habari, vikitoa picha iliyomwonesha Bibi Titi kuwa alithamini zaidi faida ya biashara na idadi ya nyumba zake kuliko kazi ya siasa chini ya TANU. Lakini Bibi Titi

alimweleza Ruth Meena kwamba alinunua nyumba moja kwa kuuza vito vyake vya dhahabu, na ya pili aliinunua kwa mkopo. Yeye alikuwa ameamua kujipatia hifadhi, kwake na kwa binti yake kwa njia hii, wakati washiriki wenzake waliamua kuoa wake wengi na kunywa pombe. Hata hivyo, alikwishapoteza kiti cha ubunge mwaka 1965. Zaidi ya hayo, mwelekeo wa kuajiri wasomi kujaza nafasi serikalini na katika Umoja wa Wanawake ulionesha wazi kwamba wale askari wa miguu, wapinga ukoloni kama yeye, walikuwa wamewekwa pembezoni. Walioathirika zaidi walikuwa wanawake, hasa wale waliokuwa na elimu ndogo. Nilipomhoji Bibi Titi mwaka 1984, hakuwa na mengi ya kusema kuhusu kuachiwa kwake. Wakati huo alikuwa anajikimu kwa kuwauzia majirani mafuta ya taa katika chupa za soda. Miaka minne baadaye, 1988, akiwa katika nyumba yake kubwa ya Upanga, bado hakuwa

na

mengi ya kuongeza kuhusu kuachiwa kutoka kifungoni. Pia, hakuongeza chochote kuhusu sababu zilizomfanya Nyerere amsamehe. Alinieleza kwa furaha isiyofichika kwamba alirudishiwa nyumba zake mbili zilizotaifishwa akiwa kifungoni. Moja, ambayo ni urithi wa binti yake, ilirudishwa na Nyerere. Nyingine, iliyorudishwa na Rais Ali Hasan Mwinyi, itarudi serikalini atakapokufa. Kufika mwaka 1988, baada ya zaidi ya miaka thelathini ya ushirikiano wa karibu, utii na msamaha

vilidhihirika pande zote mbili, upande wa Nyerere na wa Bibi Titi.

6

——

WANAWAKE WATANU...

——

Jaribio lolote la kuelewa sababu za tukio la 1985 kati ya Nyerere na Bibi Titi Mohamed kuonesha kupatana kwao hadharani litakuwa la kukisia tu. Itakuwa jambo la mashaka makubwa kukisia juu ya dhamiri na nia ya Nyerere. Pia, maana ya ukimya wa Bibi Titi kuhusu sababu za Nyerere kufanya hivyo. Nguvu ya ishara hii, wakati yeye (Nyerere) mwenyewe anaondoka katika nuru ya siasa, ilihusisha kukabili na kukubali ukimya wa huko nyuma. Kisha ilibidi kuuleta ukimya huo hadharani kwa kupitia Bibi Titi. Hivyo, huo ulikuwa wakati wa ukweli kuhusu uzalendo wa Tanzania. Uzalendo ni mchakato wa kihistoria, na humo watu hutumia uzoefu wao wa kijamii kuunda taifa. Katika utaifa, wanaweza wakaujua uhuru utoka ukoloni na kupata heshima yao kama binadamu. Hii ndiyo sababu inayonifanya nilazimike kuanzia utafiti wangu kwenye tukio hili, na kuchunguza uzoefu na kazi walizofanya wanawake

atika kujenga taifa. Katika kitabu hiki, natumia historia za maisha ya wanawake walioshiriki katika harakati za TANU. Nia yangu ni kukabili upendeleo, ukimya, pamoja na kupotoshwa kwa historia iliyopo ya ipindi cha mageuzi ya kizalendo Tanzania. Historia za maisha, kwa kawaida, huwakilisha mahusiano kati ya wakati uliopita na wakati wa

sasa. Zinatoa maelezo ya matukio ya kijamii, pamoja na hali inayoyaunganisha. Aidha, historia za maisha ya wanawake wa TANU ni matokeo ya hali mahsusi ya kiuchumi na kijamii. Historia hizi zinatoa vigezo vya kuelewa uzalendo wa Tanganyika, tofauti na vile vilivyotumika katika historia ya utaifa tangu 1965 hadi 1975. Kwa pamoja, historia hizi zinajumuisha maelezo ya ushindi wa uzalendo. Kuwa na dhana kwamba uzalendo ulikuwa kazi ya Nyerere, au ni itikadi iliyoingizwa kutoka nje, itaonesha wazi kutojali wanawake. Vitendo vyao na utamaduni wao wa siasa ulijenga, ulitekeleza na kudumisha uzalendo Tanzania.

Kutazama Upya Uzalendo Tanzania: Mtazamo wa Kijinsia Uzalendo wa Kiafrika una maelezo yake yanayoelezea mabadiliko ya miitikio ya kupinga ukoloni. Pia yanaeleza kuhusu kuibuka kwa aina

ai ——

WANAWAKEWATANU..———

maalumu ya uongozi wa kisomi Afrika kuanzia karne ya wa Kiafrika wanakubaliana katika tathmini ya Julius "mjenga taifa'. Hata hivyo, wanatofautiana kuhusu sera na siasa za tangu uhuru. Kinachovutia ni jinsi Nyerere

7

ishirini. Wasomi Nyerere kama zake za uchumi alivyofanikiwa,

kama mzalendo. Na hivi karibuni, jinsi dola ilivyokuwa na siasa imara,

licha ya kuzorota kwa uchumi. Vyote hivyo vinafifishwa na kile ninachokiita 'kukosekana na kutokuonekana' kwa nadharia ya uzalendo wa Kitanzania. Nadharia hii inatoa sababu za Tanzania kuwa taifa na kuendelea kuwa nchi ya taifa moja kutokana na mambo yafuatayo:

Kutokutokea kwa kabila moja kuhodhi mamlaka dhidi ya wengi, kati ya "makabila" 120 yaliyohesabiwa wakati wa ukoloni; Kutokuwepo kwa kundi kubwa la jamii ya walowezi wa kikoloni au lililoungana kitaifa kuweza kudhibiti watawala wa ukoloni wa Uingereza

e

au kuzuia TANU;

Kutokuwepo kwa mali au rasilimali nyingi nchini au utajiri mwingi kulimbikizana katika mji mkuu; Kutokuwepo kwa kundi changa la mabwanyenye Waafrika waliojikita; na Tanganyika kuwa serikali ya udhamini na siyo koloni kamili.

Kitu kilichoonekana wazi katika kuelezea uzalendo Tanzania, pamoja na ukosefu wa vitu hivyo vingine ni lugha ya Kiswahili. Lakini hata umuhimu wa Kiswahili unafifishwa kwa kuonekana kwamba lugha hiyo haikuhusishwa na ukoloni au na kabila moja kubwa. Kwa hiyo, lugha hiyo haikuweza kutumika kama chombo cha kuanzisha mamlaka ya kabila moja juu ya mengine. Ni Watanzania wachache wa miaka ya 1950 waliojua Kiingereza. Watu wengi zaidi walielewa na kuzungumza Kiswahili. Kwa wale waliotoka Pwani na katika miji ya Bara, Kiswahili kilikuwa lugha yao ya kwanza. Wanahistoria na wanasayansi ya siasa wameeleza juu ya umuhimu wa Kiswahili kama lugha ya wengi na kama lugha iliyojenga utamaduni

|

| |

YA

8



WANAWAKE WATANU..

——

wa siasa ambao ni muhimu kwa mafanikio ya utaifa. Kufikia miaka ya 1950, iliwezekana kuzungumzia utambulisho wa uzalendo wa Kiswahili

wenye chimbuko Tanzania. Tukiwatazama wanawake wanaharakati wa TANU, tunasukumwa kufikiri tena kuhusu matumizi ya Kiswahili, umuhimu wa utamaduni wa

Kiswahili pamoja na hali ya Uswahili Tanganyika. Hali hii iliwezesha Kiswahili kutumika kama msingi wa kuelewa na kupata utambuzi wa utaifa. Utambuzi huu ndio ulioakisi, uliokubali na kujenga utambulisho

wa kitaifa kati ya na baina ya makabila.

Wanawake Wako Wapi? Watu wanaokikumbuka kipindi cha uhamasishaji wa umma kupinga ukoloni hadi kupata uhuru Desemba 9, 1961, wataweza kurejea jinsi wanawake,

mashabiki

wakuu

wa TANU, walivyokuwa

wakipiga

kelele.

Hususan, watamkumbuka Bibi Titi Mohamed, ama kwa sababu walimwona akihutubia maandamano ya TANU, au waliwasikia watu

wakiongea juu yake, au walipata habari zake kupitia redio na magazeti. Inasemekana kwamba, Bibi Titi Mohamed na Julius Nyerere ndio viongozi wa TANU pekee waliokuwa wakijulikana nchi nzima wakati nchi inapata uhuru. Lakini, pamoja na umaarufu wake kihistoria, Bibi Titi hakuelezewa

vya kutosha katika maelezo mengi yanayohusu uzalendo Tanzania. Jina lake limetajwa tu. Wale maelfu ya wanawake wanaharakati wa TANU walioutambua uongozi wa Bibi Titi ndio hawakutajwa kabisa. Mwelekeo wa kuweka wanawake pembezoni katika kujenga historia unaakisi mtindo uliozoeleka. Mtindo huu ulianzia kwenye historia iliyoandikwa kwa Kiingereza na wakoloni, na baadaye ile iliyoandikwa na wasomi Waafrika. Matendo ya siasa yanayofanywa na wanawake yanatoweka katika historia, yakifuata ukimya uliokuwa katika maandishi yaliyotangulia. Kufutika kwa wanawake kumekithiri katika maandishi yanayohusu historia ya uzalendo Tanzania, hasa yale yaliyoandikwa kwa Kiingereza, kuliko katika maandishi machache yaliyoandikwa na Watanzania kwa Kiswahili.

?

| —

WANAWAKEWATANU..——

9

j

Wanawake wa Kiafrika wanatoweka tena katika maandishi ya Kimagharibi yenye itikadi ya ubaguzi wa kijinsia na wa rangi. Maandishi haya yaliandikwa na wake wa maofisa wa kikoloni walioshuhudia kuzaliwa kwa TANU. Hawa wanawake walikuwa wamisionari, maofisa wa ustawi wa jamii au wasafiri. Wengine walishiriki na kuandika kuhusu

harakati za uzalendo. Maandishi yao mengi yanaonesha itikadi za kijinsia za Kimagharibi pamoja na nyufa zake, pale itikadi hizo zinapoungana na ubeberu. Kutokana na maandishi haya basi, tunadondoa sura, itikadi, vipande na viwakilishi vya wanawake wa Kiafrika, ikiwa ni pamoja na wanawake wa TANU. Karibu maelezo yote yanayohusu ushiriki wa wanawake katika TANU

yanaanza, na yaweza kuishia, na ujaji wa John Hatch na swali lake: Wanawake wako wapi? John Hatch aliiuliza Kamati Kuu ya TANU ya wanaume watupu swali hili alipofika kuwatembelea mwezi Juni, 1955. John Hatch alikuwa ofisa wa Jumuiya ya Madola, akiwakilisha Chama cha Labour ambacho kilikuwa kikiunga mkono juhudi za kizalendo Afrika. Pamoja na kwamba Nyerere hakuwa Dar es Salaam, John Hatch alipokelewa na umati mkubwa wa watu waliokadiriwa kuwa 40,000. Walikusanyika Mnazi Mmoja kusikiliza hotuba za TANU. John Hatch alishangaa wakati alipoona katika umati huo, safu kadhaa za wanawake wa Kiislamu waliovaa mabaibui. Baadaye, alipokuwa akiongea na Kamati Kuu ya TANU kuhusu jambo hili, Hatch aligusia juu ya ukosefu wa wanawake wanachama wa TANU. Suala hili liliakisi udhaifu wa vyama vya kizalendo Afrika nzima, hasa katika miaka yake ya mwanzo. Katiba ya TANU iliyokubaliwa mwaka 1954 ilitaja kuwepo kwa kitengo cha wanawake, lakini kitengo kama hicho hakikuwepo. Hata hivyo, wajumbe wa Kamati Kuu walimwambia Hatch kwamba angeweza kukutana na kiongozi wa wanawake siku iliyofuatia. Wakamtuma Sheneda Plantan, shemeji yake Bibi Titi kumsihi mumewe

| |

|

|

| | |

ili amruhusu

mkewe aonane na Hatch kama kiongozi wa wanawake. Mumewe akakubali, naye Bibi Titi akakubali kuonana na Hatch, mradi tu aweze kufanya hivyo akiwa na rafiki yake Tatu Mzee. Mkutano ulifanyika,

|

wA

a

10

——

WANAWAKEWATANU.———

Hatch akaridhika, na Kitengo cha Wanawake cha TANU kikazaliwa. Maelezo ya kuzaliwa kwa Kitengo cha Wanawake cha TANU, kilichobuniwa

na

viongozi

wanaume,

John

Hatch

akiwa

mkunga,

yanapatana vizuri na maelezo ya ujenzi wa uzalendo Tanganyika. Jambo ambalo halikuelezwa ni jinsi Bibi Titi, mwimbaji kiongozi wa ngoma ya Bomba, mwenye umri wa miaka 30, alivyogeuka kutoka kuwa kiongozi wa kubuni, akawa kiongozi halisi wa TANU. Halafu, ni kwa vipi maelfu ya

wanawake walitokea kuwa wanaharakati wazalendo kutokana na upevu wa siasa wa Bibi Titi pamoja na shauku kubwa ya kazi yake? Bibi Titi alipohutubia mkutano wa kwanza wa Kitengo cha Wanawake cha TANU, Julai 8, 1955, wanawake 400 walijiunga na chama. Kufika Oktoba, 1955, miezi minne tu baada ya kukutana na John Hatch, Oscar Kambona aliyekuwa Katibu Mratibu wa chama aliandika barua makao makuu ya Shirika la Fabian huko Uingereza. Barua hiyo ilieleza kwamba Bibi Titi amefanikiwa

kuwaandikisha

wanachama

wanawake

5,000.

Kambona alisema, "Pamoja na kwamba ana elimu duni, anafungua milango ya kuleta mapinduzi kuhusu wajibu wa wanawake katika jamii ya Kiafrika." Aliendelea, "Tatizo la kuwakomboa wanawake hapo baadaye limeondolewa.” Joan Wicken, ambaye baadaye alikuwa mshauri wa karibu wa Nyerere, aliafikiana na maneno ya Kambona wakati alipotembelea Tanganyika mwaka 1956-57. Alitabiri kwamba matokeo ya kazi ya wanawake wa TANU zaidi ya 6,000 bila shaka yatawaweka wanawake kwenye nafasi nzuri. Alikiri pia kwamba viongozi wa Umoja wa Wanawake hapa (makao makuu) wako sawa na wajumbe wengine wa Kamati Kuu kwa kila hali. Alisema kwamba Bibi Titi ataacha alama kubwa

katika

historia

ya wanawake

wa

Tanganyika,

kama

vile Bibi

Pankhurst alivyofanya kwa wanawake wa Uingereza.

Historia za Maisha ya Wanawake Zinavyotumika kama Mkakati wa Kuvunja Ukimya Maelezo yaliyopo kuhusu uanzilishi wa TANU yanashindwa kuweka bayana uhusiano wa matukio yanayogusia chanzo cha mwamko wa



WANAWAKEWATANU..——

n

kisiasa kwa wanawake. Maelezo ya mwamko huu hayapo kwenye masimulizi ya jinsi viongozi wa TANU walivyoeneza uzalendo vijijini. Walipinga taratibu za mazao

na mifugo zilizowekwa

|

na wakoloni,

walionesha kutoridhika na machifu, na wasomi wachache walikuwa na

matamanio ya kupata kazi bora. Katika kukiandika kitabu hiki, nilitaka maneno yaliyotamkwa na wanawake wanaharakati wa TANU - mazungumzo makini ya wanawake wazalendo wa Tanzania - yasukume, yavutie, na yatoe mwanga kwa njia malumu katika utafiti huu unaohusu uzalendo wa Tanganyika/Tanzania. Haikutosha kunasa maneno na sauti zao ili

ziwekwe kwa matumizi ya utafiti mwingine. Sura nyingi zina maelezo ya kina kutoka kwa wanawake wenyewe. Wakati mwingine, maelezo yao yalitoka nje ya maswali tuliyoyauliza pale mzungumzaji alipoona kwamba anatueleza habari muhimu. Itakuwa vema kujua kwamba sio lazima maswali ya utafiti yabainishe mwelekeo wa maelezo yanayotokana na mahojiano. Jambo hili hutokea hasa pale mahojiano yanapohusisha kumbukumbu za mzungumzaji na jinsi anavyoyapokea na kuyajibu maswali. Maswali waliyoulizwa yalilenga kupata habari muhimu kuhusu jinsi wanawake walivyojikusanya na kuhamasishana, na mengine yalilenga kupata mitazamo na mawazo yao kuhusu harakati za uhuru. Mchakato huu ulijumuisha kunasa mahojiano jinsi walivyozungumza. Baada ya hapo yalitafsiriwa kwa Kiingereza ili masuala na maswali yaliyojitokeza yaweze kujadiliwa. Kisha mahojiano yalitafsiriwa tena katika Kiswahili, na kuwarudishia wahusika ili waweze kuthibitisha yale waliyoyasema. Mchakato mzima ulizalisha matoleo matano. Kufuatana na jinsi wanawake hawa walivyoyaitikia na kuyajibu maswali yangu kuhusu ushiriki wao katika TANU, ninaamini kwamba walijiona kuwa ni wadau wa siasa iliyounda TANU, pamoja na historia ya Tanganyika. Walijiona hivyo kutokana na matendo yao, ambayo

waliyaeleza kwa ufasaha, wakirejea kipindi cha shughuli zao za kisiasa

|

|

| | )

12

——

WANAWAKE WATANU..

———

katika miaka ya 1950. Maelezo mengine yaliongozwa na maswali yangu ambayo yalilenga kipindi cha 'kabla' au 'baada' ya harakati za uzalendo. Mahojiano yangu na wanaharakati wa TANU yanadokeza kwamba kuonekana kwa mtu binafsi kuwa mdau kihistoria, hutegemea sana hali ya siasa wakati huo. Hutegemea pia ushiriki wake na jinsi alivyojihisi kuwa sehemu ya kundi katika mazingira ya tukio husika la kihistoria.

Uwasilishi wa Historia ya Maisha ya Bibi Titi Mohamed Historia ya maisha ya Bibi Titi Mohamed imewasilishwa mara tatu katika kitabu hiki. Jambo hili linaibua masuala muhimu kuhusu jinsi nilivyotumia maelezo yake ya binafsi. Kwa hiyo, nitatoa maelezo mafupi kuhusu wajibu wangu kama mwandishi na mhariri, umuhimu wa Bibi Titi katika utafiti huu, pamoja na jinsi maelezo yake na yangu yalivyoathiri uwasilishi wa maisha yake ya siasa na maelezo kuhusu

uzalendo. Kati ya wanaharakati wote, Bibi Titi ndiye mwanamke aliyejulikana sana na aliyekuwa na nafasi muhimu katika TANU. Alipendwa na wengi. Habari zake zilielezewa vizuri na vyombo vya habari wakati wa harakati

za kupigania uhuru (1954-1964).

Mara nyingi alipigwa picha akiwa

karibu na Nyerere, kwenye maandamano au mikutano ya hadhara akiwa anahutubia umati wa watu. Bibi Titi alikuwa tayari amekwishajijengea uwezo wa kuongea hadharani hata kabla hatujaonana naye. Mwaka 1984, wakati wa mahojiano yetu ya kwanza, yeye alikuwa amekwishatoa hotuba kuhusu maisha yake ya binafsi na ya kisiasa. Alikwishatoa mihadhara kuhusu uzalendo kwa wanahabari wa ndani na wa nje ya nchi. Kipindi cha kuanzia mwaka 1965 hadi 1973 kilikuwa kigumu kwa Bibi Titi. Alipoteza kiti chake cha ubunge katika uchaguzi wa mwaka 1965, akakataliwa kuwa mgombea wa taifa wa UWT. Wakati huo pia alijiuzulu uongozi katika TANU kutokana na maadili ya uongozi ya Azimio la Arusha. Kufikia mwisho wa muongo, alikuwa amehukumiwa kifungo cha maisha kwa kosa la uhaini. Pamoja na kwamba Nyerere alimsamehe

—. —

WANAWAKEWATANU..——

13

mwanzoni mwa mwaka 1972, kushitakiwa kwa uhaini, kuwekwa kifungoni pamoja na uvumi uliotokana na kesi hiyo, Bibi Titi asingeweza tena kupata nafasi isiyo na dosari katika siasa na historia ya uzalendo Tanzania. Nilitambulishwa kwa Bibi Titi na rafiki yake wa siku nyingi, Bwana Kanyama Chiume. Nilishirikishwa vizuri katika uhusiano na maongezi yao, lakini ni baada ya mimi kurudi tena, mwaka

|

|

1988, ndipo Bibi Titi

aliponiita shoga, yaani rafiki wa kike, na akaendelea kuniita hivyo siku zote. Tulikutana mara saba katika kipindi chote cha miaka minane, na kweli tukawa marafiki waliostahili kuitana shoga. Nilifurahia ucheshi wake, akili yake na vile alivyokataa katu kujiona kama kafara.

| |

Mahojiano yetu, yaliyochukua siku nzima au zaidi, yalikuwa ya kina na yenye hisia kali. Naamini kwamba shauku ya Bibi Titi kutaka kuongea na mimi haikufifia kwa kipindi chote cha mahojiano. Alitaka historia ya siasa za wanawake wanaharakati wa TANU iandikwe na ichapishwe. Alitaka rekodi hiyo ijulikane na itambuliwe. Alinikubali mimi kwa sababu aliamini kwamba ningeweza kufanya hivyo. Hakukuwa na mtu mwingine aliyekuwa ameonesha shauku ya kufanya kazi hiyo. Hata hivyo, kufikia mwishoni mwa miaka ya 1980, imani yake kwangu ilikuwa imebadilika. Katika mahojiano na Ruth Meena, Bibi Titi aliweza kuwagombeza wanawake wa Tanzania kwa kutomjali. Hapohapo alihoji uhalali wa wanajinsia Wazungu (kama mimi) waliokuwa wanatafiti maisha ya wanawake na kuwafanya kama vielelezo kwa manufaa yao

| |

binafsi, wakati wanawake wasomi Waafrika wapo. Kauli hii ililenga zaidi

|

wanawake wasomi Waafrika na masuala waliyoshughulika nayo. Pia, ilionesha upeo wake mkubwa wa kisiasa ambao ulimwezesha kuzungumza na wasomi wanawake wa nje na wa Tanzania.

| |

Mwanzoni, nilimwuliza Bibi Titi maswali yaleyale niliyowauliza wanawake wengine. Hivyo, maelezo yake ni marudio ya kina zaidi ya

hadithi aliyoieleza mwanzoni. Mara nyingi alisisitiza umuhimu wa kuwatambua wanawake wengine kwa majina. Pia, alikataa kuzungumzia mambo yenye utata katika maisha yake, au maisha yake wakati alipotuhumiwa kwa uhaini.

| |

|

14

—--

WANAWAKE WATANU...—

Haja ya kuandika historia ya kina ya maisha ya Bibi Titi bado ipo. Katika kuandika kitabu hiki, nimejaribu kuonesha mawazo yake na ya wanaharakati wengine kwamba kujenga na kutekeleza uzalendo, katika miaka ya 1950 haikuwa kazi ya mwanamke mmoja. Ilikuwa kazi ya wanawake wote, wa vijijini na wa mjini. Ninaonesha jinsi wanawake walioshiriki katika mageuzi ya kizalendo walivyohamasishwa, maisha ya

mwanzoni ya Bibi Titi alipoingia katika siasa akiwa hapa Dar es Salaam na baadaye katika harakati za siasa nje ya Dar es Salaam. Maisha ya wanaharakati wa Moshi na Mwanza yanaonesha jinsi ukoloni ulivyoathiri TANU na uzalendo. Ninawasilisha tena maisha ya Bibi Titi baada ya uhuru na kuonesha mabadiliko yaliyotokea katika harakati za wanawake na mwendelezo wa uzalendo. Hivyo, katika kitabu hiki, maisha ya Bibi Titi yameunganisha maelezo ya shughuli

na harakati za kizalendo

za wanawake

wa TANU.

Pia,

maisha yake yamekuwa kielelezo cha mapungufu na uwezo wa kisiasa na ushiriki wa wanawake wa Tanzania. Maisha yake ni kielelezo cha vikwazo vya kijinsia vinavyoendelea kuwakabili wanawake. Mtaalamu mmoja anatushawishi kuona umuhimu na nguvu za wanawake wa

haukupatikana katika kipindi cha miongo mitatu ya kwanza ya uhuru wa kisiasa wa Tanzania. Nao wafanyakazi na vyama vyao, vyama vya ushirika, jamii za kidini au watemi, pia hawakushinda. Hata hivyo, hali hiyo haikanushi umuhimu wa historia zao za kijamii au ushiriki wao mkubwa katika ujenzi wa uzalendo. Vivyo hivyo, ingawa wanawake wa TANU hawakuweza kuleta mapinduzi katika maisha ya baadaye ya wanawake wa Tanzania, haikanushi umuhimu wa kuandika wasifu wao

kwa pamoja. Haitengui umuhimu wao katika ujenzi wa uzalendo wa kitanzania.

-— ——

WANAWAKE WATANU..———

15

SURA YA PILI Itikadi za Kikoloni na Uhalisi wa Maisha ya Mijini

Unaishi peke yako au una mke? Ni nani anakupikia?

Wakoloni waliotawala nchi za Afrika zilizoko kusini mwa Jangwa la Sahara hawakulipendelea hata kidogo wazo la Waafrika kuishi mijini. Woga wa

kushindwa

kuwadhibiti

uliathiri mitazamo yao. Woga

huu

ulielezwa kama vile ni wasiwasi juu ya Mwafrika asiyekuwa na akili timamu wala kabila. Nadharia za ukoloni wa Uingereza zilieleza kwamba maisha ya mjini yaliathiri utamaduni wa Mwafrika na hivyo kudhaniwa kuwa chanzo cha magonjwa kama kichaa, magonjwa ya zinaa, ukoma na mengineyo. Waafrika walioishi mijini walifikiriwa kuwa ni watu

yao. Sura hii inachambua jinsi wakoloni walivyowaelewa maisha ya wanaume

na wanawake

na kuelekeza

Waafrika. Pia, inaonesha athari za

taswira waliyoijenga kwa wanawake Waafrika walioishi Dar es Salaam. Hoja yangu ni kwamba watawala wakoloni hawakuwaona wanawake Waafrika, isipokuwa tu pale matukio au hali fulani ilipolazimisha waonekane. Natazama maisha ya wanawake wa Dar es Salaam katika miaka ya 1950, hali zao kiuchumi na kijamii ambazo ziliwezesha ushiriki wa wanawake fulani katika harakati za siasa, wakati wanawake wengine waliishia kwenye ukimya.

W 16



WANAWAKE WATANU..

——

Wanaume kama Wazalishaji chini ya Ukoloni Hapa Tanganyika, kama ilivyokuwa katika nchi nyingine zilizotawaliwa kuvumiliwa kama mtu anavyovumilia ukame au mafuriko. Katika miaka ya 1920 na 1930, wanaume wengi wa Tanganyika walilazimika

mengine. Walikwenda kwenye mashamba ya mkonge na ya mazao mengine ambako walifanya kazi kwa walowezi wa kizungu. Hata hivyo, wakoloni walihitaji wafanyakazi wachache Dar es Salaam na katika miji mingine nchini. Ubaguzi wa rangi uliota mizizi nchi nzima, hasa Dar es Salaam, ukitenganisha Wazungu, Wahindi na Waafrika katika nyanja zote za maisha. Wanaume Waafrika walifanya kazi nyingi za vibarua, ikiwa ni pamoja na upagazi bandarini, matengenezo ya barabara, ufagizi maofisini na uboi majumbani. Kati ya wafanyakazi karibu 400,000 walioandikishwa mwaka 1953, ni watu 15,000 au asilimia 6 ndio waliokuwa wafanyakazi

maofisini katika ngazi za chini. Wapo watu wachache waliojaribu kufanya biashara lakini ushindani na Wahindi waliotawala kila aina ya biashara, tangu za rejareja hadi biashara kubwa, uliwashinda. Waafrika hawakuwa na stadi za biashara, mitaji, mali ghafi wala mitandao ya kuungana mkono kama waliyokuwa nayo Wahindi. Hivyo, Waafrika wengi, wanaume kwa wanawake, walijaribu kujikimu kwa kuuza hiki na kile barabarani au sokoni. Serikali ya ukoloni ilihitaji nguvukazi ya kiume. Wanawake wachache walihitajika, kama vile walimu, wafanyakazi hospitalini na katika ustawi wa jamii. Wanaume wahamiaji walionekana kuwa 'wengi, — hivyo taratibu za kuwasafisha wale ambao hawakuwa na sababu maalumu ya kuwa mjini (vibarua) ziliwekwa. Kwa hiyo, mahitaji ya nguvu kazi ya ukoloni ndiyo yaliyoweka msingi wa kuamua kama wanaume Waafrika

walihitajika mjini au la. Wanawake Waafrika walikuwa viumbe wageni walioishi sehemu zisizojulikana, sehemu zilizo ndani ya dunia ya wanaume. Mtazamo huu wa kikoloni ulioona miji kuwa ni sehemu za

" ——

WANAWAKEWATANU..——

7

wanaume tu ilificha vipengele muhimu vya itikadi za kikoloni kuhusu wanawake Waafrika waishio mijini. Hususan, zilificha maisha yao kabisa. wanawake, ila wanaume walipaswa kung'olewa huko na kudhibitiwa. Shauku ya wakoloni kung'oa na kudhibiti wanaume Waafrika

ilijumuisha nyanja zote za maisha yao - atafanya kazi ipi na wapi, atalima mazao gani, ataanzisha au kujiunga na chama gani, na hata atamiliki ng'ombe wangapi. Itikadi za Kikoloni kuhusu Wanawake

Itikadi ya kikoloni ya kung'oa na kudhibiti kwa upande wa wanawake Waafrika ililenga katika ujinsi wao na wajibu wao wa kuzaa. Nyaraka za kikoloni zimejaa maelezo na mawasiliano kuhusu matatizo na masuala ya haki za wanaume kudhibiti au kupata huduma za ngono. Masuala haya yalijumuisha uzinifu - kwa kiasi gani wanawake wazinifu waadhibiwe au kufungwa; kiasi gani cha pesa au mali kitolewe kama mahari; faini gani itolewe kama adhabu ya kuwapa wasichana mimba. Adhabu ilitolewa kwa kumuiba msichana ambaye siyo stahili ya mwanamume mhusika; mila na sheria za ndoa na talaka; kudhibiti umalaya; na malalamiko ya wanawake kuhusu kupigwa au kutelekezwa.

Masuala yaliyohusu wanawake kama kulipa kodi, kupangiwa sehemu za kazi na mishahara kwa walimu wanawake Waafrika yalitazamwa kama vile yamo ndani ya mahitaji, haki na wajibu wa wanaume na wale waliowategemea. Vipengele viwili vifuatavyo kuhusu itikadi ya kudhibiti ujinsi wa wanawake Waafrika ni muhimu katika kuelewa mfumo wa kutawala wanawake: e

Kwanza, wanaume na wakoloni walielewa kwamba wanawake ni

tegemezi kwa wanaume. Njia za kudhibiti na kuhakikisha utegemezi unadumu ni pamoja na kuoa watoto; kupiga sana wanawake; kutelekeza wake bila sababu maalumu na kudai haki

18

——

WANAWAKEWATANU..——

ya watoto wa kike wakiwa wameshakua wakubwa. Kuungana huku kimawazo kati ya wanaume na wakoloni juu ya kudhibiti wanawake hakukupata upinzani Tanganyika kama Kenya. Vita dhidi ya ukeketaji iliyoendeshwa na Wamisionari katika miaka ya 1920 huko Kenya ilizuia uwezekano wowote wa wanaume kushiriki ajenda hiyo na wakoloni. Huku Tanganyika, katika miaka ya 1930, Waingereza walijaribu kutahadharisha kuhusu athari za ukeketaji pamoja na wanawake kufanywa watumwa. Wazo hilo halikukubalika. Wasiwasi huo ulikanushwa na maofisa wa ukoloni waliosema kwamba hawajawahi kusikia jambo kama hilo, na kwamba

wanawake

wa Tanganyika wana

haki zao za

kijamii na hawawezi katu kuwa watumwa.

0.

Pili, ilidhaniwa kwamba wanaume walikuwa na mamlaka juu ya wanawake kama ambavyo Wazungu na watawala wa kikoloni walivyokuwa na mamlaka juu ya nguvu kazi ya wanaume, uhamiaji (mjini) na uzalishaji wa mazao ya biashara. Utekelezaji wa udhibiti wa wanawake uliachiwa wanaume waufanye katika nafasi zao kama

waume,

baba, kaka na wajomba.

Watawala

wa

kikoloni

walirejea tena na tena katika mipaka ya sheria kuhusu jambo hili. Masuala yaliyohusu wanawake wa Musoma yalikuwa na ugumu wa kipekee. Haya yalihusu; ndoa za kushurutishwa ikiwa ni pamoja na kuwaoza watoto; na kwa upande wa wanaume, taratibu za kurudisha ng'ombe wa mahari; na wanaume walioachika kudai utunzaji wa watoto, hasa wale waliofikia umri wa kuolewa. Tamko la mshauri wa mahakama lilidhihirisha kuunga mkono imani hiyo kwamba wanaume wanawadhibiti wanawake na kwamba hawatakubali kuinua hadhi zao. Hivyo, kuingilia mambo hayo kunaweza kuharibu mambo zaidi. Serikali ya kikoloni ilitaka kilimo kisichohitaji uwekezaji, hivyo walisimamia nguvu ya wanaume kuwadhibiti wanawake. Sababu ni kwamba wanawake walikuwa wazalishaji wakuu wa mazao ya chakula

aa

ai

| —

WANAWAKE WATANU..

na ndio waliohimili kaya.

——

19

Pia, wanawake ndio waliolisha wafanyakazi

(wanaume watu wazima na watoto) na hivyo kutoa nafasi kwa hiyo nguvukazi kuingia katika mazao

ya

biashara.

|

|

mfumo wa ajira rasmi au katika kilimo cha

Ndoa

ilibaini

waziwazi

kwamba

mwanamke

aliruhusiwa kuzaa watoto na nani na alimlimia nani ili kupata chakula pamoja na huduma nyingine za nyumbani. Katika kudumisha hali hii, wakuu wa wilaya wa kikoloni walitumia muda mwingi kurudisha nyumbani wake waliowakimbia waume zao. Kufikia mwaka 1950, wakoloni walishangazwa na ongezeko kubwa la ndoa zilizovunjika, wanaume wengi kuhamia mijini na ukatili dhidi ya wanawake.

|

Sasa kifanyike nini?

Ubaguzi wa Rangi na Kupuuzwa Mwaka 1866, mji wa Dar es Salaam ulianzishwa ili kuendeleza maslahi ya kiuchumi ya Sultani Sayyid Majid wa Zanzibar. Wakazi walikuwa Wazaramo, Wahindi na wachuuzi wa Kiarabu. Mfumo wa watumwa na

mabwana

ndio

uliotawala

jamii

hii. Mwaka

1887,

|

Wajerumani

walipotawala, waliuvunja mfumo wa utumwa na kuanzisha mfumo wa

ajira, ambao

ulitumia

rangi kama

kigezo

kikuu cha kupata

kazi.

Wanahistoria wanasema kwamba hali ya maisha kwa Waafrika walioishi Dar es Salaam katika miaka ya 1930 na wakati wa Vita Kuu ya Pili ya Dunia ilikuwa ya dhiki na balaa. Waafrika walioishi kwenye ukanda wa pwani ya Afrika Mashariki walianza kuingia dini ya Uislamu katika karne ya 19. Jambo hili liliendelea bila kuingiliwa na Wajerumani kwani ilionekana kuwa Uislamu una manufaa. Waafrika wengi waliohamia mjini walibadilika kutokana na mazingira ya ustarabu wa pwani, yaani kuiga mavazi ya aina fulani, kuzungumza Kiswahili na kuwa Waislamu. Huo ulikuwa wakati ambao watumwa, watu wa hali ya chini na wale waliotoka vijijini, walioongea na wasiojua Kiswahili, wote walikazana kupata fursa ya kuingia katika uchumi uliokuwa unaanza kukua. Idadi ya wakazi Waafrika Dar es Saalm ilikua polepole kabla ya Vita

| | | | |

|

"

| 20

D



Kuu

WANAWAKE WATANU..——

ya Pili ya Dunia,

lakini

iliongezeka. Kufika mwaka

kufikia

mwaka

1948,

idadi

hiyo

1956, idadi ya Waafrika ilikuwa 101,000.

Wakati huohuo, uwiano wa wanaume kwa wanawake ulipungua kutoka 141:100 hadi 131:100 kati ya mwaka 1948 na 1958. yalikuwa hayatoshelezi kabisa na

mji ulikosa huduma

za msingi

kama vile maji ya bomba, huduma za usafi, taa za barabarani, usafiri

na viwanda. Hata baada ya serikali kupunguza athari za kupuuzwa kwa muda mrefu, katikati ya miaka ya 1950, sehemu walizoishi Waafrika zilikuwa za hali ya chini kupindukia.

Ustawi wa Jamii kama Mkakati wa Udhibiti Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia ilikuwa kilele cha ubeberu na mwanzo wa kudhoofu kwake. Vita Kuu ya Pili ya Dunia ililazimu ukoloni kunyonya rasilimali zilizokuwepo katika nchi kwa kiasi walichoweza. Baada ya Vita Kuu ya Pili ya Dunia, watu waliwashinikiza watawala wakoloni Waingereza kuwapa haki zao za kisiasa na kiuchumi. Wanajeshi Waafrika walirudi kutoka vitani wakiwa na uelewa na chuki ya kutawaliwa. Hapa Tanganyika, wakoloni walitafuta njia ya kupunguza makali ya mabadiliko ya kisiasa kwa kutekeleza maendeleo rahisi ya jamii. Kwa vile wanaume, hasa wale waliotoka vitani, ndio waliotarajiwa kuleta fujo, maendeleo ya jamii yalilenga kufanya shughuli 'muafaka' ambayo ni kuanzisha kituo cha jamii cha Waafrika. Ilionekana kwamba wanawake nao wapate elimu ya watu wazima na wahusishwe katika shughuli za kiutamaduni. Kwa vile idadi kubwa ya watu walikuwa Waislamu,

ilipendekezwa

kwamba

kuwe

na

usiku

maalumu

wa

wanawake mara moja kwa wiki. Pia kuwepo chumba tofauti cha kusomea. Mwaka 1946, kamati ya kituo cha ustawi wa jamii iliamua kuwaruhusu wanawake waitumie nafasi hiyo tangu saa nane mchana hadi saa kumi na nusu jioni. Kufikia mwisho wa.karne, Klabu ya Ilala

iliyokuwa ndani ya makazi ya wasomi na watu wenye kipato cha juu, ilikuwa inatumika mara kwa mara kama mahali pa wanawake kujifunzia kushona,

Kiingereza,

kituo cha

kulelea

watoto,

kliniki ya mama

na

ui ——

WANAWAKE WATANU..——

21

|

watoto, kusoma na kuandika. Mahudhurio ya wanaume katika masomo ya Kiingereza na kusoma yalikuwa hafifu. Wanawake walichukua fursa

hii kujifunza kusoma na kuandika Kiswahili pamoja na kuazima vitabu

vya kujisomea.

|

Klabu ya Alerandra Hall, iliruhusu Idara ya Ustawi wa Jamii itumie ukumbi kwa ajili ya dansi na sinema kwa ruhusa ya serikali. Hata hivyo, wanaume hawakupenda sana kufanya kazi za jumuiya, lakini walionesha shauku kubwa kwenye dansi za kizungu ambamo wanaume walikwenda na

|

wasichana na sio wake zao. Kufikia mwisho wa 1940, Shirikisho la Huduma

la Wanawake wa Kizungu lilianza kutoa masomo ya kushona na kufuma, sherehe za chai na mauzo ya vitu vilivyotumika. Wanawake Waafrika walitaka kujifunza kusoma na kuandika Kiswahili, jambo lililoleta taabu, kwani hakukuwa na walimu. Mwaka 1948, ofisa wa kwanza mwanamke wa

ustawi wa jamii aliajiriwa. Kufikia mwaka 1949, yalikuwepo matawi 15 ya Shirikisho la Watumishi Wanawake yaliyoenea nchi nzima. Mwaka 1951, Kitengo cha Wanawake Waafrika kwenye shirikisho hilo kilikuwa na matawi 26 na vituo vitatu mjini Dar es Salaam. Pia, mipango ilikuwa mbioni kuanzisha vilabu vya wanawake Waafrika. Mwaka huohuo, Baraza la Wanawake wa Tanganyika lilianzishwa chini ya ufadhili wa Lady Twining, mke wa Gavana wa Tanganyika. Madhumuni yake yalikuwa kukuza umoja miongoni mwa wanawake wa Tanganyika, kubadilishana habari na kujenga mtandao na mabaraza mengine kwa kupitia Baraza la Kimataifa la Wanawake. Wakati huohuo pia, utawala wa Lord Twining ulipata wasiwasi kwamba shughuli za ustawi wa jamii hazikuweza kuzuia kuibuka kwa tabia za ki- Mau Mau. Wakoloni waliona Mau Mau kama ugonjwa wa akili uliotokana na wao kushindwa kuwapatia Waafrika ustawi wa maisha na burudani. Waafrika walizoea kuburudishwa na sherehe, uwindaji, wizi wa ngo'mbe, utoaji kafara na adhabu kali zilizotolewa haraka bila kupingwa. Shughuli za ustawi wa jamii zilizojumuisha masomo ya kushona na afya, au makanisa yaliyochukia mila za kipagani bila kuwapa Waafrika shughuli mbadala, hazikuweza kupunguza

| | |

| |

)

AN 22

—--

WANAWAKE WATANU...——

manung'uniko ya Waafrika. Wakoloni walitambua kwamba vijana walikuwa na nguvu lakini hapakuwa na shughuli za kuwasisimua kiasi cha kukidhi mahitaji ya hisia zao ili wasijenge tabia za ki-Mau Mau. Walipata suluhu. Waliamua .kwamba vijana wapewe shamrashamra. Hizi zilijumuisha michezo, mashindano ya ngoma za asili na dansi za kizungu,

maonesho

ya

kilimo,

mashindano

ya

kuendesha

baiskeli,

ulipuaji wa fataki na michezo ya tenisi kwa makarani na walimu wa Kiafrika. Kukatokea changamoto. Maofisa wa Serikali za Mitaa hawakutilia maanani mpango huo, kukawa na uhaba wa wafanyakazi,

mamlaka zilizohusika zikashindwa kuafikiana kuhusu ni ipi ianzishe na ni ipi isimamie shughuli za mpango wa kuendesha shamrashamra. Wengine walilaumu Wamisionari kwa kufuta ngoma za asili, na wengine wakatahadharisha kwamba mpango ulipendwa na watu wachache mno na wanawake waliwekwa pembezoni. Wakoloni waliiangalia Kenya kwa wasiwasi kwa sababu ya mabadiliko yaliyokuwa yakitokea huko. Walijaribu kuzuia mabadiliko ya siasa yasitokee kwa kuendesha mashindano ya michezo, hasa mpira wa miguu. Hata hivyo, kufikia mwaka 1955, vituo 40 vya kile kilichoitwa ustawi wa jamii vilikuwa vimekaribia kufa. Ingawa mwaka

1954, kituo

cha Arnautoglo, Dar es Salaam, kilitengeneza faida, ilikuwa wazi kwamba wakoloni waliodhani kwamba mkakati huo ungeweza kuzuia au kuchukua nafasi ya mageuzi ya kizalendo walikuwa wamejidanganya wenyewe.

——

WANAWAKEWATANU..——

23

SURA YA TATU Wanawake

Waafrika Walioishi Dar es Salaam

Ukaguzi wa kwanza wa idadi ya watu Dar es Salaam ulifanyika mwaka 1956. Kutokana na ukaguzi huu, iliwezekana kupata idadi, ijapokuwa sio kamilifu, ya wanawake walioishi Dar es Salaam katika miaka ya 1950. Picha iliyotokana na ukaguzi huo inaonesha kwamba maisha binafsi ya wanawake yalitofautiana kufuatana na umri, ndoa, umiliki wa rasilimali na muda wa ukazi jijini.Umuhimu wa vipengele hivi na mahusiano yake

ulitofautiana

miongoni

mwa

wanawake,

wengi walikuwa

Waisilamu

(asilimia 90) na wasiojua kusoma (asilimia 88). Wanawake wachache sana walikuwa wasomi, ambao wengi wao walikuwa Wakristo. Kufikia miaka ya kati ya 1950, hili kundi la wanawake wachache wasomi,

lilijumuisha wale wenye elimu ya kutosha kuajiriwa kama walimu, watoa huduma hospitalini na mjini. Maisha ya wanawake wa Kiislamu waliozaliwa Dar es Salaam yalionesha mchanganyiko wa Uislamu na mila zitokanazo na tamaduni za pwani zilizoathiri maisha ya mjini. Wanawake wengi waliwekwa ndani tangu walipobalehe mpaka walipotafutiwa waume. Hata baada ya kuolewa, waliendelea kukaa ndani. Hata hivyo, ni muhimu kusema kwamba kuwekwa ndani hakukuwa na maana ya kutengwa, bali ubaguzi wa kijinsia. Hivyo, wasichana na wanawake vijana wa Dar es Salaam, wa umri wa kuolewa, waliishi maisha yenye mipaka zaidi kuliko wenzao wa Talaka zilikuwa kitu cha kawaida, kama ilivyokuwa kuwekwa ndani. Kufuatana na dini ya Kiislamu, talaka haiambatani na ukosefu wa maadili.

Hivyo, ilionekana

kuwa

ni sawa

kwa msichana

talaka yake kutoka ndoa ya kwanza. Mtalikiwa aliweza

kutazamia

kuolewa na

24



WANAWAKE WATANU..

——

mwanamume aliyemchagua na kumpenda bila mahari. Kisheria, akipata watoto katika ndoa ya pili, watoto hao watakuwa wa mume wake wa pili. Kama

akipata

watoto

bila kuolewa,

basi wanakuwa

wake

kwa

mujibu wa sheria ya Kiislamu. Wanaume waliohojiwa walisema kwamba ndoa za pili zilikuwa za matatizo, kwani zilihusisha zaidi wanawake waliopenda maisha ya mjini. Wanawake hawa walikuwa wagumu kuridhisha, kwani walitaka kuwa na wafanyakazi,

kuvaa

na kula vizuri na kwenda

dansi na sinema.

Kwa

kifupi, hawakuwa wanyeyekevu. Kwa hiyo, kulikuwa na manufaa zaidi kwa mwanamke kutoolewa kuliko kuolewa, kwani thamani yake kama kimada ilizidi ile ya kuwa mke. Katika kundi la watu wenye umri wa kati ya miaka 15 - 45, asilimia 15 ya wanaume na asilimia 36 ya wanawake walikuwa wamekwisha achika. Katika kundi hili la wanawake, asilimia 57 walikuwa wameolewa mara moja, asilimia 25 mara mbili, asilimia 6 mara tatu na asilimia 2 waliolewa zaidi ya mara tatu. Wanaume na wanawake wengine waliohojiwa walikuwa wakiishi katika 'ndoa huru'. Inawezekana kabisa kwamba hali hii ilkuwa ya kawaida Dar es Salaam. Kinachodhihirika wazi ni kwamba wanawake walipata nafasi kubwa zaidi ya kuchagua mume pamoja na maisha waliyotaka kuishi, baada ya kujikomboa kutoka ndoa ya kwanza. Pia, kiwango cha uhuru aliokuwa nao mwanamke mtu mzima ulitegemea uwezo wake wa kujikimu. Kufikia mwaka 1950 ukahaba, kupika pombe na kuuza samaki ndizo zilikuwa shughuli zenye kuleta kipato kizuri kwa wanawake wa Dar es Salaam. Shughuli nyingine za kujipatia fedha zilikuwa ni pamoja na kupasua na kuuza kuni, kutengeneza na kuuza keki, kalimati, maharage na nazi. Ni asilimia 7 tu ya kaya za Dar es Salaam ndizo zilizokuwa na mashamba ya kulima. Wanawake wachache sana waliajiriwa katika sekta rasmi. Nafasi chache za ajira zilizokuwepo zilihitaji uwezo wa kusoma na stadi maalumu za kazi. Hadi mwaka 1952, wanawake wa Kiafrika waliokuwa na ajira walikuwa asilimia 6; asilimia 3 walikuwa vibarua. Asilimia 39 ya wanawake wote walioajiriwa nchini walitoka nchi za jirani za Msumbiji

Aa Aa

aaa

au —

WANAWAKEWATANU..——

25

na Zaire. Asilimia 82 waliajiriwa katika sekta za kilimo, misitu na uvuvi. Kwa pamoja, sekta hizi ziliajiri zaidi ya nusu (asilimia 56) ya wafanyakazi wote, asilimia

8 ikiwa

ni wanawake.

Tofauti

za mishahara

kati ya

wanawake na wanaume ilikuwa kubwa katika sekta ya kilimo, pamoja na kwamba wanawake wengi walikuwa wafanyakazi wa muda mrefu, na sio vibarua. Mshahara wa mwanamke ulikuwa chini ya shilingi 70 kwa mwezi ingawa jumla yao ilikuwa asilimia 99.98. Asilimia 4 tu ya wanawake ndio walioajiriwa katika sekta ya umma. Hao walikuwa

asilimia

1.4 ya wafanyakazi

wote

katika

sekta

hiyo.

Ingawa tofauti ya mishahara haikuwa kubwa sana, tofauti iliongezeka jinsi vyeo vilivyopanda. Mwaka 1956, wanawake waliokuwa na ajira ya kulipwa bado walikuwa asilimia 5.5. Kati ya wanawake 22,334 walioajiriwa nchi nzima,

asilimia 80 walikuwa katika kilimo. Mwaka 1957, Manispaa ya Dar es Salaam iliweka kiwango cha senti 32 kwa saa kama kiwango cha chini cha mshahara wa mwanamke mtu mzima. Kiwango hiki kilikuwa pungufu ya senti 10 chini ya kiwango kilichowekwa kwa mwanamume. Hata kufikia uhuru, mwaka

1961, wanawake walikuwa bado ni asilimia

4 tu ya watu waliohesabiwa kuwa na ajira Dar es Salaam. Katika hali hii isiyotabirika ya uzalishaji na biashara ndogondogo mjini, ni vigumu kuona sababu ambazo zingewafanya wanawake wapende ajira, hasa ya viwandani, kuliko kujiajiri wenyewe. Kwa senti 32 kwa saa, hata kahaba wa thamani ya chini kabisa angepata zaidi ya mara tatu. Ukahaba ulitoa changamoto maalumu kwa itikadi za kikoloni na Kiafrika ambazo ziliafiki dhana ya mwanamume kumdhibiti mwanamke ndani ya ndoa na hivyo kudhibiti uwezo wake wa kujipatia kipato. Hivyo, ukoloni uliruhusu ukahaba uendelee kwa kiasi kidogo ilimradi ufanywe kwa kujificha. Ukweli ni kwamba makahaba walihitajika, kwani asilimia 39 ya idadi ya wanaume Dar es Salaam hawakuwa na wake. Wanaume walipendelea kuoa wanawake kutoka

|

|

J

Ai —--

26

WANAWAKE WATANU..—

wazalishe chakula. Hivyo, wanawake walioamua kufanya ukahaba, walifanya uamuzi wa busara wa kiuchumi. Katika hoja hii, najaribu kuonesha jinsi kila msichana alivyokuja kuhisiwa kuwa kahaba. Utawala wa jiji la Dar es Salaam haukuweka taratibu kali za kudhibiti ukahaba. Wanawake waliweza kukamatwa kwa kutembea usiku 'bila kurunzi au taa'. Hivyo, wanawake waliotembea

usiku bila taa walishukiwa kuwa makahaba. Katika utafiti uliofanywa kuhusu wanawake Waafrika walioishi Dar es Salaam, wanaume waliohojiwa walisema kwamba mwanamke wa mjini ni mzigo kiuchumi, ambapo wa kijijini ni rasilimali. Jambo hilo lilikuwa na utata kidogo, kwani wanawake wa mjini walijulikana kwamba ni wachapa kazi na ni werevu kwenye biashara. Pia ni wepesi katika kuweka akiba kuliko wanaume. Kwa wanawake wachache, uwezo wa kifedha uliongezewa nguvu na

uwezo wa kijamii. Mwaka 1956, asilimia 11.2 ya kaya zote Dar es Salaam, ziliongozwa na wanawake. Kulikuwa na makabila mengine yaliyozidi kiwango hiki. Kwa mfano, wanawake wa Kimanyema waliongoza asilimia 35 za kaya, Wanyasa asilimia 19. Kiwango cha chini kilikuwa asilimia 2 ambazo ziliongozwa na wanawake wa Kimatumbi. Wamanyema walimiliki nyumba vilevile. Kufuatana na rejesta ya nyumba za kupanga ya mwaka

1956, eneo la Kisutu, nyumba 51 (asilimia 45)

kati ya 113,

zilimilikiwa na wanawake. Kati ya wamiliki 59 wa nyumba waliohesabiwa Kariakoo na Ilala , nyumba 19 (asilimia 27), walikuwa wanawake.

Hali ya wanawake wa mjini kumiliki nyumba haikuwa ya Dar es Salaam pekee, bali ilionekana Tanganyika nzima na hata Afrika yote. Tukiondoa ukungu ulioficha maisha ya wanawake Dar es Salaam, tunaweza kusema kwamba, kwa

ujumla, nafasi na uhuru katika mahusiano ya kijinsia mjini Dar es Salaam yaliwapa wanawake fursa ya kufanya maamuzi na kudhibiti ujinsi wao kuliko walivyofanya wanawake wa kijijini. Hali hiyo ilichukiwa na wakoloni, viongozi wa dini na wanaume wengine. Zaidi ya hayo, wanawake wa Dar es Salaam

. ——

WANAWAKEWATANU..———

27

Ukoloni, Tabaka, Dini na Mwanamke Mwafrika wa Mjini Kufikia miaka ya 1950, siasa za kijinsia Dar es Salaam zilidhihirisha wazi mfumo wa kikoloni uliotumia nguvu kazi ya wanaume waliohamia mjini

Kabla ya mwaka

1952, asilimia 42 ya wanaume

na asilimia 87 ya

wanawake waliohamia mijini, nchini Tanganyika, walikuwa wameoa na kuolewa. Kwa vile walikuwa hawana ardhi, wanawake hawa

hawakutarajiwa wazalishe chakula chao na watoto wao. Lakini, hili Ya i . ; Ba. lilikuwa nusu tu ya tatizo. Kisa cha hoja ya wanaume wa mjini

wa mjini hamfanyii kazi mume wake, hivyo, mume hapati kipato kutoka kwake. Wale ambao waliweza kujipatia kipato, waume wao hawakujua wanapata kiasi gani, na walikuwa hawana njia ya kuwalazimisha wake zao wawape kipato chao. Jambo hilo lilianza kuleta migogoro katika ndoa, kwani wanawake walikuwa hawaoni haja ya kumvumilia mwanamume, kama yeye mwenyewe ana uwezo wa kujikimu. Kwa hiyo, uwezo wao wa kuzalisha mali, bali ni uwezo wa kuwa na mamlaka juu

ya kipato chao na maisha yao. Ofisa mmoja wa kikoloni alitoa hoja kwamba njia ya kuimarisha familia za wafanyakazi Waafrika ni kuwaajiri wanawake katika kazi za nyumbani. Hata hivyo, alikiri kwamba, ili mfanyakazi Mwafrika aendelee, alihitaji mke aliyesoma, kwa vile tatizo lake kuu lilikuwa ujinga uliomkumba mke asiye na kisomo. Wazo hili lilielezea na kuimarisha mienendo ya maisha na tofauti za kitabaka ambazo zilikwishaanza kuonekana Dar es Salaam. Lakini Waafrika walioishi Dar es Salaam hawakutofautishwa na tabaka pekee. Kufikia mwaka 1950, kulikuwa na tofauti ya wazi katika maisha ya wanawake wengi wa Kiislamu ambao hawakujua kusoma na kuandika na yale ya wanawake Wakristo wachache waliokuwa wamejifunza Kiingereza shuleni. Mwanzo wa utengano wa makazi kati ya Waislamu na Wakristo ulianza tangu miaka ya 1920 na 1930, Waislamu walipokataa kukodisha nyumba zao kwa

| |

Ai

| 28



WANAWAKE WATANU..

———

Wakristo. Jambo hili likalazimu kuanzishwa kwa makazi ya Wakristo. Utengano huu uliimarishwa na itikadi za kijinsia zilizoathiri maisha ya wanawake. Ni muhimu basi tukatazama hali ya wanawake wasomi wa Tanganyika ili tuweze kuelewa uhusiano wao na mchakato mzima wa uhamasishaji wa uzalendo. Wanawake wasomi wa Tanganyika walikuwa tofauti na wenzao wa Nigeria, Kenya, Sierra Leone na Afrika ya Kusini,

ambao walikuwa wanaharakati wa shughuli za uzalendo. Wanawake hapa Tanganyika hawakuwa hivyo. Hali iliyojitokeza Tanganyika inahitaji maelezo mahsusi yatakayofafanua jinsi uzalendo ulivyojengeka. Utoaji wa elimu ya mfumo wa kimagharibi kwa wasichana ulichelewa kufika nchini Tanzania. Elimu hiyo ilitolewa na wamisionari wa Kikristo na sio serikali. Kufikia mwaka 1938, ni asilimia 4.34 tu ya wasichana 520,000

wa umri wa kwenda shule ndio waliokuwa shule. Karibu wote walikuwa shule za misheni. Wasichana wa Kiislamu waliokwenda shule za serikali walikuwa asilimia 3 tu. Mwaka 1946, hakukuwa na msichana hata mmoja miongoni

mwa

wanafunzi

917 waliokuwa

wanasoma

sekondari

nchini

Tanganyika. Na wasichana hawakuingia sekondari mpaka mwanzoni mwa

|

|

miaka ya 1950. Wasichana 5 waliingia mwaka 1951, wasichana 7 mwaka 1952 na 25 mwaka 1954. Mwaka 1962, mwaka mmoja baada ya uhuru, ni

wasichana 6 pekee waliokuwa kidato cha sita katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Tabora. Hivyo, katika nchi nzima, ni hao wasichana 6 tu ndio

waliokuwa wanajitayarisha kwenda chuo kikuu. Kuhusu utoaji elimu ya kimagharibi, nje ya shule ya msingi, wanawake wa Tanganyika walikuwa nyuma ya wanaume kwa vizazi viwili vizima. Julius Nyerere mwenyewe alihitimu Shule ya Sekondari ya Wavulana Tabora kwenda Makerere mwaka 1943. Kizazi chake kilikuwa cha mwisho cha wavulana waliomaliza sekondari nchini bila kundi la wasichana. Katika miaka ya 1950, wanawake wasomi jijini Dar es Salaam walikuwa wametengwa

mara tatu: kwa idadi yao ndogo; kwa dini yao;

na kwa elimu yao. Vyama na taasisi zilizokuwepo zilikuwa za kisiasa na

|

.

| —

WANAWAKE WATANU.——

29

| |

zililenga

wanaume.

hazikuanzishwa

Klabu

za

Wanawake

zilizolenga

wasomi,

na wanawake wa Tanganyika kwa sababu madhumuni

ya klabu hizo yalikuwa kuzuia wanawake wasiingie katika siasa. Hivyo, ukweli wa hoja ya kwamba kukua kwa uelewa kuhusu uzalendo ilitokana na utoaji elimu ulihusu wanaume tu na sio wanawake. Kutokana na hali hiyo, isingwezekana wanawake wasomi wa Tanganyika katika miaka ya 1950 kuwa wanaharakati. Elimu yao au maisha yao ya mjini yalikuwa kikwazo. Kwa sababu

kadhaa

zilizoingiliana, ni wanawake wa Kiislamu wa Dar es Salaam wenye umri wa makamu, na ambao hawakusoma, ndio

waliokuwa wanaharakati. Harakati zao ndizo zilizoakisi na kujaza ujasiri katika uzalendo nchini Tanganyika. Harakati zao ziliwezeshwa na vitu kadhaa: ukazi wao mjini, utamaduni wao wa Kiswahili, uwezo mkubwa

wa kupokea mabadiliko katika mahusiano yao ya kijinsia na ya ndoa. Pia, wanawake hao waliweza kuanzisha na kushiriki katika vyama vilivyowawezesha kufanya shughuli zilizowapa kipato. Vitu hivihivi viliwezesha pia mahusiano yao na TANU, nayo TANU ikatumia vema stadi zao za kujipanga. Pamoja na itikadi za kikoloni na Kiafrika zilizowafunga wanawake katika kutimiza wajibu maalumu, wanawake wanaharakati wa mjini hawakufuatwafuatwa sana. Walikuwa huru zaidi na wanaume tajiri.

|

|

)

| ——

30

WANAWAKE WATANU..

———

n Aa NA ATA

SEHEMU YA PILI Wanawake na Ujenzi wa Uzalendo Kwa nini wanawake hawa walipenda siasa za kizalendo? .

Walitarajia kupata au kufanikisha nini?

>

Mchango wao kwa Utaifa, kukua na kuendelea kwa TANU ulikuwa nini?



WANAWAKEWATANU.——

31

SURA YA NNE Bibi Titi Mohamed:

Dar es Salaam

Bibi Titi Mohamed ni mmoja wa viongozi wazalendo waliokuwa na nguvu, uwezo mkubwa na umuhimu wa pekee nchini Tanzania. Alizaliwa Dar es Salaam, na alikuwa mwanamke wa Kiislamu wa kawaida kabisa. Wazazi wake walitokea Rufiji, mama yake alijulikana kama Mmatumbi mwenye nguvu za kuogofya, na baba yake, mzee wa mjini mwenye nafasi. Bibi Titi alisoma shule ya msingi kwa miaka minne tu. Hilo halikuwa jambo la kawaida hata kidogo kwa msichana wa Kiislamu katika miaka ya 1930. Wakati ambapo wasichana wa kizazi chake walishiriki katika vikundi vya ngoma, ni wachache mno walioweza kuwa waimbaji viongozi. Kuwa mwimbaji kiongozi kulihitaji uwezo mkubwa wa kuimba na kuigiza pamoja na haiba kubwa. Hivyo, pamoja na kwamba alikuwa ni mwanamke wa kawaida wa mjini, Bibi Titi alikuwa na silika iliyomwezesha kushirikiana na kukaa na wenzake, na hivyo kuweza

kuwahamasisha na kuibuka kuwa kiongozi. Bibi Titi amehojiwa mara nyingi kwa sababu ya umaarufu wake kisiasa. Maongezi yake yanaibua dhamira muhimu katika historia ya uzalendo nchini Tanganyika. Hizi ni pamoja na umuhimu wa vikundi vya ngoma vya wanawake, na jinsi wanawake wa TANU walivyokuwa wanaharakati shupavu. Wanawake wanaharakati hawa walithubutu kuvuka mipaka ya nafasi walizotengewa kama wanawake na kuingia hadharani. Maongezi ya Bibi Titi yanaweka wazi jinsi wanawake wanaharakati walivyoweza kueleza masuala ya ukandamizaji wa kijinsia na ukosefu wa usawa kwa ufasaha mkubwa. Pia, walivyoweza kuhusisha masuala hayo na ujumbe wa TANU uliohusu usawa kwa wote.

32

——

WANAWAKE WATANU..

——

Bibi Titi anazungumza: “Mimi nilizaliwa mwaka 1926. Baba yangu, Mohamed bin Salim, alikuwa mfanyabiashara, na mama yangu, Hadija Binti Salim,

alikuwa mkulima na mama wa nyumbani. Nilipokuwa mdogo nilisoma Kuran halafu nikaenda Shule ya Serikali ya Wasichana, Uhuru. Tulikuwa wasichana

wa kwanza kusoma shule hiyo, na

nilisoma hadi darasa la nne. Ilibidi niache, kwani nilivunja ungo na sikuweza kutoka ndani. Nilikaa ndani kwa mwaka mmoja na nusu...Ukiwa ndani humo unafundishwa kupika, kufagia, kutandika kitanda, kuosha vyombo. Hakuna mchezo tena, unakaa

kama uko kifungoni. Tena uko kama mfungwa, huwezi hata kuchungulia dirishani. Ni vigumu kukueleza nilivyojihisi...ni dini yetu, na nilifahamu kwamba ndiyo mila zetu. Haya, nilikaa ndani hadi nilipokuwa na umri wa miaka kumi na nne na kuolewa na Mzee bin Haji...Unaonana na mume wako kwa mara ya kwanza unapoolewa, halafu unakuta kwamba ni mzee na wewe ni mtoto,

huwezi hata kuongea naye...

“Mume wangu alikuwa mekanika, mimi nilikuwa mke wa nyumbani. Nilikuwa na mtoto mmoja msichana, Halima Mzee...Tuliishi pamoja kwa miaka mitatu au minne, halafu akanipa talaka... Niliolewa na mwanamume mwingine, Buku bin Athumani, tuliyekaa naye kwa muda mrefu. Yeye alikuwa karani mkuu, Idara ya Maji. Tulipendana, lakini alikufa. “Nilipokuwa mdogo, kulikuwa na chama cha siasa kilichoitwa Tanganyika African Association hapa Dar es Salaam. Sikuhusika nacho, wanawake walishiriki katika Maulid. Baadaye tulianzisha Roho ni Mgeni... Nilikuwa mwimbaji kiongozi, yaani, sheheratib. Kikundi chetu kilikuwa cha dansi na muziki na wanachama walikuwa wanawake watu wazima, mimi nilikuwa mdogo kuliko

wote...Madhumuni ya Roho ni Mgeni yalikuwa umoja, ushirikiano katika mazishi na sherehe. Maulid ilipofika, tulisoma Maulid.

aa

——

WANAWAKE WA TANU

Bibi Titi akiishi Temek e, 1984

33

34

——

WANAWAKEWATANU..



“Nadhani naweza kusema kwamba kuimba kuliniwezesha kuingia katika siasa kwa sababu nilikuwa mahiri wa kutunga nyimbo na kuongoza ngoma. Vikundi vya ngoma havikuwa vya kikabila. Viliunganisha watu kutoka makabila mbalimbali. Mtu yeyote aliyependa kujiunga, alijiunga, kwani sote tuliongea Kiswahili. “TAA haikuwa na vikundi vya wanawake, bila hivyo wasingehitaji kutuhamasisha kujiunga na harakati za kizalendo katika miaka ya 1950. Mume wangu wa kwanza alikuwa mwanachama wa TAA na kila mara alikuwa akiniachia senti hamsini nimlipie ada wakati akiwa hayupo. Kulikuwa hakuna wanachama wanawake.

“Kusema kweli, TAA ilipovunjika na TANU ikaanzishwa Julai 7, 1954, watu wengi walijiuzulu. Wengi walitelekeza TANU iliyokuwa inapigania uhuru wa nchi hii. Hata watu kama Abdulwahid Sykes aliyekuwa rais wa TAA aliondoka...Siku hiyo Abdul alipojiuzulu, alimtambulisha kijana Julius Nyerere ili achaguliwe... yeye Nyerere alikuwa katibu wa TAA huko Tabora. Abdul alisema, "mimi siyo tena

rais wa hiki chama kipya, mpeni kijana huyu hiyo nafasi....” Wote hao walikuwa wafanyakazi walioogopa kupoteza kazi zao. “Nilisikia kuhusu TANU hapahapa Dar es Salaam. Shemeji yangu, Sheneda Plantan, ambaye alikuwa mwanachama wakati TAA inageuka kuwa TANU, ndiye aliyetuletea kadi na kutueleza kuhusu Nyerere na UNO...Kadi yangu ilikuwa namba 16 na ya mume wangu, Boi Suleiman, namba 15.”

“Abdulwahid Sykes alikubaliana na kijana huyu, (Nyerere) alimwona kuwa ni mwerevu na mpole sana...Sheneda alikusanya fedha ili Nyerere apelekwe UNO, lakini UNO ikaleta wajumbe wake hapa. Ukusanyaji fedha kwa TANU uliendelea... na Bwana Mkubwa akaondoka kwenda UNO, akifuatana na Justin Mponda

kutoka Songea. Mponda alisema kwamba Nyerere ndiye mtu pekee kutoka Tanganyika aliyetaka uhuru...Mponda alisema hatujawa tayari kujitawala.

——

WANAWAKE WATANU..———

35

“Halafu tulisikia kwamba John Hatch anakuja. John Hatch aliwatia Watanganyika imani. Alisema, 'Mna haki ya kujitawala...lakini ombeni uhuru kwa amani, sio vita...mkitumia vita hamtaweza kuwashinda Waingereza, kwa hiyo ombeni tu, ni

haki yenu kisheria.

“Kulikuwa na sherehe ya John Hatch katika ofisi ya TANU. Kabla ya hapo, Hatch alisema, 'niliona watu wengi walifika mkutanoni, lakini mna kitengo cha wanawake? Au wanawake wanaitwa kusikiliza tu na kisha kuambiwa waondoke?” “Viongozi wa TANU wanawake.

wakasema,

'Ndiyo, tunacho kitengo cha

Hatch akasema, 'Nataka kuonana na kiongozi wao. Ah; wakasema, 'utaonana naye kesho.

“Ukweli ni kwamba hawakuwa na mwanamke wakati huo. Unaelewa? Kila mtu alikuwa amefungia mke wake ndani ya nyumba. Kwa hiyo hakuna mtu aliyetaka kuchukua mke wake na kusema, 'huyu ni mke wangu, huyu ndiye(kiongozi), kila mtu alikataa. Wakajiuliza, 'Sasa tufanyeje?” Ndipo Sheneda aliposema, 'Nitakwenda kumleta Titi. 'Bwana, ha! Titi ameolewa; wakasema.

Lakini mme wake ni rafiki yangu. Nitaongea naye na atakuja.

“Kwa hiyo Sheneda akaja kwangu, akaonana na Boi, mume wangu...Nilimwambia Sheneda kwamba aende kumchukua Tatu Mzee ili tuwe wawili, akakubali...Dossa, mmoja wa viongozi, akatufahamisha kwa Hatch akisema, 'Huyu ni Bibi Titi binti

Mohamed, kiongozi wa Kitengo cha Wanawake.

“Lakini sikuwa kiongozi wa kitengo hicho, wala sikuwa makamu. Ohoo,

John

Hatch

akachukua

mkono

wangu

na

kusema,

r

36



WANAWAKEWATANU..

——

'Namwomba Mungu kwamba utaweza kuchukua jukumu hili bila shida. “Kutoka hapo, niliambiwa wanawake.”

kwamba

nitakuwa

mwenyekiti

wa

Bibi Titi, Kiongozi wa Kitengo cha Wanawake akiwa na Julius Nyerere, 195

— ——

Uhamasishaji

Kujiunga

WANAWAKE WATANU..——

37

na TANU

“Nawaambieni kwamba tunataka uhuru, na hatuwezi kupata uhuru kama hamtaki kujiunga na chama. Tumewazaa wanaume wote hawa. Wanawake ndio nguvu ya dunia hii. Sisi ndio tunaozaa dunia. Nawaambia kwamba inatubidi kujiunga na chama kwanza...' “Mkutano

wa kwanza wa hadhara niliohudhuria kuandikisha wanawake ulikuwa katika kilabu cha pombe...Wakati huo, swali nililokuwa nikijiuliza ni kwamba; nitapata wapi wanawake? Nitawaendeaje ghafla namna hii?...

“Tuliwapata wanawake 40 katika kilabu ya pombe, tukawachukua ofisi ya TANU. ...Wanawake walikuwa wa kwanza kujiunga na TANU. Wanaume walisikiliza hotuba za Nyerere lakini waliogopa, waliogopa kweli, lakini wanawake walijiunga. Waliunga mstari katika ofisi ya TANU wakinunua kadi. Wanaume walipeleka wake zao kuwanunulia kadi. Mimi nilificha kadi mia tatu na hamsini za watu walioogopa kuziweka ndani ya nyumba zao. Wanawake hawakuwa na woga hata kidogo, hawakuwa na kazi za ofisini

“Kambona aliporudi nilianza kuwapanga wanawake katika idara. Tulianza kukutana katika ua wa ofisi ya TANU lakini haukutosha, kwa hiyo tukawa tunakutana Anartouglo. Tukachagua viongozi wetu...Bi Kaundime kutoka Temeke; Asha binti Waziri, Temeke na

Binti Kaundime, mwingine Saada binti Kipara. Hawa ndio wanawake waliokuwepo. Kulikuwa na wengine Kinondoni, Magomeni, Buguruni na Kigamboni... Tulitembea nyumba hadi nyumba, usiku na mchana, tukingoja mlangoni na kuwasihi wafike kwenye mkutano kesho yake. Tulitembea kila mahali... "Sikusema kitu pale Arnatouglo, wakaniuliza kwa nini nimewaletea wanawake kama sitazungumza. Halima na mimi tukachaguliwa kutoa hotuba ...wakakubali kutuandikia...

—-

38

WANAWAKE WATANU...——

“Bwana eeh, nilishtuka, nilisimama kama vile Mungu kaniamuru.

Sikutazama watu nisije nikaona aibu, ilikuwa siku yangu ya kwanza, siku ya historia. Nilizungumza vizuri na watu wakanisikiliza...

“Nilisema: Sisi ni nani katika dunia hii? Mungu ametupa mamlaka. Tusijisikie wanyonge kwa sababu ya jinsi yetu. Mungu amepanda mbegu ndani mwetu, na mbegu imeota...Mungu ametupa UWEZO huo...Bila ushirikiano wetu, hatutapata uhuru wa nchi yetu. Lazima tujiunge, ni muhimu sisi kujiunga (na chama). Hakuna jingine. “Nilizungumza kwa muda mrefu na watu wakafurahi...

“Ilikuwa Oktoba 1955 Nyerere alipofika Dar es Salaam kutoka Musoma. Tulijiandaa na kuwambia watu kila mahali kwamba Nyerere ataongea Jumamosi. Karibu watu 40,000 walikuja Mnazi Mmoja. Niliongea na Nyerere, na ukweli, huu ndio ulikuwa mwanzo wa safari yetu.” Vipengele vya muundo, uongozi na nidhamu vilikuwa muhimu katika kujipanga kwa shughuli za harakati za kizalendo. Vipengele vyote hivi vilizingatiwa katika vikundi vya ngoma. Wanawake walioshiriki walielewa fika mfumo wa madaraka na umuhimu wa nidhamu pamoja na kuratibu matukio. Wanawake walimwitikia Bibi Titi kuhusu kuhamasisha watu na kuunga mkono TANU. Wanaume walisikiliza hotuba za Nyerere lakini waliogopa. Kwa maoni ya Bibi Titi, huenda Nyerere alikuwa na tatizo la lugha. Alitumia Kiswahili sanifu, cha kisomi. Alihitaji kutumia lugha ya kawaida, ya watu, kujua jinsi ya kuiongea na kuwafanya watu wacheke na kufurahi. Kama Bibi Titi alikuwa kiongozi wa wanawake,

ni kwa sababu ya uwezo wake mwenyewe

wa kuvutia

watu. Kama Kitengo cha Wanawake kilikua na kupanuka, ni kwa sababu, mwaka

1955, kwa kupitia kazi ya Bibi Titi, wanawake

walihamasika na kuweka kuhamasisha uzalendo.

nguvu

zao

zote

katika

AAA

Dar es Salaam

kujipanga

na



WANAWAKEWATANU..

———

39

SURA YA TANO Bibi Titi na Harakati za TANU Nje ya Dar es Salaam

Alipokuwa

Dar es Salaam, ambapo ni kwao, Bibi Titi aliweza kutambua

uwezo wake, na baada ya kufanya hivyo, kuondoa wasiwasi na kujiimarisha kwenye jukwaa la siasa za mjini. Kufikia mwishoni mwa mwaka 1955, Bibi Titi Mohamed alikuwa kiongozi muhimu wa TANU. Alikuwa ameonesha wazi uwezo wake wa kuhamasisha makundi makubwa ya Waafrika walioishi Dar es Salaam ili kuunga mkono harakati za kizalendo. Bibi Titi aliona kuhamasisha nje ya Dar es Salaam kama changamoto na akaichukua kwa shauku, akitambua lengo la TANU katika kuleta uhuru na umuhimu wa nafasi yake katika kufanikisha hilo. Katika kipindi hiki cha historia ya maisha yake, Bibi Titi anaelezea juu ya uzoefu na shughuli zake za TANU nje ya Dar es Salaam. Katika upanuzi wa harakati nje ya Dar es Salaam, mikutano ilikuwa inapangwa sehemu zenye utawala adui au zile zilizokuwa zinashindana kushika madaraka. Ilibidi wanachama wapya waandikishwe, fedha zikusanywe, matawi mapya yafunguliwe na fomu nyingi zijazwe ili kufurahisha

maofisa wa serikali waliotafuta sababu za kusitisha upanuzi wa TANU. Naye Bibi Titi alihitaji kuchagua kati ya siasa na ndoa. Bibi Titi anaeleza:

“Safari yetu ya kwanza tulikwenda Tanga, Januari 17, 1956. Tuliokwenda ni Bwana Mkubwa, mimi na Rajabu Diwani...Tulikwenda Tanga na Korogwe, tukazunguka mkoa mzima kwa muda wa siku ishirini na moja, kisha tukarudi Dar es

Salaam. Kamati Kuu ilipokaa iliamua kwamba ninao uwezo wa

40

——

.. WANAWAKE WA TANU

Bibi Titi akiwa mbele ya ofisi ya Tanu, 1956

——

WANAWAKEWATANU..——

41

kusafiri peke yangu.. Unajua, nchi hii ni kubwa, tusingeweza kusafiri pamoja kila wakati. Kwa hiyo, mimi nilikwenda upande wangu na Bwana Mkubwa wake. Siku hizo ilikuwa ni mimi na yeye tu tulioweza kufanya hivyo. ...Nilisafiri sana, na sio kwa niaba ya wanawake tu, hotuba zangu zote ziligusa wanawake na wanaume na nilifuatana na wanaume katika safari hizi. “Niliweza kusafiri kwa miezi mitatu mfululizo. Ningeweza kuwa Mwanza, halafu nikaenda Musoma ambapo ningepata telegramu iliyonitaka niende Dodoma. Nikiwa Dodoma napata telegramu nyingine kwenda Mbeya...

“Bahati nzuri, Mungu alinipa kipaji cha kuhutubia vizuri. Hotuba zangu zilizokuwa na msisimko zilivutia watu sana nje ya Dar es Salaam. Wanaume waliguswa kuona mwanamke anasafiri kuendeleza harakati nchini mwao. Walipata motisha, hasa kwa vile nilihutubia wakati maofisa wa usalama wapo. Nilipata kichaa! “Kuhusu wale waliowaita wanawake wa TANU kuwa ni malaya, sisi tuliwaona wajinga. Tulijua kwamba utakuja muda watambue faida ya kazi yetu, baada ya sisi kushinda. Mimi sikujiunga na TANU nikitarajia chochote...Rafiki zangu walikuwa wananiuliza, unataka kuwa malkia wa nchi? Sikutaka kuwa malkia. Nilitaka kuwa huru. Sikutarajia chochote zaidi. Nilitaka kujenga nchi yangu, kufanya maisha yetu yawe bora, nilitaka elimu kwa watoto wetu, na nilitaka kupata ardhi...Wazungu walikuwa na mashamba makubwa na sisi tulikuwa vibarua tu. Vibarua katika nchi yetu? Kwa nini? Hilo mimi sikulipenda...nilitaka maendeleo kwa watu. “Wakati huo, matatizo ya wanawake

hayakutofautiana sana

wale wa mjini. Matatizo ya wanaume na wanawake yalikuwa tofauti. Wanaume walidhaniwa kuwa bora kuliko wanawake. Wanawake walidharauliwa, hata kama wana elimu, walionekana:

42

AA

——

WANAWAKE WATANU...———

kuwa hawajui kitu....Wanawake hawakuwa na fursa yoyote kabla ya uhuru. TANU ilibadilisha hili, kwani wanawake walijitolea katika harakati za uhuru, waliwatangulia wanaume.... “Kazi na madhumuni ya Kitengo cha Wanawake ilikuwa kuunga mkono TANU...Kazi yetu ilikuwa ya siasa. Tuliitwa wajinga, tusio na aibu, kwa vile tulikuwa hatuna elimu. Tuliitwa 'wanawake wa kawaida, 'wale wasomi walikuwa YWCA na TCW...Walishughulika na maendeleo ya wanawake, mambo kama malezi ya watoto, kutunza nyumba, kazi za mikono na kadhalika. Hawakuhusika na

walikaanga vitumbua, walisuka mikeka, vipepeo na makawa, wakauza. Hao ndio waliopigania uhuru. Wanawake wasomi walikuwa hawashiriki maandamano, walikuwa wakinywa chai kwa mirija huko kwa Lady Twining, nasi tulistarehe katika sehemu zetu Ilala, Magomeni na Temeke.... “Elimu kwa wanawake ilikuwa kidogo sana kabla ya uhuru. Tulizumgumza masuala haya katika Kitengo cha Wanawake na kuyapeleka katika Kamati Kuu. Hili tulilipigania sana. Wanawake wanastahili elimu sawa na wanaume, wanatakiwa kuwa sawa na wanaume. Mwanamke anaweza kuwa daktari, mwalimu mkuu,

profesa wa aina yoyote ile. Eeeeh. “Wanawake wa rika zote walishiriki katika TANU. Vijana walikuwa TANU

Youth

League.

Hatukuwa

na tofauti za kidini, tulikuwa

wamoja, tulijenga umoja wa nchi hii... "Tulikwenda Usambara tukitokea Korogwe na Bwana Nyerere mwaka 1956, halafu tukaenda Vugha, Bungu, Bumbuli... “Tulipata shida Musoma, kwani kulikuwa na Mtemi aliyetaka kumkamata kaka yake Nyerere. Nilikuwa nakusanya fedha hadi

——..zzzaza

zaa

——

WANAWAKEWATANU.————

43

saa tisa usiku kwa ajili ya kesi ya Nyerere ili asifungwe....na nilipoondoka Musoma, Selemani Kitundu aliweza kupeleka shilingi 10,000 Dar es Salaam.

“Nilifika na

Mwanza nikakuta Paul Bomani ameweka mipango mizuri

alishawaarifu

Geita,

Uzinza,

Maswa

na Magu

kwamba

kutakuwa na mkutano (wa siri). TANU ilikuwa imepigwa marufuku Mwanza, kwa hiyo hakukuwa na tawi na hivyo maandamano yasingeweza kufanywa. Tulikusanya shilingi 28,000, tukazipeleka Dar es Salaam. Nikaenda Dodoma alipokuwa Haruna Taratibu, tukakusanya fedha, nazo zikapelekwa Dar es Salaam. Kisha nikaambiwa niende Mbeya nilipomkuta Mohamed Kissoky. Hadija Swedi alitokea Morogoro akienda Iringa, akanikuta Mbeya, napo tukakusanya fedha. Nilipata habari tena, nikaambiwa niende Tabora. Nyerere na Tom Mboya walikuwa huko. Nyerere alimwambia Tom Mboya kwamba nimekuwa nikisafiri kwa miezi mitatu mfululizo. Mboya akamjibu akisema, 'Nyumbani kwetu Kenya, hatuna mwanamke kama huyo.

Azimio la Tabora

“Mkutano wa Tabora, Januari 1958, ndio uliozalisha Azimio la Tabora, na ndio uliotufikisha kwenye kupata uhuru. Waingereza walimwambia Bwana Nyerere kwamba lazima TANU ikubali kura

yenye sehemu tatu: yaani, tupige kura kwa madaraka yenye Wazungu, Waafrika na Wahindi. Suala hilo lililetwa katika Kamati Kuu, ikatubidi tuitishe mkutano wa taifa kulijadili. Mkutano huo ulifanyika sokoni Tabora. “Watu hawakukubaliana kabisa na pendekezo la Waingereza. Majadiliano yaliwezekana kutokana na busara ya Nyerere. Aliwaeleza watu kwamba wakoloni walitaka kuchelewesha uhuru, na tukiwakatalia inawezekana tukakosa serikali yetu.

AA

——

44

——

WANAWAKE WATANU..——

Ikiwa hivyo, itabidi tuipiganie tena kwa muda mrefu na hivyo tutawakatisha watu tamaa ya sisi kushinda. Nyerere alishauri kwamba tukubali pendekezo hilo, halafu tukipata uhuru tutafanya tunavyotaka, tutatengeneza katiba yetu na uchaguzi utakuwa huru kwa hiari ya nchi... “Nyerere alikumbwa na tatizo. Nina hakika hakulala kwa siku tatu. Kila mtu alitaka tupigane. Walipinga pendekezo vikali. Siku ya tatu, Abdallah Sembe alimtetea akisema kwamba yeye ni kiongozi wetu aliyetuongoza kwa muda mrefu. Wakati huo Nyerere ameachia kiti ili atetee hoja yake. Mwalimu Kiheri wa Tanga akaongoza mkutano, akatetea msimamo wa Nyerere....Siku ya nne, watu wakakubaliana kujipa muda wa kutafakari kwa sala msikitini. Siku iliyofuatia, ikakubalika kuwa na sehemu tatu,

ilimradi watu wasilazimishwe kuhusu nani wampigie kura. Watu wachague Wahindi na Wazungu wanaowapenda. Watu walikwishaanza kufikiria, kwani Mponda aliyekataa tusipate uhuru huko UNO alikuwa mzungu? Au Rattansey aliyetuunga mkono Umoja wa Mataifa ni Mwafrika? “Tulifikia maelewano, tukaitisha mkutano mkubwa wa kihistoria

katika nchi yetu ambapo ni rais pekee aliongea, akasema maneno ya kuwapa watu moyo. Kutoka hapo, tulichagua wajumbe wa kugombea Legco....Nyerere alichaguliwa katika mchujo wa mwisho, lakini hakukaa. Alijiuzulu na kutumia muda wake wote kujenga chama.” Kuachika

kwa Bibi Titi

"Boi mwenyewe aliniruhusu kuingia TANU, tena ndiye aliyenunua kadi yangu ya uanachama. Sio hivyo tu, TANU ilimwandikia barua kumwomba nisaidie katika shughuli za TANU. Lakini mwishowe hizi safari zilimshinda. Nilikuwa nakaa nje ya nyumbani kwa miezi

——

WANAWAKEWATANU..——

45

mitatu, na nikirudi naweza nisikae hata siku kumi kabla sijasafiri tena. Boi akaniambia kwamba anataka kuoa mke mwingine. Nikamwambia sawa, niache na kazi yangu kwa sababu nimeshaizoea... Kwa hiyo Boi akamuoa Khadija, lakini walishindwana, wakaachana. Akaniambia kama nampenda niache hiyo kazi. Nikamwambia siwezi, kama unataka kuoa tena,

endelea. Akakataa, akasema hawezi kuoa tena. Nilifunga mizigo yangu nikaondoka. Tulikwenda Musoma, Ukerewe na Mriti... Nilipata talaka Novemba, 1959...”

Katika maelezo haya tunaweza kupata picha kuhusu umuhimu wa Bibi Titi katika uongozi wa TANU na ulazima wa yeye kuwa katika safari hizi.

Tunaweza

pia kuona jinsi wanawake

wanaharakati

walivyoitumikia

TANU na kulinganisha msimamo huo na ule wa vyama vya wanawake vya miaka ya 1950.

Bibi Titi hakuwa mwanamke mwanaharakati pekee aliyepata talaka. Hadija Swedi, mwanaharakati mwingine wa TANU, alipewa talaka mwaka 1957. Bi Swedi anasema kuwa watu walimshauri mumewe kwamba mke wake asipoacha shughuli za TANU yeye atapata matatizo. Bi Swedi hakuacha shughuli za TANU na alimuonya mumewe kwamba kuna watu wengi walikwishaelewa maana ya TANU na wamebakia wanachama, hivyo yeye (Bi Swedi) hataacha. Bi Swedi anadhani kwamba talaka ya Bibi Titi ilitokana na mume wake kuogopa kupoteza kazi. Msimamo wa TANU kuhusu usawa kwa kila mtu ulimaanisha kwamba siasa inashirikisha wanawake na wanaume. Lakini waliendeleza dhana ya kuomba ruhusa ya waume, ikieleweka kwamba wale wanaume waliochukia TANU kwa kuwazuia wake zao, hata hivyo wasingeunga mkono chama. Lucy Lameck, ambaye alikuwa mmoja wa wanawake wachache wasomi waliolunga mkono TANU wakati wa harakati za kupinga ukoloni, alitambua kwamba wanawake wa TANU waliopewa talaka wangeachwa kwa vyovyote vile, sio kwa sababu ya chochote walichoshindwa kuwafanyia waume zao, bali kwa vile walivyokuwa wakifanyia TANU.

46

——

WANAWAKE WATANU...———

Pamoja na kwamba Bibi Titi alihusika sana katika midahalo na mikutano mingi kuhusu mwelekeo wa TANU wa kupambana na ukoloni, yeye hakuhusika kwa undani katika kupanga mikakati na kujenga itikadi. Bibi Titi alikuwa mwanaharakati na mwenezi wa habari, yeye alikuwa 'sauti' ya watu iliyopevuka, alikuwa kielelezo kamili kwamba wanawake walikuwa na nafasi katika uongozi wa TANU. Alidhihirisha kwamba matendo na uelewa wa watu wa kawaida ndio uliokuwa roho ya uzalendo uliokuwa unajengwa na TANU. Kama Bibi Titi anavyoeleza, TANU ilifikia kilele cha kukua kwake wakati wa mkutano wa Tabora. Wazo la kukubali serikali ya utatu, ambamo Wazungu 20,598, Wahindi 76,538 na Waafrika milioni 8

wanapata viti sawa katika Legco, lilikwaza Waafrika wengi. Jambo hili lilisababisha washabiki kadhaa wa TANU kuondoka na kuunda chama pekee cha upinzani kabla ya uhuru kilichotokana na wazalendo. Nyerere alishinda kwa kuhimiza njia ya upatanishi, pamoja na kucheza na mitizamo potofu ya wakoloni ya ubaguzi wa rangi, mkakati uliodhihirisha kwamba TANU imepevuka kuliko watawala wakoloni walivyodhani.

——

WANAWAKE WATANU..——

47

SURA YA SITA Wanawake

wa TANU: Kuinuka

kutoka Gizani

Wanawake wanapodai kurudishiwa historia yao kwa utashi wao wenyewe, wataijenga na kuitambua historia hiyo wao wenyewe. Wanawake wanaoweza kuanzisha na kuendeleza mitandao ya kijamii ndio pia wahimili wa mitandao ya familia na undugu. Huwa na uwezo wa kuanzisha shughuli zinazoimarisha umoja, na hutarajiwa kuelewa matukio, mawazo na mahitaji ya wale waliopo kwenye mtandao na kutumia habari hizo kwa manufaa ya wote. Sura hii pamoja na sura ya Saba na ya nane inawaleta kwenye mwanga na kuwatoa gizani wale wanawake waliounda TANU. Zinawapa sauti wanawake wachache kati ya wengi waliosaidia kuunda maudhui ya uzalendo nchini Tanganyika. Jambo hili linafanyika kwa kumulika kumbukumbu za wanawake wanane wanaharakati wa TANU. Wanawake hao walitueleza juu ya maisha yao, mimi na Kanyama Chiume, nyumbani kwao, mwaka

1984. Kama wanahistoria, kila mara

tunakabiliwa na haja ya kuchagua kuhusu tuwasilishe kiasi gani cha yale yaliyosemwa, tufupishe kiasi gani na tuache kiasi gani. Kusudi langu hapa ni kukabili kutojulikana kwa wanawake wanaharakati wa TANU wa miaka ya 1950 pamoja na kuondolewa kwao katika historia ya uzalendo Tanzania. Wanawake hawa tuliowahoji na wengine wengi ambao hatukuwahoji, walihusiana na wanawake wengine wa TANU. Kwa sababu ya mahusiano na mfungamano huu, uzoefu wa hawa wachache utasaidia kuang'aza mwanga maisha ya hao wengine. Tatizo la kutojulikana ni moja tu ya masuala kadhaa yanayonikera. Nataka kuonesha jinsi u-nafsi wa wanaharakati hawa ulivyowekwa doa

AAA 48

—--

WANAWAKE WATANU..———

na siasa ya kizalendo. Matendo, mahusiano na mitandao ya wanaharakati wa TANU yaliunda na kujenga uzalendo nchini Tanzania. Kama Julius Nyerere alikuwa muhimu katika kuwashawishi UNO na dunia ya Magharibi kwamba watu wa Tanganyika walikuwa 'taifa kwa kiwango wanawake wanaharakati, linalojengeka', basi hawa kikubwa, walikuwa msingi wa yeye kusema hivyo. Karibu miaka 40 imepita tangu wanawake wa Dar es Salaam walipokutana pamoja kusikiliza na kuambiana kuhusu TANU. Wakatembea, wakajipanga na kukusanyika tena na tena kwa moyo wa dhati. Kutojulikana kupo katika maandishi ya kihistoria, lakini kwa wanaharakati hawa, haiwezekani wasijulikane miongoni mwao wenyewe kwa wenyewe. Kwa makusudi kabisa, walitumia utambulisho wao kijamii, pamoja na mitandao yao kusambaza ujumbe wa TANU. 'Wengi wetu wamekufa,

walirudia

kila wakati, na kisha kueleza

kwa

kirefu majina ya wale ambao bado wanakumbukwa. Ilidhihirika kwangu kwamba wanaharakati hawa walikuwa 'jamii hai,' yaani, kundi linalolea

kumbukumbu za watu wake kwa sababu wanaishi katika upatanifu na amani. Kutokana na historia za maisha yao, inawezekana kuunda historia ya pamoja ya lile kundi kubwa, wale maelfu ya wanawake ambao kufika mwaka 1955, walikuwa na kadi za uanachama wa TANU. Wanawake walioelezewa hapa walitambuliwa na wanaharakati wengine. Walikuwa viongozi asili, bila mafunzo, walioibuka kutoka jamii ya Kiislamu ya Dar es Salaam na kuchukua wajibu wa uongozi.

Ngoma, Lugha na Mijadala ya Siasa za Uhuru Jambo linalofanana katika historia za maisha ya wanaharakati wa TANU ni jinsi walivyo na utambulisho wa pamoja uliovuka mipaka ya uhusiano wa kikabila. Mahusiano ya kikabila yaliyowezesha wanawake kusaidiana yalikuwepo, bali hayakuyaathiri maisha yao ya siasa. jijini Dar es Salaam mnamo Vikundi vya muziki na dansi vilivyoshamiri miaka ya 1950 vilionyesha mahusiano mema katika shughuli za

——

WANAWAKE WATANU.

———

49

wanawake wa makabila mbalimbali. Vikundi hivi vilikuwa wazi kwa mwanamke yeyote aliyetaka kujiunga navyo. Kituo cha Arnautoglo kilipofunguliwa Desemba 1952, burudani kwa wanawake zilikuwa kati ya shughuli za kawaida za kituo hicho, jambo lililochochea vikundi vingine vya burudani kuanzishwa. Kati ya hivyo, Egyptian, Alwatan, lelemama na Bombakusema vilikuwa vikundi vya muziki vya wanawake ambavyo vilishiriki moja kwa moja katika uhamasishaji wa TANU. Kiswahili kilikuwa lugha ya nyimbo na ushairi katika vikundi vilivyopendwa na watu. Pia, kilirahisisha mawasiliano. Uwezo wa kuzungumza Kiswahili uliwapa wanawake wa mjini fursa kubwa ya zao za kikabila. Wanawake waliozungumza Kiswahili waliweza kuelewa mara moja mijadala ya siasa za uhuru na kuingiza nyimbo na kauli mbiu za TANU katika ngoma zao. Kwa namna

hii, vikundi vilikuwa mstari wa

mbele kupata mwamko wa kisiasa na kuweka hadharani uasilishaji wa Kiswahili kwa kupitia TANU. Kama

kundi

lililofungamana,

wanaharakati

wanawake

wa

TANU

walikuwa na watoto wachache. Wengi walijihusisha na mitandao ya vikundi vya ngoma kabla ya kuingia TANU, walikuwa wanawake wa makamo waliojikomboa kijamii na kiuchumi. Kundi hili lilikwishavuka mipaka ya ukabila na kuunda undugu ulioendelea kupanuka kupitia vikundi vyao vya ngoma. Wanaharakati

wa Siasa: Dar es Salaam

Tatu Mzee

Tatu binti Mzee alichaguliwa na Bibi Titi Mohamed kushika nafasi muhimu wakati aliposisitiza kwamba amsindikize kukutana na John Hatch ili kutuliza wasiwasi wake kuhusu kuwepo kwa kitengo cha wanawake katika TANU. Tatu Mzee alizaliwa katika mji wa Kikale uliopo Rifiji, wakati Vita Kuu ya Pili ya Dunia ilipokuwa inakaribia kuisha. Baba yake, Mzee bin Abad, alikuwa Myao kutoka Kilwa na alifanya kazi New Africa Hotel, na

—-

50

WANAWAKE WATANU...———

baadaye akafanya kazi ya udobi. Mama yake Tatu, Hadija binti Fundi, alikuwa dada wa mke wa kwanza wa baba yake Bibi Titi. Baba yake Tatu alipopata kazi, familia ilihamia mjini na Tatu akabaki na bibi yake. Baba na mama yake walipoachana, mama alirudi Rufiji kulima, akiwa anajikimu kwa kuuza vitumbua. Tatu Mzee hakuwahi kwenda shule. Baada ya kutoka ndani kama mwali, aliolewa na mume wake wa kwanza Hamisi bin Suleiman, aliyekuwa mhandisi wa maji. Tatu Mzee hakufanya kazi nje ya nyumbani wala kujihusisha na kazi ya siasa kabla ya kujiunga na TANU. Kama ilivyokuwa kwa Bibi Titi, Tatu Mzee alisikia habari za TANU kutoka kwa Sheneda Plantan na kutoka kwake

walinunua kadi zao za uanachama. Tatu alikaa na kadi ya uanachama bila kujua la kufanya mpaka Sheneda aliporudi tena na kusema, "Nyie wanawake mnahitajika na chama. Tupo wanaume tu. Wanawake wanahitajika wawahamasishe wengine kujiunga katika TANU.” Jitihada za nyumba kwa nyumba za kupata wanachama zilitiliwa shaka na wanawake wenzao. Iliwabidi wajibu maswali kama: TANU itawezaje kufanya mambo iliyosema itafanya? Hawa watu wa TANU wanawatumikia nani hasa? Hizo fedha zitatumikaje? Kwa akina Bi Tatu na wanawake wahamasishaji wengine, kuwaendea makundi kulionekana rahisi kuliko kwenda nyumba kwa nyumba. Walitafuta vikundi vya Lelemama na wapika pombe kwa sababu sehemu hizo zilikuwa na mkusanyiko wa watu,

ambao waliendelea kusambaza

ujumbe wa kujiunga na TANU. Kama wanawake walitiliwa shaka, wanaume waliofanya kazi serikalini waliogopa kupoteza kazi zao kama wakijihusisha moja kwa moja na TANU.

Hivyo, wanawake

walikuwa

muhimu,

sio tu kwa

wanawake wenzao, lakini pia kuandikisha wanaume kundi,

wanawake

waliweza

kuwashinikiza

wanaume

kuandikisha

wa mjini. Kama na

kuwafanya

wajiunge. Tatu Mzee alisafiri nje ya Dar es Salaam kwa shughuli za uhamasishaji, lakini zaidi alisafiri sehemu za pwani. Jinsi TANU ilivyokua,

WANAWAKE WATANU...————

Tatu Binti Mzee

51

WA WANAWAKEWATANU..

——

52



ndivyo wanaume na wanawake walivyochaguliwa kwa usawa, na wanaharakati waliitumia fursa hii. Pamoja na Bibi Titi Mohamed, Tatu Mzee alikuwa mmoja wa wajumbe wanawake wa kwanza katika chombo muhimu cha maamuzi, yaani, Kamati Kuu ya Chama. Halima Hamisi

Kama ilivyokuwa kwa Bibi Titi na Tatu Mzee, Halima Hamisi alielezwa kuhusu TANU na Sheneda Plantan, ingawaje Bibi Titi ndiye aliyemshawishi ajiunge. Halima Hamisi, aliyependa kujitambulisha kama "Mswahili, alizaliwa Bagamoyo mwaka 1925. Baba yake alikuwa mwalimu wakati wa ukoloni wa

Kijerumani na baadaye, wakati wa ukoloni wa Uingereza, alikuwa karani na mfanyabiashara. kushona nguo.

yake, Shiri binti Gulu, alikuwa fundi mahiri wa

Mama

Halima alisoma shule ya Kuran na Shule ya Msingi ya Mwambao, Bagamoyo, hadi darasa la nne. Hakuweza kuendelea na shule kwani ingembidi aende Dar es Salaam, kitu ambacho hakikukubalika wakati ule. Watu waliamini kwamba watoto wakienda kusoma Dar es Salaam watajenga tabia chafu. Hivyo, mwaka mmoja baada ya kumaliza shule, akiwa na umri wa miaka kumi na mitano, Halima aliolewa. Mume wake

alikuwa dereva wa Ikulu, na mara nyingi alimwendesha Gavana. Akiwa Dar es Salaam, Halima alijishughulisha na vikundi vya ngoma na baadaye alifundisha somo la dini katika Shule ya Kiislamu ya Mtaa wa Lumumba. Shule ya Kiislam ya Habib Punja ilipofunguliwa mwaka 1952, Halima alikwenda kufundisha humo, na ndipo alipokutana na Sheneda Plantan. Anasema: “Sikumkubalia

mie. Unajua,

wakati huo wanawake

walikuwa

hawaamini wanaume. Sikukubaliana na mawazo yake, niliyaacha hivyohivyo...lakini kwa vile umeniita (Bibi Titi) basi nitakuja.... Kama

ilivyokuwa

kwa

wanawake

wanaharakati

wengine,

Halima

aliomba kibali cha mume wake kwanza kabla ya kuamua kujihusisha na



WANAWAKE WATANU..———

53

TANU. Mume wake alimruhusu kwa maandishi kuwa kiongozi wa TANU. “Mume wangu aliandika kwamba naweza kuendelea kusaidia kama kiongozi wa TANU, kama malengo yao yalikuwa mema. Lakini baba yangu, aliyesoma wakati wa utawala wa Wajerumani alikasirika sana na kuniambia waziwazi kwamba kufanya mambo dhidi ya serikali ni hatari kabisa... Baadaye, alipoeleweshwa vizuri alishawishika kujiunga na TANU na akawa mwenyekiti wa chama huko Bagamoyo.'

Halima Hamisi alitumia kiwango chake kikubwa cha elimu katika shughuli za TANU na Kitengo cha Wanawake kuliko wanaharakati wengine wa Dar es Salaam. Kwa vile aliweza kuandika, alikuwa katibu. Lakini katika shughuli za uhamasishaji, elimu yake ilikuwa kikwazo, kwani wakazi wa Dar es Salaam hawakuamini kwamba watu wenye kisomo wanaweza kuwa wakweli. Halima Hamisi, Tatu Mzee na Bibi Titi walisafiri pamoja. Wakiwa watatu pamoja, hawakuamsha uhasama kwa watu kama ambavyo ingekuwa ni mwanamke mmoja anayesafiri na wanaume asiohusiana nao. Kwa mawazo yake, wanawake walikuwa washabiki wa TANU wenye nguvu, licha ya kisomo chao kidogo. Wanawake walijisikia kubaki nyuma kiuchumi na Halima, alikuwa mmoja wa wanawake wachache walioshuhudia ubaguzi katika ujira. “Nilipokuwa mwalimu nilikuwa napata shilingi 35 kwa mwezi. Wanaume walipata shilingi 60, na Mwalimu Mkuu alipata shilingi 80...”

Halima Hamisi na Tatu -Mzee walikuwa washirika wa karibu wa Bibi Titi katika jitihada za mwanzo za uhamasishaji. Kwa jitihada zao, pamoja na za vikundi na watu binafsi waliokuwa na mahusiano ndani ya jamii mbalimbali, TANU ilianza kupendwa na watu, kuanzia Dar es Salaam na

hatimaye nchi nzima. “...Niliolewa na mtu wa Rufiji, aliyekuwa dereva, akaniacha kabla

TANU haijaanza. Nikaolewa tena, halafu mume akaniacha kwa

———--

54

WANAWAKE WATANU...——

sababu ya TANU. Nilimwambia, kama hutaki TANU basi, niache.

Sisi tulipenda TANU kwa mioyo yetu yote.” Akikumbuka siku za mwanzo za TANU, alisema:

“TANU ilipoanza hawakukutania Anartouglo, walikutana chini-ya mti wa mwanzi. Walikuwa watu saba: Nyerere, Abdul Sykes, Dossa Aziz, halafu Titi na wengine, Oscar Kambona, Tatu Mzee, Mgeni Saidi. Nyerere alikuwa bado mwanafunzi, alikuwa akija amevaa

kaptula...Niliwaskia walipokuwa wakiongea chini ya mti, na walipokuwa wakienda Mtaa wa Lumumba niliwaona...' Mwamvita alikuwa mwanaharakati wa TANU kwa sababu:

“Tulikuwa tunatafuta maisha bora ya baadaye kwa watoto wetu na tulitaka uhuru, uhuru wa kuamua tulichotaka... Tulitarajia uhuru ulete amani... usawa, tuwe pamoja na tuishi kwa amani. Hatukutarajia kupata fedha. Hata kama sio matajiri, hatuna nyumba kubwa, tunapaswa kuwa na umoja na tuheshimiane.”

Kama wanaharakati wengine wa Dar es Salaam, Mwamvita alitumia muda mwingi akiandikisha wanachama wapya na kukusanya fedha kwa mahitaji ya chama. “Tulitembea kwa miguu siku nzima bila chakula. Ukichukua chai nyumbani na ukijaliwa kupata karanga, unanunua. Wakati mwingine

tuliweza kupata fedha za chakula kutoka ofisi ya TANU, lakini ilibidi wapige hesabu kwa makini. Wakati mwingine tulipewa shilingi mbili tu, na kama Oscar Kambona hayupo, hatukupewa kitu...” ' Salima Ferouz

Salima Ferouz alizaliwa Kilwa, akaja Dar es Salaam wakati wa Hitler. Baba yake, Ferouz bin Maftaha, alikuwa Myao. Alikuwa akiuza pembe za

——

WANAWAKE WATANU..

.———

55

ndovu akiwa na Waarabu. Mama yake, Zalfa Msuli, alikuwa mkulima.

Salima hakwenda shule, na alipokaribia umri wa miaka kumi na mitano, aliolewa na kuachika baada ya muda mfupi tu. Mnamo mwaka 1940,

alikwenda Zanzibar. Aliporudi alikuta tayari TANU inapigania uhuru kwa manufaa ya watu. “Niliuza vitumbua kupata fedha ya kununua kadi. Nilijiunga kwa sababu nilitaka uhuru na kuondokana na utumwa.... Ukoloni ulikuwa mgumu. Tuliwekwa ndani, au tuseme tuliolewa. Unakaa ndani na kuletewa kila kitu ...kinachoendelea nje hukijui, hujui kinachoendelea duniani. Kwa hiyo tulifikiria, kama tusipopata uhuru sisi, watoto wetu wataupata, lakini tufanye kazi tuondokane na utumwa... "Sisi wanawake tulikuwa na nguvu...tuliongoza njia kwa sababu ya uonevu wa watoto wetu na jinsi tulivyowekwa ndani...tulifanya kazi pamoja, tukajiunga na Kitengo cha Wanawake na kutumikia TANU, tukichangisha fedha na kuwahamasisha wengine wengi wajiunge...

“Waliokuwa wanashughulika walikuwa wengi, lakini wengi wameshakufa...hawaonekani tena juu ya ardhi...tumebakia wachache na tuko nusu usingizini....' Wakati anasema maneno haya Salima alikuwa mwenye majonzi, ambaye afya yake ilikuwa dhaifu.

mwanamke

mzee

Mashavu binti Kibonge Mashavu binti Kibonge alizaliwa Tabora wakati wa 'kibanga nazi', yaani kati ya Vita Kuu ya Kwanza na ya Pili ya Dunia. Wazazi wake, Baba Kibonge na Asha binti Hasan walikuwa wakulima kutoka kabila la Wamanyema. Akiwa bado mdogo, wazazi wake walikimbia njaa na kuhamia Dar es Salaam.

j

56

——

WANAWAKE WATANU..——

mazuri, yalikuwa yangu maisha mdogo, “Nilipokuwa ya hatukuruhusiwa kufanya kazi yoyote kabla ya kuolewa...Baada kuvunja ungo, niliolewa na mume wangu wa kwanza, nikaendelea kukaa ndani bila kufanya kazi yoyote.... Walinichagulia mume na tangu nikiwa na umri wa miaka kumi, kwa hiyo niliolewa bwana mmoja aliyeitwa Seleman bin Hamisi.”

Bi Mashavu hakuweza kukumbuka vizuri

kwamba

ni lini alijiunga na

TANU, lakini alisema:

“Mwanamke alijiandikisha TANU, halafu alimwambia mwanamke mwenzake ndani ya nyumba, na hivyo wanawake wote ndani ya nyumba walijiandikisha. Baada ya hapo, wanawaambia majirani. Hivyo ndivyo wanawake walivyokuwa wanachama wa TANU.

“Kuhusu hisia zangu juu ya ukoloni, niliona watu wakihukumiwa, wakifungwa na kunyongwa. Husemi chochote, huna sauti.” dukuduku Kama walivyosema wanawake wengine, Bi Mashavu, kalitoa

na zake kuhusu elimu, pamoja na ufahamu wake juu ya jinsi yeye wa wanawake wengine, hasa Waislamu walivyonyimwa elimu wakati ukoloni. TANU iliahidi kusahihisha jambo hilo mara uhuru ukipatikana. katika Bi Mashavu alisisitiza juu ya umuhimu wa wanawake uhamasishaji wa TANU pamoja na sababu zilizofanya wanaume wasite kushiriki. Alisema ni “Nikwambie ukweli, wanawake ndio walioleta TANU. Ukweli wengi kwamba wanawake ndio waliofanya hivyo. Wanaume

waliogopa kufukuzwa kazi. Waliambiwa na waajiri wao kwamba yeyote atakayejiunga na TANU atafukuzwa mara moja....Lakini wanawake walikuwa mashabiki wa nguvu wa TANU na wengine waliachika kwa sababu ya shughuli zao za siasa.

——

WANAWAKE WATANU..

——

57

“Huwezi kusema kwamba biashara walizofanya wanawake ziliwapa kipato cha kutosha. Kuna tofauti kati ya kuwa na kipato kinachotosha na kujikimu. Kujikimu kunamaanisha kwamba unapata kitu ambacho familia inatumia hapohapo. Maana ya kipato kinachotosha ni kuwa na ziada ya kupeleka benki. Hakukuwa na mwanamke hata mmoja aliyeweza kuweka fedha benki kwa kufanya biashara za aina hii...halafu wanaume hawakupenda wake zao wafanye hizo biashara. Walitaka wake zao wakae ndani tu, na kuwahudumia.” Bi Mashavu aliona kwamba kazi ya kukusanya fedha za chama ilikuwa muhimu kwa wanawake. Wengi wao waliweka vitu vyao rehani kama walikuwa hawana fedha ya mchango.

Binti Kipara Binti Kipara alikuwa Mmanyema aliyezaliwa Kigoma kabla ya Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia. Wazazi wake, Kipara bin Kitate na Nia binti Mgimba,

walikuwa na asili ya Congo, lakini waliandikishwa kama manamba. “Baba yangu hakuwa na kazi. Alikuwa manamba waliokuwa wanajenga barabara. Niliwaomba Waingereza wamwachie kwa sababu ya uzee, kwa hiyo nilimwokoa akarudi nyumbani kulima. “Nilipokuwa mdogo mama yangu alinikataza kwenda shule kwa sababu alihofu ningekuwa Mkristo, na kama hatukusoma Kiarabu tungepigwa. Kwa hiyo, hatukwenda shule yoyote ile." Binti Kipara aliolewa na Mwarabu, Hamrain Amed. Hakumbuki alikuwa na umri gani, lakini alipovunja ungo alikuwa amekwishaolewa. Baadaye aliolewa na Shabani Marijani aliyemleta Dar es Salaam. Alisikia habari za TANU kutoka kwa mpangaji aliyepanga nyumba aliyoijenga. "Aliniambia Mwafrika,

kwamba

siku

kwa hiyo kanunue

moja

nchi

yetu itatawaliwa

kadi... nikaenda, nikanunua

na kadi

Aa

———-

58

yangu....John

WANAWAKE WATANU...——

Rupia

na

John

Hatch,

yule

Mwingereza,

waliwahimiza watu wanunue kadi.

Binti Kipara alikumbuka kwamba Wakristo na Waislamu walimuunga mkono Nyerere, jambo lililokuwa muhimu sana kwa mafanikio yake. Wote walimpenda Mwalimu. 1984, nilipoonana na Binti Kipara alikuwa Kufikia mwaka anasumbuliwa na magonjwa. Alieleza wasiwasi wake kwamba alikuwa hajapata mabati mapya aliyoahidiwa miaka miwili iliyopita. Aliamini kwamba ni kwa sababu alikuwa hamfahamu mtu mkubwa serikalini ambaye angemkumbusha Mwalimu juu ya mahitaji yake, pamoja na wajibu wa Mwalimu kwake kama ilivyokuwa wakati uliopita. Mwasaburi Ali

Wakati namhoji Mwasaburi Ali mnamo mwaka 1984, alikuwa msikilizaji katika mahakama ya Mwanzo. Baba yake, Ali bin Musa, alifanya kazi serikalini wakati wa utawala wa Mjerumani. Mama yake, Nyembo binti Mwinyi, alikuwa mama wa nyumbani. Aliolewa akiwa na umri wa miaka kumi na mitano, akaendelea kukaa ndani hadi akawa na watoto watano. Anasema: “Wanawake hawakuwa

na sauti, chochote tulichotaka kusema

ilibidi tufuate kilichokwishasemwa na mtu mwingine... ndiyo sababu tuliongeza juhudi.... Hata kama mwanamke alikuwa na la kusema, bado alionekana hana thamani.

Mwasaburi alizungumzia mafanikio ya wanawake: “Matumaini ya usawa yamekuja kuwa kweli, kwa sababu sasa unaona wanawake madaktari, mahakimu na wengine ni karani maofisini. Zamani mwanamke alikuwa jikoni, mtu asiyekuwa na nguvu yoyote.... Hatukuwa na fursa ya kwenda popote, lakini

——

WANAWAKE WATANU..———

59

baada ya uhuru nilikuwa mjumbe wa Kamati Kuu ya UWT na mpaka sasa mimi ni mjumbe wa Kamatu Kuu ya CCM. Fatuma Abdallah Fatuma Abdallah, mmoja wa wanaharakati wa TANU mwenye shauku

kubwa, alizaliwa Ubungo, nje kidogo ya mji wa Dar es Salaam. "Sikumbuki nilizaliwa lini, kwani tulikuwa hatuhesabu miaka. Mimi ni Mmatumbi. Mama yangu, Shida binti Mkweju, alikuwa Mzaramo. Baba yangu, Abdallah Athumani Mbonde, alikuwa dobi, na mama, mkulima.

“Nilipokuwa mtoto, nilimsaidia mama kulima mpunga na kufukuza ndege. Sikwenda shule... niliolewa na Abdallah Mwitanga nilipokuwa na umri wa miaka kumi na mitano.

“Kwa bahati nzuri, ilikuwa baada ya talaka ya kwanza na kuolewa tena ndipo niliposikia habari za TANU. ..Nilikuwa nauza kuni, nikakutana na John Rupia, akasema kwamba wanawake wanapaswa kuchangamka, kwani kuna kitu kinakuja...ilikuwa siri kwamba TANU ilikuwa inaanzishwa. “Sasa kuna siasa. Tunaye Baba wa Taifa letu. Tuna uhuru wetu. ...Baba yetu wa Taifa alisema,

'Ha! Wanawake, kazi yetu bado ni

ile ile. Sio?...Nataka watu wenye nguvu za kuanza kufanya kazi. Tubadilishe sura ya Magomeni nzima, ili watu wakija waone kwamba sisi ni imara. “Tutaibadilishaje?”

tulimuuliza.

Tuibadilishe kwa kuondoa vibanda vyote, tujenge nyumba mpya. Wageni wakija waone kwamba mji umejengwa vizuri. Wanawake mnakubali?” “Ndiyo, tunakubali. ...Tukaenda Mwembe Chai, tukajenga nyumba kumi bila kulipwa chochote. Ulikuwa mchango wetu...

sa ——

60

WANAWAKE WATANU..———

wengine wengi, Bi Fatuma

Kama

kwamba

muhimu

Nyerere,

aliwakumbuka wale wanawake sana katika miaka ya 1950. Hitimisho:

Mwendelezo,

Rais

alisisitiza kuwa na

kiongozi

wanaharakati

Kumbukumbu

ni jambo zuri na wa

ambao

CCM,

bado

aliwategemea

za

Pamoja na Jamii ya Upendo

Mwanzoni nilisema kuwa hali na mifumo fulani ilikuza ufahamu na hisia za umoja katika kundi la wanawake wanaharakati wa Dar es Salaam. Lakini 'hali' na 'mifumo' pekee haviwezi kuelezea ni kwa nini wanawake

hawa, na maelfu ya wanawake

kama wao, walitokea kuwa

wanaharakati wa TANU. Ni kitu kimoja kusema kwamba ilikuwa rahisi kwa wanawake wa umri wa kati, walioachika, Waislamu, wasio na elimu

wala watoto wadogo, kuwa kwa wanawake vijana wa maelezo hayo hayatoshelezi mvuto katika siasa za TANU

wanaharakati wa TANU, kuliko ilivyokuwa Kiislam au Wakristo wasomi. Lakini hata kufafanua ni nini hasa kilikuwa kiini cha kwa wanawake Waswahili wa mjini.

Katika mahojiano haya, dhamira kadhaa zilidhihirika: >

Wanawake walivutiwa na mawazo ya utu na haki ya kujitawala; haki ya kuamua wanachotaka; usawa kati ya watu wote bila kujali rangi, jinsia au elimu pamoja na kutokuwepo kwa ubaguzi wa aina yoyote. Wanawake hawa waliyatazama malengo haya na hali sambamba na kujitawala uhuru ya kupata vile kama kikoloni, na unyonyaji wa zilizosababishwa ukandamizaji; ubaguzi; hali ngumu ya maisha, ukosefu wa usawa; ukosefu wa elimu na ajira pamoja na ukosefu wa heshima kwa Watanganyika. Ni wazi kwamba masuala ya jinsia yaliathiri uzoefu wao wa ukandamizaji wa kikoloni. Hivyo, msimamo wa TANU wa kutokomeza ubaguzi wa kijinsia au dini uliwagusa sana wanawake hawa waliotamani watoto wao, hasa



WANAWAKEWATANU..———

wa kike, wapate elimu na kazi walizonyimwa ukoloni wa Kijerumani na Kiingereza.

61

wao

chini ya

Wanawake walitumia itikadi ya TANU kutoa changamoto kwa ile hali ya maisha yao ya ukosefu wa usawa kijinsia pamoja na ukandamizaji. Hali hiyo ilidhihirika wazi katika jamii zao. Katika mahojiano yote, wanawake walirejea maisha yao ya kuwekwa ndani pamoja na ukosefu wa uhuru katika ndoa. Walirejea hisia zao kwamba wanaume waliwaona wanawake kama viumbe wasiojiweza, wasiokuwa na utu. Haraka, wanawake walitambua

fursa ya kutumia TANU kama njia ya kuleta mabadiliko yaliyozingatia usawa kwa wote na umuhimu wa wanaume na wanawake kufanya kazi pamoja kama njia ya kuleta heshima na utu. Mwelekeo huu mpya ulitoa changamoto kwa hali yao ya kijamii. Katika mtazamo huu, harakati za kijinsia na zile za siasa zilihimiliana. Hata pale wanawake walipoeleza kwamba walihitaji ruhusa za waume zao kushiriki katika siasa, walijua wazi kwamba chama kiliunga mkono haki yao ya kushiriki shughuli za umma. Jinsi wanawake wanaharakati wa TANU walivyoongezeka, ndivyo ilivyokuwa vigumu kwa waume zao kuwanyima kushiriki, wakiogopa kubezwa na jamii. Wanawake walijithamini zaidi jinsi walivyoona matokeo ya jitihada zao na walivyotambua kuwa nguvu ya umoja wao ni nguvu yao kisiasa.

62

——--

WANAWAKEWATANU...

——

SURA YA SABA Wanaharakati wa Kilimanjaro na Moshi Mjini 1958. TANU ilienea haraka nchini Tanganyika kati ya mwaka 1956 na yika Serikali ya ukoloni ilianzisha chama cha upinzani- United Tangan o Party (UTP). Twining alikuwa na njozi ya chama mbadala ambach kingepata nguvu za kifedha kutoka katika viwanda vya katani, vyombo machimbo ya madini, kahawa, biashara, wakulima Wazungu, na u) na (Mzung vingine. Chama hiki kingeendeshwa na katibu makini na wasaidizi wawili - mmoja Mhindi na mwingine Mwafrika o kingepigania haki za jamii ya mbari mbalimbali, chama ambach ya haraka kingetoa fursa sawa kwa wote na kuleta maendeleo ya

kiuchumi kwa Mwafrika. Siasa za Kikabila na TANU katika Jimbo la Kaskazini

ya Mji wa Moshi ulikua kutokana na mahitaji ya kiuchumi, kisiasa na jaro. Kiliman usafiri wa watu walioishi kwenye miteremko ya Mlima Sehemu hii ilitoa changamoto ya pekee kwa wahamasishaji wa TANU. Wachagga walilima kahawa kama zao la biashara na walipeleka watoto na wao - asilimia 90 mwaka 1956 - katika shule nyingi za Kiluteri Katoliki zilizokuwa zimesambaa kwenye miteremko kufikia mwaka 1951. walimiliki Wakati huo, kulikuwa na wachuuzi Wachagga 3,000. Waafrika

asilimia. 80 ya maduka na walikuwa wanapanga mkakati wa kuwafukuza Wahindi Kilimanjaro. Ushindani kati ya misheni za Kiluteri na za Katoliki zilikwishaugawa mlima na watu wake. Kwa hiyo, wamisionari kutoka na Uingereza, Marekani, Ufaransa na Ujerumani walipofika, waliungana maofisa wa kikoloni, wakamalizia tu picha ya mgawanyiko huu.

——

WANAWAKE WATANU..————

63

Moja ya changamoto iliyoikabili TANU ni uzalendo wa Kichagga ambao ulikuwa unakuzwa na Thomas Marealle, mjukuu msomi wa mtemi mashuhuri, Mangi Marealle. Thomas Marealle alikuwa mzungumzaji mkuu wa TAA wakati akifanya kazi Idara ya Ustawi wa Jamii, Dar es Salaam hadi alipoitwa na kushawishiwa kupigania umangi mkuu. Alishinda kirahisi. Siku ya kutawazwa kwake kuwa Mangi Mkuu ilikuwa tukio lililosheherekewa kila mwaka kama siku ya Wachagga. Kukaundwa bendera na wimbo wa Wachagga. Gavana Twining akawa na matumaini kwamba uzalendo wa kikabila, utajiri pamoja na elimu uchagani, vitakuwa motisha ya kutosha kukipinga TANU Wakati ambapo TANU ilikuwa inaenea haraka katika sehemu nyingi za nchi, ni mafanikio kidogo tu yaliyopatikana sehemu za Mlima Kilimanjaro. Tawi la TANU la Wilaya ya Moshi lilikaribia kufungwa mwaka 1957 kwa kukosa fedha. Kufikia Feruari 1958, kati ya watu 365,000, wanachama walikuwa 7,710. Kati ya hao, wanachama 2000

walitoka Hai ambako Mangi Abdiel Shangali aliupinga utawala wa Mangi Marealle. Kabla ya 1950, wanawake binafsi wa Kichagga - wake au mama wa wamangi au wapenzi wa watu mashuhuri- waliweza kuiathiri mifumo ya siasa katika jamii zao. Hata hivyo, mwaka 1937, wanawake wa kawaida waliongoza 'mgomo wa kahawa' uliotokea wakati wa utawala wa Kiingereza kutokana na punguzo la bei ya kahawa. Wanawake walivamia mashine na vyombo vya kupimia, wakawatukana wale walioshiriki na wakoloni na wakawakabili polisi waliopelekwa kutuliza fujo hizo. Hivyo, kama ilivyokuwa katika sehemu nyingine za nchi, wanawake wa Kilimanjaro waliweza kujieleza kisiasa wakati wa ukoloni kwa kufanya matendo ya moja kwa moja na sio kwa kupitia chama.

Wanawake wa Kilimanjaro na Klabu za Maendeleo Wakati TANU inaanza kuingia Kilimanjaro mwaka 1955, maofisa wa ustawi wa jamii walikuwa wameshaanza kuwahamasisha wanawake na wasichana wa Kichagga.

Maofisa wakoloni walikuwa na wasiwasi na

64

———

vijana wanaume

waliokuwa

Moshi, Arusha, Mombasa

WANAWAKE WATANU..———

wamefeli

mitihani

na kukimbilia

mijini

na Tanga. Wale waliomaliza darasa la nane

walionesha kupenda sana TANU, ambapo waliomaliza darasa la nne waliishia kuwa wahalifu. Maofisa Wazungu wa Ustawi wa jamii walipendekeza kuundwa kwa klabu za wasichana na wavulana ambako wangefundishwa

Kiingereza, hesabu, uraia, elimu ya viungo, kuimba,

useremala na uashi. Masomo ya kupigana ngumi, kuogelea na kukwea kwa kamba yalikusudiwa yatoe mkondo wa kufifisha nguvu za vijana za kupenda maisha. Wasichana wangejifunza kusuka mikeka na vikapu, sayansi kimu na malezi ya watoto. Netiboli ingewachangamsha viungo. Pamoja na michezo, miradi ya kufanyiwa nyumbani ilihimizwa, ikiwa ni pamoja na kufuga kuku, kilimo cha mbogamboga na ufugaji wa ngo'mbe na mbuzi. Klabu za wasichana ziliwashirikisha wale waliomaliza darasa la nne tu na sio wale ambao hawakwenda shule. Klabu zile za wanawake zililenga akina mama wenye 'heshima,' walioolewa, ambao waliruhusiwa kuingia katika klabu kwa kura za wajumbe wa kamati ya klabu.

;

.

.

AA

A

i

Ad A-

Wanawake wa rangi tatu: Mzungu, Mwafrika na Mhindi wakiwa pamoja. Klabu za miaka ya 1950 zililenga muungano wa namna hii



Klabu ziliwahimiza

WANAWAKE WATANU..

wananchi

wazingatie

———

65

maendeleo

yao, hususan

wanawake Waafrika walihimizwa kujihusisha kikamilifu katika jamii yao. Klabu zilikusudia kuwapa fursa ya kufahamu vitu vingi zaidi na kufurahia maisha kwa kuimba, kuigiza na kushiriki katika mashindano.

Wanawake wa TANU wa Mjini Wanawake walijiunga na TANU kwa sababu mbalimbali, ikiwemo shauku ya kupata uhuru kutoka ukoloni. Waliingia TANU bila uzoefu wa siasa, jambo ambalo walilirejea mara kwa mara katika mahojiano. Pia, wanawake walielezea kuhusu tabia ya wanaume ya kutowapa heshima. Hata hivyo, matendo ya wanawake yalikuwa ya kisiasa. Walijipanga na kuandamana kutoa malalamiko yao kwa utawala ulioweka taratibu zinazodhoofisha,

walilalamikia

shida

za

kiuchumi

pamoja

na

ukandamizaji wa tawala za kienyeji. Lakini, wanawake hawakuwepo katika safu za uongozi au uanachama wa TAA, au katika vyama vya ushirika vya wananchi. TAA ilikuwa chama cha wasomi na wale waliokuwa na ajira serikalini au wafanyabiashara matajiri. Hali ya wanawake kutomiliki ardhi au mazao ya biashara kuilisababisha kutokuwepo kwao katika vyama vya ushirika. Hata hivyo, kulikuwa na mabadiliko yaliyokuwa yanaanza kutokea miongoni mwa wanawake, na kwa manufaa yao ambayo yaliathiri Shauku yao ya kuelekeza nguvu zao TANU. Mabadiliko hayo yalikuwa mvuto wa misheni, ongezeko la upataji wa elimu, ufadhili wa klabu na kuendelea kudhibitiwa na waume, baba, tawala za kienyeji na kamishna wa wilaya.

Wanawake wa Kilimanjaro na Moshi waliojiunga na TANU na kuwa wanaharakati katika miaka ya 1950 walikuwa na sifa bainifu zilizofanana na wenzao wa Dar es Salaam, ingawa maelezo yao yalitoa

mwanga

uliomulika

uzoefu wa ukoloni katika eneo lao.

Ili kuelewa jinsi walivyofanana

na kutofautiana,

natoa

historia za

maisha ya wanawake wa TANU zilivyokusanywa Moshi, mwaka 1988.

Aa 66

——

WANAWAKEWATANU...



Halima Selengia Kinabo

Nilipokutana na Halima Selengia Kinabo, mwaka 1988, katika ofisi ya kwa Basila Urasa, alikuwa kiongozi wa kikundi cha wanawake ambacho

miaka 25 kimemiliki Hoteli ya Shangazi. Kwa mujibu wa tafsiri ya Anita Marangu. Baba yake, Selengia, alikuwa Mangi. Mama yake aliyeitwa Hija, alikuwa mkulima wa migomba, kahawa, ulezi na maharage. Mama yake aliachana na mumewe, akalea watoto wake watatu peke yake. Bi Halima hakupelekwa shule, lakini alimghasi kaka yake amfundishe kusoma na kuandika. Pia, alimchunguza mama yake akifanya biashara ndogondogo, akafanya kazi na mama yake hadi alipoanzisha biashara yake

mwenyewe. Halima alipokuwa na miaka kumi na mitano, aliolewa na Athumani Abdallahrahmani, akazaa naye watoto wawili. Baadaye, waliachana. Bi Halima anaeleza jinsi alivyoingia TANU: “Kila mara nilipokuwa natoka kazini, nilikuwa nakutana na Mwenyekiti wa TANU, Yosufu Olotu. Alikuwa akiniambia, 'Bi

Halima, jiunge na TANU.' Nami nikimwuliza, 'TANU ni nini?'

“Naye akinijibu, 'TANU ni uhuru.' Maana ya uhuru ni kwamba tutajitawala. “Mbona nasikia TANU ni mbaya?” nilimwuliza “Aliniambia, 'Hapana, siyo kweli."

“Nilikutana naye mara nne, na kila mara alinishawishi nijiunge. Mwisho nikajiambia, kwa nini anaendelea kuniomba hivi? Mwishowe, nilipojiunga, nami nikawa nashawishi wengine wajiunge...”

——

WANAWAKE WATANU..——

67

Bi Halima aliendelea kueleza jinsi viongozi wa TANU wa hapo walivyokutana na kujadili matatizo ya kukabiliana na UTP na habari zingine dhidi ya TANU. Walihitaji kufanya uamuzi wa kumwita Nyerere kuja kutathmini hali na kuona jinsi ambavyo angesaidia. Wazee watano walipokuja kumwuliza kama atamweka Nyerere nyumbani kwake, alikubali. Yeye na Bhoke Munanka wakakaa kwake. Munanka alikuwa Katibu wa TAA huko Mwanza mwaka 1950. TAA ilikuwa inasuasua na akaifufua yeye pamoja na Paul Bomani na Saadani Kandoro. Pamoja na kwamba Munanka hakupendezewa kabisa na wazo la serikali ya utatu, bado aliendelea kuwa mshiriki mwaminifu wa TANU. Hivyo, kati ya watu wengine waliokuja na Nyerere, alikuwepo pia Bibi Sophia Mustafa, mama wa Kihindi kutoka Arusha, mjumbe mwakilishi wa jamii ya Kihindi, na Derek Bryceson, chaguo la TANU kutoka kambi ya Wazungu. Baada ya Nyerere kuondoka kwenda kuhutubia mikutano huko Majengo,

Kilema,

Mamba,

Useri

na

Arusha,

Halima

naye

alifunga

milango na kufuata. Wanawake ndio waliokuwa walinzi wa Nyerere na Halima alieleza kwamba wanawake ndio waliosambaza habari za matukio yaliyopangwa kutokea. Kuhusu hali ya wanawake, Halima alisema walichosema wanawake wote, kwamba hawakuwa na sauti. Kama wanaharakati wengine wa Dar es Salaam, Bi Halima alielewa kwamba mbali na uhuru na utu, matunda

ya kujitawala yangetegemea sana mipango thabiti na kazi ngumu. Mwamvita Salim

Mwamvita anakumbuka kwamba alikuwa amekwishazaliwa wakati Waingereza walipopandisha bendera yao, baada ya Wajerumani kushindwa katika Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia. Baba yake, Mzigua kutoka Tanga, alikuwa amekufa. Mama yake, Asha, alikuwa Mmasai, naye alikufa Mwamvita akiwa na umri wa miaka mitano. Aliishi maisha magumu ya uyatima, akaolewa na Omari Mziray ambaye alimwacha akiwa na miaka ishirini na mitano. Hakupata watoto, lakini alilea watoto watano wa dada yake.

A aa A w WA 68



WANAWAKE WATANUo



Alielezea ushiriki wake katika TANU:

“Nilikuwa siko katika kikundi chochote kabla ya TANU. Nilisikia habari za TANU kutoka kwa marehemu dada yangu mdogo aliyekuwa Dar es Salaam na mmoja wa waanzilishi wake. Alinipelekea ujumbe kwamba TANU yaja, nisikatae kujiunga. Tangu Nyerere aje hapa, tumekuwa naye hadi tukapata uhuru. Tuliwahi hata kumvisha baibui ili wakoloni wasimtambue. Nilikuwa mlinzi wake, nikipika chakula chake kama alivyofanya Zainabu Hatibu na Fatuma Makwaia. Lakini mimi ndiye niliyechaguliwa mahsusi na TANU kumlinda asije akadhurika. “Nilikuwa katika kikundi kilichokuwa kinacheza ngoma kupata fedha zilizokwenda TANU. Nilikuwa pia na ukumbi wa dansi KNCU, na fedha kutoka huko pia ilikwenda TANU. “Wanawake walikuwa jasiri kuliko wanaume. Hatukuogopa kufa...Nilikuwa nawaambia wanaume wanunue kadi halafu waweke sandukuni mpaka tupate uhuru, ndipo wazitoe. Kwa vile Mwamvita aliongea Kimasai, alikuwa mtu muhimu mno katika kuanzisha matawi Umasaini. Matawi “Nilifikiria ningefia Umasaini. yalianzishwa na sisi. Nilikuwa nawafundisha TANU, walinielewa na kununua kadi.... wazungu kadhaa sehemu ya mkutano

unapenda TANU?' Nikajibu, 'Sana.' Wakauliza,'Unaipenda kiasi gani?” Nikawajibu,'Kama roho yangu.'

'Na kama usipokuwa na TANU?' wakauliza.

yote unayoona Wamasai kuhusu

Siku moja walikuja wakaniuliza, 'Mama,

——

WANAWAKE WATANU..———

69

“Itakuwa kama roho yangu imechukuliwa.' Niliwaambia ukweli. Walicheka na kuondoka. “Matatizo ya wanawake yalikuwa tofauti na yale ya wanaume. Huku mlimani, wanawake walifanywa kama punda. Walisafisha zizi, walikata majani ya ngo'mbe, walichanja kuni na kutunza mashamba huku waume zao wakiishi mjini. Baada ya uhuru, sisi

tuliokuwa jasiri tulikataa, tulisema siyo haki binadamu kutendewa

kama myama" Zainabu Hatibu

Alizaliwa Desemba 29, 1939. Mama yake, Mwamvita Athumani, alikuwa

na wazazi mchanganyiko wa Mmasai na Mchagga na wazazi wa baba yake, Hatibu, walikuwa Mpare na Mmasai. Baba yake alikuwa mganga katika hospitali ya Mawenzi. Zainabu alisoma hadi darasa la sita, kisha akaenda shule ya Koran. Aliacha kusoma alipofika miaka kumi na mitano, akaolewa na Mwarabu, mmiliki wa hoteli, mjini Moshi. Zainabu alikuwa kijana, miaka kumi na sita au saba, alipojiunga na TANU. Alijiunga na Umoja wa Vijana wa TANU baada ya kusikia habari zake kutoka kwa wanaharakati, akina Abdul

Rahman,

Bakari Abdi na

Akida Hamisi. Anaeleza: “Kulikuwa na makundi matatu katika Umoja wa Vijana. Kundi la kwanza lilikuwa la waimbaji, la pili lilikuwa la wanawake vijana, akina Mwamvita na wengine ambao walikuwa walinzi hapa Moshi. Kundi la tatu lilishughulikia wageni. “Mimi nilishughulika sana kwenye TANU mpaka tulipopata uhuru. Niliwahudumia

wageni, niliwapa chakula, wakilazwa

niliwatunza...hata nilikuwa namwomba niwapikie chakula...

Mawenzi

baba yangu fedha ili

“Tulijiunga na Umoja wa Vijana kuimarisha TANU. Tulikuwa vijana

AA WANAWAKEWATANU..

——-

70



kwelikweli, siyo hawa wa leo...Tulikuwa kama CID, wapelelezi wa kikoloni, tukipeleleza watu na kutoa habari. Tulikuwa tukionekana Moshi asubuhi, lakini tunafanya mikutano Arusha, watu walikuwa

hawawezi kujua tuko wapi.” Morio Kinabo

Morio

Kinabo

alinikaribisha

sebuleni

kwake

Pasua, Moshi, Oktoba

8,

1988. Alikuwa mtoto wa Mangi Kinabo Namfua wa Rombo. Kwa vile alikuwa mtoto wa Mangi, maisha yake ya utoto yalikuwa mazuri, lakini aliona maisha ya watu wengine yalivyokuwa mabaya. Morio alisoma shule ya misheni kwa miaka miwili, kisha akaacha. Ndoa yake ilikwishapangwa, na kwa vile wasichana hawakuruhusiwa kufanya chochote, hakuona haja ya kusoma, kwani akitoka nje tu heshima yake inaharibika. Bi Morio aliolewa

na Lot kutoka

Rombo.

Lot alikuwa

kibarua, na

waliishi Mombasa kwa miaka saba. Hata hivyo, Morio alichoshwa na maisha hayo, na aliposikia kwamba kiwanda cha kukausha kahawa kinaajiri wanawake, alirudi Moshi na kuwa mmoja wa watu mia saba walioajiriwa. Baada ya muda alichaguliwa kuwa msimamizi wa wanawake ambao aliwafundisha kuchambua kahawa. "Katika kiwanda,

mshahara

wangu

kama

msimamizi

ulikuwa

shilingi 60 kwa mwezi. Hizo zilikuwa fedha nyingi, kilo ya nyama iIkuwa senti 50 tu. Wachambuzi walipata shilingi 40. Niliwatetea hadi wakapata shilingi 60, na mshahara wangu ukaongezeka hadi shilingi 120 kwa mwezi. Nilifanya kazi kwa miaka kumi na minane. “Nilijiunga na TANU kwa sababu tuliamini kwamba uhuru ni kitu

kizuri. Mimi nilikwishashuhudia ubaguzi nikiwa msimamizi wa wanawake mia sita na wanaume mia mbili au tatu. Kwa mfano, wafanyakazi hawakuruhusiwa kunywa maji nje, walitumia mabomba ya chooni. Siku moja nilimkabili mzungu na kumwambia kwamba sitaki kufanya kazi tena. Akauliza, 'kwa

——

WANAWAKE WATANU..——

71

nini? Nikamwuliza kama aliona ni haki tunywe maji kutoka chooni. Aliniuliza kama hilo jambo ni baya, nikamjibu kwamba ni baya, maji ya kunywa yanapaswa yatoke kwenye bomba lililo nje. Walikuwa wanatudhalilisha kwa kutufanya tunywe maji kutoka chooni. Aliniambia atanifukuza kazi, nikamwambia sijali. Tunatafuta usawa kati ya Mwafrika na Mzungu...

“TANU ilipoanza, tuliuza kadi kwa siri. Viongozi wakanichagua kuhutubia katika mikutano wilaya nzima..." Katika siasa, Bi Morio alileta uzoefu na uelewa wake wa hali ya maisha ya wanawake pamoja na wafanyakazi na watu maskini wa mlimani. Rombo ilijulikana kuwa ni sehemu maskini kuliko zote. Bi Morio aliamini kwamba alibugudhiwa sana kwa sababu ya shughuli zake za kisiasa, na alitishiwa maisha na watu walioipendelea UTP. Kubugudhiwa kwa Morio kunaweza kuwa kielelezo cha uhasama uliokuwepo kati ya TANU na UTP. Pia, hali hiyo inaonesha ni kwa nini kazi za siasa zilionekana kuwa siyo nzuri kwa wanawake.

Violet Njiro Alizaliwa Marangu mwaka 1930. Baba yake, Semalik Samu, alimiliki duka la nyama. Mama yake, Ndeambilisia Mtui, alikuwa mkulima. Akiwa

mtoto mdogo, Violet alilima pamoja na mama yake. Ingawa baba yake hakwenda shule, lakini alitaka watoto wake wasome, hivyo, Violet alisoma hadi darasa la sita. Baada ya hapo alitaka kuwa nesi, akaomba

shule huko Kenya, akapata. Kwa ruhusa kurudi kuhudumia vijiji vya mlimani. Aliolewa akiwa na miaka ishirini Wakahamia Moshi ambako alifanya kazi Akiwa kazini, alisikia habari za TANU

ya baba yake, Violet alisoma na

na mmoja na Gideon Njiro. katika hospitali ya Mawenzi. kwa mara ya kwanza. Karibu

apelekwe jela alipoulizwa kama amenunua kadi ya TANU.

72

——

WANAWAKE WATANU..———

Violet alieleza: "Sikudhubutu kukubali, watu walikuwa wananyamaza tu, kwa hiyo nilijibu, Hapana, wala sijui chochote kuhusu jambo hilo.

“Tutakupeleka jela sisi, tumeshaona kwamba unaanza chama kibaya cha siasa hapa.' Tulinyamaza tu, na muda si mrefu TANU ikawa kila mahali...” Violet Njiro alivutiwa na siasa kwa sababu ya hali ya maisha yake ya kazi. Licha ya mshahara mdogo, alipoolewa alifanywa kuwa mfanyakazi wa muda na angeweza hata kufukuzwa kazi. Mwanamke akipata mtoto anafukuzwa kazi hapo hapo. Kwa kuzingatia usawa kwa watu wote, TANU ilisaidia kuwakomboa

wanawake. Kabla ya hapo, wanawake walikuwa hawaruhusiwi kutoka nje, na walitegemea kupigwa na waume zao wakati wowote wakikutwa wametoka. Elizabeth Gupta

Elizabeth alizaliwa mwaka 1922, katika wilaya ya Same. Baba yake, Tenga, alikuwa Mnyamwezi kutoka Tabora. Alifanya kazi katika reli ya Tanga, katika kambi ya Same. Huko, alikutana na mama yake Elizabeth, Shuhute

Mgoloka,

na

kumuoa.

Familia

ilihamia

Tabora,

ambako

Elizabeth alisoma shule ya msingi kwa miaka sita. Baadaye, alifanya kazi ya kibarua kabla baba yake hajahamia Moshi alikofanya kazi ya mtunza

ghala katika shamba la katani la Mjerumani. Alipokuwa na miaka ishirini na mmoja, aliolewa na Aljansi Gupta, wakahamia Ifakara, Morogoro. Bi Gupta alisikia habari za TANU mwaka 1955, akanunua kadi yake mwaka

1956 baada ya yeye na mume

wake kurudi Moshi na kuishi

Isingekuwa busara kwa Bi Gupta kutojiunga na TANU. Alikuwa na shauku ya kumaliza ugandamizaji wa kikoloni, ambapo kulikuwa hakuna mwenye sauti, wanawake wala wanaume. Wanawake waliumia zaidi kwa kugandamizwa tena na waume zao. Wanawake hawakuthaminiwa



WANAWAKE WATANU..———

73

kabisa, hata mbwa alithaminiwa zaidi kwa vile alilinda mlango.

Bi Gupta alihusika zaidi katika kwaya ya TANU na Umoja wa Vijana. Anakumbuka vizuri wakati walipotakiwa kuchagua serikali ya utatu, Tabora, ambapo Zuberi Mtemvu,

National Congress, walikuwa yake ya ushabiki wa wengi.

na chama

wanajaribu

cha kibaguzi cha African

kunyang'anya

TANU

nafasi

“Kazi yetu ilikuwa kuimba. Tuliposhinda uchaguzi, nikaingia idara ya usalama na Ulinzi. Ilikuwa kazi ngumu. Tulikuwa tunalinda nyumba moja huku Nyerere amelala nyumba nyingine. Wakoloni walipotuona tunalinda nyumba, wao walijua kwamba Nyerere yuko ndani. Tulikuwa tukijificha kwenye magunia, askari wa kikoloni wakipita wanafikiri ni magunia ya mkaa.... Bi Gupta alisaidia kujenga ofisi za TANU.

“Nilisaidia kujenga ofisi ya chama ya Mabogini, ilikuwa nyumba ya Abdi Nuru aliyoitoa kwa chama. Nyumba nyingine ilikuwe ya Bi ambacho kimoja alitoa chumba Muhogo, nilikarabati mwenyewe...nilitoa mali na rasilimali zangu kwa TANU...”

Kanasia Tade Mtenga Kati ya wanawake niliowahoji Moshi na ambao nilipata shida kupanga mkutano

nao,

alikuwa

Kanasia

Tade

Mtenga.

Alikuwa

mmoja

wanawake walioendelea kujihusisha na TANU, na inawezekana sababu hakupata muda wa mahojiano nami.

wa

ndiyo

Mwishowe tulipoonana naye, alikuwa akifanya kazi kama Katibu wa

CCM wa Moshi Vijijini. Ingawa alikwishawahi kuwa Mbunge katika miaka ya 1960, kulikuwa hakuna chochote katika mazingira yake kilichoonesha kwamba aliwahi kuwa mmoja wa lile kundi la wazalendo lililotawala Tanganyika baada ya uhuru. Katika sebule yake ndogo, kelele za magari yaliyopita mbele ya nyumba zilishindana na kelele za ng'ombe

74



WANAWAKE WATANU..

cha More, Mwika, mwaka 1934.

———

Baba yake, Jonathan Ngowo na mama

yake, Nathenjwa Ngowo, walikuwa wakulima. Akiwa mtoto, alimsaidia

mama yake kuchuma kahawa na kutafuta kuni.

Alianza shule ya msingi katika misheni ya Mwika na baadaye akaenda

Shule ya Wasichana

Machame,

na kumaliza

mwaka

1955. Alisomea

ualimu hapohapo Machame na kufundisha Shule ya Msingi ya Msaranga kwa kipindi kifupi. Mwaka 1956, aliolewa na Tade Mtenga na kuhamia Moshi mjini alikojifunza uhasibu, kutunza vitabu vya hesabu, Kiingereza na kupiga chapa. Baada ya kufaulu, alifanya kazi kama keshia katika hoteli ya KNCU.

“Wakati huo, 1958, nilijitolea kufanya kazi ya TANU ya kufundisha kisomo cha watu wazima. Nilikuwa nafundisha masomo ya kufuta ujinga na Kiingereza. Nilijiunga na TANU mwaka 1959.” Alisikia habari za TANU kwanza kwa kusoma katika gazeti akiwa shuleni mwaka 1955. "Mtu yeyote angefurahia uwezekano wa kuwa huru baada ya kuona tabia za wakoloni. Ndiyo sababu nilijitolea kufundisha ili tufute ujinga. Sasa baada ya uhuru tunaamua tunachotaka kufanya, tuna rasilimali zetu, tuna uwezo wa kuchagua viongozi wetu... Mwaka

1958, watu walikuwa wanajiunga na TANU kwa siri, hasa wale

walioajiriwa serikalini. Mwaka huohuo, Bi Mtenga alikuwa mjumbe wa Jeshi Maalumu la Polisi. Mwaka 1959, tarehe 20 Mei, Bi Mtenga alijiunga rasmi na TANU alipopata kadi yake ya kwanza ya uanachama. Tangu mwanzo, alihamasisha wanawake wajiunge. “..Tuliamini kwamba kwa jinsi katiba ya TANU ilivyoundwa,

——

WANAWAKEWATANU..———

75

wanawake walikuwa na sauti ya kuzungumzia suala lolote lililowahusu...Hata hivyo, wanawake walikuwa wengi, hata sasa wanawake ndio wengi katika nchi hii. Huwezi kudharau walio wengi... Wakati ule wanawake, hasa Waislam, walikuwa hawaendi kwenye mikutano ya hadhara. TANU ilipata shida kuwafanya waelewe, wajiamini...lakini Bibi Titi, aliyekuwa kiongozi wa Kitengo cha Wanawake na ambaye alisafiri sana na Nyerere na viongozi wazalendo wengine, alikuwa mahiri. Alifanya kazi kubwa sana wakati ule...hadi wanawake wakajiamini, wakasema, 'Aaah, kumbe inawezekana!' “Mwaka 17958, watu walikuwa wanajiunga na TANU kwa siri, hasa

wale walioajiriwa serikalini. Mwaka huohuo, Bi Mtenga alikuwa mjumbe wa Jeshi Maalumu la Polisi.

Bi Mtenga alipenda kusisitiza juu ya kazi yake baada ya uhuru katika UWT na; serikalini. Alikuwa mmoja wa wanawake wachache wa TANU ambao walivuka kipindi cha mpito, kutoka kabla ya uhuru na kuingia kipindi cha siasa baada ya uhuru. Aliweza kushika kazi ya ofisini hadi alipokufa kwa ajali mwaka 1990. Umri wake na kiwango cha elimu yake wakati wa uhuru vilimsaidia, kama ulivyomsaidia mtazamo kuwa mwangalifu katika maswali na masuala nyeti ya siasa.

wake wa

Natujwa Daniel Mashamba Natujwa Daniel Mshamba alikuwa mwanaharakati wa TANU, kuanzia miaka ya 1950. Natujwa aliendelea kuhusika na serikali na siasa hadi mwaka 1988 tulipoonana katika ofisi za CCM Kiboriloni. Alikuwa mwakilishi wa CCM wa Moshi Vijijini. Bi Mashamba alikuwa mwanamke pekee niliyemhoji ambaye alizungumzia kuhusika moja kwa moja na tukio la kihistoria dhidi ya ukoloni. Tukio hilo ni mgomo wa kodi za Mbiru uliotokea katikati ya mwaka 1940, katika Wilaya ya Same. Natujwa alizaliwa Januari 13, 1934. alikuwa mwalimu wa shule ya msingi

Baba yake, Yohana Mcharo, na mama yake, Nimwindie,

76

——

alikuwa

mkulima.

alifukuzwa

mkoani

sana mpaka mama

WANAWAKE WATANU..———

Alipokuwa

na

miaka

kumi

na

mitatu,

baba

kwa sababu ya ushiriki wake katika mgomo

yake

wa

na watoto walipoondoka kumfuata mumewe. Kila

walichokuwa nacho kiliuzwa, shamba, kahawa, kila kitu, na mama yake

akaapa hatarudi tena. Natujwa alisoma Shule ya Msingi Ilembula, na baadaye Kyimbila Shule ya Wasichana ya kulala. Baadaye alikwenda Shule mpya ya Wasichana ya Loleza. Baada ya kumaliza darasa la tisa, alikwenda Shule ya Wasichana ya Tabora, akamaliza darasa la kumi mwaka 1952. Alitaka kuwa daktari, lakini

hakukuwa na chuo cha uganga nchini kilichokubali kuchukua wanafunzi wanawake. Serikali ilishindwa kumsaidia. Aliambiwa kwamba kama anataka udaktari, basi baba yake amlipie, aende Mulago, Uganda. Baba yake hakuweza kumlipia, kwa hiyo Natujwa akajifunza kupiga chapa. Baba yake aliporuhusiwa kutoka kifungoni, familia ilirudi Upare.

“Tuliporudi tulipokelewa vizuri...tulipewa nyumba ya kuishi na jirani, tukapewa ardhi na watu wakatusaidia kulima... Walituachia

nyumba mpaka majirani.”

baba alipojenga nyingine kwa msaada

wa

Waliishi hivyo hadi TANU ilipoanzishwa.

“Walipomwuliza baba kama angeniruhusu nifanye kazi ya TANU, baba alifurahi. Nilikuwa bado mdogo, hivyo aliwaambia Bi Mashamba aliajiriwa kwanza katika Halmashauri ya Pare, Wilaya ya Same. Alipokuwa pale, aliombwa kuchapa kazi za TANU lakini baada ya muda akagundulika. Alionywa, lakini akaendelea kuchapa kazi hizo kwa siri.

“Nilitozwa faini ya shilingi 30 walioitoa kwenye mshahara wangu wa shilingi 75 kwa mwezi. Walinitoza faini mara mbili, kisha

——

WANAWAKE WATANU..——

77

walinitaka nijiuzulu, kwa hiyo nikaondoka. Wala hawakuniandikia barua ya kunifukuza kazi.

“Nilipokuwa na miaka ishirini na saba, niliolewa na Daniel Mashamba, tukaenda kuishi Kisiwani, ambako alikuwa ofisa wa mkoa wa biashara na viwanda. Mimi nilifanya kazi za TANU.

Niliipenda TANU kwa sababu kilikuwa chama kizuri na pia sikupenda jinsi baba yangu alivyofanyiwa vibaya na Waingereza na jinsi walivyodharau Waafrika. Juu ya hayo, sikutaka kutawaliwa na wageni tena. “Kwa vile TANU ilikwishaweka malengo yake ya baada ya uhuru, wanawake wangefaidi kwa kupata elimu, ili wafahamu haki zao. Matatizo ya wanawake yalikuwa tofauti na yale ya wanaume. Akina baba hawakutaka kusomesha watoto wao wa kike kwa sababu waliamini kwamba wasichana wasomi walikuwa hawatolewi mahari ya kutosha. Jambo lingine ni kwamba, mila za kikabila ziliwakaba

roho

wanawake,

nao

walikuwa

hawawezi

kusema kitu. Wanaume walifanya maamuzi yote na wanawake waliarifiwa tu.

“Matatizo haya yalizungumzwa katika chama cha TANU. Bibi Titi Mohamed aliwaelimisha wanawake kuhusu haki zao. Wanawake walichaguliwa katika nafasi za uongozi katika TANU, kwa hiyo wengi walijiunga, wakaongeza idadi ya wanachama hadi UNO ikakubali kutoa uhuru.

“Wakati wa kupigania uhuru, maisha yalikuwa magumu. Tulitumia muda wote katika shughuli za TANU. Ilibidi tutafute njia nyingine ya kujikimu- kulima maharage, au mahindi au vitunguu...” Kati ya Mashamba na Mtenga, hakuna aliyezungumzia ajenda ya kisiasa kwa wanawake wa miaka ya 1980. Wote walisifu juhudi za UWT za kusaidia wanawake. Walisifu serikali na CCM.

78

——--

WANAWAKEWATANU..

——

Lucy Lameck Lucy Selina Lameck Somi alizaliwa Kilimanjaro katikati ya miaka ya 1930. Baba yake alikuwa mkulima na wakati mwingine alifanya kazi ya usafirishaji. Mama yake, Petronilla Lameck Somi, alijihusisha sana na siasa, wakati Lucy na dada zake watatu walipokuwa wadogo. Lucy, kwa ujana wake na kiwango chake cha elimu, alikuwa wa wa TANU. wanaharakati wanawake mwa kipekee miongoni Alitambuliwa kitaifa kama sauti yenye shauku kubwa ya kupigania hali za maisha ya wanawake baada ya uhuru.. Lucy alisoma shule ya msingi kijijini kwake, Moshi Njoro. Alisoma shule ya kati huko Kilema na sekondari huko Tanga, ambako alisomea

vilevile miaka mitatu ya unesi na ukunga. Lucy alikiri kwamba alikuwa kati ya watu wenye bahati kwa wakati ule. Baada ya kumaliza masomo ya unesi, Lucy alichagua kurudi Moshi mwaka 1955, kuliko kwenda Huko Moshi alihudhuria masomo ya jioni ya kufanya kazi Tabora

kupiga chapa na hatimkato, akaanza kufanya kazi KNCU. “Nilijiunga na chama kama mwanachama wa kawaida, lakini nilikuwa nahudhuria mikutano na kuandikisha watu hadi mwaka 1957. Kila mara Nyerere alipokuja Moshi, alimtembelea mama yangu nyumbani, akanifahamu mimi na kutambua kazi niliyokuwa nikifanya. Tulikuwa tunakula pamoja kila jioni, kwa hiyo akawa rafiki wa familia. Nyerere alimfahamu mama yangu kwa vile mama alikuwa anajihusisha sana na siasa kwa miaka mingi. TANU ilipoanzishwa, sote tulifanya kazi ya kuandikisha wanachama. “Mama yangu alikuwa naakili... watu wengi wa serikali waliogopa kumkarimu Nyerere wakati huo... lakini mama yangu hakuwa na kitu cha kupoteza. Tulikuwa maskini, tusingeweza kuwa maskini zaidi ya hivyo tulivyokuwa. Hivyo Nyerere akakubaliwa kama mwanafamilia bila wasiwasi...Mama yangu hakujihusisha na siasa za Uchagani. Katika jamii, hutokea watu wenye akili wanaoweza kuona mbele...

WANAWAKE WA TANU

Lucy Lameck, 1960

YA WANAWAKE WATANU...——

——

80

“Nilichaguliwa kuwa TANU, mwaka

mjumbe wa kamati ya Wilaya ya Moshi ya

1956 hadi 1957, nilipoondoka kwenda chuo cha

Ruskin. Katika Chuo cha Ruskin, Orford, nilisoma diploma ya Utawala, Sayansi ya Jamii, Saikolojia na Uchumi. TANU na marafiki zake ndio walionifadhili... akina Joan Wicken, Billy Humes na John Hatch na wengine wachache. Kulikuwa na Watanzania wachache Osford...tulikuwa tunaonana London, katika nyumba

ya Afrika Mashariki. Mwalimu.

Akiwa

Lakini hasa aliyetuhamasisha

huko,

wanafunzi

kutoka

sehemu

alikuwa nyingine

Uingereza walikuwa wanakuja tunakaa naye, na kumsikiliza na kumwuliza maswali... “Mwaka

1960, nilikutana na kikundi cha Wamarekani waliotaka

kuwafadhili wanafunzi wa Tanzania kwa kozi fupi. Wakanifadhili nikaenda

Marekani,

Chuo

Kikuu

cha

Michigan.

Nilisoma

mahusiano ya kimataifa halafu nikatembelea majimbo machache nikizungumza juu ya nchi yetu na matamanio yetu ya kupata uhuru. Nilielezea katiba ya TANU ilivyo, kazi za TANU na kazi ilyokuwa inafanywa na chama... “Nilirudi nyumbani mwaka 1960, nikafanya kazi katika chama kwa miezi michache. Hali Ilikuwa ngumu wakati ule, tulikuwa hatuna fedha...kufikia mwisho wa mwaka, Rais aliniteua kwenda bungeni, alifanya hivyo kwa mujibu wa katiba.

“Ni vigumu kuelezea ni kwa nini nilijihusisha na TANU nikiwa mdogo hivyo. Nakumbuka vizuri kwamba sikupenda kabisa |

kufanya kazi chini ya mfumo wa ukoloni kwa sababu kulikuwa na ubaguzi wa wazi wa rangi. Kwa mfano, manesi wa Kiafrika walitendewa vitu tofauti na Wazungu. Chakula kilikuwa tofauti, nyumba, saa za kazi, saa za kula, mtazamo wao mzima kuhusu sisi ulikuwa tofauti... ni mkusanyiko wa vitu vingi. TANU ilipokuja, ilikuta watu waliokuwa tayari kukiunga mkono. Halafu, unafika mahali unajikuta kuwa ni wa daraja la chini katika nchi



WANAWAKE WATANU..———

81

yako...Kulikuwa na shule za Kizungu kwa watoto wachache wa Kizungu, shule za Wahindi kwa Wahindi walioshika uchumi wa nchi, halafu tulikuwa na shule masikini, zilizokwisha, hizo zilikuwa

za Waafrika...” Lucy Selina Lameck hakuwa

Kitengo cha Wanawake.

mwanaharakati

Alikuwa

wa kawaida aliyeongoza

na elimu ya juu kuliko wanawake

wengi wa wakati wake na hakuwa Mwislamu. Vitu vyote hivi vilisukuma na kuwezesha maisha yake ya siasa hadi miaka ya 1980. Alifariki Machi 21, 1992.

Hitimisho Kama kikundi, wanaharakati wa Moshi walikuwa vijana kidogo zaidi ya

wenzao wa Dar es Salaam, pia walikuwa na elimu zaidi. Huko Dar es Salaam, wanawake wasiokuwa na elimu ndio waliojihusisha zaidi na harakati

za siasa, hasa

wale

ambao

hawakuolewa.

Kwa

wanawake

waliokulia nje ya Kilimanjaro, elimu na ajira za baba zao ziliathiri vizuri fursa zao za elimu. Wanaharakati sita wa Moshi walikuwa na ajira katika

sekta rasmi, na uzoefu wao wa ubaguzi wa rangi na jinsia katika sehemu za kazi uliwawezesha kuelewa ukoloni. Kulikuwa na ndoa chache zaidi zilizovunjika

miongoni

mwa

wanaharakati

watoto wengi zaidi. Pia, walitoka

wa

Moshi. Walikuwa

katika dini mbalimbali

na

- Waislamu,

Wakatoliki na Walutheri. Viwango

vikubwa

vya elimu

vilimaanisha

kwamba

wanaharakati

wanawake wa Moshi waliweza kuvuka kipindi cha mpito kutoka kabla ya uhuru kufikia kufanya shughuli za uhamasishaji za TANU, kikiwa chama

tawala. Waliweza pia kuingia UWT, chama kilichozaliwa kutoka Kitengo cha Wanawake.

Aua

AA

82

——-

WANAWAKE WATANU...



SURA YA NANE Wanaharakati

kutoka Mwanza

ya Mwanzoni mwa miaka ya 1950, watawala wa kikoloni waliona Wilaya no uhusia Moshi kuwa imeendelea na ni rahisi kuitawala, bila ya kujali ya wa mashaka uliotokana na siasa za kikabila kati yao. Tofauti na hali uwa Moshi, watawala hao walishangazwa na shughuli za kisiasa zilizok cha kiasi , Mwanza zikiendelea huko Jimbo la Ziwa, ikiwepo mji wa Kama ilivyokuwa kulazimika kupiga marufuku matawi ya TANU.

za Kilimanjaro ambako shughuli za kizalendo ziliweza kupindua siasa kikabila, ni vikundi vya ngoma na vya kazi ndivyo vilivyowaleta pamoja watu na tawala za kichifu zilizotenganishwa na ukoloni. Jambo lingine lilikuwa ni Waafrika wachuuzi waliozungumza

Hao Kiswahili ambao walifika Usukumani na kuweka vituo vyao huko. walikuwa wanaume wa mjini. Walizungumza Kiswahili, walistaarabika kiasi ya kutokana na kusafiri, kufanya biashara na walikuwa na elimu a Kuran. Pamoja na wengine waliosoma misheni, kwa pamoja waliund kundi la wenyeji wasomi, wa tabaka la kati, ambalo ni muhimu

sana

katika nyakati za mwanzo za ujenzi wa vyama vya kizalendo.

Wanawake Wanaharakati wa TANU wa Mwanza

kwa Niliwahoji wanawake wanaharakati wa TANU wa Mwanza siasa za madhumuni ya kupanua uelewa wangu kuhusu wanawake na na anisha kizalendo Tanganyika. Hata hivyo, sikupata watu wa kunikut mahojiano wanawake, na muda wangu ulikuwa mdogo. Matokeo yake anywa niliyofanya hayakuwa na kina yakilinganishwa na yale yaliyof sehemu zingine.



WANAWAKE WATANU..

———

83

Mambo kadhaa muhimu yalijitokeza. Kwanza, tofauti na wanawake wa Moshi au Dar es Salaam, wanaharakati wa Mwanza walikuwa wanachama wa tawi la TAA lililokuwa na nguvu mwanzoni mwa miaka ya 1950. Pili, ingawa walimuunga mkono Nyerere kwa dhati, wanaharakati hawa walikuwa tayari wanasiasa kabla ya ujio wa Nyerere huko. TANU ilikuwa imepigwa marufuku jimboni humo, hivyo uzoefu wao uliwaongoza kujipanga kwa siri. Tatu, wanaharakati hawa waliendelea kujihusisha na vikundi vya ngoma ambavyo vilikuwa muhimu mno kwa kuimarisha TANU katika miaka ya 1950. Hivyo, waliweza kunipatia mifano ya nyimbo ambazo sikuzipata sehemu zingine.

Agnes Sahani Agnes Sahani anatambulika kuwa mwanaharakati mashuhuri. Hata hivyo, alisita kuongea kuhusu shughuli zake za kisiasa na kuzizungumzia kijuujuu. Agnes Geikwa Sahani alizaliwa mwaka 1918, katika Wilaya ya Kwimba, Jimbo la Mwanza. Alikuwa mtoto pekee wa Sahani Ugolo Chenya, mkulima, aliyekuwa askari katika vita ya mwaka 1914. Mama yake, Kagura Kwiede, alikuwa mkulima.

Agnes alisoma shule ya misheni ya Kijima kwa miaka minne hivi. Alipofikisha umri wa miaka ishirini aliolewa na ofisa wa mifugo, Jeromini Basunji. Walipata mtoto mmoja ambaye alifariki. Hakuishi na mume wake kwa muda mrefu, na baadaye aliondoka kwenda Mwanza. Alifanya kazi katika hospitali ya Mwanza kama mlezi wa watoto kwa miaka tisa. Alilazimishwa kuacha kazi kwa sababu ya kushiriki katika siasa.

"Siku moja nilikwenda mkutanoni, nikachelewa kazini....Mkuu wangu wa kazi akaniambia, 'Kama unapenda chama, unaweza kuacha kazi

ukafuata chama.' Kila mara alikuwa akiniuliza kama napenda chama au kazi...' Mwishowe niliamua kuondoka...Walikataa kunilipa wakisema kwamba niliamua mwenyewe kuacha kazi...”

WA

AAA

84



Ka

au

WANAWAKE WATANU..———

Agnes Sahani alikuwa katika kamati ya ushauri ya TAA na baadaye akawa mwanaharakati hodari wa TANU. “Sikuwa mgeni katika siasa. Niliona ni vema kushiriki katika siasa za nchi yangu, kuungana na wananchi wenzangu kuleta uhuru na kujenga nchi.”

Nilipomwuliza kuwa alitegemea wanawake kujiunga na TANU, Agnes alisema:

wangefaidika

vipi kwa

“Sisi ni wanawake lazima tuwe tayari kuungana na viongozi wetu, wanawake na wanaume wa Tanganyika...Matatizo ya wanawake na ya wanaume hayakutofautiana kwa sababu wote ni wananchi...” Nilipomwuliza akiwa TANU alifanya kazi gani, aliniambia,

“Nilifuata mambo ya siasa yetu yalivyokuwa, sina cha kusema kwamba kilikuwa changu...”

Nilipomwambia kwamba alikwenda kumwona Nyerere Butiama alisema: “Ilikuwa kuhusu kulima, kuhusu vyama vya ushirika. Wahindi walikuwa wakinunua pamba yetu, sisi tulitaka kuilima, kuivuna na

kuiuza sisi wenyewe, siyo kwa kupitia mtu wa kati. Mimi nilikuwa mshiriki

katika

Chama

cha

Wakulima

cha Jimbo

la Ziwa,

kilichoongozwa na Bomani. Agnes Sahani alisema kwamba maisha yake baada ya uhuru yalikuwa mazuri:

"Sina shida. Nashirikiana vizuri na viongozi wote Tanzania...Katika bodi ya TANU, tulishirikiana na kufanya kazi pamoja...hadi leo, sijaacha....Siwezi kusema kuwa wanawake wasomi hawapendi mambo ya chama au wasio wasomi wanapenda...kila mmoja ana

WANAWAKE WA TANU

Agnes Sahani ji, 1988

85

86

——

WANAWAKEWATANU..

———

uhuru wa mawazo yake. Wapo wanawake wasomi katika uongozi ambao wanatufundisha kuhusu mambo ya chama...siwezi kusema kwamba wanawake wasomi hawapendi chama kwa sababu chama ndicho. mtetezi wao. Wataachaje kukipenda? Chama ni mtetezi wa wanawake wote.”

Aziza Lucas Aziza Lucas alizaliwa Ilemera, Wilaya ya Mwanza,

mwaka

1928. Baba

yake, Lucas Maneno, alitoka Ukerewe. Mama yake alikuwa Msukuma. Wote walikuwa wakulima. Aziza alikuwa mmoja wa watoto kumi na mmoja. Bi Aziza hakwenda shule. Alipokuwa na umri wa miaka ishirini aliolewa na Shabani Magi, wakahamia Kirumba, Mwanza, ambako alishindwa kulima kwa sababu hawakuwa na ardhi. Mume wake aliuza mbao.

Aziza alijiunga na TANU pamoja na mumewe mwaka 1954 na walikuwa na hamasa kubwa. “Kusikia tu kwamba tunaweza kujitawala. Unajua, ukiwa mtu huru, unafanya kazi yako kwa moyo mmoja, bila matatizo. Tumaini letu lilikuwa kwamba watu wa Tanganyika wangekuwa wamoja, wabaki na umoja bila ubaguzi. Kwa wanawake, tulitumaini kwamba tukipata uhuru hatutagandamizwa tena na wanaume kama ilivyokuwa zamani. Tutakuwa huru kwenda popote..”

Alipoulizwa kuhusu

wanaharakati wa TANU

waliopo Mwanza, Bi Aziza

aliwataja Binti Mwajuma Msafiri, Tatu Mohamed, Pili Juma, Mwantumu

Mto na Mama Nyembo. Aliendelea kuisifu TANU kwa kuwaelimisha wanawake na kuwapa nafasi za uongozi. Mchango wa wanawake katika TANU ulikuwa kuhudhuria mikutano, kupika chakula na kuwakaribisha viongozi.

——

WANAWAKE WATANU..———

87

Bi Aziza, alieleza kwamba dini na harakati za kupigania uhuru vilikuwa vitu viwili tofauti.

"Dini inapigania roho ili uende mbinguni, kwa Mungu; siasa ni harakati za hapahapa duniani.” Tunu Nyembo “Ninaitwa Tunu, Bi Tunu Nyembo. Mimi ni Mzaramo kutoka Dar es Salaam, lakini nilizaliwa hapa Mwanza, Mtaa wa Rufiji, mwaka

1928. Baba yangu, Selemani, alikuwa fundi mwashi na mama yangu Fatuma alikuwa mkulima. “Maisha yangu hayakuwa mabaya nilipokuwa mdogo kwa sababu baba yangu alikuwa mwashi. Nilikwenda shule ya kidini hadi nilipovunja ungo. Nilipofika umri wa miaka ishirini na mmoja, Nyembo alinioa tukahamia Dar es Salaam kwa muda, lakini baadaye tulirudi hapa.

“Nilisikia habari za TANU kwa mara ya kwanza mwaka 1954 hapa Mwanza...Kuna mtu alikuwa akiuza kadi kwa siri, na hizo kadi ziliuzwa kutoka nyumbani kwangu, kwa sababu alikuwa akipanga hapo. Kadi ziliuzwa kwa shillingi mbili kila moja. Walikamatwa, wakiziuza, mume wangu, Munanka na Agostini. Mume wangu alitozwa faini na wao wakafungwa. “Pamoja na yote haya, niliendelea...mpaka Mwalimu UNO... mwishowe bendera ilipanda mwaka 1961.

akaenda

“Wanawake walikuwa na nguvu wakati ule...wengi wamefariki sasa. Walio bado hai ni Mama Ntungi, Zuhura Musa, Agnes Sahani, Aziza Lucas, Pili Juma,

Chiku Mzee, Shera

Waraga,

Mwamvua Kibonge na Mwajuma Msafiri. Wakati ule, pamoja na kushughulika na TANU, nilikuwa na kikundi

changu cha ngoma na mpaka sasa mimi ni mwenyekiti wa Rumba City... Tangu uhuru nimekuwa nafanya biashara..."

KA

88



WANAWAKEWATANU..

———

Halima Ntungi "Jina langu ni Halima Ntungi. Nilizaliwa hapa Mwanza, sijui mwaka, wakati huo wazazi walikuwa hawapeleki watoto shule...Baba yangu, Ntungi, alikuwa mtemi, na mama yangu Nzilani, alikuwa mkulima.

“Nikiwa bado mdogo sana, mama yangu aliondoka na kuolewa na mtu mwingine, nikalelewa na bibi. Baada ya vita, alirudi kunichukua nikaishi naye, mpaka nilipoolewa na Hasan nikiwa na miaka kumi na nane. Nilizaa naye watoto wawili, kisha tukaenda Dar es Salaam,

halafu Tanga na mwishowe tukarudi hapa....Nimejenga nyumba hii kwa mikono yangu.

“Nilijiunga na TANU wakati bado inaitwa TAA na mpaka sasa nipo CCM. Nyerere alipokuja hapa Mwanza mwaka 1958, nilipokea kadi yangu ya TANU kutoka mkononi mwake, nilifurahi sana....Nilikuwa nimeona mateso yaliyotutokea wakati wa ukoloni...nikaona ni bora kuwa na uhuru... Ukoloni ulikuwa

mbaya,

hakukuwa

na amani.

Ulikuwa huwezi

kumiliki chochote bila kuulizwa umekipata wapi, na mimi ni binadamu ninayefanya kazi!..Kulikuwa na matatizo mengi...Uhuru ulileta vitu tulivyo navyo sasa...kila mtu ana nafasi yake... “Wanawake walifanya kazi muhimu kadi nyingi kuliko wanaume, tulipiga Kitengo cha Wanawake. Niliteuliwa mkoa na katika wilaya. Kwa miaka Tawi la TANU, nilikuwa pia diwani mwakilishi wa CCM mkoani...”

sana kwa chama. Tulinunua kura. Nilikuwa kiongozi katika katika kamati ya ushauri ya sita nilikuwa mwenyekiti wa kwa miaka minne. Sasa ni

Mwajuma Msafiri Mwajuma Msafiri alizaliwa Dar es Salaam mwaka 1933, akiwa wa kabila la Bwadi

kutoka

Kigoma.

Baba

yake,

Msafiri,

alikuwa

mlinzi

wa

——

WANAWAKE WATANU..——

89

Wajerumani na mama yake, Tausi, alikuwa mkulima. Mwajuma alisoma shule ya Kuran kwa miaka miwili hivi, akaona kwamba ameshasoma vya kutosha

kuhusu

kuswali. Akiwa

na umri wa

miaka

kumi

aliolewa na Mohamed Said aliyekuwa mfanyabiashara. Bukoba, Dar es Salaam na mwishowe wakaja Mwanza.

na mitatu,

Walikwenda

“Nilisikia kuhusu TANU mwaka 1954. Mtu aliyeitwa Debe Moja, mwuza maji, aliniita akaniambia kwamba kuna mtu anagawa kadiza TANU. Aliniambia kwamba rais atafika Jumapili kuhutubia watu....alikuwa akifanya mikutano na tulikuwa tunakwenda kila mara mpaka kulipoundwa chama cha wanawake na cha wazazi.... “Wanawake walijitolea sana kupigana dhidi ya ukoloni. Tulijifunga kanga kiunoni mpaka uhuru ukaja. Tulipiga vifijo na vigelegele mpaka tukapata uhuru. Tulibeba kadi za TANU, tukabeba kadi za

UWT, tukabeba kadi za chama cha wazazi. Wanawake walijiunga na Umoja wa Vijana....walikuwa kama polisi wa siku hizi. “Ukoloni haukuwa mzuri, maisha hayakuwa mazuri, watu hawakuwa na uhuru na hatukuweza kupata elimu. Mkoloni hakujali elimu ya watoto wa Kiafrika au maendeleo yake... Wakati huo hakuna hata mwanamke mmoja aliyefanya kazi Ofisini, ni wanaume tu, tena waliomaliza darasa la nne au la nane... Walikuwa wakivaa kaptula, siyo suruali kama mabwana. Lakini sasa wanawake ni mawaziri, tuko hospitali, tunakwenda Ulaya, kila mahali, tunajisikia tu Watanzania waliokamilika. Kabla ya uhuru, wanawake walikaa ndani, akipata mtoto tu, amekwishazeeka, akiolewa amezeeka, hana ufahamu wowote wa dunia...

“Nilifanya kazi katika chama na baadaye UWT. Nilikuwa katika Idara ya Wazazi na mpaka sasa nafanya kazi. Nilichaguliwa katika Tawi.laTANU, halafu nikaingia katika Kamati ya Ushauri ya Tarafa,

|

90

——

WANAWAKE WATANU...

——

halafu ya wilaya. Nikawa Makamu Mwenyekiti wa UWT Wilaya, na sasa ni mwenyekiti wake.... Pili Juma

Pili Juma alijitambulisha kuwa ni Mmanyema

na alizaliwa Mwanza mjini.

Tulipokutana, mwaka 1988, alikuwa na miaka hamsini na sita. Baba yake, Juma Mirambo, alikuwa mwashi. Alifariki wakati Pili ana umri wa miaka saba.

Pili alisoma shule ya Mwanza Mjini, kisha akaenda Shule Wasichana Tabora alipohitimu darasa la nane mwaka 1948. Aliolewa Ali Mohamed akiwa na miaka ishirini na mmoja.

ya na

Pili alisikia habari za TANU huku na kule.

“Nilisikia habari zake kutoka kwa waume wa rafiki zangu walipokuwa wakipita njiani karibu na sisi tulipoketi...Nilifurahia hizo habari, moyo wangu ukajaa hamu. Kwa nini nisizijue hizi habari vizuri?...Moyo ulitamani kufahamu madhumuni ya TANU. “Ukoloni ulituonea kupita kiasi. Wazee walikuwa wakichapwa na kufungwa na kamba... lakini TANU ikaamua kwamba binadamu wote ni sawa. “Wanawake walikuwa mstari wa mbele wakipigana...nilikuwa Umoja wa Vijana, na pia nilikuwa katibu wa chama kwa miaka kumi na mitano. Agnes Sahani alikuwa mwanamke hodari, halafu Makongoro binti Selemani...-hawa walikuwa katika kitabu cha uhuru...walifanya kazi kuunganisha wanawake...hii ndiyo ilikuwa kazi muhimu... Mwamvua Kibonge Bukumbi. Mama yake, Zena, alitengeneza na kuuza vitumbua; na baba

r

AA AaAaAAaAaAaAaAaAeAeAeEAEAEAEeAeEAEAEBEuwA—E—A AAA

——

WANAWAKE WATANU..———

91

yake, Kibonge, alikuwa askari. Mwamvua anakumbuka kuwa utoto wake

ulikuwa mzuri. Chakula kilikuwa kingi. Aliolewa akiwa na umri wa miaka kumi na mitatu kwa mumewe wa kwanza aliyeishi naye kwa miaka mitatu. 'Bahati mbaya sikuweza kumvumilia, nilikuwa mdogo sana,” alisema.

Mwamvua alijiunga na TAA mwaka 1952 au 1953. “Tulitembea nyumba kwa nyumba, hodi karibu, tunataka kuwa

huru. TANU yaja...chukua kadi, ni shilingi mbili....Wakati wa ukoloni, ulikuwa ukiingia ofisini unajikuta unatetemeka kwa sababu ungeulizwa unataka nini hapa... unatoa jasho...”

Bi Mwamvua anakumbuka wakati Nyerere alipopita Mwanza akienda Butiama, alisema kwamba tukipata uhuru, wanawake watakuwa watu,

watapata heshima wanayostahili. Mchango wa Mwamvua kwa harakati na kwa TANU ulikuwa kutunga ngoma zilizochezwa katika ukumbi wa maonesho.

“Watu waliokuja kuona ngoma walitoa senti kumi, na tulipata fedha nyingi wakati huo...tukampa Mwalimu....Juhudi zetu zilikuwa nyingi. Nilifanya kazi TANU hadi nyumba ya marehemu mama yangu ikaanguka, paa liling'olewa na mvua nyingi. Nikaenda Sengerema, ambako wazee waliahidi kunisaidia” Zuhura Mussa

Kwimba. Baba yake, Mussa, alikuwa mwashi na mama yake, Mwibombi

Kahalaga, alikuwa mkulima. Zuhura shule. Alipokua, aliolewa na mtemi, Maswa katika Jimbo la Shinyanga. alimwacha mumewe, akaja Mwanza

alizaliwa peke yake na hakwenda akahamia Ruguru Ntilima, kupita Mwishoni mwa miaka ya 1940, alikojiunga na TAA.

KA

92

——

WANAWAKE WATANU..

———

“Nilikuwa mwanachama wa TAA, halafu ikapigwa marufuku. Muda ukapita hadi ilipoanzishwa TANU nikawa mmoja wa wanachama waanzilishi....Nilikuwa mwenyekiti wa TANU wa jimbo zima pamoja na Shinyanga na Mwanza. Nilikuwa nakwenda Dar es Salaam kuwakilisha jimbo.” Zuhura Mussa, pamoja na wanaharakati wengine, alikiri kwamba viongozi wenyeji wa TAA Mwanza, katika miaka ya 1950, walijulikana zaidi kama wazalendo kuliko Nyerere. TANU ilipopigwa marufuku, ilifanya Nyerere ashindwe kujitambulisha waziwazi mpaka yalipotokea maasi ya Geita ya mwaka 1958. Maasi haya yalikuwa pigo kubwa kwa utawala

wa

kikoloni

na TANU

ikajipatia

ushindi,

na

Nyerere

akawa

kiongozi wake bila kupingwa.

Chausiku Mzee Chausiku Mzee alizaliwa Magu. Baba yake, Mtemi Mgerema, alifariki wakati Chausiku bado mdogo sana. Mama yake alikuwa mtoto wa Mtemi Mnyamongolo. Chausiku alisoma kwa miaka minne, lakini akaacha shule akiwa bado

mdogo ili akaolewe. Aliolewa na Mwarabu, Mohamed bin Nassoro. Aliachana na mume huyu, akaolewa na Alfari Hassani; akahamia naye Mwanza, akajenga nyumba na kuingia katika siasa. Bi Chausiku aliingia katika siasa muda mrefu kabla ya kusikia habari za Nyerere. Walikuwa wakifanya mikutano yao kwa siri, nje ya mji wa Mwanza, wakisaidiwa usafiri na Mhindi mmiliki wa vinu vya kuchambulia pamba. Aliendelea kuwapa usafiri muda wote kabla ya TANU kupata gari. Mhindi mmiliki wa Tanganyika Bus vilevile aliwapa gari la kufanyia shughuli za siasa. Bi Chausiku anakumbuka maandamano ya Geita na Mwanza;

“..Tulipigwa mabomu ya machozi na wote tulifungwa. Baada ya ' hapo, tuliweza kufungua tawi la TANU Geita, halafu tukaenda

———

WANAWAKEWATANU..———

93

Maswa, Ngudu, Shinyanga, Tabora mpaka Bukoba. DC alikuwa

akituvuruga, mwishowe tukafanyia mikutano mbugani, akapeleka polisi kutufuata... “Tulifikia makubaliano na Mwingereza, akatupa uhuru, wakatuaga kwa amani bila kumwaga damu. Gavana alipoondoka, tulimsindikiza... tukarudi na rais wetu, tukafagia Ikulu, tukamsimika Rais halafu tukaanzisha UWT.

Nilikuwa mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake mkoa huu. Mume wangu akawa ananibughudhi, mwishowe nikarudi Geita. Alikuwa akinikatalia kuongoza msafara...Alikuwa akinitoa ndani ya ndege au treni kwa nguvu, mbele ya viongozi wenzangu. Nikaona, ya nini? Nikajiuzulu. Nilikuwa nikipigwa kila nikirudi nyumbani....

Hadi sasa mimi ni mwanasiasa, sijaachwa nyuma na sijajiunga na chama kingine...”

94



WANAWAKEWATANU..

———

3 SEHEMU YA TATU Uzalendo na Harakati za Wanawake Baada ya Uhuru e.

.

Kwa nini Bibi Titi alisukumwa nje ya nuru ya harakati za kisiasa baada ya uhuru? Ukimya uliofuatia unatoa changamoto gani kwa wanaharakati? Ajenda ya wanawake wa TANU ya kuendeleza harakati za kisiasa baada ya uhuru ilibadilishwa na kufanywa ya ustawi wajamii. Ni kwa nini? Wanaharakati wa jinsia katika Tanzania ya leo wanajifunza nini kutokana na harakati za kisiasa za wanawake wa TANU?

———

WANAWAKEWATANU..——

95

SURA YA TISA Bibi Titi Mohamed: Uhuru na Baada ya Uhuru Katika maadhimisho ya uhuru wa Tanganyika kutoka kwa Waingereza, usiku wa Desemba 9, 1961, Bibi Titi Mohamed na Julius Nyerere walikaa kwenye jukwaa moja, wakiwa pamoja na waheshimiwa wengine. Ilikuwa muda mfupi tu, kabla ya Nyerere kuwa Waziri Mkuu. Wakati huo, Nyerere alikuwa ndiye mwanasiasa pekee aliyebaki kwenye Kamati Kuu ya TANU ya kwanza ya mwaka 1954. Kwa mujibu wa Iliffe, yawezekana kuwa Nyerere na Bibi Titi walikuwa ndio viongozi pekee waliojulikana nchi nzima wakati Tanganyika inapata uhuru. Bibi Titi mwenyewe hakuizungumzia siku hii ya kupata uhuru, ambayo ilikuwa na maana ya kipekee na iliyosherehekewa nchi nzima. Lakini Lucy Lameck, aliyeshiriki tukio hili, alikumbuka:

“(Maadhimisho) yalikuwa kitu tofauti kabisa. Sikuweza kulala, tulicheza siku nzima,

tulicheza dansi kila mahali barabarani.

Kuona bendera yao inashuka na yetu inapanda, ilikuwa ajabu kabisa. Hupati hisia za namna hii tena. Huo ulikuwa muda katika historia ambao hautokei mara mbili...ungekuwepo usikie nderemo, wanawake wakipiga kelele, machozi yakiwatoka... maajabu!" Uhuru wa kisiasa ndio ulikuwa lengo kuu kwa Bibi Titi. na wanawake wanaharakati wa miaka ya 1950. Hata hivyo, uzalendo na nguvu waliyowekeza katika TANU haikuishia katika kuwapa nguvu ya dola. Hivyo, kitabu hiki hakihusu harakati za kupata uhuru pekee, bali kinahusu pia wanawake wanaharakati na mwendelezo wa utamaduni wao wa siasa za kizalendo baada ya ukoloni.

96

—-

WANAWAKE WATANU...——

Mwanzoni mwa miaka ya 1960, Bibi Titi aliweza kuendeleza uono wake wa kizalendo akiwa kiongozi wa Chama cha Wanawake cha Afrika.

Lakini, katika miaka iliyofuatia, alipata shida kuongoza

chama

cha

wanawake ambacho hakikuwa cha kisiasa. Hivyo, alikosana na TANU ambayodlikuwa inazidi kuwa na mamlaka makubwa yaliyojikita makao makuu, katika serikali ya chama kimoja.

Katika sehemu: hii ya mwisho ya historia ya maisha yake, Bibi Titi anaelezea kazi yake ya siasa, mahangaiko na matatizo yaliyomkumba baada ya uhuru. Anaeleza:

“Sisi wanawake tulihamasisha watu mpaka tukapata uhuru. Safari yangu ya kwanza nje ya nchi nilikwenda India, mwaka 1958. “Ni mimi niliyewashawishi

wanawake

wa Afrika kuanzisha

Mkutano wa Wanawake wa Afrika, mwaka 1962. Ni mimi niliyepanga mkutano huo, niliyewashawishi wanawake wa Guinea kushiriki... Diallo, Katibu Mkuu wa AAPC, alikuja hapa

71960. PAFMECA walikuwepo vilevile. OAU ilikuwa bado haijaanzishwa. Diallo aliona jinsi nilivyokuwa nimepanga mambo ya chama na jinsi nilivyowatayarisha wanachama, walivyokuwa wamefurahi. Akapendezewa. Walipoondoka wakanikaribisha katika Mkutano wa Wanawake wa Afrika ya Kaskazini na Magharibi...

“Katika mkutano huo tulizungumzia matatizo ya wanawake ya elimu, maendeleo, malezi ya watoto, na jinsi ya kushiriki katika siasa. Tulijiuliza: hata tukishiriki, tutafanya nini hasa? Tutafaidi nini? Tutapata mamlaka gani baada ya uhuru? Wanawake walijadili masuala haya, na nikawaambia kwamba masuala haya yako kila mahali...Niliwaambia kwamba inabidi tupange Mkutano wa Wanawake wa Afrika nzima. Nchi nyingine zilikuwa walikuwa bado bado hazijapata uhuru na wanawake

——

wanakandamizwa.

WANAWAKE WATANU..————

97

Ingawa sisi tunaotoka Tanganyika tuna sauti,

hatujui itaishia wapi, ni lini mwanamume atachukua hatamu. Ni lazima tuwe na umoja wa Afrika ili tupiganie elimu na malezi ya watoto. Lazima tuwe pamoja katika Afrika moja ili tusikike kila mahali. “Mwezi Juni, mwaka

1962, Mkutano

wa Wanawake

wa Afrika

ulifanyika hapa nchini. Chama cha Wanawake Waafrika kiliundwa hapa Tanganyika. Mkutano kama huu ulikuwa haujawahi kuwepo, hivyo huu ukawa mkutano mkuu wa mwaka. Kiongozi wa mkutano alikuwa Hawa Keita kutoka Mali. Nilikuwa mjumbe wa kamati... Wakati huo, Bwana Mkubwa alikuwa amejiuzulu Uwaziri Mkuu ili akajenge TANU na kumwachia Rashidi Kawawa Uwaziri Mkuu.” Nilimwomba Bibi Titi atueleze kuhusu kupoteza kiti chake cha ubunge mwaka 1965, wakati wa Uchaguzi Mkuu wa kwanza tangu uhuru na wa kwanza kufanyika chini ya katiba mpya iliyoifanya Tanzania kuwa nchi ya chama kimoja. Mwanzoni, wanawake kumi na sita walipendekezwa, wanane wakiwa wamechaguliwa na chama. Bibi Titi alipoteza jimbo lake la Rufiji-Utete. Alipata kura 7,343 dhidi ya mpinzani wake M. Mtauka, aliyekuwa katibu wa TANU huko, aliyepata kura 18,145. Uchunguzi uliofanywa kuhusu uchaguzi huu umetoa sababu kadhaa zilizomfanya Bibi Titi ashindwe. Kwanza, alizaliwa na kuishi Dar es Salaam, kwa hiyo, alikuwa halifahamu jimbo lake vizuri. Pili, walisema

kuwa hakutumia busara kama alivyotarajiwa, kwani alielekeza kampeni zake kwa kiasi kikubwa kwa wanawake. Tatu, alijihusisha kwa kina na shughuli za UWT, TANU na Serikali na kutoa nafasi ndogo mno katika kuridhisha jimbo lake.

"Sijui ni kwa nini nilishindwa katika uchaguzi wa 1965. Sijui kama kulikuwa na sababu maalumu. Yawezekana sababu ilitokana na moja ya matendo yangu. Nilikuwa Waziri Mdogo wa Ustawi wa

98



WANAWAKE WATANU..——

Jamii wakati huo, na nilipewa mwanamke mmoja kutoka Ustawi wa Jamii ili nifuatane naye. Nilidhani kwamba anafuatilia maendeleo ya kazi tu, sikuwaza kabisa kwamba alikuwa na madhumuni mengine. Kila tulipokwenda, alikuwa kama mpelelezi... "Kulikuwa na tatizo la muda mrefu huko Rufiji. Kulikuwa hakujawahi kuwa na kanisa katika sehemu hii iliyojaa Waislamu tangu wakati wa Wajerumani na Waingereza. Baada ya uhuru, mapadre kutoka misheni ya Kipatini huko Kilwa wakaomba sehemu ya kujenga kanisa. Watu wa Rufiji wakapeleka ujumbe wa watu Dar es Salaam kuja kuniona na kuniomba niwafanyie mpango waonane na Rais. Watu walisema kwamba haya mambo ya kujenga kanisa yanakuja haraka sana, yanaweza kuleta madhara. Walisema kwamba kama Wajerumani walitawala kwa miaka thelathini na Waingereza kwa miaka arobaini na hawakufanya hivyo, itakuwaje serikali iruhusu kanisa lijengwe miaka minne tu baada ya uhuru? Walipokwenda kwa Rais, yeye akawaambia hana la kufanya, hawezi kuingilia mambo ya dini. Nyerere aliwajibu hivyo. Mapadre wa Kipatini wakala njama na maadui wangu. Wakadai kuwa haijulikani Titi yuko upande gani.

“Walisema kuwa ni mimi ndiye niliyechochea watu kupinga ujenzi wa kanisa katika wilaya. Sikufanya kitu kama hicho... Kuzuia watu wasifuate imani yao siyo jambo la kuvumilia katika wilaya yetu. Dini yetu haisemi hivyo. Mtu akiomba kujenga kanisa katika sehemu yenye Waisilamu, na akasema kwamba Wakristo wanataka kujenga kanisa katika sehemu hiyo, huna haki ya kumkatalia. Lakini watu walichanganya vitu, walichanganya dini na ujinga. Waliponiomba nichukue ombi lao, nilifanya hivyo, nikaonekana kuwa ni mtu mbaya. 'Kwa nini Titi anakubaliana nao? Kwa nini alikataa kanisa lijengwe? Lazima ni yeye aliyechochea wazo hilo.



WANAWAKE WATANU..——

Bibi Titi akipinga matokeo ya uchaguzi wa Ubunge, 1965

99

——

100

WANAWAKE WATANU..

——

"Inawezekana pia kushindwa kwangu kukatokana na ndugu yake Kaswende. Sina hakika. Lakini ndivyo ilivyokuwa. Nilifahamu kwamba huyu mtu alitumwa kuleta migongano katika kampeni

yangu... “Baada ya mwaka 1965, migogoro ilianza kujitokeza kati ya wakuu wa mikoa na makatibu wa TANU nchi nzima. Kulikuwa na utata, ni nani aliyewajibika kwa kitu gani, na wakati mwingi kulitokea mikwaruzano. Wakati huo, Kambona alikuwa Waziri wa

Maendeleo ya Jamii. Alisema kuwa amewaambia wajumbe wa Baraza la Mawaziri na Kamati Kuu kuwa kulikuwa na migogoro kati ya wakuu wa mikoa na makatibu wa TANU, na kwamba ni muhimu kufanya mkutano ili kila mmoja ajue wajibu wake. Mkutano ungefanyika Tabora, na kutoka huko watu wangekwenda Arusha kwa mkutano wa Kamati ya Utendaji ya Taifa, lakini kabla hatujafika Arusha, tukasoma katika magazeti kuhusu Azimio la Arusha. “Nilisafiri kwenye ndege moja na Kilian Kapinga wa COSATA, naye aliniuliza, 'Umesoma magazeti?' “Nikamjibu, 'Nimesikia na nimeona. Azimio la Arusha limefika lini?

Mtu yeyote aliye kiongozi hawezi kuwa na hiki na kile? Tulijadili lini haya? Tuliongea lini?

“Kapinga akasema, 'Nitapinga hili kwa nguvu, kama jina langu linavyosema.' “Nikasema, 'Aidha tuambiwe au tuulize mambo haya yamekujaje.' Nilimwambia Kapinga hivyo.

“Wakati huo kulikuwa na wajumbe sitini na watatu katika Kamati ya Utendaji, pamoja na Rais. Watu sitini walikuwa wajumbe, pamoja na wale wa Kamati Kuu. Wengine watatu walikuwa Rais, Makamu wa Rais na Katibu Mkuu. Itakuwaje watu sitini na watatu wabadilishe sheria zinazoongoza maisha ya watu milioni kumi na

——

WANAWAKE WATANU..——

101

tano au zaidi, kwa kuwaambia tu kwamba hili halitakuwa lile na lile halitakuwa hili? “Tulifika tukakuta mambo ni moto. Kila mtu anasema lake, nami

nikasema langu. Sheria hii ni mbaya, tunataka kuangushana hapa. Tulishauriana na watu kuhusu chama kimoja, na sasa twende tukawaulize hili suala, kwa sababu sheria hii inaingilia mila na tamaduniza watu wa nchi hii. Turudi kwa watu tuwaulize, kisha tuchukue maoni yao na kuyajadili katika mkutano, tufikie uamuzi kama tulivyofanya wakati tunaamua kuhusu nchi kuwa ya chama kimoja... “Ilivyoonekana, suala lilikwishafanyiwa uamuzi. Bwana mmoja, Ibrahim Changas, Mkuu wa Mkoa wa Singida, alisimama na

kuninyooshea kidole na kusema kuwa mimi ni mwongo, akadai kwamba nimekwishajenga nyumba kumi. Mwingine kutoka Musoma akasema kuwa mwanamke huyu ana nyumba tayari, ndiyo sababu anakataa hili azimio. Tukawaulize watu? Watu wataulizwa nini?....Watu walipinga vikali niliyokuwa nimesema... Baada ya mkutano huo, Rais mwenyewe alihutubia watu na kuwaambia kuwa Azimio la Arusha sasa ni sheria ya nchi.

Azimio la Arusha na sera ya "ANU ya Ujamaa na Kujitegemea yalikuwa matamko muhimu katika uongozi wa Nyerere. Dhamira zote - ujamaa, utaifishaji, maendeleo ya jamii, mielekeo mipya ya elimu, kujitegemea katika sera ya mambo ya nje na kufifia kwa tabaka la wasomi - yote yaliongozwa na mtazamo unaolenga kupata maendeleo kwa kujitegemea. Bila kujali kama sera hizi zilifanikiwa au la, zilihitaji misaada mingi kutoka nje. Hali hii ilikuwa ndio chanzo cha hali ngumu ya uchumi iliyotokea katika miaka ya 1980. "Hicho ndicho ninachojua kuhusu suala hili... kusema kweli maneno ya uchungu yalianza kuzungumzwa. Wale tulioweza kustahimili Azimio la Arusha tulibaki katika Kamati Kuu, wale walioshindwa, walitoka.

102



WANAWAKE WATANU..

———

“Baada ya sisi kuondoka, yakaja madai ya kupindua serikali, kwamba lilikuwa kusudio letu. Kusema kweli, sikujua chochote. Nilishirikiana na Oscar Kambona mpaka alipoondoka nchini, yeye alifahamu zaidi yangu...Alijaribu kunishawishi niondoke nchini, lakini nikamwambia waziwazi, sioni kosa tulilofanya...kwa nini tukamatwe?...Sikuiba kitu, sikufanya kosa lolote, sikumtukana mtu, au serikali au chama. Sasa kwa nini nikamatwe?

“Kambona aliniambia kuwa kutakuja siku nitaondoka, nikamwambia sawa, lakini sioni sababu ya kuondoka nchini.... Wasomi kadhaa wamejaribu kuelezea sababu zilizofanya tabaka la watawala wa Tanzania kukubali maadili ya uongozi yaliyowanyima kujilimbikizia mali. Kama alivyosema Bibi Titi, sio viongozi wote wa TANU walikubali Azimio, lakini walikuwa tayari kuachia fursa ya kiuchumi iwapite ili wakubalike kisiasa. Hata hivyo, Azimio liliacha mianya. Kwa mfano, viongozi waliokuwa na mali wangeweza kuziandikisha kwa majina ya watoto wao. Wangeweza pia kuajiri, ilimradi wawe vibarua na sio wafanyakazi wa kudumu.

Oscar Kambona alishushwa cheo kutoka Waziri wa Mambo ya Nje na kuwa Waziri wa Tawala za Mikoa. Alikwishakimbia nchi hata kabla ya kufukuzwa TANU, pamoja na wabunge wengine wanane. “Mume wangu aliambiwa aniache, kwani nitakamatwa karibuni. Aliambiwa,'Utajikuta katika hali ngumu ukiendelea na mwanamke huyu.' Halafu siku moja nikapata barua kutoka kwa mwanasheria ikiniambia kwamba sijalipa deni la nyumba kwa miezi miwili, kwamba nilipe mara moja ama nyumba itachukuliwa.... "Miezi sita baadaye nilikamatwa na kuwekwa kizuizini, Oktoba 1969. Nikakaa jela kwa miaka miwili na miezi miwili....Jela ni jela. Ni mbaya, haiwezi kuwa nzuri. Maisha ya mfungwa yeyote hayawezi kuwa mazuri... Nilikuwa peke yangu katika chumba,

———

WANAWAKE WATANU...——

103

nilipewa chakula cha daraja la pili - wali, nyama na maharage. Sikufanya kazi yoyote, sikuruhusiwa kutoka nje. Nilipata magazeti kwa hisani ya ofisa mmoja wa jela, ingawa sikustahili kuyapata. Nilikuwa napata barua, mama na binti yangu walikuwa wanakuja kuniona...” Bibi Titi alikaa kizuizini hadi February, 1972 ambapo aliachiliwa na kurudi nyumbani ambako alikuta nyumba zake zote tatu zimetaifishwa..

“Niliondoka nyumbani kwangu Upanga saa tano usiku mwaka 1969, sikurudi mpaka tarehe 317 Agosti, 1988. “Niliachiwa kutoka kifungoni bila masharti... Niliachiwa kwa msamaha wa Rais. Sikushangaa nilipoachiwa, sikutarajia lakini sikushangaa. Rais hakuja kuniona. Tulionana nilipokwenda kudai nyumba yangu irudishwe. “Sikufanya uhalifu.. Nilijiona kama mtu aliyefungwa kwa makosa. Sikufahamu kosa nililotenda...nikafikiri kwamba wao wenyewe, baada ya kufanya uchunguzi wameona kwamba sina kosa la kuniweka jela, kwa hiyo wakaamua kuniachia. Ingekuwa nimefanya kosa kubwa kama ilivyosemekana, kushirikiana na wanajeshi kupindua serikali, basi ningeshangaa kwamba mtu kama huyo anaweza akaachiwa.

“Baadhi ya watu niliowekwa nao kizuizini walikaa huko kwa muda mrefu, karibu miaka kumi na mmoja... “Baada ya kutoka kifungoni, niliuza mafuta ya taa. Ndiyo biashara pekee niliyofanya. Maisha yalikuwa magumu .sana...Nyumba yangu moja iliporudishwa, niliweza kuipangisha kwa shilingi elfu tatu kwa mwezi....Nilirudishiwa nyumba ya kwanza mwaka 1976 kwa msaada mkubwa wa Tabitha Siwale, aliyekuwa Waziri wa Ardhi. Nitamkumbuka maisha yangu yote...yeye ndiye aliyeweza kumwona Nyerere na kumshinikiza hadi nikaipata. Alikuwa

104

——

WANAWAKEWATANU..——

hodari, mwanamke yule. Wanaume waliogopa kumkabili Nyerere na kumwambia amrudishie Titi nyumba yake. “Kuhusu ushiriki wangu

katika siasa sasa, nakwenda

kwenye

sherehe kama nikialikwa, lakini sijihusishi wakati wote... Mimi ni mwanachama wa UWT na wa CCM.

“Ingawa wanawake wanasema kwamba hawajaendelea, mimi ninayewafahamu tangu wakati ule, naona kwamba wameendelea sana, kwa sababu serikali inataka kuwasaidia.

Tatizo liko kwa

wanawake viongozi, Siyo kwa wanawake kwa ujumla.” Katika shauku yake ya kuanzishwa kwa Mkutano wa Wanawake Waafrika, Bibi Titi alisisitiza msimamo wake juu ya uwezekano wa ushirika wa wanawake wa Afrika yote, utakaomwezesha mwanamke

Mwafrika kuwa na sauti katika safu za siasa. Kwa maoni yake, alipata ushindi wa kipekee alipofanikiwa kushawishi mkutano wa pili wa Wanawake wa Afrika ufanyike Tanganyika. Katika miaka ya mwanzoni mwa 1960, wanawake viongozi kutoka Uganda, Tanganyika na Kenya walikutana katika warsha kadhaa zilizopangwa na Margaret Kenyatta. Katika moja ya warsha hizo iliyofanyikia mjini Nairobi kuanzia Aprili 11 hadi 18, mwaka

1964, Bibi Titi alitoa moja ya hotuba zake kuu kwa

Kiswahili, kwa sababu Kiswahili ni lugha inayozungumzwa zaidi Afrika Mashariki, na wageni walihitaji kujua kwamba lugha hiyo inaenziwa. Hivyo ndivyo Bibi Titi alivyohusianisha mawazo yake kuhusu umuhimu wa nguo za Kiafrika, utamaduni na lugha na mitazamo ambayo leo inaitwa ya uwezeshaji. Bibi Titi hakuwa peke yake kati ya waliokuwa TANU ambao walishindwa katika uchaguzi wa 1965. Maofisa wa TANU ishirini na wawili kati ya thelathini na mmoja walishindwa, na kumi na sita kati ya wabunge thelathini na mmoja walipoteza ubunge. Kushindwa katika uchaguzi wa 1965 lilikuwa ni pigo kubwa kwa Bibi Titi na kiashiria kwa TANU na serikali kwamba wanasiasa wanapaswa kuhudumia majimbo yao bila kujali sifa za kazi zao. Kama tukiona upinzani wa Bibi Titi wa

———

WANAWAKE WATANU..——

105

Azimio

la Arusha na Maadili ya Viongozi kuwa ni suala la kulinda maslahi binafsi tu, basi tutakuwa tumefumbia macho suala zima la ushirikishwaji, ambalo ndilo limepelekea nchi kwenye mtindo uliopo wa 'ujamaa na kujitegemea.”

Kesi ya Uhaini Kuhusu maasi ya Januari 1964, yaliyofanyika mara baada ya mapinduzi ya Zanzibar, Bibi Titi alieleza kuwa woga na wasiwasi ulitanda, serikali na

umma ulishtushwa vibaya. Alipojaribu kuwauliza maofisa wenzake kulikuwa kumetokea nini alikamatwa na kupigwa. Sio mahali pake hapa kurejea maelezo yote ya Bibi Titi kwa sababu ni marefu, lakini kuna mambo mawili aliyoyasema ambayo yaliathiri maisha yake. Kwanza, ni kuhusu Kambona, rafiki na mshiriki wake kisiasa, kuwa mzungumzaji wa serikali wakati Nyerere akiwa mafichoni; na pili, ni kuhusu mume wake

kumkana Bibi Titi alipokuwa amekamatwa,kwa kuogopa kupigwa.

106

——

WANAWAKE WATANU..———

SURA YA KUMI Kutoka Kitengo cha Wanawake hadi

Umoja wa Wanawake

Bibi Titi anaeleza:

“Tarehe 2 Novemba, mwaka

1962, Mheshimiwa Nyerere aliagiza

kwamba vyama vyote vya wanawake Tanganyika vivunjwe; yaani, YWCA, Baraza la Wanawake Tanganyika na UMCA, ili viungane kuunda Umoja wa Wanawake Tanganyika (UWT).

;

“Umoja wa Wanawake ulikuwa tofauti na Kitengo cha Wanawake cha TANU. Kitengo cha Wanawake hakikuwa na Rais, kilikuwa na makatibu. Umoja wa Vijana, Kitengo cha Wanawake na Wazee vyote vilikuwa na makatibu. Uchaguzi ulipofanyika, mwaka 1959, mimi nilikuwa Ulaya, kwa hiyo Lucy Lameck akachaguliwa. Wanawake wakamkataa. Wakasema wanamtaka Titi, kwa hiyo mimi nikawa katibu UWT. Niliwavuta wanawake wa aina nyingi, wakiwepo wasomi. Hao walikuwa na wasiwasi na mimi, walisema kwamba siwapendi...lakini niliwapooza hawa wanawake... niliitisha mkutano, tukachagua kamati na kugawana kazi. Kazi za mikono zikaanza. Wakawakusanya wanawake pamoja na kuwafundisha usafi, upishi, malezi ya watoto....elimu ya watu wazima na ususi... Vitu vyote hivi havikuwepo katika Kitengo cha Wanawake cha TANU. Hatukuwa na muda wa kufanya vitu hivi,

vilifanywa na Baraza la Wanawake uhuru...”

la Tanganyika kabla ya

Kukosa elimu kwa Bibi Titi kulikuwa chanzo cha misuguano ndani ya UWT. Aliheshimika kwa kazi yake muhimu ya kupigania uhuru, na kama kiongozi aliyeweza kushirikiana na wanawake wa kawaida. Lakini |

| |

——

WANAWAKE WATANU..——

107

wanawake wasomi, vijana, ndio walioamini kwamba wana vitu vya kuwafundisha wanawake hawa wa kawaida. Hivyo, kipindi cha mpito kutoka 'siasa' kwenda 'maendeleo ya wanawake' hakikuwa rahisi. Siasa

ilibaki kuwa kipaji kikuu cha Bibi Titi.

“Nilikuwa Rais wa UWT mpaka tarehe10 Juni, mwaka 7967. Kabla sijaondoka UWT, niliongea na wanawake wengine wanishauri ni nani achukue uongozi baada ya kustaafu. Nilimhimiza Sophia agombee na akachaguliwa Mwenyekiti wa Mkoa wa Dar es Salaam. Lazima ufanye kazi hii kuisaidia nchi yako na mume wako pia,' nilimwambia. Chama kinaathirika kama kukiwa na udhaifu katika uongozi. “Nilipokuwa Mbunge, nilipigania haki sawa, nikijua kwamba wanawake walitoa mchango mkubwa kwa TANU. Kama haikuwa kwa juhudi za wanawake, uhuru ungekuwa mgumu kupatikana kwa sababu wanaume walikuwa waoga. Lakini sasa baada ya kupata uhuru yatubidi tujitahidi zaidi kujipatia maendeleo,

kuboresha maisha yetu. Ni lazima wanawake wapate elimu, wapate kazi serikalini. Kitu kilicho muhimu kwa wanaume kupata maendeleo, kiwe muhimu pia kwa wanawake. Ingawa mimi kama kiongozi wao sina elimu, walio na elimu wasinyimwe haki zao... “Kabla ya uhuru tulikuwa kama watumwa. Maendeleo waliyo nayo Wahindi ni matokeo ya misaada kutoka kwa Waingereza baada ya Vita Kuu ya Pili ya Dunia. Waingereza waliwaamini Wahindi zaidi, benki zao zikawapatia mikopo, zikatunyima Sisi. Baada ya uhuru na sisi tukapatiwa mikopo ya kujengea nyumba. Mimi nilikuwa na nyumba tatu baada ya uhuru.. Benki zilitafuta watu wenye fedha na wasiokuwa nazo, wote walipata mikopo. Kati ya viongozi wanaume, aliyeunga mkono wazo la usawa kwa wanawake alikuwa Nyerere. Yeye alikuwa ameshuhudia wanawake. Hata tuliposema huko bungeni kwamba wanaume

108

——

WANAWAKE WATANU..

———

waadhibiwe kwa kuwapa wasichana mimba, Nyerere alisimama kidete nyuma yetu...Kati ya wanawake wachache bungeni (tuliopigania suala hili) tulikuwa mimi, Lucy, Barbara Johansson na mwanamke mwingine aliyekuwa ameolewa na Mgoa huko Amboni,

Tanga.

Wanaume

walitukasirikia,

Nyerere alisema

ni

lazima sheria hiyo ipite, ili wanaume wanaolaghai wasichana na kuwapa mimba walipe faini, wafungwe au watunze hao watoto.”

Nilipokuwa naandika kuhusu UWT mwanzoni mwa miaka ya 1980, nilishiriki katika masimulizi haya yaliyoweka chanzo cha UWT katika Kitengo cha Wanawake cha TANU, na kwamba uongozi wake na wanachama walitoka hukohuko. Wakati huo, nilikosoa UWT kwa udhaifu wao, ikiwepo nilichoona kuwa ni mtazamo wa "juu-chini" wa

matatizo ya wanawake kuzingatia miradi ya uchumi inayowafaidisha wao wenyewe, ambao tayari walikuwa na ahueni, na dharau kwa wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, nilifikia uamuzi kwamba maendeleo

ya UWT yalikwamishwa na ukosefu wa ufanisi, ukosefu wa fedha na ukaribu wao kwa Chama cha Mapinduzi. Kutokana na mazungumzo na wanawake

wa Tanzania, nilikubali kwamba

UWT iliathiriwa

na fitina,

misuguano kati ya wasomi na wasiosoma. Nilitoa hoja kwamba mambo yote haya yalionesha dalili ya serikali ya kutotaka kuondokana na maneno matupu na kufanya vitendo dhahiri vitakavyoshughulikia mahusiano hasi ya kijinsia katika jamii ya Tanzania. Pia, serikali kutolikabili suala la utegemezi wa wanawake wa vijijini, pamoja na kutokuwa na mamlaka juu ya nguvukazi yao katika kaya. Wanawake wengi niliowahoji katika utafiti huu, hawakuona tatizo katika mabadiliko kutoka Kitengo cha Wanawake cha TANU kuwa Umoja wa Wanawake.

Ilikuwa rahisi kwa wanawake wanaharakati wa Moshi,

ambao walikuwa vijana na wasomi

zaidi kuliko wenzao wa Dar es

Salaam, kuona kwamba mwelekeo wa UWT wa miradi ndio mwendelezo

——

WANAWAKE WATANU..——

109

sahihi wa kusaidia wanawake katika nyanja zote. Lakini sikuuliza kama wanaona utata wowote katika majukumu ya Kitengo na UWT. Aliyekuwa katibu wa CCM mwaka 1988, Kanasia Mtenga, alisema kwamba mwaka 1962, wakati alipokuwa Makamu Mwenyekiti wa UWT, alijiona yuko peke yake. Titi alikwishakumbwa na matatizo, hivyo ilibidi awashawishi wanawake kwa wanaume kwamba chama cha wanawake bado ni muhimu, siyo kwa kupigana na wanaume kama walivyohofu, bali kwa kuwasaidia wanawake kujiendeleza. Tofauti kuu, kwa mtazamo wa Bibi Titi, ni kwamba taasisi moja iliongozwa na katibu na nyingine iliongozwa na rais. Sasa ni dhahiri kwamba UWT haikuwa mwendelezo wa harakati za wanawake wa TANU. Mkutano Mkuu wa Wanawake wa Afrika uliofanyika Dar es Salaam mwaka 1962, uliweka wazi katika rasimu ya katiba yao kwamba UWT ni ya kupigania ukombozi wa wanawake ili waweze kushiriki katika shughuli za kijamii na za kisiasa Afrika. Lakini Nyerere na washauri wake waliamua kwamba wanawake walihitaji kuendelea na kuendelezwa, na kwamba vikundi vilivyokuwa tayari vinafanya kazi hii viungane chini ya chama kimoja kitakachoshirikisha wanawake wote na kudhibitiwa na serikali. Msomi mmoja alipatwa na mshangao kuwa mara baada ya uhuru, wanawake wamekuwa wajinga na walio nyuma kimaendeleo, wamekuwa walengwa na siyo watendaji na wenye kujituma kuleta maendeleo. Suala la namna ya kuhamasisha wanawake likawa tatizo mara baada ya uhuru. Hiyo ilikuwa kejeli. Kama UWT ilivyokuwa wazo la Nyerere, wizara mpya ya Ushirika na Ustawi wa Jamii ndiyo iliyoandika katiba ya UWT kwa msaada wa washauri wa nje. Kikiwa chama mama kilichoundwa kuhifadhi vyama vingine, UWT hakikuchukua nafasi ya Kitengo cha Wanawake cha TANU, bali TCW ambacho mwenyekiti wake wakati huo alikuwa Mama Maria

vyama vilivyokuwa na maslahi mbalimbali pamoja na wanawake kutoka vikundi mbalimbali. Mrengo wa uhamasishaji wa kisiasa wa Kitengo cha Wanawake wa TANU ukafa. Mrengo wa kuzingatia usawa, sio tu kati ya

110



WANAWAKE WATANU..———

wanawake na wanaume, bali miongoni mwa wanawake, nao ukafa.

Hata hivyo, programu ya UWT ilikuwa katika mikono ya wanawake waliopania kufanya chama kiwe cha maoingwa watakaoleta ujuzi wa masuala ya kiuchumi katika kukabili mahitaji ya wanawake. Huko ndiko Nyerere alikotaka UWT iweke nguvu yake. Wanawake wengi, vijana na wasomi waliokuwa kitovu cha uongozi UWT, waliteuliwa kutoka taasisi na wizara za serikali, kutafuta fedha, kutoa miongozo katika mafunzo na warsha za uongozi, na katika miradi ya lishe ya aina mbalimbali na ya kuongeza kipato. Kumbukumbu za mkutano wa UWT wa 1965 zinatuonesha nafasi ya chama cha wanawake katika Tanzania huru. Nyerere, akiwa Baba wa Taifa, alifungua mkutano

huo kwa kuwakumbusha

washiriki kwamba

serikali imeanzisha UWT ili kuunganisha wanawake wote walioshiriki katika siasa na ambao hawakushiriki, tajiri na maskini, wasomi na wasio na elimu. Aliwaambia kwamba yawabidi watambue maadui wa ndani na nje wanaotaka kuvunja umoja. Aliwataka wachague viongozi

wanaokubalika. Kwa hiyo, katika hotuba moja, Nyerere alisimika mamlaka ya serikali kwa UWT na kuonyesha mwelekeo wake. Akizungumza kwenye mkutano siku ya pili, Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Bwana Mgonja, alizungumza katika njia iliyofifisha ari ya siasa kwa wanawake na kuimarisha mamlaka ya serikali. Wakati Kitengo cha Wanawake kilikuwa kinahamasisha wanawake wajiunge katika harakati za kujenga taifa, Mgonja aliwaambia wanawake kwamba wakilea watoto watakuwa wamelea taifa zima. Aliwasifu wanawake kwa juhudi zao katika kupigania uhuru, lakini kwa sasa walichotakiwa kufanya ni kulima, kufuga kuku, kuchimba visima na kupanda miti pamoja na kushiriki katika kisomo cha watu wazima. Mgonja alionya kwamba itabidi utamaduni

wa

Kiafrika

ukuzwe,

kwani wakoloni

waliudharau.

Alisahau kwamba vikundi vya ngoma vya wanawake ndivyo vilivyoshika hatamu

katika

uhamasishaji

wa

kizalendo,

wanawake zilikuwa hai na Kiswahili yaliyowasilisha ajenda ya TANU kikamilifu.

kazi za

kiliwezesha

kitamaduni

za

mawasiliano

——-

WANAWAKEWATANU..

———

111

Washiriki walijibu hotuba ya Mgonja kwa njia iliyodhihirisha utegemezi wao kifedha kwa Wizara ya Ustawi wa Jamii. UWT ilitaka wizara ilipie semina na walimu. Katiba ya UWT ilikubalika bila mjadala mrefu ingawa ingefaa kuangalia vipengele kadhaa. Kipengele kimoja kiliwanyima uanachama watu wezi,

wachochezi

na wale wanaoongea

vibaya

kuhusu

chama.

Kingine

kiliwanyima uanachama wageni kutoka nje. Hivyo, katiba ya UWT ilionesha kukubali kwamba kuwa macho dhidi ya maadui na watu wabaya ndio suala kuu kichama. Oscar Kambona, aliyekuwa Waziri wa Tawala za Mikoa, ndiye pekee aliyezungumzia umuhimu wa Kitengo cha Wanawake, ingawa kwa kujisifu kuwa ndiye aliyewapata wanawake shupavu kama Bibi Titi, Tatu Mzee na wengine. Alisema kuwa wanawake wanahitaji kufanya kazi kwa bidii, kwani hakuna taifa linalodhaniwa kuendelea kama wanawake hawajaendelea.

shughuli na siyo kukazania sehemu za mijini tu. Makamu wa Kwanza wa Rais, A.A. Karume, ndiye aliyefunga mkutano. Akiwasifu wanawake katika juhudi zao za ujenzi wa taifa, aliwasihi wanawake wafanye kazi kwa bidii kuwasaidia wanyonge na maskini wa rangi zote, pamoja na kulea watoto. Alionya dhidi ya ubaguzi wa rangi au dini, na kuwahimiza wanawake wajitegemee. Ajenda za mkutano kutoka wilayani zilionesha wazi safari ndefu ya kujikomboa waliyosafiri wanawake. Safari hii ilianzia katika uhamasishaji wa kizalendo wa wanawake wa TANU katika miaka ya 1950 hadi kufikia juhudi za UWT za kujitafutia nafasi katika taifa

lililowaona wanawake kama wapewa maendeleo. Washiriki walijadili kwa kirefu juu ya umuhimu wa vazi la taifa na kukubaliana kwamba nguo fupi zisiruhusiwe kuvaliwa kabisa. Washiriki kutoka

Geita walitaka kanga zisiandikwe maandishi yoyote, kwani yanayoandikwa ni matusi. Masuala mengine yalihusu bei ghali ya kadi ya TANU na UWT kwa wanawake wengine na sharti la kuwa na kadi ya TANU ili upate ya UWT.

112

——

WANAWAKEWATANU..———

Juhudi zilifanywa kuzungumzia suala la ubaguzi wa kijinsia, hususan kama UWT inaweza kuzuia wanaume wasiwafukuze au kuwaacha wake zao baada ya kuwazalia watoto wengi. Mkutano ulilaani vikali suala hilo, na wakati huohuo ukalaani wanawake waliozoea kuiba wanaume wa

wenzao. Mwishowe waliongea kuhusu tatizo la wanaume wanawake. Hili lilionekana kusababishwa na wanawake kwamba dawa ni kufanya kazi kwa bidii zaidi.

kuwadharau wenyewe

na

Hizi basi, ndizo juhudi za chama cha kitaifa cha wanawake, chenye

uelekeo wa siasa za dola, kilivyoshughulikia matatizo mapya ya wanawake na maendeleo mwaka 1965. Sasa ilkuwa ni serikali huru ya Kiafrika iliyokuwa ikiamua ni nini chama cha wanawake kifanye na kijali masuala gani.

——

WANAWAKE WATANU..———

113

SURA YA KUMI NA MOJA Lucy Lameck

lucy Selina Lameck hawezi kuwawakilisha wanaharakati wa TANU waliokiongoza Kitengo cha Wanawake wa TANU wakati wa miaka ya 1950. Hawezi pia kuwakilisha wanawake walioongoza UWT baada ya uhuru. Alimaliza sekondari, akasomea uuguzi, akapata elimu ya juu Uingereza na Marekani. Alikuwa msomi kuliko wanawake wengi wa kizazi chake na hakuwa Mwislamu. Vipengele vyote hivi viliiwezesha kazi yake ya siasa hadi kufikia miaka ya 1980. Alifariki Machi 21, 1992. Lucy Lameck alizungumza: “Nilikuwa na bahati. Mwaka

1962, Nyerere alitambua mchango

wa wanawake katika chama, na alifahamu fika kwamba kushiriki

kwao kikamilifu kunahitajika katika kuendeleza nchi. Kwa hiyo, aliniteua Waziri Mdogo wa Ustawi wa Jamii na Ushirika. Nilifanya kazi na vikundi vya wanawake na vyama vya ushirika, ambavyo navyo vilielekea kusaidia vikundi vya kiuchumi vya wanawake. Wakati huo, mabadiliko ya ushirika katika nchi yetu yalikuwa na nguvu Afrika nzima. “Nilikuwa Naibu Waziri mpaka mwaka 1965 nilipoamua kugombea ubunge katika jimbo la uchaguzi la mkoani kwangu. Ingawa nilipata upinzani wa nguvu, nilishinda. Mwaka 17966, nilihamishiwa Wizara ya Afya na Nyumba, nikawa hapo hadi mwaka 179772. Hivyo, nilifanya kazi kama Naibu Waziri kwa miaka kumi, kisha nikaruhusiwa kuondoka na kuweka nguvu katika shughuli za wanawake na jimbo langu.

114



WANAWAKE WATANU...

———

“Mwaka 71970 niligombea tena, mpinzani wangu akiwa Mwenyekiti wa Chama wa Mkoa. Wenyeviti wa Chama wa Mkoa ni watu wenye nguvu kubwa, lakini kwa vile nilikuwa bado napendwa, nilimshinda. Alinipinga tena mwaka 1975, sikushinda mwaka huo, lakini nilishinda tena mwaka 1980.

“Bado tuko katika harakati, bado tunafanya yale tunayoyaona kuwa ni sahihi. Kihistoria, wanawake wamekuwa shupavu sana katika kuimarisha chama, ndiyo sababu tunaweza kusema tunachotaka kusema na tukasikika...Na hatukuanza kwa kuvaa nguo ghali na dhahabu, tulikuwa wanyenyekevu, wanawake wa Lakini niongeze kuwa

tuliona tunaye mtu anayefaa (Nyerere)

ambaye tunaweza kumwamini na kumkabithi nchi yetu, tulihisi

kwamba yu mkweli, angetuachia nafasi ya kupumua, kungekuwa na uhuru na haki, kusingekuwa na ubaguzi wa rangi na watoto wetu wangekwenda shule...

“Ukiniuliza kama kulikuwa na mwanamke

aliyefikiria suala la

mshahara bora, nina wasiwasi sanad. Ni kweli, wanawake walikuwa na matatizo, na wanawake wa TANU walikuwa na

matatizo...lakini ninachotaka kukuambia ni kwamba sasa tuna nafasi nzuri zaidi ya kupigana dhidi ya dhuluma hizo kuliko ilivyokuwa kabla ya uhuru. Ningeongea na nani kabla ya uhuru? Nani angenisikiliza? Nisingenusa bungeni, wala kufika karibu.”

Katika mahojiano yaliyoendelea, Lucy Lameck aliongea kwa shauku kuhusu umuhimu wa kuendelea kupiga vita mila na desturi zinazozuia wanawake kutofikia usawa na wanaume. Aliamini kwamba ni lazima harakati hizi ziwepo katika ngazi zote za jamii, kuanzia ngazi ya chini ya umma, kwenye chama na bungeni. Alisisitiza kwamba Tanzania imepiga hatua kuliko nchi nyingi za Kiafrika katika sheria zinazohusu wanawake, kuhusu na kuongeza kwamba kuna umuhimu mkubwa wa tafiti matatizo ya wanawake zinazofanywa na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam

——

WANAWAKEWATANU.——

115

na asasi nyingine. Wanaume watashawishika juu ya umuhimu mabadiliko kwa kutumia taarifa za kisayansi pekee.

Lucy alilaani kitendo cha kuwafukuza mimba,

wakati

walimu,

wanafunzi

shule wasichana

wenzao

na

waliohusika hawakuadhibiwa. Pia, alilaani kwamba

wanaume

wa

waliopata wengine

imekuwa vigumu

(kwa serikali) kukubali elimu ya familia ifundishwe shuleni. Alisema kwamba wanawake walipata ajira kirahisi katika benki, hoteli, posta na sehemu zingine kwa vile waliaminika zaidi. Mahitaji ya wanawake vijijini ndiyo hasa yaliyohitaji kuangaliwa, na akasisistiza ugumu wa kushughulikia mahitaji hayo katika nchi maskini kama hii. Njozi ya Lucy Lameck kwa wanawake ilikuwa kuanzishwa kwa asasi za mafunzo mbalimbali katika kila wilaya, zitakazotoa elimu ya kilimo na ustawi wa mama na mtoto, pamoja na teknolojia inayofaa kwa kupunguza ugumu wa kazi za wanawake . Kuhusu wanawake kuwa na haki na mamlaka juu ya vile wanavyozalisha, alisema “Hiyo inakuja. Siyo mapema kama tunavyotaka, lakini inakuja. Ndiyo.” Katika kitabu hiki, nimeonesha uzoefu wa kihistoria wa wanawake wa TANU kwa kutumia maelezo yaliyowasilishwa kwangu katika miaka ya 1980. Nguvu ya wanawake wa TANU, kama wajenzi na watekelezaji wa uzalendo nchini Tanzania, iliundwa na kuathiriwa na hali iliyokuwa mbele yao. Hali hiyo ilifungwa katika muktadha wa mahitaji ya TANU ya uhamasishaji katika miaka ya 1950. Nguvu ya wanawake ilitokana

vilevile na uzoefu wao kihistoria pamoja na ukweli wa maisha waliyokuwa wakiishi. Hivyo vyote viliunda TANU na kuonesha aina ya uzalendo uliotokana na historia ya kijamii na kiutamaduni ya Tanganyika. Wanawake wanaharakati wa miaka ya 1950 hawakuweza kufanikisha kazi za kizazi kilichofuata au kupata ukombozi wa wanawake katika miaka ya 1990. Lakini wanaharakati hawa waliweza kueneza uzalendo,

pamoja na mawazo ya usawa na heshima kwa kupitia matendo yao na kwa kuwahamasisha wengine kushiriki kikamilifu katika siasa.Michakato ya ujenzi wa uzalendo nchini Tanganyika iliunganishwa katika uono na

116



WANAWAKEWATANU..———

matendo yao ya kijinsia, ambayo yaliendelea kuwezesha uzalendo wa kitaifa baada ya ukoloni. Utu, heshima na usawa, vipengele hivi vya ufahamu wa kizalendo bado vinahitajika.

Baadhi ya wanawake wanaharakati wa TANU

Wananchi wa Tanganyika walijipatia uhuru wao kutoka kwa Waingereza mwaka 1961 kupitia mapambano yaliyoongozwa na jumuiya yenye, nguvu chini ya uratibu wa chama cha TANU. Wanawake wazalendo walikuwa ni viongozi mashuhuri katika medani zote kwenye ngazi mbalimbali.

Kitabu hii kinauliza maswali kadhaa: Aa

Ni kwa nini utaifa wa Mtanzania ulichukua sura mpya baada ya uhuru kuliko ilivyokuwa katika nchi nyingine ? ”-

Ji

Na

hai

fa

Je, tunauelezeaje ukweli kwamba, licha ya tabia, utaifa wa Tanganyika umebaki kuwa alama tu ya utambulisho kwa

wanawake? 3

YA

!

Je, ukiangalia! ukweli kuwa utaifa na utamaduni katika Tanganyika vilikuwa kazi zilizoendeshwa na wanawake wa TANU, matokeo ya kazi yao ni wapi

Je, tunauelezeaje ukweli kuwa utaifa hapa Tanzania haukujengwa /na kikundi cha wanamapinduzi au haukuwa ni matokeo ya kuibuka kwa matabaka :kutaka kudhibiti dola?